Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeFriday, February 3, 2017

UONGOZI NI DENI,... ni dhamana..


 Majogoo yana tabia yake, kwenye mitaa, akija jogoo mgeni ni lazima kutatokea kupigana na majogoo wenyeji, kupimana nguvu, na wakikutana majogoo wenye nguvu sawa, wanaweza kupigana siku nzima, kisa nini hasa, kwanza ni kuonyeshana ubabe nani zaidi, lakini pia kumiliki mitetea,…na kutawala,  hayo ndio maisha yao..na maumbile yao…, ubabe ubabe.

Mitetea nayo hujibaragua kwa hayo majogoo, hasa wakiona huyo jogoo ndiye mwenye nguvu, hata vifaranga havichezi mbali, kwani kwa kawaida majogoo hupenda vifaranga, na wakati mwingine huwaita virafanga kwenye chakula…wakifanya hivyo hata mitetea nayo huja karibu karibu, na hapo jogoo anakipata kile anachokitaka.

Wakati nafurahia maisha haya ya kuku, nikasikia mkuu wa taifa kubwa akisema yeye ni taifa kubwa na ana uwezo wa kufanya mambo kwa masilahi ya taifa lake,hata ikibidi kuwahamisha wageni wote, ambao kwake yeye anaona ni adui wa taifa lake, ..ubabe, lazima ajionyeshe kuwa yeye ni nani, na taifa lake ni nani….!

Ni kweli wapo wakorofi, wapo wenye sera mbaya, lakini pia kuna wenye shida, sizani kama mtu atakimbia nyumbani kwake au nchini kwake kama kweli hakuna shida, na shida nyingine chanzo ni huko huko, …tujiulize silaha zinatoka wapi…, propaganda za kuwagawa watu wapigane ili kuwe na namna ya kupata mali ghafi, zinatoka wapi …ni ujanja ujanja wa ukoloni mambo leo…

Kwa ufupi, sio kwamba wao wamependa, wameona sehemu nzuri ya kuishi ni huko,… lakini leo hii wao sasa wanaambiwa mkafie kwenu, `kama hamuwezi kujitawala tuje sisi tuwatawale…' ni kebehi,… japokuwa ukweli mwingine unauma!

Hata hivyo pamoja na mengine nimefurahia sana sera ya huyu bwana mkubwa, sera ya kupiga vita ni hiki kizazi cha hatari , kizazi ambacho kinataka kueneza maisha ya ‘Sodoma na Gomora’, hawa watu wanataka kuiangamiza dunia,…hawa watu ni kizazi kile kilichlaaniwa na sasa kimekuja na mtindo mpya wa `haki za binadamu’, jamani huo ni ubinadamu au ni unyama, kwa hili mimi nampongeza huyu mkuu kwa kulivalia njuga hili janga.

Na wakati sijaendelea kulitafakari hili mara nikasikia mkuu wetu wa kaya naye akiongoza vita vya kupambana na janga jingine kubwa, la ‘madawa ya kulevya’.. ambalo limewashinda viongozi wengi,..sijui kwanini, nasikia kuna ‘kuogopa’ maana mtandao huo ni mkubwa, una wakubwa na matajiri wa hali ya juu, lakini uongozi ni nini…, kiongozi ni yule anayefanya mambo kwa masilahi ya watu wake bila kujali hatari yake, kwani uongozi ni dhamana, uongozi ni deni, na usipoifanyia kazi hiyo ambayo ni dhamana kwako,  utakuja kuulizwa mbele ya haki.

Wengi wa viongozi wanapoingia madarakani wanajaribu kutimiza wajibu wao,...kuonyesha wao ni nani,  lakini baadae wanafikia sehemu wanaonjeshwa asali ..na asali hulambi mara moja,…na ukilamba sana unalewa, dhamana inasahaulika, na matokea huja kuwa `nguvu za soda..', nawaombea viongozi wetu wasifikie huko, vita hii iwe ni endelevu…

Nakumbuka kisa cha viongozi wa imani, walikuwa hawalali, usiku wanapita mitaani wakiwa wamejibadili kama raia wa kawaida, nia ni kutaka kujua hisia na matatizo ya raia zake, walikuwa hawalali, hawali wakashiba, hata kuvaa vizuri wanaogopa,…..hawanenepi..watanenepaje wakati hata kula wanaogopa, kwani wakila wakishiba, wanajiuliza hivi na raia zangu wameshiba…hawa ndio viongozi wa kweli..., raia wangu kwanza, mimi mwenyewe baadae…

Wakati sasa umefika, tuwasaidie viongozi kama hawa, ambao kweli ndio tuliokuwa tunawataka, …tuondakane na majanga haya yasiyokwisha, ..tunaona raha gani tukiwaona vijana wetu wanateketea kwa madawa ya kulevya, ushoga, usagaji..ulevi, wizi na ujambazi, wakati huo huo watu wengine wananeemeka, wanajenga mahekalu kwa kafara la vijana wetu….inaumiza, na dhambi kubwa sana mbele ya mungu,..ndio maana hata ile baraka na neema ya sili inakimbia, tukikaa kimia, kwasababu eti sio watoto wangu wanaoumia,…ni leo kwao kesho matatizo hayo yatahamia nyumbani kwako, na ukienda mbele ya haki una mashitaka makubwa….


Tumuombe mola atusaidie vizazi vyetu viondakane na majanga haya hatari, na viongozi wetu watimize wajibu wao kwa uadilifu, na wale wote wenye nia mbaya ya kuangamiza wenzao kwa masilahi yao, washindwe na wafichuliwe. 
Ni mimi: emu-three

No comments :