Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeTuesday, November 17, 2015

RADHI YA WAZAZI-54‘Nimesema huyo sio baba yangu, huyo sio baba aliyenizaa mimi, msiwasikilize hawa watu  ni matapeli, ni waongo muheshimiwa hakimu .....’ilikuwa sauti ya shahidi wakati hakimu alipowataka mawakili atete nao.

Na kwa muda huo hakimu hakimtilia maanani kwani alishawaita mawakili na kwa muda ule walikuwa wakielekea  mbele kukutana na hakimu, hata wakili muendesha mashitaka hakutaka kumtuliza shahidi wake, akafuata amri ya hakimu.

Na mawakili walipofika mbele ya hakimu wakaanza kuongea,...maongezi yao yaliichukua muda kidogo tofauti na ilivyotarajiwa  kuwa ni maongezi mafupi ya hakimu kuonya au kutoa maelekezo fulani au kupata ufafanuzi fulani, ikawa ni mabishano ya pande mbili, lakin hatimaye wakamaliza maongezi hayo,

Baadaye mawakili hao walirejea kwenye nafasi zao, na hakimu akasema;

‘Nimeongea na mawakili wa pande zote mbili na kutokana na unyeti tukio hili kwenye hii  kesi ...kesi hii inaiharisha hadi siku nyingine itakayopangwa....’akasema hakimu na kugonga kirungu chake, na kesi hiyo ikaahirishwa,

Tuendelee na kisa chetu

                                                **************

Kesi iliahirishwa, watu wakaanza kutoka kila mtu akiongea lake, mawakili wakawa wamesimama kwenye nafasi zao, na kila mmoja akiwaambia watu wake wasiondoke kwanza.
Wakili mtetezi akasogea pale alipokuwa mshitakiwa kabla hajasimama kuondoka, akamnong’oneza sikioni, na mshitakiwa akasimama na kutembea kumfuata wakili huyo , na wengine wakafanya hivyo hivyo hivyo.

Kundi hili likawa limesogea mbali kabisa na kundi la muendesha mashitaka ambaye naye alikuwa na watu wake , wakionekana kuongea mambo yao.

Na ilionekana kuna ujumbe mnzito kutoka kwa hakimu , ujumbe ambao ulitakiwa ufanyiwe kazi na mawakili hao kila mmoja na watu wake, na kutokana na umuhimu wake, mawakili hao walikuwa wakihakikisha watu muhimu hawaondoki, wakawa wanamsogelea kila mmoja aliyeoneka kutakiwa kwenye ja,mbo hilo

Na kwa muda ule shahidi, aliyekuwa akitoa ushahidi wake muda mchache uliopita, alionekana kuwa na haraka ya kuondoka  na kwa jinsi alivyoonekana ni kama hakutaka kuongea na mtu, usoni alionekana kukasirika, kinyume na walivyotarajia watu wengine ..

Wengi walitarajia kuona tabasamu au namna ya kutahayari kwa kile kilichotokea, kwani mtu huyo alikuwa kamgundua mzazi wake ambaye alikuwa hamfahamu labda ingeonekana dalili ya yeye kujikurubisha kwa baba yake, na hata kuomba msamaha, lakini dalili hiyo haikuonekana kabisa!

Shahidi huyu hakutaka hata kumuangalia mshitakiwa, akatoka ile sehemu ya mashahidi na kuanza kutembea akielekea mlangoni, lakini kabla hajakatisha sehemu walipokuwepo muendesha mashitaka na kundi lake, akasimamishwa na muendesha mashitaka..

‘Usiondoke kwanza kuna mambo muhimu ya kuongea na wewe...’akaambiwa na muendesha mashitaka, akamwangalia muendesha mashitaka kwa uso uliojaa hasira, akasema;

‘Mambo gani ya kuongea, ....kama ni kuhusu huyo mzee, sitaki kusikia lolote, na hata hii kesi naiona haina maana tena, badala ya kunisimamia ukamshinikiza mshitakiwa naona umemuacha wakili wao kunisakama tu, ....mimi sitaki tena , amueni mnavyotaka, sitaki kabisa ,, .....’akasema akitaka kuondoka

‘Nataka niwaambie alichoongea muheshimiwa hakimu, ni muhimu sana, na huwezi kuondoka mpaka usikie maagizo hayo.....’akasema muendesha mashitaka

‘Kwanini, kwani ni lazima, .....?’ akauliza na alipoona muendesha mashitaka kakaa kimia akasema

‘Sawa,.... haya sema ni mambo gani, hakimu kasema nini....?’ akauliza na muendesha mashitaka akaendelea kukaa kimia,  kama vile anatafakari jambo

‘Muheshimiwa,  msimamo wangu ni huo huo, kama ningelifahamu mapema kuwa ni hawa watu, sijui kama ningefika hapa, lakini nimetii amri ya mahakama tu....’akasema akilalamika

‘Hawa watu ni watu wakorofi,  mimi nawafahamu sana, na nijuavyo huyo anayeitwa Profesa alishafariki, nashangaa kusikia kuwa bado yupo hai,....nahisi hawa watu ni mapacha, nina uhakika yule Profesa ninayemfahamu mimi ni marehemu, kuna mchezo unachezwa hapa, sielewi...huu ni ubabaishaji ,...’akasema na muendesha mashitaka akawa anatoa ishara wengine wa upande wake wasogee pale waliposimama.

‘Huyo profesa ndio huyo huyo hakuna mwingine...’akasema wakili huyo

‘Una uhakika gani, mimi namfahamu maana niliishi naye, na alirejeshwa huku nchini akiwa mahututi hajiwezi, na ....aliambiwa hatamaliza wiki, na watu waliomleta walirudi wakisema walimuacha akiwa anakata roho......’akasema

‘Na zaidi ikaletwa taarifa kuwa ameshafariki...niliambiwa na watu wenye uhakika mpaka watu  wakawa wakionana na mimi wananipa pole ya msiba...’akasema

‘Ni taarifa zisizo na ukweli, kwanini hukuaniambia kabla,..nikaweza kulifuatilia kwa undani....’akasema wakili huyo

‘Nikuambie kitu, sikujua kuwa ni hiyo familia, sasa nimejua kama kweli ndio wao wenyewe, muheshimiwa unatakiwa uwe makini hao watu ni matapeli, waongo,...’akasema akimuangalia huyo wakili.

‘Ndio maana nataka tuongee, nijue chanzo cha haya yote, ilikuwaje, ....na mwisho tuje  tukubaliane na kuna mambo zaidi niweze kujua la kufanya kabla hatujaedelea zaidi...ila kwanza ni muhimu tuhakikishe tunalimaliza hili...’akasema

‘Mimi sioni kama kuna zaidi.....kesi iendelee hao watu wawajibike...ili mimi niishi kwa amani....hili lililojitokeza halina msingi kwangu kabisa...’akasema

‘Halina msingi kwako,...? akauliza wakili kwa mshangao

‘Ndio,....’akasema kwa kujiamini

‘Aaah, ngoja kwanza, unajua alipotuita muheshimiwa hakimu, alilichukulia kuwa wewe kwako itakuwa kama mshituko kama kweli ulikuwa huwafahamu hao watu kuwa ni familia yako, kwahiyo ni vyema tukakaa tukalimaliza hili, na huenda hilo likaleta faraja, na haya mengina yakawa hayaa maana tena, ila kuna sababu ya kutoa adhabu kwa mkosaji, lakini hilo lije baadaye,..kwahiyo mimi nataka nikusikie wewe unasemaje.....’akasema.

‘Mimi naona hakimu,...simuelewi.....’akataka kuongea jambo lakini akakatisha.

‘Hakimu kachukulia hekima zaidi, ...hili jambo limemgusa yeye kama mzazi, ....mwanzoni kama muendesha mashitaka nilijitahidi kulipinga nikisimamia kwenye kosa lenyewe, kwani nilikuwa na vigezo vyangu, lakini ilifika sehemu nikaona kweli kuna haja ya kuliangalia hili jambo kwa macho mawili.....’akasema akimuangalia huyo shahidi

‘Jambo gani...? wakati msingi wa kesi hii ni vurugu, kujeruhi, je hayo hayakufanyika, ushahidi haupo?, kuna jambo gani zaidi ya hilo...muheshimiwa mnataka nini zaidi?’ akauliza akionyesha kushangaa

‘Ndio kuna kesi hii ipo mikononi mwangu, lakini bado nina hisia zaidi ya hii kesi, wakati mwingine kunatokea jambo kati kati ya kesi, na kuleta maulizo mengi, na hapo unatakiwa utumie hekima zaidi,....’akasema

‘Hekima! .....una maana gani kusema hekima itumike, ? ina maana hekima ni zaidi ya sheria au...?’ akauliza shahidi huyo

‘Kwenye kesi hii lilipojitokeza hili jambo, wengi tulishikwa na mshangao, unajua hukuaniambia hili kabla...sasa alipoliongelea muheshimiwa hakimu nikana kuwa haja kweli ya kupata uhakika,...kutoka kwako....’akasema

‘Uhakika....! uhakika upi?’ akauliza kwa mshangao,

‘Ndio ni lazima kwanza nipata uhakika kutoka kwako, jinsi gani ulivyolipokea hili, ikizingatiwa kuwa huyo ni mzazi wako, na inaonyesha wewe ulikuwa humjui,,....limekuja kama jambo la kushitukizia, kiukweli, mimi  limenigusa kama mzazi, hata hakimu imekwa hivyo hivyo, japokuwa hajaongea moja kwa moja,...’akasema na shahidi akabakia kimia

‘Ndio maana imenibidi  niwasikilize , sio kwamba nimekubaliana na upande wa utetezi, hapana, ila hili kwanza liwekwe sawa, ili tufanye yaliyo sahihi,...kisheria kwa upande mmoja lakini pia kiubinadamu kwa upande mwingine...’akasema muendesha mashitaka na shahidi huyo akawa kama katahayari, akasema;

‘Kwahiyo unataka kusema nini muheshimiwa...., ina maana na wewe unakubali kuwa aliyoyafanya huyo mzee ni sahihi, kuja kuleta vurugu, kuumiza watu, kwa vile tu ni .....ni mtu mzima, kwa vile tu imekuja hiyo hoja, huoni kuwa wamekutega, huoni kuwa lengo lao ni kupoteza muda, ,..?’ akauliza

‘Sijasema kuwa alichokifanya ni sahihi, hili kisheria lipo pale pale mtenda kosa hata awe nani, sheria itafuata mkondo wake, ...’akasema

‘Sasa ni kwanini...ni kwa vile imesemwa kuwa yeye huenda akawa ni baba yangu, ....huo ni uzushi tu, haina ukweli, ni utapeli tu,, kwanza mimi sijakubaliana na hilo kuwa yeye ni baba yangu.... je ndio hilo unalotaka kuliongelea au?’ akauliza kwa mshangao

‘Kwanza unielewe, sijasema kuwa hakuna kosa, alichofanya mshitakiwa ni kosa, ikihukumiwa hivyo mbele ya mahakama, na ndio maana baada ya kujirizisha kuwa mshitakiwa atakuwa katenda kosa nikaamua kuisimamia hii kesi, ...’akasema

‘Si ndio hivyo, basi kwanini mnagwaya kuchukua hatamu, kwanini hakimu anaipiga hii kesi kalenda, kama kashindwa tunaweza kuomba hakimu mwingine mimi sina muda wakuja kupoteza hapa, nina kazi zangu, nina mambo mengi kweli kweli,ya kufanya......’akasema

‘Nikuulize swali,....wewe umejisikiaje ulipoambiwa huyo ni baba yako?’ akaulizwa

‘Vibaya sana, nimejiskia vibaya sana...nikuambie ukweli, nilitamani nitoke pale kizimbani nikimbie,...sikufahamu kuwa hili jinamizi linazidi kuniandama...’akasema

‘Kwanini...?’ akaulizwa wakili huo akishangaa

‘Kwasababu....ni hadithi ndefu...siwei kukuambia ila hayo ya nyuma achana nayo tugange haya ya sasa hivi....huyo mzee aah...’akasita kidogo na muendesha mashitaka akasema;

‘Ndio maana sisi kama mawakili, tumeliona hili kwa namna nyingine kuwa pamoja nah iii kesi kuna mambo yamejificha ambayo tusipoyatatua kwanza tukakimbilia kushindana kisheria na kimahakama tunaweza kuleta mtafaruku mkubwa huko mbele, ....’akasema

‘Kwa vipi, na wakati kesi ipo wazi..’akasema

‘Limejitokeza hili swala, katikati ya kesi, na sisi kama wazazi,limtugusa, tukaona ni swala linahitajika kusawazishwa kwanza, kwa mustakabali wa mahusiano mema kati ya mzazi na mtoto..’akasema.

‘Mimi sikuelewi hapo, hilo la .... linahusiana vipi na uvunjifu wa sheria,....?’ akauliza

‘Wewe ulikuwa humfahamu mzazi wako sio...?’ akauliza wakili

‘Hahaha, hivi nyie watu vipi, ina maana mnafumbia macho shera kwa vile umeambiwa huyo ni mzazi wangu, na hata hujalithibitisha hilo, hivi wewe muheshimiwa hilo ndilo liharibu kesi ya msingi, hapana, mimi siwaelewi, kwanini,......?’ akauliza

‘Ndio maana nataka kusikia kutoka kwako, ukweli wote ulionao wewe....usilichukulie hili jambo kwa mzaha, hili ni jambo nyeti sana, pamoja na ya kuwa kuna uvunjifu wa sheria, lakini....’kabla hajamaliza shahidi huyo akadakia na kusema;

‘Unaona eeh, mimi nahisi umeongea na hao watu wamekuweka sawa useme,wanavyotaka wao, au sijui umewaogopa hao wazee, unaogopa kulogwa, au.na hakimu mbona simuelewi, hawa watu vipi,....mimi nataka haki yangu...na nilitaka hili jambo limalizike kwa amani, lakini kwa hali hii, ...ndio maana sikutaka kuja hapa, ‘akasema

‘Kwahiyo wewe unatakaje....?’ akauliza wakili

‘Ninatakaje...!?...unaniuliza hilo swali mim tena,..hohoho....!’ akaliza kwa mshanga

‘Ndio, ....nakuuliza hivyo nikiwa na maana, ...nilijua utabdili mawazo baada ya kusikia hivyo, na nilijua utafurahia sasa hili swala tulimalize hivi kimazungumzo zaidi ,yaani  wewe mje mkae na baba yako, muelewane, yaishe yaliyopita, huoni ni furaha kwako, umemuona baba yako ambaye ulikuwa humfahamu..’akasema wakili

‘Kweli wewe unazungumza hivyo, wewe mwenyewe uliniambia hii ni kesi ya jinai,sio kesi ya madai, mkosaji katenda kosa bay asana...leo hii unaongea mengine, ...kuna kitu gani kinaendelea...?’ akauliza kwa mshangao

‘Unielewe kijana....’akasema wakili na shahidi huyo akamkatisha na kusema

‘Unasikia muheshmiwa, mimi sitakubali, .....nataka huyo mzee awajibishwe,afungwe...kwa kosa alilofanya,.....iwe fundisho kwa wazee kama hao....’akasema

‘Oh, siamini, kuna nini kati yako na huyo mzee,...kwani ulikuwa unamfahamu kabla, ina maana haata kama ni baba yako...mzazi, upo tayari afungwe?’ akaulizwa

‘Nani kasema huyo ni baba yangu...sio baba yangu huyo, hao ni waongo kabisa..na kwani hakufanya kosa...’akasema

‘Nahisi hapa hujakubali kuwa ni baba yako mzazi au sio, Je ikidhihiri kitaalamu kuwa huyo ni baba yako mzazi utasemaje...?’ akaulizwa

‘Utaalamu kwa vipi...muheshimiwa mimi sikuelewi,....?’ akaulizwa

‘Kuna vipimo vya kulithibitisha hilo..kuthibitisha kuwa huyo kweli ni baba yako mzazi.’akaambiwa

‘Unasikia mimi sitakia kabisa kupimwa, maana moyoni najua huyo ni baba yangu, ..hata kama mtapima, mpime ili iweje,..kinachotakiwa ni nini, vipimo au moyoni mwangu. Najisikiaje kuhusu hao watu, niwaambie ukweli, vyovyote mtakavyofanya mnajisumbua,..’akasema

‘Nikuulize kwanini hutaki, kwanini humtaki baba yako,..niambie ukweli, ili nijua cha kufanya, maana mimi ni muendesha mashitaki, ni haki yako kudai fidia, ni haki yako kama umetendewa kinyume na sheria, sheria ichukue mkondo wake, kuna nini hujaniambia....?’ akauliza

‘Kila kitu nimeshakuambia,..hawa watu ni wakorofi, sasa hivi wananitishia amani, wanadiriki kusema kama nisipoondoka kwenye hiyo nyumba nitapata mabaya.....nikajua kumbe lengo lao lao sasa ni nyumba!, ...sasa unaona ilivyo, kwahiyo nikilogwa tu nikakubali tu kuwa hao ni wazazi wangu, watakuja na ajenda nyingine ya kudai nyumba,mimi naona mbali ....’akasema

‘Nakuuliza tena hili swali, je upo tayari kumuhukumu baba yako aende jela,...hata kama umethibitisha kuwa kweli huyo ni baba yako mzazi?’ akaulizwa

‘Kama kafanya kosa sheria ichukue mkondo wake, sheria haingalii baba au mtoto, au sio, nimekosea hapo,...? Ukitenda kosa uwe baba au mtoto utahukumiwa ipasavyo, wewe ni wakili unalifahamu hilo, au sio.?...sasa kwanini mnataka kupindisha sheria...’akasema

‘Unajua kwanini sisi tumefikia hatua hiyo, ni kuwa wewe ulikuwa huwafahamu wazazi wako, na mzazi wako alikuwa hakufahamu,...limetokea hili ambalo linaweza kuleta uhasama mkubwa, kwa mzazi wako kuja kujenga chuki dhidi yako,...sasa tukaona tuking’ang’ania sheria, haya tusema huyo mzee afungwe, unafikiri ni nini kitafuata baadaye, si chuki, visasi, na wewe hutakuwa na maisha mema, hili nakuambia kiukweli,....’akaambiwa

‘Hahaha...wewe ni mtu wa ajabu sana, siamini, hivi sheria zina makengeza....hapana siamini,....mimi nadai haki yangu, nimetendewa makosa halafu nimefuata sheria, tena mimi nije kusha maisha yasiyo mema, mlitaka nichukue sheria mikononi mwangu au....’akasema akitikisa kichwa kwa kushangaa

‘Ni kweli sheria ipo, na ni kweli sikutakiwa kuangalia hilo,...kuwa ni nani kafanya kosa,... ila hili tunaweza kulisawazisha kwanza, kuhakikisha kuwa wewe unamtambua baba yako,...halafu baadaye tutaangalia sheria inasemaje,....’akasema

‘So what....’ akauliza.

‘Ili kuondoa chuki kwenye familia,  ili wewe na familia msije kuwa maadui wakubwa...wewe ni mtoto, huoni ni jambo la ajabu sana kugombana wewe na mzazi wako, halafu uje umfunge,  hii ni hatari, sio vizuri, unaweza ukapata matatizo makubwa sana....’akaambiwa

‘Matatizo makubwa kama yapi, kwani mimi nimekwenda kuleta fujo nyumbani kwake...? mimi nina kosa gani, niambie, kwani mimi nimekwenda kudai kuwa niwe mrithi wa mali yake, , ..sijafikia au kufikiria hivyo,...’ akasema

‘Sio hivyo unavyofikiria wewe....’akasema wakili

‘Sio hivyo, sasa wanataka nini kwangu,,..nikuambie kitu, nimehangaika mwenyewe na maisha yangu hadi hatua hii unayoiona ninayo,...nimefika ulaya kama chokoraa, sina baba wala mama, wasamaria wakanilea,....wakanisomesha, ..  sikumuona baba wala mama,leo hii kwa vile....muheshimiwa, mimi nawastahi sana, lakini anyway....’akasema akitaka kuondoka

‘Sikiliza wewe ni sawa na mtoto wangu, nikuase hili,..nafahamu wewe hujui mazara ya haya yote, ni bora ukubali kwa hivi sasa, hata kama moyoni mwako haujaridhika kuliko kukataa moja kwa moja,...nikuambie ukweli utayaona maisha ni magumu na utawatafuta hao wazee usiwaone utakuja kujuta wakati umeshachelewa.....’akaambiwa

‘Watafanya nini, wataniloga,...kwani hawajavuna sheria muheshimiwa,hata Mungu halioni hilo,... hebu acha imani potofu hizo wewe ni mwanasheria hukumu kutokana na vipengele vya sheria mambo mengine niachie mimi mwenyewe, ..kama maisha magumu kwani itakuwa mara ya kwanza, nimelelewa na nani....’akasema

‘Sikiliza nahisi wewe hujaamini kuwa huyo ni baba yako, tunahitaji tulithibitishe hilo kitaalamu....unasemaje..?’akaambiwa

‘Kwa vipi?’ akauliza

‘Tutachukua damu yako tupime na huyo mzee, tuone kuwa kweli ni baba yako na kama sio baba yako hapo tutajua kweli familia hiyo ni ya matapeli...watafungwa wote....unasemaje kuhusu hilo....?’akaambiwa

‘Mchuke damu yangu, hahaha.....hilo halipo na sitaki kabisa...na ili iweje kwenye sheria za makosa kama hayo kuna kipengele kama hicho, kuwa ikitokea mtoto kamshitakia mzazi, kwanza ithibitishwe ...kuwa kweli ni mzazi wake, ipo hiyo....’ akawa kama anauliza.

‘Ndiyo ili tuweze kulithibitisha hilo, huoni na wewe litakusaidia ili uwe na maamuzi yenye kujirizisha, ni kweli siku hizi watu wanaweza kutunga uwongo tu kwa masilahii ....nakubaliana na wewe,sasa ili sote tujirizishe ngoja tufanya hivyo....’akasema huyo muendesha mashitaka

‘Nafikiri hujanielewa, na naona hamtanielewa, ninachoona ni mimi kuondoka zangu,....nina mambo mengi ya kufanya siwezi kukaa hapa tukipoteza muda tu, ni nini tutakipata hapa baada ya  haya yote hapa, ...’akaonyesha mikono kama kukata tamaa

‘Hataupotezi muda kabisa ni jambo jema na hili tunalifanya kwa nia njema kabisa....’akasema

‘Tunapoteza muda kabisa hapa,....hebu nambieni, kuna faida gani hapa, kama nyie watu wa sheria hamtaki kutimiza wajibu wenu,.... ndio maana tunazidi kuwa na watu wakorifi, magaidi kwa vile nyie watendaji mnawalea tu...., kuongea kuongea,, ...inanisikitisha sana, ..’akasema akigeuka huku na kule kama kutaka mtu wa kumuunga mkono

‘Nielewe kwanza....’akataka kuongea huyo wakili

‘Kosa limefanyika lipo wazi, ...hamtaki kuchukua hatua,...we are wasting our time for nothing, men, am faded up....mimi sasa naondoka zangu.....’akasema na kuanza kuondoka

‘Subiri, hii ni amri ya mahakama, ni muhimu unatakiwa kutii amri hiyo,  tuna mambo ya kukamilisha kabla hujaondoka, ni lazima tuhakikishe tumekubaliana hili jambo, ili tuwesze kumwambia muheshimiwa hakimu tumafikia wapi,.....’akasema wakili

‘Mambo gani hayo,ya kukubaliana wakati nyie mnanilazimisha, mimi sijakubaliana na nyie, na sitakubali kwa hilo, kama mnataka iwe hivyo mtakavyo nyie, kupotezea hilo kosa, na haki yangu ipotee hivi hivi, mimi sipo na nyie kabisa, mkitaka kuamua nyie kwa ubabe wenu, fanyeni, lakini sio kusema mimi nimekubaliana na nyie hapana....’akasema

‘Kijana, ....mimi siwezi kukulazimisha kuwa ukubaliane na mawazo yetu, sisi tuliona labda tufanye hivyo, ili kuwaunganisha kwa nia njema, wewe na baba yako ambaye ulikuwa humfahamu,..kumbe hutaki.’akasema muendesha mashitaka

So what.....?’ akauliza

‘Tulijua labda kwako itakuwa ni faraja kumpata mzazi wako,..kumbe wewe hutaki, hutamki mzazi wako,..inashangaza sana,..’akasema wakili akitikisa kichwa

‘Nakuuliza ili iweje, ..kama sheria imevunjwa na ni kosa kwanini tufumbie macho, ..hivi ina maana gani ya kupoteza siku zote hizo mhakamani, gharama muda, ...hilo mbona hamliangalii, ningelikuwa na uwezo, ningewaondoa tuweke watu wenye kujua wajibu wao..’akasema

‘Sikiliza kijana  kama wewe hutakubaliana na wazo letu hilo basi, sisi tutatimiza wajibu wetu, na mwamuzi ni hakimu, kama mzazi wako atapatikana na hatia, basi atafungwa,na halikadhalika kama itakuwa kinyume chake, sheria itafuata mkondo wake,na wewe utawajibika vile vile, ...’akasema

‘Sikuelewi muheshimiwa ina maana sasa wewe unageuka kuwa mtetezi wa huyo mshitakiwa au...niambie ili nijue ...kama itakuwa kinyume chake kwa vipi, kwani hakufanya fujo, hawakumjeruhi mtu, kwanini unazungumza hivyo, kunitishia au....’akasema

‘Nakuuliza tena, je upo tayari.mzazi wako afungwe....maana sitapenda baadaye yatakayotokea niwe wa kulaumiwa,...?’akaambiwa

‘You know, sizani kama tutaelewana hapa, ..am sory, mimi naondoka.....’akasema huyo shahidi na kuanza kuondoka, na wakili huyu muendesha mashitaka akawa anatizama upande wa pili alipomuona mama mmoja akiongea na wakili mtetezi, akawa anakumbuka mama mmoja aliyeonekana na matatizo ya macho akiwa kaongozana na binti mmoja, akaikumbuka ile sauti yake ikisema.....

‘Muokoeni mwanangu....ifuteni hiyo kesi kwani inaweza kuleta matatizo makubwa ....; kipindi hicho alikuwa na haraka na kesi nyingine hakuweza kumsikiliza zaidi, leo anamuona pale akiongea na wakili mtetezi

‘Huyu anaweza pia kuwa ni mama yako mzazi, je mama yako mzazi naye humfahamu,...’ akauliza kumbe alikuwa akiongea peke yake, kwani shahidi yule alishaondoka
‘Wewe...rudi hatujamalizana.....’ alikuwa keshachelewa

                                                       ************

Wakati hayo yakiendelea upande huo, huku kwa upande wa mshitakiwa na wakili wake napo kulikuwa na maongezi kama hayo yakiendelea, wakili mtetezi alikuwa akielezea kile walichoongea na hakimu; na sasa alikuwa akiongea na mshitakiwa, ambaye sasa tumegundua kuwa ni mzazi wa shahidi.....

‘Je mzazi huyu atasemaje baada ya yote hayo yaliyotokea.....

Tuishie hapa, tutakuja kuona upande huo kulitokea nini, na je mama atasaidia nini...,


WAZO LA LEO: Hekima inaweza kuwa msaada mkubwa kwenye majanga mengi ya mifarakano inayotokea hivi sasa duniani, kuliko vita na kumwaga damu...na mara nyingi imeonekana kuwa kiini cha matatizo mengi kakipewi kipaumbele, kinachoangaliwa zaidi ni tatizo lenyewe, ubabe, na masilahi. 

Na wakati mwingine matatizo hutengenezwa ili ubabe uchukue nafasi yake kwa masilahi ya wenye hisa! Tunasahau kuwa Hekima  na busara ni silaha njema kwa muafaka wa kudumu kwenye matatizo yoyote, kuliko kutumia ubabe na minguvu ambayo hujenga chuki na visasi visivyoisha.

Ni mimi: emu-three

No comments :