Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, May 26, 2017

MPENZI WA FACEBOOK-36



Docta aliyakuwa akishuhudia hayo yote, akajua keshampoteza mpelelezi, alijilaumu kwanini hakumtahdharisha kuhusu huyo mtu , na ilitakiwa ahakikishe kuwa silaha, hiyo ipo mbali na huyo mtu, kama mpelelezi angelikuwa na utashi wake mwenyewe angelijua jinsi gani ya kufanya, lakini kwa hali ile, mmh…akajiona kafanya kosa na anahitajika kuwajibika kwa hilo…, kwa haraka akawapigia simu askar waliokuwepo humo, ili waingie ndani waone kama wataweza kumuokoa huyo mtu.

‘Mpelelezi ni mtu muhimu sana…’akajisemea.

Na wakati anafanya hivyo, mara mitambo ikagoma, kukawa na ujumbe kuwa kuna mtafaruku wa mitambo…muingiliano wa mitambo, na sasa imefanya mtandao mzima kushindwa kuendelea.

Alimpigia jamaa yake, na jamaa yake akasema, inahitajia muda wa kusubiria, na kama hao jamaa wameshaanza ‘ku-reboot,’…basi muhimu ni kuhakikisha hawawezi kuendelea kabla mtandao huo haujaanza tena kufanya kazi.

‘Lakini…mtandao wao umeshazimwa…haupo hewani tena…’akasema docta akiongea na huyo jamaa

‘Umezimwa ndio,… lakini bado wana vifaa vinavyoweza kutumika sehemu nyingine, wana simu zenye huo mtandao, wanaweza wakawa na visaidizi vya nje vya komputa, (external drive)....na mbaya zaidi ni kama wana ‘kifungio’ cha huo mtandao…’akaambiwa, na docta hakutaka kumuambia kuhusu hiyo ‘key’ aliyo nayo huyo kiongozi wao.

‘Oh, sasa nifanyeje mpaka sasa, kama vile virusi vilishindwa kuharibu kila kitu..?’ akauliza

‘Subiri, na mimi nione kama kuna njia mbadala..’akaambiwa, na kwa muda huo ndio akawasiliana na mkuu kuona kama wanaweza kwenda kumuokoa mpelelezi, kama bado yupo hai.

‘Mkuu fanya juhudi , kadri uwezavyo, ukamuokoe mpelelezi, ….’akasema docta.

 'Tatizo kama tulivyopanga awali, watu wakiingia huko ndani kwa wakati huu, wataleta vurumai, ukumbuke jengo hilo ni kubwa,…na lina ofisi nyingi,..kuacha hiyo ofisi yao wanayotumia kwa biashara zao na mambo yao, na sisi tunataka tufanye kazi bila kuingilia makazi ya watu wengine,…na nia hasa ni kuhakikisha ushahidi wote unapatikana....'akasema mkuu huyo msaidizi.

 'Mpelelezi anahitajia huduma ya haraka,… sijui kama mtamkuta akiwa hai,..tatizo mtambo umezima siwezi kumuona tena..'akasema docta.

 'Ngoja tuone la kufanya, maana hata yule kiongozi wao katutoroka, sijui hawa maaskari wana nini, niliwaambia kabisa wahakikishe huyo mtu hawatoki..na nasikio alikuwa na silaha iliyokuwa inapiga risasi nyingi, risasi..zinakuwa kama zinamuandama mtu aliyelengwa.siwaamini…’akasema

‘Oh, kumbe ameshaipata hiyo silaha, sasa hilo ni balaa…’akasema docta.

‘Silaha gani…?’ akauliza mkuu

‘Na unajua hata msaidizi wako kapoteza fahamu, na hao mabinti halikadhalika…na hata mama yao, tulijua huyo mama amekufa, kumbe bado yupo hai amekuwa kama kachanganyikiwa…na vyema alipopoteza fahamu, na mmbo hayo yametokea kwa mara moja,…imekuwa ni ghafla sana kwetu…’akasema

 'Hilo nalifahamu sana..ni katika hali ya kuwarejeshea kumbukumbu zao, nilishaondoa uchafu waliopandikiziwa, uchafu ule ulikuwa kama mzigo mwilini mwao, na ulipoonadoka, ni lazima wadondoke, na kupoteza fahamu, na kilichokuwa kimebakia ni kuwarejeshea kumbukumbu zao na utashi wao wa kawaida, ....’akasema docta.

'Kwahiyo huwezi kuwaona kabisa….?’ Akauliza mkuu.

'Nakuambia mtambo mzima umegoma…nahisi yule mtu wao alipofyatua ile bastola, akitaka kumuua mpelelezi, risasi iligusa ile komputa kubwa inayoongoza huo mtambo…au pia ni kutokana na muingiliano wakati wanataka kurejesha mawasiliano yao, na wakati huo, mimi nautumia..umona hapo..ni shiida..’akasema docta.

'Sasa tutafanyaje…?’ akauliza mkuu, alionekana kuongea na watu wengine kabla hajasikilizana na docta.

'Muhimu ten asana ni kupata huo ufunguo wa ajabu….na hiyo bastola…hivyo ni vitu hatari sana vikiangukia mikononi mwa hao watu…’akasema docta

‘Bastola…una maana hiyo bastola, iliyokuwa inatoa risasi kiajabu…’akauliza

‘Hiyo ni hatari sana, inatafutwa sana….na muhimu ipatikane, vinginevyo,..nyote nyie mtauliwa….’akasema docta

‘Ok…askari wamesambaa eneo lote hawezi kutoka humo…’akasema huyo mkuu.

'Je hao askari huko n- nje,....unawaamini, sawa sawa…?’ akaulizwa

'Sina shaka na hilo…wapo vijana wangu hawababaishwi na pesa, wanajua ni nini wanachokifanya…..’akasema huyo mkuu.

'Nina mashaka kuwa huyo kiongozi anaweza kutoka nje na asijulikane kuwa ni yeye

'Kwanini….?’ Akauliza docta

'Ujanja wao wa kujibadili sura….wanavyaa ngozi,…kama ulivyoona ile ya huyo kiongozi, nina mashaka, bado ana ngozi nyingine mwilini,…huyo jamaa ni hatari sana , mwenyewe anajiita shetani wa kibinadamu,.., ‘akatulia.

‘Sasa muhimu cha kufanya kama hatujachelewa, hakikisheni hakuna mtu yoyote, wa jinsia yoyote, ambaye ataruhusiwa nje mtu yoyote, bila wewe kumtambua..na huko uwanja wa ndege, …nilikuambia hilo, wahakikishe kuona ni nani na nani kaingia leo,….’akasema docta.

‘Ok, hilo nimeshawatuma vijana wangu…hakuna mtu yoyote kiongozi au watu wetu waliokuja na ndege leo mpaka muda huu….’akasema mkuu.

‘Safi kabisa……tutaona uwaongo wao….’akasema docta.

‘Mimi hapo sijakuelewa….’akasema mkuu.

‘Utakuja kuelewa baadae…’akasema docta..

‘Mimi bado najaribu kuwasiliana na jamaa yangu wa huko ulaya, tuona kama nitaweza kuwaokoa hawa watu…’akasema kwani mtu wake wa huko nje alianza kumpigia..lakini siku ikakatika.

'Kuwaokoa una maana gani tena, si umesema umeshaondoa uchafu waliokuwa wamepandikiziwa hao watu au sio…?’ akaulizwa

'Hawa watu ni mashetani, waliweza kuwawekeza hao watu walio wataka kwenye mitandao yao,…inakuwa kama unavyowekeza jambo kwenye komputa,..hii ni kitu kigeni sana..hakielezeki…, katika moja  ya majaribio yangu, na tafiti zangu, ilikuwa hiyo..kuona kama kweli jambo kama hilo linawezekanaje…, je yawezekana nguvu za giza ukaweza kuziingiza kwenye mitandao…sasa hawa jamaa wamejaribu,….’akasema docta

'Nakumbuka uliwahi kuniambia kitu kama hicho mimi mpaka sasa siwezi kukubaliana na hilo,haiwezi kuingia akilini,..na hayo ya imani za giza, utayawekaje kisheria,…ndio maana mimi nahangaikia kupata ushahidi unaoshikika, sio mambo hayo ya kiimani imani tu…’akasema mkuu.


'Unajua mkuu siku zote nilikuwa nawatafuta hawa watu, hata nikiwa huko mikoani, nilijua naweza kujifunza kitu kwao, lakini nimegundua kuwa hao sio watu, ni mashetani, nilijua wana kitivo cha wataalamu, wanaofanyia kazi hiyo uchunguzi, kama kweli nguvu za giza unaweza kuziingiza kwenye mtandao ni kweli wana wataalamu humo wanaojua komputa vizuri,…lakin mtu wao, huyo hana jema, zaidi anataka kuiangamiza dunia…..

'Lakini ni watu gani hao…inaonekana kama unawafahamu kabla,.. ni huyo huyo…kiongozi wao, na huyo mtaalamu na hao tuliowakamata, na huyo kiongozi wao ni nani hasa, ..mwanzoni nilimuona,…anafanana kama..eeh, hebu subiri…’akasema alikuwa akiwasiliana na watu wake. Akawa anatoa maagizo na baadae akaendelea na docta;

‘Oh, …docta, wamefanikiwa kuingia ndani…’akasema mara tena akawa anawasiliana na watu wake..

‘Ok, ok….sasa..hakikisha wote wanakamatwa, na mchukueni mpelelezi kwa haraka afikishwe hospitalini…unasema bado yupo hai…’akatulia.

‘Oh….ok, mbebeni hivyo hivyo…fanyeni haraka, na huyo mtu wao ambaye alikuwa humo, yeye ndio bingwa wao,…mnasema nini, .. hamjampata?? ,…haonekanani kwanini,… katokea wapi…mtafuteni haraka,….’akasema.

‘Nani, Binti??!….ok….nani kasema alikuwepo binti…wapo wengi, na..huyo ni nani, ..binti, ….? Sasa kaenda wapi,…alikuwa kwenye chumba peke yake, ni nani huyo…kwahiyo, …hayupo, kaenda wapi…mtafuteni sasa, …..hao wafungeni wote haraka …’kwa vile huyo mkuu alikuwa hajazima simu akiwasiliana na docta,  docta alikuwa akisikializa jinsi amri zinavyotolewa huko upande wa pili.

Baadae mkuu akarudi hewani kwa docta, sasa akawa ndio …akauliza;

‘Kuna binti wanasema alikuwa kwenye chumba chake peke yake, …wengine walikuwa sehemu tofauti, ..najiuliza tena na tena, hawa mabinti wa nini, na kwanini walikuwa wamefungiwa huko ndani..na hawajulikani ni mabinti wa watu gani,…je unaweza kufahamu walikuwa humo kwa kazi gani, maana ni warembo kweli…?’

‘Hahaha…hao ndio chambo kwenye mitandao….wanatumika kuwateka watu…kama nilivyokuambia awali, picha ya mrembo kama huyo ikiwekwa kwenye mtando, kimvuto, mtu atavutika nayo,..na kwa jinsi atakavyomuangalia kwa matamanio, basi akili yake hutekwa na hao mashetani…ni ujanja ujanja fulani wa kuteka akili za watu, na hao watu wanakuwa watumwa wa shetani…’akasema docta

‘Hata sielewi…’akasema mkuu

‘Unasemaje kuhusu huyo kiongozi wao tuliyempata,..japokuwa katutoroka…, nina uhakika tutamkamata tu….’akasema huyo mkuu.

‘Ni mpaka mumkamate…huyo sio mara ya kwanza kuingia humu nchini..alishawahi kuja akafanya mambo ya kutisha, baadae akatoweka hivyo hivyo…na nahsi ndio huyo huyo,karudi tena…’akasema docta

' Inavyoonekana, huyo wanayemuita kwa jina la mkuu, sio huyo kiongozi tuliyempata hapo kwa hivi sasa au sio,.?’ Akauliza mkuu.

‘Sina uhakika na hilo, yawezekana akawa ndio huyo au mtu mwingine kapewa hiyo kazi, kwa kutumiwa, ndio maana anajibadili sura..’akasema docta.

‘Kwa maana hiyo,….huyo mkuu yupo mahali, hatujaweza kumpata…?’ akauliza na docta akasema;.

‘Vyovyote iwavyo,  bado kuna mtu mwingine nyuma ya pazia, huyu kiongozi inawezekana kweli akawa  anatumika tu,…unajua hawa watu ni wajanja sana, kiongozi wao analindwa na kufichwa sana, kama mchwa au nyuki wanavyomlinda malikia, ….’akasema docta.

‘Tutampata tu…hata afichwe vipi…’akasema mkuu.

‘Kwa kutumia nguvu zenu, itachukua muda, mnaweza kuwakamata watu wengine kabisa na huyo mtu akatoweka tena,…sina uhakika kama ndio huyo …inahitajia muda kumgundua, lakini ngoja tuone..mtandao utasema….’akasema docta.

‘Je mpelelezi hawezi kutusaidia kwa hili…naona kama alishaweza kuingia kwenye anga zao…sijui kwanini hakupenda kunielezea jambo hili mapema…’akasema mkuu.

‘Sababu ndio hizo, …walishaiweka familia yake reheni…na kwasasa mpelelezi hawezi kutusaidia kitu, kupona kwake kutachukua muda…kama bado yupo hai…’akasema docta.

‘Mhh…kwahiyo una maana kuwa ni kweli  mpelelezi alishaingizwa ndani ya kundi hili, kwa lazima fulani, sio kwa hiari, na…nimeshaanza kukuelewa, lakini kwanini wamchukue yeye, kwanini…na kwanini mkuu wangu wa kituo, hakutaka kuniweka wazi kuhusu hili, nahisi hapa kuna jambo, unasemaje docta..?’ akauliza

‘Ndio hivyo,…mpelelezi takuwa kashindikizwa kwa kupitia familia yake,…na huyo binti yake alitakiwa sana…wana maana yao, kiukweli huyo binti kaponea tundu la sindano…na vipi hali yake, anaendeleaje maana siwaoni tena huko…?’ akauliza docta.

‘Huyo binti hajaweza kuongea mpaka sasa hivi…kapagawa, yaani ukimuona ni kama zezeta fulani hivi, katoa macho tu.….hajijui…’akasema mkuu.

‘Unajua na yeye pia ni miongoni mwa watu waliologezewa, kulogezewa hapa nina maana , watu hao walipandikiziwa ushetani fulani kichwa ni mwao..lakini yeye, baadae waliyatoa,…waliona yeye, sio lengo la makafara yao, ila baadae walipokosa mtu, wakaona hata yeye anafaa, anaweza kutumika vile vile.., kwa masharti yao…kwanza ana damu ya hizo familia japo kwa mbali, pili binti huyo bado ni mbichi, kwa mambo yao ya kishetani,…’ docta akakatizwa .

‘Ana damu yao kwa vipi..?’ akauliza lakini kabla docta hajajibu mara huyo mkuu akasema;

‘Docta,…. mpelelezi keshatolewa, katapaa damu, docta anasema ni mpaka wafike hospitalini waone kama wanaweza kumuokoa,  hivi sasa  anapelekwa hospitalini, kapoteza fahamu…’akasema huyo mkuu.

‘Ina maana ile risasi imempata sehemu gani…?’ akauliza docta.

‘Docta anasema imepitia sehemu ya tumbo, ..humo imekwaruza, lakini sehemu ya kwapani…ndio kuna tatizo,  maana wanasema risasi moja imetoboa meza, na kuharibu kabisa keyboard ya komputa, na nyingine ndio iliyompata mpelelezi..…, ngoja afikishwe huko hospitalini , tutajua kama ni mtu wa kupona au ndio basi tena…’akasema mkuu.

‘Oh,…sijui tufanyeje,…maana kama watawahi kurejesha mambo yao, kabla mimi sijaweza kuingia huko, inaweza kuwa balaa kwa hawa watu, hao watu wanaweza wakawa na matatizo ya akili, maisha yao yote….hata sijui itakuwaje…’akasema docta.

‘Jitahidi docta, hilo lipo mikononi mwako..na mungu atakusaidia…’akasema mkuu.

‘Ni kweli, …lakini kwa hivi sasa, siwezi kusema lolote, nashindwa hata kuamini, muda umepita sana, na huyu jamaa anapiga simu, kila nikipokea inakata…kuna tatizo mahali…ngoja nitoke humu ofisini..’akasema docta.

‘Docta usiondoke humo….hiyo amri ya polisi…’akasema mkuu huyo.

‘Hahaha, sasa hivi sifuati amri yoyote, nafuata amri ya mungu peke yake, nikiwafuata nyie, hawa watu, msaidizi wangu, wale mabinti, mama yao… watakuwa kwenye hatari kubwa, na mwisho wa siku nitakuja kulaumiwa mimi, kwani huko mumefikia wapi…?’ akauliza

‘Mhh..,hata siamini eti wanasema huyo jamaa katoweka kama alivyotoweka huyo kiongozi wao, hawajui alipitia wapi… na wanahisi kuna sehemu wamejificha, ssasa kajificha wapi, ndio haijulikani, wametafuta kila sehemu hakuna mtu kama huyo,….na mawasiliano ya kunasa matukio humo ndani ilishazimwa,..’akasema.

‘Najua atakachokifanya…’akasema docta

‘Kuwa hata yeye alikuwa akitumia sura bandia…’akasema mkuu

‘Ahaahaha…, ndivo hivyo, wameona ndio njia rahisi ya kuficha maovu yao, lakini hiyo ni danganya toto,…wewe subiria mtandao ufanye kazi yake, ninachoombea kwa sasa ni wawili hao, wasikutane kwa sasa…’akasema.

‘Kiongozi na huyu mtaalamu wao…?’

‘Ndio, hao pia, lakini nazungumzia hawa wapenzi wawili,…mkuu endelea na kazi,…..hakikisha njia zote zimezuiliwa …uwe makini kwani kuna njia za chini kwa chini, …zilijifunga muda ule,..kabla mtandao haujajifunga, sasa sijui kwa hivi sasa na kwa vile huyo jamaa ana huo ufungua wa ajabu, anaweza kufungua na kupita…’akasema docta.

‘Mtandao bado…?’ akauliza mkuu.
‘Oh…mbona hivi….ngoja hebu suria niongee na huyu mtu wangu kwanza, naona kama mambo yanazidi kuharibika,…’akasema docta, na mkuu akawa naye anaongea na watu wake.

*************
Docta na mkuu walipopigiana simu tena, mkuu akawa na maswali kwa docta, akauliza;

‘Hebu niambie, kuhusu hiyo silaha, maana imekuwa ni gumzo kwa askari wangu, hiyo silaha imatokea wapi..?’ akauliza mkuu.

‘Historia yake ni ndefu kidogo, ..silaha hiyo, kiatu, vilikuwa ni vifaa vya watawala wa enzi hizo, huko uzunguni, lakini inasadikiwa kuwa silaha hiyo iliundwa huku kwetu, na ikapelekwa huko, kipindi mtawala wa enzi hizo, aliporotoka,….na kwenda kuishi huko ughaibuni.

‘Kwanini alitoroka..?’ akauliza mkuu.

‘Alitaka kuimiliki hiyo silaha na kiatu ,na alitaka akajiimarishe huko akirudi, anakuja kutwaa madaraka, na kutawala sehemu kubwa ya nchi, lakini haikutokea hivyo, akapatwa na umauti akiwa huko, na vitu hivyo vikabakia kwa jemedari mmoja wa vita..

Jemedari huyo, akawa anavimiliki hivyo vitu, lakini hakujua undani wake, akawa anavitumia tu…lakini vikaanza kumletea madhara,… na alipoona anataka kufa, akaacha urithi kwa familia yake kuwa vifaa hivyo vitafutiwe namna ya kuviondoa kwenye familia yao…akawaarifu kuwa vifaa hivyo ni janga kwenye familia hiyo..

‘Kijana wake,..msomi, sasa… alikuwa kiongozi fulani wa kijeshi, kijana huyo hakupendelea mambo hayo ya urithi nk…akataka kuhakikisha mambo hayo ya kizamani yote anayaondoa kwenye hiyo familia,..na enzi hiyo ndio, ambayo, mzee alikwenda huko kwenye mafunzo, na kushiriki kwenye jeshi la umoja wa mataifa.

Mzee akiwa jeshini alikuwa kweli bingwa wa silaha, shabaha, na mtaalamu wa kuunda zana za kivita kwa haraka sana… Wenzetu wazungu walimpenda sana, kuna kipindi mzee aliweza kushirikiana na hao wazungu, nia yao wao ni kuiba ujuzi wake.

 Mzee hakupenda kuajiriwa huko ulaya, kama angelikubali tu angelikuwa mtu mwingine kwa hivi sasa.., unajua tena mambo ya zamani, wazee wake walimkatalia kabisa kufanya kazi huko. …

‘Mimi sijaelewa, kwanini..ok...., umesema alipewa viatu na bunduki kama zawadi, sasa inaingiliaje kwenye matatizo yote haya…’akauliza mkuu.

 ‘Labda nianzia hivi,…kuvipata hivyo viatu, na bunduki, sio jambo la bahati …ilipangwa kuwa atakuja mtu,,,,mtu hayo atafnya jambo kubwa sana,.. yalisemwa na huyo aliyeviacha hivyo vitu, alikuwa na karama fulani za utabiri wa baadae.. akawaelezea familia yake hivyo lakini hakuna aliyetilia maanani, lakini lililopangwa litokee , litatokea tu, …maana kama nilivyosema awali, vitu hivyo asili yake ni afrika..unaonaeeh…’akasema

‘Wanavyodai, mizumu ya afrika ilivihitajia vifaa hivyo virejeshwe huku, hapo hakuna mungu wanachojua wao ni mizimu, huku afrika, ilitokea muda familia hiyo inayohitajia hivyo vitu ikapatwa na matatizo, ikaambiwa kuna vitu vinahitajiaka virejeshwe, familia hii haikujua, na ikapuuza, maisha yakaenda mbele..…ni mambo ya imani wanajua wazee wetu zaidi...’akasema docta

‘Sasa ukichunguza familia ya mke wa huyu mzee wetu huku…, ukarudi kinyume nyume, utakutana na hiyo familia, vifaa hivyo vilivyotokea,…familia ya mke wa mzee, huko nyuma ilikuwa ya machifu, viongozi watawala..na utawala wao ulikuwa wa nguvu sana, na mambo ya giza giza, si unajua mambo ya kizamani…’ akatulia docta.

'Lakini kuna mgongani kati ya familia mbili,..rejea maelezo yangu, kuna huyo alitoroka na vitu hivyo akaenda huko nje, na kuna familia ilibakia hapa, ambayo ndio ya mke wa mzee, na familia hiyo nyingine ina uhusiano na huyo aliyetoroka na hivyo vitu, ambayo lidai kuwa ndiyo ilitakiwa iwe watawala enzi hizo..kizazi kikazaa chuki hizo, ..na chuki hizo, za tamaa, sisi ni sisi zimeendelea hadi leo....

'Eneo alilonunua mzee..lilikuwa mali ya familia hizi..lilikuwa kubwa tu, lakini likaja kugawiwa baadae utawala ulivyobadilika kutoka wa kikabila na hadi kuwa wa kitaifa,..lakini hulka na tabia bado zipo, kizalia, cha hapa kwangu , hapa kwetu bado zipo..eneo lilobakia lilikuwa na mgogoro mkuba huko nyuma...lakini haya yapo chini kwa chini...

'Sasa basi...kuna huyu mtu alitoweka, alikwenda wapi....swalii hilo jibu lake ukilipata unaweza kuhitimisha hii kesi, na mengine yote yanazunguka, mbinu zinatafutwa, kiini chake kimejificha,...hulka, tabia, vizalia, vinazua mambo, ..ajenda imejificha, na sio rahisi , hata kwa hao wanaohangaika kujua sababu ilikuwa ni nini hasa, shetani anachochea tu......sasa ukiwaelezea watu hayo yote, wanakuja kukuuliza kwa ushahidi gani, na huyu mtu ni nani, mbona havieleweki.....ushahidi ni hivyo vifaa...ni nani sasa..ndio tunamtafuta...tukimaliza hili kesi imekwisha, ....'akasema docta

'Mhh...'akaguna hivyo tu mkuu, aliona ni mambo mengi juu ya mambo ambayo hayawezi kumsaidia kitu.

'Sasa niakuambie kitu...kuna kitu kilikuaj kugunduliwa baadae..na mzawa mmoja,...wa huyo mtu aliyekimbilia huko,...ufunguo wa mitandao...huyu mtu alikuwa na miujiza yake...akawaweza kugundua mambo mengi tu...ila alikuwa mbinafsi..yaani hapendi mambo yake yajulikane, na watu wengine akafanya mambo yake na mashetani, hadi akapata ufunguo...ni asili fulani huwezi kuijua, ufungua huo awali ulikuwa na namba tatu tu..sita sita sita...au tisa tisa tisa....

'Una maana gani....si ndio hayo wanazungumza watu...?' akauliza mkuu

'Hizo namba alizitumia huyo mtu kuwasiliana na mashetani wake..na alipokufa, ufunguo huo ukabakia kwenye hazina yake,..baadae watu wakagundua kuwa ufungua huo unaweza kutumiwa kwenye kitu chochote...ukitaka kufungua mtandoa,..milango...ukawa unatumika kuibia ..ulipoingia kwa watu wabaya..huu ukawa unatafutwa sana...

Swali ulifikaje kwa hawa watu huku...hilo mimi sijagundua....ila upo mikononi mwa huyu kiongozi, kama upo kwa huyu kiongozi aliupata wapi....hapoo ukiunganisha mambo unaweza ukapata jambo..lakini kwa ushahidi gani...huyu mtu ni muhimu sana, akipotea matatizo haya yatajirudia tena...'akasema docta.

'Ok, sawa....'mkuu akasema hivyo, aliona muda unakwisha na hajapata hicho anachokihitajia.

‘Swali ilikuwa je vitu hivyo ,vimewezaje kurejea kwenye hii familia...'akasema docta.

'Ama kwa viatu na bastola, hilo tumalipata..maana ,..kila kitu hutokea kwasababu fulani..kuna tukio lilitokea hadi vifaa hivyo vikafika mikononi mwa mzee, wakati huo ni kijana, mpiganaji, mtaalamu..lakini sio kwamba vilihitajika kuwa kwake,..hapana, kwake ilikuwa kama daraja tu…vilitakiwa vifike kwa familia ya hicho kizazi husika, na wakati huu, kizazi kilichobakia ni mke wa mzee, na ndugu hawa wengine, ambao hawajijui..na hata huyu mke wa mzee,..hajui hilo mpaka kwa undani wake,.sasa uone miujuza ya aina yake ilivyotokea.

‘Siku moja mzee huyu, tunatumia jina mzee, japokuwa kwa muda huo hakuwa mzee,…walikuwa kwenye doria, pamoja na mafunzo, walitakiwa kutumikia jeshi, kwahiyo walikuwa wametmwa kwenye kisiwa kimoja kulitokea maasi.

 Mzee, na mwenzake wakawa wanatembea maeneo hayo, hawakujua kuwa sehemu hiyo kulikuwa na njama za kumteka binti wa tajiri mmoja, ambaye pia ni kiongozi wa polisi wa huko..maharamia hao walimtaka huyo binti ili awe ni surti la kuachiwa wenzao.

Sasa wakati mzee na mwenzake wanatembea , wakiwa wawili tu,  …mara kukatokea maharamia hao, walikuwa maharamia kweli, wanateka wasichana, mabinti wadogo, wanazalilisha…

Binti wa huyo tajiri, kiongozi wa polisi, akiwa na gari , yeye na mama yake wakapita maeneo ambayo ilikuwa ni mtego wa hao maharamia,…wawili hawa wakawa wamsimama tu hawana habari, wakiangalia mandhari ya huko,…mara wakamuona binti, akitokea kwenye gari,…akienda kwenye eneo la miti, kuna bustani na maua,nia yake kuchuma maua,..

Wakati huyo binti anaelekea huko,  mijamaa iliyovaaa sura mbaya ikatokea, wawili wakamkamata huyo binti, wengine watano, wakavamia gari lao,..mama na watoto wengine wakawekwa chini ya ulinzi…

Mzee akawaona, ..muda huo walikuwa wawili tu yeye na mwenzake, japokuwa walikuwa na silaha, lakini kundi hilo lilikuwa ni la watu wengi wenye silaha….na kutokea kwao ilikuwa ni jambo la haraka sana na kumshika yule binti wakamuingiza kwenye gari, wakataka sasa kuondoka kwa kasi….mzee na mwenzako wanaliona hilo tendo, na wao wapo humo kwa ajili ya kulinda…

Yeye ni mtaalamu wa shabaha,….akaishika silaha yake, gari lile likawa sasa linataka kuondoka, lakini …wanawasubiria wale walimchukua binti..waje waingie, mzee yeye, akainua silaha yake, akalenga shaba kwa dereva, …hakumkosa..pega begani…wengine,…mmoja baada ya mwingine aliwalenga mabegani tu…kwa umabali ule ilihitajia shaba, na kulenga shemu hiyo hiyo tu…

Na mwenzake akawa anawasiliana na wenzo kikosini,…wanafika pale maharamia hao wote majeruhi…hawajiwezi….ni bahati tu. Bosi huyo wa polisi kusikia kazi waliyoifanya wawili hao, alifurahi sana…

Baadae ndio wakapewa kazi ya  kuhakikisha maharamia hao wote wamekamatwa, au kutokomezwa kabisa, na mzee akapewa jukumu hilo kama kiongozi wa kikosi hicho, na kweli kundi hilo likamalizwa na eneo hilo likawa na salama, na ndipo mzee akapewa zawadi hizo …

Taarifa zilikuja baadae ni kuwa mzee alipewa zawadi hizo kwasababu ya shabaha, hizo, sababu nyingine zilifichwa kiaina,,…ila ndio ikawa nafasi ya vifaa hivyo kurudi tena Afrika, na kwa wahusika, lakini hakuna aliyefahamu hilo kwenye hiyo familia…

Mke wa mzee, akaja kuambiwa kuhusu vifaa hivyo, na kaka yake wa kambo, kaka yake huyo walikulia pamoja, kama unavyojua familia zetu, watoto wa baba huyu wanaishi na baba huyu…ikatokea ndugu hawa wawili kuivana sana, mpaka ilifikiriwa vibaya, lakini wao walijenga urafiki huo kama ndugu tu.hakukuwa na mengine kama walivyovumisha watu wengine.

Huyu ndugu yake,… alikuja kupotea kimuijiza,..haijulikani wapi alikwenda, lakini akaja mtu mwingine wanafanana naye…akajifanya ndio ndugu ..sijui ilikuwa ni sababu gani, wengine wanahisi ni wapelelezi waliokuja kuvitafuta hivyo vifaa…maana huyo ndugu alikuwa na mambo yasiyojulikana huku kwetu, …kula vitu vizivyoliwa, na wengine wanasema walimsikia kuwa anakula hata nyama za watu, akaja kukamatwa na polisi.

Hata hivyo alitoroka polisi na kupotea kabisa….

Miaka ya baadae,..ndio tetesi zikazuka kuwa kumezuka kundi la kichwi, wanakula watu, wanafanya mambo ya ajabu,…kama unakumbuka eneo hili kulikuwa hakukaliki kipindi fulani, lakini watu hawafuatilii matukio, hawakujua kuwa yule yule aliyeondoka ..ndio huyo huyo alirudi na kuanzisha kitu kama hicho…na baadae walipozidiwa huyo jamaa tena akatoweka.

‘Unataka kusema nini, kuwa huyo jamaa ndio huyu kiongozi wao…?’ akauliza mkuu.

‘Sina uhakika…lakini kwa vipi huyu mtu awe anakuja, anakamatwa anatoroka, anapotea, anarudi tena…ni nani huyu …’akasema docta.

‘Sasa ni nani…?’ akauliza mkuu

‘Nitakumalizia historia hiyo baadae maana naona mitambo kama inataka kuanza, na sitaki kupoteza muda tena…’akasema docta.

‘Sawa…ngoja na mimi nimalizie hii kazi, naona vijana wangu wameingia ndani na nimepata taarifa kuwa kuna mapigano kidogo huko ndani ya hayo mapango waliyoyatengeneza…’akasema huyo mkuu.

‘Atakuwa huyo kiongozi wao, kama ana hiyo bastola, muwe makini sana…’akasema docta.

‘Sawa mimi mwenyewe  naelekea huko, kama utaweza kurejesha hiyo mitambo na kuwa hewani tena uniambie…’akasema huyo mkuu…na docta hakumjibu maana akili yake ilikuwa kwenye kusoma ujumbe uliojitokeza kwenye komputa yake, ujumbe uliomfanya mwili ufe ganzi kwa muda…

NB: Ni ujumbe gani tena huo…sehemu hii ilikuwa ndefu, ina matukio mengi nimejaribu kuifusha hivyo.


WAZO LA LEO: Tusikate tamaa tunapokutwa na matatizo, maana matatizo hayo yanaweza kuwa ni namna  ya kutututoa sehemu moja kwenda nyingine, ambayo huenda ikawa ni bora zaidi, au kutuokoa kwenye hatari,…muhimu ni kujibidisha kutenda mema, na kuyachukulia matatizo yetu kama mitihani ya maisha, kama ni maradhi, basi huku tunamuomba mungu , huku tunatumia dawa, huenda maradhi hayo ni namna ya kujenga kinga fulani mwilini mwetu,  mungu mwenyewe anajua zaidi. Tuzidi kumuomba mungu atusaidie kwenye mitihani, atuongoze kwenye njia njema na kutufanikishia malengo yetu mema. Aamin…
Ni mimi: emu-three

No comments :