Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeTuesday, March 14, 2017

KITANDA HAKIZAI HARAMU-17


'Mzee,  I have something for you, ..nina ujumbe wako...'akasema huyo jamaa akiongea kwa kuchanganya Kiswahili na kiingereza.

'Ujumbe gani, unamhusu huyu.mtoto au?...mimi sijui lolote,... unajua..'nikataka kuendelea kuongea, yeye akawa anatoa kitu kwenye mfuko wake wa koti,..hapo machale yakanicheza, nikajua sasa...inawezekana jamaa anataka kutoa bastola, ..

Yule jamaa alinipatia karatasi…

'Mzee, don’t worry, mimi ni mjumbe tu,...'akasema na sasa akawa ananikabidhi ile karatasi.

'Ya nini...hii karatasi?'nikamuuliza

'Imetoka kwa mwanao, isome, na mpigie simu, namba imo humo, nyuma ya hiyo karatasi...'akasema , sasa kiongea Kiswahili vizuri, nikajua ni wenzetu , …

'Na huyu mtoto...?'nikamuuliza na yeye hakusema neno zaidi akageuka na kuanza kuondoka.

Tuendelee na kisa chetu..

****************

Nilipoona jamaa anaondoka, na hakuweza kunisaidia lolote kuhusu huyo mtoto na mimi sina muda, ndio nikampigia ukulele kwa kusema;

 'Hey...'nikasema lakini huyo jamaa hakusimama! Akawa anatembea kama vile hana habari na mimi, na mara huyooo akakata kona na kupotelea upande wa pili. Sikutaka kumfuata...niliona napoteza muda wangu, lakini sasa... huyo mtoto…

‘Mambo gani haya..’nikasema sasa nikiwa namtizama huyo mtoto pale alipolazwa...…kiukweli sikuwa na muda, nahitajika muda angalau niweze kupumzika kidogo, kutwa nzima nimekuwa kwenye mikutano, kukutana na watu.basi nilikuwa nimechoka, na saa tisa niwe tayari uwanja wa ndege.

Kwa muda ule sikuwa na haraka na hiyo karatasi niliyopewa,..niliona ni wahuni tu wanataka kunipotezea muda wangu, akili yako kwa wakati huo ilikuwa kuhusu huyo mtoto,.

Nikachuchumaa, na kuanza kumkagua yule mtoto kuhakikisha kama kweli ni mtoto wa kibinadamu au hawa watu wanataka kunichezea viini macho,...au ni mtego,…na mara kile kichanga kikajinyosa, nikajua kweli ni mtoto, na akili ikaanza kufanya kaza sasa, kama ni mtoto nifanyaje, akianza kulia hapo si itakuwa ni taabu.

Kwa haraka akili ikanituma nimuhudumie huyo mtoto nione yupo kwenye hali gani kabla sijwapigia simu mapokezi, na huruma tena, unajua wengi wanafiria sisi wanaume hatuna huruma, sio kweli wanaume tuna huruma sana,hasa kwa watoto, na hasa ukishafikia umri kama wakwangu, huwa tunatokea kuwapenda watoto sana!.

Nikaanza kukifunika vizuri, na katika kufanya vile kile kitoto kikawa sasa kinajinyosha nyosha..najua hapo kinatafuta nyonyo, na katika kujinyosha nyosha huko, sehemu kubwa ya uso ikabakia wazi...

 Sasa nikachukua muda huo kukichunguza kwa makini,  kitoto kichanga, na wakati nafanya hivyo, nikaona kitu kigumi kwenye zile nguo, nikawa nakitoa, ili niweze kuikunja vyema ile nguo aliyofunikiwa, na taulo la watoto kubwa tu.. nikalikunjua na ikadondoka kitu kama kadi ni hizi kadi za mtoto za kiliniki, ambazo hupewa mzazi kwa ajili ya vipimo vya vya mtoto.

 Nikamfunika kwanza yule mtoto vyema, na sasa nikawa naifunua ile kadi, dhamira yangu nijua huyo mtoto ni nani na mzazi wake ni nani…kama itasaidia japokuwa kwa vyovyote vile nilitakiwa nimkabidhi huyo mtoto kwa wahusika wa hoteli.

Kadi ilikuwa bado mpya, na inaonekana mtoto huyo alikuwa bado hajaanza vipimo na hata chanjo, ni kadi mpya kabisa, ila ina jina…

What…’nilijikuta nikisema hivyo tu..nilitizama tena yake maandishi, akili ikiwa bado kwenye mshangao…

Mara simu yangu ikaita,..kwa haraka nikaishika na kuangalia namba ya mpigaji...

Unknown namber…’ imeandika hivyo.

‘Oh,..atakuwa ni nani tena huyu..?’ nikauliza, na kwa haraka nikamua kuipokea hiyo simu.

‘Mzee, ..natumai ujumbe wangu umekufikia, na pia ninafahamu kuwa unahitajia muda wa kupumzika, lakini hili ni bora zaidi,...kwani usipochukua hatua itakula kwako..... usipofuata hayo nitakayokuelekeza, unaweza hata ukachelewa safari yako…’sauti ikasema.

‘Sema…’nikasema hivyo.

‘Ni hivi..tuwekane sawa, samahani nitakuuliza maswali machache tu...., ni muhimu sana mzee kulihakiki hili jambo..’akasema.

‘Maswali gani wewe…unajua unanipotezea muda, na huyu mtoto….’nikasema.

‘Ndio ..ni kuhusu huyo mtoto…’akasema.

‘Ni wa kwako au sio....nilijua tu...nimeshaelewa haya sema kwanini unakuja kumtekeleza hapo mlangoni kwangu, unataka nifanye nini na huyu mtoto wako…?’ nikamuuliza.

‘Kwanini unasema hivyo mzee, nani kakuambia huyo ni mtoto wangu , kwa vipi...?' akauliza

'Kwa vipi...!!' nikasema kwa kushangaa.

'Mzee, hebu jiulize….mimi nitampachikaje mimba mke wa mwanao…. 'akasema

'Mke wa mwanangu anakujaje hapa...?' akauliza

'Ndio hapo nataka unielewe,....ili nihakiki jambo, kwani bado sijawa na uhakika,…, kama kweli niwazavyo ni sawa au la…ni hivi mzee, unajua wewe ni mtu wa heshima sana, tena kiongozi, na unatakiwa uwe mfano bora. kwa jamii au sio.’akasema.

‘Kwanini unasema hivyo..?’ nikamuuliza.

‘Hivi nikuulize mzee, mke wa mwanao Soldier, aliondoka lini hapo nyumbani kwako…?’ akauliza

‘Unataka kusema nini…huyu mke wa mwanangu anakuhusu nini, haebu achana naye kabisa..unamtakia nini...?’ nikauliza.

‘Mzee unajipotezea muda wako, nijibu haya maswali ili niweze kukuambia jambo muhimu, kwa faida yako…’akasema na mimi nikaona nisipoteze muda.

‘Aliondoka muda, nafikiri sasa ni mwaka hivi….’nikasema.

Well, well, nilijua tu....Unaona,…mwaka umetimia, na kitu hivi…kwanini aliondoka..?’ akaniuliza

‘Yeye aliamua kuondoka tu pale mke wangu alipoondoka, kwenda kwao……hata hivyo mke wangu anarudi mara kwa mara…hilo halina shaka,….’nikasema nikitaka kumjibu maswali yake ili nimalizane naye.

‘Sawa kabisa mzee wangu, …na je wakati huyo mke wa mwanao, anaondoka alikuwa mja mnzito…?’ akaniuliza

What….!Hivi wewe ni maswali gani hayo ataupataje huo ujauzito wakati,…..mume wake hayupo..’nikasema

‘Ndio hapo...unaona mzee, hapo hapo....unajua mzee hata mimi naingiwa na mashaka,..siamini, lakini ushahidi upo... sio kwamba nakufikiria vibaya, ….samahani hapo mzee, lakini itakuwaje, unajua ni bahati sana, na mungu ni wa ajabu sana, ilitakiwa itokee hivyo, mimi niwepo, nikutane na hilo tukio, mtoto kaokotwa, na kuletwa ofisini kwangu, anafanana….unajua watu walifikiria vibaya, lakini watasemaje, wakati mimi sina muda mrefu eneo hilo.

‘Unaona ilivyotokea,..’akasema.

‘Hizo ni hadithi zako unatunga kijana humpati mtu hapa..., unajua nikushauri kitu, tunga kitabu, utapata pesa kuliko kuchafuana na watu,  uzushi mbaya, utakuja kukuumbua, acha kabisa hiyo tabia….’nikasema

‘Mzee huu sio uzushi, uzushi wakati kitu unacho hapo, ushahdii kamili…mzee, si umeweza kumkagua huyo mtoto vyema anafanana na nani, utasema anafanana na mtoto wako au sio…?’ akauliza

‘Anafanana na wewe…’nikasema

‘Hahaha,...nilijua utasema hivyo... mzee, mimi sijawahi kufika huko….nilikuwa nchi za wenzetu, wote wanafahamu...nimerudi hivi karibuni tu na kupewa hii kazi maalumu, …lakini sasa mimi siwezi kubeba dhambi za watu wengine, ni kweli anaweza kufanana na mimi maana na mimi nafanana na mwanao, na pia nafanana na wewe au sio..lakini swali rahisi la kujiuliza mke wa mwanao alikuwa akiishi wapi,..au sio…, na mwanao kasafiri muda gani..., utasema nini hapo…’akasema

‘Mimi nitakata simu… sitaki kusikia tena huo ujinga wako…’nikasema.

‘Ukikata simu itasaidia nini mzee, mimi nataka kukusaidia wewe, maana hayo ya mtoto hayanihusu, ni wewe na tabia yako ya kutunga mimba na kuzitelekeza..ushahidi namba moja ni hiyo karatasi uliyopewa,...unanisikia vyema,.. huyo mtoto sio wangu, abadani, ..hata tukienda kupima, utaumbuka bure tu mzee wangu, huyo ni mtoto wako…’akasema  na kunifanya nizidi kupandwa na hasira.

‘We-we…aah’ nikawa nakosa cha kuongea.

‘Mzee usipaniki,…kuna jambo nataka kukushauri mzee wangu,…usije ukaumbuka, maana nikiliweka hilo hewani kuwa umetembea na mke wa mtoto wako, …na ukaamua kumfukuza, unafikiri jamii itakuelewaje, hebu lifikirie kwa makini hilo, mimi ni mwandishi wa maswala ya wakimbizi, nawatetea haki zao kwa hivi sasa..…’akasema

‘Sikiliza wewe mtoto, hivi, unafikiri mimi siwezi kuongea, au kukuchukulia hatua, au kujitetea, andika na mimi nitaandika, kuna tatizi gani hapo…na wewe, hatua hii uliyofikia, naweza nikakufanya kitu kibaya, uka….’akanikatiza.

‘Mzee mimi nataka kukusaidia tu..je mfano ningelisema namfahamu huyo mtoto na baba yake..maana anafanana naye,..., nikawaelekeza watu kwako, unafikiri ingelikuwaje,…?’ akauliza

'Ungefanya tu...'nikasema

‘Mimi nilipoiona hiyo sura ya huyo mtoto nikajua ehee…mzee kazi zake hizo…’akasema

‘Wewe mtoto, chunga ulimi wako,...'nikasema

'Sasa mze hulioni hilo,.....sema ukweli mzee wangu...'akasema

'Wewe unasema mke wa Soldier ndiye alifanya hivyo ulijuaje…?’ nikamuuliza

‘Kuwa ndiye mama wa huyo mtoto au sio...kun mtu alimuona, …nilimuonyesha picha yake, akasema huyu mwanamke alifika huku, akiwa na mwanaume mwingine ambaye kwa maelezo yao, nikegundua ni kaka yake ….kwahiyo kama unaweza kumkabili kaka yake,…muulize, kama ataweza kukuambia ukweli….’akasema.

‘Wewe unacheza na hao watu, utapata shida….’nikasema.

‘Ndio maana nimekuambia wewe ufanye hivyo, kwa kukusaidia,..mchukue huyo mtoto maana ni damu yako, rudi naye kijijini kamtafute mke wako…na huko utamkuta mke wa kijana wako ameshafika,kwanza muulize alikuwa wapi…unaona na kauli kuanzia sasa mtoto ni wa mwanao....watu wakiuliza sana, waambia haiwahusu....’akasema

'Hivi wanifanya mimi mtoto mdogo au....?' nikauliza

‘Mzee hii ni kwa ajili yako, utaumbuka mzee, fanya hivyo mzee, ukifika mbane huyo mke wa mwanao, kama hatakuambia ukweli,  najua kabisa atawaficha,…maana waliifanya hiyo kwa siri… 'akatulia

'Lakini muhimu ni sura ya mtoto, anafanana na nani,,,,mchunguze kwa makini ana kufanana fulani na mama yake..mchunguze, vyema, japokuwa kwa kiasi kikubwa anafanana na wewe, lakini kwa kiasi kingine kuna ushaibihi wa mama, mdomoni...hebu muangalia vyema..'akasema na kunifanya na mimi nimuangalia yule mtoto.

'Halafu… pili, huyo mke wa mwanao, alikuwa akiishi wapi awali, akaondoka akaenda wapi..., kwa muda gani, unganisha hayo yote utajikuta mzee upo matatani…’ akasema.

‘Huyo mke wa mwanangu…’nikataka kusema na yeye akanikatisha kwa kusema;

‘Huyo mke wa mwanao, alipoona ana uja uzito, ..najua utakataa, nikisema wako, …alichokifanya yeye ni kukimbia hapo nyumbani akaenda huko anapokujua yeye, akakutana na kaka yake, na kaka yake akamuambia aitokee hiyo mimba, akakataa..akaendeela kuilea,..., akazaa na alipoona mtoto anafanana na wewe akaamua  kumtupa huyo mtoto….’akatulia.

‘Kwanini avumilie mpaka azae halafu amtupe huyo mtoto…?’ nikamuuliza.

‘Hayo maswali utakuja kumuuliza yeye mwenyewe ila kwa mawazo yangu ni kwa vile huyo mtoto anafanana na wewe,na mlikuwa mnaishi naye humo ndani, akaona itakuwa ni aibu akaamua kufanya hivyo…’akasema

‘Na wewe huyo mtoto alifikaje kwako….?’ Kaulizwa

‘Nimeshakuambia, mimi nimetumwa huku hivi karibuni, na wakati nafika nikakutana na hilo tatizo, mtoto kaokotwa,mimi napenda sana watoto, na huyo mdada aliyefika hapo ndiye aliyemuokota…huyo ni masikini lakini ana roho nzuri, kafanya usamaria mwema kuirudisha damu yako, mshukuru sana,….sasa kazi ni kwako mzee..’akatulia.

‘Mimi hapo sikuelewi,na sitakuelewa, na hilo sijui nikikutana na wewe nitakufanyaje….’nikasema.

‘Wewe ukifika…najua atakukana sana tena sana,..ila mshawishi huyo mke wa mwanao amlee huyo mtoto,..kwanini amtupe,… ni mwanae kwanini amkatae,… fanya ufanyavyo, amkubali huyo mtoto kuwa ni wake..mengine nitakuja kukuambia, tutasaidiana mzee, hiyo kashfa haitajulikana, unasikia…’akatulia

‘Siwezi na siamini hilo…kwanini wewe mtoto unapenda kuniumiza, unataka nife…?’ nikauliza

‘Sitaki ufe mzee kwa kihoro, kwa presha,…hapana mzee, ufe kwa siku zako ndio maana nakusaidia,huyo mtoto ni damu yako,mnafanana naye, hata ukisema anafanana na mwanao, haiwezi kuingia akilini kwa watu, mwanao yupo wapi…na huyo mke wa mtoto wako alikuwa anaishi wapi, hebu mbaneni vyema atakuja kuwaambia..….’akasema.

‘Sitaki kukusikiliza tena…’nikataka kukata simu.

‘Sasa kwa haraka haraka mzee, kuna jambo jingine kwenye hiyo karatasi uliyopewa, mbele ni vipimo vya DNA, ushahidi wa tabia yako, ni ushahidi wa kuthibitisha kile nilichokuambia..kuwa mimi nitautafuta ukweli, kuwa je mimi ni mwanao wa damu au la…mimi sitaki, na sipendi wewe uwe baba yangu, lakini nilitaka niujue ukweli, sasa ukweli nimeshaupata..kwahiyo nitakuja kuufanyia kazi, kuna mambo tunatakiwa mimi na wewe tutubaliane, ili, iendelee kuwa mimi sio mtoto wako…’akatulia.

‘Hahaha, wewe kijana unafikiri mimi ni mtoto mwenzako….eeh, yopte hayo kumbe ilikuwa mbinu, eeeh, haya endelea….’nikasema kwa kujipa tumaini lakini akilini nilishaathirika.

‘Mzee hilo peke yake la kuwa ulifanya hivyo ni kashfa kwako, ulifanya nini na mke wa mwenzako , tena rafiki yako,..ni swali ambalo litakuharibia sifa yako, na ukichanganya na hili la sasa, mzee, utakufa kwa presha,…fikiria sana…’ akasema

‘Acha nife…’nikasema

‘Mzee usiseme hivyo, wanaoo tunakupenda, …. ndio maana nataka kukusaidia, njia rahisi,… fanya hivyo nilivyokuambia, mchukue huyo mtoto,…na nimeamua kukusaidia, kwa hilo maana hicho kichanga kinahitajia huduma na nikaona ni vyema nimtafute mtu ambaye ataweza kukusaidia hadi ufike kwenu,  atakuja yaya hapo, wa kukusaidia, kama unataka lakini, halafu ukifika kwenu yeye atarudi, ..mimi mpaka hapo nimetimiza wajibu wangu….’akakata simu.

Kitoto kikaanza kulia….

NB: Haya, hivi jamani mnaelewa hapo, kumbe..mke wa Soldier, aliondoka , pale mke wa kiongozi alipoondoka, unakumbuka siku mke wa kiongozi alipoziona picha, aliamua kuondoka, na alipoondoka tu, na mke wa Soldier naye akaondoka…


WAZO LA LEO: Kuna watu wanapenda kutumia mitandao hii ya jamii vibaya, kuhadaa wengine , kutunga uwongo, ..kuweka mambo yenye kuharibu jamii nk…tuogopeni haya, kwani huu ni ushahidi mkubwa , ambao utakuja kukushitaji, unapoandika unaweza kuona ni jambo la kawaida, hakuna atakyekuona, nk..lakini umesahau kuwa yupo anayekuona hata ukiwa umejificha pangoni. Tuweni makini jamini, kwanini tusitumia mitandao hii kusaidiana, kusaidia jamii, na kila unachokiandika jiulize je akikisoma mwanangu, mzazi wangu nk..kitafaa….ni hayo kwa leo.
Ni mimi: emu-three

No comments :