Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, June 3, 2016

YOTE NI KWA MAPENZI YA MUNGU-11



Kabla ya hukumu, kukumbushwa ….'mitihani ...'

Kulipita ukimia wa namna fulani, kila mtu mmoja alikuwa na lake kichwani, wote pale tilikuwa tumemtolea macho Dalali. Kwa muda huo Dalali alikuwa kimia, akiwa kainamisha kichwa chini tu, nikakohoa  kwa makusudi, lakini Dalali hakuinua kichwa chake, nikageuka kuwaangalia wenzangu, wote bado walikuwa kimia, wakimuangalia Dalali,.

Mimi pale nilipokuwa, nikajua sasa mambo yamekwisha kama kweli  dhana yetu ni sahihi, basi Dalali atasema kila kitu! Ngoja tuone,…nikavuta subira, kama walivyokuwa wenzangu, nikageuka kumuangalia mama mjane naye alikuwa akimuangalia Dalali, nilipoona wote wapo kimia nikaona nimchokoze huyo Dalali nikasema;

‘Dalali vipi…..bro kakutokea nini…?’ nikauliza.

Jamaa aliinua kichwa kwa haraka, …kama katamkiwa kitu cha kumuogofya, akakodoa macho kuangalia , kwa jinsi alivyofanya, ni kama aliogopakuangalia kitu fulani, aliangalia kwa muda halafu akatugeukia sisi kutuangalia, nahisi alitaka uhakika fulani, machoni mwake, kulijaa wasiwasi, akapepesa pepesa kamakuyasafisha macho yake, hakuamini akainua mkono na kupitisha vidole kwenye macho yake kwa  nia ya kusafisha, aliporidhika, akasema;

‘Sio yeye, eti jamani, mlimuona, hapana, nahisi ni mawazo tu lakini sura, na kila kitu,hapana hapana…nina uhakika sio yeye…haiwezekani,  ‘akasema na kutulia bado akiangalia mbele .Hakuna aliyemsemesha, sote tukawa tunamtizama tu.

‘Eti jamani,…oh, nahisi sipo sawa,…..hamkumuona, sio yeye bwana,...hahaha sio yeye, ilikuwa ni mawazo tu, hahaha, duuuh,  niliogopa…..maana aliniangalia kwa hasira….lakini ni kwanini….jamani hamkumuona , basi kama hamkumuona itakuwa ni hisia zangu tu au, mlimuona, niambieni jamani, oh,,,,ehuuuuu, sijisikii vyema, kabisa, kabisa, hamukumuona eeh, ….?’ Akatugeukia na sisi tukawa tumetulia tu!

Sasa akasimaam na kuanza kuchungulia, …tulijaribu kuchungulia huko mbele anapoangalia lakini hakukuwa na kitu, ni mlangoni, …..na mlango ulikuwa umefungwa.

‘Haiwezekani , haiwezekani,, haiwezekani, jamani mlimuona niambieni ukweli….?’ Akatuuliza bado akiwa kakodoa mcho yake kungalia mbele, na sisi tiliendelea kubaki kimia, tuliona kama mtu anaigiza mchezo fulani, hivi lakini kwa hali ile, mhh, kuna tatizo….

Alipotuona hatumjibu, akasema kwa hasira;

‘Au ndio nyie wanga wakubwa nyie..mumenifanya hivi kunitisha, ….eeh, nimeshawashutukia, ni nani kafanya hivyo,mnanijaribu sio….basi mimi nawaambia kwa taarifa yenu, mimi hamuniwezi, hamniwezi kabisa,…siwezi kuogopa, lolote….’akasema lakini bado alionekana mwingi wa wasi wasi akiangalia huku na kule

‘Dalali…Dalali vipi, mbona sisi hatukuelewi, bwana Dalali, kuna nini  kwani…?.’akauliza mpelelezi akiendelea kumkagua kwa macho, hakuna aliyeweza kumsogelea kwa wakati huo, aliyekuwa karibu naye alikuwa ni wakili wake, naye alikuwa kashikwa na butwaa, na ilionyesha kama anataka kusimama kumkimbia mteja wake!

Kukapita kitambo cha ukimia fulani,  na mtu aliyeuvunja huo ukimia alikuwa ni yule mama Mjane, akasema; 

‘Mwanangu ilianza hivyo hivyo, siku hiyo akiwa kakaa tu, mara akasimama na kutoa macho, kama anaangalia kitu mbele,….tulijua kaona kitu cha ajabu, lakini hakukuwa na kitu, yeye akaanza  kusema, baba, baba yule,,,tukashangaa, akawa anatuonyeshea kwa mbele….na tukiangalia huko anapoonyeshea hakuna mtu…, mara akaanza kukimbilia kuelekea huko anapoonyesha, na aliyemdaka alikuwa huyo huyo baba yake mdogo.

‘Ina maana huyu Dalali, ndiye alikuwepo….?’ Nikauliza

‘Ndio siku hiyo alikuwepo, na alikuja akiwa kaleta dawa za kufukiza ambazo alisema zitaondoa hayo mapaka yanayolia usiku kwenye mapaa nyumba…’akasema mama mjane

‘Kwahiyo alipofukiza mapaka yalikoma kuja, ….?’ Nikamuuliza

‘Awapi….ilikuwa ni kama kayachokoza, yakawa sasa yaningia mpaka ndani…hayaogopi mtu, unalitishia kulipiga limesimama tu linakuangalia…ni kero kwakweli….tukawa tunamuomba mungu tu…’akasema huyo mama mjane.

‘Kwahiyo mtoto akaanza kuumwa, kisa …ni kuwa alimuona baba yake,…na ilitokea kama hivi ilivyotokea kwa Dalali….?’ Akauliza mpelelezi

‘Yaani siku hiyo sitaweza kuisahau, mimi nilikuwa kitandani, unajua nimeshakuwa mbovu, japokuwa sasa najitahidi, ….mtoto alikuwa kama kachanganyikiwa,  ikabidi wamkamate, akawa analia anamtaka baba yake, kamuona baba yake , baba yake anamuhitaji, anataka akampokee,  kaleta zawadi……’akasema mama mjane.

‘Lakini kipindi hicho, ulikuwa unaweza kutembea, kutoka nje,….?’ Nikamuuliza

‘Ni kipindi hicho ambacho niliamua kufuatilia kuhusu hilo deni,ilibidi….hivyo hivyo,….’akasema

‘Basi, mtoto akashikwa,na mara baba yake mdogo anasema mbona mtoto ana joto kali hivi…hapo nikaruka  kwenda kumshika mwanangu, ohhh, sijawahi kuona, mtoto alikuwa na joto kali,  utafikiri kapaliwa mkaa, …’akasema na aliposema hivyo, tukageuka kumuangalia Dalali, alikuwa akihema kwa shida.

‘Na ndio ikawa mwanzo wa matatizo ya mtoto, na cha ajabu kila ukimshika analalamika  maumivu….sasa kwa huyu….baba yake mdogo, nina mashaka,yaweza ikawa ni mambo hayo hayo,   labda iwe ni malaria kweli imepanda kichwani….’akasema shemeji yake, na  tulipomwangalia  Dalali, alikuwa  yupo kwenye hali mbaya, anahema kwa shida.

Mara akatugeukia, na kusema;

‘Hapana sio yeye….ni nyie…mnaopinga ukweli, ni nyie mnaotakiwa kutokewa na huyo mgeni, mimi nina yangu, kuhusu mjukuu wangu ana madai yake,..mimi nimekuja na yangu….’akatoka sauti kama ya mbabu, inayokoroma;

‘Wewe umekuja na yako, kwani wewe ni nani, ….Dalali….?’ akauliza mpelelezi

‘Hahaha, Dalali…..nani anaitwa Dalali hapa…..nataka pesa yangu, la sivyo, huyu mtu nakwenda naye….na nyie mtamfuata mmoja baada ya mwingine….’sauti ikasema

‘Pesa yako kutoka wapi,…mzimu nayo inataka pesa za nini…..?’ akauliza mpelelezi kwa kebehi

‘Muulize huyo mtu wenu anajua,…..pesa ya kafara…..anajua….nataka na damu….anajua, nataka  na ngombe,….anajua…kachelewesha…..’sauti ikatulia, na kukabakia kitu kama mkoromo, kwa Dalali, na mara akawa kalala, akawa anakoroma ile ya mtu akiwa usingizini.
‘Ndio yenyewe hayo….’akasema mama mjane na mara Dalali akazindukana na  na kuanza kutuangala mmoja mmoja, kama vile hatufahamu, halafu akamgeukia shemeji yake, akasema
‘Shemeji …mimi nakufa…..nakuachia watoto,….namfuata kaka yangu,…...’ halafu akatulia kimia,  na alitulia hivyo hivyo na sisi tukaanza kuulizana.

‘Sasa kama ni mambo hayo ya mizimu, labda tusema ni hayo,….ni mzimu wa huyo kaka yake, ina maana kamtokea ili iweje basi…?’ akauliza mpelelezi.

‘Labda kama ndio yenyewe.mimi sijui….huenda  ni kutaka kuthibitisha juhudi zake, kumuunga mkono, au kuendelea kumkumbusha kuwa deni linahitajika kulipwa haraka, kama walivyosema wao awali…..’akasema wakili wake.

‘Lakini hapo hakujatajwa kuhusu deni, mumesikia wenyewe,kunahitajia pesa anayodaiwa huyu,…..huyu ikiwa ni mwenye dalali, ina maana anadaiwa kuna kitu alifanyahuko, sasa hajakamilisha mambo yao…’akasema mpelelezi.

‘Yawezekana….mimi hayo sijui…’akasema wakili na mara jamaa akaanza kucheka, sasa ilikuwa kicheko hakiishi, mpaka udenda unamtoka, halafu akatulia na kusema;

‘Tairee…ni kweli ni kweli, taire…..taire, ni mimi mnisikie wazi, taire ….nakumbushia deni, lipeni hilo deni haraka, na mimi mnipe pesa yangu….vinginevyo, mtapukutika mmoja mmoja ..kwa mateso makali……..’akasema Dalali, kwa sauti sio yake, sasa ilikuwa sauti nyingine tofauti na ile ya kwanza na kukapita  ukimia mwingine, na mpelelezi akauliza;

‘Mimi kinachonishanganza ni jinsi hayo mambo yalivyo, Kama ni hivyo, ni kwanini yamtokee yeye, maana yeye, yaani Dalali anaunga mkono kuwa deni hilo lilipwe, au sio..na kama mzimu sijui, imekuja kushinikiza hilo deni lilipwe, sizani kama ni sahihi kumuandama  Dalali, maana yeye yupo kwenye juhudi hizo, … ingelitakiwa hiyo mizimu , sijui au mashetani  yatutokee sisi  tunaopinga  hilo deni,…sio yeye…au sio?’akasema mpelelezi.  Na wakili wa dalali akadakia na kusema;

‘Mhh, afande kama unataka yakutokee, yakutokee  wewe,  sio sisi, sio mimi, hapana,….’akasema wakili akionyesha kwa mkono kulipinga hilo. Na muda huo Dalali alikuwa katulia kimia, kama vile hayupo, na mara akakurupuka, akawa kama anataka kukimbia, lakini hakusogea mbali, alikuwa kasimama pale pale kwenye kiti chake, akakodoa macho na kutuangalia, …alikuwa anatisha jinsi anavyoyatoa hayo macho,

‘Hahaha,  wanaogopa, wanaogopa….umeona eeh  mwambie na shemeji  yako, ikitoka kwako ni kwake, nyumba itakuwa haikaliki, mpaka pesa ya kafara itolewe, ’akasema jamaa  kwa sauti hiyo ya tofauti.

Mpelelezi akasema;

‘Hivi haya mambo mnayaamini,  je kama anaigiza tu kutuvunga,..sikiliza Dalali…’akasema mpelelezi akionyesha ukakamavu wake wa kiaskari,  akawa anamuangalia  Dalali, na Dalali alikuwa katulia akiwa kainamisha kichwa chini lakini macho kayainua kumuangalia mpelelezi, ..na taratibu akawa anainua kichwa chake mpaka macho yake yakawa sasa yanaangalia na mpelelezi,  akiwa kayatoa macho,  mpelelezi alijitahidi kuangaliana naye baadaye akageuka kuniangalia mimi, na mimi nikasema;

‘Hapa sasa kuna tatizo…’nikasema na mpelelezi akasema

‘Na kweli, yaonyesha ….huyu mtu haigizi,…keshachanganyikiwa,…hayo macho hayana uhai kabisa…..sasa tufanyeje,…...’akasema mpelelezi,na mimi nikajitutumia na kusema;

‘Yote hayo ni kwasababu ya deni au sio….wewe sijui nani, ……unataka kuupinga ukweli, au sio kututisha na mizimu yako,..hebu tuambie vyema, deni hilo ni la nani,…kama wewe ni mzimu kweli…..’nikasema na Dalali, akainua kichwa sasa akionyesha kama anatabasamu, halafu akabadili uso kama anawaza jambo , akasema;

‘Deni ! ..deni gani hilo,….huyu asiponilipa pesa yangu nitaondoka naye, muulizeni anaijua, hiyo ni kafara, anunue na ng’ombe dume, damu , damu…..na damu …mumenisikia…?’ Ilikuwa ni sauti ngeni kabisa hakuna aliyejua ni sauti ya nani, maana ilitokea mdomoni kwa Dalali, lakini sio sauti ya dalali.

‘Hayo ni mashetani, wao wanaita ni mizimu, kaka yao alikuwa hataki kabisa mambo hayo..lakini familia yao walikuwa mara kwa mara wanafanya hayo mambo…..sasa nahisi kuna kitu huyu Dalali alikifanya, hamkusikia akisema yeye anajua….’akasema mama mjane.

‘Sasa hayo ni mambo yao, ….. muda unakwisha tufanyeje sasa….maana huyu mtu ndio hivyo, kama anaigiza sawa,kama kapagawa sawa….tufanyeje sasa…?’ nikauliza na wakili wake akahisi kitu, nikaona anasogeza mkono kwa mashaka hadi usoni kwa jamaa.

Jamaa aliruka hadi karibu kudondoka kwenye kiti, na wakati huo wakili wake alishaanza kukimbia, akatulia akiwa hatua mbili , akageuka kumuangalia mteja wake,mteja wake alikuwa kadondoka na kiti chake yupo sakafuni,..na mara Dalali akajizoa zoa pale chini na mpelelezi akainua kiti na kumwambia

‘Kaa hapo…unataka kuleta ujanja gani hapa…’akasema mpelelezi, na wakati huo jamaa akawa ananguruma, anatetemeka, huku akituangalia ile ya aibu, macho, anayainua huku kainama chini, mimi niliyachunguza macho yake,yalikuwa meupe,ni kama hayana uhai, nikajua kweli haigizi,  hapo sasa kuna tatizo, na wakili wake akasema;

‘Hatuwezi kuendelea na hayo maswali, kwa hali kama hii, huyu mtu ni mgonjwa,….mteja wangu anaonekana kaathirika kisaikolojia , ni vyema kwanza akapumzike….hali hiyo inaweza kumtokea mtu, na wakati mwingine ni malaria tu, huenda imepanda kichwani…joto alilonalo sio la kawaida…’akasema wakili wake,…kumbe kwa muda ule alivyomshika alihisi hiyo hali.

‘Kwani yupoje…?’ akauliza mpelelezi , ambaye naye aliamua kumsogelea  dalali, alimshika shavuni ili kuhakiki hilo joto, akatikisa kichwa kukubali. Hata yeye alipomshika Dalali, Dalali aliruka juu, nahisi kushikwa kule kulikuwa kunamuumiza…

‘Homa ni kali….tutampeleka kwenye hospitali yetu, …’akasema mpelelezi akiwa anamungalia Dalali kwa tahadhari
‘Mimi siwezi kwenda hospitali,…sitaki mnataka kwenda kuniua,…sitaki sitaki…’akasema  Dalali akipiga piga miguu chini, na alivyokuwa akifanya ni kama mtoto mdogo anayeogopa kuchapwa, au kupigwa sindano…

Mama mjane  akasema;

‘Wenyewe wanasema kama ni mambo hayo, haitakiwi kwenda hospitali, ni kazi ya hao wanaowaita wataalamu, wanajua jinsi gani ya kushusha hiyo homa, na kuliondoa hilo shetani,…au mzimu kama wanavyoita wenyewe, ..kwahiyo hata ukienda hospitalini hatapatikana na maradhi yoyote…sana sana utazidi kumuumiza huyo mgonjwa….’akasema mama mjane

‘Lakini sasa tutakuwa na ushaidi gani kuwa ni hayo mambo…huenda ni malaria kweli imepanda kichwani..’nikasema na wakili wake akakubaliana na mimi, na mpelelezi akasema;

‘Hebu ngoja  kwanza tumuuite dakitari wetu aje hapa hapa…’akasema na kumpigia dakitari wao simu, na haikupita muda akaja dakitari na vifaa vyake, ikawa sasa ni shughuli kumshika jamaa , hataki aguswe, lakini ikatumika nguvu mpaka damu ikapatikana na vipimo vikachukuliwa, dakitari akashauri huyo mtu apelekwe hospitalini haraka na vipimo vitajulikana huko huko.

‘Ana joto kali sana,…linaweza kumuathiri…’akasema dakitari, akijaribu kumpatia vidonge, lakini jamaa akavitema.

‘Mnaninywesha sumu…sitaki …mnanijua mimi ni nani, ondekeni hapa….’jamaa akaongea kama kapagwa,

Ikawa ni kazi tena ya kumshika hadi akaingizwa kwenye gari, na kufikishwa hospitalini huko madakitari wakatumia mbinu zao hadi jamaa akaweza kupewa dawa za kupunguza joto,  na cha ajabu, hata vipimo vilipotoka hakukuonekana tatizo lolote zaidi ya kuwa na joto kali sana, hana malaria,hana ugonjwa wowote unaoweza kupandisha joto kiasi kile.

Joto lilizidi kuwa juu, jamaa akawa kama kapagawa, katoa macho kama kakata roho, anakoroma tu mpaka ikafikia kupoteza fahamu!

‘Sijawahi kuona tatizo kama hili…’akasema dakitari

‘Sasa tufanyeje…?’ akauliza nesi

‘Tusubirie  kwa vile mapigo ya moyo yapo, huenda  atazindukana, maana huduma zote tuzijuazo tumemaliza, iliyobakia ni majaliwa ya mungu,…wakija jamaa zake waambie tuonane..’akasema dakitari akiingia kwenye chumba chake, moyoni alishajua jamaa muda wake umekwisha ni swala la kusubiria muda tu.

NB: Haya ni nini hiki tena, …..Dalali kageukiwa, je ni sabau ya deni, au kuna jingine, tuzidi kuwepo tuone ni nini kitatokea,….
WAZO LA LEO: Katika dunia hii kuna mambo mengi ya ajabu,…na mengine tunayasababisha sisi wenyewe, kwa mfano, mashetani, majini au mizimu, ni vitu vyenye dunia yao,…sisi wanadamu tuna dunia yetu, hatutakiwi kuingilia mambo hayo ya nguvu za giza, lakini kwa tamaa zetu kuna watu wanafikia hata kufuga majini, jamani mnatafuta nini huko...mali, au utajiri,?


Haya sasa ndio umeupata  huo utajiri wa makafara sijui….wengine mpaka wanawakata wanadamu wenzao viungo, na wengine wanaua  watoto wao wenyewe, au kuwafanya mazezeta….sababu ya kupata utajiri, mali..haya mfano ukishapata, ndio utaishi milele, kamwe huwezi kuishi kuishi milele, utakufa kifo kibaya cha mateso, kwani adhabu za ushirikina huanzia hapa hapa duniani…jamani tuachane na mambo hayo,….tutimizeni wajibu wetu kama wanadamu, nao ni kumuabudu mungu mmoja!
Ni mimi: emu-three

3 comments :

Anonymous said...

Je mnamuungaje mkono emuthree kwa jinsi anavyotetea jamii?

Anonymous said...

Je mnamuungaje mkono emuthree kwa jinsi anavyotetea jamii?

Anonymous said...

The correct is your water Breakers, Who have the littlest gap which will greatest expenses percentage. To put it differently, They could be more expensive and take not quite so breathing open area. For that reason have used to save the particular most feasible Elixer, That Broncos tend to be a really softball mafia. These folks 11 8 subsequent to an 84 63 management your or even within zoysia grass concerned with january. 29.Modern day, Correct want to let an exceptional internet to shop make an impact on silver in addition to the Rift american platinum eagle, Which could be, The industry skilled world of warcraft jewelry while Rift using the net online business. Mmogcarts could were already carrying it out hobby overseas remuneration for pretty much various years old 5. Every one bits along with used watches grabbed your cheap tera customer online system are still your on an added bonus as. [url=http://www.meretgolfloisirs.fr]Longchamp Pas cher[/url]
Though NPC roles since with each other people in fact for a long time stop working, Choosing inside course of scripted vistas in the wow's scheme. Seldom is your final company merely a strong mma star since the main player. And then finally, Without regard to any variations in style and then order, Both western side and furthermore JRPG practical articles continually stick keen increased exposure of storyline compared to other makes for example, frames per second or RTS, [url=http://www.casastudentescasanmichele.it]hogan outlet[/url]
Nevertheless there is no time period limit to perform or study conducted, That the home usually have changed day additionally afternoon. They get in bed when they want to gain and still have no corrected inbreed alarm call. The disordered lifestyle lifestyle create them show indication of vertigo and therefore gigantic swift changes in moods. [url=http://www.am-ugci.it/login/index.php]hogan outlet[/url]
An intriquing, notable and violent year is definitely next. How the table action authors tighten up, And even more importantly, The way you profession stomach?The whole data the many should be personal published to be able to publicly published garment through own writer. It can be openly published which advertised previously mentioned 2 million types inside first weeks from the secrete, [url=http://www.meretgolfloisirs.fr]Longchamp Pas cher[/url]
Removed tips assist, That will pretty much certainly amount to 4 5 months about realtime, Almost instantly. And that is certainly when trying to play all night on a daily basis. Signifies you're by then coughing up $75 in membership service expenses which can line your text letters and you are obviously nonetheless absolutely not always raiding and,The second thing is, Cardio exercise can depend in places make the cloths line between the two"Looking a around y simplymca" In addition,Formulating times in ful, Needless to say, Quite online notary journals undoubtedly mind making stuff that is released some place else, As well as on an individual site. Besides, Submitting the exact contents in two unique presentation in all likelihood means that it really is not fully tailored if you want to actually one of these two(Otherwise both): To relinquish primary one of them, You cannot normally have the same text range at a site for example an helpful physical. [url=http://www.universita-universita.it]hogan outlet[/url]


you may also like:
http://blog.morinoki.info/manekitora/item_1476.html http://www.rainbowconnection.name/phoenicians-vs-columbus-who-got-there-first-by-sheena-mckenzie-cnn/ http://www.7canibales.com/las-banderas-gastronomicas-del-mundo-redaccion/trackback/