Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeTuesday, May 5, 2015

NANI KAMA MAMA-71


 Na wakati wanaongea nini kifanyike zaidi simu ya nesi ikaita ghafla na namba iliyoita ni namba ngeni kwenye simu ya huyo nesi, akaiweka hewani ili kusikia ni nani kampigia.

‘Halloh wewe ni nesi , ndugu yake….’ sauti ikawa inasema kwa kukatikakatika, mawasiliano yalikuwa sio manzuri, nesi akasema;

‘Ndio mimi nesi wewe ni nani, na unapiga simu kutoka wapi?’ akauliza nesi

‘Mimi napiga simu kutoka kijiji kwenu, ni jirani na ndugu zako, wanasema uende nyumbani kwa dada yako haraka iwezekanavyo…’ simu ikawa imekatika na hata walivyojaribu kupiga tena ikawa haipatikani.

Tuendelee na kisa chetu..

***********

Basi msafara ukaondoka, docta nesi mlinzi na mtoto kuelekea kijijini,  ilibidi wamchukue na mlinzi kwani madocta walihisi huyo mama huenda atakuwa kaelekea huko kijijini, kwahiyo walihitajia mtu wa kusaidia kama atalet fujo. Njiani waliongea ya kawaida, hawakutaka kuliongelea jambo linalowakabili, hawakutaka kumtia mtoto kitu cha kujiuliza, japokuwa walijua kuwa huyo mtoto bado ni mdogo.

Na mara kwa mara nesi alikuwa akijaribu kupiga simu, kuwapigia ndugu zake huko kijijini, lakini simu hazikuweza kupatikana, hakukuwa na mawasiliano kabisa. Na docta alipoona nesi anahangaika kupiga simu mara kwa kwa mara akasema;

‘Mimi nahisi hakuna tatizo kubwa sana huko kijijini kwenu...kama kungekuwa na tatizo ni lazima wanekupigia simu tena…’akasema docta

‘Sasa kwanini simu zao zote zisifanye kazi, na kwanini mtoa huo ujumbe kuwa ndugu zangu wana matatizo  awe ni mtu wa jirani, ndio kina nitia mashaka...’akasema nesi

‘Hiyo isikutie shaka nesi,…nahisi simu zao hazina chaji,.. nina wasiwasi na umeme, ukumbuke siku mbili sasa hakuna umeme hata huku mjini tunatumia generator..., sasa inategemea kuwa simu ya mtu aliichaji lini…’ akasema docta.

Walifika eneo la kijijini, kwa vile huyo docta, hakuwa mwenyeji sana, ilibidi  nesi awe anamuelekeza docta njia gani apite hadi wakafika nyumbani kwa dada yake, na walipofika kwenye hiyo nyumba, nesi kwa haraka akateremka kwenye gari na kukimbilia ndani.

Nesi haakujali kuwa yeye ni mwenyeji na ana wageni kaja nao, alichojali kwa muda huo ni kutaka kujua kama kuna tatizo lolote hapo nyumbani,…akawaacha wageni wakiwa ndani ya gari yeye akateremka, na kuelekea mlengoni mwa hiyo nyumba.

Kulikuwa kimia tofauti na alivyozoea, utafikiri kumehamwa, akahis ni lazia kuna jambo limetokea, akausogelea mlango,akataka kugonga, akasita,….

 Hakugonga mlango tena akaamua kupiga hodi ;

‘Hodi wenyewe mpo….’akasema na kukawa kimia, akageuka huku na kule, akitarajia kumuona yule mdada , mfanyakazi wa hapo, hakukuwa na cha mdada, wala mtu yoyote zaidi ya kuku, waliokuwa wakikimbizana huku na kule.

‘Hodi jamani, dada,…..’akasema  na baada ya muda mlango ukafungulia, na hapo akapumua kidogo, ..aliyefungua mlango alikuwa ni shemeji yake,…dada yupo wapi!?,

Moyo ukamdunda tena, …dada yupo wapi,… wasiwasi ukamrudia tena, aliogopa hata kuuliza, kwani mara nyingi anapofika hapo nyumbani mtu anayekuja kufungua mlango ni dada yake au mfanyakazi wa hapo, lakini…leo aliyefungua mlango ni shemeji, na usoni anaonekana mwenye huzuni…mwenye wasiwasi….

‘Kuna usalama hapa shemu, maana nimepokea simu yenye utata kutoka kwa jirani, …hebu nitulize moyo wangu kwanza, dada yupo wapi…?’ akauliza huku anatizama huku na kule.

‘Dada yako…?’ shemeji yake naye akawa kama anauliza swali badala ya kujibu, na kumzidishia mwenzake shinikizo la moyo.

‘Ndio shemeji, dada yupo wapi, mbona kimya, na…yeye haonekani, kuna tatizo gani…?’ akauliza mdogo mtu akitaka kupita kuingia ndani lakini shemeji alikuwa kasimama mlangoni, kama vile anazuia mdogo mtu asiingie, baadaye akasogea kumpisha apite, na nesi kwa haraka akaingia ndani, na shemeji yake akamfuata.

‘Kwanza nambie ….huyo..kich---a, huyo..mpo na nani?’ shemeji kauliza akiangalia lile gari, kwa kupitia mlangoni, hakuweza kumalizia maneno yake.

‘Shemeji,…dada yupo wapi..?’ nesi akauliza kwa ukali mpaka shemeji yake akashituka na kumuangalia shemeji yake akajibu;

‘Dada yupo ndani kalala, hajisikii vyema,….nimerudi kazini kuhakikisha hasumbuliwi,….amelala, tumeche apumzike, najua akisikia sauti yako ataamuka..’akasema

‘Anaumwa…?’ akauliza.

‘Haumwi,..ila kuliko na vurugu hapa, vurugua ikamletea dada yako kudondoka akapoteza fahamu, ikawa mshikeshike…’akatulia

‘Mhh dada ana nini, unajua ilitokea kule hospitalini..lakini alizindukana kwa haraka, akasema hakuna tatizo…hivi mumeshakwenda kupima,…’nesi akauliza kwa akionyesha mashaka fulani.

‘We acha tu…’akataka kuongea na kuaksikiak mlango wa gari ukifunguliwa nje, na kufungwa, nesi akakumbuka kuwa ana wageni, akasema;

‘Oh, unaona nimekuja na wageni,…shemeji kuna wageni nimekuja nao,..’akasema nesi akatoka nje kuwakaribisha na wageni na shemeji yake akamfuatia nyuma, ni kama vile hakutaka shemeji yake aingie ndani ya kumuamusha ndugu yake.

‘Karibuni wageni..’akasema nesi, na wakati huo walishateremka nje ya gari, wakiwa wamesimama, na docta alikuwa akinyosha,na upande wa pili wa gari alikuwa kasimama mlinzi akiwa kambeba mtoto.

 Shemeji mtu alipomuona yule mlinzi kambeba mtoto, akamgeukia shemeji yake ambaye alikuwa kasimama kati kati yao, yaani shemeji yupo nyuma, na mbele wapo hao wageni, akasema;

‘Yule mtoto wa-na-ni…ni yule mtoto mumemlata tena…?’ akauliza lakini nesi hakumjibu akawakaribisha hao wageni waingie ndani,na shemeji mtu akabakia kasimama mlangoni, anashindwa kuwazuia wageni.

Nesi akamchukua mtoto na kuelekea chumba ambacho akiwemo ndicho anakitumia, akafungua na kwenda kumlaza huyo mtoto, baadaye aakrudi, na aliporudi tu, shemeji mtu akasema.

‘Mbona-mbo- tena mnaniletea balaa hapa nyumbani kwangu.  mngelijua nini kimetokea muda uliopita msingediriki kumleta huyo mtoto humu kwangu. Shemeji yako kafikia kupoteza fahamu kwasababu za kizembe..’akatulia

‘Kwani kulitokea nini..?’ akauliza nesi

‘We acha tu, kulizuka ugomvi hapa, ugomvi huo ungeliweza kumsababishia mke wangu mambo mengina….’ Akasema shemeji mtu na kabla hajamaliza nesi akamkatisha.

‘Kwani dada ana matatizo gani...?’ akauliza nesi huku akiangalia mlango wa chumba wanachotumiwa wanandoa hao.

‘Unakumbuka safari yetu ya mwisho kuja kwako, tulikuambia kuwa tumekuja na jambo la furaha, lakini ukatuletea habari zako za huyo mwanamke balaa, ukaharibu furaha yote tuliyokuja nayo, na tukasahau hata kukuambia nini dhumuni la safari yetu…’akasema shemeji yake

‘Mhh ni kweli ...jamani hata sikumbuki maana matatizo ni mengi, yaani hata kuja hapa bado tumekuja tukiwa hatuelewi, matatio yanaongeeka kila siku....’akasema nesi akigeuka kuangalia mlango wa chumba kama dada yake atatokea

‘Kiukweli dada yako hanisikii...siwezi kusema ana matatizo makubwa sana ni ya kawaida tu,najua keshakuambia…ila anahitajika kupumzika sana kama alivyoshauriwa…ndio maana namshauri dada yako asijiingize kwenye vurumai au kwenye matatizo yatakayomletea shinikizo la damu, lakini hanisikii, alivyokuja huyo kichaa, ndio basi …’akasema huku akionyeshea kwa mikono.

‘Kichaa, kichaa huyo ni nani, ni-ni....yule mama kaja huku....?’ akauliza docta ambaye alikuwa kimia, hakutaak kuingilia maongezi ya wawili hao kwanza, lakini aliposikia kuwa kuna kichaa, akajikuta akiingilia na alimuangalai shemeji mtu, na shemeji mtu akawa katulia hakusema neno, na docta akamgeukia mlinzi na kusema;

‘Nilijua tu...’na mlinzi akawa anatabasamu kuashiria kuwa hata yeye anasadiki hilo mlinzi

‘Yaani nyie acheni tu...sikutaka kabisa huyu mtu aingie hapa kwangu, lakini dada yako akamuonea huruma akamkaribisha, hata nyie mlipofika na kugonga mlango, nikajua ni yeye tena karudi, ...ndio maana nikakimbilia kufungua, nipambane naye,.....ni kwanini mkamruhusu huyo mtu kuja huku, kaja mangua ya huko hospitalini…’akauliza shemeji mtu sasa akimuangalai docta.

‘Mhh, aliwezaje kufika huku kwa muda mfupi, alitumia gari gani, kapatia wapi nauli...?’ nesi akauliza na kumfanya docta abakia kimia.

‘Mhh mimi sijui ...mimi ninachoangalia na kujali ni huyu nduguu yako, yeye hanielewi,... Jamani mimi nimeshasema simtaki huyu mwanamke hapa nyumbani kwangu, kwanini mkamuachia kuja huku? ....’akauliza akimgeukia docta na docta kabla hajajibu nesi akaingilia kati.

‘Alipofika hapa alisema anataka nini..?’ akauliza nesi, na shemeji akamgeukia nesi na kusema;

‘Anasema eti kaja hapa kumchukua mtoto wake, anadao mtoto wake yupo hapa kwangu….eti kakumbuka kila kitu, kwahiyo tusimdanganye…’ Akasema .

‘Hebu shemeji tuambie ilitokeaje…mpaka dada apoteze fahamu , kwanini, huyo mama alipigana na dada, au ilikuwaje, na huyo mama yupo wapi..?’ akauliza nesi


‘Huyo mwanamke mimi sijui kaenda wapi, na sina haja ya kujua, ila alipofika hapa alianza kubwata kuwa amejua kabisa kuwa mtoto wake yupo hapa, akaanza kutafuta huku na kule utafikiri yupo nyumbani kwake... ‘akasema

‘Alipofika alikukuta wewe upo nyumbani?’ akauliza

‘Nilikuja kwa bahati tu, dada yako alikuwa akijisikai vibaya, nikaja kuangalia anaendeleaje. Na wakati nafika, dada yako alikuwa kwenye mabanda ya kuku, nikawa nimekaa ndani nikimsubiria mara nikasikia hodi..’akatulia

‘Mtu kapiga hodi na moja kwa moja yupo ndani, …namtaka mtoto wangu, najua yupo hapa…kaingia huku katoka kaingia huku katoka, nikaona sasa huyu ananitafuta ubaya, ikabidi mimi nimzuie, akaanza kugombana na mimi,na mara mke wangu akatokea kutuamulia.

Katika heka heka hizo za kutuamulia, mke wangu akasukumwa na huyo hayawani, wewe…alinigusa pabaya, nilitembeza mkongoto, mpaka yule mwanamke akadondoka chini, nilijua nimeua, lakini mwanamke yule ana roho ya paka, alikaa kidogo akaiunuka na kuanza kuandelea kudai kuwa anamtaka mtoto wake...’

‘Una maana ukampiga mama wa watu , shemeji nawe, mtu mwenyewe bado mgonjwa, unapiga utafungwa..’akasema nesi

‘Waje wanifunge, mtu ataingiaje  nyumbani kwako na kuanza kutafuta chumbani wapi..kama kwake vile..siwezi kuvumilia, ..’akasema

‘Alipofika unasema alikuwa na vazi la hospitalini,..alikuwa kajifunika uso wake?’ akauliza mlinzi

‘Atajifunua,…hahah ili muone hiyo sura yake, hatamaniki …’akasema na akawa kama anawaza jambo

‘Kwanini, kwani ulishawahi kumuona sura yake..?’ akauliza docta.

‘Huyu mwanamke alipokuja hapa bado alikuwa hajanitambua vyema,sijui kama mnavyosema alikuwa kapoteza kumbukumbu…lakini tulipoanza vurumai, akawa kama kaniambua, akabakaia kaduwaa…’akasema

‘Shemeji kukutambua kama baba wa nyumbani au?’ akauliza nesi.

‘Unajua ile kuduwaa, kama vile umeona mzuka au kitu gani, ndivyo ilivyotokea kwa huyo mama,..nahisi sasa kanikumbuka…’akasema na docta nesi na mlinzi wakawa kimia .

‘Ghafla, eti… ananisogela na kupiga magoti mbele yangu eti akiniomba msamaha ya kuwa haikuwa kusudi lake. Nilitamani nimmalize, kwahasira…nilijikuta nikikivuta kile kitambaa alichojifunga usoni, na kubakia uso wazi…’akasema

‘Mungu wangu….shemeji, ..’akasema nesi.

‘Hutoamini mke wangu siku zote alikuwa hajawahi kumuona huyo mwanamke akiwa wazi kiasi hicho, hata hivyo yeye hamjui vyema kuwa ni nani. Lakini mke wangu alipomuona jinsi mwanamke huyo alivyoiharibika uso akataka kukimbia,…ulikuwa mshituko mkubwa sana kwake, ndio akadondoka na kupoteza fahamu.

Nikawa nahangaika na mke wangu, sikuwa na mawazo na huyo mwanamke tena, ….kabla sijafanya mpango wa kumpeleka hospitalini, ndio akaja jirani, simu zimezima hazina chaji, nikamwambia anisaidie tumpeleke hospitalini, nahisi ndiye akkupigia simu kukusumbua bure…’akasema.

‘Hebu kwanza, samahani niingili kati kidogo..’akasema docta

‘Huyo mama yupo wapi?’ akauliza docta

‘Sijui…’akasema shemeji

‘Shemji unasema sura ya uso wake, imeharibiwa, si ni yale mapanga alikatwa katwa na wale wahuni waliomungilia siku hiyo walipochoma nyumba moto,au..?’ akauliza nesi.

‘Sijui….’akasema sehmji kama vile hataki kumuongelea huyo mama.

‘Kwani shemeji hukumuuliza vyema kuhusu yaliyomkuta hadi kuharibika huo uso… ‘akauuliza nesi, na wakati huo docta naye akauliza swali jingine.

‘Hakuna mtu aliyejua wapi kaenda..?’ akauliza docta.

‘Niwaambia kitu sitakii kuongea kuhusu huyo mama hapa nyumbani kwangu, simtaki, na nilishamsahau…kwanini anazidi kunitesa..’akasema

‘Ina maana shemeji ulikuwa ukimfahamu huyo mama kabla…na huenda unajua kwanini aliharibika huo uso, kuacha hilo la kukatwa katwa na mapanga, au…’ akauliza docta.

‘Aliharibikaje huo uso …mimi nitajuaje…?’ akauliza shemeji, sijui kwanini alirudia hilo swali, lakini nahisi kuna kitu kilikuwa kikimkereketa moyoni, ingawaje matamshi yake baadaye yalionyesha tofauti.

‘Mimi kuharibika kwake huo uso hakunihusu na kwanini nimuulize,…ili iweje?’ akawaangalia nesi docta na mlinzi kwa zamu.

‘Lakini ulikuwa ukimfahamu kabla…?’ akauliza docta

 ‘Ndio namjua sana huyo mwanamke, namjua sana kipindi akiwa msichana, namjua toka utotoni, namjua ….hadi siku ile aliponisaliti. Huyu mwanamke alikuwa mchumba wangu…’ alapotamka hapo kila mtu aliguna.

NB: Jamani nipo kwenye mitihani, mitihani ya kimaisha, najaribu kupambana nayo, lakini akili haijawa sawa , naombeni niishie hapa kwa leo

WAZO LA LEO: Mara nyingi migomo ikitokea wanaoathirika ni raia wa kawaida, unapoigomea serikali kwa matakwa mbali mbali,…ni nani anaumia? Tuchukulia mfano halisia mgomo wa madocta, wameigomea serikali, wanaoumia ni nani,…haya leo hii kuna mgomo wa madereva wanaigomea serikali, ni nani anaumia…Ni yale yale ya wanapogombana mafahali wawili, zinazoumia ni nyasi, au sio..nyasi ni nani? Sasa ni wakati wa raia kujua wao ni nani katika nchi, na wanapochagua viongozi wao wajue kuwa mwisho wa siku matatizo yakitokea wao ndio wahanga. Uchaguzi 
Ni mimi: emu-three

No comments :