Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, March 17, 2017

KITANDA HAKIZAI HARAMU-20



‘MIMI haya nayafanya kwa ajili ya mama yangu,…nilidhamiria kufanya mabaya zaidi ya hili…, lakini nimeona haina haja,..muhimu mzee, ni ufanye hivyo uandike hiyo hati na mzee mimi sina tamaa, napenda haki kabisa, kwenye hiyo hati hakuna kupunjana…na unajua watoto wa kiume wanapata nini……’akasema na kutaka kuondoka. Na mara simu ya mzee ikalia…

Kwanza mzee akaangalia mpigaji ni nani ,akaona ni namba ngeni, akaiweka hewani na kuanza kuongea;

‘Ni nani mwenzangu…?’ nikauliza.

‘Ni mimi mwanao Soldier, baba…tunatarajia kufika huko kesho kutwa au mbele yake kidogo, nitawajulisha, …’ ilikuwa sauti ya Soldier.

Mzee, alikuwa kama kapigwa barafu usoni , akaganda…na alisahau hata kusema neno kwa mwanae….

‘Mzee vipi nani huyo…?’ akauliza Dereva

‘Soldier….’akasema kwa sauti yenye mkwaruzo….

Tuendelee na kisa chetu…

***********

'Mzee huna haja ya kuogopa, mambo nimeshayaweka sawa, la msingi twende sambamba tu, hutapata shida..anasema anakuja lini…?' akauliza

'Kesho , kesho kutwa,...hawajajua ...'akasema

'Lakini mzee cha msingi, .....lakini mzee una uhakika ndio yeye, maana nilisikia maneno mengi,..wengine wanasema alikufa kwa bomu…’akasema.

‘Weee, hebu toa uchuro wako hapa, mbona unapenda sana wenzako kufa, mbona wewe hujafa…’akasema mzee.

‘Nakuambia nilivyosikia, watu wanasema yeye alijifanya shujaa, akajipeleka kwa maadui, akatekwa, na akateswa sana, na wakati anatoroka, akalipukiwa na bomu,…hakuonekana kabisa…sasa sijui, kama kafufuka…’akasema.

‘Nakuomba uondoke, maana la maana kwangu, zaidi ni kuniweka roho juu, nenda kaongee na mama yako maana mnafanana tabia, kujifikiria wenyewe tu…’nikasema.

‘Sasa mzee, naona zoezi liende haraka, kesho , au hata akifika usiku huu, tunakuja kwako, hiyo hati ni muhimu iwe tayari, hatutaki mtu mwingine aingilie, la sivyo siri itavuja,je unapenda mtoto wako aijue siri yenu…?’ akauliza.

‘Nakuomba uondoke,…’nikasema.

‘Poa mzee, nikija sitaki longo longo, la sivyo kijana wako atakuwa wa kwanza kulifahamu hilo, kuwa ulitembea na mke wake…’akasema na kuanza kuondoka, na kwenye simu yake kukaingia ujumbe, akaufungua, na kusoma;

‘Nitafika asubuhi na mapema,….nipokee uwanjani-wakili’

***********

Taarifa zilizagaa mapema kuwa vijana waliokwenda mstari mbele kwenye vita vya kusaidia majirani, wamerudi na taarifa iliyovuma sana, ni kuhusu Soldier, alikuwa shujaa, ..kwani alitekwa, kwa ajili ya kuwasaidia raia, na akateswa karibu ya kufa, lakini hakukata tamaa, aliweza kulisambaratisha kundi la magaidi.

‘Vijana wetu ni mashujaa,wakija wanatakiwa walakiwe kishujaa, ni lazim tutayarishe sherehe ya kijiji.unasemaje kiongozi..?.’wazee na wazazi wakaliongelea hilo na kweli likapita na watu wakawa wanatoa kila mtu kwa uwezo wake, mpaka ikafikia kiasi cha kufanya shughuli angalau kidogo.

Baba yake Sooldier ikabidi awasiliane na mkewe, na katika maongezi yao, alimsihi mke wake, asije kuliongelea jambo lolote kwa mtoto wao, kila kitu amuachie yeye,..

‘Mimi nitaongea naye…najua atashtuka akimuona mtoto….’akasema

‘Sasa utasemaje, maana mke wake alimuacha, hana uja uzito, na kama angekuwa nao mtoto angekuwa sasa anasoma chekechea…’akasema mkewe.

‘Yeye kama anakumbuka, atanielewa, kama nijuavyo, mimi huenda alikutana na binti,…akavutika kwake, unajua ni muda mrefu, vishwawishi havikosekani, …alipo mpa uja uzitohakujua,…inawezekana…sasa ngoja arudi tutaongea naye…’akasema

‘Lakini mume wangu una uhakika huyu sio mtoto wako, niambie ukweli maana nikija kufahamu..sizani kama nitakusamehe, na wla sitakaa na wewe, nitaondoka bila kuaga..’akasema.

‘Mke wangu hayo niachie mimi…siwezi kufanya hivyo…nalewaga lakini sijafikia huko…’akasema.

‘Huyo bint ana jambo, na kasema anasubiria mumewe arudi, akirudi tu, ataliongelea na ataondoka zake, sasa ni jambo gani…’akasema mkewe.

‘Hayo niachie mimi..kuna ushahidi mkubwa wa kuthibitisha hayo…watu wanasema eeh,nimezaa na mke wa rafiki yangu, ..waongo, mimi nina ushahid wa kulithibitisha hilo, tena wa kitaalamu..nimeongea na Dereva, na kumuonyesha, sasa hivi kaamini, ..kabisa kuwa mimi sio baba yake, hayo ya watu ni uwongo…’akasema.

‘Hahaha..mume wangu, usinidanganye, hakuna ushahidi wa kunidanganya mimi, huyo dereva ni damu yako…na sasa huyo mtoto sijui…ila kama ni kweli, mume wangu,..hutaamini nitakachokifanya,..ngoja mtoto arudi…’akasema na akakumbuka jambo.


*********

‘Mama nimesikia mume wangu anarudi…?’ akauliza mke wa Soldier

‘Ndio…unataka kumuandalia nini..?’ akaulizwa na mama mkwe wake.

‘Sina cha kumuandalia maana akirudi ndio itakuwa muda wa kuagana mimi nay eye, na sijui nitawezaje kuachana na huyu mtoto, nimemuona ni mtoto wangu kabisa…sitaki tuachane naye…’akasema.

‘Ni wako ndio…au unataka kusema vipi, nilishakambia huyo ni mtoto wako, umenielewa…?’ akaambiwa.

‘Mama sitanii, huyo mtoto namuhisi ni damu yangu, nimempenda kweli…, nilivyokaa naye ..kumlea, yaani …sitaki tuachane naye kabisa, huyu sasa ni mtoto wangu, na nikiondoka na ondoka naye...’akasema.

‘Si ndio hivyo, ukubaliane na mume wako tu…na muhimu ujue jinsi gani ya kumuelezea huyo mume wako…, nasikia huko alipokuwa alitekwa,… sasa, huenda katika kutekwa huko, alilazimishwa kutembea na huyo binti, ..baadae alitoroka, na hakujua huku nyuma kamuachia binti wa watu mimba …’akasema.

‘Mama unaamini hayo, wanaume waongo, kamuachia kwani walilazimishwa, hilo sio kweli hakuna kitu kama hicho….nina imani kuwa alitembea na huyo mwanamke kwa tamaa zake tu hakujali kuwa kaacha mke wake huku nyumba akipambana na mitihani kibao....mimi sijali itakavyokuwa,..maana kila mtu ana dhambi zake, na ili tusichafuane, basi kila mtu atajua hamsini zake…’akasema.

‘Mwanangu, usifanye lolote..unasikia, mimi nitaongea na mume wako nitaujua huo ukweli..huoni mimi mpaka sasa napambana na baba yako..simuelewi,…yaani amekuwa sio yule mume ninayemtambuau mimi….’akasema mama.

‘Hata hivyo, nampenda mume wangu,  siwezi kumkimbia hivi hivi tu…, ..ninajua muda gani wa kulifanya lolote, lakini sio kwasasa..kwanza tuwape muda hawa watu, …sisi mungu katujalia hilo, uvumilivu, huruma na kusemehe…ngoja kwanza tuone ukweli ulivyo, huenda..nasema tu huenda kuna sababu ya msingi..sasa ni wao kututhibitishia hilo, …unanielewa..’akasema mama yake.

‘Hapana mama, haya yangu ni machungu zaidi wewe hujui tu..wewe utasema hivyo kwa vile unamtetea mwanao,..lakin hujui ni machungu gani nimeyapitia, ulipoondoka nilipatwa na mengi, siwezi hata kuyasimulia.., ..oh,…sizani kama hata mwanao atayafurahia hayo,..hapana ngoja tu nikajaribu kuyasahu huko kwetu..’akasema.

‘Kwani kuna kitu gani kikubwa kimetokea, mbona hutaki kuniambia mwanangu,…mume wangu alikufanya nini, alikufanyia jambo baya…alikubaka..ali…hebu niambie ukweli mwanangu, kama kakufanyia ubaya, ohooo, niambie..sasa habi namuendea, sisubiri, huyo mwanae aje,.. alikufanyia nini..?’ akamuuliza kwa hasira.

‘Mama we yaache tu..tusije kumwagia mafuta kwenye moto…ngoja mume wangu arudi, kwanza niujue huo ukweli,..na mimi nitausema ukweli, halafu..maamuzi yatafuata, mimi mama nimeamua kukaa hapa kwa ajili yako tu,..kwa ajili ya ushauri wako,…na kwa ajili ya huyu mtoto asiye na hatia…Ujue mama wazazi wangu na familia yangu wameshaniambia nirudi kwetu…, na wametoa onyo, kama nitaendelea kubakia huku, litakalonipata ni juu yangu mimi mwenyewe….’akasema.

‘Hakuna kitu kitakupata mwanangu, …ilimradi nipo kwenye hii familia, hutaumizwa tena,..nakuahidi mwanangu..najua lazima una jambo kubwa, na sijui huyo mume wangu kakufanyia unyama gani maana sasa naona ndio tabia yake,.…sasa ukitaka kuniambia, niambie sasa kabla mwanangu hajarudi,…’akasema.

‘Mama siwezi kukuambia,…mpaka huyo kidume arudi…’akasema na akakumbuka jambo, na kusema;.

‘Ngoja nimpigia kaka yangu, alisema huyo kidume akirudi nimuambie,anataka kukutana naye…’akasema.

‘Wanini kaka yako ..unataka aje kupigana na mwanangu au..mwanangu katokea vitani, tumpokee kwa shangwe, mengine yaje baadae, nakuomba tafadhali usije kufanya lolote siku ya kurejea kwakwe muacha apumzika kwanza, unanisikia …?’ mama akamwambia.

‘Hapana mama inabidi niongee na kaka kwanza kuna mambo ya kujadiliana mimi na yeye ni nini hatima yangu, najua nikitoka hapa nitakwenda kuishi huko alipo…tumekubaliana hivyo, sitaki kwenda kuishi na wazazi wangu, mimi nakuahidi mama sitafanya lolote kwa mwanao hadi muda muafaka ufike, nitampokea kama kawaida,…atajisikia yupo nyumbani nakuahidi mama….’akasema akianza kumpigia simu kaka  yake.

**************

Wakati huo huo…Dereva alikuwa akongea na mama yake, na ilionekana kuna kutokuelewana kati ya wawili hawa, mama siku hizi alishaanza kucha kulewa, kumrizisha mwanae,..

Dereva akasema;

‘Mama haya yote nayafanya kwa ajili yako, mimi sitarajii kuishi huku, mke wangu akirudi tu, …naelekea mjini, huko ndio itakuwa maisha yangu. Sasa haya ninayoyafanya nafanya kwa nia ya kukusaidia wewe…nataka uje kuishi maisha bora, na uyasahau machungu yote ya nyuma, watu wakuheshimu,…’akasema

‘Lakini mimi sitaki kupata mali kwa njia hiyo, sawa wamenifanyia hivyo yamepita, ..waache mungu anajua cha kuwalipa, ilimradi mimi nimekupata wewe inatosha tu…’akasema

‘Mama usikubali kuonewa kwenye hii dunia, dunia hii ni mapambano…kwanini wao wasimuogope mungu, wewe ndio umuogope mungu,..kila mtu anatakiwa afanye hivyo,…sasa kama waliamua kutumia njia hiyo, sisi take kimia tu,..tumuachie mungu, waje wafanye tena, tumuachie mungu, hata mungu atatuona sisi ni wajinga, sisi tuwalipizie kwa njia hiyo hiyo…wewe niachie hiyo kazi, utakuja kuona umuhimu wa hili jambo…’akasema

‘Sitaki hiyo tabia mwanangu nimeshakuambia uishi kutokana na jasho lako, …tabia hii itakupeleka kubaya, unataka mimi niwe naishi kwa presha, nikikuwazia wewe, ..hujui mimi nakuhofia wewe, wakikufunga, wakiku..ua…’akasema

‘Mama usifikiri mimi napenda hivi..hapana, lakini ni lazima nihakikishe umepata haki yako, ni lazima nihakikishe machozi yako yamefutwa, waliokutendea haya bado wapo, kwanini tusichukue hatua, hili litafanyika mama..na kama watalipinga..siku hiyo sijui itakuwaje,..mama sipendi yale mashetani yanitokee, lakini ikitokea wamelipinga hili naomba yanitokee tu, niwafunze adabu…’akasema

‘Mwanangu unasema nini…ooh, sitaki hayo mashetani yakurudie tena, mungu wangu…, hayo yakikutokea unakuwa sio binadamu hata mimi mama yako unaweza kuniua, hapana, usiombee hayo..naomba yasije kutokea tena..siwezi kusahau…hapana ni bora tufe masikini tu…’akasema mama yake.

‘Mama…haki lazima ipatikane, kwa namna yoyote ile na ikishindikana ..sijui, ngoja tuone nasikia mtoto wake anarudi…’akasema

‘Soldier…?’ mama yake akauliza

‘Ndio…’akasema Dereva.

‘Halafu ndio unataka kuyafanya hayo mambo yako, ..unamfahamu huyo mtoto wake lakini, ni askari huyo,  ..atakufunga, mwenyewe katokea vitani..hana huruma, …sitaki kuyasikia hayo mambo yako tena, kama hutaki kukaa hapa kesho fungasha ondoka…’akasema

‘Mama,  huyo ni askari na baba yake alikuwa ni askari pia,…nani zaidi kati ya baba na mama, mimi nimeamua kupambana na baba, …mimi nini akili, nina macho, nina masikio…nitayatumia vyema, siogopi yoyote anayeingilia anga zangu,…’akasema huku mama yake akitikisa kichwa kama kukataa.

‘Mama mimi nimepata yoyote atakaye muumiza mama yangu, kaniumiza mimi, …mama wewe utaona tu, lazima nilipikize hicho walichokufanyia,…na huyo mtoto wao akija, huyo huyo ndiye nitamtumia kama chambo, mzee akijaribu kukataa, namwambia nitamuwambi mtoto wake kuhusu uchafu wake…hahaha, mama hapo patamu, wewe subiria pambano lianze…’akasema.

‘Mwanangu nisikie, mimi sitaki na wala sitaki kusikia tena hayo mambo yako, hivi wewe umekuwaje, mimi sijakulea hivyo,…mimi sikuelelewa hivyo, haya yaliyotokea ni sababu yao, sio hulka yetu…ndugu na jamaa zangu wamenitenga tayari, naoneana mchafu…sasa nakuomba mimi usinihusishe kwa hayo mambo yako..’mama akasema.

‘Mama, hakuna kurudi nyuma hapa, kila kipo tayari, unaogopa nini mama, unasahau waliyokufanyia…umesahau kuwa kutokana na hayo ndio maana upo hivyo, sasa mimi ninataka kurudisha hadhi yako…’akasema.

‘Nimekuambia hivyo, kesho ondoka, sitaki kukuona hapa kijijini, utanitia presha…’na mara simu ya huyo mama ikalia, alipoangalia akakuta jina la mama yake Soldier.

‘Mama yake Soldier,..ananipigia leo kuna nini..mmh..’akasema akiiweka simu sikioni


WAZO LA LEO:  Mioyo yetu huumia sana pale tunapotendewa mabaya, na ni rahis sana kusema msamehe, muachie mungu, kwa wenzako,…lakini je tunapowatendea wenzetu ubaya, hatumuoni mungu, au tutende tu, tukijua tutasamehewa. Ni vyema kila tulitendalo, tufikirie mbele, je mimi ningelitendewa hilo ningelijisikiaje,..ukiona ni chungu kwako, basi ujue sio tamu kwa mwenzako!
Ni mimi: emu-three

No comments :