Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeTuesday, March 21, 2017

KITANDA HAKIZAI HARAMU-23


Watu wote walikuwa wamegeukia mlangoni wakiangalia huo ugeni uliokuja, kumuona mgonjwa, na kilichovuta hisia za hao, ni hiyo tabia ya kubakie nje. Badala ya kuingia ndani na mama yake Soldier, ni kama wanaogopa ..
 
'Ni kwanini wageni wanahofia kuingia ndani, hapa ni hospitalini, hamuna haja ya kuogopana...?'akauliza dereva aliyekuwa na shauku ya kuwaona hao wageni .
'Sio wote wana tabia kama zako wewe...'akasema Soldier.

'Mimi nina tabia gani bro…?'akauliza dereva akitabasamu.

'Utaijua tabia yako pindi ukisimama ndani ya chumba cha gereza..'akasema 

'Kwanini niwekwe huko, gerezani, hahaha…Bro mimi ni mtoto wa mjini, najua ni nini ninachokifanya, nina elimu ya kutosha kujilinda, nafahamu sheria,...siwezi kuogopa kufungwa, kwa vile mimi nina uhakika sijafanya kosa,...'akasema.

' Unasema una uhakika hujafanya kosa,..kupiga watu kuwaumiza sio kosa, umewajeruhi watu, angalia hali ya mzee hapo ilivyo kisa ni nani,..haya huku unawahadaa watu kwa mlungula, ili matakwa yako yatimizwe hayo sio makosa…?’ akawa kama anamuuliza.

‘Hahaha, bro bwana, tatizo lako hujui hayo matatizo, mimi sijui ilivyokuwa, na sipendi hali hiyo, hujui jinsi gani inavyonitesa…’akasema

‘Sasa...mimi kama mwana usalama nitahakikisha sheria inachukua mkondo wake, wewe si hujui, basi ukiwa kwa pilato, utajua,.....siwezi kuona mzee kalala hapo kitandani, hawezi kuinuka sababu yako...halafu unajifanya una huruma,....maisha gani ya ujanja ujanja, na tamaa za mali...'akatulia alipoona hao wageni wanaanza kuingia.
‘Sijamalizana na wewe, jiandae kabisa tukitoka hapa tunapitia polisi…’akasema na kabla Dereve hajasema neno hao wageni walishaingia, na mazungumzo hayo yakakatika.

Soldier alishaanza kukasirika..kila akiliwazia hilo tukio, alihisi mwili ukimchemka, na hata wageni hao walipoingia yeye hakuwa na shauku nao, akilini alikuwa akiwazia jinsi gani ya kumuwajibisha dereva. Jinsi gani ataweza kumchukua hadi polisi bila kumuathiri baba yake..

‘Huyu mtu inabidi nimuwajibishe, na ….’akatulia kuwaza na kusogea mbali, ili kuwapisha hao wageni kusalimiana,…

Walioingia mwanzoni walikuwa ni akina dada wawili, wa kwanza alikuwa yule yaya wa mtoto, lakini kwa muda huo hakuwa na mtoto, ina maana mtoto kamuacha na mke wa Soldier, na wa pili ndiye aliyevuta hisia za watu zaidi….

Mdada huyu alikuwa kavaa kitu kama ushungi,…ni kitambaa kilichoweza kufunika kichwa chote, na kuacha sehemu ya uso..na akavaa na mawani,…huyo mdada alihakikisha kuwa sehemu yote ya uso haionekani, uvwaaji huo uliwavutia wengi, hata huko nje alipokuwa anapita…kwani haikuonekana kuwa alivaa hivyo kiimani ya dini,…kwasababu ya vazi lake la chini, ilionekana ameamua kuvaa hivyo huenda ni kwa ajili ya  kuficha uso wake, sasa ni kwanini aufiche uso wake…

 Baadae wakaingia watu wengine wawili, hawa walikuwa ni mwanamke na mwanaume, wanajulikana, walikuwa mke wa Soldier na kaka yake...
Soldier alipowaona hao wawili akazidi kusogea mbali kabisa, hakutaka hata kusalimiana nao, akafika kwenye dirisha na kuangalia nje…,
**********
'Mtoto yupo wapi?'ilikuwa swali la baba yake Soldier aliposalimiana na mkwewe huyo, yaani mke wa Soldier.
'Yupo na bibi yake..tusingeliweza kuingia naye huku ndani, wametushauri madakitari tusiingie naye, kwa taratibu zao...'akasema mke wa Soldier, na baba yake Soldier akageuza uso kumtafuta mwanae alipo alitaka kuongea jambo, lakini alipoona mwanae hayupo karibu wakaongea mambo mengine, na aliyeongea sasa alikuwa dereva.

‘Mambo mengine wanajua wao wenyewe, inabidi uwatii tu, ina maana mtoto hatakiwi kumuona mgonjwa..kama ni mama yake, au baba yake…’akasema

'Ni sawa wafanyavyo,..unajua afya za watoto ni tofauti na zetu, wao ni rahisi kuambukizwa magonjwa, ndio maana wanachukua tahadhari hiyo…’akasema mama wa soldier.

‘ Sawa hamna shida, lakini Soldier yupo wapi…’ akauliza na kabla hajajibiwa akasema;
‘Hata hivyo ninashukuru mumekuja kuniona,..mimi hali yangu, usiku ndio ilikuwa mbaya sana, na sikujua kuwa nitaweza kuamuka tena, ndio maana nilipoweza kuamuka tu, nikawaita wanangu..nashukuru kuwa na nyie mumeweza kufika, huenda safari yangu imekaribia..’akasema na kumfanya mkewe amtupie jicho.
‘Si mnajua mtu hafi mpaka awaone wote aliopangiwa wamuone,..yaani hata mtu alikuwa wapi, kama alipangiwa aonane na ….ni lazima atafika tu, na yule ambaye hakupangiwa , atajitahidi lakini atakumbana na vikwazo, akifika anakuta mtu alishafariki…sio nasema kwa vile nahisi ninakufa…, hata chakula, kila mtu anafungu lake la riziki hawezi kuondoka duniani mpaka fungu lake alimalize, tunaambiwa hivyo na imani zetu za dini...;akasema 

'Wewe sasa umekuwa mtu wa kutangaza dini, na yote hayo ni kuogopa kufa.., wangapi wanaumwa wanaishi na wazima wanakufa..'akasema mkewe.

'Nimefurahi tu..mke wangu, maana niliowakosea wanafika mmoja mmoja na kwahiyo napata muda wa kuwaomba msamaha...na ufanyeje sasa, kama sio kuyaongea hayo…'akasema .

'Hebu achana na lugha yako ya kutuvunja nguvu, wewe hujui jinsi gani lugha yako hiyo inavyotuumiza wenzako..'akasema mkewe.

'Hahaha kumbe mke wangu bado unanipenda..'akasema na mkewe akabakia kimia na wengine wakawa wanatabasamu…

Kwa muda huo Soldier alikuwa kasogea mbali kabisa, alikuwa kasimama akiangalia kupitia dirishani, na mke wake mara kwa mara alikuwa akijitahidi kumtupia jicho la kujificha, lakini hawakuweza kwenda kumsalimia, wakawa wamemzunguka mgonjwa.

*************
 Soldier alitaka kutoka nje, lakini alijua bado baba yao alikuwa akimuhitajia, kwahiyo, akawa amebakia pale pale, akikwepa kulisogelea hilo kundi la watu wwaliofika kumuona mgonjwa.
Alihisi kuwa akisogea kwenye hilo kundi, atajikuta akizozana na watu, pale, yupo dereva, ambaye ndio katoka kuzozana naye, japokuwa alijitahidi kujizuia lakini akashindwa, sasa kaja adui yake wa asili, shemeji yake. Huyo hakuna siku walikutana wakaacha kuzozana, na sana sana wanaishia kutupina ngumi.

Yupo mkewe, ambaye tangia arudi,wameshindwa kuelewana, mpaka ikafikia mkewe kuondoka kwenda kwao, kisa hasa ni kwanini mkewe hataki kumuelezea ukweli kuhusu mtoto, huyo mtoto ni wa nani, kama ni wake kazaa na nani,…na sasa ndio kasikia jipya ambali hakupenda hata kulifikiria maana haiwezekani, eti baba yake ndiyo kazaa na mkewe, haiwezekani kabisa, hilo haliingii akili mwake, na hakutaka hata kulifikiria.
Lakini sasa lipomuona mkewe na alionekana akisalimiana na baba yake bila kikwazo, akaanza kulikumbuka hilo, na sasa akawa anafikiria kile ambacho hakukitaka kukifikiria awali,;
‘Je kama ni kweli,…kuwa baba yake ndio kazaa na mkewe,…haiwezekani, hilo halipo ..sikubali , sitaki, uwongo…’akajikuta akipiga ukuta ngumi.

‘Huyu dereva ni mzandiki, ndio maana nataka akafungwe…’akasema wka sauti ndogo,
‘Huyo mtoto ni wa dereva,..kama ni wa dereva, ina maana alitembea na mke wangu, ..haiwezekani, …oh, mbona hali hii inanitesa hivi,..nitaua mtu…’akapiga ngumi ukuta tena, na kuwafanya watu wageuke kumuangalia.

Alipowazia hilo akataka kugeuka kuwaangalia hao watu walioingia lakini bado akili yake ikagoma kufanya hivyo akabakia akiwa kasimama, akiwa amewapa mgongo wenzake, na alikuwa yupo mbali kidogo na wao.

********.
Na wakati huo ndio baba yake na mama walikuwa wakiongea, alipenda hiyo hali iwe hivyo, wazazi wake wapendane, waoneane huruma.
Kiukweli moyoni anawapenda sana wazazi wake, na aliapa kuilinda ndoa ya wazazi wake mpaka dakika ya mwisho.

Ilimsikitisha sana pale ilipotokea baba yake anaumizwa na dereva, mbele ya macho yake, na mhalifu bado yupo huru, alipowazia hilo sasa akageuka kutaka kumuangalia dereva, asije akatoroka, kuna mambo mengi yanamfanya amchukue dereva waende naye kituoni, pamoja na hilo la kuumiza watu, lakini alishawahi kuongea naye, na inaonekana dereva ana ushahidi utakaomuwezesha kumfunga kaka wa mkewe.

Kaka wa mkewe anasadikiwa kuwa anajihusisha na uuzaji wa madawa ya kulevya, lakini bado hakuna ushahidi wa moja kwa moja..lakini dereva alitamba kuwa anao huo ushahidi na huyo kaka amekuwa akimlipa pesa nyingi tu kumziba mdomo.

‘Lakini nitaupataje huo ushahidi wakati hatuelewani…na ili niupate huo ushahidi inabidi nimuweke huyu mtu ndani, niongee na polisi wafanye hivyo, lakini sasa,  ..nikimuweka ndani nitakosana na baba, baba anampenda mwanae, baba anaogopa kukosana na mke wa rafiki yake, baba alishachukua dhamana ya kuilinda hiyo familia, baba ana mambo ambayo amemuahidi dereva na akifanya kinyume chake ataumbuliwa, sasa..nifanyaje hapo…’akajiuliza

‘Huyu kaka yake mke wangu anadhaniwa kuwa anauza madawa ya kulevya,…na mimi nimepewa jukumu la kumfuatilia,…’akawaza.

‘Ni kweli ni moja ya kazi zetu watu wa usalama….lakini haya majukumu mengine ni ya polisi, na wameniomba niwasaidie, hakuna shida, nitaifanya hiyo kazi,,.. lakini sasa, mbona mke wangu anamtetea sana kaka yake, anasema watu wanamuhisia tu vibaya kaka yake, na alishasema siku nikimfunga kaka yake ndio mwisho wangu mimi na yeye, mpaka tumezozana kuhusu hilo, je nikipata ushahidi kutoka kwa dereva, …ina maana ndio itakuwa mwisho wa ndoa yangu, .nifanyeje hapo…mmmh, ngoja nione…’akajiuliza.

‘Kwanza ni lazima nianze na huyu dereva,…nitamchukua hadi kituo cha polisi, akahojiwe, tutambana mpka tutaujua huo ukweli…nitalifanya hili leo wakati baba akiwa huku hospitalini, na nitahakikisha baba halijui hili…najua mama yake atakuwa wa kwanza kukimbia kwa baba…’

‘Aaah, baba atanielewa tu, ni lazima nimuwajibishe huyu mtu, ili iwe mwanzo na mwisho wa kuwasumbua watu, na humo humo ninaweza kujua kama kweli aliyoyasema kuhusu baba yana ukweli au anamsingizia tu ili kupata mali, …mmh,..lakini sasa …ushahidi, anasema ana ushahid wa kaka wa mke wangu ..nitaupataje, anaweza kunitega kwa hilo..ngoja…’ hapo akageuka kumuangalia dereva, kuhakikisha kama bado yupo…, sasa badala ya kumuangalia dereva….

Macho yake yakavutika na jambo jingine, na kumfanya macho yake yafunguke kwa mshangao, mshangao wa kutokuamini hicho anachokiona, akajikuta sasa akigeuka mzima mzima..hakuamini macho yake...

NB: Ni nini alichokiona Soldier,


WAZO LA LEO: Mtenda wema anaweza kujitahidi sana kutenda wema, anaweza akatenda wema tisa, na bahati mbaya akakosea jambo moja tu,… jambo hilo moja tu likaja kuharibu wema wake, na akaonekana kama hakufanya kitu, kwa kosa hilo moja ni kwanini lije liharibu wema wake.., ni kwasababu mtenda wema anapofanya wema wake anakuwa na maadui wengi, maadui ambao hawataki wema , kwao wao, wema unawazibia nafasi ya kufanya maasi yao,…Ewe mtenda wema usivunjike moyo kwa hayo, endelea kutenda wema, kwani wema ni kwa ajili ya wanyonge na wema  njia yake ni ya peponi,…
Ni mimi: emu-three

No comments :