Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, February 14, 2017

FUPA LILILOMSHINDA FISI-4


Mzee alifika ofisi ya mambo ya usalama, akabisha hodi, na kuingia sehemu ya maelezo akaelezea shida yake kuwa anataka kuonana na mkuu wa mambo ya usalama, akahojiwa ana shida gani, akajieleza, lakini hakusema undani wa kile alichokuwa nacho.

‘Ninaitikia wito wa mkuu, kuwa kila mwenye jambo la kusaidia kwenye hii vita ya kupambana na mdudu mtu na uchawi wa malegeza ajitokeze ...’akasema

‘Una ushahidi gani..?’ akaulizwa

‘Je ina maana tunatakiwa kujielezea kwako maana nijuavyo mimi tumeambiwa tukajieleze moja kwa moja kwa mkuu…’akasema

‘Sawa usijali..ni lazima nikuulize hivyo, kwani kujieleza tu haitoshi, muhimu ni ushahidi..’akaambiwa

‘Usijali….’akasema na yule mdada akaelekea ofisi iliyoandikwa, ‘Mkuu wa mambo ya usalama, na akaingia humo, baadae akatoka.

‘Haya unaona mlango huo hapo mbele, ingia mle , utakutana na mtu ambaye atakuelekeza cha kufanya…’akaambiwa, na  yeye akafanya kama alivyoagizwa, lakini kila hatua alihisi moyo ukimuenda mbio, …wasiwasi na mashaka.

Alipoingia kwenye hiyo ofisi akakutana na mtu mwingine mwanaume kavalia kikazi, akaulizwa maswali machache, ..jina wapi anapotoka, umri….halafu akaonyeshwa sehemu ya kukaa, na kuambiwa asubirie kidogo, na haikupita muda mara akaingia huyo mkuu mwenyewe akiwa kavalia mavazi yake ya kazi,..begani kumechafuka;

‘Samahani ndugu kwa kukuchelewesha kidogo,..najua wewe umekuja kutoa ushirikiano…..na nafahamu kuwa usingelifika hapa kama kweli huna taarifa muhimu sana,..sisi ni watu wenu, tunahitajia msaada wowote kutoka kwenu, …usiwe na shaka kabisa, usalama wako utalindwa…’akaambiwa

‘Ndio mkuu, …mimi siogopi tena kuhusu usalama wangu …mungu mwenyewe anatosha, ninachotaka ni kusema ukweli,…maana mimi kama mzazi ni mmoja wa waathirika wa matatizo haya yanayoikumba nchi yetu,…na kwa vile nimeshaumizwa, ..basi sioni haja ya kunyamaza, kama nikuniua waniue tu….’akasema mzee

‘Usijali kabisa..hakuna mtu wa kukuua…niamini mimi…haya sema unajua nini na kwa ushahidi gani….yule pale kazi yake ni kuandika kila kitu unachoongea, na nia ni kuweka kumbukumbu zetu za siri, ..hazitatoka hapa mpaka tujirizishe…unaelewa eeh?’ Akaulizwa, na kabla hajaanza kuongea mara simu ya mkuu huyo ikapigwa, na mkuu akaiangalia, na kwa haraka akaizima, huku akiwa kakunja uso, kuashiria kukasirika hivi...

‘Mkuu…mimi ni mkulima na mfugaji lakini fani yangu nyingine mimi ni mpiga picha,…..’akaanza kujieliezea kwa kirefu tu, na jinsi gani alivyoweza kukutana na tukio,…

‘Nililiona lile gari mahali aple, nikajua ni vijana wako wapo kazini,..….’akasema

‘Lipoje hilo gari?’ akaulizwa

‘Lile gari la landrover lina michirizi mekundu, unalitumia sana wewe ukitutembelea kijijini…..’akasema

‘Gari langu la kazi, lilifikaje maeneo hayo….Ok, …..ilikuwaje…?’ akaulizwa

‘Ninajua ni vijana wako wanalitumia, nilijua wapo kazini,,….lakini cha ajabu nilichokiona ni hiki hapa…’akasema na kutoa zile picha alizokuwa nazo,…
Mkuu, alishikwa na mshituko, …na macho yake yalishindwa kuficha mshangao,….akasema

‘Shiit…hawa vijana watanitambua, ina maana wanatumia gari la serikali kwa mambo yao binafsi, sasa kuna nini cha ajabu ulikiona, maana kweli hili gari letu, mhh,..hebu ngoja, hebu hiyo picha nyingine,…wanaaah,..yap, huu ni ushahidi safi sana, kumbee, sasa nimewabamba, nilikuwa nahisi jambo kama hili…ngoja, …’ mkuu huyu, akatoka kidogo baadae akarudi…

‘Samahani ndugu yangu, unajua hili tatizo ni kubwa sana,…na imenipa changamoto kuwa niwe makini sana, kuna watu wamenizunguka, na ….wanaweza hata kunichafulia ofisi yangu, sasa ni hivi..huu ni usahidi muhimu sana kwetu,..huwezi kuondoka na hu ushahidi, nilitaka taaribu zote zifuatwe, hawa vijana wakamatwe mara moja, ..’akasema akiwa kama anawaza jambo.

Baadae akachukua mfuko wa nailon, akaandika juu yake,…’Ushahidi…no,….kutoka kwa shahidi….’

‘Tumbukiza humu…..’akasema

‘Mwandishi umeshaandika kila kitu, nipe hiyo nakala aweke sahihi yake,…’akasema akiongea na yule mtu mwingine aliyekuwa akiandika,…

Mzee akaanza kusoma kilichoandikwa mle,..waliandika kila kitu alichoongea kwa usahihi mkubwa, alipojirizisha, akaweka sahihi yake kwenye zile karatasi,.

‘Sasa  kazi iliyobakia ni yetu sisi kulifanyia hili kazi..ninashukuru sana, tukipata watu kama nyie, basi kazi hii itakuwa rahisi sana…’akasema huyo mkuu.

‘Umesema unaishi wapi…’akaulizwa na yeye akajieleza.

‘Sasa usije kuongea lolote kwa mtu yoyote kuwa ulifika hapa..tunahitajia usalama wako,..ili wakati ukifika uwepo…wewe ni mtu muhimu sana kwetu…, nina imani, muheshimiwa akipata hii taarifa utakuwa miungoni mwa watu watakaozawadia donge nono…’akasema mkuu huyu akitabasamu.

‘Hamna shida mkuu..nimetimiza wajibu wangu….’akasema huyo mkuu.

Baadae aliaga na kuondoka kwenye hiyo ofisi, …

***********

Ni siku ya pili kilio kikasikika, ….na mara kukaonekana kundi la watu wakiwa kwenye pori la jirani, kwenye kijiji anachotoka mzee, mpiga picha, …na taarifa zikazagaa…!

‘Mwili wa mpiga picha umepatikana porini , akiwa kajinyonga…..’

Taarifa zikafika kwa mkuu wa mambo ya usalama….

‘Haiwezekani……’ndio kauli yake ya kwanza alipopokea taarifa hiyo!

'Vita imeanza…..hawatashinda...tutaona.....'alisema mkuu huyo.


WAZO LA LEO: Vita ya haki hupiganwa kwa haki,..na watakaoshinda ni wale waliosimamia hiyo haki bila kupindisha, ..watetezi wa haki hawatarudi nyuma, wakijua kuwa wanachokitetea ni cha haki . Kamwe haki haichanganywi na batili….!
Ni mimi: emu-three

3 comments :

Anonymous said...

Hongera xaaaaana

Anonymous said...

Tatizo humaliziii stori zako,....

Anonymous said...

i like your style, just like a movie...