Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeThursday, July 14, 2016

HAPPY BIRTHDAY -DIARY YANGU


  

Simini kuwa ni mwaka mwingine unaingia,….namshukuru sana mwenyezimungu, nawashkuru sana marafiki na wadau wenzangu…

Siku nilipoamua kuandika mambo ya diary yangu(shajara yangu) kwenye mtandao ili kila mtu ayasome, nilihofia sana, maana sikuwa na uhakika na mitandao…. Nakumbuka nilivyopenda kuweka kumbukumbu zangu kwenye shajara(diary), kila tukio nalihifadhi katika mtindo wa kisa. Ndoto yangu ilikuwa kutunga vitabu, kuwa mwandishi wa tamithilya, ..oh, sijui lini itatimia.

Kiukweli mpaka sasa kuna mambo mengi mazuri yenye kufundisha kufurahisha lakini bado sijaweza kuyaandika yote...kawaida yangu nataka niandike kitu chenye uhalisia, sio kufikirika tu,..lakini pia kiwe na hekima, ili kizazi chochote kiweze kusoma. Nia yangu ni kuelimisha, kuonya na kusaidiana. Inaniuma sana nikiona, mayatima, wajane, masikini wakinyanyaswa...

Huu ni mwaka mwingine sijakata tamaa, ninachofurahi ni kuwa wapo ambao wanaiona kazi yangu kuwa inasaidia jamii….nawashukuru sana. Ni kazi ngumu kwa vile wakati mwingine unakuwa huna pesa ya kununulia vocha, lkn nimejitahidi kadri ya uwezo wangu, kuwakilisha kile nilichoona kinafaa.

Siku ya leo ninachoweza kuwaambia ni kuwa wale wote ambao hawajafika ndani ya diary yangu, (http://miram3.blogspot.com/) wajitahidi kufika humo kuna visa vingi sana…kuna matukio mengi ambay yanasubiria kuandikwa kama story. Matukio hayo ni ya kweli, ila mimi ninachofanya ni kuyaongezea ladha yawe story, tatizo ndio hilo..gharama na muda…

Ama katika kulifanya hili kuna wengine hawafurahishwi, labda walitaka niandike vile na vile, wasisite kunishauri, maana diary yangu kwa kiasi kikubwa mwandishi na mtunzi ni mimi mwenyewe, sijawashirikisha wtu wengine bado,  ila wapo walionihadithia habari za maisha yao nikajaribu kuyaweka kinamna ya visa..nawashukuru sana, siwezi kuwataja maana hawakutaka wajulikane!

Basi kwa wale ambao hawaja-LIKE diary yangu facebook, nawaombeni mfanye hivyo, kama hujafanya hivyo, itanibidi nianze kuwafuta ili niweze kuwaongeza wengine waliopo tayari kulike. Kulike kunasaidia wewe na mimi tuwe pamoja, uone kila kitu ninachokiandika, pia inanipa moyo na mimi.

Ahsanteni na mungu awazidishie Baraka, wale wote tuliokuwa nao pamoja na wote waliojitokeza kunipa moyo, kukomment, kulike...sina cha kuwalipa ila mola ndiye atawalipa...


Happy birthday diary yangu(http://miram3.blogspot.com/)

Ni mimi: emu-three

No comments :