Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, July 22, 2015

RADHI YA WAZAZI-22



'Unafahamu kuwa kijana wako naye amegeuka kuwa adui yako , kaungana na watu wasiokutakia mema,.....?' akaulizwa

'Kijana wangu yupi...!?' Profesa akauliza kwa mshangao

'Kwani wewe una vijana wangapi,.....?' akaulizwa na kabla hajasema neno akaambiwa kwenye simu

'Ni huyo huyo kijana wako aliyekuwa akikuweka hapa mjini kipindi cha nyuma kama hukumbuki vyema, .....umemkumbuka eeh...huyo kijana alikuwa akikufanya upate pesa za wafadhili, na baadaye, sijui ikawaje...alipojitegemea kitumbua kikaingia mchanga....'akaambiwa

'Haiwezekani.....'akasema profesa akitoa macho ya kutoamini

'Sasa ikawaje......' kaka mtu aliyekuwa akisikiliza kwa makini simulizi hilo toka kwa mdogo wake,....baada ya kusikia mtoto wake sasa anatajwa ndio akauliza hilo swali

Tuendelee na kisa chetu

                **********

‘Kijana wako ameungana na yule mama mtemi kuhakikisha unapatikana ushahidi kuwa wewe ni wakala wa watu wanasumbua wakazi wa hapa kwa shughuli ya mlungula(blackmail)...’akasema

What ! Hawezi huyu huyu kijana wangu , hapana huyo hawezi kunifanyia hivyo mimi ni baba yake mlezi, nimetoka naye mbali, haiwezekani...’akasema profesa

‘Kayasema hayo akiwa na binti wa huyo mama, na kwa hiyo ndio akakubaliwa kuwa mchumba wa huyo binti , si unamfahamu huyo binti wao, wanayempenda kama nini,...?’ akaulizwa

‘Nisimfahamu wakati mimi nilikuwanafanya kazi kwao, au unamaana gani kuuliza hivyo...?’ akauliza nay eye

‘Unamfahamu kwa maana kuwa alishakuwa na mahusiano na kijana wako,...na akawa anakataliwa huyo binti kuwa na ukaribu na kijana wako....unalifahamu hilo?’ akaulizwa

‘Mhh...hilo la kukataliwa silifahamu, maana kijana mwenyewe alishakuwa mbali na mimi....’akasema

‘Huyo kijana hakutakiwa kabisa kuwa karibu na huyo binti, wakawa wanakutana kwa kujiiba, siku wakabambwa,kijana akataka kupelekwa polisi, binti akamtetea.....’akasema

‘Mhh, ilifikia hapo, ....sijakutana na huyo kijana muda sasa...’akasema

‘Ndio hivyo, mwanzoni walimkataa kwa vile walimuhusisha na wewe, wakaona kuwa binti yao, hawawezi kuwa na mahusiano na kijana wako, kwa vile wewe ni mtu mbaya, kwa tabia yako!’ akaambiwa

‘Hawa watu nitawafanyia kitu mbaya....hawanijui, eeh....’akasema

‘Upo tayari kupambana na huyo mama...?’ akaulizwa

‘Nilishamweka pabaya, akaniwahi, lakini....’akatulia

‘Huwezi bwana, ..huyo mama humuwezi kamwe, na kwa vila alishakufahamu, ujue akitaka kukweka ndani anakuweka ndani,....si ndiye huyo anakudai,...’akaambiwa

‘Sasa kama kakubaliana na huyo kijana wangu kwanini asiniheshimu,kwa vile tumeshafunga udugu...’akasema

‘Sasa sikiliza, huyu kijana wako Ili kuwathibitishia kuwa yeye hana uhusiano na wewe ,...ndio akasema yupo tayari kuhakikisha wewe unakamatwa kwa makosa ya kuwamkorofi kwenye jamii, ....’akasema

What, I cant believe this....Haiwezekani, haiwezekani kabisa....kama huyo kijana atafanya hivyo nitamharibia maisha yake yote, anafahamu alipotokea una uhakika na hilo,....’akasema profesa

‘Hebu nikuulize kwanza, ...Je wewe kweli ni mzazi wake...?’ akauliza mtaalamu, na profesa alikuwa na jibu la haraka, akasema;

‘Hapana mimi sio baba yake kabisa, mimi ni baba mlezi  tu, nilimuokota akiwa porini, nikaweza kumfikisha hapo alipo, na sasa anataka kunisaliti...’akasema profesa

‘Mimi sasa sijui,...ila ninakuonya kwa hilo, uwe makini sana, maana naona kila aliyekuwa karibu nawe anageuka kuwa adui yako, uajua hii inaashiria nini..?’ akaulizwa

‘Mhh kuwa nitafukuzwa haya maeneo au sio...?’ akasema na kuulizwa

‘Sio kufukuwa, wewe sasa jela inakukodolea macho,...’akaambiwa

‘Jela, lakini...’akataka kujitetea

‘Lakini nini! .... Na pia ukumbuke unapokuwa kwenye shughuli hizi, na wenzako wakahisi kuwa unaweza kuwa ni tatizo, hawatasita kukumaliza, ukapotea duniani...’akasema

‘Eti nini...ina maana mtaniua.....!?’ akauliza kwa mashaka

‘Tutakuua! ? Nani kasema tutakuua, nakuelezea hali halisi, hivi nikuulize kama kuna njia nzuri za kujipatia pesa, na ndio kazi yenu, na kukatokea mmojawapo ni kikwazo cha kupatia masilahii na akiwemo anaweza kuwatumbukiza hatiani, kama ni wewe kiongozi, utashauri nini...?’ akaulizwa

‘Kwani kuna kiongozi wa mambo haya kila mtu anajifanyia aonavyo, na wewe unatumika tu kama mchanga dili wa mlungula(blackmail)...au wewe ndio kiongozi wao....’akasema profesa

‘Mimi nimekuuliza swali tu...., usije ukasema nimekulenga wewe, ila nimetolea kama mfano kwako, ikatokea hivyo, mtu anakuwa ni kikwazo, kwa haya mambo yetu....na mkimuacha anaweza kuwatia hatiani, unafikiri ni ipi njia sahihi...?’ akaulizwa

‘Lakini mimi sio tatizo, mambo kama haya yanatokea kwa yoyote, au sio, ni moja ya changamoto kwenye hizi kazi, sioni kama ni tatizo kubwa,mimi nitapambana nao....au una wazo lolote....au mumekaa kunijadili kuwe mniondoe ,mniue..?’ akauliza

‘Nani kasema hivyo, mimi nafahamu weweni mjanja, na unajua mwenyewe jinsi gani utakavyojiokoa, kwa ushauri wangu kwa jinsi hali ilivyo, ....ikibidi njia sahihi ni wewe kuondoka eneo hili,...lakini ikibidi,kwa hivi sasa ni muhimu kuimaliza hii dili.. ...’akasema

‘Niondoke, niende wapi na kibali changu cha kuishi huku ni eneo hili....na nikitoka hapa nitakwenda wapi na mimi hapa ndipo ninapohemea...’akasema profesa

‘Lakini ukumbuke, yule mama mtemi anakutafuta na sasa anataka umlipe pesa nyingi tu, utazipatia wapi hizo pesa, na sizani kama utaweza kupata pesa kwa hizi sasa za kuweza kumaliza deni lake, na hata ukimlipa pesa sizani kama atakuacha, ataendelea kukukamua. Si unajua alivyo...’akasema

‘Haya huyo kijana wako kajitolea kumsaidia huyo mama, ambaye sasa keshakuwa mama  mkwe wake,...huoni huyo mama sasa keshakuweka pabaya, kijana wako anamtaka binti, na njia rahisi ni kupitia wewe, wewe ukamatwe , uwekwe ndani, ili kijana ampate huyo binti...hayo ndio makubaliano yao...’akaambiwa

‘Hawaniwezi, huyo mama anajua kabisa nafahamu siri zake, na kijana naye anajua mimi ndiye niliyemuweka hapa Ulaya....wakijaribu kunifanyia lolote, kabla sijaingia jela,...’akatulia

‘Na ukumbuke kuwa,... huyu mteja mpya hajakufahamu kuwa ni wewe, siku akija kukugundua, umekwisha!’ akasema

‘Mhh, kwahiyo...?’

‘Karata yako hii ni muhimu sana,...usipocheza vyema, ukapata pesa, ya kukutosha, ukamalizana na hao maadui zako, hasa huyo mama mtemi, ndugu yangu tutakusahau...hilo siwezi kukuficha...’akaambiwa

‘Lakini nakumbuka nilikuuliza kuwa je kuna uhakika wa kuzipata hizo pesa, kama benki wameleta utata, kama mke wa huyo jamaa kaingilia kati...huoni hilo ni tatizo, kama haiwezekani, basi tutafute dili nyingine kabla mambo hayajaharibika....?’ akauliza profesa

‘Pesa kupatikaa nina uhakika zitapatikana,...na nina uhakika huyo jamaa alivyo, umemshika kubaya, huyo jamaa mkewe ndiye mwenye kila kitu, kwahiyo anaogopa sana huyo uchafu wake, uje kuonekana kwa mkewe, anachotafuta kwasasa ni kuhakikisha, anapata wapi hiyo video ipo,na wahusika ni akina nani,....’akaambiwa

‘Sasa huyo mama mtemi akija kumuambia kuwa muhusika ni mimi, huoni kuwa mimi nipo matatani...?’ akauliza

‘Ni mpaka huyo mama mtemi agundue kitu kama hicho...huyo mama mtemi anapeleleza kutaka kujua wapi unapozipatia hizo pesa, hajagundua, anakisia tu, akigundue, anaweza akaichukua hiyo dili akawa ndiye anazichuma hizo pesa....’akasema

‘Haiwezekani....’akasema profesa

‘Mimi namfahamu huyo mama kuliko yoyote, mbele ya pesa huyo mama hana urafiki,....hilo la kusema kabadilika....sahau, ila, kwa vile anataka kujijengea jina, atakuwa ndumila kuwili tu...sasa wewe endelea kucheza karata yako vyema kwa huyo jamaa...’akasema

‘Mhh, hii dili ni hatari, kama ningelijua nisingeichukua, sasa....’akasema profesa kabala hajamaliza,mtaalamu akasema

‘Wewe endelea kuleta pesa kutoka kwa huyo mtu, kwani huyo jamaa hana ujanja, ila kwa sasa anatapatapa tu, kwani kafikia hatua ya kutaka kutafuta mpelelezi...’akasema

‘Oh, ....una uhakika na hilo...?’ akauliza profesa akizidi kuchanganyikiwa

‘Mimi ninayokuambia sio maswala ya kuambiwa nafahamu na nina uhakika kwa kila kitu, mimi huwa sibahatishi...’akasema

‘Mhh, huoni sasa hilo ni tatizo....hii dili naona sitaiweza...itanipeleka kubaya?’ akauliza

‘Hiyo dili ni kazi yako, ni dili nzuri tu kama ukicheza vyema, mimi hayo nimekupa kama angalizo, na ukimbana vyema huyo jamaa atachanganyikiwa, wewe ni profesa bwana, hii pesa si ya kuachia....kama umeshindwa nimpe mtu mwinine aimalizie...naweza kuiuza kwa bei mbaya..’akaambiwa

‘Lakini si umesema huyo jamaa kamtafuta mpelelezi, huoni kama nitakuwa hatarini....nitajulikana,na mimi nitakwenda wapi..?’ akauliza

‘Hayo ni mambo ya kawaida,..., na wapelelezi wote wa hapa nawafahamu, hiki ninachokuambia ni uhakika kuwa huyo jamaa katafuta mpelelezi, na ni jana tu, huyo jamaa alikwenda kumuona yule mpelelezi...’akasema

‘Mpelelezi yupi...?’ akauliza

‘Mpelelezi mmoja  wa njaa kali, anayefanyia kazi hapa kwenye ofisi zangu...’akasema

‘Oh,...ina maana kumbe keshamtafuta mpelelezi tayari,  na ni nani huyo mpelelezi,ni...Njagu  nini...?’ profesa akauliza

‘Ndio huyo huyo...’akasema

‘Hilo sasa ni tatizo,maana huyo mpelelezi ndiye aliyechukuliwa na huyo mama mtemi,...akanigundua kuwa ni mimi....my, God,...this now is disaster.’akasema

NB: Tuishie hapa


WAZO ZA LEO: Tumshukuru mungu kwa kilajambo,tunaweza kuoana huenda tumeonewa, au ukafikia hata kukufuru kuwa kwanini mimi, lakini yote hayo yanaweza yakawa ni heri kwako,ikawa ni njia katika kufikia mafanikio fulani,ikawa ni mwanzo wa neema..kamwe tusikate tamaa.

Ni mimi: emu-three

No comments :