Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeFriday, March 31, 2017

KITANDA HAKIZAI HARAMU-31 (MWISHO)


'Wakati polisi wanakuja nikuulize swali wewe mdada;...'akasema Soldier

‘Uliza tu…’akasema huyo mdada aliyekuwa kajifunika usoni, kwa sauti ya kinyonge…

‘Ina maana kweli kwa muda wote huo ulikuwa ukiwauguza wagonjwa mbali mbali akiwemo huyo mtu...ina maana kweli  hukuwahi kumuona huyo mtu usoni, ukaifahamu sura yake…?’akaulizwa

‘Hutaamini, wanaume wote humo walikuwa wamefunikuwa uso na walikuwa na sehemu yao tofauti na sehemu ya wanawake, na hakuna ruhusa wanawake au wanaume kufika sehemu za wengine..kuna ulinzi mkali sana, wanawake kazi yao kubwa kupika, kufua,..na kazi za kutafuta kuni.

Mimi nilikuwa nakwenda sehemu waliyoitenga kama hospitali, na huko pia wagonjwa wanaume wamefunika usoni……'akasema

'Haiwezekani, ndio hapo naona hadithi yako ni y akutunga tu...'akasema Soldier

'Haiwezekani,...hata kidogo tu...kumuona, au hakuna aliyewahi kuumua usoni,...'akasema Soldier.

'Kiukweli wapo, na huyo mtu niliwahi kumuona sura kidogo tu…..’akasema


‘Kama ulimuona kidogo tu, ni nani sasa kati ya hawa wawili, ni Soldier au Dereva…?’akaulizwa, na kabla hajasema kitu polisi wakafika.

Tuendelee na kisa chetu.....

                           *****************

 Kabla hajasema kitu polisi wakaingia, na walijua ni nani wanayemtafuta, kwani walipoingia tu mmojawapo akamsogelea shemeji wa Soldier, na kumwambia;

‘Upo chini ya ulinzi….’aliongeza maneno mengine na shemeji bila wasiwasi akanyosha mikono na kuweka pingu, halafy akasogea aliposimama dada yake na kumnong’oneza kitu, halafu akatembea kama kutangulia kutoka nje, na kama vile kasahau kitu akamgeukia Soldier na kusema;

‘Umeharibu,…na utajuata kwa hili…amini usiamini, umeharibu ndoa yako, na hata kama itakuwepo, lakini kwangu mimi sikutambui kama shemeji yangu..wewe ni aadui yangu..amini hivyo…’akasema na bila kujali akaanza kutembea kutoka nje, lakini polisi mmoja akamzuia, asitoke kwanza.

‘Jamani ni vyema kuwafahamisha hili, kwasabababu huenda tukitoka hapa kunaweza kuwa na maneno mengi,…’kabla hajamaliza dada mtu akauliza;

‘Tunataka kujua kwanini mumemkamata ndugu yangu kwa kosa gani…?’ akauliza na polisi akamgeukia jamaa na kumuuliza

‘Unakubali tuyataje makosa yako…?’ akaulizwa

‘Makosa gani, sina makosa yoyote, mnahisia tu…’akasema kijeuri.

‘Huyu jamaa anajishughulisha na biashara haramu, anajishughulisha kama wakala wa kuwauzia waasi silaha, waasi ambao wanasumbana na serikali ya majirani zetu…huyu jamaa pia anajishughuliza na kuuza madawa ya kulevya, bangi…na madawa yanayotumiwa na waasi kutezea watu…pamoja na hayo ana biashara zake, huko,…magari na hajalipa kodi…’akasema huyo askari.

‘Mna ushahidi gani kwa hayo..?’ akauliza dada

‘Ndio maana tumekuja kumshika, na akifika huko kituon atahojiwa kwa mujibu wa sheria, na haki zake zote zitalindwa…’akasema huyo askari

Na wakati huo wale waliovalia kijeshi wakawa wanaongea jambo na Soldier, waliongea kwa muda, ikawa wao ndio wanasubiria, na baadaye Soldier akageukia akamuangalia mdada, yule aliyejifunika uso…

‘Samahani dada yetu, ..kuna mambo tunatakiwa twende pamoja tukayathibitishe huko kituoni, kwa usalama hatuwezi kuyaongea hapa hadharani,…’akasema na Yaya akadakia na kusema;

‘Dada yangu hawezi kwenda huko ana mtoto mdogo…’akasema

‘Lakini mtoto mdogo huyo aliweza kukaa na wewe na mke wangu kwa muda bila ya yeye kuwepo, na hatuendi kushinda huko tutarudi naye…’akasema Soldier.

‘Kila la heri mwanangu tupo pamoja…’akasema baba mtu akiwa kitandani na haoo… wakaondoka, na wakati wanatoka nje, mke wa Soldier akawa anawafuatilia kwa nyuma huku machozi yakimtoka, na alipofika huko nje, akasema kwa sauti;

‘Unamfunga kaka yangu eeh, …kwa kosa la kusingiziwa, umeharibu kila kitu,..mimi na wewe basi tena, naondoka zangu, kwanza ulishavunja miiko ya ndoa, halafu sasa unazidi kuiharibu familia yangu, sitakusamehe kamwe…’akasema na kurudi ndani kwa hasira.

******************


  Kutokana na tukio hilo zikapita siku mbili, mke wa Soldier akawa kaondoka na mtoto na wale wageni wawili, na dereva bado alikuwa akisumbuana na polisi, lakini kesi yake haikuwa na nguvu sana, baadaye kulipotulia, baba, akaitisha kikao cha wanafamilia, mke wa Soldier na wageni wake wakaitwa waje,…na kweli walifika, na walifika na ndugu yao mmoja, ni baba mkubwa wa mke wa Soldier.

 Koramu ikatimia, baba na mama, Soldier na mkewe, ingawaje walikuwa hawana mawasiliano kila mtu kakaa kivyake,alikuwepo mdada na mdogo wake, pia mama wa dereva, na dereva mwenyewe, na wazee wawili ndugu zake baba yake Soldier….na yule dakitari upande wa mke wa Soldier naye alialikwa, haikujulikana safari ameitwa kwa jambo gani.

‘Jamani mimi sio mkaaji sana, nimeshukuru kuwa pamoja na hayo sisi bado ni ndugu moja, mumeoa kwetu , na pamoja na tatizo hili bado tunatambua kuwa ndoa ipo sijui wenyewe watatuambia nini….’akasema huyo mgeni baba mkubwa.

‘Ama kwa jamaa yetu huyo aliyekamatwa, kwa kushukiwa na makosa mbali mbali, tumeshafanikiwa kumuwekea dhamana, na ana wakili wake mnzuri, kwahiyo tuna imani kesi hiyo itakwisha , maana mambo ya vita huko yamekwisha na kuna maridhiano fulani yanaendelea.

Najua kwa namna fulani jamaa yetu, huyo ana makosa yake, lakini kama alivyosema ni katika kutafuta biashara, na alijiunga na wenzake kufanya biashara ya silaha kama biashara nyingine hakujua kuwa hao ni waasi na kufanya hivyo ni makosa, kwahiyo yeye akachukuliwa kama kusaidia polisi,…unajua tena, wakili kasema kesi hiyo haina nguvu, ataona jinsi gani ya kulisaidia hilo…’akasema

‘Lakini sio kwa njia hiyo aliyotumia yeye, nakubali alikuwa mfanyabishara lakini biashara nyingine hazikubaliki, sasa sijui kama wakili ataweza kulitetea hilo, tunaombea iwe hivyo na ajirudi, na aache tabia yake ya visasi…’akasema Soldier

‘Hilo tunalijua sana,..niliwahi kumkanya sana mtoto wangu huyo kipindi cha nyuma mpaka tukakosana naye, unajua alivyokuwa m-mbishi, lakini sasa kajifunza, aliyoyapata huko, anakiri kuwa hatarudia tena, ila katuma ujumbe kwako kuwa, hamjamalizana  yeye na wewe, mimi sijui ana maana gani..

‘Aaah, huyo nimeshamzoea, najua ipo siku tutakaa pamoja tu, maana hakuna lenye mwanzo na lisikose mwisho wake,…mimi sina kinyongo naye, na akiwa tayari tusameheane mimi sina tatizo, na kwanini niwe na kinyongo naye, sioni umhimu wake…’akasema

‘Na kwa hili baba mkwe, naombeni sana, tuayamalize haya tugange yajayo..kuna mambo mengi yametokea, na sisi ni wanadamu kukosea kupo tu, lakini mbora wa wote ni yule anayekubali kukaa, na kuongea na kutafuta suluhu watu wakasamehena…naomba sana, mke wangu alikubali hili, na tuyamalize haya kwa amani,…’akasema Soldier.

‘Nimefurahi kusikia hivyo…na ndicho kilichonileta mimi, kuona jinsi gani mtarekebisha matatizo ya ndoa yenu, …nimemuhoji mke wako,…naona bado ana duku duku, kwanza anasema kwa nini unamficha ukweli, na hata baada ya kujulikana ukweli bado hutaki kukiri kosa,…hasa kuhusu huyo mtoto…na pili kuhusu kaka yake…hilo la kaka yake halina nguvu tena..ila hilo la mtoto…’akasema huyo baba.

‘Mzee, sioni kwanini turudie huko nyuma, nafikiri yeye ameweza kukaa na dada hapo, na kama ingelikuwa ni uwongo, angeshaambiwa, ..mimi simjui huyo mdada, zaidi ya kukutana naye hapa, na kama tulikutana naye huko, sikuwa n aufahamu huo…nafikiri docta anaweza kuliongelea hili kitaalamu kama ni lazima…’akasema.

‘Haina haja…nimeshaongea na dada, na nimeelewa, lakini kama alivyosema baba, mimi ninachotaka ni wewe kukiri kosa, na kumkubali huyo mtoto kuwa ni wa kwako, basi…’akasema mkewe.

‘Mimi sina kipingamizi cha kukiri kosa, ila nasema hayo yalifanyika nikiwa sina uwezo wa kutambua, na mpaka sasa sikumbuki,…kama ni mtoto wangu hewala, namkubali, lakini bado tunahitajia uhakika wa kisayansi,…na ndio maana mimi nikakubali damu yangu na mtoto vikapimwe, na leo yupo yule docta ndugu yenu, atuthibitishie hilo..na mlienda wote hospitali, mimi sikuwepo,..sijui mumekuja na majibu gani…’akasema Soldier.

*************


‘Niweni radhi kwa kikao chenu cha kwanza, najua hivi vipimo vya sasa vya DNA, havitakuwa vya uwongo kama vile vya dereva, hivi ni halali, maana mimi mwenyewe nimevisimamia, nia sasa ni kutengua kitendawili cha mtoto je baba halali ni nani,…Dereva anasema yeye sio baba halali, halikadhalika, Soldier, na hatuna jinsi nyingine ya kulitatua hilo bila kutumia vipimo hivyo, au sio…’akasema docta

‘Mimi namkabidhi baba wa familia hii aifungue hiyo bahasha, hakuna anayefahamu,..hata mimi nimekabidhiwa na wataalamu wa vipimo, na nikawaambia siangalii mpka tufike huko kwa wanafamilia wenyewe…unajue tena…’akasema docta.

‘Ila mzee kabla hujaifungua hiyo bahasha, ningelipenda kusema neno ..unajua haya maisha yalivyo huwezi kujihakikishia kuwa unaweza kufanya kila kitu sawa sawa,..kuna madhaifu mengi ya kibinasamu, mimi nina yangu, dereva, na kila mtu ana yake,...na hili nataka Dereva ulielewe, mimi kama kaka yako kama ningeliamua kufutilia kesi yako sasa hivi ungefungwa…’akasema Soldier.

‘Kwa kosa gani…?’ akauliza Soldier akionyesha mshangao.

‘Utapeli….kugushi, kudanganya, …blackmail….hayo ni baadhi tu, wakati huo huo umepewa dhamana ya kusaidia watu, wakimbizi, na ulikuwa ukitoroka na kwenda nchi ya jirani, hilo ulifikiri hujulikani, na ndio maana nilijua fika kuwa wewe unaweza kuwa baba wa huyu binti..’akasema

‘Bro, hayo tuyaache kwanza..ukweli utajielezea kwa vipimo hivyo, mimi naviamini sana..’akasema

‘Ndio nakubali hilo, ila kama kaka yako lazima nikuonye, sitajali kuwa wewe ni ndugu yangu, ikifikia kwenye sheria mimi nitaosha mikono yangu, wewe uliaminika, na waajiri wako, hebu jiulize kama waajiri wako wakisikia hivyo watakuamini tena…’akasema Soldier

‘Ok bro..nimekubali kosa.., hayo yamekwisha bro…mimi sirudiii tena hayo makosa, nakuhakikishia hilo, sasa hivi nina furaha kubwa mke wangu ana mimba….hahaha, raha sana, pili yale matatizo ya mama yamekwisha, sasa mama yupo safi, tutaishi naye nitamlea na kuhakikisha hapati matatizo….’akasema

‘Sawa, tutaona hayo…muhimu tulimalize hili….’akasema soldier. Halafu akamgeukia mdada na kusema;

‘Nilichotaka kusema ni kuwa, mdada, kwanza niombe radhi, kwa hayo yaliyotokea nasema ukweli kutoka moyoni mwangu sikumbuki lolote kuhusu hayo uliyosema, nakumbuka kuteswa, lakini yaliyofuata huko baadaye sikumbuki….na sijui ilikuwaje, naomba kama hali hiyo ilikuwepo hivyo,..nisamehe sana,…na namuomba mungu kumbukumbu hiyo isije kurejea akilini mwangu…’akasema

‘Mhh..bora iwe hivyo…’akasema huyo mdada.

‘Kiukweli sitaki nije kukumbuka hayo kama yalikuwa hivyo, …ila hao watu walikuja kupata kipigo, na kusambaratika kabisa, na sikujua kuna watu wa huku kwetu wanahusika,…ok, nashukuru kwa msaada wako , sijui nitakulipa nini, kama ulivyoelezea, unanidai kwa hilo…’akasema.

‘Umlipe sasa..ikibidi mchukue awe mke wako, itakuwa bora zaidi,…’akasema mkewe kwa sauti ya huzuni.

‘Nini…dada unazungumza nini tena…tulishaongea mimi siji kuvunja ndoa yenu, nimekuja ili tuwekane sawa,…’akasema na Soldier naye akasema;

‘Hapana usiseme hivyo mke wangu…ila hebu fikiria hiyo hali na mtu alijitolea kufa kwa ajili yangu,.. mimi sijui niliponaje..kama nilikuwa hivyo. Ndio maana wakati mwingine nahisi kama ni hadithi tu, wasingethibitisha hili hao askari, mpaka kesho nisingelikubaliana na hilo….’akatulia

‘Wamekuambia eeh, sasa hakuna shaka tena, au sio…?’akasema huyo mdada akiwa kambeba mtoto wake.

‘Lakini bado sijaamini..kuwa huyo ni mtoto wangu, nimegundua kuwa dereva mlikuwa majuana naye kabla, kweli si kweli…?’ akauliza Soldier.

‘Ni kweli, aliwahi kufika hospitalini, …nakumbuka..lakini sio kujuana  kimapenzi, …’akasema huyo mdada

‘Sasa hapo utaniambia nini…nikubali tu kirahisi hivyo…’akasema Soldier, na wakati huo baba alikuwa kaishikilia ile bahasha juu.

‘Kwahiyo basi kwa lolote lile, napenda kutamka, kuwa huyo mtoto atakuwa sehemu ya familia yetu, kama mke wangu yupo radhi, …mke wangu kampenda sana huyo mtoto, na tumuombe mungu akitujalia watoto wengine, mimi na mke wangu, basi mtoto huyo kama ni wangu kweli, atakuwa ni kaka yao wa kwanza…’akasema

‘Hongeraaah…unaona bro, sasa tupo pamoja, kwa kauli hiyo, nakuheshimu kaka yangu, mimi nisingeliweza kumkataa huyo mtoto kama angelikuwa ni wangu…’akasema Dereva, akipiga makofi.

‘Lakini hatujasikia vipimo vya DNA, vipoje,…’akasema Yaya, na dada yake akasema;

‘Sina shaka na hilo,  …sasa hivi naanza kuhisi baba wa mtoto huyo ni nani, nasikitika sana kwa hayo yaliyotokea.., sijui kama nitaweza kuyasahau, kwangu mimi itaendelea kuwa ni ndoto ya majinamizi,… namuomba mungu hayo yote yaweze kuisha kichwani .…’akasema huyo mdada, sasa akionyesha kama anataka kulia.

‘Usijali, dada, hayo hayana maana tena, hakuna aliyependa hilo litokee, …usihuzunike, na jamaii haiwezi kukuchukulia vibaya, nina imani utaweza kumpata mume mwema ambaye ataweza kukusahaulisha machungu yote hayo….na sina shaka, mke wangu atanisamehe,…’akasema Soldier akimgeukia mke wake.

Mke wake alikuwa kimia, na alipoinu auso wake kulionekana kuwa na machozi, alikuwa akilengwa lengwa na machozi, sijui alikuwa akitaka kulia kwa lipi hapo, na huyo mdada alipoona kuwa mke wa Soldier analia, akamsogelea na kumshika begani huku akisema;

‘Mpendwa dada yangu, wewe sasa ni ndugu yangu, nakuomba usiingiwe na huzuni,au chuki dhidi ya mumeo, …naomba ndoa yenu iwe ya amani na furaha, …dada yangu mshukuru sana mungu wako, kwani kwa hali ilivyokuwa , usingeliweza kuwa na mume tena, ungelikuwa unaitwa mjane, japokuwa wangelikupamba kwa maneno matamu ya kisiasa eti mke wa shujaa…kiukweli huyu mume wako ni shujaaa,..mateso aliyoyapitia hakuna mwanadamu angeliweza kuhimili..

‘Mimi mwenyewe nilishudia kwa macho yangu mumeo akipitia mateso makali, kama ndio yeye alikuwa huko, maana sijui..ila nahisi ndio yeye, vinginevyo, siwezi  kujua,,..nilimuona akiteswa…mpaka anapoteza fahamu, hawachoki kumtesa, mateso yalizidi mpaka anapoteza kumbukumbu..na aikuwa kama punguani, sikujua kuwa leo ninaweza kukutana naye akiwa katika hiyo hali…siamini kuwa ni yeye, nahisi ndio yeye, mimi sijui, …mpende sana mume wako, na mshukuru sana mungu wako…’ akasema na kumgeukia tena Soldier.

‘Sikupenda nishike hii mimba haraka hivyo, wazazi wangu wananihitajia sana,..lakini ya mungu mengi, na kama nilivyosikia huyu dereva akiimba ‘kitanda hakizai haramu ..sio lazima tendo la kupata mimba litokee kitandani, ila hata porini… sipendi kusiki watu wakisema huyo mtoto ni wa haramu, uharammu wake ni nini,  narudia tena huyu mtoto sio mtoto haramu kwani ametokea kwenye mazingira magumu..na akikua ana hitajia kusikia historia yake , wapi alipotokea.

‘Sikujua kama nitaweza kujifungua salama, sikujua kama mtoto huyu atapona, nilizaa kwenye uchungu mkali, kwahiyo ombi langu la mwisho, nawaombeni jamani niondoke na huyu mtoto wangu, na mungu akipenda tutakuwa tunatembeleana, maana ni lazima nirudi kwetu, nikawaone wazazi wangu..’ akasema

**********

Ikaja muda wa kuifungua ile bahasha kila mtu macho yakiwa pale, wenye viroho hafifu ikawa ni shida kwako, na hatimaye barua ikafungulia, na baba alipoona kilichoandikwa akamkabidhi mke wa Soldier, akamwambia soma hapo chini kumeandikwa nini, na mke wa Soldier akasema;

‘POSITIVE…’

‘Sema tena…’akasema Dereva

`POSITIVE…’ akasema mke wa soldier sasa akimuonyeshea mama mkwe wake.

‘Sema tena…’akasema mama

‘Positive….’akasema mke wa Soldier na kumkabidhi hiyo barua, yule mdada, ambaye ni nesi akaikagua kwa makini na hatimaye akasema;

‘Ahsante mungu, yametimia, sasa sina shaka tena kuhusu baba halali wa mtoto…’akasema huyo mdada akitoa machozi…na jina la utani, nitamuita huyu mtoto komandoo…’ akasema sasa akijariibu kutabasamu, na taratbu mke wa Soldier akawa anamuanglai amume wake,…macho yakakutana, na kilichofuata hapo ni kilio…

Mke wa Soldier alipomaliza kulia, taratibu akamsogelea mume wake…na bila kusema nini, akamvaa mume wake, tofauti na walivyofikiria watu, akamkumbatiana mumewe, na mikono ya mumewe ikawa inasita kujibisha lile kumbatio, baadae naye akafanya hivyo, huku mkewe machozi yakimtoka na alimshikili amumewe kwa nguvu na baadae akasema;

‘Nisamehe sana mume wangu..najua hujakosea, najua hayo yote ni mapenzi ya mungu, na tumuombe mungu ndoa yetu iendelee kudumu, nisamahe kwa kauli zangu chafu…nasamehe kwa yote…nakupenda sana mume wangu…’akasema na Soldier alikuwa hasemi kitu, ni kama kashikwa na butwaa fulani. Baadae akasema;

‘Nakupenda sana mke wangu…’

**************
                                                      MWISHO.

WAZO LA LEO: Binadamu kukoseana ni jambo lisiloepukika,..kwani mawazo, hulka tabia na imani zinatofautiana, hatuwezi tukafanana au kukubaliana kwa kila kitu, muhimu ni kuhimiliana,kuwa na subira, kusameheana, kuvumiliana, na kuweka mbele upendo na amani tukijua sisi sote ni watoto wa Adamu na Hawa, na tukijua kuwa hapa duniani ni mapito tu ispo siku sote tutarejea kwa mola wetu.

‘ndio maana nasema nimechanganyikiwa maana wote wanafanana..na kama nilivyosema sikuwahi kupata muda wa kumchunguza, maana muda wote ni mteso, na ukiwatiba ni haraka haraka umesimamiwa na wao…kiukweli nilipogundua nina mimba, nikawa na hamu sana ya kumfahamu huyu mtu…lakini sikuwahi kumuona sura yake kamili kiasi cha kumtambua…’akasema

NB: Nawashukuruni sana kuwa nami kwenye kisa hiki,… natumai mumejifunza pamoja nami, na tuzidi kuombeana heri, ili tuweze kuja na kisa kingine kizuri zaidi, NIMEKUWA nikiandika kwa shida, kwa kukosa vitendea kazi, lakini ipo siku mambo yakuwa vizuri,

Kama kuna maoni, hoja, mawazo msisite kunitumia kwa email,(miram3.com@gmail.com) au hapa hapa kwa facebook(inbox)


TUPO PAMOJA
Ni mimi: emu-three

No comments :