Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeWednesday, May 24, 2017

MPENZI WA FACEBOOK-35


Mpelelezi akasubiria amri…mpelelezi kwa muda huo alikuwa hana nguvu zake za kawaida,…watu hao walikuwa wamelegezwa nguvu zao za kawaida.., na docta alichofanya ni kumwekea nguvu nyingine za kuweza kuhimili hali ya amri nyingine lakini bado hakuweza kuziondoa hizo nguvu mpaka mtandao uzisafishe na inachukua mdua kidogo…, lakini kwa vile ile mitambo sasa hivi inamilikuwa na docta, docta akawa ndiye anamuongoza mpelelezi.


Mpelelezi, akaamrishwa aende kumkagua huyo mdada…ambaye alimkuta kwenye kile chumba, …,kingine kabla ya kuachana na huyo mdada, alichoambiwa zaidi ni kufungua pingu alizokuwa,nazo huyo mdada, baadae akaambiwa aangalie shingoni kwa huyo mdada kuna kitu kavaa kama mkufu, akifungue na kukiacha humo.humo shingoni.‘Huyu mdada kama namfahamu….?’ Alijiuliza mpelelezi, lakini hakuweza kuwaza zaidi, ila akajikuta akimuulia;


‘Wewe ni nani..?’ mpelelezi akauliza, na yule mdada akacheka, ni kama vile unamuuliza super star, anayejulikana dunia nzima,…na unapomuuliza mtu kama huyo anahisi kama unamtania tu!

‘Mpenzi wa facebook…’alijiuliza lakini hakuwa na muda , yeye akavutwa na amri nyingine ya kutoka kwenye hicho chumba


***********

Kama ilivyokuwa,kwa msaidizi wa docta, mpelelezi naye alikutwa na hayo hayo, kwani docta naye alikuwa akifanya vitu vyake, kuhakikisha kila aliyewekezwa kwenye hiyo mitandao haramu, ambapo akili na utashi wa mtu unaondolewa na kuwa mtumwa wa nguvu za giza.

Mpelelezi ambaye alikuwa kwenye hilo jengo la biashara , akiwa anafanya kazi kwa kufuata anavyoamrishwa na docta, alitoka kwenye kile chumba alichomkuta yule mdada, na kuelekea huko alipoelekezwa kwingine….

 Sasa alielekezwa kwenye chumba maalumu, ilitakiwa afike hapo mapema, maana hapo ndio kwenye miongozo ya kila kitu, lakini kwa vile docta alishachukua mamlaka ya kuongoza mitambo yote, akawa hana wasiwasi, lakini ukumbuke watu hao ni wataalamu pia, ilipotokea hivyo, na wao wakawa wanatafuta njia ya kurejesha ule mtambo ufanye kazi kama kawaida.

Docta alishtuka hilo, na alipokumbuka kuwa wenzake wanawe wakawa wameshaanza kurejesha nguvu zao, ndio akaona kuna umuhimu wa kumtuma mtendaji wake ambaye ni mpelelezi.

Mpelelezi akaamrishwa,kwenda kuingia kwenye chumba maalumu, chumba hicho kiliwekwa sehemu madhubuti, na watu wengine hawaruhusiwi kuingia humo zaidi ya wafanyakazi wa idara hiyo, akafika mlangoni , mlango ulikuwa umefungwa, na kufungua kwake ni mpaka uwe na namba za siri, ..yeye akaambiwa asubirie tu, baadae mlango ukafunguka, a ulipofunguka tu, …wakatokea watu wanne wamevalia majoho meupe kama madocta…

Walikuwa kama hawakutegemea kuonana na mtu, na walipomuona mpelelezi, sijui kama wanamfahamu maana , walipomuona tu, wakainua mikono juu…kama kujisalimisha,…mpelelezi akawa anasikiliza amri ya kufanya..
'Angalia shingoni mwao, wavue hiyo mikufu na uishikilie wewe mwenyewe, hakikisha hupotezi hiyo mikufu…’akaambiwa, na mpelelezi akafanya hivyo.

 Alipomaliza kuwatoa ile mikufu shingoni, ilikuwa kama kawaondolea nguvu fulani mwilini mwao, maana ghafla wale watu wakaporomoka na kudondoka chini…wakawa kama wamepoteza fahamu..
 Mpelelezi hakutakiwa kuwagusa tena, akaambiwa aingie ndani kwenye hicho chumba maalumu. Na alipoingia akahisi mngurumo wa chini kwa chini, kuashiria kuwa humo ndani kuna mtambo wenye nguvu, na jinsi unavyofanya kazi ndio unatengeza mngurumo huo…kulikuwa na baridi sana…
'Angalia kulia kwako, kwa juu, kuna ‘main switch sever’ tafuta kitufe cha kuizima hiyo serve kuu, ‘akaambiwa, na bila kukosea akaiona hiyo server kuu ambapo kuna nyaya nyingi zinazoelekea sehemu tofauti tofauti,akaiona ile swicho, akaizima

Na alipoizima mara chumba chote kikawa kimia, ule mngurumo uliokuwepo humo ndani ukazima…na kukabakia milio ya kulalamika tu, kuwa mitambo haina nguvu yake ya asili…na umeme!

 ‘Sasa sogea mbele kidogo, angalia upande wa kushoto kwako, kuna chumba kipo, kimezungushiwa viyoo, ni bullet proof hiyo..risasi hzipenyo huko ndani, lakini cha muhimu kwenye humba hicho ni mashine maalumu ya kutunza kumbukumbu, kama akiba,…umekiona mlango kumeandikwa…

'Main server room…’

Akaingia kwenye hicho chumba na kumkuta jamaa akiwa na mihangaiko, jamaa huyo alikuwa kainama chini na aliposikia mtu akiingia hakugeuka, na kwa vile alikuwa akifanya jambo akiwa kachuchuma, akasema;

 'Nimeshindwa kufanya ‘back up’ kwa haraka, na muhimu kwa sasa ilitakiwa tupate  ufunguo kutoka kwa mkuu…’akasema na mpelelezi kusikia hivyo, akajiukuta akirudia hayo maneno ‘mkuu’!

'Mkuu..', kuna kitu kilimgonga kichwa, na kujikuta akihis maumivu sio kitu , bali ni hali aliihis kichwani kama anagngwa na kitu.

 ‘Mkuu, ni nani huyo…ni mkuu wake wa kazi au ni bosi wa hao watu labda ndio wanamuita boisi wao hivyo..’akajiuliza bila kupata majibu. Na wakati anawaza hivyo jamaa aliyekuwa kama kachuchuma au kupiga magoti, akifanya kitu chini ya kuunganisha waya waya fulani, mara akasimama, kwa haraka akageuka.

 Alivyogeuka kwa haraka, na huku akiinua mkono, bastola tayari ilikuwa mkononi mwake…

‘Wewe ni nani…’Inspecta akaulizwa na inspecta hakusema kitu alikuwakabakia kimia hawezi kuongea kitu kama hajaambiwa labda iwe ni jambo la namna ya kipekee, na jamaa alipoona hajibiwi akamuangalia mpelelezi usoni, huku anatikisa kichwa, huku akisema;

 ‘Hahaha, kumbe ni wewe, najua kwanini huongei,..docta huyo anafanya vitu vyake au sio,…..hahaha,…hata hivyo nimesikia kuwa  hivi sasa wewe ni msaliti..na unafahamu adhabu ya msaliti ni nini kwenye hili kundi,mimi kama mmoja wa washika dau, nina kura yangu, sihitaji kukuambia ni ipi, ila kwasasa sina jinsi ni lazima niitekeleze kwa vitendo,…’akasema akitayarisha kufyatua bastola yake, lakini kabla hajafanya hivyo, akasikia mlio wa hatari kwenye server…

‘Subiri….’akasema akichunguza wapi mlio huo unatokea huku kashikilia bastola bado akimlenga mpelelezi.
‘Ok, sio tija,…sasa hebu kwanza, niambie ni kitu gani kimekuleta humu ndani, abda tusema umetumwa au sio…maana wewe unafahamu fika, watu hawaruhusiwi kuingia humu,  ambao sio wafanyakazi wa idara hii..’akasema huyo jamaa akiwa kama anawaza jambo

Mpelelezi bado hakumjibu kitu, akabakia kasimama tu

'Unajua nilijua wewe ni mjanja sana, sasa ona, …masikini, binti yako yupo mkononi mwa yule bosi,…unamfahamu alivyo, usoni anatabasamu anacheka, lakini rohoni ni mnyama, anakuua huku anatabasamu,..ogopa sana watu wa namna hiyo,…binti yako hana kosa, sasa atauwawa muda si mrefu, na wewe , ulitakiwa uwe umeshauwawa, tatizo hivi sasa hatuna mawasiliano, sijui..ok, ..mimi nitamalizia hii kazi, isiwe shida…’akasema huku akiangalia huo mlio ukizidi kutokea tena.

‘Binti yangu yupo wapi…?’mpelelezi akatokwa na hayo maneno,

‘Binti yako, hahaha..yupo huko makaburini, kaenda kutolewa kafara…si unajua mambo hayo yalivyo,…unauliza jibu,…..mimi hapa sijui kinachoendeleahuko, ila nafahau jambo kubwa, kuwa kuna mtu ,……huyo anayeitwa docta kaingiza virusi kwenye mtandao wetu….atauliwa kinyama…’akasema

‘Kwanini unataka kuniua mimi….sina kosa, binti yangu hana kosa…na wewe …’mpelelezi akatulia, mlio ulizidi kuongezeka, na jamaa anashindwa kuinama kuiangalia kwa chini , maana kashikilia bastola.

'Ungekubaliana na sisi, ungeyafaidi matunda ya kundi hili…, hebu angalia miradi tuliyo nayo, …ni mingi ajabu, pesa zinaingia kila siku…na ilivyo, kama tulivyopanga wewe ungekuwa mkurugenzi , familia yako ingeajiriwa kwenye vitengo vingine kama mameneja, mbona mkeo alielewa tu…sijui wewe una nin..ni hiyo hulka ya jeshi, mbona wenzako wanayo, na ni zaidi yako, wapo, wananeemeka tu….’akasema
‘Nakuuliza binti yangu ana kosa gani…?’ akauliza mpelelezi sasa kwa sauti ya hasira, na jamaa akaweka vizuri bastola….

‘Usiulize majibu….na usinilazimishe kupasua huo ubongo wako, kabla muda wako wa kufa bado…hii …huu mtambo ungelifunguka, nikajua kinachoendelea ningelishakuua, lakini je ni kikuua kabla ya muda,..nitaharibu,….lakini ngoja tuone…’akasema akichungulia huku kashikilia bastoka kwa mikono miwili akirudi kinyume nyume.

‘Binti yangu yupo wapi…ni kwanini yeye…?’ akauliza mpelelezi

 ‘Yupo wapi…tatizo lako akili yako hapo haipo, ..umeshalogezewa, haujijui…kama ungelikuwa unajijua,…aah,… bint yako lazma awe kafara, kwani damu yake inaendana na mizimu....shauri lako, mimi kwa hivi sasa siwezi kuzuia hilo..namuonea huruma tu, binti mrembo kama huyo anakuja kufa kinyama, unajua wanachokifanya huko….anauliwa huku anajiona, damu,…inanyonywa,….na shetani…hata sitaki kuona….mtambo ungelikuwa hai ningekuonyesha …’akasema akiangalia kwenye server.

‘Sasa kama wewe sio mnyama kama wao, kwanini ukajiunga na kundi hilo..na kama kweli ulimpenda binti yangu, kwanini hujaweza kumtetea, …si una kura ya dhahabu wewe…kura turufu…?’ akaulizwa

‘Hahahaha, kumbe unanitambua….hahaha, lakini nikitoka hapa, hakuna atakyenitam bua tena, napotea kabisa kwenye hii dunia,…hahaha…umeuliza nini vile…’

‘Ok, kuhusu binti yako au sio…?’ akauliza na mlio ulikuwa ukiendelea kulia, mpelelezi alitamani kuchukua hatua lakini miguu, na mwili ulikuwa hautaki umezuiwa.


'Kiukweli mimi nilimpenda sana binti yako,…lakini cha ajabu kabisa akanikataa, ..najiuliza huyo mwanamke anataka nini, wanawake wapo wengi wananitaka,…kwani, watu wanataka nini, mali ninayo….sura, eeh, mwili…wanataka nini, sijui..na bint yako kama …kama alivyonikataa yule bint wa yule mzee,..basi tena…’akatulia.

‘Binti wa mzee…?’ akauliza mpelelezi, akijaribu kufikiria huyu mtu ni nani…

‘Mimi nilishawaambia yoyote atakayenikataa mimi, atakumbana na kizimba cha mizimu,…mimi sifanyi kitu, wao wanajua…maana nina huruma, …lakini mbele ya hiki kitu sina huruma,…huyo binti wa mzee, yupo wapi,..au binti yako yupo wapi,...wote sasa watageuka kuwa asusa ya mizimu.

 'Ninachojua kwa sasa, na adui yangu mkubwa kwa sasa ni huyo….., sijui docta gani huyo, kaweza kuiba mitandao yetu, na kuharibu mawasiliano yetu..ameharibu ndoto yetu ya kutawala dunia kwa kupitia mitandao, kuitawala dunia, watu na mashetani..hahaha..’akacheka sana, halafu akasema;

‘Unajua ukisoma sana,..ukayajua mambo… unakuwa kama mwendawazimu..ukimuambia mtu hii ndoto, hakuelewi…lakini wataelewa tu…’akasema, sasa ule mlio ulikuwa wa kuendelea kuashiria kuwa kama ni tatizo limefikia kubaya.

‘Aah, unajua umepotezea muda wangu mwingi, sijui kwanini sikuui tu….kuna kitu hapa… Kuna ufunguo wa kila kitu, `universal key’….unaujua huo, wengine wanaita magic key…wengine ufunguo Malaya…yaani ni ufungu wa ajabu sana…huo unatafutwa kila kona, lakini sisi tunao…hahaha…’akacheka, na ghafla akanyamaza.

Nikuambie kitu, hata kama huyo docta, atachukua mawasiliano yote…akayamiliki , lakini sis bado tunayo, hii, ‘main server,’…Humu kumbukumbu zote zipo, hata kama watawashika wote,….wataharibu kila kitu, lakini bado… je nikuulize kitu, huyo docta anaweza kuharibu, server ya ….giza, maana sisi tunafanya wazi na gizani, huko anaweza kufika…’akatulia akimuangalia mpelelezi.
‘Nyie watu mna wazimu…’akasema mpelelezi.

 ‘Na huyo docta anajua kuwa wenzake pamoja na elimu hiyo, wana maaskari wasioonekana, ....unawafahamu maaskari hao, wamesambazwa kila kona...kwenye mitandao, kwenye majumba ya starehe, …na kila sehemu yenye mkono wa pesa..hata majumbani…mwa watu maalum.., hao atawezaje kuwashinda..au kuwazima…eeh,…’akatikisa kichwa.

 ‘Sasa hivi ukiingia kwenye mitandao,eeh… ili uweze kupata nafasi lazima uweke moja ya herufi zetu,… herufi hizo ni ishara ya maaskari wetu,..zimejengwa na ngucvu za giza…hebu nikuulize swali,  unawafahamu hao maaskari wetu…?’ akauliza akiwa kama anawaza jambo.

 'Hahaha....huwezi kujibu hilo, maana hakuna anayeweza kuamini hilo…sisi, unajua, tunaweza kuongea na mashetani...sio raisi kuamini,…na hatutumii …kama wanavyofanya hawa waganga wa kienyeji,….tunatumia digital.....sayansi tupu…hahaha…kusoma kuzuri….'akawa anasogea upande, kwani alihisi mlio mwingine, wa hatari kwenye mitambo iliyopo humo ndani.

'Sio shida, hata kama umezima switch kubwa, bado humu ndani kuna akiba ya kuhifadhi nguvu …uwezo wake inaweza kuhifadhi nguvu hata zaidi ya masaa 48, nyie mnajisumbua tu…ngoja kazi imalizike muone maajabu, maana mumechokoz nyuki….’akasema sasa akionyesha kujiamini.

Mpelelezi, akasikia amri ikimwambia ajitahidi awezavyo kumzuia huyo mtu asiendelee na hicho anachotaka kukifanya, kwani mpaka sasa, asilimia 80 ya kurudisha mtambo wao umeshakamilika,na ukikamilika itakuwa vigumu kuwazuia, na huenda …wakawaua wote waliopo kwenye mitandao yao….’akaambiwa

‘Na binti yangu…?’ mpelelezi akajikuta akiuliza kwa nguvu.

‘Huyo sasa hivi damu inakauka mwilini…wataionyonya kama …eeh, yaani wanavyofanya, wanatumbukiza mrija hapa shingoni, kwenye huu mshipa mkubwa, wanazamisha mpira, wanaanza kuvuta damu…zamu kwa zamu, mpaka mtu anakauka..anavyolia , ..basi shetani linafurahia..hahahaha…’akasema

‘Bint yangu, atauwawa..kinyama hivyo…’akasema na hapo hakuweza kuvumilia, hakujua jinsi gani alivyoruka hewani, alimshangaza hata huyo jamaa, na jamaa hata kabla hajafyatua hiyo bastola alihisi mateke mawili yakitua mwilini mwake, moja kwenye mkono ulioshika bastola na likingine likitua kifuani.

 Jamaa akarushwa mzima mzima na kutua juu ya meza, iliyokuwa na komputa kubwa inayoongoza ile server, ..na baadhi ya vitu juu ya meza vikatawanyika…

'Oooh...what, umefanya nini…..'aliguna na kusema kwa hasira na mpelelezi hakupoteza muda, akachukua chuma cha kutobolea makaratasi kilikuw akikubwa akambamiza ncho kichwani..na jamaa hapo hapo akapoteza fahamu.

Na mara mpelelezi akahisi mwili ukianza kuisha nguvu…alihisi vibaya masikio yanakuwa kama yanazibuliwa…

‘ Kumbuka usipozima hiyo server, ndio itakuwa mwisho wako na mtoto wako..’sauti ikamwambia..

 Hapo akajitutumua, akipepesuka hadi pale kwenye computa ya server,…

‘Bonyeza kitufe cha ‘delete.’ Akaambiwa, na yeye akafanya hivyo, lakini hakukuwa na mabadiliko yoyote, …na alipoona huyo jamaa kalala juu ya meza, anamzuia, akamsukumia chini ya meza, kumbe alidondokea karibu na ilipodondoka bastola, lakini jamaa huyo kwa muda huo, alikuwa hajazindukana.

Mpelelezi akaona alama inaonyesha ujazo wa asilimia tisini na tano…..akaambiwa

 Aakachukua kipanya cha komputa, akaanza kukichezesha hadi kwenye sehemu inayoonyesha muendelezo wa hiyo kazi , akabonyeza sehemu ya kuzuia, ..mara ujumbe ukasema, una uhakika unataka kusimamisha marejeshe ya kumbukumbu zako

 ‘Bonyeza ndio’

Akafanya hivyo kwa haraka…, na mara ule ujazo ukaanza kurudi nyuma kwa haraka na alama za asilimia zikawa zinapungua, mapaka sasa unakaribia sifuri,…

Sasa kumbe yule jamaa chini keshazindukana,…na alipofungu macho, cha kwanza kukumbuka ni kazi yake kwenye Server…akajaribu kuinuka akajigonga kwenye meza, na kumfanya mpelelezi ashituke, na kutaka kuinama kuchungulia chini,…

Yule jamaa alikuwa tayari kashikilia bastola, akiielekeza kwenye sehemu ya chini ya mpelelezi, juu mapajani, ina maana akifatua, anaharibu kila kitu….mpelelezi akanywea, na huku mwili ukianza kumuishia nguvu…

‘Malizia kazi…’sema ndio..kuna ujumbe unasema kazi ya kufuta imekamilika je ianzishe komputa, ….haikuwa na maana sana, lakini huyo jamaa aliyeyepo chini angeliweza kurejesha, kama hatachelewa,…

Kosa alilolifanya mpelelezi, jamaa alipodondoka, hakuichukua ile bastola…sasa ipo mikononi mwa huyu shetani….na mpelelezi alipojaribu kusogea akiwa kanyosha mkono kubonyesha kitufa cha ‘yes..’ mlio wa risasi ukasikika….

NB: Na kwa leo tunaishia hapo.

WAZO LA LEO: Hata tuwe wajanja vipi, elimu, utajiri,..uwezo wa kuongea, lakini bado hatuwezi kuingilia mamlaka ya mungu, mola ambaye atakalo liwe huwa, …hana mshikirika, …Tumuombe mola wetu atujalia maisha mema, yenye baraka tele…Aamin.


Ni mimi: emu-three

No comments :