‘Pole sana shemeji,
nafahamu kuwa upo kwenye wakati mgumu sana, nakumbuka sana dada aliniomba
sana,…..’ilikuwa sauti ya kike, na kwangu mimi sikupenda kabisa kusikia sauti
ya kike hapo nyumbani kwangu, nilitamani sauti ya kike iwe ni ya mke wangu.
Najua mke wangu hayupo, ..ndio maana sikutaka sauti..kama hiyo niisikie tena,
inanikumbusha mbali…
‘Lakini ile sauti
ilinifanya nishtuke na kukaa vyema, kwani nilikuwa kama nimepitiwa na usingizi,
na niliyekuwa nikimuota kwa muda huo mfupi, alikuwa ni mke wangu, kanijia na kuanza kuniliwaza, na akawa
ananielekeza jambo…kabla sijaelekezwa ndio nikashutuka, sasa suti iliyokuwa ikitoka kwa mke wangu
kwenye ndoto, ni sawa na huyu mdada .Kiukweli sauti za wawili hawa zinafanana.
‘Mhh…samahani
lakini nilishakuambia uondoke, urudi kwenu, maana sasa hivi sitaki ….sitaki….samahani
unielewe, sio kwamba nakufukuza, lakini una..sauti…oh…’nikasita.
‘Kuondoka
nitaondoka shemeji…., japokuwa itakuwa kinyume na matakwa ya dada, ..dada
aliniambia nikusaidie, …mpaka hatua ya mwisho, sasa nikiondoka sasa hivi
itakwua ni vibaya hujaweza kupona, hujaweza...ndio maana sipendi kuondoka…’akasema
kwa sauti ya upole.
‘Sihitaji msaada
wako, unanielewa, maana badala ya msaada unazidi kuniumiza, unazidi
kunikumbusha, si-si-, wewe ondoka tu, mimi nitakuwa sawa..…’nikasema.
‘Dada aliniambia
…..’akataka kusema jambo na mimi sikutaka kabisa kumuambia, haraka nikasimama
na kuelekea chumbani.
Kule chumbani
nilikaa nikiwaza nifanye nini, kwni docta ameshaniweka mahali pa gumu sana, na
ahadi ni deni… na mara akili ikaniambia kwanini nisichukue hatua tu, kama ni
kufa nitakufa tu…kwnini nisifunge safari tu, niende huko alikonituma docta,
litakalo tokea na liwe…yaani ilikuja hali hiyo na bila kupoteza muda,
nikaingiwa na nguvu za ajabu. Nikatoka nje na kumkuta huyo mdada akijiandaa
kuondoka.
‘Samahani
usiondoke, mimi nina safari, na nyumba haiwezi kubakia peke yake….samahani
lakini, kwa kauli zangu za awali, naomba unielewe tu…,
nimechanganyikiwa…’nikasema.
‘Wala usijali
shemeji…lakini nilishapanga kwenda kusalimia nyumbani unajua ni muda mrefu
sijafika huko.., ila kwa vile una safari ya muhimu naweza kusubiria tu, ukirudi
na mimi nitaondoka…’akasema.
‘Sawa….nitashukuru
kwa hilo…, mimi nitaondoka kesho alifajiri, na sina haja ya
kukuamusha,…’nikasema na kurudi chumbani kwangu. Kiukweli sijui kwanini, kama
huyu binti asingelikuwa mvumilivu angelishaondoka mapema, maana nilimuonyesha
chuki za wazi, …kila alifanyalo kwangu nililiona ni baya, japokuwa alikuwa
akifanya kwa usahihi….alijitolea sana kwa ajili yangu, lakini sijui kwanini….
**********
Ni kwei nilifunga
safari hadi nyumbani kwa wakwe wa docta, nia kukutana na mkewe, mke wa docta!
Na…., nilifika mchana tu… , sikuwapigia simu kuwa ninatarajia kufika huko…,kwahiyo
ilikuwa safari ya kuwashutukizia tu,….Nilipofika hapo nyumbani nilikuta kupo
kimia, nikapiga hodi…
Aliyefungua alikuwa
binti mmoja, nikajitambulisha kwake, na yeye akasema watu wote wapo
hospitalini, baba mwenye nyumba anaumwa sana, ….hata yeye alikuwa akijiandaa
kwenda huko huko..
‘Oh, anaumwa
nini..ok, basi tutaongozana..’nikasema,
Basi nikamsubiria, akijiandaa, baadaye tukaondoka
naye hadi huko hospitalini, na wa kwanza kukutana naye alikuwa mke wa docta, alikuwa
nje akiwa anahangaika na simu yake kama anatafuta namba,…aliponiona kwanza
alishutuka, halafu akaniangalia kwa macho yenye mshangao…., tofauti na
nilivyotegemea cha kwanza tu akasema;
‘Umefuata nini
hapa….?’ Akauliza na kabla sijajibu akauliza swali la pili;
‘Ni nani kakuletea
taarifa kuwa unahitajika hapa…?’ akaniuliza akiwa bado ananiangalia moja kwa
moja usoni. Mwanamke huyu ana ujasiri fulani , anaweza kukuangalia machoni moja
kwa moja bila kupepesa macho!
‘Ninahitajika, na
nani…?’ nikamuuliza na yeye akaniangalia na ilionyesha wazi kuna mshangao fulani usoni mwake, akasema;
‘Sasa umefuata nini
hapa……?’ akaniuliza, sasa akimuangalia yule binti niliyekuja naye, halafu
akagauka kuniangalia mimi;
‘Nina mazungumzo
muhimu sana , mimi na wewe….’nikasema
‘Kuhusu nini….?’
Akasema sasa akionyesha sauti ya kijasiri,nikajua sasa hapo ipo kazi, hekima
inahitajika,….
‘Kiukweli, kuja
kwangu hapa ni sababu ya mume wako…..’nikasema.
‘Anaumwa….?’
Akaniuliza akiniangalia kwa mashaka
‘Ndio,…anaumwa…. na
wewe ndiye dakitari wake…’nikasema, na kumfanya acheke, halafu akasema;
‘Kwanza kabla ya
yote, unatakiwa kuonana na baba yangu, hapa tu tulikuwa tunatafauta namna ya
kukupata kwa simu….mimi nilishafuta simu yako kwenye simu yangu, …hata
baba..sasa ghafla baba anakuhitajia….’akasema
‘Mhh..kwanini,
ananihitajia mimi, anataka kunifanya nini….hapana, mimi nimekuja kwako, sio kwa
baba yako, ..kwani yupoje, anaumwa sana,..au….?’nikawa nauliza maswali mengi
huku nikibabaika.
‘Mimi sijui ,
twende haraka ukaonane naye, ..umefanya vizuri sana kuja…., sijui..ina maana hakuna
mtu aliyekupigia simu kuwa unahitajika..?’ akaniuliza akitangulia kuelekea huko
alipolazwa baba yake..nilisita kumfuata lakini baadae taratibu nikaanza
kumfuata nyuma, kama mbwa anayemuendea chatu!
‘Hakuna mimi
nimekuja na yangu, nimekuja kukufuata wewe….’nikasema na wakati huo tulishafika
chumba alichokuwa kalazwa huyo mzee, tukaingia…nikawa nimesimama pale mlangoni,
naogopa kuingia.
Mle ndani …..
niliwakuta watoto wa huyo mzee, na mkewe wakiwa wamemzunguka huyu mzee,…aliyekuwa
kalala kitandani,…alikuwa kawekewa maji ya dripu,
na alikuwa kama yupo usingizini.
‘Oh, umempata wapi
huyu mtu…?’ ilikuwa sauti ya mke wa huyo mzee, na kabla hajajibiwa yule mzee
akafungua macho, na tukawa tunatizamana, na yule mzee, cha ajbu kabisa akatabasamu
halafu kusema;
‘Nilijua utakuja tu…nimekuota
kuwa unakuja,..oh, kama ninahitajika kuamini nguvu za mungu, basi mimi sasa natakiwa
niwe na imani hiyo…na sijui ..kama nitaendelea kuishi basi mimi nitabadilika
kabisa…nataka uniambie jambo moja…je…. wewe umewezaje kufanikiwa kiasi hicho…?’
akaniuliza na kila mtu akawa kanikodolea macho mimi.
‘Kufanikiwa,..sijakuelewa
mzee… kwani vipi…..?’nikasema na kuuliza
‘Nimeambiwa ili
niweze kufanikiwa, nikuulize wewe…..wewe unajua kila kitu, wewe umeweza, na upo
njiani kufanikiwa,..ila..bado ..una mitihani michache tu, sasa sijui ulifanya
nini, niambie kabla milango ya koho koho.. ….toba, haijafungwa…’akasema huku
akikohoa.
Kwakweli
sikumuelewa, nilikaa kimia kwa muda, lakini sijui kilinijia kitu gani, nikaanza
kumuelezea mzee yale niliyokuwa nikiyafanya, nilimuelezea kwa kifupi tu…, na
yeye alikaa kimia akiniskiliza kwa makini…, hadi nilipomaliza, na
nilipomuangalia machoni, nilishangaa kuona michirizi miwili ya machozi, …..
‘Ndio hivyo
mzee….’nikasema
‘Basi kwanza
naanzia kwako..nisamehe sana..nisamehe sana, ….najua nimekukosea, najua
nimewakosea wengi, nami naanzia kwako, uniambie hapa hapa, kuwa je umeshanisamehe…’akasema
huku akijaribu kujiinua lakini hakuweza.
‘Mzee mbona mimi
ndiye nimekukosea, niliyo-yafanya kwa binti yako, ni makosa makubwa sana,
nilikuwa natafuta njia ya kuja kuonana na wewe, lakini nilikuogopa , nilijua
kuja kwangu kwako,…..ni kujitakia umauti…’nikasema
‘Ooh…sasa ndio hilo
tatizo,na matokea yake ndio haya. ..na najua nipo kwenye mtihani, ila naanza,
..namuomba mungu anisaidie…nitajitahidi kufanya kama ulivyofanya wewe,…binti
yangu yupo wapi…?’ akauliza akigeuza uso huku na huku..alikwua akimtafuta binti
gani sijui!
‘Nipo huku
baba….’ilikuwa sauti ya mke wa docta.
‘Sasa…sasa hivi
ondoka na huyu mtu, mguu kwa mguu hadi kwa mume wako, kampigie magoti, mwambie
namuhitaji hapa haraka, ili tuyamalize haya mambo, nakuhitaji wewe na huyu mtu muende
huko pamoja,..kama kweli unanipenda mimi kama baba yako…utekeleze haya ninayokuambia….haraka
iwezekanavyo…’akasema.
‘Baba…aah, lakini
baba siwezi kuondoka, kwa hali kama hiyo uliyo nayo…’akasema huyo binti kwa
sauti ya unyonge.
‘Ukiendelea kubakia
hapa ndio nitazidi kuwa na hali mbaya, dawa yangu ni hiyo,…ukamuite docta, na
….mke wangu nitakupatia majina ya watu fulani uende ukawaambie waje hapa,
haraka…kama kweli mnataka mimi nipone… nimesema haraka….kabla sijaanza kukoroma
kukata roho ….’akasema huyo mzee.
Na kweli ikawa ndio
nafasi yangu ya kuweza kumpata mke wa docta, ili niongee naye na kumuelezea
dhamira yangu ya safari, na niliona hapo mzee karahisisha kila kitu, kwahiyo
ikabidi tuondoke hapo hospitalini na njiani sikujua niende huko nyumbani kwa
huyu mke wa docta ili apate muda wa kujiandaa, au nitafute hoteli, maana huyo mdada alikuwa kanuna kweli…, hataki
kuongea..
Mara…. mdada
akasema;
‘Huyu baba ana nini…eti
anataka mimi niende kumpigia magoti huyo mshenzi..mimi niende kwa huyo mtu…hata
siku moja..baada ya yote haya yaliyotokea,…kwanini mzee kasahau haraka hivi…mmh…,
sio mimi, …siwezi…’akawa anasema tukiwa njiani..
Mimi nilianza kazi
ya kum-bembeleza, na kujaribu kumueleze kila kitu… mpaka nikaona sasa kalainika, ….na baadaye
akasema;
‘Mimi nitakwenda
huko, kwasababu ya baba tu….. ila siwezi kuongozana na wewe, hapa tu najisikia
vibaya sana kuwa na wewe karibu, nasikia kutapika., ..wewe tangulia huko mjini,
sitaki uendelee kuwa hapa…, mimi ninaweza kuja huko baadaye, kwani bado ninahitajia
muda wa kulitafakari hili…’ akasema.
Na kweli mimi
nikatangulia kuondoka kurudi mjini…, na niliporudi huku mjini sikuonana na
docta moja kwa moja siku hiyo…, kwani yeye alikuwa kazini…na hata ningeonana
naye ningesema nini..nikabakia nyumbani kwangu nikiendelea na toba zangu,…nilishabadilika
kabisa, nilishakuwa mtu wa imani…
Siku ya pili
yake,….. mara nikapokea simu ya huyo docta, kuwa ananihitajia haraka nyumbani
kwake…..
‘Oh docta samahani
sana…., unajua jana nilichoka sana na...na, sikuweza kuja kuonana na wewe kukupa taarifa ya
mke wako, unajua nilimkuta baba yake anaumwa,na..na…’nikasema nikianza kujitetea na yeye akanikatiza na kusema.
‘Wewe njoo haraka nyumbani kwangu …’akasema na kukata simu. Nilijiuliza kuna nini, na ilionekana wazi docta ana jambo, sauti yake iliashiria hivyo...jirani ni muhimu sana , nikakumbuka maelezo ya mwalimu wangu wa imani.
Basi sikuwa na namna, japokuwa nilikuwa bado sijajipanga jinsi gani ya kujitetea kuwa ni kwanini nimeshindwa kuja na mkewe.., Kwa haraka nikatoka nyumbani
kwangu na kuingie kwenye geti la nyumba ya docta.., nilipofika nikagonga mlango, ….
‘Fungua upo
wazi….’sauti ikasema kutoka ndani, nikafungua mlango, ile jicho la kwanza, nilichoona mle ndani,.. nilishikwa na butwa, nikasimama na kuanza kupikicha macho yangu,….sikuamini….
WAZO LA LEO: Ujirani una haki zake, na ukweli ulivyo, ujirani ni muhimu
sana, ndio maana watu wa imani wametukokotezea sana KUUTHAMINI UJIRANI.., kuwatendea majirani zetu ihsani, wema, na kuwa
makini na matendo yetu ili yasiwakwaze majirani zetu.
Wengi wetu hili tunalipuuzia sana, tunatenda
mambo mengi ya kuwauzi majirani zetu, tunapiga miziki kwa sauti kubwa bila
kujali jirani yako anaathirika vipi na starehe zetu,…tunakesha na ngoma,
hatujali kuwa kuna wagonjwa, wasiopenda kelele, wanateseka kwa ajili ya
shughuli zetu, basi tuwaambie kabla ili wajiandae..au, tuwaombe radhi, lakini
ni nani anafanya hivyo jamani hatuna huruma na wagonjwa,…
Haya kwa ujumla ni
madhambi na anayefanya hili, atakuwa na kesi ya kujibu mbele ya mungu. Na tueambiwa
`hana imani na hataingia peponi yule
anayembughudhi jirani yake...mnalijua hili?
Tumuombe mungu
atusamehe kwa makosa haya maana wengi wetu tunafanya haya bila kujua…kuwa ni
makosa makubwa, na tunakuomba mwenyezimungu utuongoze tuishi vyema na majirani
zetu..ili amani na upendo vidumu maishani mwetu. Aaamin
Ni mimi:
emu-three
1 comment :
Duuh, huo sasa ni mtihani,...JIRANI, mm wengi wanafanya hivyo!
Post a Comment