Dereva akiwa kabadilika, alimuendea mama yake na kusema;
'Hasa wewe…nakutafuta sana..lazima
nikufundishe adabu, unadiriki kusema uongo, kuwa mimi sio damu ya huyu hawara
wako…..mzandiki mkubwa wewe, mara ngapi mumekuwa naye,..mimi nawaona tu…mimi
sitaki uchafu huo nimechoka..sasa nakumaliza wewe kwanza…’akawa sasa
anamsogelea mama yake.
‘Nisamehe mwanangu
nitasema kila kitu…usinitese, usiniue mimi ni mama yako…’akasema sasa akipiga
magoti huku anatetemeka.
‘Umeniuzi,…ni lazima
nikufundishe adabu….wewe na mwenzako, ni kwanini mnasema mimi sio damu halali
ya ….bwana wako..kwanini….’akasema sasa akiwa keshamshika mama yake na kumuinua
juu, na anataka kumbamiza chini…mama huyu ana matatizo ya presha na kama hali
hiyo itazidi anaweza kuathirika vibaya, sana..na kama atarushwa kama
walivyorushwa wengine sizani kama anaweza kuhimili
Baba wa Soldier
akaliona hili , akajua asipofanya jambo, …mke wa marehemu watamsahau,
akajitutumua na kukaa vyema , akasema kwa sauti.
‘Nitasema kila kitu
mwanangu…nitaitoa siri yote ya baba yako…nitasema kila kitu muachie mama yako
utamuua, huyo ni mama yako…..na mimi nitasema kila kitu,…tafadhali…’akasema
mzee.
‘Haya waambie ukweli,
simuachiii huyu mtu, mpaka usema ukweli wote…kuwa mimi ni damu yako, kuwa wewe
na mama ni wapenzi, kuwa…. Mimi ni haki sawa na familia, hii, ongea kila kitu…
‘Haya subiria,
niongee…….’akasema mzee
Tuendelee na kisa chetu….
***********
Ukumbuke haya yote
yanasimuliwa na baba yake Soldier, na kwa jinsi mzee alivyozidi kuongea, ilifika mahali dereva akawa anabadilika kidogo kidogo, kwani kwa muda wote huo, alikuwa bado
kamuinua mama yake hewani akitaka kumbamiza chini, lakini kila muda ulivyozidi
kwenda dereva naye akawa kama anaanza kuishiwa nguvu…
Ikafika muda, dereva…, akachuchumaa,...mzee anaendelea kuongea, huku mama yake dereva kainuliwa juu, ikafikia muda dereva akakaa mkao wa kukaa,...mzee alikuwa bado anaongea
Na baadae akamshusha
mama yake na kumshikilia kama anataka kumtia kabari…na mzee anaongea, na wengi walikuwa wakimsikiliza mzee, hawakuwa na mawazo y ahuy mtu tena.
Na ilipofika sehemu hiyo
tuliyoishia sehemu iliyopita, ghafla dereva akaporomoka chini…,na mama yake
naye akamfuatia, na wote wakawa wamelala sakafuni, kimiaah..
Kitendo kile kiliwafanya wote waliokuwemo humo ndani kusimama kwa uwoga, na wengi
waliangalia usawa wa mlango, tayari kukimbia.
Dereva na mama yake sasa walikuwa wamelala sakafuni, mama kalala, kichwa kaweka
kufuani kwa mwanae. Wapo kimia kabisa…
‘ Hebu waangalieni hao watu kama wapo sawa...’ akasema yule mzee mualikwa akiwa
karibu na mlango, alikuwa tayari anataka kukimbilia nje.
Na ni nani angewasogelea, kila mmoja alitoa jicho la uwoga,
na aliyeweza kusogea pale baada ya kupita dakika chache, ni docta docta, kwa
tahadhari akawasogelea, na kuanza kuwakagua, na alipoona kuna usalama, akaanza
kuwapima mapigo ya moyo, na baadae akasema:
‘Wapo sawa..naona walipoteza fahamu kidogo, lakini naona wameshazindukana,…wapo
sawa…’akasema docta.
'Docta una uhakika, maana hayo sio mambo ya hospitali, yana wenyewe hayo....'akasema
mzee.
Na mara dereva akafungua macho yake na kwa
haraka akakurupuka, na kumsukuma mama yake ambaye alikuwa bado hajazindukana
vyema, na kwa haraka akasimama, alikuwa kama mtu aliyeshtuliwa kwenye usingizi
na ndoto mbaya, akawa sasa anaangalia huku na kule.
Kwa kitendo kile, cha kuzimama kwa haraka, wengine walishafika mlangoni, wakikimbia,
kutaka kutoka nje, ambaye hakuweza kusimama na kusogea pale alipo alikuwa baba
yake Soldier.
Dereva, akili ikamtulia akaangaza macho, na kushangaa kuona watu wanamkodolea
macho, akatikisa kichwa na kusema:
'Kumetokea nini jamani?’ akauliza.
Hakuna aliyemjibu, watu walikuwa na wasiwasi , huenda jamaa anaweza akaanza
makashi kashi mengina wakaishia kuvunjwa viuno na mbavu,..na Dereva alipoona
watu wapo kimia, wanamuangalia tu, naye akaanza kuingiwa na wasi wasi, na
katika kuangaza huku na kule macho yakatua kwa mama yake, alipomuona mama yake
kalala sakafuni, akamsogelea kwa haraka na kusema:
'Mama nini tena, kumetokea nini jamani, mama kafanya nini….na mama
umekuja-unafanya…sasa akaanza kukumbuka, na kushika kichwa, halafu akasema
‘Sasa mama, kwanini ulikuja huku,… nilikuambia haya uniachie
mimi..?'akasema na kwa muda huo mama yake akawa naye akaangaza macho huku na
kule na akili ilipokaa sasa, akazizoa zoa na kusimama, akawa anataka kuondoka.
‘Mama tulia kwanza haujawa sawa, unaona unavyo yumba yumba….’akasema
Dereve.
'Tuondoke, twende zetu nyumbani...'akasema mama yake akimshika mwanae mkono, na
watu walipoona kuna amani, ikawa sasa kuangaliana,..na hapo ikaonekana hali ya
baba yake Dereva haipo sawa.
'Docta hali ya mzee sio nzuri, tufanyaje?'ilikuwa kauli ya Soldier, na docta
akamsogelea baba yake Soldier na kuanza huduma ya kwanza.
Mzee akawa analalamika maumivu, na docta akasema:
'Huyu inabidi afikishwe hospitalini kwa haraka, yawezekana kuna athari ndani
kwa ndani..'akasema docta.
'Sawa mimi nitamchukua kwenye gari langu...'akasema dereva.
'Wewe mimi sikuamini, ukija kutusweka kwenye makorongo..hapana, tutatafuta
usafiri mwingine...'akasema Soldier.
'Kwanini niwasweke kwenye makorongo, mimi ni dereva, nina
leseni?"akasema dereva akionyesha uso wa kushangaa.
‘Hakuna muda wa kubishana hapa, muhimu mgonjwa afikishwe
hospitalini…’akasema docta.
Hatimaye mzee akabebwa na kuingizwa kwenye gari, haraka akafikishwa hosp, na
ikawa mwisho wa kikao hicho kwa siku hiyo.
************
Zikapita siku mbili, hali ya mzee ikawa inaendelea kuwa mbaya, na siku ya tatu,
taarifa zikaja, baba anataka kuongea na Soldier na dereva
Na wote wawili wakafika harala mbele ya mzee, akiwa kalala kitandani….akasema;
'Wanangu, nimewaiteni,najua kuumwa sio kufa, lakini pia kuumwa ni dalili ya
kuwa huenda umauti umekaribia, mengine ni majaliwa ya mungu..’akaanza kuongea.
‘Mzee usiwe na shaja, utapona, haina haja ya kupoteza
matumaini,…’akasema Dereva.
'Nimewaiteni kwa jambo moja, siku ile kila jambo liliwekwa hadharani, hakuna
utata tena na yaliyopita naomba yapite,…mjua sasa nyie ni ndugu, hakuna
mjadala, kama rafiki yangu angelikuwepo hai, hili lisingelikuwepo, lakini kwa
hayupo nimebakia mimi…mimi ndiye baba yenu wote, naombe mlielewe hivyo.
‘Hamna shida …’akasema dereva, na Soldier akatikisa kichwa
tu.
'Sasa nawaombeni jambo moja, kwanza kuhakikisha familia ipo kitu kimoja,
ondoeni tofauti zenu, jueni kuwa nyie ni damu ya baba mmoja, ndio yaliyotokea
yalitokea isivyo stahiki lakini mkumbuke, mambo mengine yanaweza yakawafanya
watu wakapokea mapokea ambayo kwa wengine yanaweza kuwa ni mshangao…hamjui ni
jinsi gani hayo yalitokea, lakini..tumuombe mungu atusamehe tu…’akasema
‘Mzee , mimi nakuomba utulize kichwa chako….uangalia afya
yako….haya mengine hayana msingi…’akasema Soldier.
‘Ni kweli kabisa mzee….’akasema dereva.
‘Pili, fanyeni jitihada mama zenu warejee ile hali yao ya zamani, mnajua akina
mama zenu kipindi cha awali walikuwa kama mapacha , wanaume hali kadhalika,
sasa nyie fanyeni hivyo hivyo, muishi kama mapacha, nawaombeni sana, msahauni
yaliyopita….’akasema
‘Baba hayo yaache kwanza…’akasema Soldier
‘Usijali mzee, muhimu ni afya yako …’akasema dereva
‘’Na jingine, naona
ni la tatu eeh, Soldier fanya mpango mkeo arudi, najua kaondoka kwa hasira lakini
nimefurahi kuwa mtoto hakutaka kumucha, kampenda mtoto kuonyesha kuwa ni wake,
nilijua atamkataa..'akatulia.
'Sasa atamkataa wakati ni mtoto wake…’akasema Dereva.
‘Una uhakika gani kuwa ni mtoto wake…?’ akauliza Soldier
‘Uhakika upi tena, kama sio mtoto wake ni wa nani,…unaona
anavyofanana na wewe …lakini mimi sijui, kinachonikwanza, ni jinsi gani mke awe
na roho ya namna hiyo,…kutupa mtoto…hivi nyie mnalionaje hilo, yawezekana kweli…’akatulia.
Soldier akaonekana kukunja uso, lakini hakusema jambo.
‘Hayo tuyaacheni vijana wangu, …mkitaka kuchokonoa chokonoa
mtafikia mahali hamtaelewana na lengo langu ni nyie wote muelewane, najua kuna
sintofahamu nyingi, lakini …’akasema baba, na dereva akamkatiza kwa kusema;
‘Sawa baba tumekuelewa, lakini ni muhimu kujua huyo mtoto ni
wa nani,… haya, tusema mama ni ..mke wa bro hapa,..lakini baba yake ni nani….?’
Akasema Dereva.
‘Kwa maelezo ya baba, wewe ulisema baba yake ni mzee, au…usitake
kupindisha pindisha maneno, wewe subiria mzee apone, …utaniambia ukweli wote,
na kama umezua jambo, utaishai jela, nakuhakikishia hilo..sitajali udugu hapa,
umenisikia?’ akasema Soldier akimkazia macho dereva, na dereva akatabasamu
akibenua mdomokwa dharau...
‘Bro, usiwe na shaka na hilo…ila kwa hilo ndivyo
nilivyoambiwa,…lakini hata hivyo, ni nani kakuambia kuwa nilisema hivyo…?’akasema
dereva akionyesha kushangaa na kugeuka kumuangalia baba yake.
‘Na nani…hahaha,ulifanya hivyo kumkomoa baba si ndio…, ili
upate urithi au…sasa utapambana na mimi…umenisikia vyema..?’ akasema Soldier.
Na Dereva akamuangalia baba yao pale kitandani, halafu akasema;
‘Tumuache mzee kwanza apone, najua yeye ana majibu rahisi ,
lakini mimi ..sikumbuki kuongea kitu kama hicho…mbele yako,…’akasema
‘Uliongea na mzee, ukimshinikiza ili akupatie urithi, na
kukuandikia hati ya urithi,..hayo uliyafanya kwa siri, lakini landa pale
alipokuwa anaongea baba , wewe hukuwa wewe, nasikia ikiwa hali kama hiyo
hujielewi, lakini kwangu utanielewa,……’akataka kuendelea kuongea, lakini baba
akawa anamzuia kwa mkono kuwa asiendelee kuongea.
‘Bro…hebu kwanza hayo tuyaache…yatafikia muda wake, tatizo
hunijui…utakuja kunijua kuwa mimi sio mtu wa kutishiwa, nyau…lakini hayo
tuyaache, ….’akasema
‘Tutaona…’akasema Soldier.
‘Vijana,..watoto mbona mnanikatisha tamaa, kabisa….mumenielewa
nilichowaitia, wasiwasi wangu ni kuwa nikiondoka huku nyuma mnaweza kuanzisha
vurugu, hilo ndio sitaki mimi, …mnanisikia hebu kwanza yafanyieni kazi hayo
niliyowamambia yakikaa sawa, muone maajabu yake, hayo mengine yatajileta
yenyewe…na mniombeee mungu nipone, nitawaambia kila kitu,…kuna mambo mengi
hayajaka sawa, lakini hata mimi sijaweza kuwa na uhakika nayo….sasa nawaombeni
mnisaidie kwa hayo niliyowaambia, ili moyo wangu uwe na amani…’akatulia.
‘Sawa mzee…’wakasema kwa pamoja.
‘Mzee, mungu akujalie upone, maana tunakuhitajia sana…’akasema
dereva.
‘Hilo ni sawa…ili upate mtetezi wako..’akasema Soldier
‘Sio hivyo bro, wewe hutaki mzee apone…?’ akauliza
‘Mimi sitaki au wewe ndiye chanzo cha yote haya, hebu
jiulize isingelikua wewe, baba angekuwa hapo kitandani…’akasema Soldier
‘Kwani mimi nimemfanya nini mzee…kwani mimi ndiye
niliyemuumiza…mimi mpaka sasa sijajua chanzo cha mzee kuumua hivi…’akasema
dereva.
‘Basi utajua tu…nimeshafungua kesi, RB, yako ninayo hapa….’akasema
Soldier, na mara mlangoni akaonekana mama akija na chakula cha mgonjwa, na wote
wakatulia kimia, hadi pale mama aliposogea karibu yako,
Kwa nje kulikuwa na watu wengine wanasubiria
waingie,..lakini yaonekana walikuwa wakiogopa kuingia.
‘Ni nani hao wapo huko nje, si mumekuja nao, mbona hawataki
kuingia ndani…?’ akauliza mzee
‘Kuna ugeni ….’akasema mama akionyesha uso usio na furaha,..,
na wote mle ndani wakageukia mlangoni kuuona huo ugeni, isipokuwa mama , ambaye
alikuwa akimuandalia mgonjwa chakula.
NB: Ni akina nani hao..
WAZO LA LEO:
Inapofikia swala la ugonjwa, inabidi mambo mengine yashaulike, hata kama kulikuwa
na ugomvi, hata kama kulikuwa na uadui..inabidi wote waangalia matatizo ya
ugonjwa, kwani mgonjwa anahitajia faraja, anahitajia, huduma, na kukiendelea na
sintofahamu inaweza ikawa sababu ya kumuongezea mgonjwa , ugonjwa, au kuzua
magonjwa mengine. Tuweni na moyo wa huruma kwa wagonjwa wetu, hata kama ni
maadui zetu.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment