Profesa
aligongana na mtu, na kupepesuka, mtu aliyemgonga alikuwa mgumu kama chuma, na
athari za kuogangana naye zilimuacha akiwa na maumivu mwili mzima, hajawahi
kuhisi hivyo baadaye....
Mtu yule
alikuja kuvua mawani, baada ya kusema ‘Oh... am’ sory....’ na ndipo Profesa akamgundua ni nani....
Na kauli
yake aliyoitaja mwishoni kabla hajaingia ndani ya kibanda cha simu ilimfanya
akumbuke kitu,
‘Its you again...’
Tuendelee na
kisa chetu
*************
‘Its you again...’
Hii kauli aliisikia wapi vile, akajaribu kukumbuka ....ohoo akakumbuka, ....
Ni siku ile
walipokuwa wakisaidiana kumbeba yule jamaa wanayemla pesa za mlungula,...ndio,
aliisikia siku ile,
Ni siku ile
pale yule jamaa alipozidiwa na ulevi! Alikumbuka kabisa kusikia hiyo kauli siku
ile, lakini aliyesema hivyo alikuwa ni mtu mwingine kabisa alikuwa ni ni muhudumu
wa ile hoteli, anakumbuka vyema kabisa , sio huyu jamaa aliyekutana naye
akiingia kwenye kibanda cha simu....
Sasa iweje,
kauli ile ile, sauti ile ile, sasa imetokeaje kauli hizo zifanane, ni bahati tu
imetokea hivyo,...
Alikumbuka
kabisa kusikia kauli hiyo na kwa sauti hiyo hiyo, ni baada ya jamaa kuzidiwa na ulevi, na yeye ndipo alipojitokeza akiwa
amevalia sare za humo ndani, alifaya hivyo ,makusudi,...na hapo ndipo akaanza
kuongea na mdada wa mle ndani;
‘Mhh, huyu
jamaa vipi, mbona yupo hivyo,kalewa kupitiliza nini ...?’ akauliza na yule
kwanza akamtupia jicho, halafu akasema;
‘Watu
wengine bwana, wanajifaya wanajua kulewa, kumbe ovyo, angalia kanywa kiasi gani
mpaka afikie hali hii, mimi hata sijui tumfanyeje....’akasema mdada
‘Hebu
nimwangalia vizuri, mmmh huyu si yule jamaa yangu, anayekuja kunywa kunywa hapa,
akitaka wasichana warembo wamzunguke kama mfalme,...mmh leo vipi kazidiwa eeh,
na imekuwaje, mapaka saa hizi bado hajaondoka,mmh mdada ulitaka kumtoa pesa
nini....’akasema
‘Nilimuomba
tuje kuywa naye kidogo huku juu, sasa kumbe hakuzoea kunywa zaidi,kajifanya
anaweza kunywa ..unaona alivyo, wewe, wewe...unaoa alivyozidwa,.....’akasema
akimtikisa tikisa huyo jamaa, na jamaa likuwa kinyosha mkono kama anataka
kusema kitu, lakini anaishia kulala kichwa mezani.
‘Niacheni....nataka
kwenda nyu-nyumbani....’anasema na kulala
‘S-s-sasa ngoja
tufanye hivi tumsaidie apate nguvu arudi
nyumbani kwake isije ikawa tatizo , unamfahamu mke wake alivyo mkali, akija
hapa itakuwa hakieleweki.....’akasema
‘Tutamsaidiaje
kwa jinsi alivyo, hapa ni kumwagiwa maji labda, .. na huduma ya
kwanza,....lakini akiwa hapa tutafanyaje...unasemaje....?’ akauliza
‘Hapana
kwanini tusimpeleke chumba hicho hapo cha ya huduma ya kwanza....?’ akawa kama
anauliza
‘Oooh,
lakini sio mgonjwa, ... lakini sawa, hata hivyo, unamuona jamaa mwenyewe
alivyo, bonge la mbaba, ..tutawezaje kumbeba hadi hapo kwenye chumba cha huduma
ya kwanza...?’ akauliza mdada
‘Inabidi
tutafute msaada, hebu, wewe ....kamuite mfanyakazi mwingine mwaminifu....’akasema
huku akiajaribu kumuinua huyo jamaa lakini haikuwezekana.
Na mdada kwa
haraka akasogea kuelekea upande mwingine walipokuwa watu wakisherehekea, akaita
kwa sauti kubwa
‘Waiter,
msaada hapa.....
‘Waiter
help...’ na mara akaja jamaa mmoja akiwa kavalia sare za mlemle ndani , na kwa
zaidi alikuwa kavalia kofia jeupe, kama alilovalia profesa.....na mawani meusi,...
Kwa muda ule
profesa hakuwa na wasiwasi, yeye alijua kuwa ni muhudumu wa humo humo,...na
uvwaaji ule wa kuongezea kofia na mawani meusi, kama alivyo vaa yeye, alijua ni
mbwembwe tu, maana walikuwa
wakisherehekea siku ya kuzaliwa kwa mmoja wa wafanyakazi wa humo.
Yule jamaa
akaja hakuongea kitu, kama alijua, yeye alichofanya ni kuinama, akamuinua huyo
mlevi, akawa kama anamsimamisha, na alipoona jamaa hawezi hata kumsimamisha,
akaonyesha ishara, kuwa wengine wakae upande ili aweze kumbeba...
‘Mhh,jamaa
lina nguvu, alimuinua huyo mlevi, na kumweka begani,na kuanza kuondoka naye...
‘Huku...muingize
humo....’akasema mdada, alipoona jamaa anataka kuondoka na huyo mlevi kuelekea
sehemu ya chini.
Basi mlango ukafunguliwa wa hicho chumba cha
dharura, na akaingizwa huyo jamaa na kubwagwa kitandani, na jamaa muhudumu,
aliyembeba huyo mlezi, akasubiria pembeni.....
Profesa kwa
vile alimuamini huyo mdada, wala hakuhangaika kumuangalia yule jamaa zaidi,...yeye
alipoona huyo mbebaji kasimama akisubiri, akasema;
‘Inatosha mimi
niachieni huyu mtu,mimi ni jamaa yangu najua jinsi gani ya kumsaidia, wewe
unaweza kwenda kuendelea na shughuli zako, ..’akasema akimgeukia huyo muhudumu
mwanaume aliyembeba huyo mlevi, na kidogo alitaka kumtizama usoni huyo jamaa,
japo kavalia mawani,na yule jamaa akageuka kuangalia mlangoni kama anaondoka,
na muda ule yule mdada akaondoka kwa haraka...
Mle ndani
kulikuwa na kitanda, kuna kilakitu, kama
chumba cha hotelini zaidi kwa juu kuna sanduku la huduma ya kwanza, kulikuwa na
kabati jingine la juu kidogo, na profesa alipoingia tu mle cha kwanza kuangalia
ni juu ya ile kabati..
‘Mbona
sijawahi kukuona humu ndani...?’ akauliza profesa akiongea na huyo muhudumu
mbebaji akiwa anatembea sasa kutoka nje, lakini akaona vitu pale mezani, kama
muhudumu alitakiwa kuviondoa, na kweli jamaa akafanya hivyo
Yule jamaa
hakusema kitu akawa anakusanya vile vyombo kulikuwa na chupa na sinia alilokuwa
nalo mdada, naona mdada katika kuondoka kwa haraka alikuwa kavisahau, au
vilikuwepo humo kabla, ....
Jamaa
alipohakikisha hakuna kitu kingine kistochostahiki humo ndani, akaanza kutembea
kutoka na alitembea mwendo wa kuhesabu hatua, hadi mlangoni, halafu akasimama
akageuka kidogo, kiasi cha kugeuza kichwa, akasema...,
‘Umesemaje....?’
akauliza
‘Sijawahi
kukuona hapa kabla...’akasema
‘Mhh, ....Its you again...hahaha.....see you later..’alisema
huyo mtu na kwa haraka akaondoka.
‘Its you again ...., ni mimi tena, ...ina
maana niliwahi kukutaa naye mahali, ni wapi,..ni nani huyu..,mbona sura ngeni
kwangu, na karibu wahudumu wote wa humu ndani nawafahamu....’akawa
anajiongelesha kichwani, na wakati profesa anatafakari hayo maneno yana maana
gani, mara mdada mmoja akaingia akiwa kavaa koti refu, la kujifunika sehemu
kubwa ya mwili, sura tofauti na yule
mdada wa kwanza...
Yule mdada
alipoingia kwanza akasimama hukua kiwa kashikilia kiuona, akikagua mandhari ya
mle ndani, ...Profesa aalibakia kumuangalia huyo mdada mpya aliyeingia kwa
mshanga, ...
‘Wewe nani
unafuata nini huku...’akauliza profesa akionyesha mshangao, na yule mdada mpya
kwanza kaonyesha ishara ya kidole, kama kumnyamazisha profesa, halafu akageuka
kuangalia kule kitandani.
‘Na wewe
nambie unafanya nini na huyu mtu, unajua huyu mtu na nani kwangu....?’ akauliza
mdada,na kumfanya profesa abakia na mshangao, na akauliza
‘Ni nani
kwako huyu mtu....?’ akauliza
‘Mmmh, nimemfuata
my baby is he ok,.......’akasema huyo mdada sasa
akitembea kwa madaha, na alipofika pale kitandani, akageuza uso kimadaha,
....taratibu akaondoka lile koti la juu, na kubakia na kivwazi cha aina yake,
kilikuwa ni kivwazi cha kulalia,ni sawa
na nusu uchi tu...
‘Who are you...?’ akauliza profesa kwa
ukali
‘Nimeshakuambia
huyu ni mpenzi wangu aliniacha chini sikujua yupo huku,mmmh, niache na mpenzi
wangu, nimfanyie masaji,najua sasa hivi atazindukana, unaweza kuondoka,
....’akasema huyo mdada akiwa sasa anamuinamia huyo jamaa pale itandani
alipolazwa huyo jamaa, na jamaa alikuwa kama anaanza kujitambua, ...
Jamaa
alijitikisa, akajiinua, akapangusa uso, akapiga miayo, halafu akatikisa kichwa,
akashika kichwa,halafu akasema
‘Ni...ni..nipo
wapi....’akasema kwa sauti ya kilevi
‘Umenisahau
baby..ulinikimbia kumbe umekuja huku juu,...’akasema huyo mdada
‘Nataka
kwe-kwe ndani nyumbani.....’jamaa akasema akijaribu kusimama, lakini akawa anapepesuka, akataka kuanguka,
na mdada akamdaka, wakawa kama wameshikama kusaidiana, na wote wakaangukia
kitandani.
‘What are
you doing...?’ akauliza profesa alipoona hiyo hali
‘Hiyo sio
kazi yako, unasubiri nini, huyu ni mpenzi wangu...nataka nimsaidie
tuondoke,....’akasema mdada
‘Ok,....but
be careful, kalewa ...’akasema profesa
Mara jamaa
akawa sasa kidogo kama anajielewa, akajikuta yupo mikononi mwa huyo mdada,akawa
sasa kama anataka kujitoa kwa huyo mdada,na huyo mdada akawa kama anamsaidia
...profesa akatupa jicho juu ya lile kabati kwa kujiiba, na kutikisa kichwa,
akasema;.
‘Ok, let me
go but be careful,... lakini uwe makini na huyo mlevi,kalewa, anaweza kukufanyia ubaya,
....’akasema profesa akitoka mle ndani, akaondoka na kuja kukaa nje akisubiria,
kama atahitajika...
Alipofika
nje hakumuona yule jamaa, akatembea kidogo na kuangalia huku a kule, akakuta
hakuna mtu, na upande mwingine kulikuwa na sherehe za kumpongeza mfanyakazi
mwenzao siku ya kuzaliwa, hakuwa na shughuli nao, mawazoyake ni huyu mtu,
aliyemuambia kuwa 'its you again...
‘Ni wewe
tena...ni mimi tena,nilionana naye wapi, labda ni humu humu ndani, lakini kauli
hiyo ni kama kunikoga...’akawa anawaza profesa, ....
Haikupita
muda mara ukelele wa ‘help... help
....ananibaka..saidia huku....’ukasikika...
Na muda ule
kulikuwa na wahudumu wawili wa kike , walikuwa wakipita, wakasikia hivyo,
wakaanza kukimbilia kuelekea kwenye hicho chumba, na profesa akawa wahi na
kutangulia yeye, yeye aliingia kwanza na wale wadada wawili wakafuatia
‘Ni nini
kinaendelea huku mbona kelele za kuomba msaada....?’ wakauliza
Mle ndani
kilichokutwa,mjamaa alikutwa uchi,akiwa kweli kwenye harakati za kulazimisha,
na wale wadada kuona vile wakaanza kumsaidia yule mdada,
Profesa hakuhangaika nao,...., akanyosha mkono juu ya lile kabati,na kuchukua chombo chake , na taratibu akaondoka zake....
********
Profesa alipokumbuka hiyo kauli aliyosikia
siku ile kwenye hilo tukio akajikuta akisema
‘Haiwezekani,
haiwezekani...ina maana huyu jamaa alikuwepo kwenye lile tukio, lakini mbona
sikuwahi kumuona, nakumbuka yule aliyekuwemo siku ile alikuwa ni muhudumu wa
pale ndani, nina uhakika alikuwa muhudumu, japokuwa sikuwahi kumuoa
kabla...’akawa anaongea peke yake
Akajaribu
kukumbuka maumbile ya huyu mtu na yule muhudumu, lakini hakuweza kuoanisha
vyema, maana tukio lile lilikuwa la haraka,hakutarajia hivi,maumbile kama
yanafanana....nguvu, mhh...
‘Haiwezekani
ni lazima niongee na mdada aniambie ukweli. ...haiwezekani....’akawa anajilaumu
Kwa muda ule
alikuwa kasimama kwenye barabara, akigeuka kutafuta sehemu nyingine ili apige
simu kwa mdada kuhakikisha hicho anachokifikiria, alijua kwenye kile kibanda
alichokuwa akitumia mwanzo jamaa atakuwa yupo hapo akipiga simu.
Kwanza akajaribu
kumtupia jicho yule jamaa kwenye kibanda cha simu, ili kumuona vyema,
lakini......hakukuwa na mtu
Kwa mshangao
hakumuona mtu yoyote kwenye kile kibanda cha simu,.... ni sekunde chache tu za
kutembea kuelekea barabarani na alipogeuka kuangalia kwenye hicho kibanda,
alikuta kipo cheupe hakuna mtu.
‘Huyu mtu
kaenda wapi,...uwepesi gani huo, nina uhakika alikuwa ameshaanza kupiga simu,
na kuanza kuongea, sasa iweje, atuweke kwa haraka hivi kama upepo,....’akawa anajiongelesha mwenyewe
Profesa akageuka
kuangalia huku na kule lakini hakuweza kuona dalili ya mtu kama yule hapo karibu,
na hapo akajua kweli sasa yupo matatani.
‘Huyu mtu ni kupe akikudanga
keshakuganda, ni lazima ainyonye damu
yako....’akamkumbuka maneno ya mtaalamu alivyokuwa akimwambia.
*********
Profesa
akawa anatembea kuelekea ofisini kwa mtaalamu, alikuwa anataka kupata pesa,
pesa ndio suluhisho ya haya anayokumbana nayo sasa, bila pesa hataweza
kuwashinda maadui zake,....pesa ataipataje !
Na pia alikuwa
na maswali mengi ya kumuuliza huyo jamaa anayejiita mtaalamu, alijua bila
msaada wa huyo jamaa sasa yupo mtatani, jamaa anaonekana kujua mengi,na anaweza
kuwa msaada mkubwa kwake, lakini jamaa anaonekana pia kuwa anataka kumgeuka,
tamaa ya pesa imeshamtawala...na yeye anahitajia pesa tena pesa nyingi, sasa
afanyeje
‘Dawa
nikamuone uso kwa uso,.....nitapambana
naye uso kwa uso,kabla usiku sijaanza kuwasiliana na mtu wangu,kabla
usiku sitajaingia kazini lazima kieleweke..’
Alifika mtaa
unaoingia kuelekea maeneo hayo ya ofisi
ya mtaalamu,...na mara gari likaja kwa nyuma yake, likampita, yaonekena gari
hilo lilikuwa likielekea kwenye hizo ofisi, na cha ajabu gari hilo lilifika
mbele likasimama,....
Kwa hali ile
profesa akahisi hatari akageuka kutaka kurudi alipotokea, hakutaka kuongea na
mtu mwingine zaidi ya mtaalamu, hakutaka kujulikana anaelekea kwenye hizo
ofisi, lakini lile gari likarudi kinyume nyume kwa haraka, hadi pale alipo
Mara viyoo
vikashushwa, kwenye hilo gari, na jamaa akatokeza kichwa na kuanza kuongea
‘Profesa ,
profesa, long time never see you,...unaelekea
wapi....?’ ilikuwa sauti nyingine iliyompa mshituko, akageuka kwa haraka
kumtizama huyo mtu kwenye gari, hakutegemea kuonana naye kariuni hivyo,....
‘Nipo
tu,...sielekei mahali...’akasema profesa akitaka kuondoka lakii mguu ukawa
mnzito
‘Ni vyema
nimekuona nina mazungumzo na wewe muhimu sana....’akasema huyo mtu kwenye gari,
na hapo akajua ni yale yale huenda tayari ameshaanza kazi.
‘Kuhusu
nini,sina mazungumzo na wewe kwa hivi sasa....tulishamalizana...’akasema
profesa
‘Najua,
...lakini si unajua kazi zangu, leo nina kazi hii kesho kazi hii...’akasema
‘Hayo I
majukumu yako hayaihusu...’akasema profesa
‘Najua
mlishakubaliana na mama mtemi, japokuwa sivyo sahihi..kwani sheria ilitakiwa ichuke
mkondo wake,lakini nikaona mnajuana, na kazi yangu sio kushinikiza bali I kufichua
ukweli na uamuzi unakuwa kwa mwenyewe...kazi yangu ni kutafuta ukweli na
kuuweka wazi, au sio.....’akasema
‘Ukweli,au uzushi
tu,....kupekenyua yasiyokuhusu...mnafiki mkubwa wewe...’akasema bila kujali
‘Mhh, ....wabaya
wananisema hivyo, lakini wakweli wananiamini,...yule mama alitaka kujua ukweli,
na mimi nikamtafutia ukweli, au sio..., japokuwa analalamika kuwa wewe
hujazigatia makubaliano, umekuwa sio mkweli,..’akasema
‘Kwahiyo
ndio kakutuma kuongea na mimi...?’ akauliza
‘Mhh...hapana,
kwa hivi sasa hilo halinihusu, kasema yeye mwenyewe atakushughulikia...’akasema
huyo mtu...hiyo kauli ikazidi kumtia hofu profesa, yeye mwenyewe
atamshughulikia..
‘Sasa
unataka nini kwangu....?’ akauliza profesa kwa hasira
‘Kuna kitu
nataka tuongee,...si unajua kazi zangu, naruhusiwa kuwahoji watu, lakini sio
kwa nia mbaya, ili niupate ukweli, na leo nimeona niongee na wewe, kabla sijaingia zaidi kwenye undani wake,
...’akasema
‘Kwanini
mimi...unataka kuongea na mimi kuhusu nini....ya mama mtemi si umeshamaliza
umeshalipwa pesa yako au..?’ akauliza profesa
‘Hapa ni
barabarani,sizani kama upo tayari tumwage mtaka kwenye kuku wengi,....au
sio,ingia ndani ya gari tuongee
kiuungwana...’akaambiwa
‘Nina kazi
nafuatilia, sina muda wa maongezi, hususani na wewe...’akasema
‘Hata hii ni
kazi na huenda ikakusaidia zaidi na hata ukaghairi kwenda huko unapotaka
kwenda, ni muhimu sana mtu wangu...vipi kule unapofanya kazi kwa sasa...?’akasema
na hapo profesa akajua ni yale yale aliyokuwa hayataki.
‘Wapi ninapofanya kazi....na inakuhusu nini kufanya kazi kwangu, toka lini ukajali maisha yangu?’ akauliza profesa
‘Najua wewe
kawaida yako, hufanyi kazi mahali bila kuacha majeraha,....sasa unaingia
tuongee au unataka nipayuke hapa hapa,unaona watu wanapita wakisikia nakuulizia
haya ninayotaka kukuulizia, inakuwa sio vizuri, hata wewe mwenyewe hulioni
hilo, tuongee kiuungwana au sio...’akasema
Japokuwa
Profesa alikuwa na uharaka wa kwenda kwa mtaalamu ili akapate pesa za kwenda
kumpooza mama mtemi, lakini kwa hali ile hakuwa na jinsi, ikabidi aingie kwenye
lile gari, na kusubiria kitakachofuata...na alipoingia jamaa aliyekuwemo mle
ndani hakuwa na haraka ya kuongea...alikuwa kashikilia usukani akiwa kaangalia
mbele...
‘Haya nambie
maana nina haraka zangu....nakupa nusu saa,tena hizo nyingi, dakika kumi na
....sekende kadhaa....’akasema kwa hasira huku akiangalia saa.
‘Usiwe na haraka
saana...unajua mambo haya mambo msiyapeleke kwaharaa kihivyo...na,kiujumla
nimeshaanza kukuelewa, sasa sijui, yote inategemea wewe, maana inabidi ifanye
kazi yangu ,....na bila kufanya hivyo, unafikiri nitakula wapi.....sasa yote
inategemea wewe....sijui, labda safari hii tukaelewana,....’akasema huyo mtu
‘Kuelewana
kuhusu nini, wewe umeniharibia maisha yangu...’akataka kulalamika
‘Mimi
nikuharibie maisha yako....! Kwa vipi profesa, ...nimekufanya nini...hebu
nambie...? ‘akawa kama anauliza.
‘Mhh, hebu
nambie unachotaka kuniambia, unajifanya hujui eeh, ni nini umekifanya kwa mama
mtemi,umenitia doa, sasa nasakwa kama muhalifu, halafu unasema tuelewane na
wewe,....siwezi kuelewana na mtu kama wewe, kwanza kwa lipi, wakati
ulishamaliza...’akasema
‘Tutaelewana
tu, mbona hakuna shida kabisa,...nikuambie ukweli profesa mimi sio mbaya, mimi
huwa nafanya kazi yangu tu,...siunajua kazi yangu ilivyo, sasa mimi nimekosea
nini....’akawa kama anauliza
‘Niambie
ulichonitaka...nachelewa kwenye shughuli zangu...’akasema
‘Unakwenda
kwa mtaalamu au sio...’akasema
‘Hayakuhusu....’akasema
‘Unajua
profesa sasa hivi,tutaelewana sana, huna ujanja...ni uamuzi na tena uwe uamuzi
wa busara, na...sikutakii mabaya, ila upo kubaya sana, sasa ni uamuzi wako, ama
uelewane na mimi, au ukapambane na mama mtemi, na safari hii ujue hayupo peke
yake,...’akaambiwa
‘Sijakuelewa....’akasema
profesa
‘Umeshanielewa
sana, usitake mpaka nimwage sera, wakati wewe umeshazitekeleza kwa matendo....ni
uamuzi tu, tuelewane..funuka tushirikiane mbona mimi sina matatizo....’akasema
‘Ongea
unachotaka.....vinginevyo mimi natoka kwenye gari lako, unasikia wewe mpekuzi
wa mambo yasiyo kuhusu, mimi sikuogopi,.....nenda kwa hao waliokutuma waambie
.....’akatulia
‘Unajua
profesa, kila mtu ni mkali kwenye sehemu yake,...na sitaki tufike huko,...wewe sasa
hivi si unafanya-fanya kazi kwa yule jamaa kutoka India au sio...?’ akawa kama
anauliza.
‘Nafanya
sehemu nyingi tu,....kwanini useme kwa huyo mtu...?’ akauliza
‘Unaona
sasa..., mimi nimeshakufahamu vyema tu, ...nakudokezea hilo ili ujue kuwa
nimeshafahamu mengi,sio kwamba nakupotezea muda wako, hili huenda likawa na
manufaa kwako, tukielewana lakini, unielewe hapo, mimi ndivyo nilivyo, sitaki
kumuumiza mtu, sitaki ubaya na mtu, najua wewe unatafuta maisha, au sio, na
kila mtu ana njia zake,japo nyingine mhh,...’akatulia kidogo
‘Sasa mimi
nilikuwa a ombi kwako, ....na ombi hilo ni la kuamua tu,...ama uwe na mimi au
nikuache ufanye upendavyo, na najua kwa vyovyote kuna watu wapo nyuma yako,
wanakutafuta kwa kila hila, ....siwezi kusema ni maadui zako, ...hapana,...ila
ni wahasimu wako, natumai unanielewa hadi hapo...’akasema huyo mtu
‘Mimi sijakuelewa.....’akasema
profesa akijifanya haelewi kitu, na simu
yake ikawa inaita alipoangalia mpigaji akaona ni namba ya mama mtemi...
‘Pokea simu
yako.....’akaambiwa na huyo jamaa
NB: Naishia
hapa naona muda umetaradadi, na mambo yanazidi kubadilika, hata sijui la
kuamini, ...labda ndio kidunia.
WAZO LA LEO: Uongozi wa ujanja ujanja wa
kuwahadaa watu kwa lugha tamu lakini zenye sumu ndani yake,ni utapeli...ni dhuluma,....wewe kama kiongozi ndani ya shirika, wewe kama mtawala, mwanasiana au yoyote mwenye dhamana, kaa ukijua kabisa , kudanganya, kuhadaa, kwa visigizio vyovyote, ili upate kisicho halali yako, ili
ufaulu malengo yako, huo sio uongozi, huo ni ujambazi wakujificha, huna tofauti
na jambazi anayekwiba usiku,...na ukumbuke ipo siku utanaswa tu, maana unadhulumu, kudhulumu ni wizi, na za mwizi ni arubaini.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment