Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, February 27, 2017

KITANDA HAKIZAI HARAMU-4



Mtoto alikuwa analia, mzee mmoja akasema ‘mtoto anamuhitajia baba yake, Yaya akaambiwa amlete mbele, walipokuwepo Soldier na mkewe…na muda huo, mtoto analetwa mbele, Kule mlangoni, akaingia Dereva, ukumbuke huyu dereva alishauteka ubongo wa Soldier kwa hisia zake, huenda..huenda….

Kwahiyo Soldier alipomuona Dereva anaingia mlangoni, na mtoto keshaletwa mbele yake, kukawa na hisia fulani kichwani mwake, na hisia hizo zilimfanya ageuka kumuangalia Soldier, na tendo hilo, na kwa jinsi alivyomuangalia, lilivuta hisa za watu mle ndani na wao wakageuza kichwa kuangalia huko mlangoni….

tuendelee na kisa chetu…

***********
Soldier alipomuona dereva akiingia kule mlangoni, …alihisi mwili ukimchemka, hakujua ni kwanini,..alihisi hivyo tu, na wakati huo mtoto alishaletwa mbele yake, lakini yeye bado alikuwa akichungulia kule mlangoni lakini sio kwa moja kwa moja…

‘Haya baba yako huyo hapo…’akasema baba yake.na mtoto akawa ametulia,halii tena!

‘Unaona amenyamaza…damu ni damu tu….’ Akasema baba mtu.

Lakini Soldier kiakili alikuwa hayupo hapo, akawa mara kwa mara anatupa jicho kule mlangoni, na mara akamuona mama yake akisimama na kutembea kuelekea kule alipolekea Dereve, japokuwa dereva alikuwa hakonekani kutokana na wingi wa wtatu waliokuwa wamekaa upande huo, ….

Na mara Dereve akaonekana, akitokea kule alipokuwa na kuja sehemu ya wazi pale aliposimama mama yake, wakawa wanaongea jambo…

Kitendo kile kilimkumbusha Soldier maneno ya baba yake,…

‘..Najua, na hata ingelikuwa mimi, ningechukua hatua kali sana, lakini …usije kumvunja mama yako moyo, yote hayo ni kwasababu ya mama yako..
Mama, mama..kuna nini ….mmh…akawa anawaza, lakini alishituka akipoguswa begani na kuambiwa…

‘Soldier mwanangu tupo pamoja…’ilikuwa sauti ya baba yake ambaye alishahisi kuna jambo kichwani kwa mtoto wake.

‘Tu-tupo pamoja mzee…’akasema, kukawa sasa na minong’ono mingi kule walipokaa watu wengi, ….!

 Kawaida, minong’ono ya watu wengi hugeuka kuwa kishindo, watu walikuwa wakinong’ona, wakiuama masikio…kila mmoja akiteta na mwenzake aliyekuwa jirani yake,,na mngurumo wa kunong’ona ukazidi, na kumfanya mwenyekiti kuingilia kati na kusema;

‘Hahaha, wanadamu bwana…kitu kidogo tu kitazua minong’ono, umbeya…acheni hiyo jamani,…’akasema na watu wakacheka.

‘Haya…Unajua wazee wana hekima zao, na kwa vile mimi ni kiongozi wenu siwezi kuliacha hili likapita bure, na mkaja kutoboana masikio kwa kunong’onezana…mengi yamekuwa yakisemwa,..mara ooh, , mara eeh,…mwenyekiti, mtoto..aah, acheni acheni…au niseme…?’ akauliza na watu wakasema;

‘Semaaaah…’watu wakasema

‘Hahaha, mimi ni mzee, na macho na masikio yangu yameona mengi…. nimeona alipoingia dereva pale mlangoni imekuwa ni gumzo,...hahaha,..kwani kitanda kinazaa haramu bwana...’ Aliposema hivyo watu wakacheka .

Soldier akasikia maneno yale tena ,sasa kutoka mdomoni mwa baba yake....'kitanda hakizai haramu..'...na akilini akayapigia mstari,..!

‘Jamani, jamani …  haya yote yametoka wapi, ina maana hamuniamini mimi kiongozi wenu, lakini hata kama akiwa ni mwanangu, kwani mimi ndiye wa kwanza kufanya hivyo, kuwa eti kwa vile anafanana na mimi ..hahaha, mbona hata mimi nafanana na baba yake mbona hili hamlioni, wanaomkumuka baba yake enzi za uhai wake, waseme ukweli, hatufanani na baba yake....acheni hizo, nitawashughulikia kama mwenyekiti nikisikia mnateta mambo ya umbeya , haya malizeni kuongea ili tuendelee….’akasema na watu sasa wakawa huru kuongea kwa nguvu.

‘Haya yamekwisha tuendelee…’akasema muongoza shughuli..

Soldier aliposikia hivyo, akahema kidogo kwa kujirizisha, japokuwa hapo napo kumezuka jingine, kichwani mwake, huyu dereva ni nani, mbona simkumbuki kabla,…akajaribu kumchunguza wapi alipokuwa dereva, lakini hakumuona, hata mama yake hakuwepo ndani tena, hali hii ikazidi kumpa mashaka, …sasa mama na dereva,…mara dereva anafanana na baba, watu wanasema ni mtoto baba yake…baba anafanana na …..,kuna nini hapa…akageuka kumchunguza mtoto,…

‘Kweli mtoto anafanana na yule dereva,..na dereva anafanana na baba yake…na baba yake, …oh, .kuna mtihani hapa…’akawa anajiongelesha kichwani, na kwa kujiiba akawa anamkagua baba yake…anamafhamu lakini hili linaloongelewa sasa linamchanganya…

**********
‘Haya ni muda wa shujaa kuongea jambo…, kusalimia jamii,…na kuanzia sasa mimi nawaachia shughuli yenu, muiendeshe kiujna zaidi, mambo ya uzee, kimila tunayamaliza...mimi kwa heshima na kaa kwenye kiti changu cha uenyekiti..’akasema baba mtu na kuelekea kwenye kiti chake.

 ‘Haya ni wakati wako shujaa wetu kusalimia jamii, na kuwakaribisha wenzako ili na wao wafanye hivyo hivyo, mtusimulie kidogo ya huko, watu wana hamu sana kuyasikia,…’akasema muongoza shughuli,
Hapo Soldier akasimama na kwanza akawasalimia wakubwa na wote waliohudhuria shughuli hiyo…baadaye akaanza kuelezea kidogo kuhusu kazi waliyokwenda kuifanya huko na akaelezea kidogo mitihani  waliyokutana nayo huko, na akafikia sehemu akasema;

‘Kuna kipindi nilitekwa na maadui,..baada ya kazi kubwa tuliyoifanya, ..maadui wakawa wananisaka sana,..na ikatokea bahati mbaya, wakaniteka,…ilikuwa tumemaliza, lakini basi tu…wakanitesa sana,, hadi kupoteza fahamu na kumbukumbu,..na nilikuja kupatikana kipindi cha mwisho mwishoni tu…….wengi walijua nimeshauwawa..hata nilipopatikana, na kupelekwa kwa..docta hakuamini,…alijua nitakuwa mwendawazimu,...docta anasema mimi nina bahati sana, kwa vile mwili wangu una nguvu za asili la sivyo, …ooh,..kiukweli huko sio sehemu ya kuombea, msiombe vita jamani,..’akatulia akiwaangalia wenzake.

‘Kwa kifupi tu, namshukuru mungu tumerudi salama..na wenzangu …najua mna duku duku la kujua mengi kutoka kwetu,…ilikuwaje..mmh, sio rahisi kuyaongea ya huko tukayamaliza….’akatulia akigeuka kumuangalia baba yake, na akaangalia pale alipokuwa amekaa mama yake,..hakuwepo bado…

‘Najua kuna mengi mnatarajia tuyafanye hapa kijijini, na sisi tumejipanga kwa hilo, maana licha ya vita huko pia tumejifunza mengi.. kama, kilimo, ufugaji, na hata maendeleo ya viwanda, wenzetu kule wapo juu, licha ya kuwa nchi yao imetawaliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe…lakini wapo mbali sana, tulipata bahati y akujichanganya na raia, kwahiyo tumejifunza mengi sana,…, na sisi tumeona yale mazuri yao tuyalete huku, na mabaya kama vile ya vita tuwaachie wenyewe, maana vita sio jambo la kuombea….’akatulia.

‘Nisipoteze muda,  niwakaribishe wenzangu wasalimie, na kila mwenye la kuongea aweze kuongea, maana tuna mengi sana kutoka huko, wengine naona hawakujaliwa kufika, lakini mtawaona, tukianza shughuli zetu tulizozipanga,. ..na pia tuna ….hamu ya kusikia mengi kutoka huku, miaka mitatu ni mingi sana, mengi yametokea….nashukuru nina mtoto…’akasema akimuangalia yule mtoto…’watu wakashangalia, na kuongea ongea..

‘Sikulitarajia hili, kwangu mimi ni furaha...’akatulia na hapo kukawa na watu wanaongea ongea, hakujali

‘Nachukua furusa hii kuwakaribisha wenzangu, tukianzia na taratibu zeru za kijeshi,….’akaanza kuwaita wenzake mmoja mmoja, na baadaye wakamalizika, na muongoza shughuli akamgeukia mwenyekiti akitaka kujua kama kuna zaidi…

‘Najua umbea ya unazidi…miaka mitatu, mbona mtoto wa miezi ..mitatu,---ooh mine, kulikoni, ..hayo haywahusu, huyu mtoto baba yake ni huyu hapa..anayebisha ajitokeze…’akasema kwa sauti ya kibabe, na watu wakawa kimia.

‘Sasa Soldier, nilishau jambo, ..wazee nisameheni kidogo, huu muda ni wewe kusogea pale kuwasalimia, wake zako,..ukitoka hapo uatakwenda kumsalimia mama yako, …na mama mkwe wako….na wengineo  baada ya hapo, mnaruhusiwa kusalimiana na wengine,, kupeana mikono…..na mambo mengine yaendelee au sio…’akasema mwenyekiti!

‘Mama yako yupo wapi…?’ akauliza

Na mara mama akaingia kutokea nje, akiwa peke yake, dereva hakuonekana, ..mama alikwenda na kukaa kwenye kiti chake, na muda huo ilikuwa ndio watu wanasalimiana, kushikana mikono,..kila mtu kwa wakati wake…na Soldier naye akawa kamaliza kuwasalimia wake zake, na sasa akageuka pale alipokuwa amekaa mama yake,…taratibu akamuendea…na alipomfikia mama yake, alishangaa kuona machozi machoni mwa mama yake..

NB: Ni kwanini mama analia?


WAZO LA LEO: Kichwani mwa wanadamu kuna mengi sana, na kila mtu ana mawazo yake, hisia, dhana,..hujengeka kichwani mwetu.. na tukio dogo tu linaweza likajenga dhana nyingi tu, nyingine za ukweli nyingine sio za ukweli. Aliye na hekima, hawezi kuwa mwepesi kuhitimisha dhana yake kuwa ni kweli mpaka kuwe na ushahidi sahihi.., na itakuwa ni umbeya kusema kila unachokihisi wewe, labda kutokana na tukio fulani bila uashahidi…kuwa ni sahihi… Tujenge tabia njema kwa kutokuwa waropokaji!
Ni mimi: emu-three

No comments :