Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeTuesday, May 9, 2017

MPENZI WA FACEBOOK-25
Msaidizi wa docta alifikishwa hospitalini, na vipimo vya mkono kabla ya mashine vilionyesha kuwa huenda mtu huyo keshafariki, ..docta akasema hajafariki, kwahiyo wampime kwa kutumia mashine, na wakafanya hivyo..

Ikabidi taarifa zikifishwe haraka kwa polisi, na docta akaongea na msaidizi wa mkuu akimuelezea tukio lilivyotokea na kwanini yeye aliondoka bila kusubiria kibali chake, na mkuu huyo akasema hili tukio ni lazima lifanyiwe uchunguzi,..kwahiyo atamchukua mpelelezi wake anayemuamini alichunguze kwa makini.

Mpelelezi huyo akalifanyia kazi kwa siku hiyo nzima...na kesho yake, ikawa ni muda wa mpelelezi huyo kutoa taarifa kwa mkuu wake,... ukumbuke mkuu wa kituo hicho alikuw bado hajarudi, huyu anayesimamia haya yote ni msaidizi wa kituo., ambaye docta alikuwa anmuamini kuwa anaweza kusaidiana naye kuhakikisha tatizo hilo limemalizwa, lakini haikuw akazi rahisi.....

'Mpelelezi alikuwa amekuja na hoja nzito baada ya uchunguzi wake, alishaongea na msaidizi wa mkuu wa kituo hicho mapema alipofika, , kabla ya kukutana kwenye kikao hicho maalumu.

Tuendelee na kisa chetu...


***************
Msaidizi wa kituo cha polisi akatoa maelezo ni kwanini wamekutana, na sasa alikuwa akielezea tuki hilo la karibuni, akasema;

'Tukio hili linathibitisha udhalimu wa watu hawa,..na sasa imefikia muda tunataka kusema basi, mimi nimeletwa hapa kuifanya hii kazi, siwezi kurudi kwa bosi wangu nisema nimeshindwa kwangu hilo halipo, ni lazima hawa watu wapatikane, waingie kwenye mkono wa sheria..

'Kwahiyo hii leo, nimewaiteni nyie, ...docta, ambaye anatusaidia, najua mpelelezi kaja na hoja nzito, lakini tunahitajai kuiangalia kwa makini kwa pamoja, maana tuisje kukimbilia kuchuku hatua tukavunja nguvu ya kikosi chetu, hiki ni kikosi maalumu cha siri cha kupambana na kundi hili na yatakayoongelewa hapa yatabakia hapa hapa mpaka siku muafaka ukifika,...sawa..'akasema na wajumbe wakasema 

'Sawa...'wakasema wajumbe , ila mpelelezi akaongeza kwa kusema; 

'Sawa mkuu, lakini nimeamua hivyo baada ya kujirizisha, kuwa tukifanya hivyo, kwa kuhakikisha hakuna msaliti, hakuna mtu anatumiwa tunaweza kuifanya hii kazi kwa ufanisi zaidi,...'akasema mpelelezi.

'Ni sawa lakini ngoja tulione hili kwa pamoja kama ni kweli au si kweli,...'akasema mkuu huyo, na kumgeukia docta.

'Docta pamoja na mengine kuna hoja imekuja hapa ya kutaka kukuhoji wewe kwanza kabla hatujaendelea na kazi hii, tutaifanya kwa jinsi tunavyoendelea ili kujirisha, mimi bado nina imani na wewe, lakini wajumbe bado wana mashaka...'akatulia

'Pia tumeamua kumchukua wakili wakili ambaye tumemuomba ili aone kama tunaweza kulifikisha shitaka hili mahakamani..tunajua bado, lakini kwa hatua hii pia tunaweza kupata ushahuri wake,...atakuwa mwenzetu kwa jinsi tunavypambana na kundi hillo haramu...'akasema.

'Lakini pia leo nimemchukua mpelelezi wetu mashuhuri wa kesi kama hizi, mara nyingi tukimchukua yeye, hakuna kinachoshindikana, kwani kakutana na kesii kama hizi nyingi tu...

'Kiujumla hali ya mgonjwa, ambaye alitoweka nyumbani alipokuwa ..akaokotwa kwenye mfereji wa maji machafu..ni mbaya sana..hatuna matumaini naye sana..bila kuficha, maana sisi wote hapa ni wataalamu..., lakini hayo tumemuachia docta, kuwa lolote likitokea atupe taarifa..haraka iwezekanavyo...najua docta wetu hapa anahitajika sana huko lakini kwa sasa hapa tunamuhitajia pia..., 

‘Kiujumla bado hatujawa na kesi ya kumshitaki mtu yoyote hapa, ndio vielelezo vipo, ndio, kuna mtu kaumizwa, ..ok, tuombe mungu iwe hivyo kuumizwa tu..lakini kama atakufa, sasa tutakuwa na kesi ya mauji...na mpaka sasa kuna hisia tu, kuwa kuna kundi fulani linahusika, kundi hilo linaaminika kuwa linafanya haya likitumia nguvu za giza, kama mlivyosema, sasa je mumeweza kumshika mtu , na kama kuna mtu kashikwa au kushukiwa mnayo ushahidi wa kutosha…’akasema wakili.

‘Sasa tufanyeje, maana hawa watu ni wajanja sana,…na wana kila mbinu za kuweza kuwavunga watu, na wapo makini sana, unaona kila unayemuhisi kuwa yupo anauwawa..kwahiyo ina maana kuna ambaye bado yupo juu ya wengine, sasa ni nani, inatuwia vigumu hapo,,’ akasema msaidizi wa mkuu wa kituo.

‘Mpaka sasa hatua ni nzuri, wasiwasi wangu ni kuwa hawa watu walivyo makini wanaweza kubadili muelekeo, na kundi hilo likasambaratika kwa muda,..nakumbuka kundi kama hili lilikuwepo enzi zile za yule aliyetaka kuunda dunia yake..’akasema wakili.

Docta kwa muda huo alikuwa na mawazo yake, aliwazia mitego yake aliyoiweka, alijua anacheza na hatari…lakini alijua kama itakwenda vyema kama alivyotarajia anaweza kuhakiki ukweli wa yote hayo, na huenda ikawa ni nafasi nzuri ya kuthibitisha kile alichokigundua, japokuwa alishashuku kuwa yupo kwenye nafsi ya kutokuaminika tena, na asipofanya juhudi za ziada huenda akajikuta matatani... sasa akacheza karata yake ya mwisho.

Wakati msaidizi wa mkuu akiongea, akilini mwake alikuwa akiwaza hicho alichokifanya, akasema akilini mwake;

 'Hizi kazi wakati mwingine huwezi kumuamini mtu, ni lazima mengine niyafanye kivyangu, kujilinda na kujihami, ….’akawa anawaza na mara akajikuta sasa akiulizwa swali na hapo akakatisha mawazo yake;

'Una uhakika huyo msaidizi wako atapona kweli ..nilipitia asubuhi na kumuona alivyo, mmh yupo yupo tu….tatizo ni nini hasa kama kichwa hakikuathirika au sio..na kwanini walenge kichwa, unasema hata awali walifanya hivyo kwa mtu huyo huyo, …?'akauliza mkuu huyo.

'Kiukweli sina uhakika na kupona kwake, nimejitahidi sana, lakini hali aliyofikia ndio hiyo…sasa atakuwaje..siwezi kusema kwa sasa…, lakini sisi kama madakitari tunachopambana nacho ni kuhakikisha kuwa anapona,…na lengo letu ni hilo, kuwa atapona…kiukweli, hali yake bado mbaya,..mbaya sana hata mimi naishiwa nguvu maana ni mtu wangu wa karibu sana… ukimuona mtu mwenyewe utamuonea huruma..'akasema.

'Oh…lakini hkufanya vizuri , kwa kutoroka kwako,..nilimlaumu sana mlinzi wangu kuwa alifanya kinyume na makubaliano yetu,..ilitakiwa unifahamishe mimi kwanza,, kwa tukio hilo linanipa shida hata mimi...'akasema mkuu.

 'Niliona kuwa nikifanya hivyo itachukua muda, na ujue nilikuwa nacheza na hisia zangu tu, msingeliamini kwa haraka, hata hivyo namshukuru sana mungu, hisia,…imekuwa ni msaada wangu mkubwa kwenye matukio kama haya,.. aghalabu, haiwezi kuwa tofauti..namshukuru mungu kwa hilo..'akasema docta.

‘Mkuu huyu mtu kafanya kosa kubwa sana, usimtetee…angetuambia kwanza sisi wataalamu wa kazi hizo,...na sisi tukashiriki kumtafuta..huenda tungeligundua mengi, na ushahidi wa kuweza kutusaidia, sasa kaharibu upelelezi, na ndio nasema kafany ahivyo kwa makusudi ili kuharibu upelelezi, sio bure…’akasema mpelelezi.

 'Unajua awali…kiutendaji, nilitaka nikuweke ndani docta, hata alipokuja mpelelezi hapa lengo langu lilikuw ani hilo,..kwasababu nyingi tu, ya kwanza ni kwanini unakuwa mbele kuyagundua mambo hata kabla yetu, pili unajiamulia mwenyewe tu…hutaamimi nilishajianda kwa hilo, .’akasema mkuu

‘Sijakuelewa kabisa mkuu..., kwani hapo, kosa langu ni nini.?’ akauliza docta.

‘Nilijiuliza...ni kwanini matukio mengi unayafahamu kabla,….sisi tunatumia nguvu nyingi ,kuchunguza huku na kule,lakini wewe unagundua kitu kwa haraka,..ina maana uliju akuwa hilo litatendeka uliju akuwa huyo mtu utamkut wapi,..kiukweli nilitaka nikuweke ndani  ..'akasema mkuu

'Sasa kwanini umeghairi kufanya hivyo..?’ docta akauliza kitahayari, hakutarajia hilo.

'Kiukweli nimegundua kuwa bila wewe hii kazi hatutaweza kuifanikisha, sasa hivi naanza kukuamini , kukuamini, na kiukweli nataka hili tatizo limalizike ili tuwe na amani, unajua wakubwa wamekuja juu, wananchi wanalalamika, ina maana sisi tumeshindwa kazi, lakini ukiwashika watu, siku mbili tatu taarifa inakuja kuwa waachiwe, sasa sielewi...'akasema.

 'Nikuambie kitu afande, kadhia hii, tatizo hili limegubikwa na mitihani miwili mikubwa, shiriki na pesa…na imani hizi zina nguvu kumteka mtu nafsi yake..’akasema docta.

'Kwa vipi…’akauliza huyu mkuu, sasa akikaa vyema kumsikiliza.

'Watu wengi, ukiwagusia mambo ya uchawi, …kulogwa, mashetani..ni nani hataogopa,…au ukisema nyoka huyoo…ni nani hataogopa,… mtu anaweza kujitia kichwa ngumu kinadharia, akasema mimi siogopi, mimi siamini, lakini yakimkuta yakumkuta, ..utaona vitendo vyake jinsi vinakizana na kauli yake....’akasema

 'Katika tafiti zangu nimegundua kuwa akina mama wengi, hutegeka haraka sana kwenye imani hizi, zinazoambatana na ...shirki, ..na ukiangalia kiutaalamu utagundua ni kwasababu gani…sababu kubwa ni madhaifu yao ya asili…ambayo ni hofu..’akatulia.

‘Ok,..inahusiana vipi na hii kesi..nataka mawazo ya hii kesi, unasikia hapa naona kama napoteza muda..’akasema mpelelezi akionyesha bado ana hasira na huyu docta.

‘Nataka ulielewe hili kwanza, ni muhimu sana kwenye hii kesi, usikimbilie kutumia nguvu bila kujua sababu na mzizi wa tatizo hili..’akasema docta.

‘Sawa niridhishe…hapa sijatumia nguvu….’akasema mpelelezi.

‘Hili kundi sio kundi la lele mama, ni kundi la wasomi, waliosoma, na kusomea akili za watu,..madhaifu yao, na namna ya kutumia vitu hivyo kujipatia mali, wao sio wachawi au wanga wa hivi hivi…, kama sisi tunavyojua, wao wamewekeza mambo hayo kwa ajili yakupata utajiri, na utajiri haswa…’akasema

 'Mhh, docta....hehehe…ndio hapo nakutilia shaka, anyway..endelea..’akasema mpelelezi

'Najua nikiongea hivi utazidi kunitilia shaka, kuwa mimi nimejuaje haya…’akasema docta

'Haswa…na usiponirizisha kwa ushahidi , kiukweli sijui, mkuu, kama hamtachukua hatua, nita..anyway,…endelea..’akasema huyo mpelelezi.

'Ni kuwa mimi ni docta lakini kiasili, wazee wangu walikuwa wanajishughulisha na tiba asili, sisi ni ukoo fulani wa waganga wa kienyeji...waliaminika sana, na wakati nikiwa mdogo,babu aliniita akataka kunikabidhi mkoba..’akasema na wote wakamkodolea macho.

'Ehe, ikawaje sasa…?’ akauliza mkuu msaidizi na mpelelezi akatabasamu akijua kuwa akilichokitaka ndio hicho kinajileta.

'Nilikataa,…’akasema hivyo na jamaa wakalegeza shingo zao, na mpelelezi akatikisa kichwa kama kutokukubaliana na kauli hiyo.

'Si nasikia ukikataa unapatwa na mabalaa..’akasema mpelelezi..

'Ndio hivyo, …ni kweli awali nilipata matatizo sana, …lakini kilichonisaidia mimi ni uchamungu wangu…, nilibobea sana kwenye imani ya dini yangu. nikamuweka mungu wangu mbele…wazazi wangu walinisomesha sana dini..,kabla sijaingia kwenye elimu ya kawaida, na mungu alinijalia kipaji cha akili ya ziada…’akatulia.

 'Ok, sasa…aah, itatusaidiaje hiyo kwenye hii kesi…?’ akauliza mpelelezi.

‘Nyie mumemuuliza maswali kumuhusu yeye, ni lazima awaeleze mumuelewe,..usiwe na haraka, mimi nimeshamuelewa sana..’akasema wakili.

‘Ok, haya endelea ..’akasema mpelelezi, na mkuu alikuwa akisoma makabrasha fulani ya huyo mpelelezi.

'Sasa ni hivi,.. nilipokuwa shuleni, sikuacha imani yangu ya dini, kumuomba mungu sana, kwahiyo babu na mizimu yao haikuweza kunisogelea tena.., ila mimi mwenyewe sasa nilipomaliza chuo kikuu, nikaingiwa na hamasa, ..maana nilisomea udakitari wa mambo ya akili na ufahamu..kitaalamu wanaita: neurologist’, nikaona niufanyie utafiti huo utaalamu wa babu.

'Wa nini sasa..uache taaluma yako ya kisomi, uingie kwenye mambo yasiyo na tija…labda useme ukweli ulikuwa na ajenda nyingine ambayo ndio hii …’akasema mpelelezi.

‘Nia ni kutaka kuoanisha imani hizo za mababu, za kutegemea mashetani, na taaluma hizi za kisayansi, na jinsi gani imani hizi zinavyoathiri ubongo wa mwanadamu kwenye maisha yake ya kila siku....nasema imani hizo za mashetani, maana mizimu ni mashetani au sio,minielewe hapo…’akasema

‘Sawa, usemavyo na uelewavyo,... hayo mambo sisi hatujui…’akasema mkuu.

‘Unasema hamjui kiutendaji na sheria zenu lakini nyie mnaishi wapi,…mpo ndani ya jamii, na nyie ni wanajamii na nyie mambo kama haya yanawatokea kwenye familia zenu, au sio..au ukiwa askari mambo kama hayo hayawezi kutokea kwenye familia zenu…’akasema

‘Ok, tusema sawa, haya endelea…’akasema mpelelezi.

‘Kosa, au madhaifu yetu wanadamu ni hiyo imani kuwa eti mizimu ni mababu zetu,..huwezi kusema mizimu ni mababu, hakuna kitu kama hicho..tunapata dhambi sana..utawakuta watu wamechukua mabaki ya miili ya mababu zetu wanaitumia kwenye vitu vinaitwa matambiko…haiji akilini..’akasema docta.

‘Sasa kwanini…’akasema mpelelezi na kukatisha.

‘Hapo anatuchezea akili shetani maana tunaye kila siku kwenye maisha yetu, anatuhitajia sana kama wanachama wake,..huyo sio babu au mababu zetu, huyo ni shetani, na shetani atabadili sauti kama unavyotaka wewe ataongea kama huyo babu au bibi yako aliyetangulia mbele ya haki…hizo zote ni njama zake…’akasema docta.

‘Ok…endelea…’akasema mpelelezi.

‘Shetani akishakuweka mikononi, akiwatumia mawakala wake ambao ndio wanaotudanganya, kwa ramli, sijui na nini…kinachofuata ni nini..atahitajia damu, atahitajia kafara, atahitajia…mambo yenye kuathiri wanadamu wengine, ..ni kweli anaweza kukuapa utajiri, lakini utajiri wenye masharti kama hayo, ya kutoa kafara, .hapo ndio mauaji yanapoanza kutokea..hapo ndio,…makaburi yanachimbuliwa , hapo ndio miili ya watu inahitajika…’akatulia

‘Hapo hapo..ndio tunapopataka..ebu fafanua hapo..ina maana, waganga, au sio, ndio wanaagiza kuwa mababu, wamesema hivyo, au sio, wanahitajia kafara, wanahitajia,…miili ya watu au sio..ili upate hiki na kile, au sio…sasa…aliyesema hivyo ni mganga..kwanini tumsingizie shetani, wakati waganga wapo, kama nyie…’akauliza mpelelezi.

‘Rejea maelezo yetu…mizimu ya mababu zetu ni mashetani, wanakuja kuzitawala nafsi zetu,..sisi wanadamu hasa waganga wa kienyeji, wanakuwa kama mawakala…waganga ili waweze kupata jibu la mataizo yetu tukienda kwao, wanachofanya ni kuyaita mashetani,..mashetani hayo yameshateka ubongo wetu, yameshajua ni nini tunahitajia,..wanachofanya ni kutoa kile unachokitaka wewe kwenye ubongo wako na kumfikishia mganga, na mganga anakuelezea wewe..hapo unamuona ni mkali, unaitikia tawire..sawa…’akasema docta

‘Hahaha….wewe ni kiboko…kwahiyo ndivyo unavyofanya au sio…’akasema mpelelezi na docta kwanza akakunja uso, akawa anawaza hivi kweli huyu mpelelezi ana nia mbaya na hapo akatulia kwanza.

'Ina maana hao waganga n.k wanaitumia mizimu, mizumu ambayo  ni mashetani ambayo sisi tunadanganywa kuwa ni mababu zetu…na kwahiyo kwa mbinu hizo ndio watu wanakuja kuambiwa wakatafute damu, wakaue, wakatafute miili za watu nk…?’ akasema mpelelezi.

 'Asilimia kubwa ni hivyo…anacheza na ubongo wetu, lakini sisi wanadamu tulikuwa na namna ya kumkwepa,..kumlaani na kamwe asingeliweza kutusogelea…, shetani na ujanja wake wote, bado anamuogopa sana mwanadamu…’akasema docta.

‘Hahaha..hivi kweli shetani atokee hapo, utasimama, au umuone mtu ana mguu wa kwato…utasimama…?’ akauliza mpelelezi.

‘Sasa ndio nakuambia siri hiyo…shetani anamuogopa sana mwanadamu maana mungu yupo naye…na ili shetani akushinde, anachofanya ni kukujengea hofu...na kwa vile asilimia kubwa ya nafsi zetu, hatuna imani thabit ya kumtegemea mungu, tunaongea tu, lakini  siri ya nafsi aijuaye ni mwenyewe..tukiona kitu cha kuogya, kama vile nyoka, ..kama hivyo mtu ana kwato…mtu anafanana na marehemu..utafanya nini…’’akawa kama anauliza

‘Kiukweli utaogopa…’akasema mpelelezi

 'Kwahiyo…hebu turudi nyuma kidogo, nataka kuoanisha maelezo yako na maisha yako,..hebu rudi pale wewe na babu yako ilikuwaje…?’ aliyeuliza ni wakili.

'Basi mimi nilipomaliza chuo, na masomo yangu na sasa ni docta,…nikarudi kwa babu, nikamuomba anifundishe hayo mambo yao, alijua sasa namdanganya, alishajua kuwa sina imani ya mambo hayo, lakini ndio… alikubali kunifundisha sehemu ya dawa na tiba tu asilia…, hayo mengine ya giza aligoma kunifichulia…’akasema docta

‘Kwahiyo, ukisema hivyo, hayo ya kujenga hisia,..ukaweza kugundua mambo, yanaitwaje..maana wengine ndio hiyo ramli, au …utuambie wewe unawezaje kugundua mambo hayo, ..hapo ndio sisi tunafika hatua ya kukutilia wewe mashaka…’akasema mpelelezi

 'Sasa ni hiv, kwa vile asili yetu kiurithi ni  waganga, na uganga wa asili ni hisia, njozi nk…inakujua tu, … ukitumia viasili kama hivyo, ambavyo ni neema ya mungu, ukacheza na hisia zako vyema, huku ukimuomba mungu, unaweza kufichuliwa siri kubwa sana ya maisha yetu…’akasema docta.

‘Kwahiyo babu akakutalia, lakini wewe ulifanyeje..’akauliza wakili, yaonekana kuna kitu alikuwa akitaka kukioanisha, lakini wenzake walikuwa na mtizamo wao, waliona kama ni kupotezewa muda.

 'Mimi hayo yote elimu yangu na elimu ya babu, nikaiingiza kwenye maabara, kuoanisha na sayansi yenye mshiko,nikakusanya data, nikatafuta vidhibiti, nikatengeneza kitu kinaitwa `sayansi base’…yaani tukio likitokea, wewe unaingia kwenye mtandao wako wenye maunganisho mbali mbali…, unaliunganisha tu…unakuja kupewa majibu kurahisi tu…’akasema

  'Nilipokutana na huyu msaidizi wangu,..alikuja kwangu kama mgonjwa.. nikagundua kuwa kwa kupitia yeye, naweza kuhakiki nadharia nyingine mpya, sio mpya ila nilishaigundua ila bado nilikuwa na ifanyia kazi,..na nilihitajia ukweli wa vitendo,…ulishawahi kuwasikia mafriimasoni..?; akauliza

‘Sana tu, sio kitu cha kuuliza…’akasema mpelelezi.

‘Ni wasomi hao, walikuja kujenga hoja, ya kuchukua mambo hayo ya asili…imani za dini na sayansi tuliyo nayo, wakaziweka kwenye utekelezaji wenye mshiko, badala ya hisia za kiimani tu…wakawekeza kwenye kuchuma mali.., na sasa wana miradi,…ni akili lakini wengine wanaitumia akili hiyo kuwathiri wanadamu wenzao, wengine wanaitumia kwenye maendeleo nk…’akatulia.

‘Kwahiyo wewe kwa uchunguzi wako, unawaamini hao watu kuwa ni waatalamu na wanautumia utaalamu wao kwa maendeleo au sio, na huenda wewe ni mwanachama wao pia…’akasema mpelelezi.

‘Hapana,...mimi sijasema hivyo, na pia mimi sio mwanachama wao,...ninachotaka  kukuelezea hapo ni chimbuko la watu kama hao, kuwa wanaweza kufanana na kundi hilo….’akasema docta

‘Ok, endelea…’akasema mkuu

‘Unajua niwaambie kitu, totafuti ya mwanasayansi na mwanasiasa,au mtu mwingine, ni kuwa sisi wanasayansi,..nadharia tunaziweka kwenye maabara,tunazifanyia tafiti, zenye mshiko,…halafu tunazihakiki kwenye uhalisia, kama zinafanya kazi kweli zikifanya kazi tumefanikiwa, zikishindikana tunrejesha tena kwenye maabara…’akatulia

‘Ok, kwetu sisi maaskari, hayo yote nibla-bla, tunahitajia muhalifu, na ushahidi wa uhalifu wake…ushahidi na mashahidi…unanielewa ndugu..’akasema mpelelezi,  sasa akiangalia saa yake.

 ' Sasa ni hivi, nilipochunguza hili tukio..nilipowachunguza wagonjwa , …binti na huyu msaidizi wangu..niligundua kuwa, matatizo yao,..ni kuchezewa akili ili watu fulani wapate kitu fulani…au wafanya jambo fulani, au wapate ushahidi fulani kuwa walichofanya ni sahihi kwa mtizamo wa macho ya wanadamu, na wasionekane wana hatia...’akasema

‘Ok…so..inakujaje hapo, hao ni wagonjwa, ..inakujaje na kuchimba makaburi, kukata viungo,…na …hebu weka vizuri hapo…?’ akauliza wakili.

‘Niliwaambia, hawa watu katika moja ya kufanikisha malengo yao wao sana wanamtegemea shetani, kwanza kwa jili ya vitisho kwa watu, lakini pili kuwatumi ahao amshetani kama wapelelezi wao, ili waelekezwe mambo fulani fulani, au kuiba mambo kwenye ufahamu wa watu wengine…sasa hivi wanatumia mitandao,..mitando hii hii ya kijamii. au sio…’akasema docta

‘Kwa vipi…?’ akauliza wakili.

‘Mfano ni huu..huyu msaidizi wangu aliweza kumpata mpenzi kwenye facebook,..huyu mpenzi, yawezekna yupo au hayupo lakini wanachokifanya hawa wenzetu, wanatumia digital, kuunda, mtandao…(network) ambayo humo wanakuwa n wanachama, na miongoni mwao ni watu wao…wanatengenza picha zeny mvuto..sawa si sawa..’akasema

‘Tuambie wewe…’akasema mpelelezi,

‘Kiukweli ukiona picha za namna hiyo, kama binadamu, picha yenye mvuto,..mtu mrembo, mnzuri, au yupo uchi, ana anafanya ufuska..utavutika kuiangalia sana…., ukiangalia hiyo picha sana akili yako inazama kwenye hiyo picha au hilo tendo, na hapo wanakuvuta akili yako na kuisoma akili yako…ni shetani kwa njia ya mtandao…’akasema docta

What…hiyo kitu haipo, sijawahi kusikia..?’ akasema mpelelezi

‘Lakini ulishawahi kusikia mashetani, au sio?’ akauliza

‘Hiyo ndio..’akasema

‘Sasa kwanini huu ushindwe kuelewa,..shetani, anaweza kupaa, anaweza kujigeuza vyovyote vile, sasa kwanini ashindwe kujigeuza picha..wewe unaiangalia picha, kumbe sio picha ni shetani..its, a logocal,….ndio maana mimi nalifanyia kazi hili..’akasema.

‘Ok, nikuulize swali, kwanini hawa …kwanini msaidizi wako, kwanini huyo binti, kwanini familia hiyo ya mzee..na kwanini wewe kama docta ulikuwa na fani yako nzuri tu, auchane na udocta wenye kuaminika, ujiunge na ….udakitari wa kienyeji…?’ akauliza wakili

‘Kitu muhimu uelewe…hawa watu wanaweza kuchukua mtu yoyote au..watu wenye masihali fulani…na sio kitu kigeni, kundi , au tatizo hili halikuanzia hapa, lilianzia Nigeria, kuna wasomi waliamua kushirikisha nguvu za giza na utaalamu huu wa kidigital, wakacheza na ubongo na hisia za watu…’akatulia docta.

 'Una uhakika, maana ukitaja Nigeria mimi nilikwenda huko, kesi za namna hiyo zipo nyingi tu..na huko uzunguni, wao hawajifichi, na wewe tu ukitaka mambo ya giza wapo wataalamu wana kibali, na wanalipa kodi…sasa huku kwetu…sijaelewa kwa vipi…wameweza kucheza na mtandao…?’ akauliza mkuu.

 'Ndio hivyo afande, wasomi nao wakiwa wengi bila kazi, watajiingiza kwenye fani zozote , wanaweza kutekwa na wenye pesa, kwa masilahi ya wenye pesa…na Nigeria ulaya sio mbali kwa mambo kama hayo, watu wanawasiliana, na mitandao imerahisisha mambo hayo…sasa kwa hili…hilo kundi limeshajikita hapa kwetu, lakini ni ngumu sana kuwanasa hao watu hivi hivi….’akasema docta

‘Kwahiyo…unataka kusema nini kuwa sisi kama polisi hatuwezi kuwakamata hao watu….?’ Akauliza mpelelezi.

‘Mtamkamata mtu kwa kumshuku, onyesheni vidhibiti hakuna, siku mbili tatu mnasema aachiwe.. si ndio hivyo,…ni kazi kubwa sana kuwanasa…sasa mimi nimegundua jambo..lakini sitaki kwanza mniingilie, ninachoomba kwenu ni kibali tu…kuwa nina haki ya kuingilia mitandao..nina haki ya kutumia vifaa fulani fulani nitakavyowaomba, ,…mkinipa kibali hicho, mimi nitatumia na ujuzi wangu tutawanasa hao watu, kwa uwezo wa mungu…’akasema.

‘Kibali….kibali gani, hasa, kama ni kibali halali,.. utapata, lakini lazima tujue ni cha nini, na kwa vipi…’akasema mpelelezi.

‘Usijali hilo tutaongea mkuu wako…’akasema docta na  mkuu akatikisa kichwa kama kukubali,…, na mara simu ikalia, …ilikuwa simu ya mkuu, na muda huo huo simu ya mpelelezi nayo ikalia, na wote wakapokea kila mtu kwa wakati wake.

‘Nini..unasema nini, imekuwaje,…haiwezekani…’akasema mpelelezi, na mkuu akawa anasema hivyo hivyo kwa upande wake.

Baadaye wote wakageukiana, na kila mmoja akionyesha mashaka, na wasiwasi…na mpelelezi akamgeukia docta sasa akionyesha uso wa kiaskari…

Nb: Naishia hapa naona ni ndefu kidogo.


WAZO LA LEO: Heshima ya mtu ipo pale pale..hata kama mnakuwa hamuelewani kutokana na itikadi fulani, mzee aheshimiwe kwa uzee wake, kiongozi kwa uongozi wake mkuu wa dini kwa sifa za dini yake, hata kama sio dini yako, lakini ana heshima kwa wanamuamini basi tusimvunjie heshima kwa vile hatumiamini na kuanza kumkejli au kumtukana, itakuwa sio uungwana, …na tukiishi hivi kwa kuvumiliana na kuheshimiana, bila kukashifiana, na kutukanana,..mtu kwa mtu, jirani kwa jirani, kundi kwa kundi,.. tutakuwa tumetimiza wajibu mkubwa wa hekima na busara.
Ni mimi: emu-three
Ni mimi: emu-three

No comments :