Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeMonday, November 23, 2015

RADHI YA WAZAZI-56Wakili mtetezi akiwa anaendelea kuyawaza hayo, akawa ameshafika sehemu ambayo alitakiwa kukaa na watu wake ili, kuliwaelezea kile walichoongea na hakimu na nini kimeamuliwa mpaka ikafikia kuahirishwa kwa hiyo kesi,....

Akawa anakumbuka jinsi hakimu alivyokuwa akiongea;

‘Wakili mtetezi, nimeshutushwa sana na kauli yako uliposema huyo shahidi ambaye alisimamishwa na muendesha mashitaka....ambaye alitakiwa kuthibitisha hayo aliyotendewa, ni mtoto wa mshitakiwa na hawafahamiani.....’hakimu alisema

‘Kufahamiana au kutokufahamiana, hakuzuii sheria isifanye kazi yake,....lakini kutokana na maelezo yako na maombi yako, kunanifanya niwe na mashaka kidogo....’akasema hakimu

‘Kutokana na kesi yenyewe ilivyo, na maelezo ya mshitakiwa na jinsi ilivyo somwa awali na mshitakiwa kukubali kuwa kafanya kosa ilikuwa sio rahisi kukubaliana na ombi lako.kuwa kesi hii iwe ya madai...’akaendelea kusema hakimu

‘Lakini sasa unasema shahidi huyo ni mtoto wa mshitakiwa, nikuulize kwanza una ushahidi gani wa kulithibitisha hilo?’ akauliza hakimu

‘Muheshimiwa hakimu ushahidi upo, ukihitajika nitautoa wakati wa kutoa ushahidi wangu na mashahidi,..’akasema wakili , na hakimu aligeuka upande wa muendesha mashitaka

‘Muendesha mashitaka umesema mshitakiwa ana makosa kutokana na ushahidi ulio nao, ..sitaki kuingilia sana undani wa madai  yako kwa hivi sasa, ila nataka kwanza lifanyike jambo moja,...’akawaangalia mawakili hao wawili, na hakimu aliamua kuingilia kati baada ya malumbano ya kisheria, kila mmoja akitetea hoja yake.

‘Mimi hakimu, baada kusikia maelezo ya wakili mtetezi, ambayo yamenishitua sana,..kuwa huyo kijana kakutwa na yote hayo, kayafanya yote hayo akiwa hafahamu kuwa huyo ni mzazi wake, na halikadhalika mzazi naye hafahamu kuwa huyo ni kijana wake....’akasema na kugeuka kumuangalia wakili mtetezi.

‘Mimi sitaki kwa hivi sasa kujua undani wa kwanini hali hiyo ilifikia hapo..., kabla hatujaendelea na hii kesi nataka mlitatue hili jambo kwanza, ...hili mlifanye kama wazazi, mjaribu kuweka hisia zenu kuwa nyie ni wazazi na huyo ni mtoto wenu....’akasema hakimu

‘Kosa ni kosa mzazi anaweza kumkosea mwanae na sheria ikachukua mkondo wake na kinyume chake vilevile....lakini kwa jinsi alivyoelezea wakili mtetezi, tukiamua tuendelee na kesi jinsi ilivyo, madhara yake mbeleni yanaweza kuwa makubwa....’akasema hakimu

‘Hebu kwanza hawa watu wajuane, na kila mmoja afahamu kosa lake, na mimi kama hakimu, nataka nipate muda wa kulifikiria hili ombi la watetezi kama linawezekana,....’akasema hakimu
 Muendesha mashitaka akataka kulipinga hilo, lakini hakimu hakumpa muda, hakimu akaendelea kuongea;

‘Mimi nimeona mliangalieni hilo kwa mtizamo huo, kwahiyo kila mmoja afanye juhudi zake, wewe wakili muendesha mashitaka, hakikisha huyo kijana anakubali kukutana na baba yake, kwani sijui nyoyoni mwake anajisikiaje baada ya kusikia huyo ni baba yake na hayo yalitokea...ni kazi yako kulisawazisha hilo..’akasema

‘Huyu sasa ni  mbaba na familia yake, kwahiyo anaweza kujielewa  hawa watu wakutanishwe wakae waongee, kesi nyingine kama hizi, tutumie hekima kuzimaliza ....’akasema akitikisa kichwa

‘Ninachotaka mimi ni kupata taarifa ya matokeo yake, je hawa watu wamefikia wapi, na kama ni kesi ya madai au kesi yenyewe iendelee kama ilivyo, tutajua baada ya kukamilisha hjilo zoezi...’akasema hakimu

‘Na wewe wakili mtetezi, huyo mzee, ...ni mshitakiwa, unayemtetea, ongea naye, sijui moyoni mwake kalichukuliaje hilo, baada ya tafrani hiyo, najua atakuwa na hasira sana, kama mzazi kufanyiwa hivyo na mtoto wake.mwenyewe,...sasa nataka wewe utumie hekima zako, mzee huyo ashuke na akubali kukaa na mtoto wake waongee....’akasema hakimu

‘Na kwa vile wewe ndiye uliyetoa hilo ombi, najua utajua jinsi gani ya kulifanya hilo,...’akasema na akimwangalia wakili huyo

‘Mimi  nisingelipenda kusikia kuwa mzee huyo hajakubali...natarajia changamoto, lakini mwisho wa siku zilete matunda mema,, ila ninachotaka hili zoezi lifanyika kwa haraka iwezekanavyo., ikibidi muanze leo hii, na isizidi wiki tuwe tumeimaliza hii kesi..;’akasema hakimu.

Tuendelee na kisa chetu

                                          **********
Watu hawa walisogea upande mwingine wa mahakama,  uzuri wa mahakama hii ilikuwa kubwa, kwahiyo waliweza kuchagua sehemu nyingine na kukaa ili waweze kuongelea swala hilo bila wenzao upande wa pili kusikia nini wanachokiongea.

Waliokuwepo ni mshitakiwa mwenyewe pamoja na ndugu yake, Profesa, pia walikuwepo wazee wawili kutoka kijijini, na mwingine alikuwa msaidizi wa wakili mtetezi, wote sasa walikaa kimia wakisubiria ni nini wakili mtetezi atakiongea..

‘Ndugu zanguni, hakimu alituita, na kutuita huko kunatokana na hali iliyojitokeza kuwa mtoto.kamshitakia mzazi wake, ...na wawili hao hawajuani..’akasema akimuangalia mshitakiwa

‘Hii ilikuwa ni hoja ya kushitukizia, wenzetu wangsema ni ‘surprise issue...’akasema akimuangalia mshitakiwa

‘Kiukweli, hii ajenda sikuwa nimejipanga nayo,  mnielewe hivyo wazee wangu, na ni hoja ambayo niliipata muda mfupi, na sikuwa nimejipanga ni kwa namna gani nitaongea na wewe mshitakiwa , kwani ulikuwa na haki ya kulifahamu hilo mapema....’akasema akimuangalia mshitakiwa

‘Kama tulivyoongea na Profesa, hili jambo lilikuwa ni la kifamilia zaidi, na haikuwa vyema kuliweka hadharani,...’akatulia akiwaangalia wote kama anasubiria huo utangulizi uzame kwenye ubongo wa kila mmojawapo.

‘Kutokana na muelekeo wa kesi ikabidi nifanye hivyo, kama mlivyoona shahidi huyo, aliyetendewa hilo kosa, alishaweka wazi kuwa kweli alihujumiwa, akafanyiwa fujo kwenye makazi yake, mlinzi wake akaumizwa.....unafikiri hapo hata kama hakimu ataangalia baadhi ya uwongo wa shahidi, lakini bado mshitakiwa utaoenekana una makosa.

Kiujumla kesi kama hizi, matokeo yake huwa ni mabaya kwa mshitakiwa, hata kama kwa mfano ingelifanywa hii kesi iwe ni ya madai, ikaja kutajwa kiwango cha fidia, kwa hali zetu, bado hali ingeliweza kuwa mbaya kwetu,...ndio maana  nikaona niitumbukize hiyo hoja kwa madhumuni mawili....’ akatulia

‘Kwanza ili kuweza kushinikiza ombi letu kuwa kesi hii ibadilike iwe ya madai zaidi,ikiwezekana iwe ya kifamilia,irejeshwe nyumbani,..kwani kwa muelekeo wa kesi ulivyokuwa awali, hilo lilishakataliwa. Kama ombi hilo lilikataliwa, tungefanyaje, mimi kama wakili natakiwa niende na muelekeo wa kesi inavyokwenda, ndio maana ikabidi niitumie hiyo hoja, .sijui kama mnanielewa hapo...?’akasema na kuwa kama anauliza.

Aliwaangalia wajumbe, wazee walitikisa kichwa kukubali, na msaidizi wake, lakini mshitakiwa alikuwa kainama akiwa kimia, na Profesa alibenua mdomo kama kutaka kusema neno, lakini hakusema neno.

‘Mimi haya yote sikuwa nayafahamu awali,  Profesa alikuja kunisimulia nikiwa nimeshajiandaa na mpangilio mwingine,...aliponisimulia hilo, mmmh, nilishangaa, ina maana mimi ni wakili, namtetea baba aliyeshitakiwa na mwanae, na wawili hawa hawafahamiani...na je lolote likitokea mimi nitaelewekaje,... niliingiwa na mawazo mengi sana, nikijaribu kujiweka mimi kama mzazi, na mtoto wangu ndio kapotea kihivyo, ilinipa shida  sana....’akatulia

‘Na baya zaidi , sikuwa na muda wa kufanya lolote, labda ningekutana na huyo shahidi, yaani mtoto wenu, ili niongee naye nimfahamishe, nikijua kwa vyovote atakuja kusimamishwa kulithibitisha hilo kuwa yote hayo yalitendeka, yeye angeliweza kuongea maneno ya kupoozesha na kesi isiwe na nguvu, ..

‘Lakini hata hivyo nisingeliweza kuongea naye bila kukutana na muendesha mashitaka...napo kungekuwa na changamoto zake,...Nikawa nimebanwa na muda , huenda kama ningeyafahamu mapema yangeliwezekana kwa namna nyingine yoyote...’akasema

‘Lakini hata kama ungefahamu mapema una uhakika yangeliweza kubadili hii kesi,....?’ akauliza mzee mmoja

‘Tungeweza kwenda na madai yetu hayo kwa hakimu mapema kabla kesi haijasikilizwa, na yeye angelitumia busara yake kuwa kesi hiyo iahirishwe mpaka pande mbili hizi zikutane...na kwahiyo swala hili la baba na mtogto kutokujuana, lingetatuliwa mapema, na hatuwezi kujua, huenda kesi ingelikuwa ni nyingine.....’akasema

‘Kama mlivyoona kwenye kesi....kijana alishinikiza kuwa mshitakiwa alidhamiria kutenda aliyotenda, na nilipoitoa hiyo hoja kuwa huyo ni mzazi wako, mnaona alichokifanya, akakana kuwa sio kweli, kuwa mshitakiwa ni baba yake, inaonyesha haamini...na kutokuamini kwake , kama kesi ingeendelea ingebidi nimsimamishe Profesa...kama haamini, hakubali, kuwa huyo ni mzazi wake, hakimu akaingiwa na shaka, .....’akasema akimuangalia Profesa

‘Sasa ....ulivyoingia  Profesa , niliona mabadiliko ya huyo shahidi usoni mwake,...nashukuru kuwa wewei uliingia wakati muafaka...nikiwa naishinikiza hiyo hoja, athari za kukuona wewe, mshituko alioupata, ulisaidia sana kwangu .....’akatulia na kumuangalia Profesa

‘Kwangu ilikuwa ni msaada mkubwa wa kuweza kumgaragaza huyo shahidi,hadi hakimu kushawishika, na hekima zikamuingia akaliona hilo, ‘akatulia

‘Kiukweli.....tatizo ilikuwa kwa muendesha mashitaka, lakini na yeye hoja hiyo ilimjia bila kutarajia, hakuwa analifahamu hilo, wakati anatafakari awezeje kulikataa hilo, au kuweka hoja ya pingamizi, lakini akawa anasita akiwa hana uhakika je kweli ai si kweli kuwa huyo ni mtoto wa mshitakiwa

‘Kwa hali hiyo ya muendesha mashitaka kuchelewa kuweka pingamizi, na kutokana hoja yenyewe kuwa na utata, ..., hakimu ikamgusa....’akatulia na taratibu akageuka kumuangalia mshitakiwa.

‘Kwa hali hiyo, mzee, ...’akamgeukia mshitakiwa, halafu akawaangalia wengine akisema;

‘Ndugu zanguni, hatutakiwi kumuangusha hakimu kwa kujitolea kutumia hekima zake...’akawa anawangalia wote na sasa akawa kamkazia macho mshitakiwa

‘Ndugu mzee wetu, usijali nikitumia jina ‘mshitakiwa’ maana ndani ya mahakama hii ndivyo unavyotambulikana, ....’akamwangalia huyo mzee, mzee akionekana kuchoka, na mwingi wa mawazo, na kwa muda huo alikuwa kainamisha kichwa chini kama vile anaona aibu watu kumuangalia, au akiwa kazama kwenye mawazo mazito.

‘Najua hali uliyo nayo kwasasa ikizingatiwa kuwa hili jambo limekuja kwako kwa kukushitukizia, ...ilibidi iwe hivyo,....na kiujumla sikuwa nimepanga moja kwa moja kulifanya  hili na  hata Profesa hakujua kuwa nita;lifanya hilii,...kabla ya wewe kupewa taarifa’akasema

‘Profesa alikuwa kapanga jinsi gani ya kuja kukuambia huo ukweli, kuwa huyo kijana, ambaye alisimamishwa leo kuwa shahidi wa kuthibitisha hayoo yaliyotokea,  ni mtot o wako....’akasema

‘Lakini imekuwa hivyo mzee wangu, mimi katika mapambano ya mahakama ikawa sina jinsi ikabidi niiweke hiyo hoja kushinikiza ....’akasema akimuangalia mshitakiwa
Mshitakiwa akatikisa kichwa kuashiria kusikitika, ....akahema kwa guvu, halafu akasema;

‘Hata siwaelewi nyie watu, yaani nyie mnanifanyia hivi, mimi naheshimika na mila na desturi etu kamwe hazichezewi, mtoto kunyanyua mkono kumpiga baba yake, hakujawahi kutokea katika maisha yangu, hivi nyie mataka niuweke wapi  uso wagu, wazee wenzangu watanielewaje., hamjui jinsi gani mlivyonizalilisha, ...’akasema

‘Naelewa mzee...’akasema wakili

‘Hii ni bahati mbaya mzee mwenzetu, ....’wazee wenzake waliokuwepo wakasema lakini alitikisa kichwa kukataa, huku akisema;

‘Ni bahati mbaya!!! Nyie wenyewe manielewa, hili, lini...na nini kinatakiwa kifanyike...Unajua sasa hivi najiona kama nimevuliwa nguo mbele za watu, ...hata, sizani kama nitawasamehe nyie watu, yaani mdogo wangu mwenyewe, badala ya kushauriana na mimi kwanza unafaya mambo kienyeji, umazizarau...’akasema mshitakiwa akimwangalia ndugu yake kwa jicho la pembeni

‘Lakini mzee, kwa hali kama hiyo hatukuwa na jinsi,...labda usubirie nielezee hadi mwisho ndio utaona kwanini ikafanyika hivyo..nitakufafanulia hatua kwa hatua ili unielewe, hakitaharibika kitu.’akasema wakili mtetezi, lakini mshaitakiwa akaendelea kutikisa kichwa kuonyesha hataki hata kusikiliza, na mara akasimama....

Je itakuwaje?


WAZO LA LEO: Usikubali ukatawaliwa na hasira, kwani hasira ikikutawala unaweza kufanya jambo kwa hasira ukaja kujijutia, mbele ya hasira kuna majuto. Pindi ukihisi una hasira jaribu kuwa mbali na tukio lililokufanya ufikie hapo, na muombe Mungu akuepushia na mtihani huo.
Ni mimi: emu-three

No comments :