Licha ya nesi kujitetea lakini sheria ilitakiwa ifuatwe, kwa kosa
la kumchukua mtoto wa mtu mwingine bila maandishi yoyote, ndivyo ilivyoandikwa
kwenye kumbukumbu za kiusalama, akaambiwa mengine yanasubiria matakwa ya mlalamikaji, na pia kuna mlango wa majadiliano kati ya walengwa hao yaani nesi kwa upande wake na huyo mama kama mlalamikaji.
Tuendelee na kisa chetu.
Nesi akafikishwa kituoni, kwanza akatakiwa kujieleza, nini
kilitokea hadi akamchukua huyo mtoto, akajieleza kama alivyojieleza kazini
kwake, na kabrasha maalumu likafunguliwa kwa ajili ya kesi hiyo.
‘Kwahiyo nimeshitakiwa kwa kosa la kuiba mtoto?’ akauliza nesi alipoona akihojiwa na kuandikwa kila anachokisema.
‘Hapana hujashitakiwa bado..., kwa hivi sasa unaisaidia polisi..kama huyo mama ataamua
kukushitaki basi utakuwa mshitakiwa, lakini kwa hivi sasa, kwa vile tuna uhakika
unaye huyo mtoto aliyekuwa akitafutwa wewe tunakushikilia kama mshukuwa, kama mtu wa kuisaidia polisi kuhakikisha huyo mtoto anapatikana salama....’akaambiwa
‘Kwanini mna.....eti unasema salama, miaka mwili mlikuwa majua huyo mtoto anaishi wapi, anakula nini...halafu mnataka nilale rumande, hapana hilo sikubali kwa kosa gani…?’
akauliza
‘Taratibu lazima zifuatwe nesi,…..hili tatizo lingeisha mapema
kama ungelitoa ushirikiano ulipotakiwa kufanya hivyo,..tunajua huenda huna hatia, lakini kwa vipi, wakati wewe ni makidi wa sheria, ulitaka sisi tufanye nini, tukupigia magoti….’akasema huyo mtu wa usalama.
‘Naomba simu niongee na ndugu zangu…’akasema nesi akiomba vitu vyake ambayo vilishashikiliwa.
‘Hapo umezungumza la msingi, lakini kwanza unatakiwa uingie huko....unakiona chumba kile... ili sisi tumalize kazi zetu..’akaambiwa nesi na nesi akageuka kuangalia kile chumba akakumbuka watu waliwahi kuwekwa hapo wanavosimulia, ni kuchafu...mbu...mwili ukaanza kumsisimuka.
‘Hapana..hapana afande, siwezi kwenda huko,….ina maana mimi nabeba makosa ya wenzangu..’akalalamika,
na mara mkuu wa kituoa hicho akafika na akaelezewa kinachoendelea, akachukua
simu na kuongea na mtu baadaye akasema;
‘Umeshawasiliana na ndugu zako, kuhusu huyo mtoto?’ akaulizwa
‘Ndio nataka niongee nao..niliwaomba hivyo,......’akasema
‘Basi muachane aongee na hao ndugu zake, halafu tutajua la kufanya…’akasema huyo
mkuu na nesi akachukua mkoba wake ambao ulikuwa na simu yake..
‘Hapana usitumie simu yako, tumia simu hii ya hapa kituoni….’akaambiwa
na nesi akawatajia namba za ndugu yake , ilikuwa namba ya shemeji yake na simu ikaiita wa muda, na aliyejitambulisha mwanzoni alikuwa
mtu wa usalama kuwa hapo ni kituoa cha polisi, akaijielezea kuwa yeye ni nani.
'Kwani kuna nini...?' sauti ya shemeji mtu ikauliza kwa ukali
'Kuna ndugu yako nesi ni shemeji yako, anataka muongee naye....'akasema, nesi akachukua ile simu na kuanza kuongea.
‘Shemeji nimekamatwa nipo kituoni, ..kosa ni kuwa tumemchukua
mtoto wa watu bila kibali maalumu…’akawa anaongea kwa sauti ya kulia
'Mtoto yupi..?' shemeji akauliza akijua huenda ni mtego
'Huyo mliye naye hapo...'akasema
‘Subiri uongee na dada yako….’shemeji yake akamwambia na baadaye
akawa aanaongea na dada yake akamuelezea hivyo hivyo.
‘Mungu wangu ndio imekuwa hayo, sasa jamani si wao walikukabidhi
huyo mtoto kwanini wasifungwe hao waliokukabidhi huyu mtoto, …sasa wanataka sisi tufanye nini, …’dada mtu
akawa kachanganyikiwa, na yule mtu wa usalama akachukua simu mkononi mwa nesi akaanza kuongea yeye.
‘Kiutaratibi ndugu yenu atashikiliwa mpaka hapo mtoto huyo
atakapofikishwa kunakohusika, tulitaka mumlete huyo mtoto hapa, lakini kwa vile hatujajua
kuwa huyo mtoto yupo salama, mtahitajiak mumeleta kule hopsitalini apimwe na taratibu zote zitafanyika huko hospitalini,..., tutakutana
huko, tuone cha kufanya….’huyo mtu wa usalama akasema
‘Tafadhali msifunge mdogo wangu, mtoto tunaye hana matatizo yoyote
tumemlea kwa uadilifu kabisa kama mtoto wetu..na hatujua kuwa kuna matatizo hayo...ni makosa ya kazini kwako,..mngetakiwa muwakamati hao walimkabidhi mdogo wangu huyu mtoto.....’dada mtu akawa anongea kwa wasiwasi mkubwa...akajikuta anajieleza kupita kiasi, kitu ambacho walikihitajia sana hao watu wa usalama, na kumbukumbu
zikawekwa.
‘Hamna shaka, sasa kesho asubuhi tukutane hospitalini mkiwa na huyo mtoto wewe na mume wako...asubuhi na mapema, mnasikia..’akaambiwa
‘Lakini mdogo wangu msifunge….’akasema
‘Usiwe na wasiwasi na mdogo wako , yeye ni mfanyakazi wa serikali,
atajidhamini, na pia kazini kwao, wanaweza kumdhamini vile vile..tutaona
taratibu zinavyokuwa , muhimu mumuandae huyo mtoto kiasi kwamba hataathirika
kisaikolojia...natumai mnanielewa nikisema hivyo...’wakasema
‘Oh,…jamani kwanini hivi….’akawa analalamika huyo mama na simu ikakatwa.
**********
Ilikuwa ni asubuhi na mapema, wanandoa wakiwa na mtoto walifika
hospitali ya mkoa, na walipofika, wakauliza kwa mkuu wa hospitali, wakaonyeshwa,
lakini kwa muda huo mkuu alikuwa hajafika, ikabidi wasubirie nje ya hiyo ofisi na walijua kuwa
mdogo wao yupo polisi kwahiyo hawakutaka hata kumuulizia.
Haikuchukua muda landrover ya polisi ikafika, na nesi akateremka,
na nesi alipowaona ndugu zake akawakimbilia, na kumkumbatia dada yake,...wakaanza kusalimiana na dada mtu aakwa anamkagua ndugu yake kama hakuumia mahali, na wakati huo huo wale jamaa wawili watu wa usalama na askari wengine wawili, wakatoka kwenye gari na kusimama wakiwaangalia wana familia hao.
‘Oh aheri mumekuja..hata sijui niseme nini..oh jamani mtoto
haujambo baby..’akawa anamsalimia mtoto na mtoto alikuwa anaangalia huku na
kule hajui kinachoendelea. Mtoto huyo walizoea kumuita hivyo baby, japokuwa ni mtoto wa kiume.
‘Alikuwa amelala,, kaamuka sasa hivi…’akasema mama mlezi
Mara shemeji mtu, akasimama ghafla ni kama kakumbuka jambo, akamsogela mke wake ambaye alikuwa kambeba huyo mtoto,
akamchukua yule mtoto, na kumbeba yeye, akasogea na kukaa mbali kidogo na wao, halafu akawa
anamchunguza huyo mtoto usoni, na huku anatingisha kichwa, halafu kama mtu
aliyeona kitu cha kutisha, akainua kichwa juu, na akwa anaongea peke yake....,akasema;
‘Mungu wangu, ni sura yake kabisa…hivi kwanini sikujua hili
mapema....anafanana sana na baba yake... nilijua tu, mwisho wa siku itakuwaje, sasa iko wapi…malipo ya
dhuluma, ni hapa hapa duniani…’ akaendelea kumchungulia tena yule mtoto, sasa
hivi akamshika kichwa chake, na huku anamtizama kwa makini.
Akasema, kwa utaratibu kama ananong’oneza :
’Unajua macho yako yanafanana sana na macho ya mama yako, mama yako ana mcho kama haya …na sura yako ya usoni,....mhh ni kama ya
baba yako kabisa,… hapana kidogo kwa mama yako, kidogo kwa baba yako. Na huenda
hata roho yako itakuwa kama ya baba yako au sio…..’ akasema kama anaongea na mtoto, baadaye akainuka na kuelekea pale walipokaa mkewe na shameji yake, akimkabidhi mkewe
mtoto.
Kwa muda huo nesi alikua akiongea na dada yake lakini sikio alikuwa kalitega huko kwa shemeji yake, alisikia baadhi ya maneno maana kulikuwa na upepo, na alichokisikia kilimfanya aweza mara mbili tatu kuhusu shemehji yake na huyo mama. Na jinsi alivyomuona shemeji yake,. alimuona akiwa na mabadiliko makubwa sana, kakonda, hana raha,..na yupo kama ana wasiwasi kama hayupo sawa,
lakini hakutaka kusema kitu kwa muda huo.
Mke mtu naye alikuwa akimuangalia mumewe huku akiongea na mdogo wake, yeye hakuwa makini na hicho mumewe anachokiongea japokuwa alisikia baadhi ya maneno, hata yeye akilini alitambua kabisa kuwa mume wake sio yule mtu
anayemfahamu, alikuwa kabadilika kabisa, ile tabia yake ya huruma anayoijua kwa
mumewe imetoweka ghafala hasa baada ya kuambiwa kuwa huyo
mtoto ni mtoto wa huyo mama wa mitaani
Kwa muda ule hakuna aliyemuuliza swali na kwa muda huo wale watu
wa usalama walikuwa wanaongea yao tu….ni kama vile hawana habari na wanafamilia hao.
Mara shemeji akaonekana kutaka kuondoka, akageuka kule
waliposimama watu wa usalama, akahisi wakimchuguza kwa mashaka, akatembea hatua
kadhaa mbali na walipokaa wanafamilia wenzake, akakaa na kujiegemeza huku akiwa
kashika kichwa.
***
Baadaye shameji mtu akasimama na kuwaendelea watu wa usalama
akaongea nao kwa muda ikaonekana hakuna makubaliano, akarudi akakaa, na
haikupita muda, mkuu wa hospitali akafika, na madakitari wengine. Watu wawili
wa usalama wakamfuata mkuu huyo wa hospitali ofisini kwake na pape wakabakia askari wawili.
Ilichukua muda, haikujulikana wanaongea nini, na baadaye shemeji
akashindwa kavumulia akaeleeka kwenye hiyo ofisi na kuingia , walikaa huko kwa
muda, na baadaye shemeji akatoka na kuanza kuondoka.
‘Vipi mume wangu mbona unaondoka na kuniacha…?’ mkewe akauliza
‘Wewe subiri mumalizane nao mimi natangulia kituoni, hakuna
tatizo, muhimu kabidhi mtoto wa watu mengine tutaongea nyumbani….’akasema
akiendelea kutembea
‘Mume wangu sio vizuri hivyo….’akalalamika mkewe
‘Fanya nilivyo kuambia kwa usalama wako…’akasema na mtoto ndiye
aliyekatisha hayo mazungumzo ya wawili hawa ..kwa umri huo alishaanza kuongea
ongea maneno, yaonekana pia alikuwa mzito wa kuongea, …., akasema
‘Baba-bye, kazini…zawadi eeh..’akasema na baba mlezi hakugeuka
nyuma, mtoto akazidi kuita
‘Baba byeee, zawadi eeh..’alishazoea baba yake akiondoka kama yupo
macho babayake huyo humbeba huyo mtoto na kumuambia;`bye nitakueleta zawadi ‘
lakini leo inaonekana tofauti baba anaondoka na hafanyi kama ilivyozoeleka.
‘Baba nanihii..njoo kwanza mtoto anakutaka umuage..’mke mtu akasema
lakini mzee mzima ndio kwanza anachanganya miguu
‘Baba bye….zawadi eeh..’mtoto akawa sasa analia anataka kumfuata
baba yake, ikabidi mama mlezi aanze kufanya kazi ya ziada, akasema
‘Sikiliza baby…baba kachelewa atakuleta zawadi eeh , haya njoo
hapa ulale..’akaanza kazi ya kumbembeleza, na wkati anafanya hivyo hisia za
kuwa huyo mtoto sasa sio wao tena na huenda leo ikawa ni mara ya mwisho kuwa
naye, hisia hizo zikaanza kumuingia kwa kasi, hakuweza kuvumilia machozi yakaanza
kumtoka.
***********
Kwa muda ule nesi alikuwa katoka, akiwa na majukumu mengine ya
kikazi,na wakati anarudi ndipo akakutana na shemeji yake akashangaa kumuona
shemeji yake akiondoka, na hata alipomfikia hakusema neno, wala kusema natoka
au naondoka, ikabidi amuwahi na kumshika mkono.., akauliza
‘Vipi shemeji mbona unaondoka,…?’ akauliza
‘Mimi nimeshamalizana nao, iliyobakia ni wewe na dada yako,…’akasema
shemeji mtu akivuta mkono wake kwa nguvu, na nesi akauachia akionyesha
mshangao.
‘Lakini shemeji kuna mambo ambayo wanayahitajia, na wewe yaonekana unayafahmu zaidi,
ungesubiri tuyamalize kabisa…’akasema
‘Unanisikia mimi nimeshaongea nao, huyo mwanamke simjui….na huyo
mtoto wewe ndiye uliyemleta ukatuomba tumlee, basi iinatosha, sina zaidi..’akasema
akitembea kuondoka
‘Shemeji …shemeji..’nesi akawa anaongea lakini shemeji yake
utafikiri sio yule mtu aliyemzoea akawa hata hataki kusimama mbio mbio akaelekea
njia ya kutoka nje ya hiyo hospitali, hakutaka hata kumsubiria mkewe, sembuse
huyo shemeji yake.
Nesi akajaribu kumfuata kwa nyuma shemeji yake lakini ndio kama
anamfukuza hadi getini, shemaji akatoka nje, ya hiyo hospitali. Ikabidi nesi amrudie dada
yake ili ajue kuna nini kimetokea, kwani yeye alijua kuwa baadaye wote wataitwa
kwa mkuu na kukaa kama kikao, kuyamaliza hayo mambo, na ikibidi huyo mama mzazi
aitwe waongee kwa pamoja japokua hilo mama mzazi hakulitaka kabisa..zaidi ya
kutaka mtoto wake.
Dada mtu hakuweza kuongea klilichokuwa kinaendelea yeye alikuwa
akilia tu, hadi nesi akaona sasa mtoto anaweza kuiona hiyo hali, na kwa vile
mtoto alishalala, yeye akamchukua huyo mtoto hadi chumba maalumu na kumlaza, na
baadaye akarudi kwa dada yake.
‘Mbona shemeji kaondoka,….?’ Akauliza tena nesi
‘Hivi mume wangu ana nini…ina maana ule upendo wote wa mtoto umekwisha, ….yaani anaamua
kuondoka na kuniacha, …sijui ….’ Akawa aanongea na mdogo wake akafika na kukaa
pembeni yake, akawa anamshika shika mgongoni kama kumbembeleza, mtu na ndugu
yake hapo.
‘Shemeji inaonekana ana hasira zake sijui ni kutokana na nini,
badala ya kusubiri tutafute ufumbuzi , anachukulia hasira nahisi kuna jambo kati yake na huyo mama, una
uhakika kweli walikuwa wakiishi vyema wakati huyo mama yupo hapo nyumbani
kwenu?’ akauliza nesi
‘Hakukuwa na tatizo lolote, ila nilihisi namna ya mabadiliko ya
tabia ya mume wangu, mara nyingi nilimfuma mume wangu akimuangalia sana huyo
mama… nilimuuliza kwanini anamuangalia sana huyo mama, na alisema kuwa anamuonea
huruma mama kama huyo..’akasema
‘Hebu niambie kabla hajakuoa, mumeo hakuwa na msichana…au ?’ nesi
akajikuta anauliza swali
‘Mhh swali gani hilo tena, wewe unahisi kuwa huyo mama, alikuwa na ….hapaan, haiwezekani,
wewe huoni kuwa huyu mama ni mkubwa kuliko mume wangu..’akasema dada mtu
‘Mhh, ni shida ndio imemfanya huyo mama aonekane mkubwa, lakini,
kiumri wala sio mkubwa sana..’akasema nesi
‘Unajua mambo ya shemeji yako ya huko nyuma hapandi kabisa
kuyaongelea, nakumbuka wakati tunachumbiana aliwahi kunigusia kuwa aliwahi
kuchumbia msichana wakati huo anatafuta mke, hatua ya mwisho huyu mchumba wake
akamkimbia eti kwasababu kapata mume tajiri,…akifika hapo anakasirika na hapendi
kuendelea kuliongelea hilo..’ akasema dada mtu.
‘Mhhh…’akaguna nesi akikumbuka yale maneno ya shemeji yake
alipokuwa akiongea, kuwa huyo mtoto anafanana na mama yake na nusu na baba
yake, ..mke mtu alijua anaongea kuhusu wao, kama baba na mama, lakini nsei
alijua anaongea kuhusu mama yake mzazi na mume wa huyo mama, kwahiyo shemehi
yake anawafahamu, ndio maana alitaka waliongelee hilo mbele ya utawala
ijulikane moja.
Dada mtu hakuwa na shaka na mume wake kuhusu huyo mama akilini
aliona ni jambo lisilowezekana kwa mume wake kuwa na mahusiano na huyo mama
huko nyuma, akabadili maneno na kuuliza;
‘Nilikuona mkiongea naye pale, kakumbia nini?’ akauliza dada mtu kwani aliwaona
kwa mbali wakiongea mdogo wake na shemeji mtu.
‘Kasema tumrudishe huyo mtoto kwa mzazi wake, na hataki kumuona
tena huyo mama na mtoto wake wakirudi kwenye nyumba yake…hiyo ni amri..’
akasema mdogo mtu.
‘Lakini sasa nyie mumefikia wapi, maana …hata sijui nifanye nini,….siwezi
na sitaweza kukaa mbali na huyo mtoto, ni mtoto wangu jamani..’akasema na
machozi yakimlenga lenga.
‘Mhh, dada kwa hatua iliyofikia hatuna la kufanya,…naomba uvumilie
ujitahidi, ..na tutaona huko mbele itakuwaje, kama unahitaji mtoto ..nitafanya
mipango, unajua wapo watoto, hawana wazazi….na mungu atasaidia ipo siku utapata
mtoto wako..’akasema nesi.
‘Unajua mimi nawashangaa, mtoto ana kosa gani…yupo kwenye malezi mazuri
tu, kwanini huyo mama yake asisubiri, ..mtoto atakuwa basi huko mbeleni
tutakuja kuongea..tutakuja kumfahamisha..’akasema
‘Hilo nililiongelea, lakini wewe hujakutana na huyo
mama,..kabadilika, kawa mbogo…hataki kusikia chochote zaidi ya kumpata mtoto
wake, hataki mtu kumchukua mtoto wake, kasema yeye mwenyewe atamlea, hata kama
nikwa shida ….’ Akasema nesi
*********
Baadaye wakaitwa nesi na dada mtu kwenda kuongea kwa mkuu wa
hospitali, na walipofika maelezo yalikuwa mafupi tu, kuwa mtoto keshapata mzazi
wake, na kwa vile taartibu za kumchukua huyo mtoto hazikufuatiliwa, basi mtoto
arejeshwe kwa mama yake na mengine yote yatategemea mama yake atakavyo penda.
‘Lakinni huyo mama hajiwezi , hana jinsi ya kijikimu..’akasema
nesi
‘Kasema anaweza kuishi na mtoto wake kwa hali yoyote..’akaambiwa
‘Hivi kweli nyie mnaubinadamu, huyo mtoto katoka kwenye hali
nzuri, analelewa vyema , leo hii umchukue akaishi , sijui wapi, kwani kawaambia
anaishi wapi?’ akauliza nesi.
‘Hiyo kwa hivi sasa sio kazi yetu, kazi yetu ilikuwa kuhakikisha
kuwa mtoto huyo kapatikana na tunamkabidhi kwa mama yake, sasa kama kuna
amtatizo mengine, tutakuja kuyaona,….’akasema mtu wa usalama.
‘Kwahiyo…?’ akauliza mama mlezi
‘Mkabidhi mtoto nesi, yeye atajua ni nini cha kufanya, wewe
tunakushukuru kwa wema wako, na ….mngelionana na huyo mama, lakini kwa hasira
alizo nazo kuhusu nyie, ..hataki hata kuwaona,..alichosema anataka mtoto wake,
..’akasema
‘Lakini mbona tumeishi naye kwa wema tu, hatukuwahi kumfanyia
ubaya wowote, kwanini afikia hatua hiyo..’akasema
‘Ilikuw kumbukumbu hazijamrejea, na kumbukumbu zimemrejea anahis
huenda nyie mlifanya mpango ili afe ili mumuchukue mtoto wake,..hizo ni baadhi
ya hisia zake, kwahiyo kuna hali ya kutokuwaamini,…’akasema.
‘Jamanio ndio kafikia kusema hivyo…’akasema huyo mama
‘Unajua hapo alipo, anahangaika kupata ukweli, bado hajawa sawa,
anatakiwa awe karibu na mtoto wake, na hilo litampa faraja…’wakasema
‘Ina maana akishampata mtoto wake, itakuwaje, ataendelea kukaa
hapa hapa..au atakwenda wapi?’ akauliza nesi
‘Hilo tutakuja kufahamu,….kwanza lifanyike hilo la yeye
kukabidhiwa mtoto wake, mengine yatafuta …mama wewe unaweza kwenda, nasikia
mume wako anakuulizia huko getini hajaondoka, anasema uende haraka…’akasema
askari.
Basi angalau nikamuone mtoto kwa mara ya mwisho..’akasema na
akaruhusiwa
******
Mama mlezi akafika pale alipolazwa mtoto! Akamwangalia yule mtoto,
akajikuta machozi yanaanza kumtoka.
Kiukweli hakuamini kuwa mtoto aliyempenda kwa moyo wake wote, ndio
imefikia mwisho wake wa kuwa naye. Akaanza kulia na wakati analia mtoto
akafungua macho, mtoto akabakia akimuangalia mama yake huyo, na cha ajabu
kabisa yule mtoto akainuka na kusogea pale alipo huyo mama akamfuta machosi
akasema;
‘Mama lia….kwanini…?’ akauliza
‘Mhh mwanangu nakwenda sokoni nikirudi nitakueletea zawadi…’akasema
‘Mama- mimi -sokoni..’akasema
‘Huko kuna mbwa, ..huogopi mbwa wewe..’akasema mama mtu.
‘Mama…sini-ache. Mimi-sokoni…..’mtoto akawa kama anahisi kuwa huyo
mama anaondoka.
‘Mwanangu ngoja nikavae.., nikja nakuchukua tunakwenda sookoni
pamoja..’aliposema hivyo mtoto akafurahi, lakini mama mtu akashidwa kuvumilia,
akaanza kutoa machozi, akageuka na akajiukuta analia kwa kwikwi sasa.
Nesi kuona hivyo akamshika dada yake mkono na kumtoa nje, akamuita
nesi mwingine aende kukaa na huyo mtoto, ili asije akatoka
‘Hakikisha huyo mtoto hatoki, ngoja nimsindikize dada yangu..’akasema
na maensi na madakitari ambao walikuwepo hapo walikuwa hawajui kabisa ni nini
kinachoendelea wakabakia kuangalia tu, wakiulizana, kwani swala hilo lilikuwa
halijulikani kabisa kwa watu wengine zaidi ya dakitari mkuu na dakitari bingwa,
na nesi mmoja ambaye yupo likizo.
Nesi akamfikia dada yake akiwa kasimama, alikuwa kshikiliwa ukuta
kainamisha kichwa, akamsogelea na kumshika begani, huku akisema ;
‘Dada sasa ni bora uondoke, shemeji anakusubiria nje…’akasema nesi
‘Hapana mimi sikubali, huyu ni mwanangu, huyo mama anakuja kudai huyo
mtoto sasa baada ya miaka miwili…, sikubali kumwachia mwanangu…..’aliposema
hivyo ikaonekana dada mtu akiyumba, na
kabla nesi hajamshikilia vyema, dada yake akadondoka chini,….na alionekana
kupoteza fahamu
‘Oh nini tena dada….jamani njooni mnisaidie….’
WAZO LA LEO: Mawazo yakizidi sana ni hatari, kama
wanadamu tuna matatizo mengi, na wakati mwingine mtu huja kushindwa kujizuia,
akatawaliwa na mawazo, na hapo huwa ni ugonjwa.
Mawazo huja kuleta atharai nyingi mwilini. Mtu kama huyu pamoja na
kujisaidia yeye mwenyewe, lakini watu wanaishi karibu naye wanaweza kuwa dakitari wa kwanza, kwa
kujaribu kumsaidia kwa ushauri nasaha, kwani madhara ya hayo mawazo yanaweza
kuwa makubwa na mkja kuhangaika sana .
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment