Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeFriday, June 26, 2015

RADHI YA WAZAZI-11‘Mimi nina ushahidi wote,....’akasema huyo mama

‘Kwanza wewe mdudu,  nilikuamini sana, unakumbuka nilikuchukulia wapi, mitaani, ukihangaika na njaa, unakumbuka siku ile hata kutembea ulikuwa huwezi, nikajua nasaidia masikini, hohe hahe, omba omba nilikuonea huruma maana nilikufananisha kama wadog zangu kule nyumbani...unakumbuka,...?’ akawa kama anauliza

‘Yaani,  nikaona nikusaidie, unifanyia kazi zangu za nyumbani, ili usiabike...unakumbuka...’akasema na kuuliza tena

‘Nakumbuka nashukuru sana,ndio maana mimi siwezi kukufanyia mabaya..haki ya mungu tena, mimi siwezi kabisa kukufanyia ubaya najua uliponitolea...kwanini nikufanyia hivyo....’akasema profesa

‘Na kwa kukuamini kwangu, ukatokea kufanya kazi kwa muda mrefu, sio kwamba nilikuwa nakuamini mia kwa mia, lakini niliona nikusaidie tu..nikajisahau kuwa mwenye tabia haachi kuitumia hasa anapopata,...’akasema

‘Kiukweli, ulinigusa pabaya,. Kuwa utamwambia binti yangu, kuwa sio mtoto wangu utamwambia kila kitu jinsi alivyotokea, imeniuma sana,....ni kweli ukifanya huo uchafu wako utaniharibia, ...utafanya binti yangu kipenzi aumie sana..sijui utapata faida gani, na siwezi kuona binti yangu anaumia, ...’akasema

‘Lakini nina uhakika kauli ya kumuambia huyo binti hutaweza kuitoa tena...na kama utaweza labda iwe kauli yako ya mwisho ukikata roho, ..na hata hivyo kwa sasa hatakuamini,......’akasema kwa kujiamini

‘Aah, siwezi ila kama ni swala la kuamini, ...hapana, siwezi kukufanyia hivyo, kwako wewe hapana...’nikataka kumuambia kuwa nikipata mwanya wa kuongea na huyo binti yake ataamini tu, mimi kwa mdomo, achana name bro...’akasema profesa

‘Nikuambie kitu..., nyie watu mnataka msaidiweje,...na wewe ndiye uliyetokea kufanya kazi kwangu kwa muda mrefu, kumbe nilikuwa nafuga nyoka, kweli ngozi hii, hapana,...’akasema akivuta ngozi ya mkononi mwake.

‘Lakini....’profesa akawa anataka kulalamika, yule mama akainua mkono wa mkumnyamazisha akasema

‘Mimi nina ushahidi, usitake kubisha, mimi sio mjinga, mpaka nije kukuambia hili,..nimechunguza kila kitu, nimegundua, jinsi ulivyochukua kumbukumbu zangu pale nyumbani, hukuchukua kumbukumbu zangu ukaenda kutoa nakala wewe...’akasema kama anauliza na profesa alipotaka kusema kitu akashindwa na huyo mama akaendelea kusema

‘Nimekugundua jinsi gani ulivyokwenda kuonana na dakitari aliyehusika , ulikwenda kufuata nini kwake, hivi wewe inakuwashia nini, mimi kuwa na mtoto, unajua jinsi gani nilivyohangaika....’akatulia kidogo akiwa kashika kiuono

‘Wewe unakwiba pesa zangu unakwenda kumuhonga dakitari ili akupe nakala za jinsi nilivyofanya,...ndio alikubali...maana nay eye ni njaa kali kama wewe, nay eye kitamtokea puani, kazi hana..kakupa stakabadhi ulizotaka na faida yake ni kupoteza kazi

‘Eti unajifanya mjanja kupiga simu mitaani, ukaenda mpaka mtaa wa pili ndip unanipigia simu, nikuambie kitu simu zote za njiani zinanakiliwa, ulivyokwenda ukafanya kote huko nimekuona, ujue kuwa mimi ni nani,....’akasema akiwa kashika kiuono.

‘Sasa niambie, nini umepata na hizo pesa, .....’’akasema

‘Unajua...ni maisha tu...’akasema profesa

‘Mhh ni maisha tu, haaaa, unanipandisha mori, ingelikuwa enzi zile saa hizi damu zimetapakaa kila mahali, lakini sasa hivi sitatumia mkono wangu huu, ila utaumia, nakuahidi utaumia.......’kiukweli nilishangaa kwa jinsi gani alivyopata hizo taarifa maana ni kweli, ndivyo nilivyofanya na maana hiyo ina maana kweli keshanigundua.

‘Lakini sio kweli...ni watu tu hawanipendi wametunga tu hizo habari....’nikajitetea lakini hakunisiliza, akaendelea kusema

‘Sasa nakuhakikishia, ama zangu ama zako, kama hukuwahi kunisikia kuwa mimi ni nani kabla, basi ulizia...ulizia, na mwenye kovu kamwe usizani kapoa....mimi nitakunyesha kuwa nilikuwa nani..’akasema akjitanua kifua, na alionekama mpana kama mwinua vyuma, sijawahi kumuona hivyo kabla, akamsogelea profesa na profesa akawa anatetemeka.

‘Lakini ni nani kakudanganya, si-s-o mimi haki-ki-ki ya mungu tena , kwanini mimi nikufanyie hivyo, wakati nilishakuona kama ndugu yangu, mkaniamini.....’profesa alijitetea huku airudi nyuma, na huyo mama akiwa kamuangalia kwa jicho la kikatili

‘Kukuamini,...kukuamini wewe,.... mimi sijawahi kumuamini mdudu yoyote, hasa mwenye rangi kama yangu...’akasema huku akinyosha kidole.

‘Lakini sijawahi kufanya hivyo unavyosema...’nikasema nikisogea mbali na yeye

‘Nikuambe kitu, mimi najuana na vikundi vyote vya hapa mitaani na majirani...waulize hata polisi, wananijua,..sio kwa vile nimekuwa mtu mzima ndio ufikiria nimekwisha,..nilishaamua kuachana na tabia hizo lakini hujui moyoni mwangu kupoje....nakusikitia...’akatkisa kichwa

‘Samahani ..ni ni shida..lakini sio mimi...’akasema profesa

‘Yaani uanifanya nihisi kutapika...’akasema na kutema mate chini

‘Samahani, enzi zangii kauli kama hiyo ilikuwa ni tikite ya kuihama hii dunia...maana ukiachiwa zaidi, utazidi kuharibu na kupata dhambi, samaahni maana yake umeshatubu dhambi zako a upo tayari kwenda ahera au sio...’akasema

‘Mimi nilishaamua kutulia na mume wangu, kwanini bado watu mnanitafuta, nimechoka kumwaga damu za watu, ...’akatulia

‘Nitafaya lolote unalotaka..ila kiukweli sikufanya..sio mimi, watu tu ....’profesa akasema

‘Nikuambie kitu, ni huyu mwanaume tu, ...kwa vile aliahidi kunibadilisha, na mimi nakukabaliana naye, lakini moyoni, ujasiri umedinda kama muhimili wa nyumba,....mtu akinichokoza, sijali ni nani...wewe umenichokoza, na hustahili kusamehewa, utajua na utanikumbuka...’akasema akiinua mkono wake juu kuonyesha nguvu.

‘Ujue kuna makosa makosa yanafanyika hata mitambo inakosea,watu wanabuni mambo kuwaharibia wenzao, ...na chuki binafsi,..huyo mpelelezi wako huenda kakosea, hivi mimi unanionaje kweli mimi naweza kukufanyia hivyo...?’ nikamuuliza

Akatabasamu , tabasamu la dharau, akasema;

‘Unamfahamu yule mkusanya mizigo, nilimweka kwenye anga zangu nikamkumbusha wapi alipotoka, mimi ndiye niliyemfanyia mipango ya ile kazi anayofanya, alitakiwa kutumikia kifungo cha maisha kwa kosa la mauaji, nikamsaidia, unafikiri mtu kama huyo anaweza kunisaliti mimi...’akasema na kumfanya profesa kutoa jicho, kumbeee....

‘Ina maana alikuambia....’profesa akajikuta amesema hayo maneno

‘Hahaha, hata kabla huyo mlinzi hajafungua bakuli lake nilishakujua wewe ni mtu gani, kawaida hata nikiweka mpelelezi lazima nihakiki kazi yake,...nilishakujua wewe ni nani, unajifanya mnajimu,..una unajimu gani, muuaza miti shamba...kwanini unaharibu uafrika wetu...’akasema

‘Lakini dawa zangu zinatibu kweli...’akasema professa

‘Kama zinatibu kweli kwanini hujafanikiwa, kwanini unaishia kuiba, kuwa tapeli...’akasema kama anauliza

‘Mimi nakujau kuliko unavyojijua wewe, ....sasa, ..nakuhakikishia, utalia kama mtoto mdogo huku natoa nyama yako kidogo kidogo kama mchuna ngozi kwenye mnyama ...japokuwa mimi ni mtu mzima, lakini mikono yangu ni mirefu, inafika huko jela utakapokwenda kufungwa, utalia na kunikumbuka....’akaniambia

‘Tafadhali, ,...’nikamwambia sasa nikitamani kumpigia magoti

‘Kwanza nikuambie, sijawahi kudhulumiwa, na aliyewahi kufanya hivyo keshaliwa na mafunza,...sasa nataka pesa yangu yote, ..na gharama za kumlipia mpelelezi, na sijui wewe utazipatia wapi, hiyo sio kazi yangu,...., ukinirejeshea hizo, aaah, tutakubaliana  katika sharti la pili...’akasema na hapo profesa akapumua, lakii akajiuliza atazipatia wapi hizo pesa.

‘Sharti gani la pili,.....?’ akauliza profesa

‘Hilo ni namba moja, na sharti la pili uhame eneo hili haraka iwezekanavyo, ndio nakuona ulishafungasha kuondoka,...., lakini huwezi kuondoka bila kunirejeshea  pesa zangu, unajia nimezipata wapi, mwanamke mimi, unajua nimezipata wapi, sasa na wewe utakwenda kugezwa mwanamke, uzipatae,....utakoma kiumbe wewe...’akasema akikagua begi langu kwa macho.

‘Aaah,...sio kwamba nakimbia,... hapa nadaiwa sana kodi ndio maana nahama...ila pesa zako nitakurejeshea nipe muda....’profesa akasema

‘Hahaha,.....unadaiwa eeh, hahaha, basi nikuambie kitu, wote wanaokudai nimeshawasiliana nao wanahitaji pesa zao , na mimi nimewaahidi kuwa utazitoa, na nikiwarejeshea nitalipwa asilimia hamsini yake hiyo nikumbie waziwazi, mimi sifanyi kazi za uficho, ni lazima watu kama nyie mpotee kaibisa eneo hili, lakini kwa fundisho, na ni lazima wote waliotoa pesa zako kukupa wewe blackmailer, watazipata, ahadi hiyo nimeshawapa.......’akasema

‘Lakini mimi sina pesa...’profesa akasema

‘Hahahaha...na kabla hujazitoa...utaumia, utalia, utanikumbua..unasema huna pesa...utazipata tu..huku ukiwa umeteguka kiuno...huku damu zinatoka sehemu za siri..., na utarejea kwenu ukinikumbuka na kuniota..wenzako wanaota wanawake kwa starehe walizopata kutoka kwao..,lakini mimi utaniota kwa maumivu...’akasema, halafu akacheka kicheko cha kiume.

‘Unajua enzi zangu nikicheka hivyo maana yake nini...’akasema na kabla sijamjibu akaondoka.

NB: Habari ndio hiyo, msizarau watu

WAZO LA LEO:Kuna watu wana tabia ya kudharau wenzao, kwa vile tu wao wana uwezo, wana kipato, ni viongozi ni mabosi, basi wanapandisha mbega, wanajaa kiburi,ukifanya jambo, `unajua mimi nani...’ hata kama umedhulumu, hata kama mtu anadai haki yake..acheni jamani, ..tendenii haki na simamieni kwenye haki na kweli, haki na jasho la mtu halipotei bure ni swala la muda tu..wangapi wangapi na sasa wapo wapi..


Ni mimi: emu-three

No comments :