Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, April 12, 2017

MPENZI WA FACEBOOK-3


Nilikuwa mlevi wa facebook, nikawa na marafiki wengi tu, na kati ya hao, nikabahatika kumpata mmoja,ambaye nilimpenda sana, ...tuliwasiliana naye sana, tukajuana lakini kwa kupitia mtandao, tukawa tunatumiana picha, mpaka ikafikia mahali nikataka nikutane naye uso kwa uso...

Kukutana naye ikawa ni tatizo, awali alinielekeza na ramani aliyonipa, nikajikuta natokea makaburini,...mimi nikajua kakosea tu, nikamuomba anielekeze tena, ili nifike tuonane naye, nikiwa na hamu ya kumuona, na ikibidi tufunge ndoa

Sasa safari ya pili, ndio ilinifanya nichungulie kaburi, ...Kwani tukiwa ndani ya basi, nikiwa nimekaa kiti cha mbele, nilimuona paka mkubwa akikatisha barabara,...dereva alimuona, na hakutaka kumkanyaga, au sijui kwanini,....akafunga breki...

 Mimi nilishangaa maana pale nilipokuwa nimekaa, na muda huo, nilikuwa nimeufungua mkanda nikijua nakaribia kuteremka, ....sasa ile hali ya kufunga breki kwa ghafla, nilijikuta nikirushwa mzima mzima,...na kiichwa  kikaenda kugonga kwenye kiyoo cha mbele…

 Na ajabu iliyoje, nakumbuka,  wakati mimi narushwa  kuelekea kwenye kioo cha mbele cha hilo basi ..mbele yangu nilimuona huyo mdada akijitokeza na tabasamu lake ....tabasamu lake ni maridhawa,...huku akionyesha mikono ya kunipokea,...wawawaaaah, halafu akasema ‘mpenz wangu karibu…karibu nyumbani kwetu…’ na hapo giza likatanda usoni, sikujua kilichotokea baadae.

Baaadae ndio nikaanza kuona mauza uza

Tuendelee na kisa chetu...

***************

Nilikuwa kati kati ya mijitu ya kutisha, unajua kutisha…mimi huwa na hulka yangu, sina uwoga, ni kawaida yangu kutokutishika na jambo lolote, nashukuru kwa kuwa na ujasiri huo, lakini mbele ya hiyo midude, niligwaya,….ni watu waliokufa, unaona kabisa mifupa na miili yao ikiwa na mabaki na nyama,.

Wakawa wananifuata pale nilipokuwa nimekaa kwenye laptop yangu nikichat na mpenzi wangu,  na kila walipotaka kunikaribia kukawa kunatokea sauti ya ukali…ya kuwazua..

‘Msimguse huyu mtu bado hajakaribishwa huku,…’sauti ya kike ikasema, sauti ninayoitambua vyema, sio ya mwingine bali ni ya mdada wa facebook, mpenze wangu.

Mimi,…nikataka kugeuka kumuona huyu anayeongea, na mara kidole changu kikawa kinaandika…unajua ni kitu cha ajabu yaani pale naandika kwenye laptop, kama kawaida, nachati kama kawaida, lakini vile ninavyoviandika na kuchat navifanya kivitendo…

Niliandika kuwa nimemtembelea binti, na nipo nyumbani kwao, nikapokelewa na mijitu ya ajabu haielezeki, na aliyenipokea alikuwa binti wa face book, lakini kwa muda huo alijifunika kabisa, sikuweza kuiona sura yake..naandika na kweli nipo naye..

‘Mbona unajificha, hutaki nikuone..?’ nikamuuliza huku nikijaribu kugeuza kichwa kuwaangalia hiyo midude ya ajabu, lakini kichwa kilikuwa hakitaki kugeuka…

‘Nafanya hivi kwasababu mimi sasa ni mchumba wako, hutakiwi kuniona sura yangu mara kwa mara…ni mila na desturi za kwetu…’akasema

‘Wazazi wako wapo wapi..nitawaona saa ngapi?’ nikamuuliza

‘Hutaweza kuwaona hapa…kama mambo bado basi ipo siku utaonana nao…nahisi kama vile muda wako bado…’akasema kwa sauti ya huzuni.

‘Muda gani huo…?’ nikauliza

‘Sijaelewa hata mimi, sijui kwanini wanakuchelewesha hivyo..’akasema

‘Akina nani hao wanaonichelewesha…?’ nikamuuliza

‘Hata mimi sijui…lakini nimeshaomba kibali,…sasa sikiliza…’akasema na akawa anaangalia pale ninapoandika kwenye laptop…

‘Inatakiwa kauli yako, kuwa kweli wewe upo tayari kunioa, na upo tayari kuja huku kuishi na mimi…sasa andika hapo kwenye laptop yako, …mimi, unataja jina lako nimekubali na nipo tayari kuja huku na kuishi na mchumba wangu ambaye nitafunga naye ndoa, na kuwa mke wangu…nipo tayari kufuata masharti yote, na ikiwemo kuhama huko duniani….’akatulia

‘Kuhama duniani, kwani huku ni wapi…?’ nikamuuliza

‘Wewe anza kuandika hivyo nilivyokuwambia….’akasema na mimi nikawa naanza kuandika, na mara sikioni nilisikia kama mtu ananinong’oneza…’usiandike ukiandika utakufa…utakufa…utakufa….’ Na muda huo nilishaandika sehemu…nipo tayari…’

Ghafla nikashutuka…..

****************
 Kumbe nilikuwa kwenye kupoteza fahamu na nilizindukana, baada ya siku tatu, nilifungua macho huku nikihema kwa nguvu, nilisikia sauti ikisema,..lete hiki, fanya hivi…kumbe walikuwa wakinifanyia huduma ili niweze kuzindukana, kwani ilionekana nipo kwenye mshtuko….
Baadae nikatulia, na kuanza kufungua macho….taratibu, niliwaona watu warefu ajabu, kila aliyekuwa mbele yangu alionekana mrefu…na kila muda ulivyopita ndio taswira za watu zilianza kuonekana vyema..na baadae akili yangu ikawa sawa..

 ‘Hatimae amezindukana…’nikasikia sauti ikisema, niligeuza jicho na kumuona huyo mtu akiwa kavaa nguo nyeupe na mdomoni kavaa kitu …awali sikujua ni kwanini, lakini baadae akili ilivyotulia ndio nikafahamu nipo kwenye chumba cha wagonjwa mahututi…,

Nilikuwa nimefungwa mabendeji mengi kichwani…na shingoni kiasi kwamba sikuweza kugeuza shingo, naangalia kwa kuzungusha macho..

Masaa kadhaa yakapita na ikawa sasa najitambua, japokuwa akili bado ilikuwa haijakaa sawa, na akaja docta na kusema;

‘Umeponea tundu la sindano, una bahati ubongo haukuathirika…’alisema docta
Ubongo, ubongo wangu ulifanyaje…nikawa najiuliza na kujaribu kukumbuka kilichotokea huko nyuma, lakini bado akili ilikuwa haitaki ….sikumbuki kitu…

‘Oh, tunashukuru sana docta…’sauti nyingine zikasema pembeni mwa kitanda.

‘Lakini bado unahitajika kukaa hospitalini kwa muda, kwa ajili ya uchunguzi zaidi…’ akasema docta

Kiukweli kwa muda huo nilikuwa sikumbuki kitu, nilikuwa kama zezeta fulani , kichwani hakuna kitu, ni boksi lisilo na kitu, nikawa naitikia tu, kwa kujiaribu kutikisa kichwa lkn kichjwa hakiwezi kusogea….wiki nyingine ikapita, nikawa naanza kukumbuka kumbuka baadhi ya mambo, lakini nilikuwa bado sijajielewa vyema,…baadae ikabidi niruhusiwe kutoka hospitalini, japokuwa bado nilikuwa nipo nipo tu.

Matibabu yangu yaligharimu pesa nyingi sana, na bado nilikuwa nahitajika kufanyiwa uchunguzi wa mara kwa mara, na ulikuwa ni gharama kubwa, kwa muda huo sikujua kuhusu gharama au kinachoendelea, jamaa zangu ndio walikuwa wakichukua pesa kwenye amana zangu na kunifanyia matibabu,…gharama zilizidi wakakubaliana wauze gari…mimi naitikia kwa kichwa tu…

Gari, kwani mimi nina gari…nikawa nawaza hivyo

Baada ya miezi mingi kupita sasa nikaanza kutoka nje, na kutembea tembea,..lakini cha ajabu nilikuwa nikianza kutembea na tembea wewe mpaka napotea, na watu wananitafuta na kunirudisha nyumban, wanasema kila mara nawaambia kuwa namtafuta mpenzi wangu wa facebook, na mara kadhaa wameniona nikielekea huko …makaburini, lakini nawahiwa kabla sijafika mbali.

Hali ikaanza kubadilika, nikawa sasa nachanganyikiwa napiga ukulele, naanza kuvunja vunja vitu, ikawa mshike mshike, nikalazwa hospitalini mara kadhaa, na baadae wazee wakakutana wakaone wanipeleke huko kijijini.

‘Huyu sasa anahitajia tiba mbadala…’akasema mzee mmoja, na baada ya mashauriano ikakubalika hivyo, mimi sikuwa na la kusema lakini kawaida yangu, siamini hizo tiba mbadala, mimi najua tiba sahihi ni za hospitalini.

Huko kijijini nilitibiwa sana, na nakumbuka siku moja alikuja mzee mmoja akaniambia

‘Wewe uliwahi kuwa na mahusiano na mwanamke usiyemfahamu vyema, ambaye hujawahi kukutana naye kabla..ila mnakutana naye kwenye ndozi, au kwenye namna nyingine yoyote lakini sio kwa uso kwa uso?’ akaniuliza

Kipindi hicho nilishaanza kuelekea vyema, kama kupona pona, japokuwa ki akili nilikuwa bado sijafikia kurudi kwenye hali yangu ya awali, mtu akiniona hivi atajua nina walakini kichwani, ..niliweza kuongea na watu, lakini inafika wakati mwingine nakuwa kama nipo kwenye dunia nyingine, naanza kuongea na watu wasioonekana.

‘Mhh..nakumbuka …nina mpenzi wangu wa facebook, kila nikipanga kukutana naye inatokea tatizo na tatizo la mwisho ndio hili limenifanya niwe hivi..’nikasema.

‘Basi huyo huyo ndiye anayeutaka mwili wako baada ya roho yako kutoka…’akasema

‘Kwanini..?’ nikauliza kwa mshangao, maana mimi nijuavyo mtoa roho ni mungu, sasa huyo mtu anayeutaka mwili wangu ....nikiwa mfu anataka nini, niliwazia kuwa hayo yatakuwa ni mambo ya kishirikina tu, ambayo mimi siyapendi na wala siyaamini, ndivyo nilivyo, siamini mambo mengine kinyume na sayansi na dini.

‘Kwasababu huyo mwanamke sio binadamu ni shetani, ni mzimu …’akasema

‘Haiwezekani…hahaha..shetani, wewe uliwahi kuonana na shetani…?’nikasema na kumuuliza

‘Haiwezekani!!, …ndio maana huponi vizuri …kwanza huamini na pili bado akili yako inampenda huo mzimu, umeshatekwa naye, imabakia kitu kidogo tu,.....je huyo mwanamke huwa unamuota mara kwa mara..?’ akaniuliza

‘Kipindi cha nyuma ilikuwa namuota, lakini nilipopata hii ajali sijawahi kumuota tena…ila kuna muda nahisi kama nipo dunia nyingine na akati mwingine huwa nasikia sauti yake ikiniita, kama mwangi hivi….’nikasema.

'Kwasababu huku hakuoni, tumeshavunja hisia zake za kukuona, ila kuna muda atakutokea, na ni mjanja sana, anaweza kukutega kwa namna nyingine, uwe makini....'akasema

'Aaah...lakini hizo ni ndoto tu mtaalamu....'nikasema

‘Sasa subiria ukimuota tena utasikia atakachokuagiza..je huko awali mlikuwa mnawasilianaje?’ akaniuliza.

‘Kwa simu au kwenye mtandao…kwenye laptop’nikasema.

‘Hebu tuone huo mtandao…’akasema

Nilijaribu kufungua simu yangu, na kutafuta sehemu ya huyo mdada, lakini sikuweza kumpata, ilikuwa kama kajifuta kabisa kwenye mtandao.

‘Naona hayupo tena…’nikasema.

‘Unaona alikuwa keshamaliza kazi yake, ilikuwa wewe uwe maiti akainywe damu yako…wakati unapata ajali hukuona alama yoyote ya damu..?’ akaniuliza.

‘Ndio kwenye gari..’nikasema.

‘Bahati yako uliwahi kuiona kama usingeliiona ukaikalia sasa hivi ungelikuwa haupo tena….sasa sikiliza, achana na mawasiliano na huyo mwanamke, maana ukianza kuwasiliana naye anaingia kwenye ubongo wako, anachota akili yako na kufahamu kila unachotaka kukifanya..’akasema.

‘Sawa mtaalamu lakini mimi siamini mambo hayo, lakini kama imefikia hatua hii inabidi niachane naye, nitajitahidi sana kufanya hivyo…’nikasema.

‘Unajua kinachokusaidia wewe ni kuwa, wewe una ujasiri moyoni, huogopi, na huamini mambo hayo, ndio maana imekuwa vigumu kwake kukumaliza…na kila mara anatafuta njia ya kuingia mwilini mwako, lakini ni mpaka akujengee hofu….jitahidi ujizuie kuwa na hofu…’akasema.

‘Mtaalamu mimi sina hofu, ndio maana watu wengi waliposema huyo mpenzi wangu wa facebook sio binadamu au…sijui kwanini wanasema hivyo, maana picha na kila kitu ni binadamu, na mimi siwezi kuamini kitu ambacho sio halisia,..ndio mimi naifahamu dini, ndio ambayo naikubali japokuwa mambo yake mengine hayaonekani, lakini sio vinginevyo,... haya mambo mengine eti uchawi, mashetani, mmmh mimi mtaalamu kwa kweli, mimi siyaamini, samahani kwa hilo…’nikasema.

‘Hujayaamini mpaka sasa…?’ akaniuliza.

‘Kuwa huyo binti sio binadamu, mtaalamu nitaaminije tofauti na kinachoonekana, ni binadamu kabisa, mimi sijui vinginevyo…’nikasema.

‘Unajua kijana,…mimi nimeishi sana, na…sawa kuamini kwako hivyo inaweza kukusaidia lakini hata kwenye dini wamesema viumbe hivyo vipo, sasa …’akasema na mimi nikamkatisha sikupenda afikie kuiteka akili yangu kwa mambo kama hayo.

‘Lakini kama vipo vina mipaka yake, au sio, kwanini wanifuate mimi…?’ nikauliza.

‘Ndio hilo nataka mimi na wewe tusaidiane kulitafuta, mimi nafanya hii kazi kwa muda sasa, nimepambana na mambo kama haya sana, ..na njia rahisi ni kwenda huko …alipo huyo mwanamke…kuna jambo kubwa lilitokea huko nyuma,...yawezekana na wewe ulihusika, sasa huenda huyo mzimu anataka kulipiza kisasi...’akasema.

‘Hahaha...mtaalamu, mimi sina tatizo na wanawake, nimekuwa hivyo, maisha yangu, na huyo binti ndiye aliyeweza kuuteka moyo wangu...'akasema

'Tutakuja kuyagundua hayo, mimi pamoja nafanya haya mambo, lakini mengine nayafuatilia kisayansi, ...sifanyi tu kitaalamu, na tukio hili linanivuta sana kulifuatilia....'akasema

'Sasa tutalifuatilia wapi …maana huyo mdada mwenyewe alinielekeza na nikaishia makaburini…’nikasema.

‘Sisi tutakwenda hukohuko makaburini, sio kazi rahisi, ila inabidi ili uweze kupona la sivyo huyo binti wa kishetani, atakusumbua sana,..yeye ni mzimu, na kumshida kwake, ni lazima tuanzishe mapambano makali dhidi yake,…unatakiwa ujiandae maana huko unakwenda kuingia kwenye dunia nyingine,….lakini tutakuwa pamoja, usjali…’akasema

‘Mtaalamu mimi siogopi..nataka nifike huko, na nionane na huyo mwanamke, nihakikishe mwenyewe kuwa kweli sio binadamu, na nijue ni kwanini kanifuata mimi….na hata kama sio kupitia kwako, nitalifanya hilo peke yangu…’akasema kwa kujiamini

‘Hahaha, usijiamini sana…unaona kilichokupata, ulikuwa unapelekwa kuzimu, kwa kupitia njia hizo hizo,..hao watu wapo kila sehemu, na wanapopata mwanya wa kumtaka mtu wao wana mbinu nyingi tu…nyie hamfahamu mambo hayo, ..ndio maana wengine wanakuja kwua watumwa wa mashetani.. mimi kazi yangu ni kupambana na hayo madude…’akasema.

‘Sawa mtaalamuu nipo tayari kufuatana na wewe,..nina hamu sana ya kukutana na huyo mwanamke..’ nikasema na tukapanga nikirudi Dar tuongazane mimi na yeye ili  twende huko.

Basi usiku huo, ndio nikamuota huyo mdada, yupo sehemu kakaa analia, nilipomuuliza kisa ni nini anasema yote nimeyasababisha mimi,…

‘Kwanini..?’ nikamuuliza.

‘Kwanza ulinidanganya hukufika, na baadae watu wenu wamekuwa wabaya wakitaka kuharibu familia yangu…sasa sikiliza umetangaza vita kati ya familia yangu na nyie…’akasema kwa hasira na kila akiongea mdomoni sasa kunaonekana yale meno ya kishetani..

‘Ina maana wewe sio binadamu..?’ nikamuuliza.

‘Utajua mwenyewe….’akasema na kutoweka na mimi usingizi ukakatika.

NB: Huamini, sasa je….


WAZO LA LEO: Ukitaka kinga salama katika maisha yako ni kumtegemea mungu, yeye ndiye mlinzi sahihi wa maisha yako. Na ili ufanikiwe hilo, basi ni lazima uwe na imani thabit, ya kuwa mungu ni mmoja, hana mshirika. Tumuombe mola wetu ili atujalie tuwe na imani thabit ya kumuamini yeye, na kufuata maagizo yake. 
Ni mimi: emu-three

No comments :