Huku kwa
mshitakiwa , ...
baba wa mzazi
wa kijana,
Mzee huyu hali
yake iliendelea kuwa mbaya, na alikataa kabisa kupelekwa hospitalini, akawa
anaugulia njumbani.
‘Br hii hali
yako inanipa mashaka,....kwanini tusiende hosp?’ Profesa akamuuliza kaka yake
‘Mimi
nimezoea miti shamba, kama haifanyi kazi ujue hakuna dawa nyingine ya kunitibu,
na hata tukienda huko ni kujiangaisha tu....kama mwenzangu katangulia najua na mimi
nitafuatia...’akasema
‘Mwenzako
yupi?’ akamuuliza
‘Hahaha...bwana
mdogo wewe hufahamu, ...mimi nafahamu mengi sana, wewe uliporudi jana na
kuniambia hali ya mgonjwa,....ulisema mgonjwa anaonekana na nguvu ya ajabu, nikajua
tu....’akasema
‘Sikuelewi
bro,....mgonjwa akiwa na nguvu ya ajabu ndio anapona au ndio ....’akakatiza
‘Yategemea,
....tatizoo la mwenzangu ni tatizo kubwa, na huko kuchelewesha madakitari
kusema llte ina maana yake,...nilishajua,...wewe subiria tu,
utasikia,...’akasema
‘Mhh, bro,
hizo hisia zako sio nzuri....’akasema, na lengo lake la kutaka kumshawishi
waende hospitalini, lilikatishwa tamaa hasa pale kaka yake aliposema;
‘Mwenzangu keshatangulia,...najua
hilo, na mimi nipo njiani......’akasema na Profesa akamuangalia kaka yake kwa
mshangao, akihisi labda kaka yake keshachanganyikiwa
‘Bro leo mimi
sikuwa na mpango wa kwenda hospitalini, maana jana, mimi niliondoka akiwa
anaongea vizuri kabisa, na aliongea na mwisho alimuulizia mtoto wake kama
kawaida yake...;akasema
‘Mtoto wake
yupi...hebu aachane naye, na huyo ndiyo chanzo cha umauti wetu, mtoto unamzaa
ukiwa na furaha, kuwa umepata tunda la familia, na huyo anaweza akawa chanzo
cha kukuondoa hapa duniani...’akasema
‘Mhh....’profesa
akataka kusema neno
‘Sasa huyo
mtoto alifika?’ akauliza
‘Alifika muda
ambao huyo mama alikuwa hajiwezi, na, cha ajabu mtoto wake alipondoka muda
mfupi tu, mama huyo alizindukana,...tukajaribu kumpigia simu, na simu iliita
wee, baadaye ikakata, na ilipopigwa tena ikawa haipatikani..
‘Hayo
yameshaandikwa, huyo alishawakana wazazi wake kwa kauli na vitendo....na sijui
kama kuna jambo la kumsaidia,..’akasema
‘Lakini.....’akataka
kusema kitu profesa
‘Achana naye,
...hebu nambie kwanza kuhusu kesi , kwani nataka niondoke nikiwa sina kesi ya
kujibu, ya dunia yabakie ya kujibu mbele ya mola wangu...’akasema
‘Bro, kesi,
imesogezwa mbele, kutokana na hali yako...hakimu kaliona hilo, lakini pia, ukumbuke
kulikuwa kunasubiriwa makubaliano yenu kuwa wewe na mtoto wako mfahamiane
mkubaliane,lakini wewe umekataa hilo...’akaambiwa
‘Hahaha...hivi
nikuulize, hivi kweli kuna mzazi anaweza kumkataa mtoto wake hivi hivi tu,
...’akasema kaka mtu akionyesha uchungu usoni
‘Sijui...kwakweli
bro, mimi sijui,,..ndio maana watu wanawashangaa sana...’akasema
‘Mimi
sijamkataa huyo mtoto, ila mimi natimiza wajibu wangu, kama mzazi, yeye kama
mtoto ni wajibu wake kujirudi na kunyenyekea kwa mzazi wake, lakini sio mimi
mzazi kwenda kwa mtoto kumpigia magoti, hilo halipo...’akasema
‘Tatizo
nililoliona hapa ni kuwa nyote mna kasumba moja, tabia na hulka zenu
zinafanana, baba kama mtoto,,,;akasema na kaka mtu akainua kichwa kumuangalia
mdogo wake,
‘Samahani kulisema
hilo, wote mna mihasira,.... sasa sisi tufanyeje..... yeye kasema hawezi kuja
kukuomba msamaha kwa vile wewe ndiye
uliyekwenda kumfanyia fujo nyumbani kwake,..haijalishi kuwa wewe ni nani
kwake....’akasema
‘Sawa..hayo
tuyaache,...’ akasema kaka mtu akitaka kukwena kuliongea hilo zaidi
‘Aaah, bro ni
vyema hilo tukaliweka wazi, ili tulimalize kabisa...’akasema Profesa
‘Nikuambie
kitu, ipo siku utajaliwa utapata watoto wako, na wewe utaliona hilo, mimi najua
huyo mtoto atajirudi, kwani na yeye sasa ana familia, lakini wasiwasi wangu ni
kuwa itatokea akiwa keshachelewa, simuombei mabaya, lakini ukumbuke jambo, haya
anayoyafanya kwangu, atakuja kufanyiwa,..;akasema kaka mtu
‘Usiseme hilo
bro...’akasema Profesa
‘Mimi simuombei mabaya, mimi kama mzazi namtakia
maisha mema tu,....najua sitakuwepo mbeleni, ila wewe labda utakuwepo enzi hizo,
utayaona,.....,mimi sijui wewe
utamsaidiaje, usije kumtumpa, ....kwani wewe ndiye uliyemuharibu, ...nakuambia
hilo unielewe, kiujumla inanitia huzuni sana.....’akasema kwa sauti ya huzuni.i
‘Lakini bro
kwanza unatakiwa umsamehe....huyo ni mwanao,...vijana wetu wa siku hizi
wanachangamto nyingi, maisha yenu sio sawa na haya maisha yao ya sasa, unaona
mitaani wanavyotukanana, mtu anamtukana mwenzake anakimbilia kutoa tusi
linalomleanga mama, ni jambo la ajabu kabisa ..., ‘akasema
‘Ndio
hivyo,...’akasma kaka mtu
‘Unajua bro,
mengi yatasemwa kunihudu mimi, lakini mimi nilijaribu kumlea huyu kijana kadri
niwezavyo, ukumbuke na mazingira nayo huchangia, wapi alipokulia,.....huyu
kijana wako kuna muda alikuwa na lugha kama hizo, za mitaani, za kihuni .,
nilimuasa sana...’akasema
‘Nimeshakuambia,...na
unielewe hilo, hakuna mzazi anayemkataa mtoto wake, ..tunafanya mengine kwa nia
ya kumrekebisha mtoto ili ajielewe, ili ajirudi,yeye ni mtoto kwasasa lakini
atakuja kuwa baba wa kesho, tusipofanya hivyo, yeye atajenga msingi gani kwa
kizazi chake....’akasema
‘Nimekuelewa
bro...’akasema Profesa
‘Kijana ni
muhimu alielewe hili, mimi kama baba, najawa na hasira, lakini moyoni bado
naumia, kwani ule msingi ninaotaka kuuweka kwake, hauelewi,....yeye anafikiri
elimu ya darasani inaweza kufanya kila kitu, hapana, kuna elimu ya mazingira,
ya jamii, ya mahusiano, ya kuishi na watu, na hiyo huanzia ndani ya nyumba,....
hili ni kwa manufaa yake na kizazi kijacho...’ akasema
‘Bro,
nimekuelewa, lakini .....;akasema Profesa
‘Hakuna cha
lakini hapa,kama umenielewa, sitaki lakini, .... muhimu hapa ni mtoto atimize wajibu wake..kama
mtoto, umenisikia,.Hata kama kwasasa yeye ni baba na watoto wake, lakini
akumbuke kuwa ana wazazi,...mimi nimemaliza, nataka kupumzika....’akasema kaka
mtu huku akiwa kainamisha kichwa chini...
‘Ndio bro,
lakini ni muhimu mkutane naye, ujaribu kumuambia hayo mwenyewe, unalionaje
hilo...’akasema Profesa.
Na ndipo mlango
ukagongwa, aliyefika alikuwa jirani yao, akasalimia, baadaye akamuita Profesa
nje
‘Profesa vipi
tuongee kidogo nje, maana wewe ni mtaalamu.....’akasema huyo jirani yao, na
Profesa akatoka nje akijua kuwa jamaa huyo jirani wake huenda anahitajia dawa
zake, wakatoka na kumuacha kaka yake, akiwa kajiinamia.
Huko nje ndio
akapata taarifa hiyo ya msiba
‘Sasa mambo
yameharibika....kama kijana hakuwahi kukutana na mama yake...oh,...’alisema
Profesa akiwa kashika kichwa
*****************
Taarifa
ilipofika kwa Profesa, ilikuwa kama rungu jingine kichwani mwake, moyoni
alihisi kuwa sasa na mzigo mkubwa ambao hawezi hata kuubeba, je atamuelezaje
kaka yake,
‘Haina jinsi
lazima nimfiche.....japo kwa muda..’akasema
‘Na
akishazikwa huyo mama, ndio nitakuja kumwambia kaka kihekima zaidi,....nikimwambia hivi sasa nitamuua kaka yangu....hapana, ni lazima nimfiche...’akazidi kusema kimoyo
moyo....'
Wakati anayawaza haya yeye hakufahamu
kuwa kaka yake alishahidi hiyo hali, alishafahamu kuna jambo, na alishahisi
kuna msiba,hata kama wangetumia mbinu gani za kumficha.
Na kweli
Profesa akajitahidi kumkwepa kaka yake, hakurudi kuongea naye, nia ni
kuhakikisha kaka anatulia, hapati hizo taarifa, na alishawaambia majirani zake,
wasije kumwambia kaka yake kuhusu msiba huo....
Ilikuwa siku
ya mazishi, kesho yake, kwani msiba huo hakucheleweshwa, mazishi yalipangwa yafayike
haraka, na Profesa akiwa kajiandaa kuelekea msibani, mara alishangaa kaka yake akija kwake kwa
kujikongoja, japokuwa alionekana mwenye nguvu, hata hivyo, haikuwa ile hali ya
kaka yake anayoifahamu....
‘Kaka
unakwenda wapi?’ Profesa akauliza
‘Lazima nikamsindikize
mwenzangu nafahamu na mimi nitamfuata hivi karibuni....’akasema na hakuna
aliyeweza kumzuia, ikabidi watafute usafiri, na wote wakaelekea huko kwenye
msiba
Kweli
walifika wakamzika na baadaye wakarejea nyumbani,..lakini kaka mtu aliporejea nyumbani
, ilikuwa kama nguvu ya soda akawa hana nguvu kabisa, ikafika muda hata kuongea
hawezi...
Profesa
akaona atampoteza kaka yake bure, akaongea na wazee nia hasa wampeleke
hospitalini, na pia ikibidi waweze kumshawishi kijana aje aonane na baba
yake,....na kikao cha wazee wanandugu kikakutana.
Profesa
akawaelezea ajenda hiyo, na wazee , wanandugu kwanza walilipinga hilo, kutokana
na msimamo wa ndugu yao, kuwa wao wamechoka kumshawishi, kwahiyo hilo swala
liachwe kama lilivyo
‘Lakini huyu
mtu anaumwa, na kazidiwa, na nina imani moja ya jambo linalomuumiza bro ni
kuhusu mtoto wake...’akasema Profesa
‘Sasa tufanye
nini....?’ akaulizwa
‘Ndio maana
nataka hekima zenu, mimi nafahamu kwenye wazee hakuharibiki neno, ....’akasema
Profesa
‘Na kuna
jingine linalomuumiza kaka hadi sasa...’akasema
‘Ni jambo
gani tena, kwanza tulimalize hili ......wewe una wazo gani ?’ akaulizwa
‘Hili jingine
litaweza kuwakutanisha,...’akasema
‘Jambo gani
hilo?’ akaulizwa
‘Bro anasema
hataki kesi hii iendelee kuwepo, anataka hukumu ipitishe, kama yeye anakosa
sawa, kanisisitizia sana kuwa anahitajia hiyo kesi imalizike haraka
iwezekanavyo, ....na mtu anayeweza kusaidia kesi hiyo imalizike ni huyo kijana
wake...’akasema
‘Sasa tufanye
nini...?’ akaulizwa
‘Mimi
nitakwenda kuongea na huyo kijana, lakini nawaomba na nyie mnisaidia kuongea na
kaka yangu...’akasema
‘Je una
uhakika kuwa unaweza kumshawishi huyo kijana, peke yako?’ akaulizwa
‘Nitamshawishi,
na kama itashindikana.....kwa ajili ya kaka.nitatumia karata yangu ya mwisho,....’akasema
Profesa
*****************
WAZO LA LEO:Katika maisha haya ya dunia, kuna
mambo muhimu tunayadharau, na kumbe tukiyafanya yanatusaidia sana. Ni muhimu
tukakumbushana tu, mimi na wewe, kila mtu kwa nafasi yake au kiongozi mwenye dhamana ndugu kwa ndugu, au majirani kwa
majirani nk..ni muhimu sana , swala hili la kuelekezana mema, na kukatazanana mabaya...
Kila mtu
akichukua dhima hii akaifanya kwa moyo safi, jamii yetu itakuwa kwenye uadilifu
mkubwa, tusichukie tukikanywa na kukosolewa, kwa mabaya tuliyoyafanya, na
tufurahi sana, tukielekezwa kwenye mema, ...hata kama anayefanya hivyo kwako
unamuona hana thamani, lakini angalia thamani ya kile anachokuelekeza au
kukuonya.
Twatakiwa tuyafanye
haya kila mtu kwa nafsi yake, tukikumbuka kuwa.maisha ya mwanadamu ni mafupi
sana lakini mambo hayo yana faida endelevu..., sio kwa hapa duniani tu, ambapo
maisha ya mtu ni ya muda mfupi tu,
lakini faidia ya mambo hayo kwa mwanadamu ni ya kudumu, yana tija hadi
huko kwenye makazi yake ya kudumu....
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment