Ilikuwa ni
kijiji kingine profesa akiwa na kijana wake walifika kwenye kiunga cha makazi
ya familia mojawapo kwenye hicho kijiji, na wakapiga hodi, lakini kulikuwa
kimia kama vile hakuna watu, yawezekana wakazi wa hapo walikuwa mashambani kama
alivyofikiria huyu profesa
‘Dad, lets go back, ...there is no life here....wewe
huoni wamehama, hakuna mtu hapa, ...you
see dad,.... mtu anawezaje kuishi mahali kama hapa....’akasema kijana
akikagua kwa macho mazingira ya eneo hilo.
‘Mhh,
kijana, kua uone...hapa ndipo ulipozaliwa, nikuambie kitu hapa ndipo unatakiwa
uonyeshe adabu zako...humu, ndipo mama
yako anapoishi ndiye aliyekubeba miezi tisa tumboni, sasa ukitaka uharibikiwe,
cheza na mama yako....’akaambiwa.
‘I don’t know, whoever ...mom, or dad, mimi
sioni tofauti,...mimi najua kuwa mimi ni yatima, ulisema wakati nasoma, mimi ni
yatima, sasa unanielezea haya, mimi sikuelewi...halafu hao wazazi, mbona
hawaelekei kuwa ni wazazi wangu, hatufanani kabisa na wao...hapana, unataka
kunitia majaribuni...am very sory, I I don’t like them...’akaongea yule kijana,
ni mwepesi wa lugha tu.
‘Unaona
Kiswahili chako sasa kinaanza kuwa safi...thats
how I want you to be, like me, nafahamu lugha nyingi tu...na hatimaye
utakuwa mswahili, utakuwa mtanzania halisi, unasikia wewe sasa ni msomi, maana
unajua kiingereza, nchi msomi ni yule anayejua lugha, hasa kiingereza, unaona,
ukimaliza shule huko nje unakuja hapa nchini kwako, unakuwa mkurugenzi,....but you have to promise me one thing....’akaambiwa
lakini alionyesha kama kupotezewa muda wake, akasema;
‘Sitaki
kabisa ....i don’t like to be
mswahili.....my language is English,
na there...., is where I belong...nitarudi huko nilipokuwa
nasoma na sitarudi huku tena....’akasema. Na profesa akamuangalia kwa makini
halafu akasema;
‘This is your country boy, whether you like
it or not, unasikia huku ndio kwenu, huko ulaya ulikwenda kusoma tu....sasa
sikiliza....’akasema yule profesa na yule kijana akawa katulia tu.
‘Sikiliza
nataka uniahidi kitu kimoja, kuwa utafanya ninavyokuelekeza,...kama nilivyokuelekeza,...wewe
hutaki pikipiki....sasa sikiliza ukiwa huko nje, huko wewe ni yatima, tulifanya hivyo ili upate
elimu, ni ujanja, ndio maisha yetu, ujanja ujanja....’akasema na kijana
akanyosha mkono wa kuyapuuza hayo.
‘Ndio hivyo,
kama nisingelifanya hivyo ungesoma wewe, ona hapa ndipo ulipozaliwa, ungewezaje
kufika ulaya..hebu tumia akili yako,....sasa muhimu, ukirudi hapa hasa eneo hili, unahitajika uwatambue
wazazi wako, japo .....’kabla hajamaliza akasikia mtu akikohoa nyuma yao, wote
kwa pamoja wakageuka kuangalia.
Alkuwa ni mama
mmoja akiwa kashika fimbo, kwa jinsi anavyotembea, ilionyesha dhahiri haoni,
ila anatumia fimbo kama kiongozi wake, na kwa muda ule alikuwa akija muelekeo
wao,...na kwa mbali kulikuwa na watu wengine wanakuja, yule mama alipokaribia
pale waliposimama, ghafla akatulia, akasimama, na wale watu walikuwa mbalia
wakawa wamemkaribia,
‘Kuna
wageni, .....au wamepotea njia...’sauti ya wale watu wengine ikasikika ikisema
‘Mhh,
wanatoka wapi hawa watu..yule kama mzungu-koko.....’sauti ya mwanamke ikasema,
ni kweli huyo profesa, alifuga nywele akazitegeneza ki namna, akazifunga kwa
nyuma, huwa ana nywele ndefu na kwa vile alikuwa mweupe, wengi walimuona kama
ana damu ya mchanganyiko.
Wale watu
wengine wakawa wamafikia huyo mama, na sasa wanawaangalia hawa wageni
waliosimama kwenye njia ya kuingilia kwao, wakajua hao watu yawezekana ni wageni wao, na kabla
hawajatoa kauli ya kukaribisha au salamu, yule mama aliyekuwa kashika fimbo
akatamka maneno yaliyowafanya wote kuduwaa.
‘Nahisi
ishara ya mwanangu...nahisi.....mwanangu amekuja....mwanangu,umekuja mwanagu....’huyo
mama akasema na sasa akawa anakuja muelekeo wa pale aliposimama huyo kijana, na
huyo kijana kwanza alishikwa na butwaa, lakini alipoona yule mama anamkaribia
akamkwepa.
Kwa muda ule
wale watu wengine walikuwa wameshafika karibu na hao wageni, wamesimama,
walkuwa akina mama wawili na mzee mmoja mwanaume, na wao wakawa wameduwaa kuona
kile kitendo kinavyoendelea pale
‘Who is this
dad....is she ok, ....she is blind...whats she wants from m......’akasema yule
kijana akionyesha wasiwasi.
‘Mhh, she might be your mother....’akaambiwa
‘What.....i can’t believe this....’akasema
huyu kijana sasa akiwa kasimama mbali na yule mama, akawa anamuangalia kwa uso
uliojaa mshangao.
‘Do what I told you....’akaambiwa na ile
sauti ya profesa ilimfanya yule kijana sasa asimama, huku akionyesha hali ya
wasiwasi akimuangalia huyo mama kwa tahadhari, na yule mama akamsogolea, na kunyosha
mkono wake had ikashika kichwani mwa huyo kijana.
Yule kijana
akamuagalia profesa akitaka kufanya jambo , hakupeda kabisa hicho kitendo
anachofanya huyo mama, aliona kama anachafuliwa nywele zake, lakinii akaona
ishara kutoka kwa profesa kuwa atulia, na yule mama akaanza kumpapasa ule
kijana kichwani na mkono ulianzia kichwani, na ukawa unashuka hadi usoni,na
kijana yule alionekana kama anasikia vibaya, lakini akawa anafuata
alivyoelekezwa na profesa.
‘Oh
mwanangu, umekuja,..nilijua tu kuwa upo hai...umekuwa mkubwa kiasi hiki,
masikini....nisamehe mama yako, yaliyotokea siku ile sio matakwa yangu,
sikupenda kukuacha uchukuliwa....’akasema huyo mama.
Yule kijana
hakuvumilia tena, taratibu akaushika mkono wa huyo mama na kuondoa mwilini
mwake,....akasogea mbali na huyo mama, akionyesha hali ya kutahayari, na huyo
mama akasema;
‘Mwanangu,
umerudi mwanangu.....nisogelee mwanangu, leo nilikuwa nahisi utakuja,.....ila leo
sijisikii vizuri...naogopa hali mbaya yaweza kunitokea, lile balaa liloanya
nikupoteze, oh, oh,....’akasema huyo mama, na haikuchukua muda kweli huyo mama
akaanza kutetemeshwa na kabla ndugu zake hawajamfikia kumshika akadodoka chini,
na kuanza kutikisika a kama kujinyonga nyonga.. na haikupita muda akawa anatoa
mapofu mdomoni
Yule kijana
kuona vile, hakusibiri cha profesa wala cha nani, akatimua mbio, na kupotelea
msituni, na profesa, ambaye alikuwa akimuangalia yule mama, hakujali kumuangalia
yule kijana alivyokuwa akikimbia...yeye kwa haraka akamsogelea huyo mama, pale
alipolala, akatoa dawa zake alizokuja nazo;
‘Mnaweza
kunipatia maji ya uvugu vugu, kama yapo, kama hakuna nipeni maji tu ya
kawaida...’akasema na mama mmojawapo akafanya hivyo, akamletea huyo profesa
maji, na yule profesa akatoa dawa ya unga unga, achanganya na maji, halafu
akasema;
‘Nisaidieni
tumpe dawa hii itamsaidia, atapona...’akasema huyo ptrofesa na wale watu wakamsaidia kumuiua
huyo mama, na kupanua mdomo wake na huyo mama akapewa hiyo dawa, akanywa, na
haikupita muda, huyo mama, akainuka , kwanza akawa anashangaa, na kuuliza;
‘Kumetokea
nini...? ‘ akauliza na alipoona watu wamemzingira, akaiamisha kichwa a baadaye
akasema
‘Ooh, ni huu
mtihani tena, ooh, mungu wangu lini nitaachana na hii adhabu,....eeh muu wangu,
naomba uichukue tu roho yangu nisizidi kuadhirika hivi, maana nikidondka
sijijui, sijui.....kinachoendelea, mungu wangu nakuomba...nakuomba... nimechoka
kutaabika na kuadhirika, ...’akawa kainamisha kichwa chini akilia na mama yake
akamsogelea na kumshika mgongoni akasema
‘Mwanangu
usiseme hivyo, utapona tu,...mbona sisi tupo pamoja na wewe, huu ni ugonjwa
utapita, na utasahau...’akasema mama yake akiwa kama na yeye anataka kulia
‘Mama lini
nitapona,....wewe mwenyewe unaona miaka mingapi sasa nateseka....mume kaniacha
kwasababu hii hii, mtoto naye.....ooh mungu wangu nina nini tena katika hii
dunia, nimeshaadhirika, nimeshadhalilika, na walimwengu wameshanidharau, na
kunipuuza....nimekuwa mgumba, kipofu, na hili gonjwa lisilo na dawa.....jamani....na....’ghafla
akatulia akageuza kichwa kuangalia huku na kule, japo kuwa haoni, lakini
alikuwa kama anatafuta kitu.
‘Mwanangu
yupo wapi...?’ akauliza akigeuka huku na kule
‘Mwanangu
yupo wapi huyo ndiye burudiko la moyo wangu kabla sijakata tamaa ya mwisho,
kabla sijafariki, nataka mwanangu awe karibu yangu, mwanangu yupo wapi,
nimemuhisi, nimemgusa kwa mikono yangu mwenyewe....’akasema, na profesa akawa
anaweka dawa zake kwenye mkoba, akauliza
‘Ina maana huyu
mama haoni....?’ akauliza profesa
‘Ndio
...alipoteza uwezo wa kuona kutokana na kukaa ndani akiomboleza kupotelewa na
mtoto wake....’akasema mama mmojawapo
‘Haiwezekani....ina
maana upofu huo umetokana na kupotea kwa mtoto wake, kwani hamna uhakika kuwa
mtoto wake yupo hai, kwanini aomboleze wakati huenda, au ana uhakika gani kuwa
mtoto wake keshafariki...’akasema profesa
‘Mtoto wangu
hajafariki,.....nina uhakika....alikuwa hapa muda mfupi uliopita...’akasema
yule mama mgonjwa kwa hasira, na wote wakatulia, na aliyevunja huo ukimia
alikuwa mama wa huyo mama mgonjwa,akasema;
‘Mtoto wako
yupo wapi, tumeshakuambia sahau hilo usimkufuru mungu... miaka mingapi imeshapita,
karibu kumi na sita au kumi na saba sasa, kwa muda wote huo kama yupo hai, yupo
wapi,...’akasema huyo mama
‘Mhh, na
nahisi ...’profesa akawa anaonyesha kwa vitendo kuwa huenda huyo mama
kachanganyikiwa
‘Kiukweli
imekuwa kama hivyo, ....kaomboleza kupita kiasi, yeye anadai kuwa ana uhakika
mtoto wake yupo hai....sisi tumeshakata tamaa, na tunajua kuwa hueda
keshafariki....’akasema na kabla hajaendelea kuongea kuongea, yule baba mzee,
akasema
‘Hebu
tuambie, unafahamu lolote kuhusu mtoto wa huyu mama?’ akauliza huyo baba mzee
‘Yaonekana
kama una jambo lakutuambia...tuambie wewe, kama unafahamu lolote, maana
kiukweli kupotea kwa mjukuu wangu imekuwa pigo kubwa kwetu, ni miaka mingi,
lakini hata mimi naendelea kumuota, mara namuona, lakini nikimuita ananikimbia,
anasema hanijui, hebu tuambie una lolote la kutuambia, ....?’ akauliza mzee
aliekuwa kaongozana na hao akina mama, kumbe huyo ndiye baba wa huyo mama
mwenye matatizo
Profesa
akageuka kuangalia kule alipokimbilia yule kijana alijua yupo sehemu kajificha,
lakini hakutaka kumfuata akasema;
‘Mhh,
kwakweli sina la kuwaambia, na sijui lolote kuhusu huyo mjukuu wako..., lakini
ngoja ipo siku nitakuja mtanielezea
vizuri, nitaona jinsi gani ya kusaidia....leo sina muda wa mangezi, leo
nilikuja kuleta dawa za huyo mgonjwa....., tutaongea siku hiyo...,’akasema
‘Tunashukuru,
....’akasema mama wa huyo mama mgonjwa
‘Matumizi
yake, ..ni dawa ya unga, kijiko kimoja kwenye maji ya moto..uvuguvugu, kumpa huyu
mama mgonjwa, kila siku asubuhi kabla
hajala kitu na akilala kwa siku saba mfululizo bila kukosa..zitamsaidia, ni
dawa nzuri za matatizo kama hayo...’akasema
‘Na yule
kijana aliyekimbia ni nani?’ akauliza mmojawapo wa hao akina mama.
‘Mhh, ni
kijana wangu tu.....’akasema profesa akikwepa kuangalia na hao watu
‘Na wewe ni
nani mbona sikukumbuki....ni mgeni kabisa machoni mwangu....?’ akauliza huyo
mzee mwanaume
‘Mhh, ...labda,
.....ila mimi naitwa ...eeh, wananiita profesa...’akasema
‘Profesa,
ndio jina lako hasa...mimi namfahamu mtu mmoja kwa jina hilo, alipewa hili jina
kutokana na kufanya mazingaumbwe, ...mmh anatokea kule alipokuwa kaolewa huyu
binti yangu, na tulisikia huyo mtu alikamatwa na madawa ya kulevya huko uchina akanyongwa...’akasema,
na profesa akatikisa kichwa na kusema
‘Mhh, mimi sijui...haya
jamani kwaherini, mimi nilikuja niliposikia huyu mama anaumwa,...na kwa vile ni
mtu ninayemfahamu, nikaona nimsaidie...sihitaji malipo yoyote kwasasa, kama
atapoa, mtafikiria cha kunipa, najua atapona...niwaulize tu kitu
kimoja...’akatulia
‘Wewe
umetokea wapi....?’ akaulizwa na yule mama mwingine
‘Je kwenye
historia zenu, kuna mtu alikuwa anaumwa, yaani, baba zenu, babu..mliwahi
kusikia ugonjwa kama huo kwenye familia zenu...?’ akauliza profesa
‘Hakua hata
mmoja, ugonjwa huu umetokea huko huko kwa mume wake...’akasema mama mtu
‘Basi
atapona.....kwa hivi sasa naomba niondoke, si mnaona kijana wangu
kakimbia,..anaogopa, ...tutaongea nikija tena...na kuangalia hali ya monjwa...’akasema
akigeuka kuondoka, akamtupia yule mama mgonjwa jicho, na yule mama kwa muda huo
alikuwa kasimama akiwa kaelekeza uso wake kule alipokimbilia huyo kijana na
huyo mama akasema;
‘Wewe mtu,
nashukuru kwa dawa zako, lakini umlete mtoto wangu, najua ni wewe uliyemchukua...’akasema
huyo mama kwa sauti nzito yenye msisitizo na ukali, na profesa akashituka
kidogo, akataka kusimama, .... lakini akasita na kuendelea na safari yake, akaondoka
akielekea kule alipoelekea yule kijana wake.
WAZO LA LEO: Kuna watu wanahisi maisha ya ujanja
ujanja, kudanganya na kupata hata kisicho halali yao kiujanja ujanja , na
wengine hufikia kusema ni mungu kapanga iwe hivyo,..au ni elimu, au ni ujasiri,
...na wengine wanafikia hata kujenga kutajirika kwa hali hiyo. Huo sio ujanja,
hiyo si elimu, huo ni wizi...hiyo ni dhuluma, na utakuja kuulizwa kwa hao wote
uliowatendea hivyo ukapata kwa kupitia migongo yao, hilo deni mbele ya mungu.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment