Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeMonday, October 3, 2016

Tuwalipe wafanyakazi wetu ujira wao kabla jasho lao halijakauka


‘Chukua chakula na uenda kwenye nyumba ya ibada utamkuta mja wangu anafanya ibada,mja wangu huyo ana njaa, kampe hicho chakula..’ ilikuwa maagizo kwenye ndoto kwa mchamungu mmoja. Mchamungu huyo alikuwa akiota ndoto zake hutokea kuwa ni kweli, na hufanya kwa jinsi alivyoagizwa.

Basi mchamungu huyo alikwenda hadi kwenye hiyo nyumba ya ibada na kweli akamkuta mja wa mungu akifanya ibada, alisubiri pale mpaka yule mtu alipomaliza ibada yake ndio akampa hicho chakula na yule mja wa mungu akashukuru na kumshukuru mola wake, na kuendelea kufanya ibada.

Mchamungu huyu huyu akamuambia yule mja mwema,` ndugu yangu mja mwema.., ukiwa na shida , ukiwa na njaa karibu nyumbani kwangu, upate chakula…’ akamuelekeza hivyo, akizidi kumuelekeza nyumbani kwake ni wapi.

‘Mimi siwezi kuja kwako, kwani wewe sio mtoa riziki, mimi namtegemea, na kumuomba yule aliyekujalia wewe kuipata hiyo riziki na yeye ndiye anajua na kufahamu fungu langu ni lipi…’ mchu mungu huyu akaelewa na kugeuka kuondoka zake, hakuwa na la kusema.

                                    *******
Hawa ni wacha mungu wa kweli, waliojaa imani thabiti…wanafikia kuota ndoto na inakuwa ni kweli, na wanatekeleza hayo maagizo, lakini pia kuna waja wema wa kweli…wanatii na kumnyenyekea mola wao..na kutumiza yale waliyoagizwa na mole wao, wana imani thabiti, wanakuwa na shida, lkn bado hawasumbuki kumuomba mtu au kumtegemea mtu, au kulalamika kwa mtu, wanajua ukweli kuwa riziki yao wataipata tu

Wapo watu sasa hivi wanafikia kuwatukuza matajiri, waajiri..utafikiri hao watu ni miungu wadogo.. hawajui kuwa utajiri huo kwa hao watu umetoka kwa yule yule mola wa wote…

Lakini leo hii ni tarehe tatu ya mwezi..kuna wafanyakazi hawajapata mishara! Hebu jiulizeni, hawa watu watakula wapi, wataishije… Sawa huenda kuna waajiri wengine wamefanya hivyo kwa sababu za msingi, ya kuwa labda hawana pesa, au kuna matatizo ya kibenki, basi wawaambie wafanyakazi wao, na ikiwezekana wasema hivyo mapema iwezekanavyo kwa wafanyakazi wao, ili hao wafanyakazi wajua jinsi ya kujipanga…. lakini wengine wanachelewesha makusudi kwa visingizio mbali mbali, hawajli..  na ni roho mbaya tu, kuwatesa wafanyakazi wao.

Tukumbuke kuwa, kiimani na ucha mungu…waajiri wameamurishwa kuwa wawalipe wafanyakazi wao ujira wao kabla jasho la wafanyakazi hao halijakauka… “Mpeni muajiriwa ujira wake kabla jasho halijakauka”. Kuna hekima ndani yake kwa wenye kuelewa… , hatujui umri wa mwanadamu, je kama ikatokea huyu mfanyakazi  akafariki, na wakati alikuwa na haki ya kula jasho la mshahara wake…wewe umemuhini, kwa kuchelewesha kumlipa stahiki yake…wewe utakuja kusema nini mbele ya mungu au utasema ilipangwa iwe hivyo,…

Lakini pia kuna mipangilio ya mtu, kila mtu ana bajeti yake ya mwezi, wengine wamekopa, wengine wanataka kulipa ada za watoto wao, walishaahidi kwa walimu..wengine wana madeni, wengine wanauguliwa, wanataka kujitibia au kutibia …wewe umezuia na kumfanya huyu mfanyakazi ataabike, au umefanya  mtu huyu asiaminike tena huko alipoahidi…, au akose huduma fulani, utakuja kusema nini mbele ya mungu. Au hatuna imani sahihi ya mwenyezimungu?

Nawaombeni nyie mnaomiliki wafanyakazi kwenye nyanja mbali mbali, tujitahidi kila ikifikia muda wa mtu kulipwa ujira wake tuwalipe watu hao ujira wao,..hilo ni jasho lao,..mshahara wenyewe mnawapunja, na bado mnauchelewesha ujira wao…kihekima tukiwalipa hicho kidogo tulichowapangaia kuwalipa, tunajenga mahusiano mema kati ya mwajiri na muajiriwa…, na pia tunajiongezea Baraka, juhudi za kazi nk…Baraka nyingine hujengwa kwa kutimiza hizo haki za msingi...watu hawalalamiki!

Tumuombe mwenyezi mungu atusaidie tuweze kukumbuka jambo hili la msingi, na tumuombe atusaidie tusiweze kujisahau kwani wakati mwingine kwa madhaifu yetu ya kibinadamu tunafanya hivyo tukitarajia kuzungusha zaidi …


Tunakuomba ewe mola wetu utupe riziki za halali, kutokana na jasho letu,na wala tusighilibike kwa kutafuta riziki zisiso za halali…Yote ni kwa mapenzi yako na wala sio kwa ujanja wetu…Aaamin!

Ni mimi: emu-three

1 comment :

Anonymous said...

MBONA UPO ADIMU