Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, April 26, 2017

MPENZI WA FACEBOOK-15



‘Lakini sasa docta mbona hamjaniambia huyu ni nani, ..nahisi ni kama mtu namfahamu, nahisi nimeshawahi kumuona mahali, nahisi nahisi, mmh,…itakuwa,...mhhh, eti hatujawahi kuonana mahali ?’akasema mama akijaribu kukumbuka.

‘Mimi!! Mhh mama, mimi sikumbuki, unajua mama, kuna kipindi nilipatwa na matatizo, nikawa kama nimechangnyikiwa, kwahiyo mambo mengi ya nyuma nimeyasahau,kumbukumbu zinakuja kidogo kidogo,..napata shida sana watu nikikutana nao wananilamu…kuwa nawadharau,..nawapita tu..lakini kiukweli siwakumbuki...'nikajitetea hivyo, huku moyoni najilaumu kwa kutunga uwongo huo, japokuwa kweli nilichanganyikiwa kiasi cha kupoteza kumbukumbu, lakini sasa sio kama zamani, nakumbuka karibu kila kitu

‘Pole sana, hiyo hali imempata hata binti yangu, maana mambo mengi hayakumbuki, pale nikiongea naye inakuwa kama namkumbusha jambo, mmh, ni matatizo, na wewe ulikutwa na matatizo gani, na ina maana baada ya kukutwa na hayo matatizo ndio mungu akakuzawaidia kutibia watu, kuwaombea au..?’ akauliza mama, na mimi nikakimbili kujibu swali la mwisho.

‘Ndio hivyo mama, kiukweli mimi namshukuru mungu kwani baada ya mataizo yote hayo, nikajikuta na hicho kipaji nikimuombea mtu, ..watu wanapata ahueni, wanapona, sasa hata sijjijui mimi najiona kawaida, japokuwa nakereka,…maana sio kawaida..’nikasema

‘Sasa ukija nataka uniombee na mimi, maana usinione hivi mimi nina matatizo mengi kweli,...kama hayo ya ...lakini hayo ni mapenzi ya mungu, ila nina mengine,  sasa ukiniombea, nitafurahi sana, na ukija huenda nitakuwa nimekumbika wapi nilikuona, usikose kuja kesho, …’akasema.

‘Mungu akipenda mama yangu nitakuja nina hamu sana ya kuongea na mgonjwa wetu..niongee na nyie wazazi wangu,...huenda mungu akaleta heri zake’nikasema na mama akawa ananiangalia kwa macho ya upendo, kama ya mama na mwanae.

‘Hata yeye kasema nikukumbushe, kuwa usikose kuja kuongea na yeye..hapendagi kuongea na wanaume na hasa kipindi hiki cha matatizo, amekuwa akiwachukia sana wanaume wote kuacha baba yake na ndugu zake anaowafahamu…ni tatizo kwa kweli, sasa wewe naona ni mwanaume wa kwanza kutaka kuongea naye..yaani hatuamini, mpaka anasema anataka kuongea na wewe, basi ujue kuna jambo kubwa sana...’akasema.

‘Labda akizindukana anaweza kughairi..’nikasema kwa mashaka.

‘Hapana  nahisi ana jambo, kuna kitu kimemgusa,..si bure namfahamu sana bibnti yangu..’akasema mama.

‘Au kavutiwa naye kampenda,..anataka ikiwezekana huyu awe mkweo, nahisi ni kutokana na huduma za msaidizi wangu zimembadili hulka yake ya kuchukia wanaume, kuwa,s io wanaume wote wabaya kihivyo..’akasema docta.

‘Wala... sizani, nahisi kuna jambo zaidi ya hilo, namfahamu sana binti yangu, akiwa na jambo, anasumbuka sana na kuachana nalo ..ni kulisema au kuongea na mhusikika…kama ni mwanaume huwa ananiambia mimi niongee na huyo mtu, nimkanye, au ni..ili tu asiendelee kumsumbua...’akasema mama.

'Kwahiyo kwa hili hajakugusia kuwa ni jambo gani..?' akauliza docta

'Hajanigusia, ...hajambia zaidi ya kusisitiza kuwa anataka kuongea na docta msaidizi wako...'akasema

‘Haya nitajitahidi nije, tukijaliwa..’nikasema kwa sauti yenye mashaka

‘Natumai hata mimi nitakuwa nimekumbuka …kuwa nilikuona wapi..., lakini yaonekana ni siku nyingi,..sijui, na sina uhakika, ngoja kumbukumbu zangu zikae vyema, nikitulia nitakukumbuka, ... haya..niwaache mkapumzike ..na docta usisahau kuleta bili yako, ili nijua ni kiasi gani tunadaiwa..’akasema mama.

‘Mhh, bado,...siwezi kuileta kwa hivi sasa, maana kuna mambo ya kumalizia, usijali,…’akasema docta na ndio tukaagana, na hata wakati naondoka naona mama alikuwa akinitafiti kwa macho, nahisi keshanigundua lakini hataki tu kusema.

**************

‘Nashukuru mzee naona wote mpo hapa, maana leo ni siku ya hukumu na haya ndio matibabu yenu ya mwisho, matibabu haya yanahitajia nyie mumuhukumu mtu wenu aliyewakosea,..'akasema docta.

'Yupo wapi huyo mtu..?' akauliza baba akiwa na hasira.

'Niliwaahidi kuwa nitakuja naye, na ..ni nani nimekuja naye...'akasema

'Hatumuoni zaidi ni huyu msaidizi wako...'akasema mama

'Ndio yeye basi,...huyu ndiye mtu wenu mliyekuwa mkimtafuta..’akasema docta na mimi nikabakia kushangaa iweje docta anikamatishe mbona tulikuwa hatukuelewana hivyo

'Haiwezekani, docta, usitutania...'akasema mama, na baba.

'Ndio yeye, nimeona niwe muwazi kwenu, maana madocta hawatakiwi kuongopa..'akasema

‘Umefanya vizuri sana, na kama ni yeye ni lazima aadhibiwe, haijalishi kuwa yeye ni nani na katusaidia nini,  …’akasema mzee akionyesha macho yaliyoiva kwa hasira.

‘Lakini, kabla ya hayo ninataka wote muukubali ukweli , maana bila kuukubali ukweli hakuna kitakachowezekana, hasa wewe mgonjwa wangu…’akasema docta akimuangalia binti.
‘Ukweli gani docta…’akauliza binti.

‘Kuwa matatizo yako makubwa yametokana na mafikira, mawazo, na chuki pia,…ukawa unawaza sana ukaukataa ukweli wa muumba, kuwa kila nafsi itauonja uamuti,..kuwaza sana kusononeka sana, ni tatizo kubwa sana, imefanya mpaka uathirike mishipa yako ya fahamu, sasa kama unataka upone, uukubali ukweli…’akasema docta.

‘Sasa nifanyeje docta, maana nimeteseka sana na mawazo hayaishi kabisa kichwani, na mimi nilijua kuwa dawa yake ni kuona haki inatendeka, mimi nimekuwa nikiteseka kwasababu aliyemfanyia hivyo dada yangu hajapatikana, najua siwezi kumpata tena dada yangu keshatangulia mbele ya haki, lakini huyu aliyemfanya hivyo dada yangu mbona haadhibiwi, nataka na yeye aadhibiwe ..’akasema huyo mdada akiniangalia kwa macho yaliyojaa hasira.

‘Kwahiyo unachohitajia ni kulipiza kisasi..au sio, na huyu mtu afungwe au anyongwe, au afe na au sio..?’ akauliza docta bila chembe ya kutaka kunisaidia, nilianza kumshuku vibya docta kuwa yupo kwa ajili y akutafuta pesa tu.

‘Sio kulipiza kisasi,..mungu mwenyewe anafahamu huyo mtu atamlipizaje kisasi, ukiua na wewe uuwawe, au sio…, ila nilitaka kumuona kwanza huyo mtu sura yake simuoni vyema, ..ndio huyu eeh, …mbona kabadilika sio kama yule wa …lakini pili ….sheria ichukue mkondo wake,…' akatulia akiniangalia kwa hasira.

'Na tatu akiri kosa,..na alitakiwa akiri mbele ya wazazi wake, ili yeye na familia yake iteseke vivyo hivyo,  kama mateso tuliyopambana nayo mimi na familia yangu, au sio, sasa familia yake ni nani, wapo wapi, mbona na wao hawajafika…’akasema huyo binti.

‘Kwahiyo sasa upone maana huyu mtu nimeshamleta mbele yenu, au sio, sasa baba na mama muwe huru,…mumeshamuona mbaya wenu au sio,, familia yake itakuja huku ikishatolewa hukumu, au mnasemaje..?’ akauliza docta.

‘Lakini mimi naona kama sio yeye, huyu ni mtu mwema sana, katusaidia, kamsaidia mwanangu kwanini atufanyie hivyo, docta una uhakika kweli ndio yeye…?’akauliza mama

‘Ndio yeye ndugu zanguni,,..mwenyewe atakiri kosa mbele yenu, ndio maana nimemleta, na alikuwa tayari kufanya hivyo kukiri kosa, na itakayobakia ni nyie kumuadhibu au kumuhurumia,….’akasema docta

‘Mhh..docta, baba amemtafuta sana huyo mtu, huu sasa mwaka wa ngapi sijui, kawatumia polisi , wapelelezi, imekuwaje wewe umpata kirahisi hivyo….’akasema binti sasa akiniangalia kwa macho yenye chuki, na hasira macho yake ya upendo sasa yaligeuka kuwa ya kiuaji, hata meno yake yakawa kama ya shetani vile.

‘Mzee Mashauri, na binti yako na hata mama, niwaambie kitu, hakuna kipindi kigumu kama kile cha kutafuta mwenza, na haya wengi tulipitia, na njia za mafanikio kumpata mwenza zinatofautiana, wengine wanapitia njia ngumu sana, wanaumia na wengine walioshindwa kuhimili , na inakuwa ni sababu tu, mungu alishapanga kuwa mja wangu huyu siku zake ni kadhaa…ndio maana wengine wanaishia kujiua…’akasema docta.

‘Lakini hatujui ni kitu gani huyo mtu alimtamkia huyo binti yangu, mpaka afikie hatua hiyo ya kujiua, mimi namfahamu sana binti yangu ni mvumilivu sana, mpole…sasa mpaka kufikia hatua hiyo , ina maana alivumilia sana, ina maana huyu mtu alifanya jambo baya sana hastahiki msamaha wetu…’akasema baba

‘Ndio maana nasema siku ikifika mengine ni sababu tu, ukitaka kuhukumu, ukataka kufanya vyovyote vile, bado tutakuwa tunamkhalifu mola, tukubali kuwa mola alishampenda zaidi huyo binti yenu, na kufa kwa njia hiyo ilikuwa ni sababu tu..’akasema nikaona hapo docta ananitetea kidogo, lakini haisaidii tena.

‘Sasa docta ina maana mtu akiua na yeye asiuwawe, maana mungu alitaka huyo mtu auliwe na mwingine au…?’ akauliza baba.

‘Hapana sikuwa na maana hiyo, maana yanu ni kuwa, kwanza ilibidi tumuhoji huyu mtu ni kwanini alifanya hivyo kwa binti yenu,huenda alikuwa na sababu, pili, je ni kwanin hakuweza kufika kwenye msiba, au hata kuja kuhani, au hata kuja kuwapa pole, labda ana sababu, sasa atuambie, ili tuone kama tunaweza kumsamehe..’akasema docta.

‘Haya atuambie na atuonyeshe na ushahidi, la sivyo sisi hukumu yetu ipo pale pale, ..’wakasema na kunigeukia, nikataka kuongea, lakini mdomo haukuweza kufunguka, kichwani nilikuwa na sababu nyingi tu, ningeliweza kujitetea, lakini mdomo hautaki kufunguka.

‘Ongea bwana mdogo..’akasema docta, lakini sikuweza kuongea , nikabakia kugugumia maneno, na baadae machozi yakaanza kunitoka, kwanini siwezi kuongea, kwanini siwezi kujitetea, oh mungu wangu kwanini, ina maana ndio siku yangu ya mwisho..’nikawa nawaza hivyo.

 ‘Unaona alivyo, hataki hata kuongea, ina maana alifanya makusudi,, tunakuuliza ni  kwanini hukutaka kujitokeza kwa muda huo wote kama ulikuwa na sababu ya masingi, kwanini umekaa huko, na ikatufanya sisi kutesema, hebu jiulizeni, hata kama ingelikuwa ni wewe ungelifanya nini, ungelielewaje,…mpaka tunakimbia nyumba yetu, ina maana ulitaka sisi tuteseka mpaka tufe, sasa ni zamu yako, hukumu itolewe kwa kosa ulilolifanya….’akasema mama.

‘Mama ndio maana nasema huyo hakujua yote yaliyokuja kutokea baadae, kwanza hakupenda binti yenu ajiue, alimpenda, lakini pia alipendwa na wengi, ikawa anajaribu kuwachunguza mmoja mmoja, ni nani anamfaa, unajua kizazi cha sasa hivi kilivyo,…' nikaona sasa docta anaanza kunitetea, labda zilikuwa ni mbinu zake , kwa namna y akuwaingia hawa watu.

'Vijana wetu, wao wanajua ni kujaribu huyu na yule mwisho wa siku anabakiwa na mtu mmoja ampendaye, sasa huyo akajitokeza akamkuta mwenzake ana mtu, huyo binti yenu kuona vile akapandwa na hasira akakimbilia kwao, huko akajiua, angelijuaje huyu kuwa mwenzake kajiua…’akasema docta kunitetea.

'Kama alikuwa anampenda angelimfuatilia, ..kwanini hakumfuatilia, ina maana alikusudia kumharibia mwenzake..'akasema mama

'Kwahiyo nyie mlikuwa mnatakaje..?' akauliza docta

‘Kama alifanya hivyo mwa binti yetu,, basi na yeye ajiue, ili haki itendeke..’akasema mama.

‘Ndio na yeye aje anywe sumu afe kama mwenzake..’akasema baba.

‘Ndio na mimi nitahakikisha amekunywa au kama hataki mimi nitamywesha hiyo sumu, ili na yeye afe kwa kujiua,...'lakini hapo utakuwa umemuua, sio kajiua...'akasema docta.

'Haya mpeni hiyo sumu anywe mwenyewe...'akasema baba, lakini mimi sikuwa na uwezo wa kuichukua hiyo sumu, mwili haukuweza kuinuka, nilikuwa kama nimekufa ganzi

'Anagoma,...'akasema mama

'Basi nipeni hiyo sumu mimi nita- mnyweshe,..’akasema huyo binti.

‘Ina maana hiyo ndio hukumu yenu,..?’ akauliza docta

‘Ndioo,..’wakasema wote kwa pamoja

Docta kanigeukia, akachukua kamba na kunifunga mikono yangu yote, na kusema

‘Haya fanyeni mtakavyo, mimi naondoka zangu…’akasema docta na kuanza kuondoka, nikawa napiga ukelele ili docta arudi kunisaidia, lakini sauti haikutoka,.. na mara yule mdada akanisogelea, kuninywesha sumu, nikawa nahangaika kujiokoa, lakini mikono yangu ilikuwa imefungwa kwa nyuma.

Binti hakujali,.. akanimiminia hiyo sumu mdomoni, ikawa inapenya kwenye koo na kuzama tumboni, na wakati anafanya hivyo, akawa ananiangalia machoni, macho..macho,,, ..na mara..akanitambua.

‘Ni wewe, kumbe ni wewe…oh, nimakuua bure…’ wakati huo nimeshaimeza hiyo sumu, na sumu imeshaanza kufanya kazi, madada akawa anahangaika sasa kutaka kunikoa, lakini alikuwa kechelewa…

‘Leteni maziwa, anakufa huyu,…’

'Muache afe, kama alivyokufa binti yetu..'wakasema wazazi 

'Baba na mama, tumuokoe, hafai kuuwawa, mimi nampenda...'akasema binti

Lakini hakuna aliyemsikiliza, baba , mama wakawa sasa wanaonyesha uso wa furaha, haki waliyoitaka imetendeka, lakini sio kwa binti yao, bint alikuwa bado akinihangaikia , kuniokoa, lakini wapii, sumu ilishaanza kunikakata matumbo,nikaanza kuona dalili ya kifo…

Nilijaribu kuinua mdomo, ili kuwaomba msamaha, lakini kauli ilishafungwa, macho yakawa mazito hayafunguki vyema, nikamuona malaika wa kutoa roho akinjia na kisu kikali,..hakuwa na huruma na mimi…roho hiyo ikawa inatolewa kwa maumivu, mwili mnzima unauma,…baadae, nikawa maiti..

Wakati nakata roho, mpenzi wa facebook, akaonekana akija kunilaki,, akawa sasa ananyosha mikono kunipokea, akiwa na furaha, huku akisema;

‘Karibu mpenzi wangu wa facebook, nakupenda sana,…na mimi nikawa najitahidi kuitikia nakupenda pia, lakini koo, limekuaka, nahitajia maji, macho manzito hayataki kufunguka,…mara, …..macho yakafunguka

**********
‘Wewe amuka , unalala kama umekufa,unakoroma kama unakata roho, unaweweseka, ulikuwa unaota ndoto mbaya nini,.hebu amuka,…hujui kuwa unatakiwa kuwahi hospitali, nimepigiwa simu kuwa wagonjwa wamesharuhisiwa kwahiyo sasa ni safari ya kwenda nyumbani kwao..

‘Mmhh, mimi huko siendi..’nikasema nikijaribu kuondoa mawazo ya kwenye ndoto.

‘Kwanini..?’ akauliza

‘Nimeota ndoto mbaya sana, hiyo familia inataka kuniua mimi kwa sumu, kama alivyokufa mtoto wao..’nikasema.

‘Umeota..hahaha, je nikuulize wewe kawaida yako ukiota inakuwaje..?’ akauliza docta

‘Inakuwa kweli…kila nikiota jambo hutokea kweli, na kama sio kweli huwa sikumbuki hiyo ndoto...’nikasema.

‘Basi itakuwa vizuri..hiyo ni dalili nzuri, wala usiogope..’akasema docta.

‘Kuuliwa na sumu ni dalili nzuri..na inaonyesha ni kweli maana kwenye ndoto wewe ndio umenipeleka ukashinikiza nilipiziwe kisasi , ukanifunga kamba mikononi, na binti akaninywesha sumu…je una dhamira hiyo?’ nikauliza.

‘Hahaha, …usigope kijana.., hivi kumbe umeshasahau kuwa wewe huogopi, au ulikuwa unanidanganya, hivi wewe umeshasahau kuwa ulisema upo tayari kubeba madhambi yako, ili usamehewe, ili haki itendeke,..umesahau kuwa sababu ya mateso ya hiyo familia ni wewe…sasa imakuwaje..?’akauliza docta.

‘Kwahiyo ina maana unataka kunipeleka na kuwaambia kuwa mtu wenu ni huyu, mfanyeni mtakavyo, au sio..?’ nikauliza

‘Ndoto hiyo, inakughilibu, shetani huyo anakudanganya, jiandae tuondoke..’akasema docta.

‘Mimi huko siendi, ..siendi siendi..safari hii tutakosana tu..’nikasema mpaka docta akabakia akishangaa, na mara simu yake ikaita;

‘Haloo, nani mwenzangu…’docta akasikiliza simu yake halafu, akasema;

‘Oh binti unamuhitajia docta msaidizi, au sio…ndio yupo hapa tunakuja naye, ulitaka uongee na yeye sasa hivi au sio, ndio nitahakikisha kuwa nimefika naye , hakuna shaka ..’ akauliza sasa akiniangalia mimi.

‘Unasema , ulimuona wapi,…?’ akauliza

‘Kwenye facebook,..’akasema akiniangalia kwa macho ya mashaka

‘Kwani wewe ni nani..?’ akauliza docta , na kunifanya nishangae, ..wewe ni nani tena...na docta sasa aligeuka upande mwingine na kunipa mgongo, yaonekana alikuwa na mashaka na mtu anayeongea naye..
.
NB: Naishia hapa kwa leo


WAZO LA LEO:Dhuluma inapotendeka nafsi hujilaumu, na kama kweli una imani sahihi ya dini, unamuogopa mungu, ni lazima utakuwa unajutia,..basi kujutia huko kuambatane na toba ya ukweli, na ikibidi wale uliowakosea waendee uwaombe msamaha, …maana makosa na dhuluma uliyomfanyia mtu , inapendeza ukimuendea huyo mtu ukamuomba msamaha, hiyo inakuwa toba sahihi. Tumuombe mola wetu atuwezeshe kusamehewa makosa yetu na wale tuliowakosea, wawe wepesi kutusamahe, maana mengine tulipitiwa ,…kwa madhaifu yetu ya kibinadamu, bila wewe mola wetu kutusaidia, ukatusamehe, sisi waja wako hatuna ujanja.
Ni mimi: emu-three

No comments :