Ni sinema au ni MOVIE…(FUPA LILIMSHINDA FISI)
Wakati tunasubiria sehemu nyingine ya kisa chetu cha FISI
LILILOMSHINDA FISI NIKAONA TUANGALIE PICHA…SINEMA…TASWIRA YA PICHA…..
***************************
Ndio picha imeanza…..inaonyesha taaswira mbili, vitani na uraiani!
‘Mara anaonekana kamanda wa vita yupo msitari wa mbele
kupambana na maadui..akiwaekeleza wapiganaji wake cha kufanya…na milio ya
mizinga inasikika huku na kule….
Mara tunapelekwa ofisini, kwa mpokea taarifa,…kuna taarifa
imekuja na mjumbe!
`Kamanda anahitajika nyumbani , ana kesi ya kujibu,…’
‘Kesi ya kujibu,..kesi gani, na nani kasema …?’msemaji wa
kamanda akauliza
‘Ni kesi ya jamii, sheria inamuhitajia…’akaambiwa….
‘Hawezi kurudi nyuma..yupo mstari wa mbele akigeuka nyuma,
maadui watajua kasalimu amri, na itakuwa ni nafasi ya maadui kuendeleza
mapambano…’akasema mleta taarifa.
‘Lakini anatakiwa na sheria, na sheria ni msumeno, na yeye ni
mmoja wa watu wanaotakiwa kuitekeleza sheria kwa vitendo…’akasema mletaji wa
taarifa.
‘Kwenye vita, sheria za ndani zinasubiria kwanza…’akasema
msemaji.
Na mara tunaonyeshwa upande wa pili , uraiani…kuna zogo la
zomea zomea, mara watu wakasikika wakisema na kupaza sauti; `alatwe aletwe….’
Kwa namna nyingine wapiganaji wanawasiliana na uraiani
wanapata taarifa za nyumbani kuwa kuna vurugu,…. Wapiganaji wakapeana taarifa,
nyumbani kuna vurugu, wakahisi huenda maadui wamepenya kuja kuwavamia kwa
nyuma,…kunatokea sintofahmu…
Mmoja wa wapiganaji anamuendea kamanda na kumuuliza;
‘Kuna nini huko…?’ sasa badala ya kutuliza akili kumkabili
adui wapiganaji wanapata changamoto nyingine, wanahitajia majibu haraka ili
kutuliza akili zao…kuna nini huko nyumbani!
Wakati huo huo tunaonyeshwa mjumbe anabishana na mzungumzaji
wa kamanda…
‘Ni sheria gani ilisema sheria za ndani zinasubiria…?’
akauliza mjumbe aliyetumwa..na kwa namna fulani,…sauti yake ikawa inasikika
uraiani!!,…. watu wakasikia, na kuanza kushangilia….kelele zinaongezeka, ….
Na kwa namna nyingine…kelele zinawafikia hata wapiganaji,
wapiganaji sasa wanageuza vichwa nyuma…
‘Kuna nini huko…..’. wakati wanageuza vichwa sinema ikaganda!
Swali, hawa
wanaoshangilia, ni nani na wanataka nini…!!! Tukajiuliza sisi watazamaji wa ‘movie,
na mara movie ikaisha hapo na kusema;
‘Angalia sehemu ya pili….’
Tuache movie iendelee…lkn,…
Mimi nikabakia na maulizo
akilini, najiuliza maswali mengi kichwani,
‘Hivi hiyo vita ni ya nani, ilikuwa ya nchi au ya kung’arisha
nyota,…je hili linalofanyika lina faida au halina faida kwetu, hasa kwa kizazi
chetu, hasa kwa taifa letu..,…tusije kugeuza vita ikawa ‘vutia’ hapana...hapana...
Ninasema hivi huku nikiangalia kwa uoni wangu,…kama sio
mtoto wako, kuna jamaa yako,
kaathirika na hili janga la ‘malegeza’ mimi
nayaita haya madawa ya kulevya ‘malegeza’. Hii ni vita kubwa, duniani….haijaanzia
hapa…!
‘Vita hii ni kubwa ina kila aina ya mbinu…sio vita ya kung’arisha
nyota hii, tuweni makini sana’
Haya ngoja tuje kuiona sehemu ya pili ya picha,..
NB: Soma kisa kipya
cha ‘Fupa lililomshinda fisi…’ utayagundua haya….!
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment