Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeMonday, February 20, 2017

KITANDA HAKIZAI HARAMU-1


Hebu fikiria, mume ni askari, kaenda kwenye kazi za kivita za kimataifa , huko alikaa miaka mitatu....huko kakutana na majaribu mengi tu, lkn kwa vile , anafahamu yupo kwenye ndoa, akawa anajilinda, mengine ni siri yake..yeye alijua kuwa ana mkewe nyumbani na anamapenda sana, na hakutaka kuja kumuumiza !

Miaka mitatu shaaah...,!
Na mume huyo akiwa huko na wenzake, wanakaa wanaongea, na yeye alikuwa haishi kuwahadithia wenzake kuhusu mke wake alivyo mnzuri, mcha mungu, tabia nzuri..na anawaambia wenzake, furaha yake itazidi sana pale akirudi nyumbani salama..anamuomba mungu sana arudi salama kwani alikuwa hajaishi na mkewe kwa muda mrafu .., maana vita ni vita..

'Nataka nikirudi nyumbani furaha yangu ikamilike, na itakamilika sana, tukipata watoto, napenda sana watoto...'akasema, akiongea na wenzake.

'Ina maana hujapata mtoto bado..?' akaulizwa na wenzake wakimshangaa.

'Hapana..nilikuwaja sijajaliwa,..mimi sikuoa haraka sana,..nilichelewa, unajua kusoma tena,..na nilipoa, hata mwezi haujapita,....ndio nikapata hii misheni ya miaka mitatu,..'akasema.

'Kwahiyo kama ulimuacha mkeo ana mimba, basi tukimaliza hii miaka mitatu, mungu akipenda, utamkuta mtoto wako akiwa na miaka miwili au mitatu au sio..?'mwenzake akamuuliza.

'Ndio hivyo....yawezekana, lakini mimi sina uhakika na hilo..kuwa labda nilimuacha mke wangu akiwa mja mnzito,..hapana sina uhakika na hilo..'akasema

'Ok, kwani...?' mwenzake akataka kumuuliza zaidi na yeye akaendelea kuongea.

'Kama wakati naondoka alikuwa kashika mimba sawa, ni furaha iliyoje, mbona nitafurahi sana..unajua tatizo la huko kwetu hakuna mawasiliano kabisa hata simu za mikononi hizi hazishiki mtandao,..ni shida...'akasema
'Unajua hata sijui kama pesa ninazotuma zinafika au la..lakini najua zinafika maana mambo yote yanapitia makao makuu..na wazazi wangu wapo ...ndio maana sina mashaka na hilo..'akazidi kuongea.
'Sasa mbona mpo nyuma sana..'mwenzake akaongea.
'Ndio hivyo,..ni matatizo ya mawasiliano tu hata barua ukiandika, mpaka ifike huko ni kazi kweli, basi mimi wakati naondoka tuliongea na familia kuwa mimi haina haja ya kuandika barua ..kama lolote litatokea kubwa sana,...wataambiwa makao makuu na mimi nitapata taarifa...'akasema.
'Nyie watu wa ajabu sana,..hata barua, hata simu..mnaishi wapi huko, ni maporini au mapongoni...'mwenzake akasema.

'Ndio hivyo, ..tutajitahidi tubadilike, nikirudi mimi na wenzangu,tufanya kila jitihada eneo letu liwe na maendeleo pia....tumekuja vijana wengi kutoka huko,...tutaleta maendeleo, wewe subiria tu..'akasema.
 Maisha yakaenda, siku zikaenda, hatimaye ule mkataba wa miaka mitatu ukaisha, jamaa akiwa na furaha tele wakaagana na  wenzake, na siku hiyo ya kuagana, akili yake haikuwa pale zaidi ya kuwazia huko nyumbani kwao,...moyoni akawa amejenga taswira nyingi,..kuhusu mke wake,..na huenda akawa na mtoto,,
'Mtoto...mmh..yawezekana, mbona nitashukuru sana...' akaongea moyoni. Hata hivyo hilo la mtoto halikuwa na nguvu sana akilini mwake, kwani hakuwa na uhakika kuwa mkewe alitunga mimba kipindi kile, ilikuwa bado mapema...
'Ndio nakumbuka niliondoka mke wangu hajapata siku zake,..zilipitiliza, huenda  labda aliwahi kutunga mimba....sijui kama hivyo nimkute mke na mtoto, sijui nitafanya sherehe gani, sijui....mmh, mungu anajua, lakini vyovyote iwavyo, muhimu nimerudi nyumbani salama.....'akawa analiwazia hilo hivyo..
Akili yake hakuacha kuwazia hilo la mtoto, alijaribu kulikuwepa lakini halikuondoka, maana wenzake wote walikuwa wakilizungumzia hilo...na yeye akawa sasa anajenga taswira hiyo kuwa huenda ana mtoto, na mkewe atakuja kumpokea akiwa na mtoto...huenda atakuwa mwanaume au mwanamke, kama ni mume watakuwa wanafanana na yeye, na kama mwanamke atakuwa anafanana na mama yake....
'Kama ana mtoto, ..mmh, miaka miwili...'akasema akitabasamu..

Ukiwa na mawazo huwezi kujua kuwa muda unakwenda hakujua kuwa sasa wameshafika, alishangaa sauti ikisema wamefika...
Ndege ikatua ardhi ya nchi yao..na wakatoka kama mashujaa waliorudi nchini mwao...waliokuja kupokelewa wakapokelewa, na yeye hakutarajia kuwa atakuja kupokelewa, maana hakuwa na mawasiliano na jamaa zake kwahiyo alikusanya mizigo yake akaiweka sehemu sasa akawa anageuka huko na huko kutafuta usafiri.
Na kabla hajasogea mbali na mizigo yake mara akashikwa bega...
''MUME wangu...'ilikuwa sauti ya mkewe, na kilichofuata hapo ni mikumbatio ya nguvu..na baadaye sauti ya mtoto mdogo ikasikika mtoto analia, na ni karibu na pale waliposimama, yeye akageuza kichwa kuangalia upande ule, ilipotokea sauti.

Alikuwa kasimama binti kambeba mtoto..mtoto mdogo,...ni sawa kama kumuita mchanga, kwa muonekano hajafikisha hata mwaka,..na inavyoonekana huyo binti alikuwa sambamba na mkewe, na mkewe akasema.
'Mtoto anamdekea yaya wake....mlete huku amuone baba yake...'akasema mkewe, na yule binti akasogea na ishara ya kupiga magoti na kutoa shikamoo..na Soldier, kwanza alimtupia jicho huyo mdada,...ni mdogo, ni msichana kama miaka kumi na nane au tisa, ana umbile dogo,...na alionekana kama kuogopa,na muda wote akawa kaangalia chini.
 Soldier kwa hamasa, akamuachia mkewe akageuka kumuangalia huyo mtoto akiwa kapakatwa na huyo yaya..
'Mtoto wetu huyu...'akasema mkewe bila wasi wasi na tabasamu tele mdomoni...

'Mtoto wetu...?' akauliza Soldier, kwa mshangao na tabasamu

'Ndio ...toto, baba yako huyu...'akasema mkewe 
Kwanza mumewe akabakia kaduwaa, akimuangalia huyo mtoto....sijui ni furaha, sijui ni nini na kila muda ulivyokwenda, uso ukawa unabadilika, furaha ikawa kama inayeyuka.. akisita, akawa anamkagua yule mtoto kwa macho..kwa haraka akakisia kuwa yule anaweza kuwa na miezi kadhaa...mbona, haiji...miaka miwili ilitakiwa awe mkubwa, au.....
Bila ajizi japo kwa kusita akamchukua yule mtoto kutoka kwa yaya wake, akampakata....alihis mwili ukimcheza...na machozi yanamtoka.....alimwangalia yule mtoto akambusu...huku machozi yanamtoka kama maji....
Swali hapo....; UNAHISI ANALIA KWA FURAHA, au NI KWANINI analia....atafanya nini..ujue huyu ni askari...ohooooo!....
Yaani ni bonge la kisa....'KITANDA HAKIZAI HARAMU...'
Ni mimi: emu-three

No comments :