Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, June 13, 2016

YOTE NI KWA MAPENZI YA MUNGU-12





Mambo yalianza hivyo…

Jamaa akalazwa hospitalini akiwa na homa kali na alikuwa kama kachanganyikiwa,  ikafikia hatua akapoteza fahamu… na watu waliokuwa karibu naye, walisema alipozindukana alikuwa akiongea peke yake kama vile anaongea na  mtu asiyeonekana , lakini alikuwa akitaja maneno kama bro na mara nyingine , anasema ….nimekosa nisamhehe bro..ni kama anatubu hivi, halafu…anaanza kupiga kelele kuwa hataki kufa hataki kufaa…

‘Labda alikuwa akiongea na mzimu wa kaka yake…’nikasema na docta aliyekuwa naye karibu akasema;

‘Kwakweli sijui mambo hayo,…ya mizimu,  zaidi ya hicho nilichokuambia…’akasema docta na mara akaingia mpelelezi kabla sijapata muda wa kumuhoji vyema huyo docta, …na kumbe wakati mpelelezi anaingia alisikia yale tuliyokuwa tukiongea na docta na hakutaka kimpite kitu, kwahiyo moja kwa moja akaanza kwakuuliza;

‘Walikuwa wanaongea nini…?’ akauliza mpelelezi  kwa hamasa, na docta akatikisa kichwa kama kutokutaka kuyaongea hayo mambo, lakini akasema;

‘Kama nilivyomwambia mwenzako, unajua haya mimi kama docta siruhusiwi  kuyaongea, …. sema kwa vile mlivyoniambia jana, nikaona ni muhimu nimsikilizie tu…,  ili muweze kupata hizo taarifa, hebu niwaulize kwanz, je ni kuhusu mgonjwa tu au kuna jambo jingine,  …?’akasema na kuuliza docta.

‘Ni kuhusu mgonjwa….’akasema docta na mimi nikaona hakuna haja ya kumficha huyu docta, nikasema

‘Kiukweli docta,  ni muhimu sana kwetu kujua chochote kama kaongea,…., maana kuna utata mkubwa,  kuna deni….’nikaanza kuongea na mpelelezi akawa kama hataki kuliongelea hilo, lakini mimi nikawa na malengo yangu tofauti, nikaendelea kuongea tu.

‘Ni hivi,…kuna deni limetoka benki, na deni hilo lina ushahidi wote kuwa lilichukuliwa na marehemu,… lakini kuna hali inayotuonyesha kuwa kuna mbinu zimefanyika, huenda hakuchukua marehemu na huenda huyu mgonjwa anaweza kuwa na ufahamu nalo…’nikasema

‘Kwa vipi…?’ akauliza docta.

‘Kwanza ni ndugi yake, na pia, yeye ndiye alikuwa mtu wake wa karibu sana, sasa …kama kweli hakuchukua marehemu , basi tutaweza kuokoa mali ya marehemu ambayo inatakiwa kuchukuliwa, unaona docta…tuiokoe mali ya mjane na watoto wake …’nikasema na docta akainamisha kichwa chini kama anawaza jambo.

‘Je aliongea nini….?’ Akauliza mpelelezi

Docta akatikisa kichwa kwa kusikitika, halafu akasema;

‘Kama ni hivyo …nitawaambia kile nilichoweza kukisikia japokuwa sio sana , maana mtu akizindukana anaweza kuongea maneno hata hayashikiki, au hata huwezi kuyaelewa vyema…., labda uwe unafahamu ni nini anakizungumzia,….sasa kama ni hivyo,…oh, inasikitisha sana kama inaweza kuwa kuna mtu kafanya hivyo ili kuwadhulumu mjane na  watoto, inabidi haki itafutwe hapo…sasa huyu mgonjwa kweli anaweza kusaidia kitu, kwa maneno hayo tu, au …?’akasema docta na kuuliza

‘Ndio….ndio  maana tunajitahidi kuupata huo ukweli kwa njia yoyote ile…huenda huyu mgonjwa anaweza kujua lolote, maana hali imetokea wakati tunamuhoji huyu mgonjwa, kabla hajatuambia mambo yote , huenda anafahamu jambo, …na hasa kwa vile, yeye alikuwa karibu sana na marehemu….je aliongea nini…?’ akauliza mpelelezi

‘Sasa kwanini hamsubirii akili itulie,…nina uhakika atawaambia ukweli, kwa vile ni shemeji yake , na ni kaka wa marehemu au sio,…kwani kakataa kuwaambia ukweli..?’ akauliza docta akionyesha wasiwasi

‘Hapana….ni kutaka tu kujua…kama kuna lolote aliongea, sio kwamba kakataa kusema ukweli, hapana….je kuna lolote aliongea…?’ akauliza mpelelezi

‘Nilijaribu kuwa naye karibu kama mlivyonielekeza, na alipozindukana, mara ya kwanza, na alikuwa bado yupo kwenye marue rue, ya kuchanganyikiwa..homa ilikuwa haishuki, na  baadaye ndio akaanza kuongea , anaongea peke yake, lakini ni kama anaongea na mtu….’akasema docta na sisi tukamsogelea docta tusikie hicho alichokiongea huyo mgonjwa


‘Akiongea na mtu gani…?’ akauliza mpelelezi

‘Alivyotaja, alikuwa anaongea  na mtu aliyekuwa akimtaja kama bro…mara ya kwa mara alikuwa akitumia neno hilo bro, bro..,unasikia bro,…nakuambia bro.. vitu kama hivyo na walichokuwa wakiongea ni -ni ,…vitu kama mashamba ,mara nyumba…mara deni….havieleweki, … halafu baadaye jamaa anakuwa kama anaomba msamaha na mwishowe akawa anapiga ukulele kuwa hataki kufa…..’akasema huyoo docta.

‘Kwa jinsi ulivyosikia alipoongelea hilo deni, aliongea nini zaidi,,  …?’ akaulizwa docta na docta akasema;

‘Ndio aliongea akisema kuna deni, kitu kama hicho,  …unajua, huwezi kuunganisha zaidi ,ila nilisikia kitu kama hicho, akisema kuna deni,…linatakiwa kulipwa,… …na alitaja akisema ni deni lako…ni deni lako bro…, akawa anarudia rudia hayo maneno, deni ni lako bro, deni ni lako bro, ni lazima liwe lako,…kabla hajaanza kusema nisamehe, mimi sitaki kufa…’akasema docta.

‘Hapo haijatusaidia,…Dalali yaani huyo mgonjwa anasisitiza kuwa huyo anayeongea naye ambaye tunahisi ni bro wake,…anasisitiza kuwa deni la huyo bro wake…, kama ni hivyo, basi, hiyo mizimu inashirikiana na huyo aliyetaka kudhulumu,…je huyo anayeongea naye alisema nini..?’ akauliza mpelelezi.

‘Mimi sijui,….maana huwezi kusikia huyo anayeongea naye anaongea nini,unasikia hicho anachokijibu huyu mgonjwa….’akasema docta.

‘Unaona,….mimi  sioni kama hayo maongezi yake yana umuhimu kwetu,…. ‘akasema mpelelezi akionyesha kukata tamaa, halafu akanigeukia na kusema.

‘Eti mtu wa mitandao kuna lolote la kuweza kutusaidia hapo…?.’akasema mpelelezi. na kuniuliza mimi na mimi nikasema;

‘Kama alivyosema docta, huenda mgonjwa aliongea mambo mengi, na mambo hayo yangeliweza kutusaidia lakini alikuwa akiongea bila mpangilia au kwa sauti ya kutoweza kusikiwa vyema…., na kwa vile docta hakuwa na dalili ya nini tunakitafuta,kwahiyo hakuweza kuzingatia …’nikasema.

‘Nikweli….’akasema docta

‘Kwahiyo, mimi sizani kama maelezo yake yatasaidia kitu, mtu wa kuweza kutusaidia ni yeye mwenyewe muhusika…labda tukuulize docta kama kuna jingine zaidi uliweza kulisikia, zaidi ya kutaja deni, mashamba na nyumba, hakuna jingine aliweza kuliongea zaidi ya hayo…?’ nikauliza

‘Ni hivyo hivyo tu ninaweza kusema,,nilisikia akizungumzia  nyumba ipo, nyumba ipo…italipa deni  kitu kama hicho, na nilisikia akisema mashamba tumeuza…kitu kama hicho, na …nahisi ni hivyo tu, mhh, kwani, labda niulize,kwani huyu mgonjwa ana kosa lolote, mnamshuku kwa jambo gani,  kuwa huenda anahusikana na hilo deni mlilosema au kuna jambo jingine zaidi ya hilo…?’ akauliza, na hakuna aliyetaka kumjibu na mimi nikasema;

‘Kwani kuacha kuongelea mashamba, deni na nyumba kuna kitu kingine ulikisikia akikiongelea huyo mgonjwa, ambacho kinaweza kutusaidia kwa namna moja au nyingine, kwa kutaja tu sio kwa kuleta maana, labda alitaja nini , neno gani , au kauli gani…?’ nikamuuliza.

‘Mhh….sikumbuki,…kama kuna jambo aliongelea…mmmh….., hapana siwezi kuunganisha na kuleta maana yoyote, kama ilivyo hiyo ya deni….shamba, nyumba…, ndio hivyo…nimeweza kuunganisha na kuweza kuwaelezea kihivyo…, mengine ..mmmh, hayana maana hayaunganishiki….siwezi kusema kitu…..’akasema, lakini mimi nikahis kuna kitu anaficha, lakini sikuelewa ni kwanini!

‘Je hukuweza kusikia kauli kama ajali, kitu kama hicho….?’ Nikauliza na mpelelezi akaniangalia kama vile hakutaka niliulize hilo swali, na docta akasema;

‘Ajali mhh, ..ajali,ajali…mmmh….mhh, sikumbuki k neno…ooh, ajali, mhhh….. ndio…nimekumbuka,  aliongelea neno kama hilo..hakutamka neno, ajali,…alitamka akisident…. ndio alisema  neno hilo …kitu kama hicho, kweli yawezekana alikuwa na maana hiyo ajali, alitamka neno  ‘accident,…’ .na ndio akaanza kupiga ukelele wa kuwa yeye hataki kufa, asamehewe…..ni hivyo tu ninaweza kusema….’akasema docta

‘Kwahiyo hiyo ya kusema asamehewe, au hataki kufa, inatokana na maneno hayo ya ajali, yaani alipoanza kuongelea maneno ya ajali, au inatokana na hilo deni kwa jinsi ulivyomsikia….?’ Akauliza mpelelezi.

‘Siwezi kujua zaidi hapo…maana niliunganisha hayo maneno kwa kukumbuka na siwezi kukumbuka alitamka wakati gani, nimeweza kuyasema hayo kama  kukumbuka kuwa alitamka hivyo,,…..siwezi kuwasaidia zaidi ya hapo samahani sana…’akasema docta, na kabla hatujamuuliza swali mara akaingia mama mjane kukawa na kusalimiana, tuliona mama mjane akimsalimia huyo docta kama shemeji, ni kama wanafahamiana.
Yule mama mjane ndio akaanza kuelezea kuwa  yeye alipitia kwa mgonjwa kwanza;.
‘Mimi nilipitia moja kwa moja kumuona mgonjwa kwanza…sikujua kuwa nyie mpo huku na wakati nataka kuondoka, nesi akaniambia mpo huku, nikaoa nije niwasalimie, vipi kwani kuna jipya maana mimi nataka kuondoka,…?’akauliza mama mjane huku akionekana ana haraka.

‘Unasema ulipitia moja kwa moja kumuona mgonjwa, je uliweza kuongea naye..japo kuwa kidogo?’ akauliza  mpelelezi

‘Mhh, mwanzoni kwa shida, … ‘akasema na docta akakunja uso kama hakutaka hilo na mpelelezi akauliza

‘Mwanzoni kwa shida, una maana gani…?’ akauliza

‘Ndio….nilipofika alikuwa kama kanitambuaa  akawa anahangaika kuniambia jambo, alikuwa akitetemeka kama mtu mwenye ……kama wale wagonjwa wa madawa ya kulevya wanavyokuwa wakikosa dawa zao na wanahitajia  wazipate, si mnajua wanavyopata shida, basi ndio hivyo,,…..na baadaye akatulia, tukaongea naye kwanza kwa  shida, na jinsi muda ulivyozidi ndio akaanza kuongea vizuri….’akasema mama mjane.

‘Kwahiyo sasa hivi katulia , joto halipo tena, na sisi tunaweza kuongea naye…eti docta?’ akauliza mpelelezi na docta akasema;

‘Hapana , hapana,hamuwezi kuongea naye kwa hivi sasa…,na …hata shemeji hapa kafanya makosa kwenda kumuongelesha ..hakutakiwa kuongea na mtu mpaka mimi nione kweli anastahiki….’akasema docta

‘Waliniambia manesi hivyo,… lakini kilichonifanya niweze kuongea naye, ndio hivyo, alikuwa kama anataka kuniambia jambo,…..’akasema mama mjane.

‘Sawa …imeshafanyika hivyo, hilo ni kosa, sitaki lijirudie tena, nyie hamuwezi kuongea naye mpaka nionane na huyo mgonjwa, nihakikishe kama kweli anaweza kuongea na watu, ….’akasema docta akitaka kuondoka, na mimi nikamgeukia mama mjane na kumuuliza;

‘Dada unasema mgonjwa  kwasasa, …anaongea au sio, sio kama ilivyokuwa awali, kwahiyo kifupi  sasa hivi anaweza kuongea na mtu ukamuelewa anachoongea …?’ nikauliza na docta akasimama kusikiliza , hakuondoka kwanza!

‘Yaani, kaka, ukifika sasa hivi huwezi kuamini kuwa ndio yule alikuwa kama kachanganyikiwa,…..’akasema huyo mama Mjane na wote tukaangaliana kwa mshangao, na kila mmoja alikuwa na hamasa ya kwenda kumuona.

‘Basi naona hali imerejea kama awali…docta tunaweza kwenda pamoja, tukamuone tu, hatutamuuliza maswali, ni kumuona tu….na labda yupo kwenye hali nzuri,  huenda tunaweza kuongea naye kwa leo….’akasema mpelelezi akiwa na hamasa ya kwenda kumuona, na docta akasema

‘Kwakweli kwa leo haiwezekani kuongea naye….huyo ni mgonjwa wetu…, na kama mlivyoona , ndio katokea kwenye hali hiyo ya kuchanganyikiwa…alipoteza fahamu…, anahitajika kufanyiwa uchunguzi kwanza,….naombeni mnielewe…’akasema docta na sisi tukawa hatuna la kufanya, na docta akaendelea kusema

‘Ngojeni kwanza  nikamuangalie mimi  mwenyewe kwanza…’akasema docta na kuondoka kwa haraka, na sisi tukabakiwa pale tukiongea mambo mengine,..baadaye tukaruhusiwa kwenda kumuona..na tulimkuta kakaa kitandani akisoma gazeti, huwezi kuamini  kuwa ni yule mtu aliyekuwa kachanganyikiwa. Na alipotuona tu akaweka gazeti pembeni.

                                                       *********

Mgonjwa alipotuona tu, akaweka gazeti na kutuangalia kwa hamasa, akasema;

‘Karibuni …mimi sijambo, nataka niondoke haraka, kuna mambo yangu yanalala…..si unajua tena mimi ni jembe la familia mbili,…na nyie ndio mnasababisha haya yote, haya isaidieni familia yangu, au ndio mumekuja kunisumbua kwa maswali yenu tena….’akasema na sisi tukaangaliana tukitaka tuanze kumuhoji, lakini docta akatuwahi kwa kusema;

‘Kwahivi sasa siwezi kuwaruhusu kumhoji, ….anahitajia muda kidogo, hajakaa sawa….’akasema docta

‘Basi mimi naondoka nitarudi baadaye kuna watu nimesikia wamekuja huko nyumbani sijui ni akina nani ngoja nikawasikilize …..’akasema mama mjane akionyesha kuwa na wasi wasi

‘Labda ni watu wa kupiga mnada nyumba, waambie ….ninakuja..ni lazima nionane nao kwanza….’akasema Dalali, akiwa kama anataka kujiandaa kuondoka!

‘Sawa… tukikuhitajia tutakuambia, maana hata sisi haina haja ya kuendelea kukaa hapa, kama alivyosema docta,  ila hatuwezi kusubiria zaidi, ni muhimu tukaongea naye haraka iwezekanavyo…’akasema mpelelezi

‘Huyo kwa ujumla  mungemuita yule mtaalamu wake….’akasema mama mjane akimuangalia shemeji yake akiwa anatafuta kitu kwenye kikabati cha hapo hospitali, lakini hakumuuliza anatafuta nini.

‘Mtaalamu wake yupi huyo? ….’akauliza docta

‘Kuna mganga mmoja wa tiba asilia, ndiye wanamuita mtaalamu, …’akasema mpelelezi.

‘Ok…lakini kwa jinsi nilivyomchunguza haina haja ya kuonana na huyo mtu, yupo safi, joto sasa lipo safi, na akili yake imeshaanza kukaa vyema, tunahitajia muda kidogo wa kumchunguza kwanza halafu tutakuambieni kama mnaweza kumuhoji,…’akasema na kutulia kidogo halafu akauliza

‘Na mnasema anahitajia mtalaamu wake..huyo ni docta nani,…ni, mtaalamu wa nini…?’akasema docta akimwangalia mdada, halafu mimi, halafu mpelelezi, na mpelelezi akasema;

‘ Ooh, hawa watu bwana, wanahisi kapatwa na mashetani, na watu wanaoweza kushughulikia hayo mambo wanaitwa wataalamu,  sasa kwa huyo wanayemuita mtaalamu wake, sizani kama anaweza…’akasema mpelelezi akitikisa kichwa kama kukataa jambo

‘Kwanini,….! Maana ndiye alimsaidia  hata mtoto, akizidiwa ndiye aliweza kumtibia…na hayo ya mtoto naona kama yanafanana na …..na tatizo la shemeji…’akasema mama mjane.

‘Ni kutokana na hali aliyo nayo huyo mtaalamu kwasasa…hali yake ni mbaya sana, kalazwa hospitali ya kwetu,  chini ya uangalizi mkali…huyo hawezi kufanya lolote kwa hivi sasa….’akasema mpelelezi

‘Na yeye ana matatizo gani, ni kama haya…?’ akauliza docta, na mpelelezi akasema;

‘Huyo ana matatizo yake mengine,  tuachane naye …..’akasema mpelelezi na mama mjane akauliza;

‘Kwani  yeye litokeaje mpaka akalazwa, unajua mimi sijaelewa bado,mambo yamekuwa mengo kichwani hapa nilipo nipo nipo tu…?’ akauliza mama mjane.

‘Kilichomponza ni huko kutaka kutoroka kwake rumande , na cha ajabu alikuwa bado hajafunguliwa mashitaka yoyote aliitwa tu kwa ajili ya kuisaidia polisi,..mwanzoni alitoa ushirikiano mnzuri tu alipoulizwa maswali,…baadaye akaambiwa hawezi kuondoka, kiusalama,….akatakiwa kuwekwa rumande, ,..hapo  ndipo akawa mkali kweli….’akasema mpelelezi.

‘Jela sio nzuri jamani…hata kama ni hiyo mnayoita rumande,  ina maana kutokana na hilo ndio akazidiwa, ndio akachanganyikiwa na yeye…?’ akauliza mama mjane.

‘Yeye sio tatizo la kuchanganyikiwa,  tatizo, alijeruhiwa na risasi akitaak kutoroka, …na kabla ya hapo alileta fujo kweli…, Ilibidi polisi wafanye kazi ya ziada ya kumgongagonga  kwenye magoti mpaka akalainika…’akasema mpelelezi.

‘Sasa usiku ndio sijui aliwafanyia nini walinzi, kwani  walinzi wote walikutwa wamelala fofo, ile ya kutokujiweza. na ilikuwa ni bahati tu mkuu wa kituoa aliweza kupita hapo kituoni usiku…., na ndio muda huo huyo jamaa alikuwa akitoka mlangoni, akitaka kutoroka,…aliwezaje kufungua mlango, haijulikani, maana mlango ulifunguliwa ….hana ufunguo….sasa wakati anatoka mlangoni akaonekana na mkuu,…akaamrishwa asimame hakukubali akaanza kukimbia ndio, akaipigwa risasi ya mguuni,…’akasema mpelelezi…..

‘Sasa  ilitarajiwa labda kwa kujeruhiwa hivyo atasimama, lakini wapi akawa anakimbia na mguu mmoja, wanasema alikuwa kama anapaa, akitua kwa mguu mmoja akiinuka anaruka hewani na kuwa kama anapaa, na kwa muda mfupi akawa keshatoweka…lakini sasa alipoteza damu nyingi sana,  na sehemu aliyopigwa risasi imeanza kuoza…’akatulia

‘Mbona ni kuwa muda mfupi tu,kwani hakupatiwa matibabu ya haraka…?’ akauliza docta

‘Hata madakitari wa pale wanashangaa, maana haikuwa sehemu ya kuoza,…ndio akahamishiwa hopitali kuu, na huko  ikaonekana wakiacha …italeta matatizo,maana ilishaonyesha dalili za kansa….ikabidi amri itolewe mguu ukatwe..’akasema mpelelezi.

‘Mguu ukatwe…..’ilikuwa sauti ya Dalali..ambaye kwa muda wote huo alikuwa kimia, na alikuwa kama kajiandaa kuondoka, kwa jinai slivyokuwa kakaa pale kitandani.

‘Ndio umekatwa….ungeachwa ingeleta madhara zaidi…..’akasema mpelelezi.

‘Unajua huyo jamaa ni mbishi sana, alipoambiwa hivyo akagoma akasema yeye , hataki, atakwenda kujitibu yeye mwenyewe,  ….ikabidi itumike njia ya kumpoteza fahamu ili mguu ukatwe,….mguu umekatwa, alipozindukana kuona hiyo hali, mguu amekatwa….. ndio hapo na yeye akaanza kuchanganyikiwa, akawa hashikiki, anasema; mumenia,  mumeniua…….mpaka akapigwa masindano ya kumtuliza, na kila akizindukana, ni kelele, mumenia mumeniua… …’akasema mpelelezi.

‘Mungu wangu  kweli wamemuua…kumbe ndio maana, ….alikuja kuniaga,…..oh, masikini mtaalamu, ndio kwaheri hiyo…..sasa ni zamu yangu, hapana, mimi sikubali…’tulisikia sauti kutoka kitandani kwa  Dalali, ilikuwa sauti ya majonzi

Tuliposikia hivyo tukageuka kumuangalia, alikuwa kakaa ile ya kutaka kusimama, alikuwa  akitutizama, kwa macho yakuonyesha ana wasiwasi, na docta akamuuliza;

‘Vipi….wewe tulia ,lala ….’akasema docta

‘Mimi sijambo, ….msiwe na shaka kabisa na mimi ,ila hiyo habari ya mtaalamu ndio imenishtua kidogo, kama wamemkata mguu, wameshamuua, wangelimuachia yeye mwenyewe angejua cha kufanya, wameshamuua mtu wangu…’akasema Dalali, na mimi nikajikuta nikisema;

‘Umeonaeeh Dalali, …unajua ni kwa nini hayo yamemtokea hayo, , ….’nikasema.

‘Si ndio hivyo…kapigwa risasi…na …kiutaaratibu mtu kama yule hatibiwi hospitalini, ikifanyika hivyo, anapatwa na mambo kama hayo….angeachiwa angelijua mwenyewe jinsi ya kujitibu…’akasema

‘Dalali…ujaribu kuelewa, hatutakiwi kukusumbua, lakini hiyo ni kutokana na hiyo mikono iliyoinuliwa juu,….nimeshakuambia, mtu akiinua mikono juu akasema namuachia mungu, ogopa sana…. ogopeni sana duwa ya mwenye kudhulumuiwa, ’ nikasema na Dalali akabakia kimia akiwa kama kazama kwenye mawazo, mpelelezi akamuuliza

‘Dalali vipi unajisikiaje ?’ akaulizwa

‘Mimi sijambo….ile dawa aliyonieletea shemeji imefanya vitu vyake….unajua  niwaambie ukweli mambo mengine sio ya hospitalini, nyie hamjui tu, mnaweza kuua mtu,…’akasema  akijinyosha, na shemeji yake akageuza kichwa kuangalia pembeni , kama kuona aibu, kumbe alimletea dawa huyo jamaa bila ya sisi kufahamu. Na huenda alifanya hivyo, ili madakitari wasijue, sasa Dalali karopoka, hapo ikabidi mjane ajitetee na kusema;

‘Huyu naye bwana…ilikuwa siri sasa sio siri tena….unajua  niliona ni matatizo kama yale ya mtoto, ndio nikaamua kumletea hiyo dawa, na hiyo dawa aliileta yeye mwenyewe kwa ajili ya mtoto, na nilipomletea alipoiona tu….akaitambua, ndio  akafanya kama alivyokuwa akimfanyia mtoto, akapiga chafya na kusema,;

‘Hapa sasa basi nimepona….ahsante shemeji  yangu umeniokoa,sasa mapambano yanaendelea…alisema hivyo…..’akasema shemeji mtu akiigiza sauti ya kidume

‘Mapambano…!?’ akauliza mpelelezi akimuangalia Dalali

‘Ndio mapambano je…’akasema Dalali na kuendelea kusema

‘Ni mapambano ndio ya kuhakikisha kile nilichokianza kinakamilika,….deni lilipwe, siwezi kukubali hii hali iendelee tena, kaka yangu anapata taabu huko alipo, na sisi tutakufa mmoja mmoja, ndio hivyo kaanza mtaalamu, sijui atafuata nani…’akasema Dalali

‘Lakini mtaalamu hajafariki…bado yupo hai na yupo hospitalini anapatiwa matibabu, japokuwa hali yake sio nzuri….’akasema mpelelezi

‘Nyie hamjui tu…huyo ndio kwaheri, na hao waliomkata mguu ndio wamemuua, wangelijua wasingelifanya hivyo….na hata mimi sitakubali,… hapa tu mnanipotezea muda, natakiwa nikawahi kuweka mambo sawa,…hili sasa linahitajia nisafiri, kwa mabingwa, vinginevyo….na kwanini mumenipiga hayo masindano yenu, mumeharibu, hata sijui nitafanya nini….’akasema.

‘Sasa tulia,…kama ulivyosema upo kwenye mapambano , ni muhimu uwe na afya njema…una kazi mbele yako inayokuhitajia uwe na afya, …..’akasema docta.

‘Kazi gani…?’ akauliza Dalali, akimwangalia docta na docta akawa kama anamkwepa kumuangalia usoni, na kusema;

‘Wewe tuliza kichwa chako, huoni hawa jamaa zako wanahitajika kukuhoji, lakini siwezi kuwaruhusu mpaka uwe umatulia, uwe na afya njema…’akasema docta.

‘Hawa hawanitishi, wameshindwa, na watazidi kushindwa….hawana jipya, mimi nilishawaambia waende benki, …lakini bado wananing’ang’ania mimi,haya, …mimi nipo tayari anzeni hayo maswali yenu, maana mnaniuliza utafikiri tupo mahakamani…hahaha, hamniwezi kabisa…’akasema akikaa kitandani , lakini tulishangaa alivyokatisha kicheko na kugeuka kushoto na kulia….anavyofanya unaweza kufikiria anaigiza!

‘Hapana sio leo, hawaruhusiwi kukuuliza hayo maswali yao hii leo…wewe unachotakiwa ni kutuliza kichwa chako, …..cha muhimu kwasasa ni afya yako….’akaambiwa.

 ‘Mimi nia na lengo langu ni kuhakikisha hilo deni limelipwa…hicho ndio cha muhimu…shemeji unasema wale watu wa mnada wamefika, ….au sio?’ Akauliza akimgeukia shemeji yake, na shemeji yake alibakia kimia,halafu akasema

‘Unajua sio kwamba nang’ang’ania  hilo jambo..hapana…sababu kubwa, ni kuwa ,…kiini cha yote haya ni hilo deni, na tusipofanya hima kulilipa hilo deni, mzimu wa kaka utakuwa ukitusumbua kila siku,  na kama umeshaanza kumtafuna  mtaalamu….’hapo akasita na kugeuka huku na kule halafu akasema

‘Mnasema mtaalamu…yupo wapi…huyo ndio basi tena, ….sasa, ndio kazi imeanza,  ukitoka hapo sijui utakuja kwa nani, wasiwasi wangu ni kwa hao watoto, maana ndio damu yake,….sisi sijui kwanini, unatufuata… mimi najua  imenitokea tu kama kunikumbushia, lakini kwa mtaalamu,….hata sijui kwanini…’akawa kama anajiuliza mwenyewe.

‘Labda alishirikiana na hao wanaotaka kumdhulumu marehemue…’nikasema na jamaa akaniangalia na kusema;

‘Sio hivyo, …mara nyingi vitu kama hivyo vinafuata damu yake,…ndio maana uliona mtoto alianza kuumwa, ….wengine kama mke, kaka, ni kama kukumbushiwa tu…mnielewe lakini,….mimi niliambiwa haya yote na mtaalamu sio mimi, …oh,  na yeye ndiye angeliweza kunisaidia katika mambo haya, siyataki lakini utafanya nini, sasa eeeh, ndugu zanguni … itakuwaje, …’akasema akituangalia;

‘Lakini  Dalali, hebu tuambie ukweli, kuna nini…unajua sisi lengo letu ni hilo, tulimalize hilo tatizo, na ili tulimalize hilo tunahitajia ushirikiano wako,ili kulitambua hilo deni vyema, hatuwezi kukubali kuwa ni deni la kaka yako, kwasababu mpaka sasa kuna kila dalili kuwa hilo deni sio lake,  sasa kama sio deni la kaka yako, ni nani yupo nyuma ya hilo, lilikuwa ni deni la nani….’tukasema kama kumuuliza.

‘Nyie ndio mniambie hilo deni ni la nani…kama sio la kaka,…na swali kama hilo kweli ni la kuniuliza mimi, …hebu tumieni akili, mlitakiwa kwenda kuwauliza benki,..au sio…kwa vile huko kuna ushahidi mnashindwa kuwaingia mnataka kunisumbua mimi,…hilo deni ni la kaka…ni lake…’ akasema akisimama lakini alionyesha kuwa ana wasi wasi kwani alivyotamka hivyo akawa anageuka huku na kule kwa mashaka.

‘Sasa unataka kwenda wapi…?’ akaulizwa na docta,  Doacta akatuashiria kuwa jamaa bado hajatulia.

‘Mimi nataka kuondoka, siwezi kulala hapa….siwezi kabisa kukaa hapa hospitalini, kunanukia kifo,….mimi naondoka kabla huyu jamaa hajafika tena …’akasema

‘Jamaa gani …’tukamuuliza na akawa anageuka huku na kule kama ana wasiwasi fulani…

NB Sehemu hii iliishia hapo kwani tuliondoka, tukamuacha na dakitari wake, na tuliporudi mambo yalikuwa mengine huwezi amini…


WAZO LA LEO: Mwenyezimungu ana namna nyingi za kutukumbusha madhambi yetu ili tutubu, lakini wengi wakikutwa na mambo hayo, wanajifanya kama sio yenyewe, ...zaidi ni kujipa matumaini kuwa bado maisha yapo, ...ndugu yangu kumbuka haya maisha anayejua lini kesho ni muumba mwenyewe!

Ni mimi: emu-three

No comments :