Kwa wanaofuatilia kisa wakumbuke kuwa kisa hiki nasimuliwa na
rafiki yangu, na mapaka hapa tulipofikia rafiki yangu huyu anasimulia jinsi
alivyosimuliwa na mama yake, kwani hayo matukio ya nyuma yeye alikuwa mdogo na
hakujua ni kitu ani kilitokea, yeye hakuwa anamjua mama yake huyo
Sehemu iliyopita tuliishia kwenye swali `Je kuna nini huko…’’ ,
Rafiki yangu anayenisimulia kisa hiki alipofika hapo aliangalia saa
yake, na mara akasimama, wakati mimi najiweka sawa kusikia jibu la swali hilo.
Cha ajabu Nikamuona rafiki yangu
akisogeza kiti nyuma, na kujikunguta mapajani kuondoa vitu vilivyodondokea
kwenye suruali yake, halafu akainuka kama anataka kuondoka, mimi nikayulia
nikimuangalia.
Nikajiuliza anataka kwenda
kujisaidia nini, kwani kauli yake ya mwisho alivyoitamka, nilijua kabisa
kaitamka ili kunogeshea kisa, kumbe ilikuwa kauli ya kuhitimisha na kuniacha
roho juu. Sikukubali…kwani nilikuwa na hamu ya kujua nini kilitokea nikasimama
haraka kumzuia.
‘Vipi ndugu yangu mbona unaondoka wakati hujafika mwisho wa kisa
hiki, na mkasa wa maisha ya mama yako…’ nikamwambia na yeye akatabasamu halafu
akakunja uso kuonyesha ishara ya huzuni. Akasema....
‘Mjumbe, sehemu iliyobakia ….mmh, nashindwa kuendelea nayo kwasasa
kwababu ni sehemu inayonitia huzuni sana , na sikupenda kumsimulia mtu yoyote,
kwani ni sehemu ambayo nilikuwa nimeshaanza kuelewa.. , ingawaje nilikuwa bado mdogo,
lakini kumbukumbu za nini kilitokea, zipo akilini, kwakweli maisha yalivyokuwa
yalikuwa ni shida, taabu, unyanyaswaji na…huwezi amini.... naona niishie hapa
tu...’akasema
‘Hapana, hujanielezea kulitokea nini baada ya nesi kupokea simu
kuwa nyumbani kwa dada yao kuna matatizo aende huko haraka, je wakubwa zake
walimruhusu ….je aliondoka na mtoto, na kulionekana kama vile maakitari
wanahisi jambo, kuwa mtoto hayupo, ilitokeaje...?’ nikamuuliza, nay eye akakaa
kimia kwa muda, na sikumpa nafasi nikaendelea kumuuliza
‘Na huyo mama haonekani, kaenda wapi na je huyo mama ndio huyo
mama yako au kulikuwa na mama mwingine kajiigiza kama yeye, maana hospitalini
hayupo, na haijulikani alipokwenda, au…?’ nikamuuliza
Jamaa yangu akatulia, akageuka na kuangalia kwa wahuumu wa hiyo
hoteli, akaagiza vinywaji na chakula, akasema;
‘Unajua wengi wanahisi kisa hiki ni cha kutunga, lakini ndivyo
ilivyotokea kwa mama yangu, mama yangu kapitia maisha magumu, na hayo
niliyokuelezea ni baadhi tu, kuna mengine nikikumbuka..hata mimi mwenyewe
nalia..mama aliteseka sana, na utaona kuwa aliteseka kwa ajili yangu, ...
‘Mama yangu aliniambia kuna muda alijiwa na kitu kama njozi
achague kuishi kwa mateso hayo kwa ajili yangu, mtoto wake, au achague kufa akastarehe peponi,...lakini kwa mapenzi aliyo nayo dhidi yangu alimuomba
mungu aendelee kuishi, ajifungue kwa shida, hata kama ni kwa kuteseka, ili niweze
kuiona dunia, na ikamjia yena wakati nimeshazaliwa kuwa afe, maana
nimeshazaliwa, akaomba kuwa hata kama ni kwa mateso anaomba aishi ili aweze
kuniona, ili tu aweze kuhakikisha nipo salama.
‘Hebu fikiria kwa hali ya mama, hana aina yoyote ya kipato, hana
mahali pa kuishi,hajijui, lakini bado
alinitafuta, bado alinitaka niwe naye..mimi simjui ...yeye hadi hapo alipofikia
hanijui, ...anachojua ni kutokana na ndoto...sasa jiuliza akikutana nami atanitambuaje...
‘Hapa uone jinsi gani damu ilivyo na nguvu, jinsi gani mama
anavyoweza kutambua damu yake, hata uwe wapi akikuona atakujua...ni
kwanini...hata akiwa kapoteza kumbukumbu, lakini kumbukumbu ya mtoto wake
haipotei,..ni kwanini, hata awe hana akili sawasawa, lakini akili hiyo bado ina
mapenzi ya mtoto wake..hataki mtoto wake achukuliwe, hujawahi kuona akina mama
wenye matatizo ya akili, mabarabarani wana watoto wao, hebu jaribu kumchukua mtoto
wake uone kasheshe lake...
‘Utakuja kuona kuwa mama yangu alijua hana uwezo, lakini hakutaka
kabisa kuniachia niishi na watu wengine,...mimi simjui...nalelewa maisha
bora,.. utakuja kuona jinsi gani ilivyokuwa huko mbele kuwa hata kama utapata
ukachuma, au unaishi masha bora kamwe usije kutakabari, ukamkana mama yako,
utaumia,..’akatulia
Utakuja kuona ujanja ujanja....uliotokea, na kujua kama kweli huyu
mama wa huko hospitalini kweli alikuwa ndiye mama yangu...au alikuwa ni mama wa
uwongo,.., ..
‘Ndugu yangu usinione leo nipo hivi, ...’akajiangalia huyo rafiki
yangu ambaye kipindi cha nyuma nilipokutana naye alikuwa kakonda hai kuonekana
kama anaumwa ukimwi, lakini leo ni pandikizi la mbaba, tajiri...
‘Yote haya yasingelikuwepo isipokuwa kwa kujitolea kwa mama
kuteseka kunyanyasika, kaanzia kuitwa mgumba,..eti hazai,...haya akapata
ujauzito ...na bado akawa haaminiki, eti mimba hiyo ni ya kuzini....akapigwa,
na kuponea tundu la sindano, akiwa na mimba yangu...akajifungua kwa shida, na
baada ya kujifungua akawa hajijui...akaja kuitwa mchawi, na huk kuitwa mchawi
kaanzia kuitwa bado hajanizaa, kanizaa,..nimekuwa mkubwa najijua nina
kazi,....anaitwa mchawi, kwasababu ya macho, kwasababu ya kuharibiwa
sura,,,inaniuma sana
Alipofika hapo hakuweza kujizuia, akaanza kububujikwa na machozi.
‘Ndugu yangu, ..nani kama mama...mama yangu alitambuliakana
amekufa, na kufufuka kwa ajli yangu, na kaburi lake bado lipo,...nimefika hiyo
seheme, seheme ambayo, iliambiwa ndipo mama alizikiwa, akaja kufufuka kwa ajili
yangu....
Mama alipojifungua kunizaa mimi akapoteza kumbukumbu zote, lakini
bado kumbukumbu ya kuwa ana mtoto ikaendelea kuwepo, kumbukumbu ya mtoto wake
haikupotea kwanini,...na bado akiwa hajitambui anatembea kama mtu yupo kwenye
njozi, akaendelea kunitafuta, hapo hajijui hata yeye mwenyewe hajijui kuwa ni
nani....’akatulia
‘Narudia rudia ili upate kuelewa zaidi....’akasema
‘Kwahiyo huyo mama aliyekuwa kachanganyikiwa ndiye mama yako au
ilikuwaje?’ nikamuuliza
‘Tutakuja kujua huko mbele, maana dunia hii nayo ina mambo yake,
wanadamu wanaweza kufanya mambo ukashindwa kuamini, watu wanaweza kujisingizia
kuwa ndio wao kumbe sio wao....muhimu kumbuka kuwa kisa hiki hadi hapo
anayenisimulia ni mama yangu, maana mimi nilikuwa bado mchanga, sijijui simjui
,,na niliyekuwa namfahamu kuwa ni mama yangu, ni mama huyo wa kufikia...
‘Sawa endelea na sehemu hiyo pale nesi alipopigiwa simu,
ilikuwaje,....?’ nikamwambia ili asije kuondoka kabla hajamaliza kisa hiki
Tuendelee na kisa chetu
*******
‘Nesi alipopata hiyo simu yenye utata, aliomba ruhusa aondoke
haraka akawaone ndugu zake, lakini madakitari hasa bosi wake akatoa rai, kuwa
ni vyema waondoke pamoja na yeye, na pia
waondoke na yule mtoto, maana huenda huyo mama atakuwa kaelekea huko.
‘Na kwa muda huo vipimo vilikuwa tayari, lakini cha ajabu hakuna
aliyekumbuka hilo, ...uone miujuza ya mungu ilivyo, hakutaka hilo liwekwe wazi
mapema...’akasema rafiki yangu kutoka kwa maelezo ya mama yake.
Basi ikakubalika hivyo na wakati huo mtoto alishachukuliwa kule
alipokuwa akicheza na wenzake, unajua watoto tena, wakikutana na wenzake,
wanasahau kila kila kitu...
‘Baby twende kwa mama...’akasema nesi
‘Twende mama...’akasema akionyesha furaha kubwa,
‘Ndio twende kwa mama yako...’akamwambia
‘Sokoni...?’ akauliza maana aishaambiwa kuwa mama yake yupo sokoni
hajarudi.
‘Mhhh..nyumbani, ...’akasema na ikabidi apitie kwake, kujiandaa
kidogo na alipokuwa tayari, bosi wake akaja na gari lake wakachukuliwa na msafara
ukaanza kuelekea huko kijijini...
NB: Le ni siku ya mapumziko tupo nyumbani, nilitaka kuliweka hili
wazi kidogo maana watu wamesahau wapi kisa kilipoanzia, kuwa kisa hiki
nasimuliwa na rafiki yangu ambaye kwa sehemu sehemu kubwa alisimuliwa na mama
yake alikutana na mateso haya.
WAZO LA LEO: Tufanye nini ili kumkidhia haja mama yako angalau
aone kuwa wewe una mjali, ...na hata kama katungulia mbele ya haki, una wajibu
gani wa kufanya kuwa kweli unamjali mama yako.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment