‘Mke wangu uwe na
subira, kiukweli tupo kwenye matatizo makubwa, sijui nia ya hawa watu nini…' huyu alikuwa mzee akiongea na mke wake ili kumshawishi , binti yake achukuliwe na watu wa usalama, haikujulikana wanachukua kwa madhumuni gani.
'Mke wangu, mimi
sijui nimewakosea nini hawa watu…wangeniambia wanataka nini niwape lakini
tuzidi kumuomba mungu tu…sasa nakuomba sana mke wangu uniamini..hebu twende nje
kidogo, nataka kukuagiza jambo…’akasema na wakatoka nje.
Mimi nilibakia peke
yangu , baadae nikapokea ujumbe wa maandishi kutoka kwa docta, alikuwa
akiniagiza mambo fulani fulani ya kufanya, …haraka haraka nikaingia chumba cha mabinti,
…nikaanza kutafuta hicho alichoniagiza docta;
'Laptop...'
'Ndani ya laptop hiyo niligundua mambo mengi, na ..mojawapo ni kuwa huyo marehemu alijiua kwasababu ya kunipenda...alipoona nina mtu mwingine, na hapo hapo ana mimba, akachukua hatu ya haraka ya kujiua..ndivyo, niligundua, lakini kutokana na maelezo ya laptop,
Lakini sigundua kuwa , kumbe yote hayo, maagizo yote hayo, yalikuwa ni mtego,..mtego wa kuninasa mimi,na kuinasa hiyo laptop, niligundua hayo nikiwa nimechelewa, kwani baadae nilikaribia umauti..
Tuendelee na kisa chetu....
******************
Docta akiwa kituoni, …ni kituo maalumu cha polisi, alihisi
mambo sio mazuri,..hakuelewa ni kwanini alikuwa akihisi hivyo, hakutaka kupiga
simu huko kwa mzee, kwa tahadhari, lakini kutokana na hiyo hali, ikabidi kwanza
ampigie simu msaidizi wake, lakini simu …haikupatikana…, akashangaa, sio
kawaida yake, akajaribu tena na tena, hakuweza kumpata msaidizi wake!, akaona sasa ampigie mzee, na yeye pia simu
yake ikawa haipatikani,…
'Mhh,…hapa kuna tatizo, sio bure, hii sio kawaida..nahisi kuna tatizo, sizani
kwamba askari walitoa amri watu hawa wazime simu zao, sizani…'akasema akijaribu
kupiga tena , na tena, lakini simu zikawa hazipatikani!
Alitaka ampigie simu afande, mkuu wa zoezi hilo ambalo ni la
siri kidogo, lakini akilini akaona sio vizuri, kwani kinachoendelea hapo ni
hisia zake tu,..
‘Sasa nifanyeje, na muda….muda ni kitu muhimu sana..’akasema
Baadae akamuendea askari wa hapo kituoni, walikuwa sio kwenye kituoni cha
polisi hasa, ni sehemu nyingine malumu ambayo haitambulikani kama kituo, ila huyo
mkuu wa hilo zoezi, aliichagua sehemu hiyo kama kituo maalumu chenye usalama,
kwa dharura kama hiyo..na kwa muda ule, Docta alikuwa kabakia kwenye hiyo
nyumba ikiwa na walinzi wawili tu. Mlinzi mwingine akaomba kutoka kidogo,
akabakia mlinzi mmoja.
Docta akiwa kwenye chumba chake,,…ndio akawa anahangaika
kumpigia msaidizi wake, na kwa upande mwingine wa chumba ndipo alikuwa kawekwa huyo
binti! Chumba alichokuwa kawekwa huyo binti , kilikuwa imara, na kilifungwa kwa
nje..
********
Inavyoonekana mkuu wa zoezi hili aliamua kuchukua hatua hiyo
baada ya docta kumuendea na kumuelezea hiyo
kadhia nzima, ya kuuwawa kwa binti wa mzee, na matukio yaliyokuja kutokea
baadae,
‘Ni kweli nimesikia taarifa hiyo kutoka kwa mkuu, lakini
mkuu anasema , kifo ch ahuyo binti ni mambo ya kimapenzi, wivu….na akanywa
sumu..hakutaka kunielezea zaidi…’akasema msaidizi huyo.
‘Lakini ni zaidi ya hayo afande, mimi nililigundua hilo
nikiwa kwenye kazi zangu za udakitari kama nilivyokuelezea, na nimegundua kuwa
kuna tatizo kubwa,..na huenda likazidi kuwa kubwa,…kama mlivyoona,
haya..biashara hiyo ya viungo vya binadamu, sio kitu cha kawaida…’akasema
‘Ndio maana nimetumwa kuja hapa..tutalimaliza hilo,
nakuhakikishia…’akasema msaidizi huyo.
Docta aliamua kuonana na huyo msaidizi badala ya mkuu
mwenyewe ambaye alikuwa katoka kidogo kikazi, na akaona huyo anaweza kuifanya
hiyo kazi zaidi ya mkuu wake, kwani hata hivyo, alishafikia hatua ya
kutokumuamini huyo mkuu wa hapo,..hasa kutokana na jinsi alivyoelezea mzee, na
hata kwa hisia zake mwenyewe docta, aliwahi hata kumuambia mzee, kuhusu hisia
zake hizo
‘Kuhusu hili tatizo,
hakuna mtu wa kumuamini, kwasababu tatizo hili, limegubikwa na watu wenye pesa,
watu wenye imani kazi za giza, za utaalamu wa hali ya juu, na wanatumia
vitendea kazi vya kisasa, na yote hayo wao wanayafanya kwa ajili ya pesa,…ni wtu
hawajli kuua,..wanakula nyama za watu, …damu n.k..ni binadamu wa ajabu sana..’docta
akamwambia mzee.
‘Umeyajuaje hayo yote..docta?’ akauliza.
‘Wakati wengine wanalala,…mimi napitia makabrasha mbalimbali...nawasiliana
na wenzangu huko ulaya, unajua huu uchunguzi wa kuoanisha mambo haya ya sayansi
na sayansi jamii,..inayohusiana na matatizo ya akili, siyafanyi peke yangu..’akasema
‘Ok, kumbe…’akasema mzee
‘Ndio, nipi mimi na wenzangu huko ulaya, na wao wanaifanyia
kazi hii, kuna wachunguzi wameenda huko Nigeria,…huko ndipo kwenye shida zaidi
ya mambo haya, na mwisho wa siku tutakutana tuunganishe uchunguzi wetu,..halafu
mimi mwenyewe bado naisomea hii kazi ili kupata ujuzi zaidi,…hii ni moja ya
masomo yangu, nafanya uchunguzi usiku na
mchana, ..natumia muda mdogo sana wa kulala, ..na kwa ajili hiyo nimeweza
kugundua mambo mengi sana…hasa kuhusu hawa watu..’akasema.
‘Na kuhusu huyo mkuu wa kituo hicho hapo mbele, …kiukweli mimi
simuamini, sina ushahidi wowote dhidi yake mungu anisamehe tu, , ila kwa jinsi
nilivyoongea naye awali na kwa jinsi alivyolichukulia hili jambo, sikumuelewa,
na hapo hapo akanitoka,..hili sio tatizo dogo, sijui kwanini hakulichukulia
maanani…’akatulia kama anawaza jambo.
‘Kiukweli hata mimi docta, …huyo mtu kanitoka,
…alivyolichukulia tatizo la kifo cha binti yangu, sikumuelewa hadi leo, unajua
ilifikia mahali nikaamua nifanye uchunguzi wangu mim mwenyewe..nimehangaika,
nikapata fununu fulani..’akatulia.
‘Wewe uligundua nini hasa..?’ akauliza docta.
‘Ni likuja kugundua hivyo hivyo, kuwa kuna genge la watu
wanatumia vitisho,…wanawarubuni mabinti…wanawaingiza kwenye biashara haramu…na
mabinti wengi wanajiingiza tu, wakipata matatizo wanaoumia ni wazazi…kiukweli,
awali sikuliamini hili, mpaka liliponikuta mimi…’akatulia.
‘Lakini mzee, unahisi binti yako na yeye aliingizwa huko, …?’
akaulizwa
‘Sasa huo ni ugunduzi wangu, nisingeliweza kuhakiki hilo
jambo moja kwa moja, ila nikaona niwaone hao watu wa usalama tuone kama
wanaweza kunisaidia,..na kingine ni kuhsu hii mitandao,…hii mitandao ya
kijamii, inawaharibu sana vijana wetu, na humo wahuni wameingiza mambo yao…’akatulia
‘Ehe…kama yapi..?’ akauliza docta.
‘Unajua niliwahi kushuhudia tukio moja wanapigisha video za
uchi…ni mbaya mbaya, wanasema wanatengeza video za kuuza,..hivi tumefikia huko…sasa
angalia wanaosimamia mambo hayo..sio sura zetu, sio watu wa maadili yetu ni
kama wametumwa kuja kuharibu…’akasema
‘Umeonaeeh…’akasema docta
‘Mimi nikamuendea huyo mkuu nikamuelezea wee, nikajua labda
kanielewa, lakini hakufuatilia, ila
alisema atafuatilia, ..na kuhusu tatizo la mtoto wangu nikamuelezea ni navyo hisi
kuwa kwanza tumpate huyo aliyempachika mimba, huyo huyo anaweza kuusaidia,
tukimnasa huyo, tukamshikisha adabu tutalimaliza hili tatizo,..’akasema
sawa..nikuambie kitu iliishia hapo hapo..ndio nikaamua kulivalia njuga mwenyewe
Nikapata taarifa nikamuendea, nikajikuta sasa mimi nipo matatani, maana nilienda nikamueleza nilichokigundua,
unajua alinisema vibaya ana, akaniambia, naingilia kazi yao, na sasa niifanye
mimi mwenyewe na kitakachonipata nisije kumlaumu,…’akatulia.
‘Umeonaeeh, hiyo kauli,, kwa nini alisema hivyo...?' akauliza docta.
'Alinieleze kidogo, kuwa hao watu, kuua kwao si mchezo, wana pesa, na wana elimu ya kujilinda, lakini pia wanatumi anguvu za giza, wanaweza kufanya mambo makubwa ya kumuharibu mwanadamu hata kwa kutumia mitandao...akaniambia hivyo...'akasema mzee
'Halafu ...?' akauliza docta
'Akasema ndio maana yeye analifanyia kazi hilo kwa makini ili aweze kulinasa kundi na kupata ushahidi wa kutosha…'akasema.
'Sasa...?' akauliza docta.
'Sasa...ndio miaka mingapo imepita, hakuna lolote, nikajua anatafuta njia tu za kupoteza muda, ...'akasema
'Unajua kauli yake ya lugha za kukutisha, ina maana fulani, yawezekana
alishagundua kuwa kuna watu wabaya, …au anajua jambo kama hilo, ila kuna kitu
kinamfanya ashindwe kuchukua hatua, sasa ni kitu gani,... pesa labda, au shinikizo fulani,.., au …anyway,
tusimshuku vibaya kihivyo, sasa najiuliza ni nani wa kutusaidia hapo…maana
inavyokwenda inabidi tuwashirikishe watu wa usalama haya mambo ni nyeti sana..’akasema
docta.
‘Hata sijui…’akasema mzee.
‘Sasa tutafanyaje, maana kiujumla hili sio tatizo dogo, na kama
kweli unataka hili tatizo liishie, inabidi tulifanyie kazi hasa, jiulize
kwanini wewe, una nini kikubwa mpaka wakaingia familia yako…, hii ina maana kubwa sana, kuwa wewe kwako, kuna mdudu mtu
anaitafuna familia yako, anakujua ,na anamasihali ya hilo jambo, sasa sijui ni nani, …sijui unanielewa.., na tunapokwenda ni lazima polisi
wahusishwe,…’alimwambia mzee.
‘Nakuelewa sana, lakini sizani kama ni ndani ya familia yangu, hilo halipo ila, huyo marehemu, mlinzi nahisi ndiye yeye, maana mimi nilimuamini sana, nilikuwa namuambi akaribu kila kitu, lakini mungu kamuumbua, umeona,..sasa nakuuliza mimi nifanyeje…’akasema
‘Mimi kwa ushauri wangu, ni lazima hili jambo tumpate polisi
ambaye atalifanya nje ya polisi..sijui unanielewa hapo..ni kuwa ni kweli polisi
wetu ni wazuri lakini anaweza kuwepo mmojawapo mbaya anatumiwa, kwahiyo hata
tufanyeje, ..kila hatu taarifa zinavuja na hao maadui wanazidi kutenda makosa..’akasema
docta.
‘Lakini utafanyaje hilo, ..bila mkuu au watendaji wake
wengine kujua.
‘Mkuu wa kituo, asihusishwe,..hilo linawezekana sio mambo
yote anayajua…, lakini matokeo yake yatakuja kuingia ndani ya polisi baadae na
yeye atajulishwa rasmi baadae wakati kazi imekwisha fanyika,,,…
‘Sasa kwa vipi maana hapa kichwa kimechoka..’akasema mzee
‘Ndio maana nataka mimi na wewe tushirikiane kwa hili, maana
linaweza kuifanya familia yako ikakuchukia,..lakini baadae wataelewa tu…na
siwezi kuiacha hii kazi, maana kama nimeianza hii kazi , nikiiacha na mimi
nitakuwa hatarini, na ni seehmu ya project yangu, ni kitu muhimu sana kwangu…’akasema
docta
‘Kwahiyo tufanyeje..’mzee akazidi kuuliza
‘Nataka kumpata askari ambaye unamuamini, kati yao , lakini
kiongozi ongozi hivi,,,wana viongozi wao sio sasa mmojawapo ambaye anaweza
kutoa amri kwa watendaji wake wawili , watatu…’akasema.
‘Mhh..hilo hata siwezi kukuhakikishia,…labda huyo mgeni
msaidizi wa mkuu, nahisi tukimtumia huyo, anaweza kuaminika,..ila ..kama
anawivana na mkuu wake tutakuwa tumelikoroga,bado itakuwa kazi ngumu…’akasema
mzee.
************
Ndio hapo, Docta
akamuendea huyo msaidizi wa mkuu wa hicho kituo cha polisi akamuelezea kadhia
nzima, na huyo msaidizi wake, akamwambia;
‘Unajua ndio maana nimehamishiwa hapa, na kiukweli sijapata
ushiriakiano wowote na mkuu wangu, ..ndio nimekuja na yeye akakumbwa na
matatizo y akifamilia, kwahiyo bado sijaweza kukaa naye tukaliongelea, au
kuongelea matatizo mengi ayaya hapa, nimekuwa nikipitia kesi mbali mbali,..na
mojawapo ni hiyo…
‘Kiukweli nahisi hapa kuna tatizo kubwa…, niliambiwa nilipopata
barua ya uhamisho wa kuja hapa na wakuu wangu..huko juu.., nia kubwa ni kuweza kulisafisha eneo hilo na
matatizo mengi yanayotokea hapa, hasa hili, la..imani za kishirikina na kuuza
viungo vya binadamu kwa imani hizo, madawa ya kulevya..ujambazi wa hali ya juu…imewatia
mashaka wakuu huko na utendaji wa hapaa…nakuambia hili, ..kwa madhumuni
maalumu..’akatulia
‘Nakuelewa sana afande..’akasema docta
‘Ninachotaka mimi , nikushirikiana na raia wenye nia njema,
ili tuweze kuligundua tatizo, na hasa kiini cha hili tatizo,..ni nani yupo
nyuma ya haya yote, ni tatizo na hatutaiweza mpaka kushirikiana na raia,..’akatulia
kidogo.
‘Mimi hapo ndio nakosana na mwenzangu, mimi utaratibu wangu
wa kazi ni kuwa karibu na raia, najua kutokana na wao nitaweza kuwagundua
wahalifu,maana wanaishi nao, wanawafahamu..sasa nashukuri kuwa wewe umekuja na
wewe ni docta, wanatu mnaoaminika kisheria…tutashirikiana kwa hili..’akasema.
‘Kwahiyo kwa hili utanisaidiaje..?” akauliza docta.
‘Nitakuambia cha kufanya, …kuna hatua nitazichukua
kiutendaji siwezi kukuambia moja kwa moja ni zipi…lakini kuna hatua za dharura,
lakini zinaweza zisiwe rasmi…baadae utaona matokea yake, wahalifu wote wa eeneo
hili watakamatwa tu…ni kazi ndogo wewe utaona tu, najua tatizo la eneo hili ni
kuwa wapo watu wana uwezo wa pesa, na hawa ni hatari,lakini tutapambana..’akasema
‘Nitashukuru sana afande,…sasa mimi nifanye kwa sasa, nikae
tu, au niendelee na hicho nilichokianza, kwasababu kama nilivyokuambia hata
mimi, nipo kazini nahis utanielewa nikisema hivyo, lakini siwezi kuifanya hii
kazi yangu bila kuwahussiha nyie, je unaniruhusu..?’ akauliza docta.
‘Kwanza nikushuru sana,..umefanya jambo kubwa na la hatari,
sasa nitakuwa na wewe sambamba..tutashirikiana kwa badhi ya mambo,..nitakuelezea
cha kufanya, lakini sio hapa kituoni, tutaonana mahali..’akasema huyo mkuu
Na docta akakutana na huyo afande baadae nje ya kituo,
wakashauriana, na lakini hatua zaidi hakuambiwa aliambiwa yeye asubiria na
afuate kile atakachoambiwa, hata kama kitaumiza hiyo familia. Na ndio tukio
hilo likatokea.
********
'Nahisi huko kwa mzee
kuna tatizo, hizi hisia sio bure,..’docta akawa anawaza akili haitulii, na
wakati anawaza hivyo muda huo yupo peke yake, na alipoona hisia hizo zinamcheza
chez asana kichwani, akaona asipoteze muda zaidi, kwa haraka akamuendea mlinzi
aliyebakia hapo, akamuambia alivyohisi.
'Kwanini, unahisi hivyo, hakuna shida, kaam kungelikuwa an shida
wangelikupigia, au wangewaarifu polisi, usiwe na dhana mbaya…?’ akasema huyo
askari akionyesha kuwa kachoka na usingizi.
'Nimepigia simu kwa msaidizi wangu hapatikani, simu ya mzee
halikadhalika..haipatikani, nahisi kuna tatizo, hisia zangu haziongopi afande…’akasema
docta.
‘Kwanini unahisi hivyo, na watu wapo nyumbani kwao, kama kuna tatizo watapiga wao, na simu kuzima
labda ni mtandao au umeme, si unajua umeme wetu huu wa kuunga uunga,..’akasema.
'Niamini mimi afande na tusipoteze muda…huko kuna tatizo, sasa usije kudharau
ukaja kujutia, au nimpigie mkuu wako niongee naye mimi mwenyewe..’akasema
docta.
‘Sasa ulitaka mimi nifanyeje,… mimi nimepewa kazi ya
kuhakikisha mpo salama, na msitoroke,…kazi nyingine hainuhusu mimi,… ok,…au
niambie ulitaka mimi nifanyeje…’akasema
'Hapa hakuna jinsi,..ufanyeje , wewe endelea na ulinzi wako,
lakini mimi inabidi niende huko..nikajionee mimi mwenyewe, ujue mimi ni docta
wa hiyo familia, na ninajua matatizo yao, inawezekana kuna tatizo, haiwezekani
namba zao wote zisifanye kazi…’akasema docta
'Lakini huruhusiwi wewe kuondoka hapa unaelewa,…sio kwamba sikuelewi, ila natimiza
wajibu wangu,..unakumbuka, mkuu wangu wakati anaondoka hapa ulisikia maagizo
yake, sasa wewe unataka kunifukizisha kazi, ..’akasema
'Mpigie bosi wako umueleze hali halisi,..na mimi niliwaambia muweke mlinzi pale nyumbani kwa
mzee, nyie mkadharau, mkasema hakuna tatizo kubwa kiasi hich kwenye hiyo
familia, sasa matatizo ndio haya yanaanza..’akasema docta.
'Ok,..ngoja niongee na bosi..’akasema na kuchukua simu yake ili ampigia bosi
wake, alifanya hivyo shingo upande;
'Ongea naye, lakini wakati unaongea naye, mimi ninaondoka, cha muhimu kwako, ni kuhakikisha
usalama wa huyo binti, na akizundukana hapo, ..ninajua kabisa itakuwa mshike
mshike, ..si umeona mwenyewe alivyo huyo binti, …imebidi tumpige hiyo sindano ya
usingizi kwa ajili ya kumtuliza, na hatuwezi kumpiga tena sindano ya aina hiyo ,
sasa uwe makini…
'Hebu kwanza unajua simu yangu hii,….mmh, lakini hebu kwanza nikuuliza, kama
akizindukana na akaanza kusumbua, tutafanyaje…maana ooh, nimechoka kweli, bosi
hataki kumleta mtu mwingine, na mimi nikapumzike kidogo, unajua leo siku ya
tatu, sijapata kukiona kitanda …?’ akauliza huyo askari, akionekana kachoka
kweli, kiukweli huyo askari alikuwa kachoka, alikuwa kafanya kazi muda mrefu
bila kupumzika, ilibidi aje askari mwingine kumpokea.
'Wewe ni askari,… huwezi kuniuliza swali kama hilo, ila angalizo kwa huyo binti,
huyo binti bado ni mgonjwa, msije kutumia nguvu yoyote, na jingine anaonekana
ni mjanja sana, ole wako akuhadae halafu atoroke, …huyo binti kwasasa ni
alimasi, anatafutwa na hao watu..’akasema docta.
'Nimekuelewa, ..'akasema huyo askari huku sasa akianza kumpigia bosi wake simu.
Na wakati askari huyo akifanya hivyo, docta hakusibiria, haraka haraka akatoka
nje, na mbio mbio.., akaelekea kituo cha bajaji.
Huku anatembea huku mawazo tele kichwani…
‘Sasa itakuwaje, huku huyu binti anahitaji
uwepo wangu, hataweza kutulia kama akiniona sipo, na hawa watu hawaelewi tatizo
hili lilivyo gumu, hawa watu nimeshawafahamu sana, ni hatari…na huyu binti kwa
hali yake, hatakiwi kuongezewa shinikizo la ziada, anaweza kuzidiwa, na
kupoteza fahamu tena, na ni hatari ikitokea hivyo mara ya pili, mmh, huu sasa
ni mtihani..’akawa anawaza huku anatembea.
‘Na pia nikifika huko
kwa mzee…najua kabisa mama akiniona tu, cha kwanza atauliza kuhusu binti yake, na kwa hivi sasa hata mimi sijui
kinachoendelea, hawa maaskari hawataki kunieleza ,,mmh sasa huyu mama nitamuambiaje…na hali kama hiyo itazidi
kumsononesha baba, ambaye hahitajii mawazao zaidi…inabidi nitafute njia ya
kulituliza hili …’akawa anawaza huku anatembea.
'Labda ningewaambia askari wafuatilie wao wenyewe…hapana kwa jinsi ilivyo…, hili
jambo sio la kuwaachia maaskari wengine litavuja, na mkuu akijua kinachoendelea
kabla hatujapata ushaidi anaweza kunifunga, na hawataelewana kabisa na msaidizi
wake…kwahiyo, ngoja niende huko huko, kwa mzee..’akajipa moyo huo..na sasa
akawa keshafika kituoni.
Docta akaingia kwenye boda boda, moja kwa moja hadi kwa Mzee.
Alipofika kwa mzee, akawa anasita hata kupiga hodi, kwanza alihitaji
atahadhari, maana hajui kinachoendelea huenda wanafamilia hao wamewekwa chini
ya ulinzi, na watu hao wasiojulikana, kwahiyo kwanza alichofanya ni kuvinjari,
kukagua na alipojirizisha, ndio akausogelea mlango.
Hakugonga, akafungua kwa haraka, oh, …,aliwakuta wanandoa wawili
hao mzee na mkewe, wakiwa wamekaa sebuleni, …na hali aliyowakuta nayo,
inaashiria kuwa kuna tatizo, la kutokuelewana au vinginevyo, maana mama alionekana kanuna kweli, baba yane kaka kwenye sofa,
lakini hakuegemea, ila kainamisha kichwa chini…na docta alipofungua mlango tu, wa
kwanza kusimama alikuwa mama;
'Binti yangu yupo wapi?akauliza mama huyo mama, akiwa na macho yenye kuhitaji
kupata jibu la haraka.
'Bado yupo kituoni, mimi.nimeomba ruhusa tu mara moja,…’akasema docta akigeuka
huku na kule, kama anatafuta kitu, na alipokikosa akasema
‘Msaidizi wangu yupo wapi..?’ akauliza
'Hatujui…’wakasema wote kwa pamoja mke na mume, na docta akazidi
kuchanganyikiwa, akatizama saa, halafu akasogea hadi dirishani akawa anaangalia
nje, …halafu akawageukiwa wawili hao na kuanza kuwahoji maswali;
‘Mama yeye hakutaka kuulizwa akakimbilia ndani huku akilia;
‘Binti yangu binti….’
NB: tunaendelea sehemu ya pili yake ya tukio hilo, kwenye
sehemu ijayo
WAZO LA LEO: Msomi mnzuri ni yule , kutokana na
elimu yake, jamii, inapata faida, na sio hasara, jamii inajifunza kutoka kwake,
kwa mema na sio mabaya. Elimu ya mapokeo isiyo na tija kwa jamii, inakuwa sio
elimu, bali ni ujuzi tu wa kuongeza jambo katika akili zetu, sasa basi tufikie
hatua tuone kuwa elimu yetu inakuwa ya vitendo, yenye tija kwa jamii, isiwe ya
vyetu, au kuhesabu kidato, iwe ya kuelimisha, kuleta mabadiliko yenye maana ,
kuzalisha na kuleta matunda yenye faida kwa jamii.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment