Mzee Masikini akiwa kajichokea, uzee wa kuchoka kuliko umri
wake, ila watu wamezoa kumuita jina hilo mzee tokea ujanani, kwasababu alianza kuota mvi mapema, na watani wake wakaongezea neno `masikini'
`Mzee masikini…’ likalolea, hadi leo anaitwa hivyo!
Mzee Masikini alikuwa kaamuka mapema tu, shambani hakuendeki,...utalima nini,...akwa sasa anaikagua mifigo yake ambayo ilikuwa ikilia, na kilio hicho ni cha njaa….akageukia eneo la shambani, ardhi ilikuwa kame, hakuna hata jani moja
lilobakia, jua linawaka kama moto wa nyikani,…akatikisa kichwa, kuashiria kusikitika,
akaangalia juu kama vile anatoa shitaka lake kwa mola wake.
‘Mwaka huu…’akasema
Alitembea hatua za pole pole, mwili ulikuwa ukimuuma kila
mahali, alihisi kama anaumwa, lakini haumwi, alijua kabiosa haumwi, yeye ni
mpingo, maradhi hayamfuatilii sana, alijua kabisa ni mwili tu unalalamika, mwili
umekosa haki yake, kwa hatua za kujongea,…akasogea hadi kwenye mti , ili
angalau apate kivuli cha mti uliojaliwa kubakiwa na majani machache.
Mzee, alipiga miayo, miayo ya njaa,…akatizama jikoni, mkewe
alikuwa hayupo, alidamkia kwenda kisimani kutafuta maji…maji imekuwa ni shida…akatikisa
kichwa, akawaza afanye nini, akafkiria kuingia jikoni apike chai…lakini sukari
hakuna,..pesa hakuna.
Akaanza kuwaza, …maisha, maisha…hali ngumu,….mpaka lini..ina
maana nitakufa na umasikini wangu…!
Akageuza mawazo yake upande wa pili na kukumbuka lile tangazo
la mpiga mbiu…hakulichukulia maanani sana, kilichomjia akilini zaidi ni hizo
taarifa zilizokuja baadaye kupitia kwa viongozi wa kaya, kuwa wananchi
wanatakiwa kutoa taarifa …na wakitoa taarifa kuna donge nono…
‘Donge nono….’akayatamka hayo maneno kwa nguvu, na kujilamba
mdomoni.
‘Wananchi mnatakiwa kutoa taarifa kama kuna mtu mnayemfahamu,
au kumhisia kuhusika na na hali hii
inayowaumiza vijana wetu na hata kusababisha njaa, hali ngumu, na….kama mtu
anayo taarifa atoe, na atapewa zawadi kubwa kutoka kwa mkuu wa nchi….donge nono’
‘Zawadi gani hiyo, donge nono….ni donge gani hilo..?’
akajiuliza, lakini ajuavyo mkuu wa nchi akisema zawadi , huwa hatanii, inakuwa ni
zawadi kweli, hata hivyo yeye hakuijali sana hiyo zawadi…, alichojali ni hatima
wa vijana wa taifa, kuna vijana wake pia
ambao….wamekuwa ni wahanga wa kuharibiwa viwili wili, hawajiwezi, ..wamelegea
kama mlenda, na mmoja kapotelea ughaibuni, inasadikiwa amenyongwa, kwa vile
alikuwa anafanya biashara ya ‘malegeza..’
‘Malegeza…’ akatamka maneno
hayo akitikisa kichwa.
‘Sasa kwanini nisiwajibike…’akasema kimoyo moyo.
Akawazia maisha yake …na uhatari wa jambo lenyewe..kwani huko
nyuma wengi walipotea hivi hivi tu, kisa wamewataja wanaokisiwa kuwa wanafanya
shughuli hizo,…za uchawi na madawa ya kulegeza viungo, na ……hapo hakumalizia.
‘Na huyu mdudu mtu ni nani….mbona wanatuchanganya hawa watu…mdudu
mtu….anachukua jasho letu, pesa zetu pato letu, anawaharibu vijana wetu mauongo
yao, wanalegea lakini kwa vipi…je hali ngumu, na huu uchawi vinausiano kweli au
ni lengo la kuwachanganya wanachi...’akajiuliza
‘Ni watu hatari…wanakujua hata ukiwafikiria…’alisikia jamaa
yake akisema;
‘Mhh…siogopi kufa tena, kwani nikifa au nikibakia hivi kuna
tofauti gani… hapa kijijini mimi ndiye ninayesifika
kwa kuchapa kazi,..lakini ninapata nini…shambani kukavu, hakuna mazao, mifugo
ndio hii, itakufa hivii hivi…hasara juu y ahasara,..utamuuzia nani…?’akawa anajiuliza
‘Hii kazi nyingine ya kupiga picha haina faida tena, watu
hawana pesa,…’akajisema akiangalia kamera yake aliyoitundika mlangoni,
‘Aaah,..lazima nifanye jambo, lazima….kabla sijaadhirika,…lakini
jambo gani..?’ akajiuliza.
Mara akaona gari la muheshimiwa likipita kwa kasi, na kutimua
vumbi,..lile vumbi lilimfuata hadi alipokuwa amekaa, akaanza kukohoa, akakunja
uso, akiliangalia lile gari likizidi kwenda mbali, akatikisa kichwa;
‘Mkuu….’akasema kwa sauti, na mara akakukumbuka jambo…
***********
‘Mkuu….’akakumbuka
jambo, jambo alilokuwa akiliwazia usiku kucha, akakumbuka lile tukio…
Ilikuwa siku moja
akiwa katika kazi zake za kupiga picha, katika mitaa ya kati, wakati anapita
kutafuta wateja, mara akaliona gari , gari ambalo analifahamu ni la nani, ..akalitizama
kwa macho ya kuwazia, na yeye siku moja awe ndani ya hilo gari.
Aliliangalia lile gari kwa muda, na tamaa ya kulipiga picha
ikamjia, na kabla hajafanya hivyo mara wakateremka vijana wawili kutoka kwenye
lile gari,wakiwa na mkoba mweusi ,…na muda ule likaja gari jingine, la
kifahari..
Gari la tajiri wa jiji, tajiri anayesifika sana…ana miradi
mingi, kawekeza kwenye mashamba, ana
viwanda,…na sasa kaanzisha nyumba zake za ibada, anatoa misaada kwa watu, …kajenga
mashule, aligombea ujimbo, lakini bahati mbaya hakushinda, sijui kwanini watu
hawakumpa kura, nasikia,….hawamuamini..lakini bado anawasaidia watu.
Kwa udadsi wake mpiga picha, akaona apate picha za kuuza kwa
watu wa magazeti, maana tajiri mkuu, haishi kuandikwa magazetini, kwa sifa za
kila namna,..wengine wanasema hata akienda chooni, ataandikwa, ilimradi tu …ni
mtu mashuhuri..
Mpiga picha akaiweka kamera yake vizuri, na kuanza kupiga picha
tukio lile..alipiga tu kwa kujifurahisha..na labda hizo picha anaweza kuziuza,
ndio biashara iliyobakia, akalengesha kamera yake vyema…. Mara akaona kitu cha
ajabu…!
Kumbukumbu zilizidi kumrejea mzee,..kumbukumbu za tukio lile,
akakumbuka alivyoona kwenye runinga wanavyofanya,…mhh….ni vile vile, sasa
kwanini wasingelikutana hotelini au….alijiuliza siku ile na siku ile
hakuichukulia maanani sana, aliona ni mambo ya watu yasiyomfaa…, hakujua ni
nini athari yake, leo hii kaiona…kaiona ndani ya familia yake mwenyewe…inauma, …
‘Ni lazima ndio hizo…, ni lazima ndio wao…mdudu mtu!’akasema
‘Haiwezekani,…’nafsi haikukubaliana na hilo
Haraka haraka akatoka
kwenye ule mti na kuelekea ndani, akaingia chumbani kwake, na kuinama mvunguni
mwa kitanda. Akalivuta begi ambalo huhifadhi kumbukumbu zake muhimu, akaliinua
na kuliweka kitandani,…akaanza kutoa picha mbali mbalimbali..halafu akaziona
zile picha.
‘Huu hapa ni ushahidi kamili…sasa nangoja nini..’akasema akiziangalia
zile picha.
Akumbuka siku alipozisafisha hizo picha, na kurudi nazo
nyumbani aliwahi kumuonyesha mkewe na kumuelekezea kuhusu lile tukio, na mkewe alimuonya, na kumuhimiza azichane
zile picha, …asizipeleke kwa wachapishaji magazeti maana zitamletea matatizo,..lakini
hakuzichana, akazihifadhi tu....ni siku nyingi, lakini
mpaka leo analikumbuka hilo tukio.
‘Donge nono…’akayasema yale maneno, akawaza na kuwazia,
baadaye akasema kwa sauti ndogo…
‘Lakini ni nani ataniami….’akasema akiwa kashika shavu
Mara akachukua kakijitabu kake kadogo ambako anakutumia
kuandika mambo fulani fulani aliyowahi kuyaona, anapenda kuandika, na kama
angelipata mfadhili, angeshakuwa mtunzoi mashuhuru duniani, …lakini vipi…akawa
anapekua kurasa za kile kijitabu, akarudi hadi tarehe ya siku ile, ….aliandika
kila kitu
‘Mhh..huu ni ushahidi, lakini ni nani ataniamini…’akajisemea
tena, akakirudisha kile kijitabu, lakini kabla hajafunga lile begi lake,
akajiwa na wazo,..
‘Kwanini nisijaribu,…nitakosa nini, kwanini….hapana, lazima
nifanye jambo.
Kwa haraka akazichukua zile picha na kile kijitabu, na kuanza
kutoka nje, hakumuaga hata mkewe, moja kwa moja hadi ofisi ya mkuu maalumu wa
usalama….
Mhh…haya tuone ilikuwaje
WAZO LA LEO: Tukiamua
kufanya jambo la haki tuiangalie na haki itendwavyo, na hasa pale tunapojua
kuwa hiyo haki inataka uhakika, wa ushahid…tusijekupania jambo, likaja kuiharibu
haki na ushahidi wake ukapotea bure na mwisho wa siku ikaonekana hiyo haki ni
porojo tu! Na porojo hizo zikageuzwa kuwa silaha ya kuiharibu haki . Japokuwa
haki itaendelea kuwa haki , na ukweli wake hauwezi kufutika daima.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment