Wakati hayo yakiendelea upande wa
muendesha mashitaka na watu wake, huku kwa mshitakiwa na wakili wake nako
kulikuwa na kikao kikiendelea, kikao cha wakili mtetezi na watu wake, naye
akijaribu kuelezea kile walichoambiwa na hakimu.
Wakili huyu, akiwa karizika na juhudi
zake, walipokuwa mbele ya hakimu,kuwa angalau hatua muhimu imekubaliwa na
kilichobakia ni kutimiza masharti ya hakimu, ambaye alitaka kuhakikishiwa kuwa
kweli, watu hao wamekutanishwa, na hakuwa anafahamu ni nini kinachoendelea
ndani kwa ndani kwa watu hawa.
Wakili aliondoka kwa hakimu akiwa hana
uhakika kuwa alichokifanya mbele ya hakimu kweli kinaweza kuungwa mkono na
mshitakiwa, tatizo kubwa ni mshitakiwa ...alifahamu kuwa ama kwa jamaa zake
wataunga mkono, kumuacha Profesa ambaye anaweza kuwa ndumila kuwili, kutokana
na mambo yake,
Wakati anawaza hilo ndipo akakumbuka pale
Profesa alipomjia kwa dakika za mwisho na kuanza kumuelezea hilo swala, ...alianza
kusema kuwa ana jambo muhimu sana ambalo kaona ni muhimu yeye kama wakili wa
hiyo kesi alifahamu, ...
‘Je linahusiana na hii kesi, na je
litaweza kusaidia, ....?’ wakili akamuuliza
‘Ngoja nikusimulie ilivyokuwa, kwa
ufupi tu, ...na wewe utaona jinsi utakavyofanya,...kwani nimeona nikikaa kimia
na hukumu ikatolewa halafu nikaja kuongea baadaye sijui kama nitaeleweka....’akasema
‘Ni jamboo gani hilo, niambie kwa
haraka maana nakimbizana na muda, kuna maswala hapa ya kufuatilia, nilikuwa napambana ili
kuitoa kesi hii kutoka kesi ya jinai iwe kesi ya madai, sasa wewe wataka
kuniambia nini ....’akasema wakili akiangalia saa yake,
Na Profesa akaanza
kuelezea ....
Tuendelee na
kisa chetu
**************
‘Ni kwanini
sasa ulipogundua hivyo kuwa huyo ni yule kijana wake, mtoto wake, kijana
uliyemlea huko ulaya, ni kwanini hukutaka kumwambia kaka yako?’ akamuuliza
‘Umuenielewa
nilivyokuelezea awali....?’ akauliza
‘Nimekuelewa,
lakini sioni sababu ya kumtokumuelezea.....’akasema na Profesa akakuna kichwa
kwani hakutaka kuliweka lengo hadharani kwa hivi sasa, na wakili akaona
anapotezewa muda, akasema;
‘Kama uliweza
kumsimulia kaka yako maisha yako yote ya huko Ulaya, na kwahiyo kaka yako anafahamu
kuwa mtoto wake ulikuwa ukiishi naye na akakugeuka na kukufanyia aliyokufanyia,.....ulitakiwa
umwambie ukweli tu,....’akasema wakili huyo
‘Nilihitajia
muda wa kulifikiria hilo zaidi, maana hadi hapo mimi na huyo kijana tulishakuwa
maadui, hatuelewani,leo mpaka kesho ....’akasema
‘Sasa kwa
hali ilivyo kwenye hii kesi, wewe huoni kuwa usipomwambia kaka yako na kunaweza kutokea
jambo baya ukawa wewe ni sababu?’ akamuuliza
‘Jambo baya kama
lipi?’ akauliza
‘Kama hili
kwa hivi sasa, umeona ilivyotokea mungu anawaonya kwa namna nyingine kuwa
mnahitajika kulisawazisha hili mapema, ....mtoto na baba yake wamafikia
kuumizana japokuwa ilikuwa siri yako, ...na sasa imeenda hadi mahakamani, hatujui
kesi itakuwaje...’akaambiwa
‘Lakini hata
mimi nilikuwa sifahamu, kuwa hawa watu wamerudi, ...na baya zaidi kuwa wao ndio
wanamiliki nyumba yangu,...sasa kaka akafika huko na kukatokea hivyo, na kwa
hali kaka aliyo nayo kama ningelimuambia, mihasira ingemzidi na huenda presha
ingempanda...humjui kaka alivyo, mimi namfahamu sana,....’akasema na kutulia
kidogo.
‘Kiukweli, nilikuwa
natafuta namna ya kuanzia, namna ambayo haitakuja kuleta ubishani zaidi hata
kaka akijua, lakini sasa limetokea hili, nikawa ansita kabisa kumwambia, kwani ...’akasita
kuendelea na wakili akasema
‘Sasa kwa
hali kama hiyo unataka mimi nifanye nini...?’ akauliza wakili
‘Mimi
nimekwambia tu...kama inaweza kusaidia kwenye hii kesi, basi fanya ufanyavyo,
ila hala hala usije kuniweka kama shahidi au kutumbukiza madai yangu ,
ikaonekana kuna vita inakuja , ionekane kuwa sisi tulifanya hivyo kwa nia
hiyo...natumai hapo umenielewa...’akasema
‘Sijakuelewa,....’akasema
wakili akiwaza jambo,..halafu akasema;
‘Nikuulize
kitu, baada ya wewe kumsimulia kaka yako yote yaliyotokea huko, je hakuna siku
alikugusia kuwa anatamani kukutana na huyo mtoto wake, wayamalize...?’
akaulizwa
‘Haikuwahi
kutokea, tunaweza kukumbukia yaliyotokea tukaongea hili na lile lakini hajawahi
kusema anatamani akutane na huyo mtoto, au hata kuulizia vipi tunaweza
kuwasiliaa na huko ulaya kuona kama anaendeleaje, yeye nahisi kwake ni kama..
hayupo..tatizo kubwa ni huko kwa mama yake....’akasema
‘Kwa mama
yake, ina maana mama yake anamfahamu?’ akauliza
‘Anamfahamu,
...ni kipindi hicho hicho ...nilipowakutanisha, lakini kijana aliwakana,...na
huyo mama nasikia kila siku ni kumtaja huyo mtoto, na nasiki siku za karibu,
amekuwa akisema yeye keshahidi kuwa mtoto wake yupo mjini,...sijui alifahamu
vipi.....’akasema
‘Mhh....unahisi
kuna mtu alimwambia huyo, mama, kabla wewe hujafahamu kuwa huyo mtoto wenu
kesharudi hapa Tanzania..?’ akaulizwa
‘Hapana, huyo
mama anahisia za ajabu, yeye haoni vyema, lakini kwa mtoto wake anamuona, hata
akiwepo kwenye kundi la watu, atasema huyu hapa ni mtoto wangu hakosei, sijui
anafahamu vipi...’akasema
‘Hilo kwa
mama tuliache kwa sasa twende kwa huyu kaka yako, je nay eye vipi kuhusu mtoto
wake, maana huyu ndiye muhusika kwenye kesi,...’akasema
‘Kaka, si
unajua wanaume tena, huenda moyoni lipo, lakini hajawahi kuhangaika kwa huyo
mtoto, na kama lisingelikuwa hili tatizo, sijui kama angekutana
naye,.....’akasema
‘Ina maana na
wewe hukujaribu kufanya juhudi zozote kuona kama mnaweza kufanya nini ili kaka
yako aje kumpokea mwanae, yaishe yaliyopita..maana ni lazima angerudi Tanzania,
sizani kama angeliweza kuchukua uraia wa huko,....?’ akaulizwa
‘Hivi kwa
hayo niliyofanyiwa huko Ulaya, hata kama ingelikuwa ni wewe ungefanya juhudi
hizo...au mkuki kwa nguruwe?’ akauliza
na wakili akakaa kimia, halafu Profesa akasema;
‘Huo ndio
ukweli ulivyo, na kwa vile mimi niliondoka huko kwa mabaya, tukiwa hatuelewani
kabisa na huyo kijana na washirika wake, sikuwa na huruma ya kuliongelea hilo,
zaidi ya chuki na kisasi, kwahiyo,.sikuwahi kumuuliza kaka zaidi kama yeye ana
mtizamo gani na mwanae, nahisi hata yeye alishamsahau,, sijui lakini, siwezi
kuusema moyoo wake...’akasema
‘Na
ulivyoongea na baba yake unahisi akija kuambiwa kuwa huyo ni kijana wake, je kuna muelekeo wowote kuwa yupo tayari kumpokea
mwanae akijirudi, akamsamehe?’ akaulizwa
‘Hilo
kwakweli sielewi, ...kama nilivyokuambia, na hata kama itatokea hivyo, yeye
akamsamehe, lakini sio kwangu
mimi...kwangu mimi kwa walichonifanyia, kutaka kuniua, sizani kama ninaweza
kukaa meza moja na huyo kijana vinginevyo....sijui ...labda aje kukubaliana na
masharti yangu....’akasema
‘Masharti
gani hayo....?’ akaulizwa
‘Masharti,!....Hayo
kwa hivi sasa sitaki kuyaweka wazi, ....’akasema na kukaa kimia
‘Kwahiyo kwa
upande wako hutaki kumsamehe huyo kijana kwa hayo aliyokufanyia, sasa
tutawezaje kulisawazisha hili, na mimi nilitarajia kuwa wewe ndiye utakuwa
msaada wangu mkubwa kwa ajili ya kulisawazisha hili jambo...’akasema wakilli
‘Unajua hawa
watu walijua kuwa mimi ni marehemu, na ndilo lilikuwa lengo lao, kwahiyo hadi
wananileta huku walishajiamini wameshinda, maana marehemu atasema nini....na ,
nina uhakika watakuwa wamewasiliana na wenzao huko Ulaya, sijui wamekubaliana
nini...’akasema
‘Sizani kama
litawasumbua sana kwa vile wewe ulikubali mbele ya wakili wako....’akaambiwa
‘Wakili wangu
au wakili wao, walimuweka ili kuweza kufanikisha mambo yao, ...mimi najua
kabisa kama wakipata taarifa kuwa mimi bado nipo hai, huko walipo matumbo yao yapo joto, hasa huyo
mama Mtemi ambaye ni mama wa huyo mke wa huyo shahidi...unaona
ilivyo...’akasema
‘Lakini hayo
ya kwako na madai yako, tuyaweke pembeni, kwa hivi sasa jifanye kabisa kuwa
umekubaliana na yaliyotokea huko, ...’akaambiwa
‘Ndio maana
nikasema ya kwangu yaacheni kando kwanza, kwani nikayachanganya na hayo ya kaka,
kama atakubali kuwa kitu kimoja na mtoto wake, mwisho wa siku tutakosana naye,
tutageuka maaduni,nikianza vita vyangu.....’akasema
‘Je
utasaidiaje hili la kaka yako, kama ikibidi,...maana huenda tunaweza kulitumia
hili kama karata yetu ya mwisho mahakamani, vipi unaweza kusaidia kwa
kumshawishi huyo kijana ili akubali kuacha hayo madai yake kwa namna
nyingine.....?’ akaulizwa
‘Ndio maana
sikutaka kwenda kuongea na huyo kijana kwanza, maana hatutaelewana naye kabisa,na
humu mahakamani angesema hayo yamefanyika kwa sababu yangu mimi, kwa hivi sasa
atakuwa hajaamini kuwa mimi nipo hai,...’akasema
‘Mimi sioni
kuwa kuna tatizo kwa ajili ya kulisawazisha hilo, muhimu kwa hivi sasa uwe kitu
kimoja na kaka yako, kwa nia ya kumweka sawa huyo kijana na unaweza kusema
madai yako unasamehe,kwa ajili ya kesi ya kaka yako ifutwe...au?’ akaulizwa
‘Madai
yangu,....niyasamehe...hahaha....,labda niwe marehemu...hilo halipo, hiyo ni
nyumba yangu, waliipata kwa ulaghai walionitungia, yeye ataiacha na nitakwenda kuishi kwenye hiyo
nyumba, wewe utaona tu...’akasema na wakili alitaka kumuuliza swali lakini
akatulia kwanza
‘Huyo kijana
kwangu hana ujanja kule walikuwa wakimtegeme mama Mtemi, hapa bongo hawaniwezi,
..na kiukweli niliwazia hilo kuwa nitumie mbinu za hadaa kuwa , mimi niende
nimshawishi kuwa yeye akubaliane kuachana na kesi ya baba yake, na mimi
niachane na madai yangu, lakini kwanini nidanganye,’ akasema kama anauliza
‘Kwahiyo sasa wewe hapo unatakaje...?’
akaulizwa
‘Ndio maana
nimekuwa kimia kuhusu maswala yangu, ....sikutaka kulichanganya hili na kesi ya
Bro....na ndio maana nilipogundua kuwa
huyu kijana ni kijana wake, sikutaka kumwambia kaka hili mapema, ili kesi yake
imalizike kwanza....’akasema
‘Je kaka yako
anafahamu kuwa ulikuwa na lengo la kutafuta haki zako , kwa mfano kuhangaikia
hiyo nyumba yako?’ akaulizwa
‘Hilo
anafahamu, lakini hakuwa anafahamu kuwa wenye nyumba ni kijana wake, hata mimi
nilikuwa sifahamu hilo, kama nilivyokuambia awali...’akasema
‘Kwa hali
ilivyo, na jinsi kesi ilivyo,...mhhh, ngoja tusubirie mapambano ndani ya
mahakama, ila nawaza jambo, kama itatokea kaka yako akahukumiwa kufungwa, au
faini, au vyote, huoni kuwa itakuwa na uhasama mkubwa sana baadaye, hasa akija
kufahamu kuwa huyo ni mtoto wake,.na wewe ulikuwa unafahamu...?’akaulizwa
‘Ndio maana
nimeona nikuambie hili ili na wewe uone jinsi ganii ya kupambana, lakini kama
kutakuwa hakuna shida, na kesi ikaenda vyema mimi bado nataka hili liwe siri,
na nije kutafuta njia ya kulitatua huko baadaye mimi na kaka yangu, wakati huo
nimesharudisha haki zangu zote....’akasema
‘Unajua kwa
hivi sasa umenipa mtihani mkubwa....’akasema wakili akikuna kuna kichwa chake
‘Najua...’akasema
Profesa
‘Nasema hivyo
kwa maana hii, kesi hii imekaa vibaya, hii kesi ilikuwa ya jinai, na nilikuwa
mbioni kutafuta njia ya kuifanya iwe ya madai ya kawaida, na nilikuwa nawaza je hata kama
ikakubalika, ikija kudaiwa mapesa mengi mtakuwa nayo..., kwahiyo hadi leo kabla
hujaniambia hilo, nilikuwa na muelekeo huo,sasa umekuja na hili jambo .....’akasema
wakili
‘Kama unaona hili
litasaidia, mtoto kujua huyo ni baba yake,
na huyo mtoto atakuwa tayari kusamehe hiyo kesi, naona tumia hiyo ajenda
mahakamani, kwa namna ambayo sitahusika, ...vinginevyo, kama hakuna ulazima
liache kama lilivyo, nitajua jinsi gani ya kuliwasha huko ,mbele kwa mbele muda
muafaka ukifika,...’akasema
‘Kwani kwa
malengo yako, maana ni ngumu, kama ulikubali hilo mbele ya wakili wako
mkasainishana, sijui...sijajua undani wake zaidi, maana sijui wewe ulipangaje,
na una suhaidi au vielelezo gani vya kuja kukusaidia, ...hebu niambie wewe
umepanga kufanya nini, ....?’ akaulizwa.
‘Unajua hilo
tuliache kwanza,...nataka watu waje kufahamu kuwa mimi sio profesa wa bure
bure,... nitakuja tuongee muda huo ukifika, kama utakubali kuwa wakili wangu,
lakini sio kwa hivi sasa, ila kiukweli, mimi sina amani na huyo
kijana,....keshanitoka, huyo ni adui yangu,kabisa.. yaani natamani muda ufike
tu , ni hii kesi ya kaka tu, inaniwekea kiwingu, ikiisha tu, napuliza filimbi
ya vita, nitapambana na hao watu mpaka
dunia ifahamu kuwa mimi ni nani....’akasema Profesa
‘Nikuulize
kitu, kama itafaa, mtoto huyo wenu akaja kukubali kuwa kakosa na yupo tayari
kumkubalia baba yake, utaendelea na madai yako hayo....?’ akaulizwa
‘Hahaha
unauliza jibu,...nimeshakuambia msimamo wangu, lakini wewe kwa jinsi
utakavyoona, ni sahihi umalizane na hii kesi, mimi na huyo kijana tutakutana mbele
kwa mbele, muda ukifika, tuombeane uzima tu, na nikuambie kitu, kuna vitu
nafuatilia, na hata siku hiyo ya kesi naweza nisiwepo au nikachelewa kufika.
Kwahiyo usiponiona, usije kushangaa, nilishaongea na Bro.......’ akasema
‘Ina maana
hutakuwepo kwenye kesi ya kaka yako, ukasikiliza nini kitakachendelea, ujue
wewe ni muhusika muhimu kwake, hasa kwa haya yaliyotokea........?’ akaulizwa
‘Nitakuwepo
kimawazo, nalifahamu sana hilo, lakini vitu hivyo ni muhimu sana kwangu,
usijali, nitajitahidi kadri niwezavyo, nifike, japokuwa nitachelewa. Kwani wewe
utanihitajia kama mmoja wa mashahidi wako, siku hiyo, sizani na naomba usifanye
hivyo....?’ akauliza
‘Sijajua
bado,.....’akasema wakili
‘Jitahidi
isiwe hivyo, nisingelipenda kuwa shahidi....’akasema
Na hiyo kesi ilikuwa
hivyo, je kaka mtu atalipokeaje hilo ombi, na nini hatima ya kijana wao , je nay
eye atakuwa tayari kukaa kiti kimoja na baba yake wayamalize....
Tukutane
sehemu ijayo,
WAZO LA LEO: Chuki, visasi haviwezi kulimaliza
jambo,kama nafsi hazitariziana... hasa mali na madaraka vinapofanywa ndivyo
kipaumbele , ugomvi wa mali, uchu wa madaraka, ubinafsi, huondoa kabisa utu na
ubinadamu. Hii inatokea pale nafsi ya tamaa, na ubifasi, inapokua ndiyo inamtawala
mwanadamu, inapofikia hatua hii usitaraji amani, usitaraji upendo,
Inapofikia hatua hii basi ndugu kwa ndugu wanakosana, wanauana kwasababu ya mali na madaraka, jamii hazitapendana, nchi kwa nchi zinaingia kwenye vita kwasababu ya
mali na madaraka. Ili kupambana na haya
yote, tukumbuke jambo moja, je ukiyapata hayo yote utaishi milele, ...!
Je wewe ni wa kwanza, ..je wangapi
waliondoka na mali na madaraka yao,hakuna, sasa kama ni hakuna wewe unataka nini.....?
Tukumbuke mwanadamu kaja hapa duniani na kila mmoja ataondoka hata iweje, hata uwe nani, na kwanini basi usifikirie huko tunapokwenda tutakuwaje....utaenda kukutana na nini, na hii mali uliyoichuma hapa duniani, au madaraka uliyokuwa nayo hapa duniani, ?...
Au wewe ni wale wasiamini hilo kuwa kuna maisha mengine baada ya haya...wewe unaamini kuwa
ukifa ni basi tu....kama huamini kuwa kuna maisha mengine baada ya haya, basi
wewe huamini kuwa mungu yupo, na hiyo ni hatari, ,... tuweni makini , tujirudi kwani muda tunao
Ni mimi:
emu-three
1 comment :
Great website you have here but I was wondering if you knew of any user discussion forums that cover the same topics talked about here?
I'd really love to be a part of community where I can get advice from other knowledgeable people that share the
same interest. If you have any suggestions, please let
me know. Thanks!
Post a Comment