Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, May 16, 2017

MPENZI WA FACEBOOK-28


Msaidizi wa mkuu, ambaye hadi sasa ndio anakaimu kama mkuu wa kituo, aliendelea kuwasiliana na vijana wake,  aliowasambaza sehemu mbali mbali
Mpango wake huo awali alikuwa akiufanya yeye huku akishirikiana na mpelelezi. Lakini  kutokana na sintofahamu iliyojitokeza hivi karibuni, ilibidi abadilishe mfumo wake na mikakati yake.

Yeye na mpelelezi wanajuana siku nyingi na mkuu alikuwa akimuamini sana mtendaji wake huyu, ilikuwa yeye akipewa kazi au akiwa na jukumu muhimu sana, basi mtu anayemuamini ni huyu mpelelezi...bahati mpelelezi akapewa uhamisho wa kuja kituo hicho mapema kabla yake, kipindi hicho huyu msaidizi wa mkuu alikuwa na majukumu mengine makubwa, na alipoyamaliza hayo majukumu ndio akaambiwa anapelekwa kwenye hicho kituo na huko atakutana na huyo mpelelezi,...alifurahi sana kuwa atamkuta mtu ambaye alizoeana naye  kikazi.

Alipofika kwenye hicho kituo, kwanza aliona mabadiliko fulani kwa mtendaji wake huyo, akawa kama anamficha jambo...lakini bado akawa akimtegemea yeye, kwani mkuu wa hicho kituo alikuwa hayupo,.... akawa anakwenda naye sambamba..huku akihisi kuna jambo, kwa huyu mtu wake, na akimuuliza hapati jibu sahihi, akajua labda ni mambo ya kifamilia tu...na alipofika docta, mambo yakaanza kujitokeza!

Hakuamini kuwa mtu wake huyo wa karibu anaweza kujihusisha na makundi kama hayo na kama kweli kaamua kujiunga huko, huenda kuna sababu ya msingi, lakin hakuweza kuipata hiyo sababu kirahisi, na hadi inafikia hapo bado alikuwa hajaamnini...

‘Mpelelezi namuamini sana, huenda anafanya hivyo akitumia mbinu zake za kazi,..ni mtu nimeishi naye nimemuandaa mimi mwenyewe ni kama mwanafunzi wangu kiutendaji...haiwezekani..’aliwahi kumwambia docta hivyo, pale docta alipojaribu kumueleza kuwa mpelelezi haaminiki.

‘Sasa nitamuamini nani, kama huyu mtu wangu wa karibu naye anahusika, ina maana naweza kuuwawa na watu wangu wa karibu…haiwezekani’akasema mkuu akijadili jambo hilo na docta.

‘Wengine inafikia muda wanajiunga bila kupenda,..kuna shikinizo la kulazimishwa, kuna shinikizo la pesa, kuna shinikizo, wengine huitwa wa kulogezewa, akili inapandindikizwa mashetani..hao watu ni watu hatari kidogo,kama usipowajulia watakuafanya mtumwa wao na mwisho wake wanakuangamiza…’akasema docta siku hiyo wakijadiliana na mkuu huyu.

Sasa alipokutana na docta akajua kapata msaada mkubwa , akawa anatarajia kuwa huyu mtu anaweza kumtumia kama msaidizi wake wa mambo yanayomuhitajia, hakuataka kumweka ndani kabisa, maana  kiutendaji haiwezekani , kwani huyo mtu ni raia, hajaajiriwa kama mtu wa usalama, kwa namna hiyo akaweka mikakati yake aliyoiita ‘mipango ya kivyangu vyangu,’ …lakini kwa siri akawa anamtumia docta, akijua kuwa docta ana uwezo wa mambo ambayo hana utaaalmu nayo, lakini hakutaka hilo lijulikane kwa huyo docta.

Docta alipokiuka amri aliyopewa kuwa asitoke pale kituoni, na sasa kajiingiza kwenye janga kubwa ambali hajui kama litaweza kumalizika kwa haraka,..lakini kwa mipangilio yake, akaona hii ndio njia mojawapo ya kumdhibiti huyo mtu…

‘Huyu mtu sasa takuwa kwenye mikono yangu,..’akasema kimoyo moyo. Alijua kuwa bila ya yeye, kuna mambo hatayaweza, lakini kwa sasa akiwa kizuizini, ,..docta atakuwa hana jinsi ni lazima atimize kile anachohitajiwa kukifanya,..hata hivyo kwa jinsi kesi hii ilivyokuja, akajua sasa docta ni mzigo..

‘Sasa nitafanya nini…sizani kama docta kahusika kwa hili, ..ila ni mtego wenye maana fulani,….wanataka nini hawa watu, wanamtaka docta au kuna jambo gani zaidi ya hilo…?’ akajiuliza mkuu, na hapo akaona jibu ni kuenda kumuhoji mpelelezi pamoja na docta.

Tuendelee na kisa chetu…

**********
Mkuu alifika na kumkuta mpelelezi akimuhoji docta, na mpelelezi akaendelea kwa kusema;

‘Hii  sasa ni kesi ya mauaji docta….sasa hivi unashikiliwa kama mshukiwa namba moja, wa kesi ya mauaji… kwa vigezo vifuatavyo;

-Umekutwa kwenye tukio,

-umekiuka sheria kuwa eneo hilo lilikuwa chini ya ulinzi, na ukijua hilo, ukaivunja hiyo sheria,..kwa kuruka ukuta, na kuingia ndani kwa funguo bandia, bila idhini ya yoyote yule…unasikia docta…’akaambiwa docta.

-Kesi hii imegubikwa na mambo ya kishirikina, imani za kichawi na wewe umekiuka mstari wa mbele kuwalaghai watu kuhusiana na hilo,..wewe ni docta unayejua hayo mambo,unaweza ukawa unatumia ujuzi wako huo kufanikisha malengo yako, kwahiyo kwa kipengele hicho tu, unashukiwa kuwa unashirikiana na kundi hilo haramu kwa uficho, kwa kufanya mauaji,..kuuaza viungo bandia, kurubuni watu…’akatulia kwanza.

Alikuwa mpelelezi akimsomea makosa docta, ni  baadhi ya makosa anayoshukiwa nayo docta, kama muhumiwa namba moja wa mauaji,  na docta hakutakiwa kujitetea,..kwani kwa muda alikuwa kashikiliwa tu kuisaidia polisi na vielelezo vikikamilika atafikishwa mahakamani.

‘Mkuu unakubaliana na huyu mtu…?’ akauliza docta akimuangalia msaidizi wa mkuu wa kituo, ambaye alikuwa kasimama pembeni huku kashikilia makabrasha aliyopewa na mpelelezi, kuhusiana na hiyo kesi, na msaidizi akasema;

‘Taratibu lazima zifuatwe, mimi siwezi kukutetea wakati mwenyewe unajua ulichokifanya,…’akasema mkuu huyo sasa akiangalia saa yake kama vile anataka kuondoka. Na mara simu yake ikalia, akasikiliza baadaye akasema;

‘Mimi natoka kidogo…’akasema na kuondoka. Na wakabakia mpelelezi na docta.

‘Umeona sasa unalo..’akasema mpelelezi. Akimuashiria kwa kidole na docta akasema;

‘Hahaha…hivi unafikiri kwa ujanja huu utashindwa kuingia mikononi mwa sheria…’akasema docta akimuangalia mpelelezi.

‘Kwanini niingie mikononi mwa sheria, nimefanya kosa gani, mimi ni mwanausalama lazima nitimize wajibu wangu,…’akasema mpelelezi.

‘Mwanausalama ndio..nakubaliana na wewe kabisa maana umevaa crawn,…, lakini wakati huo huo unatumiwa na hilo kundi haramu,..unafikiri hujulikani, eeh..unajidanganya afande..’akasema docta.

‘Hahaha…, haya ngoja tuone na hizo ndoto zako za kiganga …unapiga ramli ambayo haipo, sasa nakuambia utaenda kusotea jela, na kesi hii ni ngumu sana, hujui tu…’akasema mpelelezi.

‘Siogopi kusota jela, lakini mimi najua nipo kwenye haki, natetea haki, za wanaodhulumiwa, ..silifanyi hili kwa kutafuta sifa au pesa,..sasa wewe pesa zinakuponza, nyumba ya kifahari uliyojengewa itakuwa ushahidi mkubwa sana mbele ya mungu, au unafikiri hilo halijualikani..’akasema docta na mpelelezi kwanza akashtuka , halafu akasema;

‘Utasema mengi…wengi wanafikiria hivyo, kwani mimi siwezi kujenga nyumba nzuri, kuishi maisha mazuri kwa vile mimi ni askari, ni mikakati yangu tu..mimi ingelikuwa ni wewe nisingelipoteza muda huu kwa wivu, ningehangaika kufikiria wakili gani mnzuri wa kunisaidia....nakushuri uyawekwe hayo maneno yako, na tuhuma zako ukayatoke mbele ya hakimu…’akasema mpelelezi, sasa na yeye akiangalia saa yake kama anataka kuondoka.

‘Sikiliza afande, na mimi nakushauri jambo, kabla hujachelewa, najua ni kwanini unayafanya yote hayo,..upo kwenye shinikizo, ama familia yako iteketezwe au ukubali uwe tajiri, na kuwa mwanachama wa kundi hilo, pia,..utapewa uongozi,..si ndivyo ulivyoahidiwa, lakini kumbuka jambo moja, humu duniani tunapita tu..wangapi walifanya hivyo, na sasa wapo ndani ya makaburi…’docta akasema na mpelelezi akawa katulia hakusema neno.

‘Hao watu nawafahamu sana, leo hii wanakuona wa maana, wakiona umefanya kosa dogo tu wanakumaliza, najua ni kwanini wamekulenga wewe, wewe ni askari hodari, na ingelikuwa rahisi kwako kuwanasa hao watu kwa haraka, ndio maana wa kukuwahi..najua binti yako unampenda sana..’akasema docta.

‘Achana na familia yangu wewe, bint yangu anakuhusu nini wewe…’akasema mpelelezi kwa hasira.

‘Unashituka eeh nimeyajuaje hayo au sio…nafahamu sana,…kuhusu tukio lililokupata, na wamepitia kwa binti yako, mara nyingi wanalenga kwa mtoto wako unayempenda sana…huyo wamemuweka raheni kwa vitisho vya mashetani nk, bint yako akapona..kweli si kweli…, lakini kwa masharti, usitake niseme zaidi,…sasa ni hivi ndugu yangu, hao watu hawana imani na wewe tena, siku yoyote wanakumaliza, jiulize ukiodnoka familia yako itakuwaje, una uhakika kuwa itabakia salama …’akasema docta.

Mpelelezi akageuka kuangalia nje, alijua akiangaliana na docta atajulikana kwa jinsi alivyobadilika…

‘Natumai umenielewa, sasa endelea kuchelewa,…utaondoka,!...’akasema na mpelelezi akamgeukia akitaka kusema neno, lakini akaghairi.

‘Utayakumbuka maneno yangu haya,...hao watu walivyo, wanapoiingilia familia moja, wanahakikisha kile kizazi hakibakii..wanajua mmoja wapo anaweza kujitokea na kulipiza kisasi…sasa ni lipi bora, kuliangamiza hilo kundi, na kuifanya jamii ibakia huru au upate utajiri usio na manufaa…’akasema docta.

‘Docta, mimi sijui unachokiongea, nahisi umemuongelea mtu ambaye hayupo hapa..,…wewe tuliza kichwa chako kwenye hii kesi yako.., achana na ndoto hizo za uwongo, mimi sijui unachokiongea, ..’akasema kwa hasira kidogo.

‘Hujui..hahahha…’akasema docta

‘Ndio…mimi nafanya uchunguzi kulitafuta hilo kundi kwa mbinu zangu ninazozijua mimi…wewe hunijui kabisa, na wewe nimekugundua kuwa ni miongoni mwao, utanifanya nishindwe kukamilisha kazi yangu, nina mashaka kuwa wewe umetumwa na hao watu…,  wewe walijua sana hilo…la familia yangu nk..yaonyesha jinsi gani ulivyo ndani ya kundi hilo, kwahiyo wewe utatusaidia sana kulipata hilo kundi..’akasema mpelelezi.

‘Mimi sitaacha kukuasa..maana najua huwezi kukubali kirahisi, wewe ndio msiamo wako huo lakini wao wamekuweza, umewakubalia kirahisi kwanini….wamegua penyewe…hahaha…sicheki kufurahia ile ndio ukweli ulivyo, wanajua wapi pakukupatia, najua wanafanya makosa mengi tu kama hilo la kunipandikizia mimi uuaji, hilo ni kosa kubwa la litawagharimu vibaya sana…’akasema docta na mpelelezi akabakia kimia.

‘Sasa..nikuulize swali moja kwanza, je wakati mimi naingia kwenye hilo jengo la mzee, wewe ulikuwa wapi…?’ akauliza docta.

‘Nilikuwa nje ya hilo jengo, upande wa pili wa barabara, unataka kusema nini kuwa nimekusingizia au…’akasema.

‘Ulijuaje kuwa mimi nakuja eneo hilo, wakati wewe ulitoka pale kituoni mbele yangu…nilikuona wakati unatoka,..?’ akauliza docta.

‘Nina watendaji wangu wananipatia taarifa sio lazima mimi niwepo kwenye tukio..’akasema mpelelezi, naona alikuwa akitafuta wapi wamekosea.

‘Watendaji gani, wakati watendaji wako wote waliambiwa kuwa wewe utakuwepo ofisini, na taarifa zote zipitie kwa mkuu wako…huoni kuwa mkuu wako anakutega hapo,…’akasema docta.

‘Hili ni shauri langu na mkuu wangu…kunitega huko hakuna maana yoyote kwako, ,tatizo lako ni kuwa umeacha taaluma yako ya udakitari umeingilia taaluma za watu wengine, kwanini kama uliipenda hii kazi, hukujiunga tu, ushauri wa bure, endelea na taaluma yako…’akatulia halafu akaendeea.

‘Unanisikia,… achana na mambo ya ramli, yatakupoteza muda bure…fikiria sasa hivi jinsi ya kupata wakili,..upo kwenye kesi mbaya sana, wewe hujijui tu,..je una wakili tumpigia simu au …maana pamoja na mengine bado mimi nakuheshimu sana kama docta, kwahiyo siwezi kukuacha ukaenda kula kitanzi wakati hujajitetea…’akasema.

‘Mimi sihitaji wakili…maana sizani kama nina kesi ya kujibu, ila wewe unamuhitaji tena sana..’akasema docta kwa kujiamini.

‘Kwanini unajiamini hivyo…?’ akauliza mpelelezi

‘Kwasababu sina kosa, yote haya mumeyafanya wewe na kundi lako ili kunitegea mimi, hao watu mliwaua kwasbabau hamuwaamini tena,…msifikiri haya yatakwisha hivi hivi….angalia kosa kubwa mlilolifanya kwenye hiyo set up yenu..’akasema docta.

‘Kosa gani, na …una maana gani..?’ akauliza mpelelezi na kubadili muundo wa swali haraka haraka alipogundua huo mtego.

‘Huyo marehemu haja-uwawa na bastola…kauwawa na bunduki, iliyopigwa kutoka mbali…hilo hamkulifikiria, eeh, …na bastola aliyokutwa nayo binti, …hahaha, usishutuke, ndio maana nakuambia wenzako wamekurupuka, najua walikuwa na mpango mnzuri tu..lakini…. ‘docta akatulia kwani wakati huo mkuu alikuwa amefika.

‘Ehe.. mpelelezi, nataka unielezee kwa kina, ilivyotokea…’akasema mkuu akimwanglaia mpelelezi kwa macho yanayoonyesha hasira fulani.

‘Mkuu ndio naandaa taarifa mkuu, ….nilikuwa namuhoji huyu mshukiwa
na mambo yote kwa ujumla nitakuletea…’akasema mpelelezi.

‘Una uhakika na uchunguzi wako wa awali ulioniletea..’mkuu wake akasema sasa akiwa kashikilia kabrasha la taarifa aliyopewa na mpelelezi wake.

'Mkuu nilikuambia, huyu mtu ana jambo,…kwenye taarifa yangu nimeelezea kila kitu,ila nikaweka maelezo kuwa bado kuna mambo nafuatilia, ndio maana nataka huyu mtu awekwe kizuizini asije kuharibu ushahidi..’akatulia

‘Kama nilivyoweka tahadhari huyu mtu ni hatari anatuamia  taaluma yake, akifanya mauaji, na kama ulivyoona tulimkuta akimuandaa marehemu ili ionekane kuwa huyo marehemu alikuwa akitaka kumuua mdada, na mdada akamuwahi huyo mtu lakini hakuelewa kuwa ,..’akasema mpelelezi hapo akatulia kwani kuna simu ilikuwa inaita kwa mkuu wake.
‘Ok…tatizo hapo ni muda…’akasema mkuu ajibu simu huko anapopigiwa, na mpelelezi akaonekana kusikiliza kwa makini lakini huwezi kusikia anachoongea mpigaji simu.

 Baadae akamaliza kuongea na simu na kumgeukia mpelelezi, na mpelelezi sasa akasema;

‘Mkuu kila kitu tutakionyesha sawa sawa,…hawezi kukwepa makosa huyu mtu, ana makosa,… nimechunguza, uchunguzi wa awali, kuna kila sababu za kumshikilia yeye kama mshukiwa wa awali wa haya mau-aji …ila kuna jambo, nataka kulichunguza tena, ni kuhusu taarifa ya risasi, …’akatulia kidogo na mkuu wake akaingilia na kusema;
.
‘Ndio…taarifa ya wachunguzi  inasema marehemu kauwawa kwa bunduki, ‘sniper rifle’ …kwahiyo muuaji alikuwa nje, mbali na jengo,..na imegundulikana kuwa muuaji alikuwa kwenye lile jengo refu upande wa pili wa bara bara kwa utaalamu wa tundu, umbali..nk…’akasema mkuu.

‘Ndio hivyo mkuu,… nilitaka nikueleze kuwa sijapitia taarifa ya wakaguzi na wataalamu wa risasi..na uchunguzi wa mwili wa marehemu…’akasema mpelelezi.

‘Kwa maana huyo muaaji alikuwa nje,…ya jengo…au sio…?’’akasema mkuu akiwa hamsikiliza kwanza mpelelezi.

‘Yawezekana hivyo mkuu, kwa taarifa ya wataalamu,… lakini huyu mtu anaweza kufanya hivyo, na kwa haraka akaja kuingia kwenye jengo ili kuweka vitu sawa, ndio maana tulimkuta akijaribu kumweka marehemu ili ionekana hivyo, kuwa marehemu alitaka kumuua binti na binti akamuwahi…’akasema.

‘Kwa hiyo kwa maana nyingine,  shutuma dhidi ya mshukiwa hapa, hazina nguvu kutegemeana na muda…angalia vitendo hivyo ukivioanisha, vinamuwekwa docta mbali na kosa la kuua..labda makosa mengine, ..kwahiyo bado unahitajika kumtafuta muuaji ni nani…wewe ni mtaalamu wa upelelezi, fanya kazi yako usiweke hasira na chuki mbele…’akasema mkuu.

‘Sawa mkuu nimekuelewa,… hiyo kazi niachie kwanza…, nipe muda…naona haya mambo tunayapeleka kwa haraka, sivyo inavyotakiwa…’akasema mpelelezi,
‘Najua sana hilo, ila wewe ndio ulitaka kulipeleka hili jambo kwa haraka kwa kumshika mtu ambaye hajafanya kosa na kumfanya mkosaji aweze kutoroka, kwahiyo nakutaka usipoteze muda, fanya kazi yako kwa haraka tumpate huyu muuaji..lakini professional, tumia taaluma yako…’akasema mkuu wake, akamkabidhi mpelelezi kabrasha lake kwa kumshikisha kifuani.

‘Sawa mkuu..’akasema na mkuu akageuka kuondoka lakini akawa kama kakumbuka jambo…akageuka na kusema;

‘Na wewe docta, nilikuambia nini…?’ akauliza sasa kwa sauti ya kikazi zaidi.

‘Nikae humu ofisini nisitoke..’akasema docta

‘Kwanini ulitoka bila taarifa yangu….’akaulizwa.

‘Kwasababu nilimuona mpelelezi akitoka kwa haraka, nilisikia ukimuamurisha kuwa asitoke, …na utokaje wake ulionyesha kuna jambo, ..hisia zangu, unajua pamoja na mengine hisia zangu zina maana kubwa sana, nilishakuelezea kuhusu hilo…kwa hamasa nikajua kuna jambo anakwenda kulifanya….’akasema docta.

‘Hiyo haikuwa kazi yako, wewe upo chini ya ulinzi, kukiuka kwako amri halali kunakufanya sasa uwe mshitakiwa..na hilo siwezi kukutetea…na kwasababu hiyo wewe utashikiliwa kituo cha polisi hadi hapo kesi hii itakapokamilika..’akasema mkuu.

‘Lakini mkuu…’akataka kujitetea.

‘Hakuna lakini hapa, amri ni moja..’akasema mkuu na kuanza kuondoka, lakini docta akamshtukizia kwa maneno.

‘Mkuu,… msaidizi wangu ananihitajia sana,..na kwa hivi sasa hajulikani wapi alipo..naona itakuwa kama ilivyotokea kwa binti wa mzee, na hili mimi sitakubaliana nalo tena,…na sijui kwa binti wa watu imekuwaje, maana hamtaki hata kunifahamisha, je yupo hai au amekufa….’akasema na mpelelezi akasema kwa haraka.

‘Msaidizi wako bado yupo ICU, hajaweza kutembea, na kuhusu binti wa mzee, kwani wewe pale ulimuonaje…’akasema mpelelezi akimuangalia kwa macho ya kejeli.

‘Una uhakika na hilo..?’ akauliza docta.

‘Kwanini unasema hivyo..uhakika kuhusu nini,…kuhusu msaidizi wako, labda utuambie wewe mpiga ramli..?’ akasema mpelelezi na mkuu akaingilia kati na kuuliza.

‘Kwanini unasema hivyo,…kuwa msaidizi wako…unataka kusema nini..?’ akauliza mkuu sasa akionyesha mashaka na kumuangalia mpelelezi.

‘Muulize mpelelezi wako yeye ndiye anajua zaidi,…msaidizi kweli yupo ICU… jamani msione nimefunga safari hadi kuja huku , nyie watu mnapambana na mashetani..sio tatizo rahisi kama mnavyochukulia…nawonya tena, kuwe makini na hili kundi…’akasema docta, na mkuu akamgeukia mpelelezi.

‘Mkuu huyu mtu ana matatizo, keshaanza kuota ramli zake,..huyo mtu yupo ICU, sina shaka na hilo, haiwezekani akaondoka pale mtu hata kujiinua hawezi, …’akasema mpelelezi, na mkuu akachukua simu na kupiga hospitalini anapotibiwa huyo msaidizi.

Ilichukua sekende chache, mkuu akatoa macho ya kutoakuamini…akageuka kumuangalia mpelelezi, na hata kabla hajasema neno, akageuka na kutoka nje…

Mpelelezi, akamuangalia docta kwa macho ya kuuliza na docta akaonyesha ile mikono ya kusema,;

Shauri lenu…

NB: Ni nini kitaendelea…


WAZO LA LEO: Unapotendewa mabaya, ukadhulumiwa, na ukawa huna namna ya kujitetea, kihali na mali,…usikate tamaa, ulalamika, ukajiumiza kwa huzuni …kwani yupo mtetezi asiyeshindikana, nyosha mikono yako juu na mkabidhi yeye, mtetezi wa kila mtu, yeye kwake hutashindwa, muhimu uwe na na subra, na huku ukitenda yaliyo haki!.
Ni mimi: emu-three

No comments :