Mpelelezi, akazindukana , na kujikuta kalala sakafuni , na alipomuona mkuu wake yumo humo ndani, akasimama kwa haraka na kuweka nguo zake vyema, kuhakikisha yupo kiaskri, baadae akasema;
‘Docta umenifanya nini mimi mbona nipo hivi..…?’Mpelelezi aliuliza hivyo, pale alipoona wote wanamuangalia yeye,
‘Nimekufanya nini mimi afande…?’ docta akauliza kama anashangaa.
‘Hata sielewi,…'akasema mpelelezi, akijaribu kutikisa kichwa chake, kuna kitu kilikuwa kikimsumbua, na anajua ni kwanini,...hapo hapo akasema;
'Nahisi binti yangu anaumwa...'akasema
'Kwanini...?' akauliza docta
'Kuna hali..ikinijia najua kuna tatizo...'akasema
'Najua ..nilikuambia, hao watu wamewekeza mambo yako kwenye ubongo wako..wameshakufanya mtumwa, jitoe,..kabla hujachelewa...'akasema docta, na mpelelezi akamtupia jicho mkuu, ni kama vile hakutaka hayo docta anayoyaongea yasikiwe na mkuu wake.
'Mhh...'mkuu akaguna hivyo tu.
'Mkuu samahani, ..nataka kufika
nyumbani…’akasema mpelelezi
'Una uhakika...kuwa binti yako yupo matatani, au ni sababu nyingine..'akauliza mkuu.
'Hapana mkuu, hali kama hii..ikinitokea ni lazima nitasikia simu ya matatizo..'akasema
‘Lakini hawajakupigia simu, au walikupigia kabla sijaingia humu ndani…’akasema mkuu
‘Najua tu mkuuu wakati mwingine mke wangu anajihangaisha mwenyewe bila kuniambia lakini hawezi, ..ni mpaka niwepo, mimi najua jinsi gani ya kumtuliza…’akasema
'Unajua kwa vile..unawajua au sio...wanataka nini, sasa mpaka lini,..sawa mimi nakuruhusu uende, lakini uwe makini...kama ukinihitajia nipo..tumetoka mbali, au sio..'akasema mkuu wake
‘Sawa afande ..nimekuelewa...'akasema mpelelezi sasa akionyesha unyonge fulani.
Alipoondoka, wawili hawa wakajua ni nini cha kufanya kila mmoja akakimbilia kwenye seehmu yake, na kazi ikaanza…
Tuendelee na kisa chetu
*************
Mzee aliona mkewe anachelewa kurudi, akawa sasa anamtafuta kwa
kumpigia simy yake ya mkononi,lakini alishangaa, simu ya mkewe haipatikani, akahisi kuna tatizo, anakumbuka
jana usiku, waligombana sana kuhusu binti yao, mkewe amekuwa akimuona mumewe
hafuatilii ipasavyo kuhusu bint yao;
‘Kwanini polisi hawataki tuonane na binti yetu, kuna nini
wanatuficha…’akasema mkewe.
‘Mimi sijui, wao wanadai ni taratibu zao za utendaji, huyo binti
yetu hatakiwi kuonekana na mtu yoyote kwa usalama wake…’akasema mumewe.
‘Hata sisi wazazi wake hatuna haki ya kumuona binti yetu, mimi
hapo sitawaelewa, kama huwezi kufuatilia hili, mimi nitaenda mwenyewe kesho, ni
lazima wanionyeshe wapi binti yangu alipo, na ana kosa gani..’akasema mkewe.
‘Mke wangu unafahamu hatari iliyopo, nia na lengo lao ni
kuhakikish kuwa binti yetu hafahamiki wapi alipo,polisi wanajua ni nini
wanakifanya, je….hutaki usalama wa binti yetu…’akasema mumewe.
‘Kwani ni maswala ya usalama au wao wamemshika kwa kisingizio
kuwa huenda anahusikana na hao watu wanaowatafuta…si ndivyo walivyofanua au
mimi sielewi hapa, kuna kitu gani unanificha…?’ akauliza kwa hasira.
‘Mke wangu, pamoja na hilo…nia na lengo ni usalama wa binti
yetu, hiyo shutuma nyingine ni namna tu ya kuwezesha hili, kwa usalama wa binti
yetu…’akasema mumewe.
‘Hapana,…nataka nikamuone binti yangu, waniambie wapi alipo
nionane naye basi…hapo ndio tutaelewana nao, vinginevyo, mimi nitafika mpaka
kwa wakubwa zao…sitaki maelezo zaidi…’akasema na wakalala hivyo..
Na kweli kesho yake, mkewe aliamuka asubuhi sana na kuelekea
kituo cha polisi, kutaka kuonana na binti yao….
Sasa jioni imefika, mke hajarudi,…mume kachanganyikiwa.
Mzee kuona mkewe anachelewa, akaamua kumpigia simu mkuu,
msaidizi wa mkuu wa kituo, nia ni kuulizia, kama mkewe alifika huko, na kama
alifika, kama anavyofahamu yeye, mbona hajarudi nyumbani;
‘Hajafika huku…’akasema msaidizi huyo na kumfanya mume mtu
kushindwa kuelewa.
‘Oh,…alisema anakuja huko kufuatilia maswala ya binti yetu, kama
nilivyokuulizia karibu kila siku, sisi kama wazazi tuna haki ya kuonana
naye..mkewe wangu ndio kaamua kuja huko yeye mwenyewe…haniamini…’akasema mume
mtu.
‘Ndio nakuambia mzee, mkeo wako hajafika huku..’akasema mkuu
huyo.
‘Oh ajabu kabisa…tokea asubuhi na sasa ni jioni, atakua kapitia
wapi…’akasema mzee sasa akiingiwa na mashaka.
‘Umempigia simu yake ya mkononi..?’ akauliza mkuu huyo
‘Ndio lakini hapatikani…’akasema mzee
‘Ngoja tusubirie, …kama saa moja hivi…, labda kakwama mahali
unajua huu usafiri wetu ulivyo, foleni na…’Mkuu akakatisha maneno, kuna kitu
alikuwa kakiona kwenye komputa yake, baadae kidogo, akamuuliza mzee;.
‘Mkewe wako alikuwa kavaa nguo gani..?’ akauliza na mzee
akamtajia,
‘Ok, ngoja nitakupigia baadaye kidogo, kuna kitu nafuatilia,
sawa mzee, mkeo atakuwa kapitia sehemu nyingine, huenda simu yake imekwisha
chaji au kuna sababu nyingine, lakini atakuwa salama tu…’akasema huyo mkuuu
kukata simu.
Mzee akabakia akisubiria , kama mkuu huyo atampigia simu, lakini
ukapita muda hai usiku sasa unaingia,…akawa sasa anaanza kuingiwa na wasi wasi
na mashaka…mwishowe ndio akaamua kumpigia docta;
‘Docta, nina mashaka sana, mke wangu hajarudi, alitoka asubuhi,
akidai kuwa anataka kumfuatilia mtoto ..nilijaribu kumkanya hakunisikia, sasa
usiku unaingia, hajafika hapa nyumbani, ..sijui yupo wapi…’akasema.
‘Umeongea na polisi,..’akaulizwa.
‘Ndio wamesema nisubirie…’akasema.
‘Basi fanya hivyo, mimi siruhusiwi kuingilia mambo yao,..kama
nitapata taarifa zaidi nitakupigia,…’akaambiwa na mazungumzo yakaishia hivyo.
*************
Docta, alikuwa
akifuatilia jambo kwenye komputa yake, akaona kitu kilichomvutia ni muda kabla hajaongea na mzee, na alipoongea
na mzee, akasahau kumuulizia jambo, ndipo alipokumbuka, akampigia tena mzee na
kumuuliza;
‘Unasema mkeo aliondoka tokea asubuhi, akitegemea kuja kituo cha
polisi kumfuatilia binti yake, lakini hajaonekana hadi muda huu, na simu yake
haipatikani, nikuulize kitu kwani mkeo alikuwa kavaa nguo gani…’Mzee akashangaa
kuulizwa swali kama hilo tena, na yeye akajibu kama alivyomjibu mkuu.
‘Basi,…ngoja niwasiliane na hawa polisi, tuone watafanya
nini…’akasema
‘Nimeshawasiliana nao, lakini majibu yao ndio hayo hayo ,subiria
tutafuatilia,nahisi kuna jambo ….’akasema mzee na docta hakutaka maelezo zaidi
akakata simu.
****************
Akili yangu ilianza kunirejea, na kujikuta nipo kwenye chumba
chenye baridi kali sana, sikuweza kuvumilia ubaridi huo…nikataka kuomba mtu
apunguze, lakini hakukuwa na mtu karibu,..na wakati huo huo, nikahisi naitwa, au kuna kitu kinanisukuma
niende…, nitokea humo, bila hata ya kufikiria zaidi,nikafanya kama hisia hizo
zinavyonituma, …taratibu kama roboti…
Nikatoka nje,..nilipokutana na mwanga wa nje niliona kama nipo kwenye sehemu ya jangwa,
jua kali…nikatamani nikimbie au nirudi nyumbani,..nyumbani nikiwa na maana hapo
nilipokuwepo awali…lakini kitu kingine kilikuwa kikiniambia niende…niende,
sijui niende wapi ..nikawa natembea tu, tunapishana na watu lakini ni kama vile
hawanioni…
Nikafika nje nikaona bajaji,..nikajikuta naiendea na kuingia
ndani ya hiyo bajaji, ilikuwa ni kama inanisubiria…nilipoaingia tu kwenye hiyo
bajaji ikaondoka…na ilipoanza kuondoka tu,..nikawa sijatambui tena, na
nilipozindukana tena, sasa nikajikuta kwenye chumba kingine cha kawaida,…sasa
naona, nahisi …najua kinachoendelea…sio kama njozi, ni kama hali halisi.
Nilisikia watu wanaongea kwa mbali, nikataka kujua ni akina
nani, lakini sikutaka wanitambue kuwa nimezindukana,…kwahiyo nikawa natembeza
macho, na kuyafumba, hadi nikaweza kujua nipo sehemu gani…ni kama hoteli,
hakuna baridi kama kule nilipokuwepo awali…
‘Huyu hatufai tena,…muda
wake wa kafara na binti ulishapita, hawana maana tena kwetu,…ila hawatakiwi
kuwepo duniani, watasema mengi,…watakuja kukumbuka, na itakwua balaa kwetu,…
ila yule binti bado anahitajika, kwa shughuli nyingine, tunajua ni nini cha
kufanya…yeye bado ni mtu wetu huyo, …’ sauti ikasema.
‘Ama kwa huyo, nahisi kwa muda huu alitakiwa awe amezindukana…huyu
mchukueni mkam-malize…hakikisha mnachua baadhi ya viungo vyake, kama
nilivyowaambia awali, tunavihitajia sana… mabaki ya mwili wake…tupieni wale
wanyama wetu…sitaki ije igundulikane, au kubakia salio lolote, hahitajiki
kuzwikwa, muelewe hilo…’sauti ikasema
‘Narudia tena…sitaki makosa, huyo hatumuhitajii tulishaharibu
awali, sitaki tena kosa hilo lirudiwe,…binti arudi kwao, lakini hakikisheni,
hawezi kufungua mdomo, mnajua ni kwa vipi,..’sauti ikazidi kusema.
Haikupita muda mara nikaona nainuliwa juu kwa juu…nikatolewa mle
ndani na kuingizwa kwenye gari, na muda huo nimejikausha tu, kama vile
sijazindukana, na wao hawakuwa na muda wa kunichunguza.
Niliingizwa kwenye gari la wagonjwa, na kuwekwa kwa nyuma kama
mgonjwa tu, kitanda kilichotengezwa ili mtu usiumie,…walikuwa wanne, wawili
wakaingia mbele na wawili wengine kwanza walikuja na kuhakikisha nimekaa vyema,
wakatoka na kuniacha peke yangu.
‘Nyi wawili mnatosha kuimaliza hii kazi…’sauti ikasema…na gari
likaondoka, tukawa tunakwenda, nikiwa hapo, nikawa nawaza nifanyeje…gari
likafika kwenye sehemu kama muinuko hivi likawa linakwenda taratibu…hapo
nikainuka, nahisi lilisimamishwa na trafiki,…
Kule mbele nahisi wote wawili
waliteremka kwenye gari, wakawa wanahojiwa ….hapo hapo nikajiinua, taratibu
nikafungua mlango wa nyuma, ukafunguka kirahisi tu,…kwa haraka
nikatoka,..nilikuwa sina nguvu,…lakini nikajitutumua na kutembea nikiwa
najizuia wasije kuniona..
Bahati nzuri kwa nyuma kulikuwa na bajaji inatufauta, sikujali
ni watu gani au kama ni watu wao, nikasimamisha, na aliposimama tu, sikuuliza
nikaingia ndani, ya hiyo bajaji…
.
‘Tafadhali nisaidie nipeleke makaburini…’nikasema na mwenye
bajaji alikuwa karibu aruke kwenye bajaji, sijui alinionaje, lakini akafanya
kama nilivyomuambia..akanipeleka hadi eneo karibu na huko makaburini….
‘Tafadhali nipe namba yako ya simu,…nitakutumia pesa yako, nipo
kwenye matatizo kidogo nielewe ndugu yangu…’nikasema, na yeye alipoona nimeteremka, kwa haraka
akaondoka na bajaji yake, wala hakunipa hata hiyo namba ya simu.
.
Nikaanza kutembea, ujue sasa akili ipo, lakini bado kuna hali
nyingine inanivuta nifaney jambo, …ni hali tofauti na ile ya awali,..naona,
nahisi, lakini kiutendaji bado kama namilikiwa hivi,…nikawa sasa natembea
kuelekea barabara, inayokwenda kwenye nyumba moja, nilipofika hapo,…nikaanza
kukumbuka, niliwahi kufika hapo kabla,…kwa muda huo sikujua ni ya
nani…nikaingia..na mara nikasikia watu wanaongea..
Nikatega masikio…nikasikia;-
‘Huyu niliwaambia mkishamumaliza,…damu yake ni muhimu na baadhi
ya viunbgo vyake,.. msimpe muda..nipo kwenye tambiko..mkisha muua, damu yake,na
vingo vyake mpeni dereva, anakuja,..nyie muendelee na shughuli nyingine, muda…ni
muhimu sana…’akasema mtu…nikaikumbuka hiyo sauti, niliisikia kule,…
Nikawa nimejificha, baadae wakatoka watu wawili,..watatu,..mmoja
mwanamke, ..walikuwa wamevaa manguo meusi..wanatembea taratibu, wakafika kati
kati ya chumba, wakasimama, wakawa wanafanya mambo yao, baadae nikasikia
wakisema;
‘Damu ipo wapi…’akauliza wakawa wanahangaika, baadae wakapiga
simu
‘Unasema nini haonekani, …siwaelewi…basi mmojawenu nahitajia
damu yake hapa mara moja…’akasema kwa hasira huku anatetemeka.
‘Wameharibu…wameharibu tena titafanya nini sasa, ..’akawa
anaongea huku anatetemeka, na wenzake wakawa kama wanamshikilia kwa muda,
baadae akatulia,
‘Sasa tufanyeje…hili ni kosa la pili, ..na la tatu,ina maana
mmoja wetu atakuwa ndiye kafara…mnaelewa ilivyo…sasa mtajichagua wenyewe mmoja
wenu au mtoto wake anayempenda…’akasema
‘Sasa tufanyaje..?’ wakaulizana
‘Kwani kwenye wale watu wetu,..hakuna anayefaa…?’ wakaulizana..
‘Binti wa mpelelezi bado anafaa, yupoje, muondoeni ila hali,
tunamuhitajia akiwa na hali ya kawaida, kafara lake litakuwa ni tofauti,
anatakiwa akione kila kitu, hadi tunamumaliza…yeye ni binti mdogo anafaa sana,
hahahaha…’akasema na kucheka..
‘Halafu baba yake yupo wapi..?’ akauliza na kuanza kupiga simu,
baadae akatulia, na kusema
‘Na baba yake keshaingia makaoni…ila kwasasa ,haaminiki, inabidi
amalizwe kabla hajajua kinachotakiwa kufanyika kwa binti yake…’akasema huyo
mtu, alikuwa kafunika uso ..huwezi kujua ni nani..
Baadae wakawa wanafanya mambo yao, na walipomaliza huyo mkubwa wao akasema;
‘Sasa hapo tunapoteza
muda, kwanza ni hatari…tutawanyike, tutarudi hapa kama ya …saa kumi…itafaa,
najua hapo kila kitu kitakuwa tayari,
kila mtu na muelekeo wake…mimi narudi nje ya nchi…’akasema na wakaanza kutoka
taratibu, kila mmoja akawa anatokea mlango wake.
‘Ni nani hawa…’sikukubali, kwa haraka nikatoka kuwafuatilia,
sasa nimfuatilie nani, nikaona anayefaa ni huyo huyo kiongozi wao, yeye
alitokea mlango wa nyuma,…nikamfuatilia kwa mbali,..sijui kwanini , kuna kama
kitu sasa kinaniambia fanya hivi..siogopi…nikamuona akiingia kwenye gari,…
nikaipata namba ya gari, halafu lilipoondoka tu, nikatoka kwa haraka nikaingia
kwenye bajaji.
‘Umeona gari lilitoka sasa hivi…?’ nikamuuliza
‘Ndio….’akasema lifuatilie , na jamaa, utafikiri aliandaliwa,
akasema hakuna shida, kazi ya kulifuatilia hilo gari ikaanza, tulilifuatilia
kwa mbali, na tukawa tunaingia viunga vya ndani ndani, …na baadae tukafika
kwenye jumba moja, lina geti, likafunguliwa na jamaa akatoka na kuingia humo.
Nikawaza nifanye nini, mara wazo likanijia,…nikaona nipige simu,
lakini jingine linasema usipige simu ukipiga simu utaharibu…nikabakia kimia,..sijui
ilikuwaje mwenye bajaji akanisogelea na kusema, simu yako bosi..
‘Simu yangu kutoka wapi…?’ nikauliza
‘Sijui…’akasema , basi nikachukua simu na kuanza kuongea na
mpigaji akasema;
‘Docta..nakufuatilia, endelea kufanya kama inavyokuelekeza,
usijali, tupo pamoja
‘Sawa bosi lakini…fanya ufanyalo ukamuokee binti wa mpelelezi,
anatafutwa kuwawa,..na baba yake pia…pili nimegundua jambo, nipo nje ya jumba
la ..nahisi ndio huyo mkuu…sijui nifanyeje…’nikasema
Docta, akasema;
‘Nipo pamoja na wewe, usijali, yote hayo yanafanyiwa kazi..’akasema.
‘Kwahiyo sasa nifanyeje..?’ nikauliza.
‘Wewe kaa hapo hapo, kwenye sehemu ambayo hutaonekana, wewe
ndiye king’aumizi chetu..kwa kupitia wewe tunaweza kuliona eneo lote hilo…’nikaambiwa
.
Haikupita muda, jamaa mmoja akatoka akiwa kavalia suti…na
kuingia kwenye lile gari,nilichogundua ni sauti yake,kuwa ndio yule yule
aliyekuwa akiongoza wenzake, sasa hivi sio yule mtu wa ajabu, sasa hivi akawa kavalia suti yakiheshimiwa
‘Sasa nifanyeje..?’ nikajiuliza
Hali ikaniambia,…
‘Ingia kwenye bajaji mfuatilie…’nikaambiwa.
Nilichukua bajaji, ..tulilifuatilia hilo gari, lilitembea hadi
kuingia mjini, likatembea hadi uwanja wa ndege, na gari hilo halikuingia uwanja
wa ndege, liliegeshwa nje ya uwanja wa ndege.
‘Sasa sikiliza…subiria hapa hadi ndege ya saa kumi..atakuja mgeni,…’akasema
huyo mtu, na kutoka kwenye gari, akawa anatembea kuingia uwanja wa ndege, sasa
hapo nikajiuliza nimfuate au la…hali ikaniambia nisiondoke hapo.
Baadae kidogo,nikamuona yule mtu, akitokea uwanja wa ndege
kavalia mawani y giza, nikajua labda atarudi kwenye gari, hapana, hakufanya
hivyo, sasa akaita taxi.., wakaongea naye kidogo, mara akaingia kwenye hiyo taxi,
..na kuondoka, na mimi nikamwambia mwenye bajaji, aifuate hiyo taxi..
Tukawa tunarudi kule kule…nikajua wapi wanaelekea, ila ahadi ya
saa kumi, inakwenda kutimizwa, ..nikawa najiuliza itakuwaje kwa binti na
mpelelezi, moyoni nikajipa tumaini kuwa kama alivyosema docta,
wakatalishughulikia hilo, lakini sikuwa na amani kabisa..
Tulipofika maeneo yale ya awali, sasa yeye akateremka, na kuanza
kutembea kuingia kwenye jengo la mzee, utafikiri ni la kwake, hakuwa na
wasiwasi….na mara yakaja magari mengine na baadae gari la wagonjwa…nikaona mtu
akitemremshwa….alikuwa binti…
Wakawa sasa wanaelekea ..makaburini…nikakumbuka ahadi yao ya saa
kumi…
NB: Haya sasa kisa kinaelekea wapi,…mtajibu wenyewe
WAZO LA
LEO: Katika hali halisi watu tunazidiana vipato,… mali, maumbile
nak..hii yote ni mitihani ya mungu, yule mwenye nacho na asiye nacho yote ni
mitihani kwetu sote.., kwanini ni mitihani, kwasababu yule mwenye nacho,
alitakiwa kumpa yule asiye nacho, kwa ziada aliyo nayo.., lakini je inafanyika
hivyo.Mtu anaingia kwenye hoteli anaagiza chakula kingi, anakula kidogo tu
kingine kinamwagwa, watu wanatenda mambo makubwa ya kufuru, sherehe nk, anafuja
haki ya yule aliyestahki..chakula kingi kinamwagwa, sababu ilikuwa si haki ya
huyu mtu, mali nyingi zinaharibika, …mabalaa kwa wingi kwasababu huyu mwenye
nacho hajataka kutoa kwa wastahiki, anafuja haki ya mtu mwingine iliyopitia
kwake kwa niaba tu,..mola anajua ni kwanini ikapitia kwako, mtihani huu…!
Na huyu asiye nacho, alitakiwa awe na subira, huku akitenda mambo yaliyo
mema kwa kufanya kazi kwa bidii, maana ni lazima kila mtu afanye kazi kwa kadri
ya uwezo wake, na mola atajua jinsi gani ya kumtimizia haki yake,..kutokana na
juhudi zake, anazozitenda kwa haki na kwa wema,kutokana na subira yake bila
kuingia kwenye kufuru, kutokana ,..na ucha umungu wake wa kweli…, mola
atamruzuku mja huyu mwema, kwa kadri mola ajuavyo yeye,…tena kutoka kwa yule
mwenye nacho, lakini je subira hiyo ipo..huu ni mtihani kwatu sote. Tumuombe
mungu atujalie tuwe wacha mungu wa kweli
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment