‘Kuchanganyikiwa kwangu kumenifanya
nirudi nyuma sana, kiukweli
nawashukuru sana kuwa
mlikuja kwenye wakati muafaka, kipindi ambacho nilishakata tamaa, nimekuwa
nikihangaika kuona haki itatendeka, najua kabisa dada hakuwa hivyo,..lakini
najua aliyefanya hadi dada awe hivyo ni wewe msaliti..’akasema
‘Sikuelewi…’nikasema
nikigeuza kichwa kumuangalia docta, na docta akawa katulia tu
‘Huwezi kunielewa kamwe,
na huu sio muda wa kunielewa, muda utafika utanielewa, na kwa vile wenyewe
wanakuja, umesema polisi wanakuja, sawa najua itakuwa hivyo, mtakamatwa, na
mkikamatwa mengina yatafuta huko, niliwaambia lakini…’akasema
‘Unajuaje kuwa wanakuja
kutukamata sisi…?’ nikauliza
‘Muulize huyo mwenzako
atakuwa anajua zaidi , ila nawaonya lolote litakalotokea chonde chonde, sitaki
waje kuwagusa wazazi wangu, baba yangu yangu hajapona,unaelewa zaidi docta…’akatulia
kama anawaza jambo halafu akasema;
‘Hata hivyo nawashukuru
sana..kwa kunisaidia nikapona, bila nyie sijui ingekuwje, nilishafikia hatua na
mimi nataka kujiua,… nawashukuru sana, ila sasa nawaomba muondoke, kabla hamjaiingiza hii familia yangu kwenye
matatizo, hamjui tu…’akasema na sasa akaanza kutembea kuelekea ndani..
Kabla hata hajaingia
ndani….gari la polisi likawa linakuja kwa kasi…;
‘Polisi hao wanakuja,…’
alisema docta,
Tuendelee na kisa chetu
*****************
Mara polisi wakafika na gari lao, hata kabla
halijasimama vyema askari wawili wakaruka na kutuweka chini ya ulinzi, na
baadae wakatoka askari wengine wawili, wakatembea kuelekea mlangoni,..
‘Tunataka kuonana na
binti…’akasema askari ambaye alionekana ni bosi wao.
‘Na Binti, binti
gani..?’ akauliza docta
‘Binti wa huyu mzee, mzee
mwenye nyumba hii, …’akasema , sasa akielekea mlangoni na kuingia ndani…, na
mimi nikawa namuangalia docta kuona kama
atachukua hatua gani, maana nilijua na sisi tutakamatwa. Na wakati huo wale
askari wawili wakiwa na silaha walikuwa wamesimama wakituangalia sisi
‘Duuh, hawa watu
wanataka kufanya nini sasa..?’ akasema docta, akionyesha uso wa mashaka, na
mmoja wa wale askari wawili akasema;
‘Msisogee, mkao hapo
hapo…’akasema kwa sauti kali, na docta ni kama vile hakujali ile amri yao akawa
kama anatembea, halafu akasimama, akaniangalia na mimi nikasema;.
‘Hata sijui….hawajui
kuwa wanaweza kumuathiri huyo mzee, si huyo mzee hatakiwi kuingizwa kwenye
mshituko tena, …..docta fanya jambo, uwaeleweshe hao watu, hawajui hao,
wanatumia nguvu tu…’nikamwambia, lakini docta akawa kasimama tu akingojea
‘Docta…’nikasema kwa
sauti, na docta akasema;
‘Subiri…huwezi
ukaingilia kazi za watu hivi hivi, hatujui lengo lao ni nini..’akasema na mara
tukasikia kilio huko ndani, na hapo docta akataka kukimbilia ndani lakini
askari wake wakatuzuia.
‘Mimi ni docta na hao ni
wagonjwa wangu, nina haki ya kuhakikisha wanatdea inavyopaswa, ..kama mkinizuia
na lolote likitokea mtawajibika nyie..’akasema docta, na aliposema hivyo, yule
askari akasogea pembeni na docta akaelekea huko ndani , na mimi nikafuata
nyuma..
Tulipofika ndani,
tulimuona yule askari akiwa kamshikilia huyo binti mkono, na mkono mwingine
baba kamshikilia binti yake…mama akiwa pembeni, ..
‘Sisi watu wa usalama na
kazi yetu ni kuhakikisha usalama wa kila raia, na tunapoona raia yupo hatarini,
hatuwezi kukaa kimia,…huyu tunaondoka naye, tutamshikilia kwa muda, mpaka hapo
tutakapojirizisha, kuwa yupo salama…tuna maana yetu kubwa, hakuna haja ya
kuongea zaidi, mengine mtakuja kuambiwa..’akasema huyo askari
‘Sawa kwa usalama wake, …kwa
vipi, ujue sisi ni wazazi wake, tuna haki ya kufahamu, huwezi ukaja ukambeba
huyu mtoto hivi hivi , kama muhalifu, na kama ni mhalifu tuambie, ana kosa
gani..?’ akauliza mzee.
‘Kuna makosa ambayo kwa
hivi sasa siwezi kukutajia mzee, ..tuelewe sana, tuna kibali cha kumshikilia
huyu yako hiki hapa…’akasema huyo askari, akimuonyesha huyo mzee hicho kibali, na
mzee hakutaka hata kukiangalia, akasema;
‘Kama mnataka kumkamata
huyu binti, nikamateni mimi, mimi ndio baba yake, na kama labda, …ni matatizo
yalitokea kwenye ile nyumba yangu…huyu binti hahusiki maana nyumba ni yangu,..,
kwanini mnamkata yeye, mtu alikuwa anaumwa,..siwaelewi lakini,,..’akasema mzee
‘Mzee, usipandishe munkari,
matatizo uliyo nayo hayataki..hasira…, chukulia hili jambo kama kazi ya polisi,
wana maana yao kubwa tu…, niachie mimi nitalifuatilia hili jambo, na
kuhakikisha binti anarejea salama, mimi mwenyewe nitaongozana naye, unanielewa
mzee, pamoja kuwa mimi ni dakitari, lakini pia nilisomea sheria..’akasema docta
Binti alivyosikia hivyo,
akasema;
‘Baba unaona nilikuambia
hawa watu sio watu wema, wanataka kuleta matatizo kwenye hii familia,..inaonekana
wao ndio wamewaita polisi ili nikamatwe, hukuona walivyokuwa wananihoji,
utafikiri wananishuku mimi kwa jambo fulani,.. sasa mimi baba nakamatwa mimi
binti yako…, hujui ni nini kitafuata baadae… haya baba, haya mama, mimi nakwenda
kufungwa bila hata kosa…’akasema binti kwa sauti ya huzuni,
‘Binti, hakuna tatizo
kubwa…tuamini sisi… hili tunalofanya ni kwa ajili ya usalama wako…’akasema
polisi akimshikilia mkono ili waondoke, na baba akawa anazuia..mama naye akawa
anafanya hivyo, na docta akamsogelea mzee na kumnong’oneza kitu sikioni…mzee
akashtuka, halafu, akasogea , wakati huo binti alikuwa kamshikilia baba yake
mkono ili asiondoke.
Baba akawa sasa kama
anauondoa mkono wake kwa binti wake, huku
akimuangalia binti yake huyo kwa macho ya mshangao…sasa akionyesha kukubali,
binti huyo achukuliwe…kitu ambacho kilimfanya binti ashikwe na mshangao, lakini
zaidi ilikuwa mama yake.
Sio binti au mama aliyeliona
lile tendo la docta kumnong’oneza huyo mzee, kwahiyo ile hali ya mzee huyo, ya
ghafla, ya kuonyesha kukubaliana na polisi, iliwafanya wawili hao, wajihisi
vibaya, ..baba anawasaliti, baba hayupo nao,…akili ya kibinadamu ikaanza
kufikiri hivyo, na muda huo bab akageukia upande mwingine kama anawapa mgongo.
‘Baba…’binti akaita,
baba hageuki,..
‘Mume wangu vipi tena
unakubali binti yetu achukuliwe, kuna nini hapa lakini, mbona mimi sielewi,
kumetokea nini…?’ mama akauliza kwa huzuni.
‘Tumuachie docta
afuatane na hawa watu,najua binti yangu atakuwa salama huko,…najua , hamna
shida, mimi nitakuja baadae …’akasema baba, sasa akiwa kasimama pembeni ,
lakini mama hakukubali…ikawa mshike mshike , baadae mama akasalimu amri binti
akachukulia, lakini hakuacha kabisa , akawa bado kama anafuata nyuma, na baadae
akamgeukia mume wake..
‘Kama binti yangu
atadhurika, kwa lolote lile, sitakusamehe kwa hili…umeniudhi sana, ina maana
unakubali binti yako achukuliwe tu, hujui, kwasababu gani, au unajua ni kwanini
wanamchukua, niambie sasa…’akasema mke lakini mume akabakia kimia hadi hao watu
wakaondoka.
‘Jamani mwanangu,
mnampeleka wapi binti yangu…nichukueni mimi kama mnafikiri kuna tatizo…’mama
akakimbilia nje hakukata tamaa.
**********
Baadae tulibakia mimi na
wawili hao, mama alikuwa kakasirika hataki hata kuongea na mumewe, utafikiri
mumewe ndiye aliyesababisha yote hayo, na mimi hata sikuwa najua ni nini
kinachoendelea maana docta likuwa hajapata muda wa kunielezea, haya mambo
yalitokea kwa haraka haraka.
Baadae simu ikalia,
ilikuwa yani simu ya mzee, kabla mzee hajaipokea nikamsogelea,
Angalia namba kwanza ni
nani anakupigia, mzee akaiangalia akasema haina jina ni namba ngeni
kwake,..nikawaza kwa haraka, nikasema, pokea tu, ila uwe makini,..
‘Halooh, nani
mwenzangu..’akasema mzee, na kusikiliza, alisikiliza kwa muda mrefu bila kusema
neno, baadae akawa kama anaangalia juu ya nyumba kuzunguka, halafu akakata simu
‘Mhh..hili sasa ni
tatizo..’akasema mzee.
‘Ni nani huyo..?’
nikauliza, na mzee akani kwepa swali langu, akamgeukia mkewe na kusema;
‘Mke wangu uwe na
subira, kiukweli tupo kwenye matatizo makubwa, sijui nia ya hawa watu nini…mimi
sijui nimewakosea nini hawa watu…wangeniambia wanataka nini niwape lakini
tuzidi kumuomba mungu tu…sasa nakuomba sana mke wangu uniamini..hebu twende nje
kidogo, nataka kukuagiza jambo…’akasema na wakatoka nje.
Mimi nilibakia peke
yangu , baadae nikapokea ujumbe wa maandishi kutoka kwa docta, alikuwa
akiniagiza mambo ya kufanya,…haraka haraka nikaingia chumba cha mabinti, …nikaanza
kutafuta hicho alichoniagiza docta;
‘Laptop…’ nikaangalia
huku na kule mle chumbani, kilikuwa chumba cha kike, kila kitu kimepangwa kwa
umaridadi,…nikaiona, ilikuwa kwenye kitanda kuna sehemu yake, nikaiona,.. kwa
haraka nikaichukua na kuiweka kwenye mfuko wa Rambo, na kwa haraka nikatoka
nayo, na kwa muda huo mzee na mkewe wakaingia.
‘Sasa tufanyeje..?’
akauliza mzee
‘Tuwe na subira tu…ila
mimi natoka kidogo, nafika hapo dukani, nitarudi sasa hivi, naomba mjitahidi
kuwa na subira…, najua mnavyojiskia, lakini hao watu wanatimiza wajibu wao, na
uzuri wapo na docta, mimi namuamini sana docta ..’nikasema
‘Nimekuelewa, ila
usichelewe..’akasema mzee, lakini mama alikuwa kakasirika tu, kaangalia upande
mwingine..mimi kwa haraka nikatoka mle na kutembea hadi sehemu yenye nafasi,
nika kaa kwenye kigogo..nilipohakikisha nipo peke yangu, nikaitoa ile laptop..,
na kuiwasha.
Ilikuwa na kifungio(password) nikafanya kama
nilivyoagizwa kwenye ujumbe wa simu,.. ikafunguka,..kwanza nikaona vile vitufe
mbali mbali, nikatafuta kitufe cha Facebook,…
Nikakifungua, na huko
nikatafuta kitufe nilichoagizwa, nikakifungua pia na mara…oh, nilichoona hapo
kilinifanya niishiwe nguvu,…..
Mungu wangu, kulitokea picha ya marehemu, akiwa kakaa peke yake,
kashika shavu, na chini yake kuna maandishi;
‘Kwaheri mpenzi wangu,
nilikupenda sana,…najua umeshanisahau lakini mimi sijakusau, nilikupenda ndio
maana uliponifanyia vile, sikuweza kuvumilia, nikaona njia rahisi ni kujiondoa
humu duniani, najua ipo siku utakuja huku tutakutana ..kwaheri ya kuonana…’
Kiukweli nilihsi hali ya
uchungu sana, nilitamani kulia,..na kwa chini nikaona picha nyingine,….
Hii picha ya chini yake, ni ile ya yule msichana akiwa
kwenye kaburi, lakini sasa ipo kwa mtindo wa video fupi, na nilipoibofya,
ikafunguka,…ilianza na mlio kidogo wa wimbo wa huzuni,…mara akatokea yule mdada
kwenye kaburi, akawa kama anatokeza vile kama mtu anayefufuka,kutokea kaburini
, hapo ukatokea mlio wa kutisha kama bomu limelipuka….mpaka nilishtuka!
Sura ya huyu mdada sasa
haina tofauti na sura ya yule marehemu, nahisi walifanya hivyo ili kuonyesha
kuwa huyo ni mtu mmoja,..labda kabdilika kutokana na wakati au huko alipo
kumemfany awe hivo…sijui au..hata sielewi wana maana gani,..ile sura ikatoka na
kukaja kama kitanda lakini cha maua,..yule mdada akawa kalala kwenye kile kitanda
cha mua, huku anatabasamu,.., kalala upande upande,..akiniangalia…hayo …macho,
mhh, mbona, yanafanana ..macho macho…
Nikawa nimevutika na
hayo macho zaidi.., nikawa nayaangalia, duuh..ukimuangalia macho yake ndio
hivyo unakuwa kama unazama ndani yake…na hali hiyo ya kuzama ndani yake
iliufanya mwili wangu ulegee, nikawa sina nguvu, akili na mawazo nikajihisi mtu
mwingine..
Nikahisi sauti sasa
ikiongelewa masikioni mwangu.., sauti tamu yenye mvuto, ni sauto ile ile
inayonifanya niliwazike, saut ile iliyonifanya nitokeee kumpenda huyu binti,
sauti ya mpenzi wangu wa facebook…lakini ina ujumbe mnzito..
‘Ulisaliti kwa ulionifanyia..sitaweza
kukuusahau kwa hilo , sasa unafanya nini, nimekutafuta hupatikani,..hutaki hata
kuingia facebook, umesema utakuja kwetu hujafika, kweli unanipenda wewe, au
ndio umedanganywa na huyo docta wako kuwa mimi sio binadamu, hahaha, yaani
imani yako imegeuzwa, sasa unaamini mambo ya kichwawi, kweli wewe ni mnafiki…’akasema
na mimi nikashindwa, kujizuia, nikaaandika kwenye sehemu ya ujumbe.
‘Kweli nakupenda lakini
sijui unaishi wapi…na mimi sio mnafiki, siamini mamb hayo natambua wewe upon a ipo
siku tutakutana,….’
‘Hahaha, eti hujui
ninaishi wapi, kweli wewe ni mwanaume, uwe unampenda mwanamke, halafu ushindwe
kujua anaishi wapi, …hahaha, ama kweli wewe ni mmoja wao, mnapenda kuwadanganya
akina dada, ujue mimi sidanganyiki, utakuja kunitafuta usinione…’ nilishangaa
nilijua ile ni video ya kurekodi, lakini kumbe ni mbashara. Unaandika anaona na
anakujibu papo hapo
‘Kwani hapo upo wapi..?’
nikamuuliza.
‘Kule kule
nilipokuagiza, uje…na huko huko ndio tutakutana tena kwenye safari yetu ya
maisha mapya…, usijali, nahisi muda umeshafika, nakupenda sana mpenzi wangu,
..karibu sana, wazazi wangu wana hamu ya kukuona...’akasema
‘Ahasante, nitafurahi
sana..nakupenda na mimi sana, ila safari hii usinidanganye..unanipoteza njia..’nikasema
na yey e akatabsamu akawa kama anipiga busu la mbali akiweka mikono..na macho
hayo, yakanywea, …akapotea
Yaani ni hali ambayo
huwezi kuelezea, ni kama ulikuwa sehemu na yeye, kumetulia kuna ubaridi fulani
wa kusisimua mwili na ghafla unarudi sehemu ulipokuwa, joto ..joto kali ..mmh, …!
Baadae ile picha ikawa
kama imeyeyuka, na ukumbuke naangalia kwenye laptop kwenye facebook, na chini
yake nikaona kitu kingine kikanivutia ingaaje ni tukio la kuhuzunisha…ni picha
ya watu wapo makaburini, wanakwenda kuzika, na ilikuwa picha,..na
nilipoiangalia sana nikawa kama nazama ndani …ni vitu vy ajabu ina maana
ukiiangali aile picha, unazama kuelekea kwenye hilo tukio, unakuwa sehemu ya
wale watu
Nikawa kama mmoja wa
waombelezaji, nikawa sijui ni nani anayezikuwa, nikajikuta nauliza;.
‘Ni nani kafa..?’nikauliza
hivyo lakini akilini, na mara nikasikia suti nyingine ikisema
‘Mlinzi wa nyumba ya
mzee,… leo ndio anakwenda kuzikwa, na yeye, viungo vyake vitakuwa biashara..’sauti
ikasema
‘Oh, nilisahau…lakini
kwanini viungo vyake view biashara kwani,…’nikasema
‘Ndio kawaida,…wala
usisumbuke kuuliza kwani hata wewe siku ikifika kama itakuwa hivyo, utafanyiwa
hivyo, lakini hutasikia, wala haitakuathiri kitu, maana utakuwa na mimi, si
umesema utakuja…?’ sauti ikaniuliza
‘Mhh…sijakuelewa, kuwa
na mimi itakuwa hivyo, kwa vipi..’nikasema kwa kuuliza
‘Muda ukifika
utajua,..na ukija tutaonana..nitakusubiria..nahisi itakuwa moja ya namna ya
kuzoeana, au sio…’sauti ikasema.
Mara nikarejea kwenye hali yangu, nikakumbuka
kuwa nasoma kitu kwenye laptop, sasa nikawa naangalia vitu vingine, na sikujua
kuwa wakati mwingine umepita,..baadae nikakumbuka, ooh,
‘Hivi nafanya nini..?’
nikajiuliza,..nikakumbuka kuwa nilielekezwa jambo…
‘Fungu laptop, ingia
kwenye facebook, tafuta ….ok, nimefanya hivyo, utaona maagizo yako, halafu
nitakupigia simu…’
Sijui ikawaje, nilihis
kama sio jambo la kawaida, na sizani kama ..haiwezekani, ndio baaadae ikawa
kama akili inafungua, nikakumbuka n akukumbuka huko ni pale nilipohisi kama
docta ananionya jambo....
‘Usije kuchat na huyo mtu, na kama ukichat
naye kwepa sana mambo hayo…usimuangalia macho yake kwa hisia,..ukumbuke ukifany
ahivyo, kwa hisia na ukahisi kama unazama ndani ya macho yake ujue, wewe
unakuwa ndani yake, anakusoma akili yako…na...utakuwa mtumwa wake…’
‘Mungu wangu..’nikasema
hivyo, nilipohisi kuwa nipo kwenye hatari..hatari gani, niliwaza hivyo tu…
Kitu kilichonishangaza ni kuwa nilipokea
ujumbe kutoka kwa docta, kupitia kwenye simu, ukinieleza nifanye hivyo, nilivyofanya,
…sasa nimefanya hivyo yametokea mambo hayo ambayo ni kinyume na maagizo ya
docta….mbona hivi, imekuwaje..
Hapo akili ikanicheza,
fahamu zikawa zinanirudia kwa mbali,..akili ikanijia nikaichukua simu yangu na
kuifungua, nikaangalia ujumbe niliotumiwa, ooh, sikuwa nimeangalia vyema sizani
kama ujumbe huo umetoka kwa docta…ni
ujumbe kwenye simu …mwishoni ndio aliandika mimi docta, ..
‘Ssshit…’nikasema
nilipogundua huo mtego
Hapo nikajua nipo kwenye
mtego, nikachukua ile laptop, nikairudishia kwenye mfuko, nikaamua nimpigia
simu docta nimuelezee kilichotokea,..kabla sijapiga simu mara. Simu yangu
ikalia, nikajikuta nimeipokea, na sauti ikasema;
‘Leo ni siku ya mazishi
ya mwenzenu..alikuwa mtiifu, lakini
baadae akakiuka masharti, na dawa ya watu kama hao, kama ilivyo nyie, ni hiyo,
najua kila mtu atakufa, lakini kifo kingine ni cha kujitakia, kajitakia, na
amekipata alichokitaka..najua hata wewe ndicho unakitaka, sasa subiria zamu
yako …’akasema
‘Wewe ni nani..?’
nikauliza kwa haraka.
‘Hahaha, utakuja
kuichunguza hiyo namba kwenye simu, kama utapata bahati hiyo na utagundua kuwa mimi
ni nani…’akasema
‘Unataka nini kwangu..?’
nikauliza
‘Usijali ninachokita mimi
tayari nimeshakipata, ila huyo binti, …namuonea huruma sana,..huko
mlipomficha,.. sikutaka kumfanya chochote, ila kwa hali ilivyo, kwa ajili yenu,
sizani kama nitakuwa na uwezo wa kumlinda tena, ngoja tuone, …tukimalizana na
wewe, nitajua afanywaje…’akasema
‘Kwani wewe ni nani..,ndio
wewe sio…?’ nikauliza
‘Hahaha, unataka kujua
mimi ni nani, sasa nikuambie kitu, geuka nyuma utaniona mimi ni nani..’akasema
na kweli kuna hali iliniashiria kuwa sipo peke yangu, kwa haraka nikataka
kugeuka..nimechelewa
Kabla sijafanya hivyo, kitu
kigumu kikigonga kichwa changu, na giza likatanda usoni, nikapotea kwenye giza
*********
WAZO LA LEO:
Ni muhimu sana kwenye mambo yetu tukawa na
tahadhari, ..ni ili tuwe na tahadhari hiyo kabla ya kila jambo, tumuweke
mungu wetu mbele, tuombe, tumuombe yule aliyetuumba, ili jambo hilo liwe kwenye
kinga na rehema na baraka zake mola wetu muumba.
Wengi wetu kutokana na kazi nyingi, kujisahau,
au dharau tu,..si unacho,… huwa tunajifanyia mambo yetu bila hata ya kumuomba
mola wetu, maana twaona tumepata au tunafanya kutokana na akili zetu, au ujanja
wetu, au utukufu wetu, …lakini tukumbuke kuwa yote hayo tunayapata kutokana na
rehema , na kudra za mola wetu muumba. kwahiyo basi, tujijue kama wanadamu tunajukumu
la kumuombe na kumshukuru mola wetu kwa kila jambo.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment