Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeThursday, July 16, 2015

RADHI YA WAZAZI-20


‘Pamoja na hilo kuna mengine nataka akifika wakili wa familia yetu tuyaweke sawa, kuna mambo muhimu nahitajia yaingie kwenye makubaliano yetu, kiukweli mume wangu sikuamini tena, kutoka na matendo yako,a zaidi unazidi kunidanganya..’akasemamkewe

‘Kwani mke wangu nimekudanganya nini hapo, na hayo mengine ni yepi,  au kuna kitu gani umesikia mke wangu...majungu ya watu?’ akauliza mumewe akionyesha wasiwasi na kama kukerwa

 ‘Kiukweli sio swala la kusikia, ila nimejionea mwenyewe na kuziona nyendo zako kwa macho yangu, na kwa vile mimi ni mtu mzima,siwezi kusubiria tatizo liingie ndio nianze kuhangaika, kwa ufupi mume wangu...sikuamini tena, sikuamii, sikuamini...’akasema

‘Huniamini...mmmh, ina maana mke wangu  umefikia hatua hiyo...’akasema kwa hamaki,

Tuendelee na kisa chetu

**************

Mume alirudi kwenye kiti akakaa ,halafu akasimama, na akilini akawa anasikia sauti kama inalia kwenye simu ikisema,

Kwahiyo unataka tupeleke nakala moja ya hizo picha chafu kwa mkweo.....unasemaje ili uone kuwa hawa watu hawaogopi...au tumpe mkeo nakala moja tu, ili ajue jinsi gani mume wake alivyo...’

‘Labda mke wangu keshatumiwa nakala ya picha, ndio maana kafiki hatua hii, yanaonekana kama kuna kitu kaambiwa, sio bure....’akawa anawaza akilini

Mume wangu nilikupenda sana...nikawa nipo tayari kupata shida kwa ajili yako,nikijua na wewe mwenzangu upo hivyo hivyo...’akasema mkewe

Ulinipenda, ina maana.....’akasita

‘Kutokana na hayo, nahisi kupenda kisichopendeka,nahisi  kuwa mwenzangu una lako jambo,....lakini tumeshazaa tuna watoto wakubwa, ..hata hivyo, hakijaharibika kitu,...muhimu nataka wakili akija, tuyaweke haya bayana,na mimi niwe na amani ....’akasema

‘Lakini mke wangu sizani kuna haja ya hayo yote...mimi nakuamini mke wangu, na wewe uniamini pia...mbona mimi sikutilii mashaka yoyote....’akasema

‘Nilihisi huenda nikupe muda, na kama ungeniambia ukweli wote, mimi ningelichukulia kuwa umekosea kama binadamu,...ningeyasahau hayo yote ...lakini jinsi ulivyonijibu na jinsi unavyoendelea kunificha ukweli, hukutaka kukiri kuwa umekosea, yaonyesha wazi, kuwa kweli umedhamiria ...’akasema

‘Lakini nimeshakuambia kuwa kuanzia sasa sitakwenda huko kwenye bar tena, na nilikuwa nakwenda kunywa tu, unajua tena mabinti wa pale ni wacheshi tu, na sikuwa na lolote kwao, nakunywa, wanajipitisha mimi siwajali, nikimaliza kunwya naondoka zangu....na pia hiyo akaunti ilikuwepo tu , na kuitumia ni kwa dharura tu, na nimeaidi kuanzia sasa tutaiweka wazi....sihitaji tena kuitumia, hilo halitoshi...’akasema

‘Mume wangu....kwa kauli yako hiyo na matendo yako hayo, sasa naanza kuwaamini wazazi wangu,.....’akasema

‘Kuwaamini kwa vipi...?’ akauliza

‘Ukumbuke, nilikubali tuoane, japokuwa wazazi wangu hawakuwa radhi nawe...nikafanya hilo kwa vile nilikupenda sana, lakini kumbe mwenzangu una lengo lako,...huko kwenu umeshaanza kujenga, kwa jina la mdogo wako,..utakataa na hilo, badala ya kujenga kwa jina la wanao, unajenga kwa jina mdogo wako....’akasema

‘Nani kakuambia uwongo huo...’akasema akitoa macho ya kushangaa

‘Hahaha, unashituka eeh, hilo ni moja ya mengi niliyoyagundua, kwa muda mfupi tu.....najua kuna mengi umeyafanya,...mimi sijali, muhimu tu tuingie kwenye hayo makubaliano...’akasema

‘Mkewangu sasa huko umefikia kubaya, kama wewe unaamini kila kitu,  unachoambiwa,,,huo ni uwongo ukweli ndio huo niliokuambia, sielewi kwanini ukafikia hatua hiyo, hebu nambie kuna nini kinaendelea, ...?’ akauliza akimuangalia mkewe kwa macho ya ukali japokuwa mashaka yalikuwa yememjaa.

‘Mume wangu, maisha ya ndoa ni makubaliano,na muhimu sana ni uaminifu, ndio maana wanandoa wanaopendana kiukweli hawana haja ya kufuatiliana, kwanini wafuatiliane wakati kila mmoja yupo ndani ya mwenzake..kila mmoja anamuamini mwenzake, na kila mmoja anajichunga ....’akasema

‘Hilo..hi-hilo, ni kweli kabisa, na mimi nimejitahidi sana kufanya hayo, ..nikuulize mke wangu kwanini sasa huniamini, kwani kuna kitu gani kimetokea hadi ufikie huko kote,....ni nani kakuongopea,hadi kufikia kuamini yote hayo..?’ akauliza mume mtu, lakini mke mtu akaendelea kuongea

‘Tulipofika hapa Ulaya, nilijua tutaishi maisha ya amani, tuwe na uhuru, ....maana kama ulivyoona kule nyumbani, wazazi walikuwa wakitufuatilia kila tunalofanya, nikaona nitakuwa sikutendei haki, kwani ulikuwa kama mfungwa ndani ya family yangu,...ndio nikaona tuje huku, ili tuwe na uhuru, tuwe tunaweza kufanya mambo yetu kama mke na mume kwa amani a upendo..., ilimradi yasikiuke masharti ya ndoa....’akasema mkewe

‘Ni kweli kabisa mke wangu, hata mimi nashukuru sana kwa maamuzi hayo, na mimi nakuahidi nitajitahidi kufanya yote kwa matakwa ya ndoa yetu na kama kuna kitu kimekengeuka, naahidi nitakiacha, si unaoana sasa nimeamua kuacha pombe,...nitakuwa nakunywa hapa nyumbani tu...’akasema

‘Unajua wahenga husema kunguru hafugiki, tabia ya mtu kubadilika ni nadra, atajifanya anaficha makucha yake kwa muda,  lakini muda utafika, atakumbukia ubaya wake...kiukweli waliyosema wazazi wangu sasa naanza kuyaona moja baada ya jingine....’akasema mkewe

‘U-u-meona nini...huo uwongo ndio umeona, unajua ni nini kimesababisha yote hayo, unafikiri mimi nimependa...’ akasema lakini akawa kama kashtuka hakutakiwa kusema hivyo.

‘Huo sio uwongo, ...nimethibitisha mwenyewe, na kama ilikuwa ni bahati mbaya kwanini uendelee kukana, kwanini hukiri makosa, ....ina maana umedhamiria, ina maana hata hayo niliyoambiwa dhidi yako ni kweli,....unataka ushahidi mwingine nikutolee....’akaambiwa

Mume mtu aliposikia hayo maneno, moyo ukaanza kumdunda,...akahisi huenda jamaa wameshaanza kutoa siri kwa mkewe, na kama wamefanya hivyo, moyoni akaapa kuwa atawatafuta hao watu mpaka awapate,...maana alishawapa pesa, na akawaahidi kumalizia pesa nyingine akikabidhi nyaraka za benki, sasa kwanini wamamsaliti.

‘Ushahidi...!? ushahidi mwingine.....?’akawa kashikwa na kigugumizi

‘Mume wangu kwa jinsi ninavyoona wewe sasa unahitaji uhuru uliopitiliza, uutumie huo uhuru uutakavyo si ndio...., inavyoonekana mimi nakubana sana..unahitaji namna nyingine ya maisha, ..., ‘akatulia

‘Ha-ha..pana,hivi hivi mke wangu,...naona kama unanitisha,...’akasema

‘Sikutishi, kwanini nikutishe na wewe ni mtu mzima,  wewe uliwahi kusema kwa vile ni mwanaume  unataka kufanya utakavyo,...sawa, nilikubali hilo, ndio maana sikujali, nikikuona unakunywa, unaongea na wasichana wako, niliona huenda ni moja ya starehe zako nikawa nakuacha tu..nikijua ni swala la muda, ndio uanaume uutakao, si ndio ....’akasema

‘Mke wangu nikuambie kitu, yaani kunywa, na hayo mengine ni kupoteza muda tu,hakuna kitu kibaya nimefanya, haki mungu, sijawahi kufanya lolote baya, nakuapia...unataka nifanye nini ili uamini’akasema lakini mkewe hakumpa nafasi akaendelea kusema;

‘Nimekuwa nikipita pale kwenye bar, nakuona unakushikwa shikwa...mimi kama binadamu naumia, lakini nikaona nikuache tu, ilimradi isiende mbali...najua huenda, ni kwa vile nimekuwa na kazi nyingi, sipati muda wa kutimiza yote....basi nikaona nikupe uhuru huo, si unataka uzungukwe na wanawake, wakushike shike,...basi nikajipa moyo..nikijua hayo yatakwisha tu...’akaendelea kusema

‘Lakini mke wagu nimeshakuambia kuanzia sasa ulevi basi sitaenda tena huko kwenye bar...nikitoka kazini nakuja hapa mimi na wewe tu...’akasema

‘Najua ....yameshakufika shingoni, najua uliyotaka kwa hao wanawake, yamegeuka kuwa shubiri kwako, nilijua itafika muda utagonga ukuta...najua kabisa hao wanawake walikuwa wakifanya hivyo kwa malengo yao binafsi..’akasema mkwewe akionyesha sauti ya kukata tamaa.

‘Lakini mke wangu sijafanya ubaya wowote...mbona hunielewi, kwanini wanifanya kama mtoto mdogo, haya sema unayotaka kusema...’akasema sasa kwa hasira

‘Kwangu mimi sasa nimeona  nisikufuatilize zaidi, wewe sio mtoto mdogo, na kwa vile wewe unachotaka ni mali, uhuru, starehe, ngoja nikupe hicho unachotaka, lakini ....’akasema sasa kwa sauti ya kuonyesha ukali

‘Unataka kusema nini...’akauliza

‘Kiukweli nimegundua kitu, wazazi ni muhimu sana katika maisha yetu,hilo nimeliona,..na nlitaka tukiishi vyema, tukaaminiana, basi siku twende tukawafurahishe wazazi wetu waone kuwa kweli tunapendana, kuwa kweli, wewe sivyo kama walivyokuwa wakikuwazia...’akasema akiangalia saa ya ukutani, akachukua simu na kupiga, lakini hakuongea kitu, akairudisha mezani

‘Mhh...hilo ni muhimu sana, tutakwenda tu mkewe wangu mambo si hayo,....’akasema sasa akihisi mkewe hakuwa na nia mbaya.

‘Lakini,mume wangu yale wazazi waliyokuwa wakinionya kuhusu wewe na historia ya familia yako,naanza kuyaona moja baada ya jingine...kweli tabia ya mtu inaonekana pale anapopata...’akasema sasa akiwa kamkazia macho mume wake

‘Mhh, sijakuelewa, una maana gani...?’akawa anahisi kukojoa

‘Kweli nimeamini, wazazi sio watu wa kupuuza, maneno yao unaweza ukayazarau kumbe yale maonyo yao yakawa kama  laana kwako,hata wasipotamka kitu laana, lakini kauli zao zinafinya....’akatulia

‘Mhh, unafikia mahali  unasema aheri ningewasikiliza wazazi  wangu,na sasa nakiri na najuta, kumbe ningeliwasikiliza wazazi wangu, haya yote yasingelitokea....’akasema

‘Mke wangu niambie kuna tatizo gani...?’ akaulizaa kwa hasira

‘Usijali, wakili anakuja...nimeshayaanisha yote muhimu, ..natakupa nakala yako uipitia, ili kama kuna tatizo, au kuna kitu nimesahau, ..uniambie, nia ni wewe uwe huru, ufanye utakavyo, lakini  ...’akatulia

‘Mhh...’akaguna  mume mtu

‘Nataka wakati nakupa nakala hiyo, wakili awepo, , yeye  alishayapitia, na ameyaona kuwa yote yana msingi, ..ila kukumbusha yote hayo ni kutaka wewe ukumbuke wapi tulipotoka, nataka ukumbuke mapenzi yangu, jinsi nilivyojitolea kwako, ...nisigelifikia hatua hii, ...’akasema

‘Hata laana ya wazazi isngelituathiri...napata taabu, sifanikiwi,naishi kwa mashaka, hakuna mafanikio, ni maisha ya shida tu..hii ni kwasababu wazazi hawana  furaha nami kwa maamuzi haya, na waliniambia mtoto akililia wembe muache atajikata tu ataona ubaya wake mwenyewe..’akasema

‘Kiukweli nafahamu kabisa ndoa yetu haikuwa na baraka za wazazi...na sasa naanza kuipata pata,lakini sasa...tuyaache hayo...ngoja wakili aje, najua tutayamaliza, ili kila mtu ajue lake...’akasema

‘Mke wangu ina maana....kwa-kwa-kwani vipi, ....?’ akawa anauliza na mara mlango ukagongwa, na aliyeingia na briefcase alikuwa ni wakili wao wa familia
Mume akanywea, na aliyeongea kumkaribisha wakili alikuwa mke wa familia, akilini mume alijua hapo sasa hana chake, ,...huenda huenda.......

NB Je kuna nini kwenye hayo makubaliano


WAZO LA LEO: Upendo wa mali, upendo wa kudanganyana, upendo wenye malengo ya ubinafsi, una mipaka yake,kamwe hautaweza kudumu, lazima itafikia siku ukweli utadhihiri, na upendo huo utageuka kuwa ni chuki. Tujitahidi kupendana kiukweli, ili kuleta neema kwenye familia. 
Ni mimi: emu-three

No comments :