Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeWednesday, May 31, 2017

MPENZI WA FACEBOOK-40


Mzee alizindukana, na akawa anajaribu kujiinua ili akae sawa pale kitandani alipolala,…alichoka kulala, alitaka kutoka nje atembee kunyosha mwili japo kidogo, lakini asingeliweza kufanya hivyo, mwili hauna nguvu, na wakati anajiuliza hivyo mara akasikia sauti ikamwambia;

‘Baba tulia usijilazimishe, wanasema bado unahitajika kupumzika,…’sauti ikasema na mzee akageuka kumtizama. Kumbe hakuwa peke yake,..akawa sasa anajiuliza huyu binti yake alikuja humo muda gani.

‘Kumbe umekuja…ulikuja saa ngapi…?’ akamuuliza

‘Nilikuja muda….nilipofika nikasikia wakisema umezindukana, lakini hujaweza kujitambua, ndio nikaona nisubirie mpaka utakapo zindukana,…’akasema

Baba alimuangalia binti yake kwa muda, halafu mara machozi yakaanza kumtoka

‘Baba vipi mbona unalia…?’ akamuuliza

Baba mtu alitulia kwa muda, akiwa kajiinamia, baadae ndio akasema;

‘Binti yangu nakuomba unisamehe sana, niliapa moyoni kuwa nitakulinda kwa nguvu zangu zote,nitailinda familia yangu kwa nguvu zangu zote,..lakini kwa…kwa uzembe wangu nilijua umekufa, …’akasema mzee.

‘Baba achana na hayo,… uzembe wako kwa vipi, ni hao watu ndio wabaya, na ubaya wao hauwezi kukufanya wewe mzembe,...'akasema binti,

'Wewe hujui tu....kukuona upo hai....nilishikwa na mshituko mkubwa sana....'akasema mzee.

'Unajua baba,.. siku ile nilipofika nyumbani, na…uliponiona ukadondoka chini na kupoteza fahamu, nilogopa sana, nilijiuliza ni kwanini,...na ile hali ika..nifanya na mimi, lakini sijui kwamba ni hiyo hali ya kushtuka na mimi au kuna jambo jingine...'akasema binti.

'Unahisi kuna jambo jingine, hapana...mimi tu nilipatwa na mshutuko...'akasema mzee.

'Baba unajua ni kwanini nilirudi nyumbani mwenyewe,...kuna hali ilinijia kuwa nije huko nyumbani,  kuna vitu nikavichukue,,....hiyo hali inasema kuwa vitu hivyo ndio chanzo cha haya matatizo yote, kwhiyo nivichukue..kwenye chumba chako chako, kile ambacho sisi hatuwezi kukifungua... nivipeleke mahali,...wapo sijui...na ghafla ndio nimefika, nakuona..na wewe..., ukadondoka…sikuweza kuvumilia…’akasema binti.

‘Kwahiyo wao huenda ndio walikutuma au sio..kwa mbinu zao za kishirikina au sio...?’’ akauliza.

‘Hata sijui..ila kuna hali ilisema nikafanya hivyo..nahisi labda …kuna kitu gani unacho, ambacho wanakitafuta sana…?’ akauliza binti.

‘Mimi sijui, na kwanini wasiniambie hicho kitu wanachokitafuta niwapatie ili familia yangu iwe na amani…’akasema.

‘Kwahiyo baba,…siku ile ulipodondoka na kupoteza fahamu.., na mimi nikaishiwa nguvu nikadondoka pia, na kupoteza fahamu…nilipozindukana nikajikuta nipo hospitalini, nikauliza kuhusu wewe nikaambiwa hujutambui, na hali yako ni mbaya sana..nililia sana, nikijua na …oh,…’akatulia..

‘Oh, hata sijui ilikuwaje…nilipokuona, ….nilipata mshituko mkubwa sana..kwanza nilihis kuwa …unajua hata dada yako alipofariki, nilikuwa natokewa na kitu kama hicho, ananijia akilini, au naweza kuangalia hivi,nikamuona mbele yangu..hali hiyo ilinitesa sana,mpaka nikaja kusahau….sasa wewe kunijia hivyo..nikahisi ni yale yale ya dada yako…..’akasema
‘Kwanini uhisi hivyo baba, kwani, ulisikia kuwa nimeshakufa..?’ akauliza binti.

‘Mimi …nilijua kuwa umeshafariki,, na kufariki kwako ni kutokana na uzembe wangu, nilishindwa kumuwahi yule mtu aliyataka kukupiga risasi…’akasema

‘Kunipiga risasi mimi, kwanini watake kuniua, mbona sikumbuki baba…kwahiyo wewe ukajua nimekushafariki…?’ akauliza

‘Ndio mwanangu, na ulipojitokeza siku ile nikajikutwa nashikwa na mshutuko mkuwa, lakini sio kwa vile tu nimekuona,… bali pia,nilimuona marehemu dada yako mbele yako,…yaani wewe sikuoni kama wewe , ninayemuona ni marehemu dada yako..’akasema baba.

‘Marehemu dada yangu, kwa vipi baba, hivi sijakuambia..?’ akauliza

‘Si dada yako,…kwani umesahau kuwa dada yako hayupo tena duniani…au ?’akasema na kuuliza.

‘Baba dada hajafariki…dada yupo hai, nimemuona mimi, kwa macho yangu mwenyewe, ila kwasasa sijui wamemficha wapi..ila yupo hai, hao watu sijui kwanini wanafanya hivyo..’akasema binti na baba akamuangalia binti yake kwa jicho la mashaka, akasema;

‘Binti yangu naona bado una marue rue..una maana akili yako bado haijatulia,..awali ulikuwa ukisema hivyo hivyo, mpaka ukawa unakimbia ovyo, tukahangaika mpaka ukapona..baadae ndio yakaanza haya matatizo …sasa mimi nina mashaka na wewe labda matatizo yake yameanza tena,… mtu akifa ameshakufa, hawezi kufufuka, hayo mengine ni ujahili wao tu.

‘Baba niamini mimi…nimepata taarifa zao zote jinsi gani wanavyofanya hao watu kuna mambo wakati mwingine nahisi kama nipo kwenye njozi, na wakati mwingine ninajitambua…baba kwa masikio yangu nilisikia wakiongea hilo,..yule aliyezikwa kule makaburini sio yeye,…’akasema.

‘Ni nani, ..hebu achana na mambo ya kishirikina binti….’akasema

‘Baba nikuulize wakati mnamzika dada uliwahi kumchunguza, ukamuangalia usoni, ukahakikisha kuwa ndio yeye…?’ akauliza binti.

‘Kipindi kile nilikuwa nimechanganyikiwa huzuni,..na kiukweli sikuwahi kumchunguza, sikuwahi kumuangalia usoni,..hilo sikuwahi kulifanya, ila naju akuwa ndio yeye, kweli amekufa…’akasema.

‘Wao wanafanya ujanja hata wa kuvalisha mtu sura ya bandia..unajua nikuambi e kitu, hilo jambo,..hata watu wa usalama wamekwenda kulifanyia utafiti je ni kweli aliyezikiwa pale makaburini ni dada au kuna mtu mwingine, bado hawajaleta taarifa,..ila baba, mimi nina uhakika, huyo aliyezikwa pale sio dada, ni mtu  mwingine kabisa,..’akasema.

‘Hata siamini,…achana na imani hizo, kubali kuwa mtu ni lazima afe na dada yako alishafariki, kwanini muanze kulete habarii hizo,…unahisi mama yako akisiki ahivyo itakuwaje….…’akasema baba

‘Baba , mimi sina wasiwasi na mama, mama, yupo imara, ninawasiwasi na wewe maana sasa hivi kila ukipata mshituko,….unadondoka na upoteza fahamu, …hata nilipota hili, sikutaka kukuambia, ..lakini naona ni bora nikuambie sasa ili uanza kulizoe, ili hata kama dada akitokea isije ikawa ni mashutuko kwako…’akasema binti.
‘Siwezi kuamini hicho kitu…mimi namuamini mungu kuwa mja wake keshamtaka, siku za binti yangu zilishafika,…hayo mengine ni yenu…’akasema baba

‘Ni kweli baba, mja wa mungu siku zake zikifika anatangulia mbele ya haki..siku zake zikifika..lakini kwa dada ilikuwa bado..ndio maana mpaka sasa bado yupo hai, mengine yaliyofanyika ni mazingaumbwe..ni uchawi wao , baba,…niamini nikuambialo…’akasema.

‘Nitaamini hapo nikumuona kwa macho yangu, na akipimwa na kuonekana kweli ni damu yangu, vinginevyo, ninaomba tuachane na hili, maana naona unataka kunichanga nya tena.

‘Baba ujikaze, maana itakuwa mshtuko mkubwa kwetu sote, bado hatujawa na uhakika kamili, maana hawa watu wanapenda kujivika ngozi za bandia, isije ikawa wamemvika mtu mwingine ngozi ya bandia,..inayofanana nay a dada… na sisi tukaona ndio dada..lakini hata kama watafanya hivyo kwa mtu mwingine wakamvika sura ya dada, haya dada yupo wapi,..maana huyo aliyezikwa pale makaburini sio dada!

‘Binti yangu tuyaache hayo, maana nahisi unaongea vitu vya …..sijui, ngoja tuone, haya mama yako hajambo..?’ baba akaona abadili mazungumzo na kuleta jambo jingine.

‘Mama hajambo, bado wamemshikilia kituo cha polisi, sasa hivi wanasema wamemshikilia hivyo kwa usalama wake, wanahisi akiachiliwa,  hao watu wabaya wanaweza kuja kumuua,..na mimi naona ni bora iwe hivyo…’akasema binti.

‘Kwanini..lakini…hata hivyo, labda ..na wewe walifanya hivyo kwako, huoni kwasasa upo huru..lakini hata hivyo, mimi sina amani kama nipo hapa nimelazwa na wewe upo nyumbani peke yako…nitawaomba hawa madakitari nikaugulie nyumbani..’akasema baba.

‘Baba, bora ubakia huku huku…afya yako bado..usiwe na shaka na mimi, mimi najua jinsi gani ya kujilinda, na hao watu hawana umuhimu na mimi tena, kwanza sasa hivi wapo njia panda, maana wameshagundulikana..’akasema binti.

‘Na mama yako je…yupo na hilo kundi au..kwanini watake kumuua, uliwahi kusikia huko kuwa na mama yako ni miongoni mwao..?’ akauliza baba.

‘Baba…hawezi kuwa miongoni mwao,ila wanamtaka kwasababu zao tu…kuna mambo ya kijinga yapo vichwani mwa watu..na mama akatumbukizwa kwa kulazimishiwa tu, na kwahiyo huenda akawa anawafahamu hao watu wa hilo kundi ndio maana wanataka kumuua na yeye.

‘Kwa vipi, na kwanini hakuwahi kuniambia kuhusu hilo kundi unajua ni hatari namna hii unaishi na mtu kumbe ana mambo yake ya siri…hata sitamuelewa kamwe..’akasema baba.

‘Unajua baba, ni kwanini mama hajaweza kukuambia, ni kutokana na hayo masharti yao..kafanya hivyo kwa nia ya kuilinda familia, …, angelikuambia, awali huenda ungelikuwa haupo hai..au mama mwenyewe, wenyewe wana siri zao, ukila kiapo ukija kusema wanakuua,..’akasema.

‘Lakini mtu hafi mpaka siku zake, …achana na imani hizo kuwa wangeniua, wangeniua mimi au mama yako kama siku za mtu zimefika, ninacholaumu ni kuwa,..kwanini kwanza akajiunga na hao watu, na kuingie kwenye masharti ya viapo, huoni huo ni ushirikina, ....’akasema baba.

‘Hao watu baba hawana mchezo…wana sababu zao za kumuingiza mama kwenye hilo kundi..sizani kama mama alipenda tu kujiunga…na wakishakuunganisha na ukajua mambo yao, huna jinsi, …ukitaka kutoka, unatoka ukiwa maiti ..niliwahi kushuhudia wakiua mtu, ..baba, sitaki hata kukumbuka hilo tukio..’akasema binti.

‘Mhh,…sasa polisi wanasemaje mpaka sasa…maana siku zimepita na mimi,oooh,nahisi mwili wote hauna nguvu, na zaidi…sijui …nahisi akili kam sio ya kwangu…’akasema.

‘Polisi ndio wamewashikilia baadhi ya watu,na wale watu waliotoroka, wameshakamatwa tena,..na wengine wameongea ukweli yaliyowakuta hadi kujiunga na kundi hilo haramu, wangine wanasema hawakupenda ili walijikuta wakilizamishwa…kuna baadi ya watu hasa viongozi wa hilo kundi ndio hawajamakatwa…’akasema binti.

‘Kwahiyo mama yako kashikiliwa ..alikuwa ni mmoja wa viongozi au sio…ngoja nipone, nikitoka hapa hospitalini salama,…nitakuja kuongea naye anielezee vizuri, ni kwanini akafanya hivyo,…sijui kama ndoa yetu itakuwa na amani tena, inafikia wakati sasa nashinwa kumuamini..’akasema baba.

‘Baba…’binti akalalamika.

‘Hakuna cha baba, ndoa ina masharti yake huwezi kufanya mambo mabaya kama hayo,  ukamficha mwenzi wako, familia inakuwa hatarini, kwasababu gani, alitaka nini huko…..angalia sasa familia imetaabika, kumbe mtu ninaye humu humu ndani…, anajua kila kitu..’akasema.

‘Baba alifanya hivyo akiogopa….mbona hata mimi kuna mengine nilikuja kuyafahamu lakini sikuweza kuwaambia kwa vile walishaniambia na kunilisha kiapo kuwa nikisema nyie mtauliwa…sasa mimi ningefanyaje kama kweli nawapenda…kwahiyo baba wewe msamehe tu mama….’akasema

‘Lakini wewe ni tofauti na mama yako,mama yako ni kiongozi ni mmoja wa viongozi wa hilo kundi, najua anafahamu mengi sana kuhusu hilo kundi..…sasa huyo utamsamehe kweli, ngoja haya mambo yaishe kwa amani nitajua cha kufanya huko mbele ya safari..’akasema .

‘Baba mimi nataka myamalize haya mambo kwa amani….msameheane…, nikitoka hapa nitakwenda kuongea na mama, nijue na yeye ana msimamo gani,na kwanini hataki kumtaja huyo kiongozi wa kundi ni nani, je ni huyo kaka yake…….nailiskia mbele ya mahakama nasikia alisema kaka yake ndio yupo nyuma ya haya mambo yote, na alipoulizwa kuwa ndiyo yeye mkuu wa hilo kundi, nasikia alisema kuwa sio yeye kuna mtu mwingine.

‘Wewe unamjua huyo mtu mwingine?’ baba akauliza

‘Hapana baba mimi simfahamu huyo mtu....Baba huyo mtu mpaka sasa hajajulikani kabisa…lakini sijui kwanini, mimi nahisi huyo mkuu ni huyo huyo kaka yake mama, kwani wewe humfahamu huyo kaka yake mama. Hukuwahi kumuona..?’ binti akauliza.

‘Kama ni huyo kaka yake aliyetoweka kipindi hicho, namfahamu kiasi..lakini dada yako ana kaka wengine wa baba wengine, …ambao walikuwa ni maadui zake, unajua tena mambo ya kifamilia, baba akiwa na nyumba nyingi, na familia hizo zikawa hazina mahusiano mema, baba akiondoka tu, huku nyumba kunabaki na mtihani…sasa sijui, ..’akasema

‘Lakini ndugu hao wengine si hawapo hapa mijini, hapa majini yupo nani na nani, si huyo….aliyefariki kwenye jumba, watakuwa walimuua wao..na mwingine ni huyo mwenye biashara ya super marketi..huyo naye wanamtilia mashaka..na nilisikia docta akisema yeye anaweza kuwa pia ….ndio mkuu, awali kabisa walikuwa wakimuhisi hivyo, lakini siku zilivyokwenda akaonekana sio yeye…’akasema binti.

‘Mengi tungeliyafahamu kutoka kwa mama yako..nahisi yeye ana jambo kubwa , na huko mahakamani watamgundua, ..sijui atawezaje kujitetea….mwanzoni nilijua labda anapambana nao kuhusu mali ya urithi, lakini sasa nahisi ana jambo jingine…’akasema baba.

‘Au nikuhusu bastola,…na viatu, na…ufunguo wa ajabu..’akasema binti halafu akajishuku kuwa kaongea kitu ambacho hakutaka kukiongea mbele ya baba yake.

‘Bastola, ..! Ni nani kakuambia hayo..?’ baba akauliza akionyesha kushangaa.

‘Nimesikia huko wakiliongelea hilo, kwani baba wewe unavyo hivyo vitu,na ulivipataje..?’ akauliza binti, na baba akabakia kimia hakusema neno, alikuwa kazama kwenye mawazo.

‘Baba hivyo vitu ni vya hatari sana…na yote hayo ni kwa ajili ya hivyo vitu, kama unavyo ni bora utafute jinsi ya kuachana nanvyo..’akasema binti.

‘Lakini ni halali yangu, nimepewa hivyo vitu, kihalali,  ..na kama vilikuwa ni vya hao watu, kwanini nipewe mimi…mimi ni haki yangu, ..na sizani kama nina makosa kuvimiliki..na kwanini wavitake hivyo vitu?’ akauliza baba.

‘Baba…nilivyosikia ni kuwa vitu hivyo, ni mali ya familia ya mama,…. vilichukuliwa enzi hizo, na vitu hivyo, vina mkono wa shetani..ukiwa navyo, kama sio halali yako, utaandamwa na mabalaa..na ili usiandamwe na hayo mabalaa, inabidi utoe makafara ya damu, tena damu za watu, …sasa wanadai damu inatakiwa itoke kwenye familia yako, ndio maana wanhangaika hivyo…’akasema.

‘Ni ujinga huo…maana mimi nimepewa kihalali, sio kwamba nimeviiba, na kama ingelikuwa hivyo, kwanini hao walionipa kama zawadi hawakuniambia hivyo…’akasema baba.

‘Ndivyo nilivyosikia hivyo baba, lisemwalo lipo, na kama hisia ni hiyo kwanini baba tukae na vitu vya kishetani, kwanini, mimi sioni umhimu wake ,…’akasema binti.

‘Ni nani hasa anatakiwa kumiliki hivyo vitu ulisikia wakiongea..?’ akaulizwa

‘Ni warithi wa hivyo vitu….nilisikia wakimuongelea mpanzi wa facebook, na huyu mpenzi wa facebook, unakumbuka, waliwahi kumuongelea docta ..unakumbuka, sasa huyu, kama nijuavyo mimi anaweza akawa ndiye mumiliki wa hivyo vitu, katika karne yao,…ama kwa karne yenu..mama anaweza akawa mrithi halali wa hivyo vitu…’akasema.

‘Kwanini mama yako?’ akauliza.

‘Nilivyosikia mama anatokea ukoo wa kifalme, sijui huko zamani walikuwa wakiitwaje,..lakini mama ndiye mrithi ..alitakiwa aje kuvimiliki hivyo vitu, sasa muda wake ulishapita, kwahiyo anayetakiwa kuvimiliki ni watoto wa mama, na aliyestahiki ni dada…’akasema.

‘Oh…kwahiyo ndio maana wakamtaka,…ili aolewe na mtu wao, ili waje kuvipata kutoka kwa…aaah, inakuja hivyo, lakini yote ni upuuzi, maana hivyo vitu, viatu na bastola nilipewa mimi…kwanini sasa wake kuvitaka, kwanini hawakuenda huko kwa…hao watu,…’akasema baba.

‘Hapo ndio sijui….’akasema binti.

‘Wewe kaongee na mama yako, na muhimu kwasasa ni wakili wake tuone jinsi gani ya kumsaidia mama yako…nashindwa, ningeliweza nilitaka niende nikaongee nay eye mimi mwenyewe, kama hataniambia ukweli, nitajua la kufanya,…’akasema baba.

‘Na hivyo vitu…vipo wapi?’ akauliza binti.

‘Unavitakia nini…achana navyo,..nitaviharibu lakin sitakubali mtu avichukue maana ni halali yangu , nilipewa kihalali, na sijui lolote kuhusu hayo mambo yao,…’akasema.

‘Baba….tuachane na hivyo vitu…’akasema binti.

‘Kama ….ngoja nifikirie..ila kiukweli,..sitakubali mtu avichukue…wewe nenda niachie hilo jambo, nitakuja kupata jibu muafaka, kama ni kuviharibu au kuwauzia, wao si wanavitaka nitwauzia, lakini ngoja nifikirie kwanza...’akasema na baadae binti akaondoka.

Binti aliondoka hapo, huku akiwaza jinsi gani ya kufanya ili familia yao iondokane na balaa hilo, lengo lake ilikuwa kuvichukua hivyo vitu na kuwakabidhi hao watu, ili waachane na familia yake, lakini anahisi hilo halitawezekana kirahisi mbele ya baba yake.

‘Sasa hivyo vitu vipo wapi, labda mama atakiwa anafahamu vilipo hivyo vitu…’ akawa anajiuliza hadi alipofika kituo cha polisi walipowekwa mama yake.


*************

Mimi nilishikwa na butwaa, maana uso wangu ulitakapaa ubongo wa huyo jamaa, nahisi muuaji alipanga kuniua mimi, au sisi sote wawili,… lakini shabaha haikukamilika hivyo..kwani wakati huyo jamaa akitaka kufanya jambo, nahisi alitaka kujirusha kwa nyuma ili aninyang’anye bastola,,….kwani kwanza aliudaka mkono wangu, ulishika bastola, akataka kunivuta ili niachie bastola, ..

Pale sasa anajitahidi na kutaka kugeuka ndio hiyo risasi ikapigwa, ..ni kitendo cha haraka sana,…hata hivyo, huyo wakili hakuwahi kuichukua hiyo bastola mkononi mwangu, nilikuwa nimeishikilia bara bara, hata wakati docta anakuja, nikiwa nimeshikwa na butwaa, bastola ilikuwa bado mkononi mwangu,..

‘Upo sawa…?’ akaniuliza docta

‘Hata sijui..’

‘Sasa toka humo ndani,…polisi watakuja wakitaka kukuhoji, usiseme lolote waambie siwezi kuongea kitu…kilichotokea ni kitendo cha haraka sana…na usiwaambie lolote kuhusu bastola, na huo ufunguo…hata wakikuhoji vipi, umenielewa…’akasema

‘Nimekuelewa, …’nikasema

‘Unielewe vyema…, maana hatujui yupi ni yupi yupo kwenye hilo kundi, na mimi natakiwa niondoke na hivi vitu kwa haraka, wasije kuviona, sawa, ..ila wewe uwe mjasiri, lolote jingine laweza kutokea, kwa hivi sasa siwezi kukusaidia, nataka nihakikishe hivi vitu vipo mahali salama…pambana na litakalotokea, ..huwezi kuondoka hapa kwa hivi sasa mpaka polisi wafike kukuhoji…’akasema docta kwa haraka haraka.

Ni wakati sasa ninatokandani ya gari.. ndio docta akatoa amri kuwa nilale chini kwa haraka, na mimi nikafanya hivyo, risasi zikapiga kwenye gari…pale kwenye mlango wa gari nilipokuwa nimesimama.., ilikuwa alimanusura, sijui docta yeye aliwaonaje.

Docta alinitupia jicho kwa haraka alipoona nipo salama, yeye akajiviringisha, chini, na kwa haraka ndio, akasimama akiwa kainama, na kuanza kukimbia kuelekea ndani ya geti la hospitali. Yaani hapo nikaamini kuwa docta sio mtu wa mchezo, huyu mtu anaweza asiwe ni docta tu…!

 Mimi nilibakia pale pale nikiwa nimelala,…maana askari walikuwa wameshafika, na kusimama nyuma ya gari kama kinga yao, nahisi walijua huyo jamaa anaweza kupiga risasi nyingine, lakini haikutokea hivyo…nilikuwa sasa nimechichumaa, nje ya gari, mlango wa gari upo wazi,..nahisi kutapika.

Mara askari akaja pale nilipokuwa akawa anaongea na simu ya mkononi, akasema ;

‘Oh, wamemuua,… ndio…ndio mkuu…’ akasema, baadae akatulia akisikiliza maelekezo,..akasema ;

‘Ndio mkuu…’akaambiwa, halafu akakagua ndani ya gari, akaniangalia na hakusema neno, akatembea kuelekea nyuma ya gari, na ndio kwa muda huo kwa mbele yangu nikaona askari wengine wawili wakija, muelekeo wa pale nilipokuwa…jinai wanavyokuja, akili yangu iliashiria hatari..

‘Hao watu sio watu wema, kimbia….’nilihisi nikiambiwa hivyo akilini…Ndio pale nikasimama nikitaka kukimbia, lakini hata kabla sijafanya kitu, nikasikia mtu nyuma yangu akiniambia…

‘Ukisogea hatua moja umekufa…’ na muda huo hao askari niliowaona wakija wakawa wameshafika, na walipofika, wakiwa wamenielekezea bunduki, mmoja wao akasema;

‘Mkague…’akasema na huyu aliyekuwa nyuma yangu ..sijui labda ni yule wa kwanza aliye-elekea nyuma y agari, au ni mwingine alikuja, huyu ndiye aliyenikagua, na alipoona sina kitu ndio akamwambia huyu aliyekuwa mbele yangu na mwenzake, na huyo akaipiga simu kwa bosi wao, labda akisema;

‘Hanayo, hana kitu chochote, tufanyeje…?’ akauliza na kusikiliza, alipopewa ujumbe akageuka kuondoka huku akisema

‘Muueni huyu mtu , mara moja…’

Kauli hiyo ilinifanya nishange, hawa ni askari kweli,..na bila kupoteza muda nikajirusha kwa mbele,..huku nikirusha mchanga, kwa huyu wa mbele aliyeachwa na mwenzangu akipwa amri ya kuniua,…ilinijia tu , kuwa nifanye hivyo, na mchanga ukanisaidia.

Yule wa mbele mchanga ukamuingi machoni, na huyu wa nyuma kwangu alipoona nilivyojirusha, akataka kufyatua risasi, nikamrushia mchanga kama nilivyofanya yule wa awali, na mchanga ukafanya kazi ya kunikoa,…na muda ule ule, kule getini, mlango wa kuingia mahakamani, nikawaona askari wakija, hawa, nikajua ni askari wa kweli.

Hawa jamaa walipoona askari wanakuja wakajifanya kujikasuha huku wakianza kuondoka, yaonyesha walihofia kutekeleza hilo agiza, na yaonyesha kuwa huenda sio askari, na wakaona njia rahisi ni kuondoka, na mimi nikaona jamboo jema ni kuhakikisha hao jamaa wanakamatwa, nikasema;

‘Hawa sio askari, walitaka kuniua..’nikasema kwa suti kubwa, iliowafanya wale askari waliokuja sasa hivi, walikuwa watano, wawaamrishe ha wa askari wawili wasimame, lakini hao askari wawili hawakutii amri,  wakawa wanataka kukimbia...

‘Mpo chini ya ulinzi, simameni…’wakaambiwa, lakini walichofanya ni kukimbia, na risasi ikapigwa…ikampata mguuni yule wa kwanza na wapili akageuka na kuanza kupwapiga risasi hawa askari watani, na kwa kitendo hicho, akawa kajichongea, risasi moja ikampata huyo jamaa kifuani,…akadondoka, na huku mwenzake yupo chini anaugulia jraha la risasi…
.
Mimi pale nikaona hapanifai tena..,..kushuhudia watu wakiuliwa vile, nikageuka kutaka kuondoka,. Lakini wakati nataka kufnay hivyo, nikamuona mtu,mtu aliyenitia hamasa ya kumchunguza, ..sijui kwanini shauku yangu ilienda kwa huyo mtu, huyo mtu alikuwa kavalia kofia pana, na alinitupia jicho kwa haraka, alipoona ninamuangalia akainama chini….na kuanza kutembea kuondoka eneoo hilo..

Kwa haraka mtu huyo akaingia mlango wa mahakama, nahisi alikuwa anafuatilia kitu na ndio hapo nikamtumi ujumbe wa maneno, docta, na docta akanijibu hivi;

‘Ahsante, nipo tayari, kwa hilo..nimeshamuona tayari, ni yule jamaa aliyekuwa kampangaisha mzee …sasa, sina uhakika kama ni kundi lao au ana ajenda gani nyingine,.. ngoja nimchunguze anachotaka kukifanya….’akasema docta.

Mimi nilipoona askari sasa hawana habari na mimi nikaanza kuondoka eneo hilo taratibu, nikitaka niende huko ndani, nitafute sehemu nioge kabisa, na wakati naingia kwenye geti la mlango wa mahakama, ndio nikasikia mtu akiongea kwa simu. Alikuwa kajificha kwenye kibanda kilichokuwepo hapo, akawa kanipa mgongo.

‘Yupo humu ndani ya mahakama, ..hajatoka, nahisi yeye ndio kavichuku ahivyo vitu,…kabla ya kumuua, ni bora kuvipata hivyo vitu kwanza, …na msaidizi wake yupo nje ya mahakama, naona bora na yeye amalizwe ili tubakiwe na watu wachache …’akasema.


‘Oh..na huyu mzee yumo, ....mbona itakuwa ni shida...’nikasema kwa sauti ndogo, na mara huyo mzee akageuka akaniona...;

Nb: Ngoja tuishie hapa kwa muda,...

WAZO LA LEO: Tusipende kukimbilia kuwahukumu wengine kwa kuwahisi kuwa ni wao wamefanya mabaya mpaka tuwe na uhakika na shutuma hizo. Siku hizi watu hupenda kuwashutumu wenzao , kuwa wamefanya hiki na kile, ..(matendo mabaya), hata kama hawana uhakika nao, na hata kukimbilia kusema watu hao wahukumiwe  au wauwawe…au  watumbuliwe kwa lugha ya kisasa,..vyovyote iwavyo, lakini tunasahau kuwa haki ya hukumu mtu mwingine, ni mpaka mtendaji wa kosa apatikane na hatia, je kama utamuhukumu mtu n kumbe sio yeye mkosaji, utawezaje kulilipa hilo 

Mimi: emu-three

No comments :