Mimi
nilikuwa nimeshaamua kumuelezea huyo mzee ukweli wote ninaoufahamu mimi, ukweli
ambao ilikuwa siri iliyofungamana na kiapo, Na sikupenda hata mimi kuuelezea mambo hayo maana yalikuwa yakinizalilisha mimi, na kuniweka uchi, ...kinyume na hali halisi.....sijui hata nielezeje...
Na hata tulipokubaliana na mchumba wangu kuwa iwe siri, niliona ni vyema iwe hivyo, ikawakati yetu,,,siri kati yangu na aliyekuwa mpenzi
wangu kwa sababu alizojua yeye mchumba
wangu…lakini kwanini ilitokea vile kiukweli mimi sina ufahamu huo...
Baada ya kuligundua hilo, na baada ya tukio jingine lililokuja kutokea baadaye, ...niliumia sana, sikuwaamini kuwa hayo yalitendeka kwa mtu niliyemuamini kiasi hicho,,,,na sijui ni kwanini ikaja kutokea hivyo,nilijiuliza sana , mpaka leo naendelea kujiuliza, na sijui kama nitaweza kupata jibu kama sitaweza kumpata mmoja ya hao wanaume wanne akanifafanulia. Iliniuma sana ....na inazidi kuniuma sana, kwani matokea yake ni aibu hii kubwa. Aibu ambayo ilikuja kuniharibia maisha yangu yote....na kuonekana mwanamke wa ajabu sana.....
Lakini hadi kesho nitang'ang'ania kuwa aliyenipa hiyo mimba ni huyo mchumba wangu,...mimi sijui mwingine, kwani yeye ndiye mwanaume nineyemfahamu, yeye ndiye aliyenionyesha hayo, na yeye kama ilikuwa hivyo ni yeye aliyesababisha hayo yote kutokea....
Pamoja na hayo mimi sikuwa na ufahamu zaidi, sasa mzee angetaka nimuambie nini zaidi, ...kweli hawanikubaka, lakini sijui ilitokeaje...kiukweli hata mimi nahitaji maelezo, nahitaji kukutana na hawa watu waliosababisha haya yote,....ama kwa hii siri aliyotaka mume wangu,.....hata yeye nahitajika kukutana naye tena, kwanini alitaka iwe siri, kwanini hakutaka twende polisi....
Ndio maana hata mzee alipotaka nimpe jibu nilishindwa kutamaka wazi wazi.....hata hivyo niliwahi kuona huo ushahidi.....haikuwa kubakwa,...haikuwa kubakwa,....sasa ilitokeaje...ooh mungu wangu, kwanini hivi....nikabakia kulia....na hatimaye nilijua sina jinsi, natakiwa kusema, natakiwa kujibu swali la mzee;
‘Mzee wangu,
mimi sikutaka kukujibu kwa haraka kutokana na swali uliloniuliza, nilitaka
kwanza unielewe, na uelewe hali yangu. Najua jinsi gani ulivyojitolea kwangu,
najua dhamana uliyoibeba kwa ajili yangu, na najua heshima yako, lakini kwa
huruma zako uliamua kuubeba mzigo huu, na mimi sina budi kukushukuru sana, lakini hata hivyo
mimi nasita sana kukuambia ukweli, kwani hata mimi sina uhakika sana nao…’nikatulia
‘Sijakuelewa
vyema, una maana gani ya kusema huna uhakika sana nao,…si umenielewa lakini,
mimi ninachotaka ni jibu kuwa je hao wanaume ulitembea nao au wanakusingizia
tu…?’ akauliza mzee sasa nikiona kama kakasirika, nahisi alishaanza kunihisi
vibaya !
‘Mzee
nitakujibu hilo swali lako, ila na mimi nataka ahadi kwako kuwa na wewe hutazidi kuniweka uchi, nikazidi kuteseka,
…haya ninayopambana nayo ni dhaidi ya uwezo wangu…mzee mimi nimechoka, siwezi
tena kubeba adhabu hii, hapa nilipo najisikia vibaya sana…’nikasema na mzee
akaniangalia kwa jicho la mashaka, akasema
‘Unajua
sikuelewi,…wewe uliposema hao wanaume ni wanafiki,baada ya kusikia kauli yao kuwa walitembea nawe na hadi kukupa
ujazito, niliingiwa na chembe la furaha moyoni mwangu… unakumbuka ulitamka hilo
neno awali, wanafiki wakubwa hao, sasa vipi tena…?’ akaniuliza na mimi nikakaa
kimia, yeye akaendelea kusema
‘Ulipotamka
maneno hayo, mimi niliingiwa na furaha, nikijua kumbe kweli wamekusingizia, na
ndio maana nikatabasamu kuwa ndoto yangu ni ya kweli, kuwa wewe sivyo hivyo
wanavyofikiria watu, wanakusingizia tu, na mimi nitaweza kuendelea na msimamo
wangu wa kukusaidia…’akasema mzee.
Mzee
aliposema hivyo, niliingiwa na mashaka, nikajua huenda nikimwambia mzee ukweli
wote basi yeye ataingiwa na ghadhabu na hatimaye kushindwa kunitetea, lakini
sasa nifanyeje, unajua kwa hali niliyokuwa nayo, sina ndugu, wazazi au rafiki
wa kunisaidia, ….ilishafikia hatua kumuona huyo mzee kama msaidizi wangu,…na
kweli yeye ndiye alikuwa tegemezi langu…
‘Mzee….naogopa
sana kukuambia ukweli unaotoka
wewe..naogopa ya kuwa hutanielewa…..’nikasema
‘Unasikia ….binti
usinipotezee muda…’akasema mzee
‘Haya mzee,
ngoja kwanza nikujibu swali lako la moja kwa moja, naona unashindwa kunivumilia…unashindwa
kunielewa, ..na mzee usiponielewa wewe….basi tena ….., najua utakuwa kama hao
wengine…’nikasema
‘Lakini
nikuulize kwani inakuwa vigumu gani kutamka, kuwa ni kweli ulitembea nao au sio
kweli wamekusingizia, kuna ugumu gani hapo…mbona unanitia mashaka?’ akauliza
mzee sasa akiniangalia kwa makini.
‘Mzee, bila
kunielewa, hata kama nitakujibu utakavyo, haitasaidia kitu, unaweza kuchukua
maamuzi ambayo sio sahihi, na …..hutanielewa, kwani ….yote hayo yamefungamana
na siri,…na nashangaa kwanini wenzangu wameivunja hiyo sirii…’nikasema
‘Ni Siri
gani hiyo inayoambatana na dhambi…hivi wewe huoni kuwa unaniweka kwenye wakati
mgumu, kama kuna jambo mlifanya, la dhambi, mkawekeana ahadi ya kutokulisema,
na likaja kugundulikana kuwa na mimi niliwasaidia, huoni kuwa nitakuwa na
wakati mgumu….’akasema
‘Mzee
nimekuelewa,…., lakini nachelea kutoa jibu la swali lako kwani haliwezi kukidhi hali
halisi,….ni jibu la mkato lenye mambo mengi ndani yake, ..ndio maana nilianza
kukuelewesha,..’akasema
‘Umetembea
nao au hujatembea nao….?’ Akauliza mzee kwa sauti ya ukali sasa
‘Mzee ama
kwa vile unataka jibu la mkato, sina budi kukujibu na wewe utaamua mwenyewe…kwani
hata mimi mpaka leo sina uhakika vyema ilivyokuwa,….ila viashiria na ushahidi
niliokuja kuuona ulionyesha hivyo…’nikasema
‘Nijibu tu
swali langu….sasa imetosha,naona una lengo la kupoteza muda, mpaka unanitia
mashaka, kama kuna mengine yatafuata
baadaye…’akasema mzee
‘Swali lako
mzee ulitaka kujua kuwa je hao wanaume wanne niliwahi kutembea nao,…jibu ni
NDIO, niliwahi kutembea nao…’kabla sijamaliza mzee akasimama, akawa anacheza
ile ya kimuhe muhe akaniangalia kwa macho yaliyobadilika ghafla,…chuki, hasira…
‘Unasema
nini,….ina maana kumbe ni kweli, ina maana kukuaminia kote, kuweka dhamana
yangu kwa watu kuwa sio kweli,kuwa wewe
umesingiziwa, kumbe nilikuwa nabeba mavi kwenye kapu, …nikiambiwa ni
dhahabu…mungu wangu, unajua ulichokifanya, mimi sasa nitakuwa siaminiki tena…sijui
nitawaambia vipi wajumbe….’akasema mzee na sasa akawa anataka kuondoka.
‘Sasa Mzee
mbona unaondoka,…. wewe ndiye baba yangu
nikiondoka hapa nitakwenda kwa nani na hii hali,…hatua niliyofikia nisipopata
msaada nitakuwa kwenye wakati mgumu, nahitajika vipimo, nahitajika….’nikasema
na mzee akawa hataki hata kunisikiliza tena.
‘Mzee
tafadhali nielewe,…mzeee halafu wewe ni kiongozi wa waumini, ina maana mtu
akikosea mnamtenga, mnamkimbia…hujanisikiliza, sijakuambia huo ukweli, hiyo
siri niliyotaka kukufichulia….ina maana gani sasa ukiondoka, na niende wapi mzee wangu, watanifukuza hapa,
nitakwenda wapi?’ nikauliza
‘Unajua
binti, sasa naanza kukushuku vibaya,…maana hata katika kuongea kwako kote
yaonyesha hujutii, ni kama vile unaona umeonewa,ndio tatizo lako…dhambi kama
hizo ulitakiwa utubie uionyeshe jamii kuwa umekosea, na muhimu ulitakiwa ukawapigie
wazazi wako magoti,…
'Yaanim .aaah, wanaume wanne, angalau wangekuwa wawili, wanne…
umenikatisha tamaa kabia hata ya kuendelea kukutetea…kumbe ndio maana…unajua
nilihisi mke wa mwenye nyumba analalamika kwa ajili ya wivu tu…lakini ile picha
inaonyesha ukweli ulidhamiria kutenda dhambi na mume wa mtu..ile picha kwa
yoyote akiiona…ni ushahidi tosha,… au nayo kaitengeneza huyo mke wa mtu, sio
kweli…?’ akauliza/
‘Mzee ndio
maana sikutaka kukupatia hilo jibu ulilotaka wewe, …..na hiyo picha inadhirisha
ukweli kuwa mambo mengine yanaweza kuchukuliwa juu , juu yakatenegenezewa fitina, ..lakini ukweli
halisi sio huo….nakuomba mzee wangu nielewe…’nikasema
‘Mimi naanza
kukutilia mashaka, siamini tena ndoto yangu,nahisi ilikuwa ndoto ya
shetani,…kama kweli ulitembea na hao wanaume wanne,..sio mmoja, wanne, utasema walikubaka….hapana…..nambie
ukweli walikubaka….?’ Akauliza na mimi nikawa nalia , kwikwi,….na sauti ikawa
kama haitaki kutoka.
‘Kwa
ushahidi na kauli zao, ulitembea kwa ridhaa yako mwenyewe,..huo si umalaya,….na
sasa unataka kuendeleza tabia hiyo kwa mume wa mtu…je walikubaka?’ akauliza kwa
hasira na mimi nikabakia kimia, siwezi hata kuongea kuna hali ilinishika sauti
ikawa haitoki , maumivi ya tumbo, mgongo….nikawa nagugumia ndani kwa ndani huku
machozi yakinitoka.
Mzee akawa
kageuka kuelekea nje, naona alikuwa anasita kuondoka,na hatimaye sauti ikanijia
na kusema;
‘Mzee ndio
maana niliogopa kukuelezea ukweli…jibu la swali lako kwani ulivyotaka nikujibu
ulivyotaka wewe ni wazi itaonekana mimi nina makosa, ni vyema ungenipa nafasi
nikaelezea ni kwanini hayo yalifanyika, naomba unisikilize mzee…’nikatulia.
‘Niambie
kwanza, je walikubaka…?’ akauliza
‘Sio kihivyo
mzee, ,hawakunibaka…’nikasema
‘Kwahiyo ina
maana ulitembea nao kwa mapenzi kwa ridhaa yako mwenyewe....’akasema
‘Sio kihivyo
mzee, …..ngoja nikuambie…..’nikasema
‘Kama
hawakukubaka, …mimi siwezi kusikiliza zaidi,….sitakuelewa…..’akasema na mzee
akaanza kuondoka. Hakutaka hata kugeuka nyuma kunisikiliza, ….alipofika nje
akasema
‘Sitaki hata
kuongea na wewe na tena…’mzee akasema na kuondoka nikabakia mwenyewe ,
….nikajua sasa ndio mwisho wangu….sasa nisubirie ni nini watakisema wenye
nyumba….na wakati nawaza hilo mara mlango ukafunguliwa..
Bado tupo kwa majaribio, Kisa hiki kipoFace book,...ingie kwenye page yangu ya Diary yangu utakisoma kwa mapana yake...Tupo pamoja
No comments :
Post a Comment