Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeTuesday, May 30, 2017

MPENZI WA FACEBOOK-39 Wakili yule aliweza kutoka nje...licha amri kutolewa ya yeye kukamatwa...

Aliweza kutoka kwa haraka,..., maana watu wengi walikuwa wakiingia ndani kwa muda huo wakitaka kujua kinachoendelea huko ndani, baada ya kusikia kelele, hawakufahamu kuwa anayepigiwa kelele ni huyo wakili mtetezi.

Na kama kungelikuwa na askari nje, labda wangeshamkata, lakini ilionekana kama hakuna ulazima wa kumkata huyo mtu kwa muda huo..., kwahiyo ikawa ni rahisi kwa huyo wakili, kutoka nje na kuingia ndani ya gari lake, kwa haraka akawasha gari, lakini kabla hajaanza kuondoka, mara akaguswa na kitu kigumu kisogo mwake,…

‘Baba, ….unataka kwenda wapi muheshimiwa wakili,… mtaalamu, unataka kukimbia sio….,hatuendi hivyo…’akaambiwa na sauti ya mtu aliyekuwa nyuma ya gari lake.

‘Wewe ni nani na unataka nini ndani ya gari langu na kwanza umeingiaje humu na wakati nilikuwa nimelifunga,…?’ akauliza huyo wakili, huku akiangalia kiyoo cha kuonyesha nyuma, kiyoo kilikuwa kimekunjuliwa kujifunika, ….na yeye hakuwahi kukifanya hivyo.

‘Mimi ni msaidizi wa docta,..ukitaka nikutajie jina,,….hahaha, nimeshapona mtaalamu, mlijua mtatufanya mandondocha au sio….hilo sahau, na ama, ni kwa vipi nimefungau gari lako,…hahaha..nitakuambia tu, nimefungua kwa ufungu wenu , ufunguo, wa ajabu..’akaambiwa na jamaa aliposikia hivyo, akagwaya…na kusema;

‘Eti nini, umeupataje huo ufunguo wa ajabu, kwanza ni ufunguo gani huo, kwanini unaitwa wa ajabu.,…?’ akauliza

‘Usiniulize maswali kama hujui..unajua sana..cha muhimu kwa hivi sasa ni kutokupotezeana wakati, kwa hivi sasa huna jinsi, ukubaliane na mimi, uondoke zako, au nikusukumie kwa hao watu wa usalama.

‘Sawa, unataka nini, …hata hivyo najiuliza umewezaje kuupata huo uunguo wa ajabu, ni ajabu kweli….’akasema

‘Ni rahisi tu,…jamaa yenu yule, alipotoka huko hospitalini, alifika huko makaburini,..na mimi nilishapata maelekezo, kuwa atafika eneo hilo, kwenye pango lenu la siri…unasikia….’akatulia, kwani aliona askari wakilijia hilo gari.

‘Naona kama una habari nzuri, lakini humu ndani hakuna usalama, je tufanyeje, ili tuweze kuongea bila kuogopa mtu..?’ akauliza hivyo.

‘Endesha tu,…tutoke humu…., nimeshaongea na docta, wasikufanye chochote  mimi nina maongezi muhimu mimi na wewe, kuna jambo nahitajia msaada wako…’akasema.

‘Unahitajia msaada wangu mimi, wa kisheria au…unataka niwe wakili wako, sawa hakuna shida, lakini…?’ akauliza lakini sikuweza kumpa nafasi ya kuongea zaidi, nikamuuliza.

‘Wewe unahitajika kuwa wakili wa watu wako sio mimi…..usipofanya nitakavyo, nitakukabidhi kwa watu wa usalama unaowakimbia…na ii silaha inaweza kutumika wakti wowote ikibidi…’nikasema

‘Oh..unajua siamini unachoniambia,..kuwa eti wewe una ufunguo wa ajabu,..umeupataje huo ufunguo, … maana ufunguo huo hautoki mwilini kwa bosi, …kwa jamaa mmoja ambaye nasikia anao,unao huo ufunguo kweli naweza kuuona…?’akauliza huku akiendesha gari hadi akalitoa nje ya getini, na kweli askari hawakutuzuia….nilitarajia labda angeendesha tu kuelekea huko anapoishi au sehemu ambayo anaweza kunifanya lolote, lakini ni nani haogopi kifo..

‘Ufunguo huu hapa…’nikasema na kumuonyesha kwa haraka halafu nikarudisha mkono nyuma, na jamaa akahema kwa nguvu, na kusema;

‘Kama ndio wenyewe, basi, …uliwezaje kuuchukua kutoka kwa huyo jamaa..?’ kauliza sasa akichelewa kutumia neno bosi,…na mimi nikamwambia;

‘Yeye bosi wako wakati, anatoka hospitalini..nilimuona na wenzake,…bahati yako wewe hukukamatwa, …’nikasema

‘Nikamatwe kwa kosa gani…?’ akauliza

‘Unalifahamu sana,…’nikasema

‘hebu niambie ulivyoupata huo ufunguo….’akasema

‘Niliupata kutoka kwa bosi wako baada ya yeye kutoroka hospitalini kwa ujanja, najua kuna madakitari pale ni watu wake…na alipotoka, kuna hisia ziliniongoza nimfuatilie huyo jamaa,..’nikasema

‘Ina maana hao watu waliokamatwa, wamatoroka,…habari ngeni kwangu..’akasema

‘Unajua sana, unajaribu kunitega, lakini ilivyotokea ni hivyo, huyo bosi wako alipotoroka,  niliwaona, na mimi ndio nikawafuatilia kwa nyuma, kwa kuchukua bajaji…hawakutarajia kuwa kuna mtu atawafuata nahisi hivyo,..gari lao liliendeshwa hadi maeneo ya makaburini, kwa haraka yeye akatoka na wenzake wakaondoka na hilo gari.

‘Yeye akatembea kuelekea eneo la kaburi, kaburi lile lile, alilozikwa yule binti wa mzee,… akainama na mara akaanza kusukuma sehemu ya juu, ikasogea,…kumbe kwa juu imewekewa kitu …ni mlango unaweza kuusukuma ukafunguka,…aliposogeza, akaangalia huku na kule, kuhakikisha kuwa hakuna mtu anayemchunguza,  halafu huyo akazama ndani ya hilo kaburi..na mimi kwa haraka nikafika hapo...

Wakati analifunga kwa ndani mimi nilikuwa nimeshafika kwa juu, nikawahi kuweka kitu cha kuzuia lisijifunge moja kwa moja,..kwahiyo kukabakia uwazi wa kuweza mimi kulifungua…’nikasema.

‘Najiuliza uliwezaje kuwa na utashi wa kumfuatilia, …ni docta alikuambia hivyo au…?’ akauliza
Docta hakuniambia hilo…ni hisia zangu tu,…’nikasema

‘Haiwezekani, hisia….kwa vipi mbona sikuelewi…’akasema

‘Hisia zangu ziliniambia niwafuatilie, na hisia hizo hizo zikaniambia ..nilipofika eneo hilo, nifanye hivo nilivyofanya,..nikaingia humo ndani ya kaburi kama alivyofanya bosi wako, humo liliambiwa nitakuta vitu muhimu sana, nivichukue,,...sikujua ni vitu gani kuwa muda huo… mimi nilifuta hizo hisia zangu tu.

‘Hisia gani tena, kwani wewe bado unazo hizo hisia,…aaha, najua ulishaondolewa kila kitu, imekuwaje tena…?’ akauliza sasa akiwa na wasiwasi.
‘Subiri, usiwe na wasiwasi…ndio nakusimulia hivyo…mimi kabla ya yote hayo nilishaanza kuwa na hisia za ajabu,..kuacha zile za kuniambia niende makaburini nikutane na mpenzi wa facebook, nilikuwa nimeshaanza kuwa na hisia za asili zinanielekeza mambo tu,...kwahiyo mliponiondoa mambo yenu kichwani mwangu, nikabakia na hisia zangu za asili..

‘Ulijuaje kuwa ho watu watatoroka,…?’ akuliza

Wakati nipo hospitalini,..mimi nilikuwa bado naendelea na matibabu, …ndio nikahisi hiyo hali…hisia zikanijia kuwa natakiwa nitoke humo ndani,..nilichofanya mimi ni kubadili nguo, nakutokea kwa kutumia mlango wa nyuma bila kujulikana na mtu…na wakati natoka ndio nikawaona hao watu wenu wakitoka,mmoja mmoja na kuinngia kwenye gari…na gari lilipoondoka, nikaitisha bajaji, kutokana na hisia hizo…niliambiwa nielekee makaburini, nikafika huko.

Ndio wakati nafika jamaa yako anatoka kwenye gari, na kuelekea kwenye hilo kaburi, umenielewa hapo….?’nikasema na huyo jamaa akatikisa kichwa kukubali.

Na kwa vile ule mfuniko kwenye kaburi, ulikuwa haujajifunga vyema, ikawa kwangu ni rahisi kuusukuma na kufunuka, kumbe kwa ndani kuna ngazi upande wa pembeni, kuacha sehemu ile ulipolazwa mwili… wajanja kweli nyie watu.

 Lilipofunuka, nikaambiwa niingie ndani, nikafanya hivyo, nikaambiwa nilifunge hilo kaburi kwa juu, nikiwa ndani, nikafanya hivyo,… na nilipoingia ndani, nikajikuta nimesimama kwenye kaburi lisilo na kitu, ila kwa pembeni kuna sehemu ina uwazi fulani,  ..na upande wa pili kumejengewa vizuri, nahisi ndipo maiti yupo, kumezibwa vizuri tu.

Kwe pembeni, ndio nikaona kitu kama mfuniko wa mitaro ya maji machafu, nikauvuta , uakfunguka, na ndipo nikaona uwazi..kwenye ule uwazi kuna ngazi,…za kulekea chini,  kwa haraka nikazifuata hizo ngazi, nikafika sehemu, kuna uwazi kama pango, lakini limejengewa vizuri, kuna taa zinaning’inia juu na kuweka mwanga wa kutosha tu,…lilikuwa pango kubwa, linaloeenda mbele,..nikataka kutembea kuelekea mbele,..hisia ikaniambia niangalie pembeni, nika kitu kama kuna utofauti,..nikagusa mara ule ukuta ukasogea taratibu na kucha uwazi.

Nikaingia kwenye huo uwazi, na kujikuta sehemu imejengwa kama chumba, ni chumba  kizuri tu,..kuna sehemu nyingine, nahisi ni chumba cha ndani zaidi,...nikasogeza mlango wake taratibu na nikamuona jamaa..…

Sikuwa na muda wa kuchunguza zaidi,..nikasogea kwa ndani..nikajificha kwenye sehemu iliyochongwa kama kabati…nikawa sasa namuona jamaa kwa vizuri zaidi, nahisi hakutarajia kuwa kuna mtu anaweza kuingia humo,..jamaa alikuwa kasimama akifanya kitu kwenye meza, mara, akavua zile nguo alizokuwa kazivaa.

Mimi kwa haraka nikatoa simu yangu na kuanza kumpiga video,…ni hisia zilinijia tu, kuwa nifanye hivyo,………alipomaliza kuvua nguo alizokuwa nazo, mara akaanza kujibandua ngozi aliyokuwa kavaa sehemu ya usoni,....

Alipomaliza akainua mkono kwapani akabandua ngozi tena na humo akatoa, kitu…nikakumbuka maelezo ya docta, mtu huyo ana ufunguo wa ajabu, anaficha sehemu ambayo hatuijui..kumbe alikuwa kaiweka ndani ya ngozi mwilini mwake, sehemu ya kwapani, akatoa kitu kipo kama ‘external drive’ ..aliitoa, na kuiweka kwenye kiboksi…akasema;

‘Sina muda, huu ufunguo, ..ooh, ngoja kwanza, saa zimeenda sana…’akawa anaongea peke yake…akiwa sasa hana nguo zaidi ya chupi, …

 Mimi nikaendelea kuchukua video…sasa akawa anazikunja zile ngozi alizokuwa kava, na kuziweka ndani ya boksi…alipomaliza, akasogea kwenye ukuta,.akasogeza kumbe ni kabati, lipo ukutani, akatoa, kiboksi, ..mle kwenye kiboksi, akatoa bastola, na kuiweka juu ya meza..

‘Hii naihitajia sana..’akasema sasa akiijaza ile bastola risasi zake..

Nikakumbuka ile bastola,…aliyomnyang’anya mke wa mzee, itakuwa ni ile bastola,..nikaikumbuka vyema, nikakumbuka alivyojitamba, kuwa akiipata hiyo bastola basi atakuwa yeye ni mtu wa kipekee mweny nguvu sana, kwahiyo hiyo bastola, ni muhimu ichukuliwe,,..alikuwa kaiweka mezani kwa muda huo..

Sasa, akaelekea kwenye kabati, akatoa suti,…wakati anafanya hayo yote alikuwa kageuka kunipa mimi mgongo, sasa akageuka, kutaka kuchukua kitu kingine..nikainama kujificha, na baadae nikasimama tena, kumuangalia, sasa hivi alikuwa kasimama kiupande, naweza kuiona sura yake, sasa hivi sio yule mtu aliyeingia humo ndani, ni mtu tofauti kabisa…

Sikuweza kumtambua vyema huyu mtu ni nani, kwa haraka, lakini baadae  ..nikakumbuka,..hii sura niliiona wapi kabla,…

‘Ina maana ndio huyu…ndio yeye, haiwezekani…’nikasema hivyo tu.

Huyo jamaa akachukua beseni akiwa kajaza maji, akachukua na taulo, akalilowanisha, na kuanza kujifuta futa mwilini…anaoga kwa kutumia taulo, mpaka akahakikisha yupo safi, alipomaliza, akachukua marashi akajipulizia, halafu, akasogea kwenye suti yake, akachukua fulani za ndani,akaivaa,…nahisi ni fulana maalumu, labda ya kujikinga na risasi,…akawa sasa anaivaa hiyo fulana.

‘Unapovaa fulani si unapitishia kichwa, unakuwa umejifunika kichwani, nikaona hiyo ndio nafasi ya kufanya nilichokifuata,..ni hisia, zilinituma hivyo, nikasogea kwa haraka ..nikitembelea vidole, na kuwahi pale mezani , nikachukua ile bastola, na ule ufunguo..

Nahisi alihisi kuna kitu..alitulia, na wakatii huo ndio fulani imeshapita ipo shindoni kaishikilia na mkono ili kutumbukiza mikono …mimi hapo hapo, kwa kutumia kitako cha ile bastola, nikamgonga kwenye kichwa na hiyo bastola yake, akadondoka sakafuni,…

‘Vichukue hivyo vitu kwa haraka, usipoteze muda, ni muhimu sana kwenye kesi yenu na maisha yenu ya baadae, na mpenzi wako wa facebook..

‘Na mpenzi wangu wa facebook…?’ nikajiuliza akilini.

‘Ndio,…muda wenu wa kukutana naye umefika, lakini muhimu sana utoke humo ndani, hakikisha umemfunga huyo mtu kwa kamba, kwenye kona ya hiyo nyumba, asije kutoroka…’nikaambiwa hivyo, na kwa haraka nikachukua kamba na kuanza kumunga mikononi na miguuni,..

‘Hakikisha unachukua vitu vyote vya mawasiliano…’nikaambiwa hivyo, nikachukua nguo zake, na kutafuta kama kuna simu..nikaona simu, nikaichukua, nikamburuza hadi ukutani nikamfungia kwenye ukuta, kiasi kwamba hawezi kujisogeza, ..


 ‘Nikahakikisha kuwa hivyo vitu ninavyo,..nikageuka na kufunga hicho chumba, nikatoka nje,..wakati nataka kutoka, nikasikia sehemu fulani kama kuna ukelele wa mtu au watu wakiomba msaada.

‘Hiyo sio kazi yako kwasasa, muhimu hakikisha umetoka na hivyo vitu, na uvifikishe kwa docta, haraka iwezekanavyo…’nikaambiwa, na mimi nikatoka mle kwenye kaburi, kwa haraka nikaja huku, nilipofika huku ndio nikaambiwa nimsubiri adocta humu ndani ya gari hili, sasa badala ya docta umekuja wewe…’nikamwambia.

‘Mimi ni wakili mtetezi,…nimetokea kwenye kesi , natakiwa kuwahi sehemu nyingine,..mimi sio mtu mbaya kama unavyosema, najiuliza ni kwanini uingie kwenye gari langu, kwanini usiingie kwenye gari la docta..’akasema.

‘Mimi sina lolote dhidi yako ukinitimizia matakwa yangu, nimeambiwa wewe ndiye utaweza kunisaidia,…’nikamwambia.

 ‘Kukusaidia jambo gani?’ akauliza.

‘Nataka nikutane na mpenzi wa facebook , nasikia wewe ndiye umemficha..?’ akaulizwa na hapo akatulia kidogo, halafu akacheka..

‘Mimi, hahahaha, kumbe ni huyo, sasa sikiliza kumbe hoja yako ni kumpata mpenzi wa facebook, mbona hao wapo wengi tu, kuna sehemu nitakupeleka utkwenda kuchagua umtakaye…’akasema.

‘Mimi na wewe hatuwezi kutoka hapa kwa pamoja hadi huko, kwanza nataka kukabidhi hivi vitu kwa muhusika, halafu unielekeze, ukinielekeza mimi nitatoka, na wewe utaendelea na shughuli zako…’nikamwambia.

‘Sikiliza …mimi nataka tufanya dili,…….’akasema

‘Dili gani..?’ nikamuuliza, na mara nikasikia ujume ukiingia kwenye simu yangu, nikaitizama kwa haraka, nikijua nipo kwenye mtu nisiyejua ujasiri wake, anaweza kunibadilikia humo ndani, lakini kwa jinsi gani, maana  yeye kakaa kiti cha dereva, mimi nipo nyuma yake.

‘Nipo nje ya gari, kwa nyuma,…hakikisha anakuambia wapi alipo huyo binti, maana muda unakwenda..’ulikuwa ujumbe wa docta.

 ‘Sikiliza mimi nitakusaidia, hadi huko alipo huyo, wapo wengi, ni wewe tu uchaguzi wako, lakini kwanza ningelitaka uniuzie hiyo bastola, na ufunguo huo, nitakupia pesa nyingi tu…’akasema.

‘Mimi sipo kwa ajili ya biashara hapa, nataka uniambie wapi alipo huyo mpenzi wa facebook, ….unajua ni nani, kati ya hao,…ukinielekeza huko nitaenda mimi mwenyewe au kuna mtu wangu nitamtuma, …halafu wewe nakuachia unaondoka zako..’nikamwambia

‘Kwanini usikubali ombi langu, nitakupa pesa nyingi tu…na nitaweza kuingia nawe kwenye mipango mingi ya maendeleo…’akasema

‘Sikiliza …uamuzi ni wako, nikutoe nje ukakutane na hao watu wa usalama au unielekeze alippo huyo binti, tumalizane mimi na wewe, tusipotezeane muda..’nikamwambia sasa kwa ukali.

‘Nitakuwa na uhakika gani, kuwa utaniruhusi mimi niondoke, najua baada ya hapa nitakuja kukamatwa…’akasema.

‘Hivi una uchaguzi kwa hili, kuwa unataka…..niambie muda umekwisha..’nikasema kwa ukali nikiwa na mgonga gongwa kwa nyuma na ile bastola.
‘Huyo binti yupo….karibu na makaburini, ndani ya pango hilo hilo uliloingia, unatembea hatua chache kuingia ndani ya hilo pango kuna sehemu, unakuwa kama, pamechimbwa sana,..kama kuna upanuzi …ukutani, utaona ..tofati…’akasema

‘Unafunguaje…?’nikamuuliza

‘Unatumia huo ufunguo…tunaweza kwenda pamoja ukanielekeza…’akasema

‘Hapana hebu subiria nihakikishe uwongo wako…’nikasema na kutuma ujumbe kumuelekeza docta, na baadae docta akasema niendelee kupoteza muda ili wahakikishe kuwa ni penyewe au anadanganya..

 ‘Kwahiyo wewe ni nani wao kwenye hilo kundi…?’nikamuuliza

‘Kundi gani..?’ nikamuuliza.

‘Hahaha, hivi unafikiria mimi sikufahamu,nakufahamu sana,…wewe kama huyo bosi wenu mnafanya vitu vya kufanana, ukitoka mahakamani wewe ni wakili, ukifika sehemu nyingine wewe ni mtu mwingine…’nikamwambia.

‘Nimefanya ulichotaka nikuambie, naweza kuondoka, au kama unataka twende wote huko ili ukamuona vyema huyo mpenzi wa facebook….’akasema

‘Nimeshakuambia mpaka tuhakikishe kuwa ulichonielekeza ni sahihi…akipatikana huyo binti nakuachia uondoke zako…’nikamwambia.

‘Sawa..lakini ukumbuke ahadi ni deni…’akasema.

‘Hilo usijali,…’nikasema na mara …ilikuwa ni kama radi au kitu gani, nilihisi uso wangu ukimwagikiwa na …damu,…ooh,..na kiyoo cha gari, kikatawanyika..na nikasikia nje mtu akisema.

‘Imetokea wapi…?’, na mara docta akaja, na kuniambia

‘Nipe hivyo vitu kwa haraka…na utoke humu ndani, …’akasema na wakati namkabidhi mara nikawaona askari wawili wakiwa na silaha wakija pale tulipo, na docta akasema;

‘Inama chini kwa haraka…’ na ilikuwa kama bahati, risasii zilimiminwa kwenye gari, na docta alikuwa kainama alipoinuka akaanza kukimbilia, ndani ya jengo la mahakama, na mimi nikawa sasa nataka kuondoka, mara mtu akaja nyuma yangu.

‘Ukisogea hatua moja umekufa…’sauti ikasema na mara mtu mmoja kwa nyuma akaja kunikagua, na akasema

‘Haipo..hanayo….tumfanyaje…na mara nikaona askari wakija kutokea ndani…na na sauti ikasema;

‘Muue…mara moja…’akasema

NB:Naona tuishie hapa kwa leo


WAZO LA LEO: Kusengenya imekuwa ni jambo la kawaida tu, watu wakikaa wawili au zaidi kwenye mazungumzo yao, hakuishi kuwemo utesi,..watu kuteta wengine ni kawaida, hatujui kuwa hayo ni madhambi makubwa. Tuchunge sana ndimi zetu na kuteta wengine, kusengenya kumelinganishwa na mtu kumla mwenzake nyama yake. Tumuombe mola wetu atusamehe na dhambi hizi za kusengenya, na kwenye mwezi huu mtukufu toba ni muhimu sana.
Ni mimi: emu-three

No comments :