Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeTuesday, August 4, 2015

RADHI YA WAZAZI-28'Mimi ndio mgeni wako...' sauti ikasema, 

‘Tcha tcha..tcha, siamini, wamekukamata Mpendwa, hahaha,...siamini eeh... natumai ulikuwa unanisubiri kwa hamu kukutana na yoyote, au sio,nilkuambia mpendwa ipo siku...’akasikia suti ikipenya akilini, ikimtesa moyo wake.

‘Hahaha...... nimeshafika profesa, usiwe na shaka...hahaha, geuka unikaribishe mpendwa, umeona eeh,....’akawa anaongea kwa sauti kama vile alitaka kila mtu asikie.

‘Mhh, ...nikuambie kitu, huu ni mwanzo tu,  ...na natumai sasa unatakiwa uanze kuhesabu siku zako....hahaha,..’ akaendelea kuongea kwa sauti na profesa alisimama vile vile, hakutaka hata kugeuka kumuagalia huyo mgeni.

‘Hebu geuka kwanza, unatakiwa unipokee mgeni wako, hapa nimekuletea chakula kidogo,matunda kidogo, na maji kidogo  ili uikumbuke dunia kuwa kuna watu wenye upendo na huruma, sio nyie mashetani mkianza kudai pesa hata mtu akilia vipi, hamjali, hamuwaonei wenzeu huruma, ....’akazidi kuambiwa

‘Shetani kama nyie hamstahili kuishi kwenye jamii ya wastaarabu, huko kwenye gereza la kifo ndio mahali penu,....’akasema

‘Sasa nimekuja mimi ninayelijua hilo gereza ambalo watu kama nyie ndio mnastahiki kwenda, na nikuambie ukweli mimi ndiye mtu peke yake aliyewahi kuingia na kutoka salama.....hahaha....’akatulia

‘Na usalama wagu ndio huo...unajuza zaidi,...au nikuambie tu, maana hata nikikuambia itasaidia nini, ...maana wewe ulifikia hatua ya kupekenyua maisha yangu na kugundua kidogo, ....nakupa tu kama angalizo, kuwa hata kizazi changu kilipotea huko huko.....unasikia sana....hahaha, sasa uongeze hilo kwenye mambo yako ya kuni-blacmail....

‘Kuna watu walinisulubu hadi kunitoa kizazi huku naona....damu zinanitoka, na walihakikisha hakuna kilichobakia ndani, nikapoteza fahamu kwa siku saba, nikijulikana kuwa nimeshakufa,...unasikia wewe sheteni......’akasema

‘Sasa hayo yalikuwa yanatokea huko kwa upande wa wanawake, huko kwa wanaume...ni zaidi mara kumi ya hayo ya wanawake, kama hujawahi kupata hata mtoto wa kusingiziwa basi ujue ukitoka huko, wewe sio mwanaume tena, unakwenda kuwa sio riziki...hahaha....

‘Huku kuna kila aina ya unyama na mwingine hujawahi kuusikia duniani,....kuna mijitu mikatili haijawahi kutokea,...mijitu hiyo haijui maisha ya duniani yapoje, ina tikteti za kifungo cha maisha.....hahaha

‘Huko watu hao, wanaamini kuwa, damu ya mfungwa mpya inaongeza umri, wa kuishi, kwahiyo ukifika tu, damu yako inakuwa kinywaji chayo, sasa wataipata vipi utajulia huko huko gerezani....hahaha.....nilikuambia sasa unaona eeh, hahaha...’akacheka saana.

‘Siwezi kukuambia yote maana mengine ni siri ya huko, siruhusiwi kutoa siri za huko maana ni siri za jandoni, ukifika utajionea mwenyewe.....’sauti ikazidi , profesa alihisi mwili ukimuishia nguvu.

‘Sasa sikiliza nimekuja kukuona....najua kuwa wewe ni mwanaume, na mjanja, najua una akili ya kuwaza mambo, ndio maana ukaitwa profesa, sasa kama uliitwa kiutai, basi utakuja kuumbuka,...unasikia....mimi nataka kukusaidia....’maneno hayo aliona ni kama utani.

‘Mimi nataka uongee kiume, kama  upo tayari mimi naweza kukusaidia, kwani najua hatari unayokwenda kuikuta, na zaidi mimi nafahamu wapi ni wapi utakapoponea....’maneno hayo yalimfanya profesa aingiwe na uhai, akaweza kutikisa kichwa, lakini hakugeuka, akihisi ni utani, au ni mtego.

‘Najua utahisi nakutania, lakini ukumbuke kuwa mimi nakudai, sasa ukifungwa maisha nitapatia wapi pesa zangu, ndio nikaona nije nikusaidie, ili niweze kupata deni langu, umenielewa hapo...’akasema na hapo profesa akajua kuwa hilo linawezekana huenda ni kweli.

‘Kwahiyo mimi nimeongea na mkuu wa gereza, akasema yote inategemeana na wewe, lakini kwa kiasi kikubwa inategemeana  na hao waliokushitakia, lakini kuna mambo ambayo yeye yapo ndani ya uwezo wake, ...na hayo ndio anayoweza kukusaidia, unielewe hapo.....’akasema

‘Sasa hayo yaliyopo ndani ya uwezo wake anaweza kukusaidia, hasa ikitegemeana na wewe....’akatulia

‘Lakini ...japo hajasema, na hawezi kusema akiwa humu, si unajua tena,... tu,..kunahitajika pesa,...’akatulia

‘Najua kwako pesa sio tatizo,...pesa unazo nyingi tu....na pesa ni nini, ukilinganisha na maisha yako, hebu fikiria hiyo taabu ya huko gerezani, na hao kesi haijatajwa,na hujui utasubiria muda gani, ....pesa ipo utatafuta nyingine lakini uhai wako huwezi kuupata tena ukifa umekufa, ukiumizwa umeumizwa, ukiambukizwa maradhi ndio basi tena....’akaambiwa

‘Kwahiyo mimi nikamuelewa, nikaona nije nikusaidie kwa hilo, na kusaidia kwa vile bad nakudai, lakini vinginevyo, wewe hustahili kukaa kwenye jamii ya wastaarabu,...nikuambie ukweli mimi niliwahi kupitia huko, lakini ...naapa siwezi kurejea tena huko...siwezi ,ni bora kufa....’akasema

‘Sasa najua bad hujaamini hatari iliyopo mbele yako, ...unasubiri, kwanza uonje adhabu ya huko, na watu hawaamini mpaka wafike, na hutaamini mpaka siku hakimu anagonga rungu kuwa umehukumiwa kifungo cha maisha ya kuua....’akasema

‘Mimi sijaua....’akasema profesa

‘Mimi sijui hujaua,au umeua, tatizo ni kuwa wewe huaminiki, ..nikuulize wewe hufanyi biashara ya mlungula, hujaniblackmail mimi...si ulikana mpaka ushahidi ukapatikana, ..na unajau kuwa kwenye kazi kama hizo kifo kipo nje nje,...

‘Na ukumbuke watu wakiona pesa, au yule aliyefanyiwa hivyo akiona hakuna njia nyingine unafikiri atafanya nini, na ni nani aliyesababisha hayo kama sio wewe.....umeua, sasa  ni kuua kwa namna gani....

‘Mimi sijaua, nilifika na kukuta huyo jamaa keshapigwa risasi....’akasema profesa

‘Hahaha, hayo wanaongea sana, na usipoteze muda wako kuniambia mimi ilivyokuwa ,mimi sio wakili wako,subiria aje wakili wako, na hilo ni jambo jingine nataka kukushauri, kuwa unahitajia wakili, na wakili awe kweli wakili...’akasema

‘Nitampataje na mimi nipo hapa ndani...?’ akauliza

‘Nilijua wewe ni mjanja, ina maana mpaka sasa hujatafuta wakili, hahaha, wewe ni profesa gani, kesi kama hii unahitajika kuwa na wakili, na tena wakili kweli....’akasema

‘Nitampataje, na mimi nipo hapa,....sina mtu wa kunisaidia,..nilikuwa naumwa sana, nimepona tu nimeletwa na hapa,na...na...’profesa akajikuta analia

‘Hahaha, ...unalia,....unalia profesa simaini...’akasema huyo mama sasa akimsogelea profesa akamshika mgongoni kama anambembeleza

‘Mhh, pole sana...lakini sasa unaona uchungu wake au sio, hujui ni kiasi gani nilivyolia mimi, kiasi gani ulivyowatesa watu pale ulipowapigia simu na kuwaambia kuwa una au kuna mapicha mabaya, una siri mbaya au vyovyote ulivyosema...unakumbuka hayo

‘Mtu akisikia hivyo, na huenda alifanya huenda ana tatizo kama hilo, kwanza anapata shinikizo la damu, wewe hapo unatishiakuwa  kuwa unataz hizo siri, na ukizitoa, huyo mtu ataumbuka, hebu fikiria jinsi gani mtu huyo anavyoshituka, anavyoumia moyo wake ....

‘Na isitoshe, unamzidishia kwa kudai mapesa mengi,..mtu anaumia, hajui afanyeje, ....analia anateseka akijua kuwa hayo yaliyotokea labda sio hiari yake....humuonei hata lepe la huruma unachotaka wewe ni pesa tu...’akasema

‘Wewe unazidishia chumvi....watu kama hao wana pesa, na huwa ni kweli wamefanya hayo machafu, kwanini walifanya  hayo machafu kwa namna nyingine ilikuwa njia ya kuwapiga vita kwa mabaya yao....achana na mimi , kama umekuja kunikoga ....unaweza kuondoka tu...’profesa akasema

‘Kuwapiga vita kwa machafu,...mimi nilikuwa na machafu gani...hahaha unajifanya  unalia,...siamini, wewe ulie,...au ndio huko kuigiza kwako...sasa unalia wakati, hujaenda huko kwenyewe, hahaha, ...siamini...’akawa anajaribu kumchungulia profesa lakini profesa hakukubali kugeuka kuangaliana na huyo mama

‘Profesa, profesa....kumbe ujanja wa bure, sasa nikuambie ukweli, ndugu yagu, hujalia,..utalia sana, utalia hadi chozi la damu litakutoka, ...kwa hali ilivyo, hakuna atakayekuonea huruma.....’akasema kwa sauti ya chini kidogo

‘Unajua jinsi gani watu walivyoumia,....wanaumia,hawana raha...wewe hukuwahi kuwaonea huruma, ...roho mbaya iliwatawala, ....wewe ulijali tumbo lako, ulijali masilahi yako, ukaona kuwa unachofanya ni kutetea masilahi yako,....wajiona wewe mjanja,  hukujali wengine..hukujali familia zao,.....sasa ni zamu yako, na hiyo bye bye....hilo nakuhakikishia...’akasema

‘Sijaua na haki ipo najua haki ipo,....’akasema profesa

‘Haki ipo, kwani ni uwongo, kwani hujafanya hiyobiashara ya mlungula, na sasa umeua...haki kwako wewe tu, wengine hawana haki, mlijiona wajanja hamtakamatwa....mwenzako naye nasikia keshakamatwa....’akasema

‘Mwenzangu nani...?’ akauliza

‘Unamfahamu sana,....yeye anajifanya mjanja wa mitandao....za mwizi ni arubaini, sasa ujue upo kivyako, kila mtu anajitetea kivyake, hapo hakua ujanja....’akasema

‘Wamemkamta ...mta...a....’akasema profesa akishindwa kuamini.

‘Hili zoezi lilishapagiliwa na wenyewe....usicheze na polisi,...ndugu yangu, kila jambo baya lia mwisho wake, ...karne ya ujanja wenu imeshapita,...na mwisho wa ubaya ni nini....’akawa kama anauliza na profesa akawa katuliatu

‘Sasa ndugu yangu, mimi nataka kukusaidia, na msaada wangu ni huo,...nipo tayari kukusaidia ilimradi kuna uhakika wa pesa,... mambo mengi ya kufanya yanahitaji pesa, na sio pesa ndogo,...pesa nyingi...’akasema

‘Pesa nitaipata wapi na mimi nipo hapa jela...?’ akauliza

‘Hiyo pesa mliyochukua kwa huyo jamaa kutoka India ipo wapi, ...hiyo ndiyo itakusaidia, vinginevyo, acha uumie, acha ufe na hiyo pesa itapatikana na wewe muda huo utakuwa wapi kama sio kaburini....’akaambiwa

‘Pesa ipi hiyo ,.... mbona haipo, mbona sikuwahi kuichukua, sikuupata kabisa huo mzigo,...aah, unazidi kunichanganya.....’akasema profesa akishika kichwa.

‘Wewe ndiye unayejua wapi hiyo pesa ilipo...hilo linajulikana wazi, huwezi kunidanganya mimi...’akasema huyo mama.

‘Najua huniamini mimi, lakini  wewe ndiye utakayesemani nani akaichukue hiyo pesa,kwangu sio shida,...ila ni kwa vile pesa inahitajika, ...nakudai sana....lakini kwanza muhimu kuna haya mambo yanayohitajia pesa kwa ajili yako....’akasema

‘Hujanielewa, na sijui kwanini watu hamunielewi, sikuwahi kuuchukua huo mzigo...sijui hiyo pesa ilipo....’akasema

‘Wewe uliingia, na hakuna mtu aliyewahi kuingia humo kabla yako, kamera zinaonyesha...umetoka ukiwa umeshikilia mzigo, ukiyumba yumba kama mlevi, sijui ulikuwa unaigiza ili uonekane umelewa, umeonekana kabisa...’akasema huyo mama na profesa akaguna

‘Mhh, kamera...nani kasema....?’ akauliza

‘Sasa hilo la kamerahalijafika kwa polisi, ni siri tu nakudokezea, ...na hilo linaweza kukusaidia, kama kweli hukutenda...kitu ambacho,...naamini ....japo sijaiona hiyo kamera,....kiukweli umeua, ..hao jamaa wanasema kweli umeua, ila wao wanaweza kusaidia maana polisi walivyo, watakuja kuipata hiyo kamera....’akasema

‘Kwenye lile jengo hakuna kamera, mimi nina uhakika huo.....’akasema profesa

‘Hahaha umeona eeh, kumbe ulikuwa unadhania kuwa hakuna kamera,....wenzako walikutegea, waliwahi kuweka hiyo kamera....hahaha, pesa kama hiyo kila mtu alikuwa na mbinu zake...ndugu yangu upo matatani...umeua, wanasema inaonyesha wazi...’akasema huyo mama

‘Ni nani hao,waongo, mimi sijaua....walete hiyo kamera tuone, ....kama ipo ndio itasaidia kuonyesha ukweli ulivyokuwa..’akasema profesa

‘Sasa sikiliza tusipoteza muda...unaye wakili, unazo pesa za kumlipa....?’ akaulizwa

‘Sina wakili wala sina pesa....’akasema

‘Sasa hizo pesa ndio zitumike, najua wewe huwezi kuruhusiwa kutoka, wewe huwezi kutaja wapi pesa zilipo,...hata kama ingelikuwa mimi nisingelitaja, maana huo ndio mtaji wako wa baadaye, lakini kunahitajika pesa....’akasema

‘Unajua ....hutanielewa....’akasema profesa

‘Nitakuelewa tu, niamini mimi...kesi hii ni mbaya, utaenda kufia jela, ...., mimi sihitaji kuichukua mimi hizo pesa, una watu unaowaamini, sema ni akina nani, ili waje wakuone uwaelekeze, ili pesa hiyo itumike, uweze kuokoka kwenda hilo gereza la kifo, hicho ndicho muhimu kwa sasa ....gerezani ni lazima uende, huwezi kukaa hapa kwa kesi ya mauaji,....hilo halina ujanja, sasa ni gereza jipi, ndio hapa nataka kukusaidia.....’akasema

‘Lakini mimi sijaua mtu,...hilo unielewe, wewe mwenyewe unajua fika mimi sijafanya hivyo, hilo mumefanya mbinu ili nifungwe, ...’akasema

‘Aaah, usinihusishe kabisa ....nifanye mbinu ili iweje, mimi nakudai pesa nyingi, ukifungwa nitazipata wapi,....hebu fikiria hapo, mimi sihusiki kabisa kwa hilo, ila nilijua kabisa kwa kazi kama hiyo ipo siku itafikia haya, watu wanakuchukia, watu wamejenga uadui na wewe......’akasema.

‘Watu gani zaidi yako wewe....’akasema

‘Mimi najua jinsi gai ya kukubana, sihitajii kukufanyia hivi....mimi nimeshabadilika, siwezi kujiingiza kwenye mambo haya, ila nilikuwa tayari kuwasaidia watu ili watu kama wewe wasiendelee na matendo haya machafu, lakini sio kwa mtindo huu, wa kuua, mtu asiye na hatia, hapana ,hapa sasa mumevuka mpaka....’akasema

‘Mimi mnanionea bure, mnajua kabisa mimi siwezi kuua mtu, hiyo sio fani yangu kabisa ....’akasema profesa kwa sauti ya huruma.

‘Mhh, sijui, maana kama walivyonambia, wameshakamilisha ushahidi wote,.... nimeulizia, nimefuatilia, nikitaka kujaribu kukusaidia, lakini kwa jinsi ilivyo, huna ujanja...wewe umeua, sasa sijui ilikuwaje,...ni kwanini uliua, yule jamaa wa watu ana kosa gani, alikataa kukupa hizo pesa au ilikuwaje....’akawa kama anauliza

‘Mimi sijaua,...na wala sijui aliuliwaje, na nani alifanya hivyo....’akasema profesa.

‘Najua labda, ...ulikuwa unajitetea,...au ulitaka kuzichukua hizo pesa peke yako,...au ilikuwaje, ...mmmh, ni kesi mbaya sana kwako, hata kama ni kwa kujitetea au kwa vipi hilo utaongea na wakili wako, ....mimi nilichokuja kukuambia ni hicho....’akasema

‘Muda umekwisha...’sauti ya askari ikasema kutoka mlangoni.

‘Nambie wapi hiyo pesa ilipo,....au ni nani unamuamini ili aje umuelekeze mahali hiyo pesa ilipo, ili hiyo pesa ikafanye kazi ,..kesi hii iahitajia wakili mahiri,...wapo mawakili nawfahamu, au, kama yupo unayemfahamu niambie ni  nani, si unaliona hilo, sasa ....sema haraka mimi naondoka zangu....’akasema

‘Mwambie kijana wangu aje....’akasema

‘Kwahiyo niongee na mkuu wa hapa ili afanye mipango au sio hilo tumekubaliana ...ujue mimi nachukua dhamana hapa,.....hapa hakuna longo longo, ukidanganya unajua utakalofanywa, mimi nitakuwa nimeosha mikono yangu....’akasema huyo mama sasa alikuwa haongei kwa sauti kubwa, kama ilivyo kawaida yake.

‘Mwambie kijana wangu aje asubuhi sana...’akasema kwa sauti ya kinyonge

‘Sawa,...nitafanya hivyo, nikijua kuwa utamwambia wapi hizo pesa zilipo, ili huyo kijana akitoka hapa akazichukue hizo pesa, nitaongea na huyu mkuu atafute mbinu za kukuchelewesha usilepekwe huko gerezani,...

‘Lakini pia hizo pesa zisaidie kumlipa huyo wakili wako,  na pia tuweze kuwalipa wahusika mbali mbali...ujue hili halipangwi na mtu mmoja, kuna wahusika wengi,..natumai umenielewa.....’akasema huyo kwa sauti ya chini kama ananong’ona.

‘Ni jambo gumu sana....lakini nitajua jinsi gai ya kumshawishi... huyu mkuu hapa ili aweze kutafuta mbinu za kila namna ili hata kama..... wewe uweze kubadilishwa gereza, na ujue hilo ni la haraka, na yote yanahitajia pesa, ...’akasema huyo mama sasa akiongea kwa lugha ya chini sana.

‘Sawa....’Profesa akatamka hivyo, huku kichwani akiwaza jinsi gani ya kumuambia huyo kijana, maana kiuhakika alikuwa hajui kabisa hizo pesa zipo wapi, kinyume na inavyoeleweka kuwa yeye anajua pesa hizo zilipo, yeye ndiye alizichukua,....

‘Hivi hizi pesa alizichukua nani,.....’akawa anajiuliza wakati akirudishwa kwenye chumba chake, akiisubiria hiyo kesho....

WAZO LA LEO Toka lini aliyezoea dhuluma akatosheka, na kila siku ataona alicho nacho hakimtoshi, hata kidogo alicho nacho mwenzake atataka awe nacho. Lakini tukumbuke za mwizi ni arubaini, na huwezi kuwahadaa wengine kila siku, ipo siku uwgo wago utadhihiri tu, na ndipo utakapokuja kuumbuka, jirekebishe wewe mwenye tabia hiyo maana dunia hii ni mapito tu
Ni mimi: emu-three

No comments :