‘Kuna kazi moja, ikifanikiwa
utaingiza ,dola laki moja na elifu hamsini,kama kianzio unazipata bila ubishi,
na hapo ushanilipa ushuru wangu....
‘Na kila mwezi kama kawaida utapata elifu
hamsini, kwa miezi kama mitatu,...au hata thelathini, ukimuhurumia,...na
hushuki zaidi ya hapo,...mimi unanipa zangu kumi kumi kila mwezi kwa miezi hiyo
mwili,zaidi ya hapo sitaki, kwangu zinatosha ....’akasema akijizungusha kwenye
kiti chake.
‘Unaona ilivyo,...baada ya mikupuo
mitatu, wakati bado anahaha,....unampa unafuu, mimi naachana na wewe, unabakia
wewe na mwenye kisima,maana si umeshamfahamu, nazimamitamb yangu, unafanya vitu
vyako,ukitaka....mpaka utakapohakikisha kisima kimekauka, ni wewe tu na njaa
zako...’akawa anasikia mtaalamu akiongea kichwani mwake.
‘Dola lakini na hamsini, kianzio tu,na
badoo kila mwezi nakinga mkono..ohooo,mungu anipe nini...’profesa akawa anawaza
akielekea sehemu alipoelekezwa...
Tuendelee na
kisa chetu
***********
Ni kweli
sikutarajia kuwa kazi hiyo itakuwa rahisi hivyo,mtu niliyeelekezwa kwake kweli
alionekana kuwa ni mgeni, na alionekana kuipenda familia yake..., ila pamoja na
hayo alionekana kutamani mabinti, kwa jinsi alivyoonekana hakutulia, ilikuwa ni
swala la kumtega tu...
Tabia hiyo
ya kuoenakana kupenda mabinti, ilioenakana wazi,na mabinti wakawa
wanamchangamkia wakitaka kumpukutisha alicho nacho mfukoni, lakini walisema
jamaani bakhili kutoa kilicho mfukoni
ni mgumu sana,...
Lakini kwa
watalaamu wa kusoma watu kama hao, wakaona kuna njia nyingine ya kumtoa hizo pesa
alizo nazo,...,na kwa vile anaonekana mwingi wa mabinti, na kupenda kunywa,
wajanja wakaona watumie udhaifu wake huo.
Ndipo
mtaalamu akamchunguza na kugundua kuwa huyo jamaa anaingilika, na kwa uzoefu
wake wa watu kama hao, ni rahisi sana kuingizwa kwenye mtego, na akajikuta
anatoa pesa nyingi tu bila kupenda...
Mtaalamu
alinielekeza jinsi gani ya kufanya, na yeye alishakwenda mbali zaidi hadi kujua
jamaa ana kiasi gani benki, na matumizi yake kwa siku, na jinsi gani alivyo
mbele ya familia yake, na tabia yake na familia yake...
‘Hii familia
ina pesa,benk wana akiba kubwa tu, ya pamoja, na kila mmoja pia ana amana yake
binafsi kuacha hiyo ya pamoja, ya mke ipo wazi inajulikana kwa mume,...
‘Na huko
kwao, wanapotoka, wana miradi, na mingi inatokana na familia ya mke,...mke yeye
alisomea huku ulaya, na akarudi kwao kufanya kazi,baadaye akakutana na huyo mwanaume,
wakapendana wakaoana,lakini familia ya mume ni ya kimasikini tu...
‘Kwahiyo
utaona jinsi gani mke alivyo na nguvu, sio tu kwasababu ya taratibu zao, lakini
pia kipesa..na kuoana kwao ni kutokana na mapenzi yao wawili, familia ya mke
hakupendezewa binti yao kuolewa na familia ya kimasikini, lakini binti
alishapenda,....unaona ilivyo....’akasema
mtaalamu
‘Basi mume
akawezeshwa, akasomeshwa zaidi, wakawekezewa, wakajijenga,..hata hivyo kwa vile
binti kasomea ulaya, akaona aje huku ili wawe mbali na familia, na kufanyia
kazi huku...kalowea ulaya
‘Basi binti,
akaomba kazi huku akapata kazi,..na kwa mgongo wa binti,na mume naye akapata
kazi...sasa mdondo wetu ni mume...huyu ndiye mlango wa kuipata hiyo hazina,hazina
waliyoihifadhi, ..’akasema mtaalamu akijilamba lamba na ulimi.
‘Ipo wapi
amana yao,....?’ profesa akauliza
‘Amana zao
zote ni za kimataifa kokote wanaweza kuchukua,na mume ana uwezo wa kutoa pesa
hata bila kumshirikisha mkewe,...ila kwa upendo na ushirikiano,kila akitoa pesa
nyingi, wanafanya hivyo baada ya makubaliano...’akasema
‘Sasa
atawezeje kutoa laki na hamsini, kwa mkupuoa...?’ akauliza profesa akionyesha
hamasa
‘Mume ana
akaunti yake binafsi, ambayo hata mke hajui,...humo ana dola nyingi tu, humo
anaweza kutoa hata dola laki moja kwa mkupuoa, na akiongezea kwa mkewe, itafika
na lakini na hamsini,...sijui kwanini hiyo amana yake hajamuhusisha mkewe, japokuwa ya mkewe anaifahamu...tunahisi
anamuibia mkewe na kuwekeza huko ili kukitokea lolote aweze kuwa na kianzio...’akasema
mtalaamu.
‘Unahisi
hajiamini,hampendi mkewe..wanaishi kwasababu ya mali tu.....?’ akaulizwa
‘Unajua kuna
kitu nikuambie,mapenzi yapo ya namna nyingi, kuna ya pesa na kuna ya kiasili, kuna
yanakuja tu, ...hawa kwa kiasi kikubwa ni pesa, na mke,....’akasema profesa
‘Na kosa kwa
mke, yeye, ...karizika, na kajiweka tu, kajaziana...unaona alivyo nenepa, sasa
bwana,mmmh,kaona vimwana wa huku ulaya, virika njia,..., si unajua vimwana wa
huku wanavyojua kuweka miili yao,....kavutika, hana jinsi,...anatamani,...japo
anajifanya hamnazo...siri kubwa, awali
ni awali,tusimchelewe,akijanjaruka atakuwa makini sana,siomjinga kihivyo...’akasema
‘Kama ni
hivyo eeh, haina shida...’akasema profesa
‘Sasa kwanza
la muhimu ujenge ukaribu na hiyo familia, ili mitego ukikamilika ujue jinsi gai
ya kumtisha,...si unajua....kama ulivyo cheza na mama, hahaha, japokuwa
hujaniambia,....’akasema
‘Mama
yupi...mbona sikuelewi,....’profesa akasema
‘Ulicheza
vizuri sana, nimeipenda hiyo,ila umechezea kubaya..tuyaache hayo,mimi
hayanihusu...kabisa, muhimu ni hii kazi,...hii itakufanya upate ...’akasema
mtalaamu.
‘Mhh, hii
kazi nitaifanya, na huna haja ya kunifundisha zaidi, nishajua ni nini cha
kufanya...’akasema profesa
‘Najau
utaiweza, ndio maana nikakutafuta wew,...’ akasema huyo mtaalamu
‘Jinsi
alivyo huyu mwanaume, hana ubavu wa kuhimili vitisho,hasa ukivilenga kwenye
ndoa....fanya mbinu uwazoee,na ili jamaa akianza kuhaha, wewe uwe sambamba na
yeye,ujifanye mshauri wake mkuu,...’akaambiwa
‘Mbinu ni
hiyo hiyo, unauma huku unapulizia ...na kwa vile hawajazoeana na watu, wewe
watakuona mtu muhimu kwao, jifaye jirani mwema, au utafute kazi kwao, hilo
nakuachia wewe....muhimu, wasijue lengo lako....’akaambiwa profesa
‘Hiyo kazi
ndogo kwangu, ...kama pesa ipo , utaona vumbi langu,...’akasema profesa
‘Ndio maana
nikupa kazi hiyo, ila uwe makini,...maana huyo mtu anamiliki bastola,na anajua
kuitumia vyema..na akikasirika anaweza kuivuta kiwashio na risasi ikatoka bila
kutarajia....’akasema na hapo moyo ukanilipuka, bastola....!
*********
Kwa vila ni
mgeni nikajua kabisa hatapenda wageni, hasa wa kufanya kazi nyumbani, lakini
cha ajabu nikaweza kupata kazi..na hata kuvipata vyote nilivyohitajia, maana
ugeni na ushamba uliwaponza.
‘Kwa vipi?’
akauliza kaka mtu akiwa na hamasa ya kutakakujua zaidi
‘Bro,..japo
uwa ni dhambi,najua hilo,lakini...mungu anisamehe, ujanja ujanja wa kuwaingia
watu, ninao.....’akasema mdogo mtu
‘Mhh,ulifanyaje
ukawaingia watu kama hao...?’ kaka mtu akazidi kuuliza.
‘Mtu kama
huyo unamwendea kinamna, nliona ili niweze kupata ninachokitaka ni muhimu
niwepo karibu nao, kwahiyo kwanza kabisa nilifika nikijionyesha kuwa nina shida,
nahitaji kazi za ndani,
‘Sisi
hatujui wenyeji, na kweli tulikuwa tunahitajia mtu wa kazi....’akasema.
‘Basi msiwe
na wasiwasi, ulizia watu wote, wananifahamu nimewahi kufanya akzi sehemu
nyingi, tu, msiwe na shaka kabisa na kama mnahitajia uhakika mnaweza kuulizia
mtu wa seriali za mitaa.....’profesa akasema.
‘Hamna
shaka,tutakupa kazi,lakini...usije kutudanganya...’wakasema
Na kweli nikapewa
kazi ya kulimia bustani,na kufanya usafi wa maeneoya nje,kwasiku mbili tu
nikaweza kuifahamu familia yote,na jinsi gani wanavyotoka
Walikuwa na
mlinzi,lakini mlinzi mwenyewe ni wale wa kufunga na kufungua mlango hakuwa na
utaalamu hasa wa kuwasoma watu,na mimi nikaweza kuingia ndani wakati wenyewe hawapo na kutafuta kila
ninachokihitajia,..hiyo haikuwa kazi ngumu kwangu,nikajua maisha yao,kiundani
zaidi
Nilikuwa
mcheshi sana kwa mama mwenye nyumba, na akanizoea mapema kuliko baba mwenye
nyumba....na kwa vila nilikuwa naifahamu fahamu lugha yao,..hahaha, bro usinione
naitwa profesa, mimi kwa lugha ni mkali,nikikaa na mtu akawa anaongea lugha
yao,haichukui muda kujifunza
Nikawa
nimeshakusanya kila kitu muhimu, sasa ikabakia kumjua huyo mama jinsi gani
anavyompenda mume wake, mapenzi yao ya ndani,wanaaminiana vipi,haikuchukua
muda,nikajua....
Mume kwa nje
alionekana mtu wa heshima zake, lakini cha ajabu akifika kwa mke wake hana
usemi,...kuna mila na desturi za watu, msione hapa bongo waume ni wakali kwa
wake zao, kuna sehemu inakuwa kinyume,
....huyu jamaa na ujanja wote wa nje, lakini akifika kwa mkewe ni goigoi,
anaogopa sana kumuuzi mke wake...hapo nikanyosha dole kwani hilo lilikuwa
muhimu sana
Ama kwa
mke,mke hakuonekana kujali sana,alionekana kumuamini mumewe kwa kiasi
kikubwa,kwahiyo hakuwa na muda wa kumfuatilia nyuma, yeye akirudi kazini,anakuwa
na kazi yake ya kufuma vitambaa, ni mtaalamu kweli wa kufuma vitambaa.
‘Mme wako ni
mwaminifu sana, ...’siku hiyo nikamchokoza
‘Ndio.....! Kwanini unasema hivyo?’ akaniuliza,na
alishanizoea kwa uchesi wangu
‘Namuona
tu,na nyie ndoa yenu inaonyesha ina raha sana watu wanawaonea wivu sana hapa
mitaani...’nikaanza kumchimba
‘Ni kawaida
tu,mimi sioni tofauti,muhimu kila mmoja anajali maisha yake na kujali umihimu
wa ndoa, na kwanini wanionee wivu, sio kweli...’akasema
‘Mhh,najiuliza
mfano..nasemea tu,mfano umkute mume wako na mwanamke mwingine utamfanyaje...?’
nikamuuliza, akaacha kufuma kitambaa na kuniangalia akatikisa kichwa.
‘Aaah,kwanini
unasema hivyo...mimi siwezi kumfikiria vibaya mume wangu maana
tunaaminiana...’akasema na mimi nikawa nakata kata maua ambayo niliyachuma kwa
ajili ya kupambia ndani
‘Ni mfano tu,si
tunaongea tu...usinifikiria vibaya, unajua ukikutana na watu unajifunza mila na
desturi zao,huenda nikaja kuoa huko kwenu...’nikasema
‘Kuoa
kwetu,...ina maana hujaoa...?’ akaniuliza akionyesha mshangao
‘Naweza kuoa
tena kwani ubaya....’nikasema
‘Uliuliza
swali gani vile...?’ akasema akishika kitambaa chake
‘Niliuliza
hivi,mfano ukagundua kuwa mume wako ana mke mwengine wa nje, sio lazima awe wa
moja kwa moja, ukamfuma ....utafanyaje...?’ nikamuuliza na hapo akaweka chini
kitambaa, akainama kama anawaza jambo,halafu akasema;
‘Weeeh,kama
ni kweli...hahaha,...sijui kama nitamsamehe...atajuta kunioa, lakini mume wangu
namuamini, tunaaminiana...kwahiyo siwezi kufikiria kitu kama hicho...’akasema
‘Mhh,ni
kweli,lakini yeye si kakuoa,huwezi kusema nimpe talaka au tuachane,au sio....maana
mwisho wa siku wewe mwanamke utakosa, utakwenda kwenu...sijui kwenu ipoje....’nikasema
‘Ndoa yetu
ni ya kimila zaidi,sisi wanawake ndio tunatoa mahari,kwahiyo naweza kumuacha
mume....,na ni kimuacha anakuwa hapati kitu....anarudi kuwa masikini
...’akasema huku akionyesha kutukupendelea kuliongelea hilo.
‘Mhh,...mila
zenu ni tofauti kidogo na za kwetu,naona zinampa nguvu sana
mwanamke...’nikamwambia
‘Ndio ni
mila na desturi zetu,ndio maana sisi wanawake hatuna mashaka dhidi ya wanaume
wetu,....mwanaume anatakiwa kujichunga kweli..ni kweli pamoja na hayo mwanaume
ni mwanaume,yeye ni kiongozi wa familia,kwahiyo anatakiwa kulijua
hilo....’akasema
‘Nimeipenda
hiyo,...maana huna haja ya kuhangaika na mume wako, ...weweukirudi ni nyumbani
tu,lakini mume yeye anapitia kupata kinywaji,huoni kuwa hiyo inaweza kuwa
kishawishi, atakutana na wanawake, na hujui tabia za wanawake wa huku, wanaweza
kumshawishi...huliogopi hilo,...wivu kidogo eeh?’nikamuuliza
‘Kunywa ni
jadi ya wanaume wa kwetu,na wakinywa ni lazima kuwa na watu wa kuongea
naye,wanaweza hata kuwa ni wanawake,muhimu ni kuchunga masharti ya
ndoa,..kuongea ni swala jingine,lakini asije akavuka mipaka...’akasema huyo mke
wake
‘Utakuwa na
uhakika gani, kuwa unalinda mipaka ya ndoa...?’ nikamuuliza na hapo akanitupia
jicho la udadisi
‘Kwanza hebu
nikuulize wewe mke wako yupoje,maana wewe ni mdadisi sana....?’ akaniuliza
‘Yupo
nyumbani, huko kwetu afrika...mimi huku nimekuja kutafuta maisha ...’profesa
akasema
‘Sasa wewe
unamwamini vipi mke wako huko alipo, maana swali kama hilo unatakiwa ujiulize
na mwenyewe kabla ya kuuliza wenzako....?’ akaniuliza
‘Huko
anaishi na ndugu zangu,wanahakikisha havunji miiko ya ndoa,hakuna shida kabisa...’profesa
akasema
‘Na wewe
huku atakuaminiaje maana na huko kuongea kwako yaonekana hujatulia..’akasema
‘Sisi
wanaume huwa hawafuatiliwi sana, naweza nikawa na nyumba ndogo nyingi
tu,siulizwi,muhimu mke wangu apate mahitajia yote muhimu....’profesa akasema
‘Nyie
mnawanyanyasa sana wanawake wenu,hamna haki sawa kama ni hivyo, sisi hilo halipo,mume
ni lazima atii ndoa yake, akikosea cha moto atakiona....’akasema na hapo moyoni
nikasema mambo si hayo
Sikuwahi sana kuongea na mume wake, lakini
siku moja nilipata muda wa kuongea naye, na aliniambia jambo
‘Mimi
naipenda sana familia yangu,sipendi kabisa kumuuzi mke wangu,nahakikisha nipo
safi mbele yake...na sipendi mtu kuja kuiharibu ndoa yangu...’akasema
‘Lakini wewe
nakuona mmmh,kama vile unapenda nyumba ndogo...?’ nikamuuliza kwa utani
‘Nyumba
ndogo,! ..una maana gani, hahaha hapana bhana...ni kuongea tu,..ulishawahi
kunioana nikiongea na wale akina dada, nawatania tu,...yah, kuna muda unatamani...lakini
wee, namuogopa sana mkewangu,najua akifahamu nitakuwa na hali ngumu,...sipendi
kabisa kumuuzi mke wangu na familia yangu...’akasema
‘Pale kwenye
bar unapokunywa kuna wasichana warembo sana mke wako akifahamu, au akija kukuona unavyotaniana nao, mhh,
atajisikia vibaya, hatafurahia kwakweli...’nikasema
akageuka kuangalia kule alipokuwa mkewe halafu akasema;
‘Mke wangu
anajua nakunywa pale, lakini ananiamini sana, naongea tu,sifanyia mabaya,ananifahamu
nilivyo, nikinywa naongea sana, utani kidogo, lakini wee, hapana chezea ndoa
yangu...’akajitetea
‘Mhh,mimi
kwa ushauri wangu, pale sio mahali pazuri kwa mtu kama wewe unayependa familia
yako,ipo siku utapitiwa, na itakuwa ni hatari, si unajua tena, mke wako
anavyokupenda....’nikamwambia kama kumshauri
‘Pale pazuri
sana,napoteza mawazo ya kazi,mabinti wanajua kuwafurahisha wateja,...hata hivyo
nakuwa makini,.hata nikilewa,sivunji masharti ya ndoa yangu...wakati mhh,
unahisi ...unajua eeh, ...,lakini nafikiria mara mbili tatu,faida na hasara
yake,basi naondoka mapema, ...’akasema
Moyoni
nilimuambia sasa wewe umekwisha nilichokitaka nimekipata,ni swala lakuingia
kwenye anga zangu tu...lakini bro, sikio kila mkaa kimia hajui kusema...
‘Kweli wewe
ni shetani...’akasema kaka mtu akiwa kama anaangalia sinema kichwani
mwake,kumhusu mdogo wake.
‘Hahaha
bro....bado hujasikia mambo yenyewe...., subiri nikuonyeshe maisha ya mlungula,
wenyewe huko wanaita blackmail
WAZO LA LEO: Heshima ni kitu cha bure,kama
muungwana unahitajika kujiweka jinsi jamii inavyotaka, huwezi kujiweka tofauti
eti kwa vile wewe umatokea nje, ukaiga watu wa nje wanavyofanya, jamii nyingine
wanavofanya, ukatembea nusu uchi, au ukafanya vitu kinyume na jamii ililivyo, eti
kwa vile...utaonekana ni kioja,ndio maana wanasema ukifika kwa wenye chongo, na
wewe fumba lako jicho.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment