Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeFriday, May 29, 2015

NANI KAMA MAMA-84


Basi mtoto akaambiwa aitwe ili picha ya pamoja ipigwe, lakini aliyetumwa akarudi na taarifa ya kushitua, akasema

‘Mtoto haonekani…’ 

‘Umemwangalia huko alikokuwa akicheza na wenzake..’ akauliza nesi

‘Kote nimeangalia na nimewauliza wenzake wanasema hawajui wapi mtoto ameenda..’akasema

‘Atakuwa kaenda wapi naye hana tabia ya kutembea mbali na hapa nyumbani..’akasema mama wa kufikia alipopewa hiyo taarifa. 

Mtoto kaenda wapi...

Tuendelee na kisa chetu

*************

Wakati wanahangaika huku na kule kumtafuta mtoto mara simu ya nesi ikaita, nesi kwa haraka akaichukua akijua huenda ni watu wamempata huyo mtoto, lakini alipotizama akakuta ni simu ya bosi , moyo ukamlipuka akijua sasa tatizo limefika kubaya, atasema nini kwa mabosi wake,..akajipa moyo na kuanza kuongea;


 ‘Halloh bosi, mambo huku sio shwari, maana mtoto haonekani, na tumejaribu kumtafuta kila mahali lakini haonekani kabisaa,…yeye alikuwa akicheza na wenzake nje, wakati sisi tupo na wageni…’ nesi akawa anaelezea huku akiwa na wasiwasi sana

‘Mimi sikuelewi nesi, maana unakumbuka tulivyoondoka hapa niliambiwa kwa msisitizo na wewe mwenyewe uliomba iwe hivyo na hapa utawala umekuamini kwa hilo kuwa takuwa salama, na mimi nilipofika huku nimewahakikishia kuwa mtoto yupo salama,  sasa unaniambia habari kama hiyo, unafikiri mimi nitawaelezeje utawala…’ akasema docta akionekana kukasirika.

‘Bosi haikuwa nia yetu, kwakweli tulijua hakuna matatizo kabisa…sasa sijui tufanyeje, naona tukatoe taaarifa polisi ,…; akasema nesi. Kwa vile usiku ulishaingia ikabidi wasubri kesho huku kila mmoja akiomba mtoto awe kwenye mikono salama, na waliomba huyo mama mwenye mtoto asitokee.

‘Oh hata sijui nikuambie nini….maana nilipofika hapa tu cha kwanza kuulizwa ni hicho na wakanipa angalizo kuwa mtoto huyo anatakiwa kulindwa sana….oh, nimechoka…’akasema docta

‘Unajua nimechoka…maana yule mama naye hajapatikana hajarudi , hatujui kapotelea wapi , sisi tulijua yupo huko, …hawa watu niliwaambia akirudi hapa wasimruhusu kuondoka, lakini hawakufanya hivyo….yaani, hata sijui,….’akasema docta

‘Ndio imeshatokea hivyo docta, tufanyeje maana hata mimi sijui la kufanya..nikatoe taarifa polisi..natakakibali chenu, nisije kutoa taarifa kumbe sio sahihi…nifanye hivyo?’ akauliza nesi lakini akahsi simu ipo kimia, kumbe mawasiliano yyalishakatika, bosi wake hakuwepo hewani, labda aliamua kukata simu au ni mawasiliano mabovu.

‘Docta, bosi….oooh’akajiukuta anaongea peke yake…simu haikuwa hewani.
Nesi baba mwenye nyumba na mama mwenye nyumba na baadhi ya wanafamilia wakakutana kikao cha dharura kujadili la kufanya huku wengine wakiendelea kutafuta.

‘Tuendelee kutafuta, kwani hata sasa hivi ukienda polisi, watakuambia msubiria masaa 24, ….’akasema mjumbe

Baba mwenye nyumba pamoja na kutokupendelea hilo, lakini akajitahidi na wakazi wote majirani wakawa wanahangaika huku na kule kutafuta wapi huyo mtoto yupo , lakini hadi usiku wa saa sita hakuna kilichopatikana, ikabidi walale, wakiomba mungu..

Asubuhi kazi ikawa kwenda polisi na wengine wakitafuta  huku na kule wakijaribu  kuulizia watu  wengine hadi vijiji vya jirani, lakini hakuna aliyekuwa na taarifa yoyote kuhusiana na huyo mtoto, na hata polisi walipokuja na kuulizia waliishia kusambaza taarifa kuwa kuna mtoto kapotea  kama kuna mtu kamuona mtoto mwenye sifa hizo  wawataarifu polisi na picha yake ikasambazwa, lakini haikusaidia kitu mtoto akawa hapatikani.

 Siku tatu, ya nne, ikaingia siku ya tano, hakuna cha mtoto wala taarifa ya huyo mtoto…

‘Lakini hata hivyo leo ni siku ya tano, hakuna taarifa ya huyo mtoto, na hata huyo mama hajulikani wapi alipo, ina maana yule mama naye kapotea au kaenda wapi…?’ akauliza mkuu dakitari mkuu.

‘Yaani hapo ndio inashangaza , maana haiwezekani yule mama akae siku zote hizo bila kurudi kumtafuta mtoto wake..’akasema docta mwingine.

‘Kwa hali hiyo tunaweza kuhisi kuwa huenda huyo mama yupo na huyo mtoto…’ akauliza docta mkuu, wakiwa kwenye kikao maalumu cha kutafakari kupotea kwa mtoto, aliyekuwa kwenye mamlaka yao na mgonjwa, yaani huyo mama.

‘Tunaweza kuhisi hivyo lakini haina uhakika, kitu cha kujiuliza huyo mama alifika muda gani huko kijijini, na kusitokee hata mtu mmoja kumuona…’akasema docta mkuu

‘Hapo ndio tunashangaa, maana polisi wamehoji watu mbalimbali, watoto waliokuwa wakicheza naye,…na kutangaza, kutoa picha, lakini hakuna aliyewahi kumuona huyo mtoto au huyo mama

‘Mhh, hili ni tukio la aina yake, maana ni siri, siri…mambo ya huyo mama ni ya kiajabu ajabu, na ..hili tena linabakia kwenye historia ya kazi kwenye hospitali hii…’akasema docta mkuu

‘Huyo mama, sitamsahau….naombea siku nikutane naye tena..’akasema docta aliyekuwa akimtibia huyo mama

‘Mimi wala sitaki, …kama ni heri basi yaishe kwa heri tu….imenipa wakati mgumu sana..’akasema docta mkuu

‘Pole sana mkuu, ndio kazi,…’akasema mwenzake

‘Hata hivyo, tunahitajika kukaa na nesi na familia yao, ikibidi baba mwenye nyumba, atusaidia tufike huko kwa huyo baba wa huyo mtoto…’akasema

‘Mhh, polisi wamefika huko, hakuna mtu kaam huyo…wanasema huyo mtu alipotea zamani sana..’akasema mtu wa usalama wa hapo hospitalini

‘Hana hata ndugu wengine?’ akauliza

‘Wapo, ndio wamesema hivyo, wanasema wao walishahitimisha kuwa ni marehemu,kwahiyo hawana la kufanya..’akasema huyo mtu wao wa usalama

‘Unaona eeh, huyo mama ni kama katokea hewani…na familia za huyo mama?’ akauliza

‘Hata zenyewe zilihama eneo hilo, na haijulikani walihamia wapi, walihama wakimuogopa huyo jamaa kwani wanasema aliapaapa kuwa atawafanyia kitu kibaya hiyo familia, …’akasema

‘Kwanini..?’ akauliza
‘Wanavyosema familia hiyo ilikuwa inadaiwa sana na huyo mtu, yaani baba wa huyo mama, na ikatokea mtafaruku, kutokuelewana, na haijulikani wapi huyo mama alipotoelea, huyo jamaa akadai familia hiyo ndio imefanya hivyo, kukawa na vita vya familia hizo mbili, …sasa ikatokea ghafla huyo jamaa akapotea, kutokana na mke wake mdogo..’akasema

‘Ina maana alikuwa na mke mwingine?’ wakauliza

‘Ndio wanadai mke mdogo ndiye aliyefanya mke mkubwa kupotea kiajabu…japokuwa haikuwa wazi…ila sasa ndugu wa mke huyo mdogo, na wao si o mchezo, wakajenga kisasi na huyo baba wa huyo mtoto, …ikawa ni vita, jamaa akapotea, na kipindi hicho huyo jamaa sio tajiri tena..’akasema mlinzi

‘Ilikuwaje alifirisika..?’ ikaulizwa

‘Ndio alifirisika akawa na hali mbaya, hata matatizo hayo yanatokea hakuwa na kitu, kwahiyo alikimbia akijua hana kitu nyuma..’akasema

‘Na huyo mke mdogo anasemaje kuhusu kupotea kwa mke mkubwa

‘Huyo mke mdogo aliolewa tena, na hajulikani wapi alipoolewa, kwani walipoona na mume wake wakahama hapo…’akasema

‘Hakuna cha kutusaidia hapo…’akasema docta mkuu

Hutaamini mwezi ulikatika na hakukuwa na taarifa yoyote ya mtoto aliyepatikana au kusikia mtoto anayetafuta wazazi wake au kuonekana mtoto akitangatanga. Mwishowe watu wakakata tamaa na kusubiria kama huyo mama atarudi kuulizia tena huyo mtoto wake.

NB: Nimetoa sehemu hii fupi, sehemu hii inaendelea lakini wenye kampuni wameshafika wanataka makabidhiano ya ya vitu vyao nk…si mnajua tena mwisho wa mwezi huu sitakiwa kuwa hapa tena, …Yote maisha..tutaonana nikiweza kutulia, hata kesho naweza kuendelea na sehemu hii


WAZO LA LEO:  Ubaya mfanyie mwenzako, na wakati unafanya unaweza kuona ni jambo la kawaida tu, kwa vile unaona ni sahihi, unawajibika, …hata kama unafanya sivyo ndivyo, ilimradi unatimiza hicho unachoona ni sahihi. Uongozi, dhamana za utawala una uadilifu wake, na jambo kubwa ni kuhakikisha unatenda yaliyohaki, kwa uadilifu na sheria lakini pia kwa hekima. Tujue kuwa dhamana ni deni, na uadilifu katikautendaji ni ngao ya maisha yako ya baadaye, ukitenda vibaya utajiwekea maisha yako katika mashaka na uadui..ukumbuke uliyowatendea wenzako na wewe yatakukuta hivyo hivyo.
Ni mimi: emu-three

No comments :