Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeMonday, July 20, 2015

RADHI YA WAZAZI-21


‘Labda wewe hujanielewa,mimi huwa sipendi utani, usione nimefika hapa ukafikiri nimebahatisha, nafahamu nyendo zako A to Z,...tangu ulipogusa anga zangu nimekuwa nikikufuatilia kwa makini,  mimi najua sasa mpo kwenye mpango wa kumla mtu mlungula(blackmail), sasa sijui vipi na kwa vipi,....’akasema yule mama huku akizifutika hizo pesa sehemu ya maziwa yake bila kuzihesabu.
‘Mimi nakuahidi nitakulipa pesa zako....’profesa akasema,

Ilikuwa pesa kidogo tu aliyokuwa nayo profesa baada ya kupata ile pesa ya mwanzo waliyomtoa yule jamaa, na akawa kaitumia, na kulipa baadhi ya madeni, na hapo akawa kabakia na pesa kidogo tu,.

‘Lakini ilibidi nizitoe ili kumliwaza huyo mama asije kuleta fujo...’akasema profesa akimuhadithia kaka yake

‘Mimi nataka pesa yangu, ...’akasema huyo mama akiwa kasimama mbele yangu akinitolea macho ya vitisho

‘Nitakuletea pesa yako madame,..., wewe uniamini tu....’akasema profesa.

‘Poa,...mimi naondoka, nakupa siku hizi mbili, au tusema tatu, nikija , au popote utakapokwenda ujue ninakuja kwa shari... sitakuja hivi hivi,nikuache hivi hivi...leo nimeiheshimu hii hoteli,...’akasema na kupiga ngumi kwenye ile meza na vinywaji vilivyokuwepo vikamwagika.

‘Tafadhali madame....’alisema profesa akiwa na wasi wasi na uwoga, akikumbuka habari za huyo mama

‘Ndio hivyo, uilewe hiyo,...kumbuka, safari nyingine  ...nitakuja nikiwa nimekamilika,..utanisimulia.’akasema huyo mama na kuondoka zake....

Tuendelee na kisa chetu

*********

Wakati kule kwa mume na mkewe kukiwaka moto, familia haielewani tena..., huku kwa profesa mchochezi wa kuharibu familia za watu kwa nia ya kupata pesa kwa kupitia njia isiyofaa, nako hakukuwa na amani, maana uchu wa kupata ulishawaingia na walishajihakikishia kuwa watazipata hizo pesa, lakini mambo hayakwenda sawa.

Na wakati wanasubiri fungu la pili kama walivyoahidiwa na yule mume mtu, si ndio huyo mama mtemi akamuingilia profesa, na tishio alilolitoa hapoo ndilo lililmfanya profesa kutafuta uficho mwingine, lakini hata hivyo ili awe na amani alihitajika kupata pesa za haraka ili kumpooza huyo mama mtemi.

‘Kawaida nilikuwa napenda kwenda kwa hiyo familia ya mume mtu na mkewe, ndipo nilikuwa nahemea, kwa kazi za kibarua, kama ipo napewa, na kama hakuna inabidi nitafuta sehemu nyingine, na lengo kubwa la kutafuta kazi hapo ni kua karibu na hiyo familia ili kujua ni nini kinachoendelea.

‘Kwa mara ya mwisho waliniambia hawapo sawa, wakinihitajia watanipigia simu, kwahiyo ikabidi nisiende kwanza, japo nilitamani sana kwenda hapo ili kusikia ni nini kinachoendelea...’akasema

‘Lakini kazi hizi zina mbinu zake, unatakiwa uwe makini sana...’akasema

 Basi siku ile alipokuja yule mama mtemi , na kunikuta hapo hotelini, nikaanza kuhisi mambo yangu yanaweza kuharibika, na huenda huyo mama anaweza kwenda kwa huyu mteja wetu na kumfunulia siri yetu, kwahiyo nilitakiwa kutafuta pesa ya haraka ya kumnyamazisha huyu mama

 Basi ndio nikatoka hapo kwenye hoteli, na kutafuta sehemu nyingine , ndivyo kazi zetu zilivyo, ukihisi hapa kuna hatari haraka unatafuta sehemu nyingine, lakini yote hiyo ni gharama, na ukumbuke nimepewa siku kadaa, kuwakilisha malipo ya watu kwa huyo mama mtemi,

‘Sasa ulifanyaje....?’ akauliza kaka mtu

‘Akili ilibidi ifanya kazi ka haraka, nilitakiwa kutafuta mbinu za kupata pesa, na muda ulikuwa hautoshi,...’akasema mdogo mtu akimsimulia kaka yake.
Wazo lililonijia ni kutafuta mkopo, na ni nani angenipa mkopo wa haraka, kwa hali kaam hiyo siwezi kwenda benki, ....na watu wengi hawawezi kuniamini, na mara wazo likanijia, ndio nikaenda kwenye simu ya barabarani ya kibandani nikampigia mtalaamu

‘Mtaalamu yupi huyo, ...?’ akauliza kaka mtu

Yule mtaalamu wa kuchora dili, nilijua kwa vile yeye anajua kuwa kuna uhakika wa mimi kupata pesa asingeliweza kukataa kunikopesha, ...lakini mhhh’akasema

Basi ndio nikampigia simu huyo mtaalamu;

‘Vipi mtaalamu....’nikaanza kwa mbwembwe, na jamaa akahamanika akijua mshiko tayari

‘Nambie,..mambo tayari...’akasema akionyesha hamasa

‘Mambo tayari!? Hahaha,....anichekesha, mimi nimekwama,na hapa nilipo nipo barabarani,sina mahali pa  kuishi.. nakimbizwa...’nikamwambia

‘Kwanini,...polisi,au ? ‘akauliza kwa kunikatiza,na hata kabla sijamjibu akasema

'Hapana sio polisi, ni madeni mkuu....'akasema profesa

‘Madeni,...unanitania,...kwani hilo linanihusu nini mimi...?’ akauliza akionyesha kukereka, maana alijua namletea habari nzuri ya pesa, mimi namletea shida.

‘Unajua mtaalamu, hii dili hukunisukia vyema, ni sawa ulinielekeza njia, lakini mbona haikufanikiwa, kama ulivyoona tumepata pesa kidogo, wakati tulipanga mambo mengi, na hayo mambo mengi ni gharaka, sasa huo mkupuo wa pili tumeahidiwa sijui itakuwaje...’akasema profesa

‘Sasa tatizo lipo wapi hebu ongea kinachoeleweka unanipotezea muda....kwanza upo wapi...’akasema

‘Nipo barabarani....'akasema

'Ehe ongea ...'akasema

'Mtaalamu, ndio dili ilikwenda vyema na jamaa akaahidi, na kiukweli  jamaa yupo ana haha kuzipata hizo pesa..., lakini kuna tatizo limetokea...’profesa akasema

‘Tatizo gani....?’ akauliza sasa akiwa makini

‘Hilo tatizo ni kuhusu mimi na wadeni wangu, hawa watu wamenijia juu, na nisipowalipa wanaweza kuharibu kila kitu ...’profesa akasema

So....ina nihusu nini mimi....?’ akauliza

‘Inabidi unisaidie maana itaathiri mambo mengine, inaweza ikawa kikwazo cha kupata pesa...’akasema profesa

‘Mhh, ni nani yupo nyuma ya hayo yote, anayekufuatilia ni nani ni yule bosi wako wa zamani au sio....?’ akaniuliza

‘Mhh,umejuaje, au wewe....’nikataka kulalamika

‘Mimi nawafuatilia watu wangu kwa karibu sana...na sio kwamba nina ukaribu na huyo mama, hapana,...huwa sielewani naye kabisa, na hata hivyo mimi sina haja ya kujuana naye, maana nikijuana naye nitakwamisha shughuli zangu,...ila nilishakuambia, uwe makini sana na huyo mama...’akasema

‘Ndio hivyo, nilishaachana naye lakini sikuachana naye kwa heri...’akasema profesa

‘Tatizo lako una njaa kali, na huwezi kuwa makini ...ukipata pesa wewe unajua kutumia tu, ...namfahamu sana huyo mama ni kigeugeu haaminiki,na ni hatari, hasa kwenye hizi dili, na kageuka kuwa mwiba mchungu, kwani anasaidiana na watu wa usalama,  ...’akasema

‘Ok, sasa nifanyeje...?’ akauliza

‘Sijui,.... hilo sio jukumu langu,..nilishakuchorea dili ilikuwa kazi ya kuifuatilia, na siwezi kujiingiza kwenye kazii za watu, nitafanya kazi ngapi....’akasema

‘Nafahamu hilo mtaalamu...., tatizo langu ni pesa, ninachoomba kwako ni mkopo, ili nimalizane na huyo mama, nipo kwenye hatari ndugu yangu...’profesa akasema

‘Hahaha nikukopeshe, hahaha, kwani mimi ni benki, sikiliza mimi sina utaratibu huo wa kukopesha watu, pesa ninayopata ni kiasi tu, ianitosha mimi na kwa kuwalipa watu wangu, unajua ili hii kazi ifanikiwe inakuwa na watu, wanahitaji pesa,nikipata najua jinsi ya kuipangia, sibakiwi na kitu...wewe,unalijua hilo ...’akasema

‘Lakini wewe ulinihakikishia kuwa pesa ipo ya kutosha, nikapanga mambo yangu,na ...yote ni gharama, ukasema huyu jamaa atatoa pesa nyingi..., sasa nashangaa unanigeuka, mimi nitawaewzaje kulipa haya madeni, na yapo katika bajeti yangu, ndio maana nikakubali hiyo dili...’akasema profesa

‘Kila kazi ina mitihani yake, tatizo la hii dili imekuja kuvurugwa na shughuli za kibenki , hilo nalikubali....kama kusingelikuwa na hilo tatizo, na uzembe wa huyu jamaa kutokufuatilia tayaribu za benki, pesa ilikuwa wazi kabisa, sasa hilo sio kosa langu...na mtu wako kajichoresha,kwa mkewe, yupo kiti moto...’akasema

‘Ina maana kuna tatizo kuzipata hizo pesa,....yeye aliniambia kuwa atakamilisha na pesa atazipata....’akasema

‘Yah, so kuna tatizo gani, hiyo ni kazi yako, na sio mimi nikufanyia hiyo kazi, hangaika,mimi kazi yangu ni kupanga dili na sio kuingia uwanjani kucheza, mimi hukosipo kabisa...fanya kazi yako...’akasema

‘Kwahiyo...?’ akauliza profesa

You man, you'r waste my time...., ..kwahiyo , kwahiyo, ...unataka mimi nifanye nini, mimi hilo sio jukumu langu, na mimi sina muda wa kufuatilia kazi ambazo nilishaelekeza,...kazi yangu ni kukupangia dili, na dili hiyo ilishakuwa mikononi mwako....unanielewa wewe njaa kali...’akasema

‘Najua, lakini kuna hili tatizo lipo nyuma yangu nitafanyeje...nipe pesa kidogo nikampooze huyo mama, utanipa?’ akauliza

‘Hilo la huyo mama halinihusu, halipo kabisa kwenye hii dili, ni mambo yako na njaa zako, unanielewa...hayo ni matatizo ya kutowatumia wataalamu, nafahamu kabisa tatizo hilo linatokana na kazi zako binafsi, sasa mimi siwezi kuwa mhanga wa njaa zako....unanisikia stop...’akasema

'Na kuna tatizo jingine kuhusu kijana wako....'akasema kabla sijasema kitu

'Kijana wangu, yupi...' profesa akauliza

'Una vijana wangapi..'akasema

'Kuna nini, kafanya nini.....?' profesa akauliza kwa wasiwasi akikumbuka kuwa waliachana na huyo kijana kwa kutokuelewana, na hakutaka kuwa karibu naye kwa hivi sasa kwani huyo kijana anaweza kumchukia kabisa kutokana na shughuli anazozifanya

'Hayo utayafahamu baadaye, muhimu ni hiyo kazi, kabla ya hapo ukumbuke hukunipa pesa yangu kwenye fungu la mwanzoni...na sasa unataka kulete shida....unanichosha, nilijua wewe utaifanya kazi hii ipasavyo, na ni kazi yenye pesa nzuri tu, lakini umeiharibu...'akasema mtaalamu

‘Nikuulize kitu, je una uhakika kuwa huyu mtu atazileta  hizo pesa nyingine...?’ profesa akauliza, na akahisi ukimia,..ila alisikia huyo mtaalamu akiongea na mtu mwingine upande huo wa pili.

'Nilikuwa napokea taarifa,....na inakuhusu wewe,....Ok, unasema....?' akauliza huyo mtaalamu

'Taarifa ya nini, mbona unanizidi kunichanganya,..sasa hivi umesema kijana wangu, hujaniambia kafanya nini, bado hujanijibu kuhusu uhakika wa kuzipata hizo pesa, whats going on...?' akauliza


NB: Naishia hapa kwa leo naona muda wa salio umekwisha...hali ni ngumu kidogo, lakini nitajitahidi kidogo kidogo tutafika


WAZO LA LEO: Tamaa mbele mauti nyuma

Ni mimi: emu-three

8 comments :

kolochatechee said...

hodi ni wewe katika haraka haja mkopo kulipia kuanza yako madeni ya kuanzisha biashara au nyumba ??? Kisha inakuja teksi kampuni una imani na relay juu ya 100% uhakika sababu hii ni kampuni ambapo i cashed mkopo wangu kwa mama yangu Stella dawa leo ili kuwasiliana na René Mikopo Firm halisi kupimwa na kuaminiwa na leo mimi nina furaha i got mkopo wangu wa $ 120,000 leo ili kupata kushikamana leo mrsstellareneloanfirm@hotmail.com} {barua pepe hapa chini na kupata jibu la matatizo yako yote kwa sababu Siwezi Kunyamaza ushuhuda huu mkubwa peke yangu binafsi ili i aliamua kuandika kwenye tovuti kwa sababu kula furaha kubwa kwa yangu moyo na leo mimi nina kuishi maisha mapya shukrani kwa wote Stella René


kolochatechee

Davidson Smith said...

Kampuni yetu ni shirika ya kisheria ambayo iliundwa kusaidia watu wanaohitaji msaada, kama vile misaada ya kifedha.
Hivyo kama wewe au wewe ni katika matatizo ya kifedha katika machafuko ya kifedha, na unahitaji fedha kuanzisha biashara yako mwenyewe, au unahitaji mkopo kwa kulipa madeni au kulipa bili yako, kuanzisha biashara nzuri, au kuwa na ugumu kukopa zaidi benki za ndani, wasiliana nasi leo
E-mail: davidsonsmithloanfirm@gmail.com

Maombi ya mkopo fomu:

Jina: _________
Mitaani: _________
Nchi: _________
Dini: _________
Kazi: _________
Mkopo Kiasi Inahitajika: __________
Lengo: _________
duration__________ mkopo
Mshahara kwa mwezi: _________
Simu: _________


Tafadhali wasiliana nasi kupitia barua pepe E-mail yetu:

davidsonsmithloanfirm@gmail.com

Mr Davidson Smith

Davidson Smith said...

Kampuni yetu ni shirika ya kisheria ambayo iliundwa kusaidia watu wanaohitaji msaada, kama vile misaada ya kifedha.
Hivyo kama wewe au wewe ni katika matatizo ya kifedha katika machafuko ya kifedha, na unahitaji fedha kuanzisha biashara yako mwenyewe, au unahitaji mkopo kwa kulipa madeni au kulipa bili yako, kuanzisha biashara nzuri, au kuwa na ugumu kukopa zaidi benki za ndani, wasiliana nasi leo
E-mail: davidsonsmithloanfirm@gmail.com

Maombi ya mkopo fomu:

Jina: _________
Mitaani: _________
Nchi: _________
Dini: _________
Kazi: _________
Mkopo Kiasi Inahitajika: __________
Lengo: _________
duration__________ mkopo
Mshahara kwa mwezi: _________
Simu: _________


Tafadhali wasiliana nasi kupitia barua pepe E-mail yetu:

davidsonsmithloanfirm@gmail.com

Mr Davidson Smith

Elena Nino said...

Je, wewe katika haja ya mkopo haraka ya kulipa bili, upanuzi wa biashara, miili ya ushirika au mkopo binafsi? Wasiliana nasi leo kwa ufanisi na kuaminiwa yako haraka mkopo leo katika kupitia barua pepe: elenanino07@gmail.com

Regards
Bi Elena

Anonymous said...

Je, wewe katika haja ya mkopo haraka ya kulipa bili, upanuzi wa biashara, miili ya ushirika au mkopo binafsi? Wasiliana nasi leo kwa ufanisi na kuaminiwa yako haraka mkopo leo katika kupitia barua pepe: elenanino07@gmail.com

Regards
Bi Elena

Finance Service said...

Salamu Kila moja.

i am Mr Paul Williams binafsi mkopo Taasisi, sisi ni vyombo vya kibinafsi kutoa kila aina ya mikopo kwa watu ambao ni kifedha chini na katika mahitaji ya msaada wa kifedha, sisi kutoa mikopo kwa kiwango nafuu sana bila matatizo yoyote. kampuni yetu ni vizuri kusajiliwa na uwezo wa kutoa mikopo kwa watu binafsi na kushirikiana miili katika mazingira mazuri. huduma zetu ni haraka na rahisi. kama wewe ni nia ya kupata mkopo kutoka kwetu kindly wasiliana nasi juu ya kampuni yetu email: paulwilliamsfinance@gmail.com

kutembelea sisi leo kwa ajili ya huduma zetu za kuaminika
Regards
Mr Paul Williams.
Kampuni pepe: paulwilliamsfinance@gmail.com
Wasiliana nasi sasa.

REMY.CREDIT said...

Habari
ni wewe kutafuta kwa msaada wa kifedha haja mkopo kulipia bili madeni kununua nyumba gari nk sisi kutoa kila aina ya mkopo na sisi kutoa mkopo katika 2% kiwango cha interst hivyo kama unahitaji mkopo wewe ni email yetu leo katika {REMY.CREDIT111 @ GMAIL.COM}
Fomu ya mkopo Maombi Kuwa Kujazwa Chini:

Fomu ya mkopo Maombi Kuwa Kujazwa Chini:

Jina la kwanza:......................... ....
Jina la familia:......................... ....
Nchi: ...................... ..........
Jimbo ........................ .............
Kiasi: ....................... .........
Mkopo Duration: .....................
Nambari ya simu:.....................
Idadi Fax: ........................
Kazi: ................... .......
Tarehe Ya Ku Zaliwa:......................
Mapato kwa mwezi: .................
Jinsia: .......................... .........
kuwa na wewe kuomba mkopo kabla? ..................

Sisi kusubiri jibu lako katika barua yetu [REMY.CREDIT111@GMAIL.COM}
THANKS na Mungu akubariki

Bob Britten said...

Siku njema,
Je, unahitaji haraka mkopo kuanza
up biashara, au unahitaji mkopo
kwa refinance, Je, unahitaji mkopo kwa
kulipa deni? Je, unahitaji mkopo
kununua gari au nyumba? Kama ndiyo wasiwasi
tena, Tunaweza kukusaidia !!! mawasiliano
nasi sasa kupitia E-mail kwa haraka yako
mkopo.
E-mail:
davidadelekeloancompany@yahoo.com
Asante.
Mr David Adeleke
-