Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeMonday, February 8, 2016

Nimerudi Tena, kwa majaribio, tukumbuke hii Mungu ndiye mpaji

Jembe kwa mkulima likiharibika, hana jinsi kusubiria mpaka litengenezwe, laptop iliharibika, ikabidi nipeleke kwa fundi, ...namshukuru kijana wangu kanisaidia sana, kwa hali na mali, maana kwa kipindi hiki sikuwa na jinsi ya kumpelekea fundi wa malipo, bado nipo kwa mawe...

Nimejifunza kuwa pamoja na mitihani ya maisha usichoke kumwamini na kumtegemea mungu. Ni kipindi kigumu sana, na inafikia muda unasema sasa nimepatikana, lakini yote yana mwisho na kila jamboo lina wakati wake, kwanini imekuwa hivi rejea hii :

Siku hiyo tulimzika mwenzetu, mwenzetu huyo alikuwa na mipango mingi , na wakati mwingi tukikutana naye alikuwa akituambia mipango yake, alishanunua kiwanja, na alikuwa mbioni kujenga....lakini Mungue kampenda zaidi....kaacha watoto na mke!

Wakati tunamzika nikakumbuka sana tukio lilitokea siku tukisubiria pesa ya rada. Nafikiri wengi mnafahamu pesa hiyo iliyotolewa Uingereza, kutokana na ile kashfa ya rada, Sijui kwanini akili yangu ilinituma kuliwazia hilo....Kipindi hicho kampuni yetu ilikuwa katika hali mbaya sana kibiashara.
siwezi kuitaja,....ila hatukukata tamaa tukiwa na matarajio huko mbele,..labda...

Tukiwa na mkurugenzi wetu..., tulijinyima sana, tukaishi maisha kutokana na kile kipato kidogo kilichopatikana kwahiyo hata  mshahara ilikuwa ni ya shida, tunapokea kwa mafungu, lkn tulijua hali halisi, na tukakubaliana nayo,...na hata huyo mkurugenzi wetu hakuacha kutupa moyo kuwa baada ya dhiki ni faraja.

'Nawaambieni, haya yote yatakwisha, dhiki hii yote mtaisahau, nyie anzeni kujifunza kuendesha magari, na kama huna kiwanja, tafuteni..kuna neema inakuja kutoka kwa ....' akasema na hakutaka kumalizia .

Na tulijaribu kumdadisi zaidi tukijua kuwa yeye ni mfanyakazi kama sisi, yupo mwenye kampuni, yeye akasema;

'Mimi kamwe sitawaangusha..tumetoka mbali...nitawapigania kwa kila hali...nyie anzeni kuamini hivyo...'akasema mkurugenz wetu, ...Ni kweli kulikuwa na tetesi ya kupata pesa nyingi kutokana na zabuni za serikali, hasa kutokana na fungu hilo la pesa za Rasa.

Basi siku hiyo akatufunulia wazi na kusema;

'Mnajua kutokana na pesa hiyo ya Rada, Vifaa vyote vilivyojaa kwenye ghala vitachukuliwa na serikali kwa ajili ya kusambaza mashuleni.. Aliposema hivyo, wafanyakazi wakashangilia, na wengine wakajitolea kufunga kwa ajili ya maombi ili hilo lifanyike.

'Yaani mniamini...'alisema alipoona bado sisi hatujaamini, Hebu fikirieni vifaa vyote vilivyojaa kwenye ghala vikichukuliwa tutakuwa na pesa kiasi gani, ni mabilioni ya pesa .. sizani bwana mkubwa ataweza kutuangussha tumeshaanza kutengeneza bajeti tayari.' alizidi kutupagawisha.

'Na zaidi tumeambiwa tunatakiwa tuzalishe zaidi, kwani kuna zabuni nyingine mara tatu zaidi ya hii..akasema
Wafanyakazi wakashangilia, na kweli wengine wakaenda kutafuta viwanja, wengine kutoa oda za magari, na maneno ya majigambo kila walipokuja wateja yalianza kusikika kutoka kwa wafanyakazi,..
.'sasa mtatuona...sisi sasa matawi ya juu..'

Ya mungu mengi, kweli tulifanikiwa, tukapata zabuni hizo, tukajua sasa hata mishahara itapanda, sasa tutanunua hata magari, sasa tutajenga..sasa umasikini kwaheri...sasa na sisi angalau watoto wetu watasoma shule za kulipia kama wao.

  Nikuambie ukweli yote hayo yalikuja kuwa ndoto za alinacha, kwani yaliyotokea, baadaye kila mmoja wetu hakuamini,mpaka leo siamini....

                                       **********
'Kazi hakuna...bwana mkubwa kasema inabidi mpunguzwe kazi kwani baada ya hizi zabuni serikali imesema itazalisha vifaa vya mashuleni wenyewe...'kauli ya kukatisha tamaa ilitamkwa na mkurugenzi wetu huyo, akiwa kwenye gari lake jipya..

' Sasa bosi mbona..ahadi, mbona..' tulibakia kujiuma uma tu hatuamini,

Ndugu zanguni, kwa kifupi.ilibaki kuwa kilio na duwa la kuku halimpati mwewe, ajira ikaota mbawa na ndoto ikaisha, kwani kulishapambazuka.. tukajikuta tupo mitaani! haki haipo, ndoto hakuna, ...na sijui kama haki ipo tena katika hii dunia.

Ni kweli wanadamu kila mmoja ana njozi zake, mipangilio yake, ahadi zake, na nyingi ya dhamira hizo tunafikia hata kumsahau mungu kuwa yeye ndiye mpaji...na wengine hufikia hata kujiona wao ndio wenye mamlaka ya kutoa riziki.... Hasa pale tunapopata, au tukikusudia kupata.

Utasikia `Tutafanya,...lazima, tutafika lazima...hii 'lazima ' inatoka wapi, tunajisahau kuwa sisi hatuna mamlaka ya kujua nini kitatokea siku za usoni....labda wengine ni wajanja, wanajua kuongea, ni wasomi,....labda,

Ni kweli tunatakiwa tuweke malengo, mikakati ya usoni, lkn huku tukimuomba mungu kwa sana, huku tukijua yote yatapatikana kwa mapenzi ya mungu. Na tukumbuke pia sisi sote ni waja wake, tutakuwa wajanja sana, tutapata, kwa hadaa na kila  mbinu, lakini tukumbuke yupo hakimi wa mahakimu....

Kingine ni nafasi za watu, mkipanga mambo,  huwezi kujua nafsi ya mtu mwingine, wewe unaamini kuwa asemayo ni kweli, lakini tukumbuke mwanadamu ni mwingi wa ubinafasi, mara nyingi hujifikiria yeye, na ni wachache wanaofikiria wengine.

Kwahiyo siku hiyo ya msiba niliwaza sana, nikajua kuwa kwa lolote lile tunatakiwa tusema mbele ya dhamira yetu 'mungu akipenda(Insh -Allah).'

Tumuombe mungu atupe mema kwa yale tuliyoazimia, na atufanikishie malengo yetu kwa neema zake. Atupe riziki za halali, na kutusaidia kuivuka mitihani hii migumu ya maisha. Amiii

 Tupo pamoja
Tunawatakia ijumaa njema

1 comment :

Yasinta Ngonyani said...

Kaka wa mimi karibu tena na pole sana kwa yote kama ulivyosema ni kwamba Mungu ni muweza na kwa kila jambo tufanyalo hatuna budi kumwomba baraka zake na pia kumshukuru kwa neema tupatazo.