‘Unamfahamu vyema huyo mama
unayefanyia kazi kwake...’ni swali alilokuja kuniuliza yule mgambo mpokea
mizigo...aliniuliza hilo swali, nilipofika kumpa taarifa kuwa natarajia kuna
mzigo wangu utafika kwake;
Tuendelee na
kisa chetu...
********
‘Unatoka kwa
nani...?’ nilipomwambia tu akaniuliza huu akiandika kwenye kumbukumbu zake,
nikakaa kimia, kidogo, ndipo akanitupia jicho la haraka, halafu akasema
‘Ohoo ni
wewe ni kutoka kwa yule mama au...?’ akauliza huku akiandika kitu kwenye
kumbukumbu zake
‘Mama
yupi,...?’ nikamuuliza maana muda huo nilikuwa sifanyi kazi tena kwa huyo mama,
na sikutaka huyo jamaa afahamu vyema kuwa bado nachukua kitu kwake, na siku
hiyo nilitaka nimlipe ushuru kidogo, au nimkope tu.
‘Mhh, huyo mtu
unayesema ataleta mzigo hapa na wewe utauchukua kwangu unamfahamu vyema,si ni
huyo mama, unayefanyia kazi kwake...si bado upo naye?’ swali hilo lilinifanya
nishutuke kidogo, maana siku zote namuagiza, au napokea mzigo kwake, na
anachouliza ni ushuru wake tu.
‘Mhh,kwani
nilikuambia analeta huyo mama, sikumbuki kukuambia kitu kama hicho...’nikasema
‘My friend, my friend...huwa
sisahau....hiki kichwa ni komputa inayotembea,..mwanzoni kabisa uliwahi
kuniambia hivyo, unakumbuka, ukasema ni mzigo wa mama mmoja hivi, ukamtaja kwa
sifa zake,zikuwa na muda wa kukupa angalizo, anyway, its my job, sitakiwi
kukudadisi sana, lakini wewe ni rafiki yangu au sio...’akasema
‘Mhh,
sikumbuki, lakini kwani kuna tatizo,...yule mama alikuwa ni bosi wangu...ndio
wewe ni rafiki yangu, tupo pamoja...’nikamwambia
‘Kumbe umeachana
naye, kama ni huyo mama, sio mama wa mchezo,...nakumbuka enzi zake, alikuwa
akiogopewa mpaka na polisi...hakaagi na mfanyakazi kwa muda mrefu, wewe naona
umajitahidi...’akasema
‘Kwanini polisi
wamuogope...?’ nikauliza nikijua labda, alikuwa na biashara zake, au alikuwa
tajiri
‘Huyo mama
ni jasiri sana, na vikundi vyote vya kihuni anavijua...’akasema
‘Kwanini,
hata hivyo huenda ni kutokana na biashara zake, unafahamu biashara zake...?’
nikauliza kwa udadisi
‘Mhh,
biashara zake..! unajua enzi hizo akiwa ndani ya vikundi kama kiongozi alikuwa
akiogopewa kama simba dume nkati kati ya nyati kwa ujasiri wake, wewe ni mgeni
kidogo, hapa, kipindi cha nyuma kulizuka vikundi hatarishi,...na huyo mama
alikuwa miongoni mwao.....’akasema huyo jamaa, na kunifanya sasa nitulia
kumsikiliza
‘Unasema!
Huyo mama... ! haiwezekani....Sizani kama ni-ni, huyo mama, naona umekosea, huyu mama
niliyekuwa nafanya kazi kwake kaolewa na mzungu...unasikia ni mke wa mzungu, na
wana binti mmoja...mnzuri sana...’ nikasema
‘Ehee, huyo
mama mwenye mwili mwili, sio....kapanda juu hivi eeh...eeh, si ndio huyo eeh..ya
ana binti mnzuri...japokuwa ukiwachunguza binti na wao, hawaendani lakini ndio
dunia ilivyo,...ni binti yao..na sijui...huko sijui sana...si ndio huyo?’
akaniuliza akiniangalia kwa makini usoni
‘Mhh, ndio
huyo, ..lakini kwa nimjuavyo mimi, hajawahi kuwa mitaani na wahuni, ni mama wa
watu mwenye heshima zake....au unazungumzia mama yupi...?’profesa aliuliza hilo
swali huku mwili mzima umeshikwa na mshituko, akihisi kuwa huenda, kaingia choo cha kike, na humo akamkuta mama
mkwe.
‘Ndiye huyo
huyo...nakumbuka mwanzoni ulisema ni mizigo yake, na baadaye unakuja kuzichukua
ukisema kuna sehemu nyingine unatakiwa kupeleka, nashindwa kuelewa, kwanini
usipeleke moja kwa moja wewe mwenyewe mpaka ifike kwangu ndio uje uchukue tena
kwa akili ya haraka lazima utajiuliza...lakin its not my business, its just a curious’akasema
‘Kwahiyo
wewe hutaki kazi, maana kwa kufanya hivyo ndio nakupa ulaji, au
nimekosea....’nikasema
‘Aaah,
usinielewe vibaya,...kabisa nashukuru sana, ila kibinadamu unakuta unajiuliza
uliza tu...na wewe ni rafiki yangu, shauku ikanijia,...nikuulize na kukupa a-nga-li-zo...’akasema
akionyeshea mkono wa kusitisha mazungumzo.
‘Ohoo, kumbe
unachunguza chunguza watu, nilijua wewe kazi yako ni kuchukua tu mizigo, na
huna haja ya kuchunguza chunguza watu...sasa unanipa mashaka...’nikamwambia
‘Ngoja....nakumbuka
kuna dume moja alitaka kumfanyia ubaya huyo mama, katika vikundi vyao,
walishafanya kazi zao wakapata pesa, si unajua kazi za dili, za haramu haramu,
mimi sipo huku, nakudokezea tu.... basi huyo mama, kipindi hicho ni mremb, akamwambia
huyo dume wapambane naye wakiwa uchi, atakayeshindwa, aadhiriwe, na pesa hizo
zote apewe mshindi...mimi nilishuhudia hilo tukio kwa macho yangu....’akasema
bila kujali maelezo yangu
‘Ina maana
wewe ulikuwa wapi, au ulikuwa kundi moja na hao wahuni...ikawaje..?’
nikamuuliza
‘Nakupa
picha tu...usiseme ooh rafiki yangu hakuniambia,..just imagine...put in your mind,...’akasema akionyesha kidole
kichwani.
‘Ikawaje...?’
profesa akawa na hamasa ya kutaka kujua zaidi
‘Hebu
fikiria ni mwanamke wa namna gani anaweza kufanya hivyo, wanapigana uchi, na
kichupi tu, na kichupi chenyewe...hahaha, usinkumbushe mbali, nilikuwep o
nikaona kwa macho yangu dume likiadhiriwa, mwanamke anasimama kidedea watu
tunashangilia...’akasema
‘Akamshinda
huyo mwanamume, basi huyo mwanamume alikuwa kama mimi tu...’akasema profesa
‘Kama
wewe...unamuona huyu mlinzii wangu hapa...huyu ni cha mtoto, ...enzi hizo
kuingia kwenye kundi sifa ya kwanza uwe shupavu, ..na ukiwa kiongozi uwe
umeshaua, umeshapambana na polisi ukapiga saana...huyo aliyepambana naye
alikuwa mmoja wa mashupavu wa kundi, anayeogopewa....’akasema
‘Mhh, ina
maana huyo mwanamke ana miguvu ya namna gani, ni mchawi...au walikuwa
wakimuhurumia kwa urembo wake...’akauliza profesa
‘Hahaha,
ulishawahi kumuona huyo mwanamke maumbile yake.., ana msiuli kama mwanaume,...
hutaamini, ila mavazi anayovaa yanamsitiri tu, siku hizi na utu uzima,
anajihifadhi, au sio..muda wote na miguo mipana, jiulize kwanini anavaa hivyo,
wakati wakazi wengi wa huku, wanajichia tu, wanawake wanatembea nusu uchi,
lakini huyo mama muda wote miguo mipana,......’akasema
Kweli hapo,
bro..nikaingiwa na mawazo...ni kweli katika kufanya kazi kwangu kwa huyo mama
sijawahi kumuona akiwa kavaa nguo za kuonyesha maungo yake, kwahiyo sikuwa na
uhakika saana na maneno ya huyo mlinzi.
‘Mara
nyingi,huwa enzi hizo alikuwa akiwa kazini anavaa kivazi cha rangi ya chuichui,
akivaa hivyo ujue kuna jambo nzito..., na wakati wa mapambanoo hana huruma,
anaweza kuua huku anacheka....’akazidi kuongea, ni kama vile alitaka kunifikishia
ujumbe bila kukosea, ndio maana hakutaka maswali maswali.
‘Ina maana
amewahi hata kuua...?’ nikauliza sasa nikiwa najuta nikijua sasa
nimeshapatikana, na huyo mlinzi kwanza akawa kama anakagua watu, akawa katulia,
halafu akasema
‘Hahaha,...kuua,
vikundi kama hivyo kuua sio jambo la ajabu, ni kama kula wali wenye chuya na mawe
useme hutang’ata jiwe,..huyo mama mhhh..., achana naye , kama aliwahi kuwa kiongozi
wao, utauliza kuwa hajawahi kuua..., na sio mara moja kushitakiwa kwa kesi ya
mauaji, alikuwa akiponea chupu chupu tu, kwa vile..ooh, ngoja nisiseme saana
nikaharibu soko langu.....’akasema huku akionyesha ishara ya kukatisha
mazungumzo.
‘Sasa
kwanini hajafungwa au kunyongwa....kama aliwahi kuua,...?’ nikauliza
‘Hahaha,
huyo mama kufungwa, ....ameshawahi kufungwa, mara kadhaa...na huko jela
wanamjua utafikiri kazaliwa huko, huko ana marafiki wengi tu, na alifikia
kupewa uongozi akiwa jela, kiongozi wa wafungwa....kulikuwa na chumba chake cha
amlikia wa jela....’akasema akitabsamu kama anahadithia kitu kizuri sana, au
picha yenye mvuto.
‘Ina maana
mnajuana na huyo mama..?’ nikamuuliza
‘Mimi ni
mlinzi wa siku nyingi,..najuana na watu wengi tu...wengi wa enzi zangu
ukiwauliza watakuambia, ila mimi najua zaidi ya hayo kwa huyo mama...’akasema
sasa ikiwa kama ananong’ona
‘Ina maana
labda uliwahi kufanya kazi na huyo mama,au kwa huyo mama....?’ nikamuuliza
‘Kazi
gani,..hapana...siwezi kufanya kazi kwake, hata kama akinilipa mabilioni,
hapana, ila elewa hivyo tu, kuwa namfahamu, ...’akasema
‘Sasa
kwanini umeniambia hayo yote....?’ nikamuuliza sasa nikimtilia mashaka
‘You’r y
friend..right...?’ akasema akiniangalia moja kwa moja usoni
‘Yah, of course...’nikasema
nikigeuka huku na kule
‘Mimi namuogopa
sana huyo mama, na siku ulipoleta ule mzigo ukasema umetoka kwake, nikahisi
kuwa ...kuna jambo nyuma yake, si bure, hajawahi kufanya hivyo wangu tangu
..tangu, tangu....ni siku nyingi sija...eeh,...ndio hivyo, sutaki kuongea
mengi, ondoka usije ukataka akanijia,...ana masikio yanasikia kama nini....’akasema
sasa nahisi akiwa hataki kuendelea kuongea.
‘Mhh,
nimekufa...’nikajikuta nikisema huku nikigeuka huku na kule...
‘Kama
umeingilia anga zake, sijui labda awe amebadilika kihivyo, lakini nijuavy haat
katika uzima wake bado wanamuheshimu, bado anaogopewa,bado I nyoka,....unajua
nikuambie kitu, watu kama yeye wanabadilika kinje-nje tu, lakini kindani unyama
upo pale pale...’akasema
‘Sasa mbona
anaonekana laini laini,hata akitembea, haiji akilini...tofauti na unavyosema
wewe....?’ nikauliza
‘Ni laini
kama mwanamke , hasa wakati anahitajika kuonyesha ua-nauke wake, unasikia sana,
na akiwa kwenye ulingo wa walimbwende ni mrembo kama waridi likiwa linachanua kwenye
kikonyo chake, , utasema hakuna mwanamke mrembo kama huyo,...ila my friend, she was a snake....mwenye
sumu kali...’akatabasamu kama anavuta taswira.
‘Duuh,
nimekufa...’profesa akajikuta akisema.
‘Nikuambie
ukweli, ungelikuwepo enzi zake anaitwa binti mrembo kutoka Afrika
ungelithibitisha hilo, ila sasa...mhh, akibadilika akiwa kwenye anga za ubabe,
huwezi amini, ....akitoa kipigo ni kipigo kweli...’akatulia akigeuka kuangalia
upande mwingine, mimi nikahisi nipo tayari kukamatwa, au huyo mama ameshafika.
‘Mhh,
siamini maneno yako, ulijuaje... ulimjuaje...?’ nikamuuliza
‘Mama huyo,
pamoja na urembo wake, ambao aliutumia kama chui ndani ya ngozi ya kondoo, kiukweli
alikuwa mkorofi, muhuni,jambazi, aliyebobea...nahisi huko alipotokea alitokea
chuo cha wababe wa kihuni walioshindikana...’akasema akicheza na fimbo yake ya
ulinzi kwa sauti sasa ya kutulia kuwa hatanii.
‘Mhh, sijui,
...unachoongea na yeye ni tofauti...’nikasema nikiwa na mawazo mengi kichwani.
‘Hahaha,..ndio
hapo, hata polisi wakashindwa kumweka kwenye kundi la majambazi,..lakini
tuyaache hayo, kama unahitaji kumjua vyema nenda uliza polisi yoyote wa siku
nyingi,. ...watakuambia,...wewe si uniamini, nenda huko kwa watu wa usalama,
wana kumbkumbu zake...’akasema
‘Sina haja ya
kwenda huk, kwani niende kwanza ananihusu nini mimi....’nikasema nikijifanya
sina habari naye
‘Aaa, wewe
si uniamini, mimi namfahamu tokea anaingia hapa...mimi ni mtu wa siku nyingi
hapa,...namafahmu sana...usimuone alivyo hivyo, mwili kauachi achia,...alikuwa mrembo,
ila urembo wake ulikuwa kama ulimbo kwa ndege, polisi wenyewe walijikuta
wakihadaika naye....lakini...akafungwa, akatoka, na sasa ndio huyo...anakupa
mizigo, mzigo yake ina alama ya shari...naogopa sana...’akasema
‘Polisi hawa
hawa, walihadika, inaonekana unamfahamu sana huyo mama, je huko alipotokea
ilikuwaje...? Akauliza profesa
‘Mwanaume
hata awe vipi, mbele ya mrembo kama huyo anayejua ni nini anachokifanya, mhhh,
utashikwa na kigugumizi, kiukweli mdada huyo
alikuwa moto...kwa urembo wake na alikuwa anajua jinsi gani ya
kuigiza,..ulimbwende, kudeka pale panapostahiki utafikiri sio yeye..’akawa
najionyesha kwa matendo.
‘Kwa mara ya
kwanza, Ilikuwa sio rahisi kwake yeye kukamatwa kirahisi, na akikamatwa hakai
muda, anatoka...ila baadaye, ndio akafungwa kwa makosa ya mauji ndipo alikaa
muda mrefu jela,na huo jela, si unajua tena, akawa ni kama hayupo jela...’akasema
‘Na kweli
aliua...akakamatwa?’ nikauliza tena kwa mashaka kama vile siamini, nilikuwa
nahisi jamaa anatia chumvi..
‘Hahaha...kuuua,
...nimeshakuambia sio mara moja...achana na huyo mama, .....mimi naogopa sana
nikisikia mzigo umetoka kwake, maana ukikosea maagizo yake ujue kama
hutaumizwa, utakuwa kilema, na mara nyingi, utaomba ufe tu...huwa anakicheko
chake cha shari, akikicheka, ujue damu inatoka......’akaniambia akionyesha
uhakika wa anachokiongea
‘Mhh, hili
sasa balaa...mimi najiuliza umemjuaje yeye....’akasema profesa akigeuka
kuangalia mlangoni, kwani kuna mama mmoja aliingia anafanana sana na huyo mama
wanayemuongelea.
‘Ni hayo
tu..., nilikuwa nakueleza kile ninachokifahamu zaidi ya hayo nenda kamuulize
mwenyewe, au kaulizie polisi, ...kama nakudanganya, na kama nakudanganya uje
nikurudishie malipo yote uliyokuwa ukinipia.....kwaheri, nina wateja...’akasema
akihangaika na watu waliofika kuingie kwenye hiyo casino.
Sikuweza
kupata muda wa kumdadisi tena zaidi, nikaona haina haja, nikajikuta napitia
kituo cha polisi, kuna askari mmoja namfahamu, nikamdadisi kuhusu huyo mama
‘Bado unafanya
kazi kwake , maana huwa hakai muda mrefu na mfanyakazi mmoja?’ akaniuliza
‘Kwanini....?’
nikamuuliza
‘Kwanini!...huyo
mama haamini watu, akikushuku unamchunguza, ni lazima atakufukuza, ...ana
historia mbaya, lakini sasa katulia sana, huwezi kuamini ni huyo mama aliyekuwa
akisumbuana na polisi,..nahisi huyo mume kambadili kama alivyodai kuwa atafanya
hivyo...’akasema
‘Aliwahi
kuua, kufungwa,...?’ nikauliza
‘Ndio hivyo,....
lakini binadamu hubadilika,...mimi mwenyewe sikuamini kuwa huyo mama
atabadilika, lakini tangu atoke jela, na kukutana na huyo mzungu, sijasikia habari
zake tena...’akasema huyo polisi
‘Mbona
hafanani na hiyo tabia...?’ nikauliza
‘Hahaha kwa
vile ni bosi wako sio,... mchokoze uone, ...hahaha, alikuwa akipigana na midume
mitatu, na yote anaitoa makamasi, polisi wenyewe wakitumwa kwake, wanajiuliza
mara mbili, tatu...achana na huyo mama , kama unafanyakazi kwake, uwe
mwangalifu sana, ....kwani vipi, bado upo naye?’ akaniuliza
‘Hapana
nimeona nitafute sehemu nyingine...’nikasema
‘Basi
uachane naye kwa wema, kama ni kwa ubaya,..utakuja kujuta, ...atakufuatilia
hata kama umejificha pangoni...’akasema huyo askari, na kunifanya moyo uanza
kudunda kwa mapigo yasiyo yake.
********
Basi siku
hiyo sikulala, nikikumbuka nilishampigia simu ya kutaka mshiko mwingine, nikawa
sitoki ndani, na kila simu yangu ilipolia nikajua ni yeye,japokuwa sijawahi
kutumia simu yangu ya mkononi, ..
Na kesho
yake asubuhi, ndio akanijia nikiwa nipo mlangoni nimeshafungasha mizigo yangu
nikitaka kuhama eneo hilo....patamu hapo,, siku hiyo alikuwa kaja kwangu
kavalia mavazi ya chui chui, nasikia ndilo lilikuwa vazi lake enzi hizo akiwa
na vikundi haramu.
Ni vazi linalombana na kuonyesha maumbile yake ya mwili
wake.
‘Tunaushahidi, ...jinsi ulivyochukua
kumbukumbu zangu pale nyumbani, jinsi gani ulivyokwenda kuonana na dakitari
aliyehusika ....ukamuhonga, akakupa baadhi ya stakabadhi,....na wapi ulikuwa
ukipiga simu zako....’akasema na nilishangaa jinsi gani alivyopata hizo taarifa
maana ni kweli, ndivyo nilivyofanya na maana hiyo ina maana kweli keshanigundua....
NB:Tuishie hapa
kwa leo
WAZO LA LEO: Tabia ya mtu hujengeka
toka utotoni, na ujanani ni kwenye vitendo na majaribio, ukubwani ni utekelezaji
na hitimisho,..sasa tuweni makini kwa viongozi tunataka kuchagua, wachunguzeni
walipotokea, maisha yao walipopitia, ubaya wa mtu huja kuonekana pale tu
watakapopata, kwa hivi sasa wengi wao wamejifunika ngozi ya kondoo. Ukitaka
kumfahamu mtu ngoja apate..
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment