Yote haya yalianzia ndani ya facebook, pale nilipompata mpenzi kutoka kwa marafiki wangu wa facebook, na kutokana na jinsi alivyonivutia, kwa sura , umbile na jinsi tulivyokuwa tunaelewana kwenye kuchat, nikahisi yeye anaweza kuwa mpenzi wangu na sio mpenzi tu, bali mwenza wangu wa maisha.
Kutokana na historia ya maisha ya nyuma, nilikuwa nimeamua kutulia na kutafuta mwenza kwa njia nyingine tofauti na ile ya kuhangaika huku na kule, kwani nilishapoteza wapenzi wengi, kwasababu hizi na zile, na wengine niliachana nao kwa njia ambayo inaniumiza hadi leo,...
Mpenzi wangu huyu wa facebook, niliona ndiye chaguo halali, ndiye faraja yangu ndiye mtarajiwa wangu, lakini sikuwa nimekutana naye kabla, simjui ,, ila namafahamu katika mawasiliano ya mtandao
Ikafika muda wa kukutana naye uso kwa uso, ndio matatizo yakaanza kutokea...
Mara ya kwanza kanielekeza nikatokea makaburini, mara ya pili nikapata ajali, na hiyo ikanifanya niwe kama nimechanganyikiwa...wengine wakasema kuwa huyo mpenzi wa facebook, sio binadamu ni shetani, je ni kweli ni shetani...mimi sijui,
Nikawa nimeandamana na docta mtaalamu, akiwa bingwa wa magonjwa ya kawaida ya akili, na pia akiwa mtafiti wa madawa asilia, ikiwemo hilo la kuchanganyikiwa, ...akaamua kuandamana na mim ikiwa ni moja ya tafiti zake, na katik ahiyo safari ndio tukaanza kugundua mengi yaliyojificha...
Mpenzi wangu wa zamani ambaye niliachana naye kwa njia isyo nzuri, ambaye niliwahi hata kuahidiana naye kuwa nitamuoa, lakini kwa mara ya mwishi nikamtelekeza, ...kumbe alishafariki na kufariki kwake, ni kwa kusikitisha, kwani eti alijiua, na walikuja kugundua kuwa alikufa akiwa mja mnzito, je hiyo mimba ilikuwa ni ya kwangu, yasemekana hivyo...kuwa kujiua kwake ni kutokana na mimi kumkataa, ..wakati alishajiaminisha kuwa mimi ndiye mpenzi wake, mimi ndiye mchumba wake, maana nilimuahidi mbele ya kadamnasi na kumvisha pete..
Dhuluma hii niliyomfanyia huyu binti haikuishia kwa binti huyu kujiua tu, ikaendelea kuitafuta familia isiyo na hatia,..mdogo wake binti, baba wa binti, na sijui mama itakuwaje...
Kwa hali hiyo nikajiona mimi ni mkosaji, lakini nitawezake kuikabili hiyo familia, maana baba wa binti ni mkali ajabu, na alishaapa siku ya kukutana na mtu aliyemharibu mtoto wake, ni ama zake ama huyo mtu..sasa nifanyeje,
Na wakati nawazia hilo kunatokea taarifa, kuwa mzee Mashauri, yaani baba wa binti niliyemtenda hadi kuamua kujiua, na binti (mdogo wake huyo marehemu) wapo mahututi hospitalini...kisa ni ile ile dhuluma niliyoifanya...
Tuendelee na kisa chetu..
***************
Tulijikuta tumefika hospitali, na
tulipofika hapo, tukawa tunaangalia huku na kule kama tunaweza kumuona mtu
tunayemfahamu hususani yule mzee tuliyekutana naye awali. Kufika kwetu hapo
ilikuwa ni kutokana na aliyopokea docta kutoka kwa huyo mzee…
Wakati wanaongea na huyo mzee, mimi
nilitega sikio kujua ni kitu gani kimetokea tena huko, na mara kwa mara Docta
alikuwa akinitupia jicho, na kuzidi kunipa wasiwasi, nikajua kuwa jambo analoliongelea , linaweza likawa
linanihusu na mimi na alipomaliza kuongea na simu akaniambia;
‘Kuna tatizo…’akasema
‘Tatizo gani docta..?’ nikauliza
nikiwa na hamasa ya kulifahamu hilo tatizo.
‘Mpenzi wako wa facebook, anazidi
kutuingiza ndani ya kiini cha tatizo…’akasema huku akiangalia mbele kama
anamtizama huyo mpenzi wa facebook
‘Sijakuelewa docta…’nikasema
nilipomuona kabakia kimia, na nilipomuuliza hivyo akatizama saa yake halafu
akasema;
‘Yule mzee kanipigia simu kuwa, Mzee
Mashauri kadondoka, na kupoteza fahamu…na ni kutokana na hali ya mtoto wake
kuzidi kuwa mbaya zaidi…’akasema docta.
‘Sasa kwanini akakupigia wewe, na..tufanyeje
docta…?’ nikamuuliza.
‘La kufanya ni kuenda huko…na
kanipigia simu kwasababu anasema wananihitaji,…’akasema.
‘Oh, wanakuhitajia kwa vile wewe ni
docta au kuna jingine zaidi ya hilo..?’ nikamuuliza.
‘Sijajua,…tutajua tukifika huko…’akasema.
Sikuwa na la kufanya ikabidi
niongozane na docta hadi hapo hospitalini.
*************
Ndipo
huyo mzee akajitokea, na usoni kwake kulielezea kila kitu, …kuna jambo nzito, …alitujia
na kwa haraka akasema;
'Aheri umekuja docta,…docta ilibidi nikupigia
simu baada ya kujulishwa kilichotokea kwa rafiki yangu, mara nyingie wamekuwa
wakiendelea na matatizo yao bila kunihusisha kama ilivyokuwa zamani, lakini
hili lilipotokea ikabidi waniite kwa haraka…’akasema akimuangilia docta.
‘Ok niambie ….najua ni tatizo, lakini
akilini nawazia, mimi nahusikanaje na hili tukio, kama docta au kuna jingine…’akasema
docta.
‘Unajua sasa ndio nimeanza kukumbuka
vyema, … wakati tunaongea na familia ya Mashauri maana mashauri mwenyewe yupo
kwenye hali mbaya…, kuna mtu mmoja alikutaja..Docta wewe ni maarufu
sana….’akasema
'Ehe, alisemaje ni kuhusu ugonjwa au kuna jingine…? ‘ akauliza swali hilo tena .
'Ni kuhusu ugonjwa, hususani tatizo la huyo binti, maana kutokana na hilo
tatizo ndio likamsababisha hata baba kuzidiwa,..alishaanza kuumwa umwa, lakini
tatizo la binti yake limezidisha matatizo..uzee nao mtihani…’akasema.
‘Oh poleni….’mimi nikajikuta nimesema
hivyo.
‘Kiukweli hali yam zee ni mbaya sana,
na yupo chumba cha wagonjwa mahututi, na docta anayemshughulikia, niliongea
naye, akaniambia nijaribu kutafiti kuwa mzee ana tatizo gani, huko kwenye
familia…
‘Kiukweli sikumjibu docta kuhusiana
na matatizo ya nyuma, maana sijui, huenda kuna mengine zaidi. Unajua
ukishafikia uzee, hutakiwi kuongezewa mizigo ya matatizo, akili imeshachoka,
sasa wasiojua wanataka kila tatizo kwa baba , kila tatizo kwa mzee,…hili ni
kosa, uzee unatakiwa upunguziwe mizigo ya matatizo….sasa watoto na akina mama
wanatakiwa kuliangalia hili sana…’akasema
‘Na akina mama nao wanakuwa na
matatizo hayo pia,..wanakuwa wazee pia, au sio, sasa usiseme akina mama wawe waangalifu kwa waume wao, pia wakina baba na wao wawe waangalifu kwa wake zao, uzee una mitihani yake,..muhimu ni kwa watoto wawe makini sana kwa wazazi wao, wasiwabebeshe mizigo mingi wazee wao, kwa kujiingiza kwenye matatizo, kwa kudai mambo juu ya uwezo wa wazee, au kuwaletea wazee wao matatizo au sio…’akasema docta.
‘Ni kweli…’akasema huyo mzee.
‘Sasa ndio hivyo, lakini docta
nilichokuitia hapa, sana sana ni huyo binti….’akasema.
‘Kwa vipi, huyo binti ana tatizo gani kubwa sana zaidi ya baba yake…?’ akauliza docta.
‘Hali ya huyo mtoto imezidi kuzorota
siku hadi siku,..na tatizo hilo ndilo linamuangamiza sasa rafiki yangu, sasa docta tafadhali
sana, tunahitaji msaada wako, ..'akasema huyo mzee akionyesha ishara ya mikono
kumuomba huyu docta.
'Mimi sina shida, japokuwa mimi sipo kwenye ajira
za serikalini kama docta, unajua mimi nilishajitoa huko muda mrefu,..na hapa
tupo kwenye hospitali ya serikali, mnajua sheria zilivyo…mimi nina hospitali
yangu huko mikoni ya binafsi, na matibabu yangu yamekuwa ya mchanganyiko sasa
sijui tutafanyaje hapo…’akasema docta.
'Ndio maana tunakuhitajia wewe, kwasababu wewe
unaangalia kote kote, tiba za kawaida na tiba mbadala…tunahisi matatizo ya huyu
binti, hasa….zinahitajia utalamuw ako zaidi..na nilivyosikia wewe upo tayari
kujishirikisha kwenye tiba za asili…’akasema.
‘Sawa
ni hivyo japokuwa sijabobea sana kwenye utaalamu huo bado nafanya tafiti zangu….lakini
hakijaharibika kitu, …., muhimu kwanza ni kuwaona wagonjwa, ..lakini muhimu ni
kujua historia ya tatizo,…sasa nikuulize ni nani hasa anatakiwa kuwa mgonjwa
wangu mzee mwenyewe au binti au wote
wawili…..?’ akauliza
‘Hapana
kwa mzee tatizo lake ni la hospitalini,…kama walivyompima wanasema kapatwa
shinikizo la damu…’akasema.
‘Mhh…nazani
tatizo la mzee inawezekana kabisa linatokana na huyo binti, na jinsi
ulivyoongea hawa wawili wana tatizo linaloendana, ina maana ili mzee apone,
inahitajika binti awe amepona, au sio..?’ docta akasema kama anauliza.
‘Ndio
maana tukakuhitajia wewe…’akasema huyo mzee.
‘Hebu
niambie ilikuwaje kwa huyo binti,…mpaka mzee anadondoka …kumetokea nini zaidi,
binti alizidiwa au kulikuwa na sintifahamu kati ya binti na mzee…?’ akauliza
docta.
‘Ni
kama nilivyowaambia tatizo lilianzia pale huyo binti alipopewa taarifa ya kuwa
ndugu yake kafariki, hakuamini, akachukua gari akitaka kwenda kuhakikisha,…
sasa wakati anaelekea huko hospitalini, akayumba, anasema aliona kitu,...na taarifa nyingine zinasema eti alimuona dada yake,....lakini ni katika hali ya kuchanganyikiwa na ndio akapata ajali…
Sasa
ajali hiyo ikazua mengine, maana aliathirika uti wa mgongo, lakini tatizo hilo
likaenda mbali zaidi, akawa kama anachanganyikiwa, kila mara anamuona ndugu
yake, na akimuona anakuwa akipiga ukelele, ndugu yangu huyu hapa, ..ndugu yangu kwanini unaniacha, mara, ndugu yangu hajafa,
yule pale…..kwahiyo imekuwa hivyo, …’akasema.
'Ok...sasa mimi nitawezaje kumuona huyo mgonjwa,
maana yupo kwenye mamlaka ya hapa hosp..na siwezi kuanza kumsikiliza au
kusikiliza taarifa zake bila kumuona, na kuwaona watu wake wa karibu ni jambo
jingine…, je yeye mwenyewe anaongea?’ akauliza.
‘Mhh..kuongea
imekuwa ngumu, …anaweza kuongea lakini ni kwa uchache zaidi….anayeweza kuelezea
yote kwa undani ni mama yake, maana baba yake hali ndio hiyo, kapoteza fahamu
na sasa yupo kwenye chumba cha wagonjwa mahututi, mama alivyo utamuonea huruma,
analia mpaka basi, sijui kama unaweza kuongea naye…’akasema.
‘Oh….sasa
hilo ni tatizo…’akasema docta na mimi pale nilipo nilihisi maumivu ..nilijiona
ndiye mkosaji ndiye chanzo cha hayo yote, nikawa nimeinama chini tu.
‘Sasa
tufanyeje docta , maana niliwaambia ninakutafuta…’akasema huyo mzee.
'Sio tatizo,…maana chanzo na sababu zipo wazi,…muhimu
ni jinsi gani ya kuliweka kwenye mizani hili tatizo, ili wote walipokee na
kulikubali…na…muhimu nipate muda kwanza wa kujua matatizo yote hayo kwa kirefu,
na …sijui tufanyaje, maana kuna vipimo vingi natakiwa pia nivichukue kwa huyo
mgonjwa,….’akasema.
‘Hilo
sio shida docta…, tumeshaongea na docta wa hapa, kasema anakufahamu, na alikuwa
mbioni kutushauri tukutafute, yeye keshakuruhusu uje uonane na hao wagonjwa
hasa huyo binti ...’akasema.
'Ok, itakuwa vizuri nikionana na huyo docta pia, kuna mambo ya kitaalamu tunatakiwa tujadiliane
mimi na yeye….kwahiyo unasema baba yake alipoona mtoto wake kazidiwa na yeye
akadondoka na kupoteza fahamu, si ndio hivyo..?’ akauliza.
'Mhh, ndivyo nilivyoambiwa, unajua tokea dada yake afariki amekuwa huyo binti
amekuwa mtu wa ndani, hawezi kutembea, mpaka kushikiliwa, walivyompima awali,
wanasema, pamoja na ajali, lakini pia alipatwa na mshtuko, ndio maana hayo mengine yanakuja kutokea,
unajua tena, wengine wanakimbilia kusema alipatwa na mashetani, sasa hatujui,
ni wewe docta unaweza kutusaidia kwa hilo….’akatulia.
‘Ok…mimi
nimekuelewa, na nashukuru nipo na kijana wangu hapa, atanisaidia sana, hasa
kuhusu huyo binti…’akasema anikiangalia mimi na mzee naye akaniangalia na
kutikisa kichwa kama kukubaliana na yeye.
Mimi
sikujua docta ana maana gani, nikahisi ni katika hali ya kunifanya nisiwe na
wasiwasi au ili watu wasijiulize kwanini naongazana ongazana na yeye.
‘Sasa tunaweza kwenda kumuona huyo binti sasa hivi…?’akauliza
docta na aliposema hivyo mimi moyo ukaanza kunidunda dunda…
‘Ngoja
tusikie docta atasema nini, ….au..?’ akasema huyo mzee.
‘Sawa…maana
wepesi wa hili jambo lifanyike kabla mzee hajazindukana ili akipata unafuu
asikie maendeleo ya binti yake…’akasema docta.
‘Unahisi
itachukua muda mfupi kwa huyo binti, kurejea kwenye hali yake maana wanasema
hivi sasa ndio hajiwezi kabisa…?’ akauliza huyo mzee, na kabla hajajibiwa ndio
akaja matu na kusema;
‘Mzee
unaitwa…..ndani haraka’, na huyo mzee akasimama, na kumuangalia docta, kama
vile anataka kusema waongozane.
‘Wewe
nenda kwanza kasikilize wito…’akasema docta, na huyo mzee akaondoka kwa haraka
kuelekea huko alipoitiwa, na mimi pale niliposimama nilihisi mwili ukiniisha
nguvu, miguu ilikuwa haina nguvu, sijawahi kujisikia hivyo kabla.
Tulibakia pale mimi nikiwa sina amani, nilianza
kujilaumu sana, nikijutia yale niliyowahi kuyafanya, sikujua matendo yale,
ambalo kwa wakati ule nililifanya nilijua ni mambo ya kawaida tu, kumbe mambo
yale niliyokuwa nayafanyia wenzangu, watoto wa wenzangu, yamekuwa ni matatizo
makubwa, na pia sikujua kuwa rafiki yule wa facebook angeliweza kunisukumia
kwenye hili tatizo.
‘Je
rafiki huyo wa facebook anahusikanaje na haya matatizo… maana hafanani kabisa
na huyo marehemu…sasa iweje ajiite jina la marehemu, na kujifananisha kila kitu
na marehemu…’nikawa najiuliza.
‘Siwezi
kukubali kuwa eti sio binadamu, hilo siwezi kamwe kulikubali..’nikasema.
‘Oh,
mungu wangu kwanini haya matatizo yaniandame, ina maana ndio mwanzo wa adhabu
yangu, …nifanyeje mungu wangu kuliweka sawa hili tatizo, najua nimeshakosa kwa
huyo marehemu, najua hiyo ni adhabu naisubiria lakini haya yanayoendelea
nitafanyaje ili niweze kuyasimamisha..jamani,…oh mungu wangu nimekosa, nimetubu…’nikasema
nawaza sasa nikitaka hata kuinua mikono juu kutubu.
‘Oh, mola wangu,wape subira hao niliowakosea, na kama kuna adhabu,
inayonifaa hapa dunia, basi nipatie tu, ili iweze kuwapa faraja hao
niliowakosea…namuonea huruma mama wa watu hapo alipo analia, alikuwa akimlilia
marehemu , sasa analia ….oh mungu nifanyeje sasa jamni…’nikasema huku
nikizungusha zungusha kichwa maana nilikuwa sasa nimechanganyikiwa.
Kitu
cha ajabu tokea siku ile nisikie kitu kama sindani ikichoma kichwani mwangu, na
kupata maumivu ya kichwa,..ilikuwa kama nimezibuliwa kutoka ndani ya maji,
masikio yalizizima na baada ya hapo sijawahi kuona yale marue rue, na ila hali
y akumuota huyo binti wa facebook, ikawa imeanza kupotea…
Sas
haya…..nikahika kichwa na kuzama kwenye mawazo ya kumuomba mungu…
‘Mungu
wangu, najuta na hayo niliyoyafanya, unajua madhaifu yetu sisi wanadamu, na
sikujua kuwa katika kutenda vile nitakuwa nimewakosea watu kwa kiasi hiki
kikubwa, nashukuru kuwa umenionyesha athari za dhuluma, jinsi gani
inavyosambaa, lakini mungu wangu nitafanyaje ili kuzuia athari hii isizidi
kuendelea,…’niliposema hivyo nikageuka kumuangalia docta huku macho yakiwa
yamejaa machozi.
Kiukweli chozi lilinitoka, nilishindwa kujizuia.
Niliinua macho yaliyojaa machozi na kumuangalia
docta, kumbe docta naye alikuwa akinichunguza, nilipomuangalia macho yetu
yakakakutana, akatikisa kichwa.. kama kukubali au …, sikujua kutikisa
kichwa,kule ilikuwa ishara ya kukubaliana nami, au ilikuwa,kunisikitikia, mimi nikagauka
upande mwingine na machozi yakawa yanaendelea kutoka kama maji.
Niliwaza
mengi, na kwa mara ya kwanza nilianza kuhisi woga, woga kwa hayo yanayoweza
kutokea, maana kama hali ya huyo mzee ipo hivyo, je ikiwa mbaya zaidi,
itakuwaje, na je matatizo kama hayo yakihamia kwa huyo mama….oh, sitaweza
kuvumilia,….mungu wangu nitafanyaje ….
‘Potelea
mbali, mimi sasa nitakwenda kujitambulisha lolote liwalo na liwe, haya ni
makosa yangu inabidi niadhibiwe,,…’nikajikuta nikisema kwa sauti, na mara
nikahisi mtu ananishika begani…
‘Upo
tayari kuadhibiwa…?’ nikaulizwa na mimi bila kumuangalia aliyenishika bega
nikasema.
‘Nipo
tayari…’nikasema na huyo mtu aliyenishika bega, akaniachia, nikainua kichwa
kumuangalia,..hutaamini sikumuona mtu, nikaangalia pale alipokuwa kakaa docta,
nikamuona docta akiwa anaongea na yule mzee, kumbe yule mzee alisharudi, kumchukua
docta wakati mimi nimezama kwenye mawazo,…na kwa muda huo yule mzee na docta wakawa wanatembea kueleka huko walipolazwa hao
wagonjwa.
Nikawa
sasa najiuliza niwafuate au nisubirie pale…
Lakini
ni nani huyo aliyenishika bega…nikageuka
huku na kule hakuna mtu aliyekuwa karibu na mimi…nikaanza kuhisi kuwa sipo peke
yangu, nikageuka huku na kule…
‘Ni
nani wewe…?’ nikauliza, sikuona mtu ila nilihisi kuna mtu yupo karibu yangu..
NB:
Samahanini nimechelewa kuiandika sehemu hii kutokana na mitihani ya hapa na
pale.
WAZO LA LEO: Mungu ni mwingi
wa rehema, anatujua nafsi zetu , na inapofikia kuwa kweli mja wake katubia
makosa yake, anamjua , na kusamehe kwake sio tatizo, lakini je ni kweli
tumetubia ukweli wa kutubia, hapo ndio taizo,..Tumuombe mungu wetu atusamehe
makosa yetu yalipopita na yajayo kwani mitihani ya dunia hutufanya tujiingize
kwenye makosa mengi, …
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment