Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeTuesday, November 3, 2015

RADHI YA WAZAZI-51


Baada ya taarifa ya wazee kurejeshwa kijijini, wanafamilia walikutana kabla profesa  kwenda kuonana na wakili

‘Bro hali ndio hiyo, sasa tufanyeje, kwani hata wazee wenzako naona wamekasirika kabisa......?’ aliuliza Profesa

‘Kama wamekataa tufanyeje sasa, iliyobakia sisi tutakutana huko mahakamani,......’akasema kaka mtu

‘Kaka umekiuka sheria, na mahakamani sio sehemu ya kuonyeshana ubabe, ni sehemu inahitajia sheria , kiujumla umekosea, hata iweje, kinachotakiwa ni kutafuta njia mbadala....’akasema

‘Njia gani mbadala, kama wameamua kutumia pesa yao, waache wafenye hivyo,...au ulitaka mimi niseme nini...?’ akauliza

‘Kuna swala waligusia wazee, kuwa wewe kama unaweza uende ukaongee nao, uwaombe msamaha,.....huenda hilo litasaidia...’akasema

‘Unasema nini, mimi niende kuwaomba msamaha hao watu, kwa kosa gani, wewe hukuwepo wakati huyo mlinzi anatoa maneno ya kashfa,. Ungelisikia huyo jamaa tena ni kijana mdogo tu, sidhani kama ni ...anatamka maneno ya kashfa mbele yangu, halafu niende kumuomba msamaha, mimi....’akatikisa kichwa

‘Ndio njia inayoweza kusaida bro.....’akasema

‘Halafu mlinzi na huyo bosi wao wananichangia kunipiga,....ole wao ...sikuwa na cha kujitetea, ...na sasa wao wanaonekana hawana hatia mimi ndio mwenye hatia, nilitakiwa nikae kimia wakinitukana , wakini dhalilisha....’akasema

‘Bro wewe ulikuwa kiongozi wa kijiji, je watu wakija hapa wamepigana, ulikuwa unawaamuliaje?’ akauliza Profesa na kaka mtu kwanza alitaka kutokujibu hilo swali lakini baadaye akasema;

‘Inategemea maelezo ya kila mmoja wao, nawauliza kila mmoja kwa wakati wake na tunatafuta ni nani mwenye hatia,....maelezo yao yanasaidia kujua chanzo cha tatizo,....ndio maana mimi sina wasiwasi hakimu atasikiliza chanzo cha tatizo, atajua kwanini mimi ilifikia hadi kuchukua hatua hiyo. Mimi sio mwendawazimu, .....’akasema

‘Bro....chanzo cha tatizo hakiwezi kukubalika kama wewe ulichukua sheria mkononi mwako, kupiga na kuumiza,....hilo halitakubalika mbele ya sheria....’akaambiwa

‘Najua, ...nafahamu kuwa pale hasira zilinizidi, najua kwa namna fulani nina makosa lakini nisingeliweza kukaa kimia,....’akasema

‘Kosa jingine ulikubali hivyo mahakamani...kuwa ulifanya makosa hayo....’akasema

‘Kibinadamu hata ingelikuwa wewe ungelichukua hatua niliyochukua, watu wengine wana majibu yanye karaha hasa wanapokuwa kwenye kazi zao, maofisini mwao....na nlisema ukweli mahakamani, ....’akasema

‘Hapo sasa bro ndio uliharibu, maana kama ulikubali kuwa kuna kosa, ulimpa nafasi hakimu kutafuta adhabu gani akupe, na adhabu ya makosa kama hayo ni kifungo na faini....’akasema

‘Nisingelidanganya,....ulitaka nisemeje kuwa sikufanya,.....’akasema

‘Ok, bro, sasa.... unasemaje kuhusu hilo swala la wewe kwenda huko mjini, ukaongee nao, uwaombe msamaha, ili haya maswala kama yawezekana yaisihie kienyeji....’akaambiwa

‘Mdogo wangu hilo mimi siwezi kulifanya, siwezi kuomba msamaha kwasababu sina kosa, acheni nifungwe,...halafu nilikuuliza yule mwenye nyumba sura yake ni kama naifahamu, ni nani yule, ni kijana mdogo,...sijui nilimuona wapi...’akasema

‘Hilo la kumfahamu halitasaidia kitu kwa hivi sasa....na kama unamfahamu basi itakuwa ni wakati mnzuri, mkaongea mkafahamiana na kuombana msamaha....’akasema Profesa akimuangalia kaka yake kwa makini

‘Hahaha, unajua ni kuambie kitu, ...kuonana nao sio tatizo, tatizo najua itakuwa majibu na lugha yao, hatutaelewana,...nimekuambia wao wawili walinichangia kunipiga, ungelikuwa walivyokuwa wakifanya, walikuwa kama wanaua nyoka,..wanaiga bila huruma,....’akasema

‘Huyo sijui ndio mwenye nyumba, akapiga mateke mbavuni niliodondoka, na yeye ndiye kasababisha mbavu zangu kuachana...anaonekana ni kijana mdogo japo anaonekana na mwili , unajua siku hizi vijana wanahumuka tu,...halafu akatamka maneno ya kashfa ambayo sitaweza kumsamehe hata awe nani.....ndio maana sitaki kuonana naye tena....’akasema

‘Maneno ganii?’ akauliza

‘Alisema mijitu hii yenye sura mbaya , inafanana kama michwawi ya kwenye sinema, inakuja kuleta uchuro kwenye nyumba yangu, sitaki kuiona tena, ....’akasema

‘Oh, angelijua,...lakini bro, ujue na yeye alitamka hivyo kwa hasira , hata kama ingelikuwa wewe umeingiliwa kwenye nyumba yako ungeliweza kutamka chochote...’akaambiwa

‘Kwahiyo wewe unakubaliana na kauli yake hiyo kuwa mimi ni mchawi , ndio nina sura mbaya kwa vile mimi ni mzee, lakini uzee sio jambo la kuomba, na imekuwa hivi kwa sababu ya maisha magumu, je huyo mtu yeye hana wazazi....?’ akauliza

‘Alitamka tu kwa hasira....sijui, atakuwa nao, na ...hajui tu kuwa wewe waweza pia kuwa mzazi wake....’akaambiwa

‘Na je kauli kama hiyo haiwezi kumpandisha mtu hasira...hahaha, siwezi kuwa na mtoto kama huyo asiye na adabu, ...huyo, hapana, nakuuliza hivi kauli kama hiyo kweli haiwezi kupandisha mtu hasira?’ akauliza

‘Inaweza ndio lakini....’akataka kusema neno na kaka akamkatisha

‘Kama yeye alidiriki kutamka maneno hayo bila kusikiliza upande wangu bila kufahamu kuwa mlinzi wake aliumia kwa jiwe alipodondoka,...ulitaka mimi nikae kimia’akasema

‘Yeye alipofika tu akaanza kujiunga na mlinzi wake bila kusikiliza upande wangu, yeye alisikiliza kauli ya mlinzi wake na wote kwa pamoja wakaanza kunichangia kunipiga, ulitegemea mimi nikae kimia wanipige tu....’akasema

‘Bro yule ni mlinzi alikuwa kazini, ....’akasema na kaka yake akamkatisha

‘Sikiliza mimi sitaki kuongea tena, utazidi kunipandisha hasira, tusubirie mahakama itamua, mimi nitaelezea ilivyokuwa, na hakimu naye ataelewa, na kama ataamua kunifunga hewala.....basi ...’akasema kwa hasira

‘Basi ngoja mimi niende kuonana na wakili nitamuelezea ilivyokuwa na yeye ataona jinsi gani ya kufanya.....’akasema

‘Wewe fanya utakavyo, lakini mimi siwezi kwenda kuonana na hao watu, eti kuwaomba masamaha, wameshanishitakia, wamesababisha hadi hali yangu imekuwa hivi, mimi  katika maisha yangu unanifahamu nilivyo....’akatulia

‘Kawaida mimi sipendi kabisa kuzalilishwa, hata kama ni umasikini, hata kama ni uzee, hata kama ni nini, hayo ni maisha yangu, wanafikia kusema eti familia yetu ina matatizo, magonjwa ..sijui....yanawahusu nini wao...hilo sitalivumilia, kwahiyo kama ni kwenda, nenda wewe mimi siwezi kwenda kwa hao watu,...’akasema kaka mtu

‘Bro, wewe subiria nikirudi nitakuwa na jibu muafaka, kama itabidi kwenda kuonana na hao watu, itabidi tufanye hivyo,...ila kiukweli kwa mimi kuwaona hao watu, kwangu mimi siwezi inatakiwa kaka ni wewe ujitahidi uende, sio mimi,  ikibidi utakwenda...., lakini nina imani haya maswala tutayamaliza tu, hata ikiwa ni huko huko mahakamani...’akasema

‘Sawa...maana yote hayo ni kwasababu yako, na kwahiyo, ....inabidi nikuachie wewe, siamini kuwa katika umri huu ningeingia jela, nilikucheka siku ile ulipokuwa unanihadithia kisa cha maisha yako, nilikuona wewe ni mjinga...sasa leo yamenikuta mimi...nawekwa ndani kwasababu, hata...’akasema kwa uchngu

‘Bro ndio ujue dunia ilivyo,..usije hata siku moja ukamcheka aliye chini yako, kwa vile wewe upo juu, ...hujafa hujaumbika...’akasema

‘Mimi sikukucheka kwa hilo, nilikucheka kwa hayo uliyoyafanya..’akaambiwa

‘Amabayo na wewe umekuja kuyafanya pia....’akasema

‘Mimi nimefanya yaliyo sahihi, wewe ulitenda makosa, ...mimi nimetenda makosa gani....? akauliza

‘Si ndio hayo hayo, makosa ni makosa sio lazima yawe madogo au makubwa, sio lazima yawe niliyotenda mimi na uliyotenda wewe, kama kisheria yatathibistishwa ni makosa, ujue ni makosa tu.....’akasema

‘Wao hawajatenda makosa, wao hawajachukua sheria mikononi mwao, ....walishirikiana kunipiga, watu wa usalama wakanipiga ni virungu miguuni hadi nikaathirika mifupa, mimi na uzee huu nagongwa kwenye vifundo vya miguu, wanatarajia nini, si kunimaliza...docta kathibitisha kuwa mifupa ya miguuni imeathirika, kwa virungu vya hao watu, ubavuni kwangu, mbavu zimeachana kutokana na kipigo cha hao watu mlinzi na bosi wake...sasa hakimu aniambie kama wao wanaruhusiwa kuchukua sheria mikononi mwao.....’akasema

‘Kama mimi nina makosa na wao wanayo, kama mimi hakimu atanihuku, ahakikishe na hao watu kawahukumu....’akasema

‘Lakini wao walikuwa wakitimiza wajibu wao....’akasema

‘Ni kweli hilo halitaonekana kuwa mimi nilizalilishwa , bila kujali uzee wangu, kwa vile wao wanauwezo, kwa vile hayo nyalifanyika kwenye sehemu yake ya kazi, najua yeye atasilizwa zaidi, japo alitoa matamshi ya kunizarau....najua inapofikia hapo watu wanasahau kuwa kuna kauli nyingine huumiza zaidi ya matendo,...’ akasema

‘Lakini bro yategemea hayo yamefanyikia wapi, wewe ulikwenda kwenye makazi ya watu, na yule alikuwa kazini hapo ndipo utashindiwa, ...’akaambiwa

‘Najua ....walifaya hivyo wakifahamu hivyo, kuwa wapo kwao, wanitukane wanizalilishe,  wameniiga wakaniumiza hilo halionekani tena.....lakini ...’akatulia

‘Ndio hivyo bro, walikutega kihivyo, wakijua kuwa wao hawatakuwa na hatia usikimama kisheria,....wana elimu wana pesa,...’akasema

‘Wapo juu eeh.wana elimu eeh,....wanahisi kuwa kukaa juu ni milele, kuwa na madaraka ni kuongoza milele, huyo mlinzi kapata kazi basi anajiona kafika,kweli masikini akipata.....anatusahau hata sisi walala hoi wenzake,  hajui yale madaraka ni ya miuda tu ipo siku watashuka chini ,...hata kama ni ile siku yao ya mwisho....’akasema kaka  mtu

‘Bro , yote hayo ni sawa, lakini kwa hivi sasa tuangalie sheria itatusaidiaje...mengine hayatasiadia kitu, tutabakia kulalamika tu, na ili kuyafahamu hayo, mambo ya sheria, itatusaidiaje inabidi tuhangaike, tutafute wajuzi wa washeria, waliosomea sheria,..tatizo bro,i tunahitajika pia tuwe na pesa,.....kwahiyo ngoja nikaonane na mwanasheria....’akasema Profesa

‘Haya wewe nenda kwa huyo wakili wako, kama una pesa za kumlipa..mimi sina kitu, hali yenyewe ndio hiyo unaiona, .....wamenimaliza kabisa....mimi hapa nilikuwa kiongozi niliweza kuhukumu, kusuluhisha watu wakaishi kwa amani na sheria za asili, sikwenda shule ya sheria, leo hii inafikia kwangu unatafuta watu wa sheria eti waliosomea sheria,...haya nitafanya nini ...’akasema kwa uchungu

‘Ndio hivyo bro.....’akasema

‘Nilikuwa na nguvu zangu, nilikuwa na uwezo wangu wa kujitafutia riziki yangu kwa mikono yangu mwenyewe sasa ninageuka kuwa omba omba,...wamenifanya niwe hivyo, hilo halitaonekana tena kwa vile mimi ni mnyonge....’akazidi kusema kwa uchungu

‘Lakini bro wewe ndio uliowaanza, wewe hulioni hilo....’akaambiwa

‘Mimi ndio niliowaanza, wakati nilikuwa nakutafuta wewe, kwanini hawakukubali ombi langu angalau wakanisikiliza , kwanini wakimbilie kunikashifu,....oh, hata kuinuka sasa shida, wamenivunja miguu yangu....wamevivunja mbavu zangu, ....wangeniua kabisa basi....’akazidi kusema

‘Bro, ...’akataka kuongea lakini kaka yake akamkatisha na kusema

‘Sasa sikiliza, ukifika huko, umwambie kabisa huyo wakili wako msomi, mimi sipendi nije kurejeshwa jela,..na kama itatokea hivyo tena...ikitokea kuwa nimehukumiwa eti kwenda jela,.., eti wanihukumu kifungo,aah, sijui... sizani kama watanifikisha huko jela nikiwa mzima....watafikisha maiti yangu....hisia zinanituma hivyo.....aah sijui...’akasema kaka mtu na Profesa akamuangalia ndugu yake akimuonea huruma.

‘Usijali bro, haya tutayamaliza tu, niachie mimi.....’akasema Profesa na kuondoka, huku akilini akijiuliza hata kama atampata huyo wakili atamlipa nini, maana wakili anahitajia pesa, na pesa hana, hata kama anamfahamu vipi, ndio alikuwa rafiki yake, lakini uwakili ni kazi yake haweze kuifanya kazi hiyo bure!....

‘Ngoja nifike huko kwa huyo wakili,....ikishindikana, bro, oh, sijui ‘akasema na akilini akawa anawaza jinsi gani anaweza kuificha hiyo siri,....akajikuta akisema

‘Nitakuwa sina jinsi inabidi niiweke siri hii hadharani....’akasema

‘Siri gani na wewe, hebu ondoka mimi nilale, najisikia vibaya, hapa moyo unanienda mbio kwa hasira.....’akasema kaka mtu

*******

Basi Profesa akafunga safari kwenda mjini, huko akakutana na huyo wakili rafiki yake wakati wa wakiwa shule ya msingi,,..., akamuelezea jinsi tukio lilivyokuwa, na alipofika mwishonii wakili huyo akasema

‘Hiyo kwa macho ni unaweza ukasema ni kesi ndogo tu,...hiyo sio kesi ndogo,hasa inaofika mahakamani...’akasema

‘Najua hilo....si unajua tena hali zetu ndio maana nikaja kwako....’akasema

‘Huyo ndugu yako kavamia makazi ya watu, jaokuwa alikwenda kwa nia njema, akampiga mlinzi, akamjerehi, hapo nia njema yake yote inaonekana kuwa ilikuwa kwa nia njema, wao watajenga hoja kuwa alidhamiria...baya zaidi akapigana na mwenye nyumba,...hiyo ni kesi kubwa..sio kesi rahisi,...’akaambiwa

‘Ni hasira za kaka, na inategemea jinsi gani mlinzi alivyomjibu, kuna majibu mengine yanakera hasa unapogusia hali mtu aliyonayo, ukamnyanyaaa, hata hali hiyo ni ya weli lakini kauli nyingine zinakera, zinaumiza sasa yategemea uhimili wa mtu...’akasema Profesa

‘Hata kama alizalilishwa,....akatukanwa....hakutakiwa kuleta fujo,...na hakutakiwa kumgusa huyo mlinzi kabisa maana yule alikuwa kwenye kituo chake cha kazi, akitimiza matakwa ya bosi wake..kwahiyo hiyo ni kesi kubwa , inahitajia umakini katika utetezi, na hata tufanyeje, hapo gharama haziepukiki,...unahitajika uwe na pesa nyingi, ili niweze kufuatilia kila kitu..’akaambiwa

‘Pesa nyingi ya nini...unajua nimekuja kwako wewe kama rafiki yangu, umbuka tulipotoka, unakumbuka nilivyoweza kukufanyia yale mambo yako nilipokuwa ulaya,....’ akasema

‘Hizo ni gharama za kawaida, kufungua jalada lake, kuna gharama natakiwa kuzilipia, ili kukata rufaa, kwani sikudanganyi, kwa vile alishakubali kosa, kinachofuata ni hukumu, na hukumu hapo ni kifungo na faini,...alikubali kiharaka, ndio tatizo la kutokuwatumia mawakili....’akaambiwa

‘Rafiki yangu sisi ni masikini hatuna kitu....’akasema

‘Ujue, kesi ilivyo, kaka yako ana makosa, alikubali kuwa kweli alifanya hayo makosa mahakamani, si ndio... kwasababu zake, kuwa alichanganyikiwa, nk, lakini huwezi kuchukua hukumu mikononi mwako, hilo ni kosa...kaka yako.atafungwa!...’akaambiwa

 ‘Ina maana hakuna njia ya kuimaliza hiyo kesi nje ya mahakama...?’ akauliza

‘Unielewe vyema hiyo ni kesi ya jinai, ..hii sio kesi ya madai, na imeshafikishwa mahakamani, kwahiyo kuimaliza kwake ni mahakamani,...na ili ifikie hadi hakimu akubali maombi hayo, ni hao waliofanyiwa hivyo, wafike mahakamani, ....’akasema

‘Kwani...’profesa akataka kuongea lakini wakili huyo akasema

‘Kesi ikiwa ni jinai ina maana ni serikali inayoiendesha, ,...sio hao wahusika,,..hata kama hao waliotendewa hivyo watasema kuwa wamesamehe, hayo ni yenu tu, lakini maamuzi makubwa yanategemea jinsi gani mtakavyo mshawishi hakimu....’akasema

‘Kwahiyo haiwezekani kulimalizia hili tatizo nje ya mahakama.....?’ akauliza

‘Sijasema haiwezekani,....lakini je ni jinsi gani ya kumshawsihi hakimu, mna maelezo gani, ya kuweza kumshawishi hakimu, labda nikuulize wewe na hao waliotendewa hilo kosa mumeshaongea na kuelewana...?’ akaulizwa

‘Mhhh tumeongea nao, wazee walitumwa, wakaongea na hao watu,...lakini hakuna ushirikiano, hawataki, ... wao wanadai hiyo kesi haipo mikononi mwao, kwahiyo hawawezi kusaidia lolote, ndio maana nikaona nije niongee na wewe, ili nipata ushauri wako....’akasema

‘Inavyoonyesha mpaka sasa hampo kwenye maelewano na hao watu, au sio....?’ akauliza

‘Sasa tufanyeje....?’ Profesa akauliza kabla hajajibu swali la wakil

‘Kwa kuweza kujenga hoja za kumshawishi hakimu, ni muhimu  mkaongee na hao wahusika,waliofanyiwa fujo, ili hata tukipeleka hayo maombi,ya kuomba kesi hiyo ya madai .na tutafute maelezo ya ziada ya kujitosheleza,...kitu ambacho bado kina ugumu, lakini kwanza hakikisheni mumelewana na hao watu....’akatulia kidogo.

‘Je wewe mwenyewe umeshaongea na hao waliofanyiwa na umeona kuwa wanaweza kuwa tayari kutoa ushirikiano,...?’ akauliza

‘Bado...kwanza nimekuja nije kwako kupata ushauri....’akasema

‘Ni vyema ukaongea na hao watu, wakubali, na wawe tayari kutoa ushirikiano, bila wao huwezi kufanya lolote...kwani wao wataitwa kama mashahidi, waliotendewa....’akasema

‘ Mhh hapo sasa ndio inakuwa shida,....sijui kwa hilo utanisaidiaje, wewe huwezi kwenda kuongea na hao watu...?’akauliza Profesa akimuangalia huyo wakili na wakili bila kusita akasema;

‘Wewe ndiwe unatakiwa ufanye hivyo, uende ukaongea, nao .... muelewane....,  huo ndio ushauri wangu,...’ akasema wakili akiangalia saa yake.

‘’Mimi niongee nao...mmmh hapana, siwezi....kuna sababu za msingi zinanizuia kuongea nao kwa sasa....’akasema na wakili akasimama kuashiria kuwa keshamaliza,

‘Sababu gani za msingi,.....’akasema wakili akimuangalia Profesa, na Profesa akasimama, sasa akitaka kuondoka.

WAZO LA LEO:  Ufumbuzi wa jambo lolote, lenye utata, hauwezi kutatuliwa, na kufikia muafaka wa kudumu, iwapo WASULUHISHI, au WASIMAMIZI  watakuwa na masilahi na hilo jambo. 

Ni mimi: emu-three

No comments :