‘Siogopi kuyasimulia maisha ya baba yangu, …maana maisha
yake yamekuwa ni funzo pale kijijini kwetu..alipewa majina mengi, mzee tupa
tupa…mzee wa matumizi, havinipiti…nk…, kila mmoja amekuwa akiyatolea mfano hayo
maisha yake…, hasa pale mzazi anapomuona mtoto wake anapotea, anakuwa mlevi,
Malaya..au ana uchu wa madaraka, au kama hamtunzi mkewe, basi watu hutolea
mfano kwa maisha hayo ya baba..kwahiyo hata nisipoongea mimi leo…,
yameshaongelewa sana…mungu amsamehe tu baba yangu huko alipo…’akasema
Aliposema hivyo huyo binti, niliingia na hamu sana ya kujua
maisha ya baba yake yalikuwaje japokuwa nia yangu ilikuwa ni kujua mambo
yanayomuhusu huyu binti…kwani na muda nao ulikuwa hautoshi..
‘Kwani maisha ya baba yako yalikuwaje,...?’ nikamuuliza
‘Baba…mmh…we acha tu nyie wanaume ….sijui kama nitakuja
kuwasamehe…’akasema
‘Usijali yote maisha…’nikasema
‘Yote maisha …hahaha..haya ya binti yatima yalizidi kiasi….maana
ni kizalia…we acha tu…’akasema
‘Sawa hebu tugusie kidogo kuhusu huyo baba yako,…alikuwa
chama gani vile…hahaha, hayo ya chama yaache, usije kuleta sintofahamu….hebu
tuelezee alivyokuwa, ili tumfahamu, maana yaonekana chuki zako zimeanzia huko…’akasema
jamaa mmoja.
********** tuendelee na kisa chetu*******
Kwanza binti aliinama chini kama anawaza jambo, halafu
akainua kichwa na kuanza kuongea, alikuwa akiongea kwa haraka haraka, kama mtu
aliyekaririshwa hayo maneno, na ilikuwa kama anaivuta hiyo habari kichani
mwake, na kuiona mbele yake…
‘Baba yangu alikuwa
mtu mkubwa sana enzi hizo, nikiwa na maana pale kwetu kijijini… unajua baba
alianzia kuanzia kufanya kazi kwenye wizara..akiwa mkuruguenzi fulani.., akaja
kugombea ubunge, akapata, baadaye akawa mkuu wa mkoa sijui akawa nani tena,
kusoma raha…na ukiwa mjanja kwenye kuongea mdomoni, kushawishi watu baba alikuwa
hajambo….
Lakini pamoja na hayo, watu wengi walimfahamu, kutokana na
tabia yake, ya kujiona, na hata kunata kuwa, ana pesa, na ni kiongozi, amesoma,
mtoaji imla, fanya, ni lazima ufanye, hata kama kuna sababu za msingi za
kutokufanyika….ni kweli alisoma, maana niliwahi kuiona vyeti vyake,….alisomea hiki
akamaliza , akaja kusomea hiki, yaani alikuwa kasomea nyanja tofauto tofauti….kiasi
kwamba ilishindikana awekwe wapi…
Tatizo ni hilo, tamaa, kupenda ukubwa, na kutaka afanye
apendavyo..kwasababu yeye si kasoma bwana, anajua zaidi.., na ikafikia sasa anatumia
mali ya umma kama yake…, unajua tena….lakini
cha zaidi ambacho ilikuwa ni sifa yake, ilikuwa ni hiyo tabia ya kubadili
wanawake kama nguo, madaraka yana mitihani yake…’akasema.
Hakujali kuwa ana mke,..na mama alikuwa mke mremboo tu,
alikuwa na Tabia njema, mtulivu…kila mmoja alimsifia kwa tabia yake hiyo, na
wengi walimsikitikia kwanini aliolewa na baba, wengine wakamzihaki kuwa kakubali
kuolewa kwa ajili ya pesa…ndio hivyo…mama alishinikizwa na wazazi hakupenda,…na
hakuwa na jinsi….’akasema
‘Sasa kwanini mama yako alikubali, au alilazimishwa…?’
akaulizwa
‘Hivi hamkunielewa,…..sirudii tena….’akasema kwa hasira
‘ok….sawa endelea…hakuwa na jinsi, …tunmekuelewa…’nikasema
‘Kwa tabia hiyo ya baba, mama hakutulia, alijaribu kumkanya
baba kila awezavyo, lakini baba hakusikia,..na hata alifikia kumpigwa mama mara
kwa mara, na akaambiwa kama hataki kuishi naye, njia ipo nyeupe aondoke kwao.
Unajua tena maisha ya kijijini, ukishaolewa, umeolewa,…mama
ilibidi avumilie tu, lakini ikafika muda, mama akaamua kuondoka na kuachana na
baba,…sijui kwanini mama hakuweza kusimamia kwenye uamuzi wake huo,…’hapo
akatulia kidogo.
‘Angewezaje, …wazazi wa mama ndio akina mie..hawakuwa na
uwezo ukilinganisha na familia ya akina baba, …baba yake naye ndio hao wazee
wanaopenda kuwafanya watoto wao kama mtaji, kila kitu sawa bwana mkubwa, …na
babu kila akiwa na shida, akitaka pesa za kulewea anamuendea mkwewe, hapo mama
angefanya nini….lakini ikafikia muda mama naye yakamfika shingoni, akachukua
furushi la nguo zake akaondoka.
‘Kwenda wapi…?’ akauliza mtu mmoja
‘Kwenda wapi…tatizo lenu nyie wanaume mkio, mnahisi kuwa mke
hana pa kwenda, ukishamuoa ni mtumwa wako…. mama alikuwa na kwao, sema tu….ndio
mfumo dume…mwanamke anachukuliwa kama hana kwao tena, yeye ni mtumwa kwako si
ndio hivyo....nyie watu nyie…’akasema
‘Ndio maana huolewi, ukiwa na imani hiyo…’akaropoka mtu
mmoja, na mdada akageuka kumuangalia, na mimi nikasema;
‘Wewe endelea usimsikilize huyo…..’ nikasema
‘Nyie acheni tu…..’akatulia kidogo
Kufika nyumbani anakuta ugomvi wa baba na mama…mama analia
kivyake, babu anarudi kila siku mlevi, akirudi ni kipigo kwa bibi….mama
akasimama mlangoni, akijiuliza afanye nini, arudi alipotoka au …..
‘Na wewe umefuata nini…’ilikuwa kauli ya babu akiwa bwiiii…
Mama akajaribu
kujieleza, lakini nani angemsikiliza, hata kama bibi alimuelewa mama…, lakini
ni nani mwenye usemi hapo nyumbani, ni babu, na babu ndio huyo, mtumwa wa baba’ngu,
baba yangu ndiye alikuwa mfadhili wa babu, kwahiyo kila alichosema mama
hakikusikilizwa, mama akaonekana hana maana, akafukuzwa usiku huo huo arudi kwa
mumewe.
‘Mama yako akarudi, mama yake hakumtetea…?’ akaulizwa
‘Bibi…hahaha hivi
nyie mnawafahamu wazee wa zamani …waume kwao ni ….ni kama afande, amri moja,….bibi
alijitahidi lkini wapi,…. mama akabidi arudi kwa mumewe…, ….angefanya nini, na
aliporudi akakuta mlango umefungwa ikabidi alale nje, hadi mume wake aliporudi
na hawara wake,…maana baba alijua mama hayupo, mama siku hiyo alilala chumba
cha wageni, na baba alipogundua mama yupo akajivunga, akamrudisha huyo hawara
wake wakaenda kulala , walipolala…uone ni kwanini nikukuambia nawachukia nyie
watu msione nawaonea….’akatulia.
‘Bibi anasema mama alikuwa kama mtumwa, baba akirudi
amelewa, anatapika ovyo, wakati mwingine anapitiwa na haja..si unajua tena
walevi..basi mama kazi yake kumfulia nguo…yaani bibi akikuhadithia , utatamani
ulie…lakini mama alivumulia, si mume wake bwana, na keshaambiwa na wazazi wake
hakuna kurudi nyumbani ….’akatulia.
‘Sasa ilikuwaje bibi yako huyo, akaja kuishi kwa mama yako….?’
Nikamuuliza
‘Nitakuelezea ni kwanini…..’akasema
‘Basi mama akawa anaishi na baba hivyo hivyo, ikafikia hatua
, baba anawaleta wanawake hadi nyumbani, haogopi tena…mama akaona imezidi akaenda
kushitaki kwa wazazi wa mume…wewewe…ndio alijichongea,..huko ndio kukawa kubaya
zaidi aheri hata kwao…kwanza alianza kuambiwa yeye ni nuksi, yeye ndiye kamuharibu
mume wake, ikafikia hatua kuambiwa yeye ni mchawi…..’akatulia akitikisa kichwa.
‘Bibi yangu alikuja kuishi na wazazi wangu, baada ya babu
yangu kufariki, babu alipofariki, bibi akafukuzwa kwenye makazi ya hiyo
familia,..akawa hana pa kwenda, basi mama akamchukua waishi naye, baba
hakupinga …na huyu bibi ndiye aliyekuja kuwasaidia sana wazazi wangu hasa
kipindi baba anaumwa, yeye na mama wakawa wanahangaika huko na kule, hata
kutafuta riziki…maana ndugu wa mume walipoona baba hana kazi tena, anaumwa,
hawamkujali tena..’akatulia.
Bibi anasema baba enzi zake, alikuwa hawajali ndugu zake,
ndio maana na wao walikuwa kama wametenga kifulani hivi…walisema baba ana majivuno,na
zarau…na hakupenda kuwasaidia ndugu zake, hata hivyo, walimuheshimukipindi
hicho kwasababu ya pesa, na alikuwa
kiongozi, …
‘Bibi anasema baba alianza kuumwa siku alipofukuzwa
kazi….kwani kulipita uchunguzi wa wakaguzi hapo kazini, wakagundua kuwa kuna
ufujaji wa mali na pesa kupotea, na mwisho wa siku wakasema baba ndiye
aliyefanya yote hayo, akasimamishwa kazi.
Siku baba alipopokea
taarifa hiyo, akapoteza fahamu..na tatizo likaanzia hapo, sio kwamba hakuwa
anaumwa kabla, alishaanza kuumwa umwa, magonjwa mengi tu, na alikuja kujijua
tatizo nini…., lakini hakusema kwa mtu, akawa anaendelea na tabia yake ya
kuwaharibu mabinti wa wenzake, lakini mungu hamfichi mnafiki
Siku ikafika,…muda mungu aliouweka wa mwanadamu ni mfupi tu…
alipopokea taarifa hiyo kuwa kasimamishwa alikuwa na kimada…walikuwa kwenye
hoteli,wameshatumia vya kutosha, na hawajalipa….anatarajia akifika kazini
achote, taarifa inakuja, hana kazi, na haruhusiwi kuingia ofisini,..ilikuwa ‘surprise..’
Alidondoka….akapoteza fahamu , na tatizo likazua tatizo
jingine….utajiri, cheo ..majigambo yakaishia hapo, ..
Akiwa nyumbani hana kazi, ..ana madeni kila kona..ikafiki
mahali magari yakapigwa mnada…nyumba, maana alikuwa na zaidi ya nyumba tano
hivi……wakabakiwa na kibanda tu,..kile walichoanzia maisha ya mama, hutaamini
ilifikia muda wakageuka kuwa omba omba….waliishiwa kabisa...ikawa inahitajika
tiba ya baba, hakuna pesa wafanyeje, kazi ikawa kuomba, na kazi hiyo waliifanya
bibi na mama yangu….baadaye siku yake ikafika, akafa akiwa hana thamani….mungu
amsamehe tu..lkn nyie waume mlio hai siwapendi, …
WAZO LA LEO:
Ukiwa na cheo, ukawa na uwezo wako, usijivike kilemba cha majigambo, ukajitanda
nguo ya dharau, ukavaa joho la kiburi...ukumbuke hayo yote ni mapambo ya dunia
tu, yana mwisho wake, wapo walikuwa navyo na sasa hawapo tena duniani,…na wapo
walikuwa navyo, vikageuka kuwa sumu …muhimu, tumshukuru mungu kwa neema hizo
kwa kuwajali wenzetu, tuwasaidie kuwainua, tujenge jina nzuri la wema, maana hata
tukifa bado majina yetu yataendelee kuwa hai kwa matendo hayo mema.
Ni mimi: emu-three
2 comments :
A GUD STORY, LET HAVE A MOVIE ON IT..Unasemaje
oh....inaendelea lini
Post a Comment