Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeThursday, February 2, 2017

YOTE MAISHA...


…Nilijua labda anaumwa, lkn kumbe sio ,… nilijua labda ana tatizo la kufiwa au… lkn sivyo kama nilivyodhania, kajiinamia, kalia mpaka machozi yamekauka, ..nilimuonea huruma sana,lkn utafanyaje, hukumu imeshapita na iliyobakia kusonga mbele.

‘Vijana mbona upo hivi…..’ nikamuuliza kijana huyo, Swali langu lilikuwa kama limeamusha moto uliokuwa umefunikwa na majivu, na uliwekwa mafuta ukawa umezimika kwa upepo tu….

‘Wamenionea, mtihani wa darasa la pili nilipata division one tena ya uhakika, darasani nilikuwa naongoza, nimesoma kwa shida, wazazi wangu masikini na nilijua huenda ikawa nafasi ya kuwaokoa wazazi wangu,...nimesoma huku naumwa, lakini sikukata tamaa...…sasa ….’akaanza kulia

‘Kwani umepata divisiona ngapi?’ nikamuuliza

‘Eti three,..inayokaribia na four…mimi..hapana haiwezekani, yaani wamenipita hata wale niliokuwa nikiwafundisha, uso, wangu nitauweka wapi, ..natamani hata …ardhi ipasuke nizame…nisionekane tena hapa duniani, nawaonea huruma wazazi wangu wamepoteza pesa nyingi kile kidogo walichokuwa nacho walijinyima ili nisome, sasa nitawaambia nini....siwezi,siwezi kuwaona wazazi wangu wakihuzinika tena, kwanini sisi...kwanini...…’yalikuwa maneno yaliyonifanya nihuzunika na niogope!

‘Sikiliza kijana…., unajua hata kwenye mahakama, unaweza kuhukumiwa ukawa hujaridhika, na ndio maana wanatoa nafasi ya kuapili…unanielewa,…wanaosahihisha hiyo mitihani ni wanadamu tu…ndio maana, hata kwenye hii mitihani kuna nafasi hiyo ya kuapili…si unajua kuna kukata rufaa kwa ajili ya kusahihishiwa tena, wewe kama unajiamini ulifanya vyema, nenda kajaze fomu , watakusahihishia mitihani yako tena.

‘Sasa kwanini wafanye hivyo,…ukate rufaa ndio waone makosa yao,..na hata hivyo mimi nitapata wapi hizo pesa,..wazazi wangu ni masikini…niambie sasa?’ akaniuliza, hapo nami nikabakia kimia.

Matakeo ya mitihani yameshatoka, wapo wanaofurahia, na wapo wanaohuzunika, wapo ambao wanajuta kwa hasara walizopata maana kusomesha sio mchezo, lakn mimi najiuliza upimaji huu wa mitihani hivi kweli unaleta taswira halali ya uwezo wa wanafunzi wetu…, au ndio mazoea tu.

Inawezekana kweli wengi wa waliofaulu walikuwa wakifanya vizuri darasani,..lakini je tulirejea kuangalia matokea yao ya kidato cha pili,…ufaulu wao na wa sasa, ili kuone labda kuna makosa kwenye usahihishaji, au kuna sababu nyingine… na ukiangalia wengi wa waliofaulu  wametokea shule zenye uwezo, walimu wazuri, mandhari, vitendea kazi nk…je hili kama serikali tunaliangaliaje,…hatuoni kama tunawagawa wananchi…

Kiukweli kufaulu mitihani ni moja ya nafasi kubwa sana ya kuwapima na kuwaendeleza vijana wetu..lkn mimi bado nina mashaka katika upimaji huu wa Nani zaidi…HEBU TULIANGALIE HILI KWA JICHO LA UFAHAMU WA PILI ILI TUTENDE HAKI!.

Wasiwasi wangu ni kwa hawa vijana ambao wamechanganyikiwa na matokeo haya ya mitihani, na wasipopata wazazi wazuri wa kuwanasihi vijana wetu, watoto hawa wanaweza kubadilika na kuwa wengine kabisa,…hawataona umuhimu wa elimu tena, na huenda wengine wakafikia kufanya vitendo vibaya. Tulishuhudia kipindi fulani wengine walifikia hadi kutaka kujiua.

Mimi nina imani kuwa huenda wengine wangeliweza kufanya vyema zaidi ya hayo waliofanya vyema kama wengelikuwa kwenye nafasi za hao waliofanya vyema, lakini watawezaje kukaa huko..yote maisha…hawa sasa, watarudi nyumbani, na kujiunga na makundi haramu…au ndio kwaheri tena na elimu ya shule! watafanya nini tena...Yote maisha!

 Mimi naona kuna haja ya kutafuta awamu nyingine ya kuwapima hawa ambao wanaambiwa wamefeli, labda paitwe,..elimu ya nafasi ya pili, wapimwe, kama kweli wana uwezo waweze kuendelea mbele, au wajiunge na vyuo fulani maalumu kutokana na vipaji vyao…hawa ni watoto wetu sote!


Pia, hawa wanafunzi pamoja na mitihani hii ya mwisho, lakini kuwe na maksi za mitihani ya nyuma, asilimia fulani, ihusu matokea ya nyuma , kama wanavyofanya vyuoni, na mtihani wa mwisho uwe na maksi zake, ili zijumlishwe pamoja na kuona je kweli hawa vijana wetu wameiva, huku nyuma walikuwa wanafanyaje…tuwapime hata vipaji vyao nk…. Hii ni  hatua nyingine ya kuwapa vijana wetu elimu stahiki,  ili mwisho wa siku tuwe na wakufunzi wazuri na pia vipaji visje kupotea bure.

Ni maoni tu kutoka kwa mzee wa busara…
Ni mimi: emu-three

1 comment :

WAZIRI MSUYA said...

Ni kweli baba ila tatizo ya mfumo wetu hatuna pakuyasemea hayo na hata ukisema hayasikilizwi